4. Mwamko wa Roho Aliyedanganywa

Na Yuanzhi, Brazili

Nilizaliwa katika mji mdogo huko Kaskazini mwa China na mnamo 2010, nikafuata jamaa kwenda Brazili. Hapa nchini Brazili, nilijuana na rafiki Mkristo ambaye alinileta kanisani kusikiliza mahubiri kadhaa, baada ya kwenda mara tatu bado sikuwa nimeelewa chochote. Nilijishughulisha sana na kazi baada ya hapo, kwa hivyo sikuenda tena kanisani hadi siku moja mnamo Juni, 2015, wakati rafiki yangu alinileta kanisani tena. Wakati huo, mwishowe nilipata ufahamu juu ya Bwana Yesu kama Mkombozi kupitia yale ambayo ndugu walishiriki. Hasa, niliposoma Mwanzo mara ya kwanza, nikagundua kwamba mwanadamu kweli aliumbwa na Mungu, kwamba Mungu alikuwa ameumba vitu vyote, na nilihisi kuwa Muumba ni wa kushangaza kweli. Nilipokuwa shuleni vitabu vyote vya maandishi vilikuwa vimenifundisha kuwa mwanadamu aligeuka kutoka kwa mamalia wa hali ya juu, na vitu vyote ulimwenguni viliumbwa kwa kawaida—ilitukia kwamba nilikuwa nimedanganywa kwa zaidi ya miongo miwili. Ni baada tu ya kusoma Biblia ndipo niligutuka kabisa, na kutoka hatua hiyo, nilimwamini Bwana Yesu.

Mwishoni mwa mwaka wa 2015, nilirudi tena Brazili baada ya miezi mitano nchini China. Wakati huu, niliamua kupata kazi ya kudumu na kutulia vizuri. Hata hivyo, mambo hayaendi vile yalivyopangwa kila wakati. Mambo hayakuwa yanaenda vizuri kazini au katika maisha yangu ya kibinafsi, yakiniacha nikiteseka na nikiwa mwenye wasiwasi. Jioni moja, nilimpigia simu yule rafiki Mkristo kulalamika, na aliniambia, “Jitulize na umwombe Bwana na uone jinsi Bwana anavyokupangia kila kitu.” Kwa hivyo, niliutuliza moyo wangu na nikamwomba Bwana, “Bwana Yesu! Nimekumbana na shida kadhaa kazini ambazo sijui jinsi ya kushughulikia. Bwana, natumai kuwa naweza kupata msaada kutoka Kwako.” Nilishangaa, siku nne baadaye, bosi wangu aliniita na kuniambia nirudi kazini. Nilifurahi na nikawa na shukrani kwamba Bwana Yesu alisikia maombi yangu. Nilipokea neema zaidi ya Bwana baada ya hapo, kwa hivyo nilianza kuhudhuria mikutano kila wiki kulipa upendo Wake, hata ningepaswa kuchukua likizo kutoka kazini.

Kuanzia Juni 2016, sio tu kwamba nilikuwa nahudhuria mikutano ya kanisa, lakini pia nilishiriki mistari ya Biblia na marafiki kwenye Facebook, na pia ningevinjari kwenye Facebook kuona yaliyomo ili niweze kupata ufahamu zaidi kumhusu Bwana. Niliongeza marafiki wengi ambao wote wangeshiriki nami mistari ya Biblia wanapokuwa na wakati. Hii ilikuwa thawabu sana kwangu. Siku moja nilipokuwa navinjari kwenye Facebook, niliona video iliyokuwa na maelezo “Mungu Anashuka Na Hukum”—hili lilinivutia mara moja. Kwa hamu, niliibonyeza. Nilishangaa sana kwamba ilikuwa imefanywa vizuri. Kwa kifupi, ilikuwa ya kuvutia! Nilivutiwa na kuimba kwa sauti kubwa, kwa nguvu, maneno ya nyimbo ambayo yaligonga mioyoni mwao, na shauku ya kila mtu katika uimbaji huo. Kuangalia kwa ukaribu, niliona kuwa video hiyo ilitoka katika Kanisa la Mwenyezi Mungu. Niliwaza: “Waimbaji wote kweli wanajitolea kwa hamu na ghamu—ni kama kwamba wanaimba ili Mungu asikie. Kanisa la Mwenyezi Mungu linaonekana kuwa sio baya hata hivyo! Hii ni mara ya kwanza kusikia habari zao; nikipata nafasi napaswa kuwasiliana nao.”

Siku moja, nilituma kiunga cha video hiyo kwa rafiki wa Facebook, Dada Yang, ambaye nilijadili naye Biblia mara kwa mara. Aliipenda sana pia, na akasema kwamba alikuwa na hamu ya kujifunza zaidi juu ya Kanisa la Mwenyezi Mungu. Alihisi kwamba kanisa hili hakika lilikuwa la kipekee sana na kwamba lilijazwa na kazi ya Roho Mtakatifu. Kisha nikashiriki video hiyo kwenye ukurasa wangu wa Facebook, lakini nilishangaa, rafiki yangu mmoja aliitazama na kuniambia kuwa Kanisa la Mwenyezi Mungu halikuwa zuri, na pia alinitumia kila aina ya mambo hasi kulihusu. Kuona nyenzo hizi zote ambazo zilimkufuru Mwenyezi Mungu na kulihukumu Kanisa la Mwenyezi Mungu kwa kweli zilinitia hofu na nikawaza: “Kanisa hili linaonekana kuwa sawa—mtu yeyote anawezaje kuwa na shida nao?” Nilipoenda kuitazama video hiyo tena, ghafla nilikumbuka kitu ambacho mchungaji wangu alikuwa amesema wakati mmoja katika mahubiri, kwamba Makristo wa uwongo watatokea katika siku za mwisho. Nikiiacha njia ya Bwana Yesu, si nitakuwa nimeisha? Nilijua kwamba hicho kilikuwa kitu ambacho singeweza tu kupuuza, kwa hivyo niliamua kutoitazama tu wakati huo. Niliwasiliana na dada Yang mara moja na nikamwelezea hali hiyo. Jibu lake lilikuwa, “Hatuwezi kutegemea tu upande mmoja wa hadithi kuamua ikiwa ni kweli au si ya kweli. Hii hailingani na mafundisho ya Bwana. Sote ambao ni waumini katika Bwana tunangojea kurudi Kwake, na sasa hivi, watu wengine wanasema kwamba Yeye tayari amekuja. Lazima tuchunguze hili. Hatuwezi tu kufuata umati, tukihukumu na kushutumu bila kufikiria. Acha tuwatafute watu wengine kutoka katika Kanisa la Mwenyezi Mungu na tulichunguze. Tutaona jinsi walivyo kweli—hakuna kitu kilicho halisi kinachoweza kufanywa kuwa bandia, na hakuna kitu kilicho bandia kinachoweza kufanywa kuwa halisi.” Niliwaza: “Dada Yang yuko sahihi. Kwa kweli hii ni mara ya kwanza kumsikia mtu yeyote akihubiri injili kwamba Bwana amerudi, na kuongezea sijui kama mambo hayo kwenye Mtandao yanayolishutumu Kanisa la Mwenyezi Mungu ni ya kweli au ya uwongo. Ninaona kuwa video na sinema zilizopigwa na Kanisa la Mwenyezi Mungu ni nzuri. Napaswa kwenda kujifunza juu yake—hiyo ndiyo njia ya pekee ya busara ya kuchukulia kurudi kwa Bwana.” Na kwa hivyo, nilikubali kuichunguza kazi ya Mwenyezi Mungu ya siku za mwisho na Dada Yang.

Dada Yang aliwasiliana nao kupitia maelezo ya mawasiliano yaliyoachwa mwishoni mwa video na kuishia kuwasiliana na Ndugu Zhang wa Kanisa la Mwenyezi Mungu huko Amerika ya Kaskazini. Mara tu tulipokuwa mtandaoni na yeye, mimi na Dada Yang tuliibua swali moja: “Sisi sote tunajua kuwa Bwana atarudi katika siku za mwisho; hata hivyo, Bwana Yesu alisema: ‘Basi iwapo mtu yeyote atawaambia, Tazameni, Kristo yuko huku, au yuko pale; msiamini hili. Kwa kuwa wataibuka Makristo wasio wa kweli, na manabii wasio wa kweli, nao wataonyesha ishara kubwa na vioja; ili kwamba, ikiwezekana, watawadanganya walio wateule zaidi(Mathayo 24:23-24). Ndugu Zhang, unaonaje kuhusu suala hili la Makristo wa uwongo kujitokeza katika siku za mwisho kuwadanganya watu?”

Ndugu Zhang alisema: “Bwana Yesu alisema mambo haya kutuonya: Atakaporudi katika siku za mwisho, Makristo wa uwongo pia watatokea. Mapenzi ya Bwana ni kutufanya tuweze kukuza utambuzi ili tusije tukadanganywa na Makristo wa uwongo. Hata hivyo, Hakusema hivi ili tumkatae kabisa mtu yeyote anayesema kwamba Bwana amerudi, au hata kwenda kiasi cha kumhukumu na kumshutumu. Huku ni kutoelewa kwetu maneno kwa Bwana Yesu. Bwana Yesu alikuwa wazi kuhusu kile ambacho ni Makristo wa uwongo: ‘Kwa kuwa wataibuka Makristo wasio wa kweli, na manabii wasio wa kweli, nao wataonyesha ishara kubwa na vioja; ili kwamba, ikiwezekana, watawadanganya walio wateule zaidi(Mathayo 24:24). Ishara za wazi za Makristo wa uwongo ni kwamba wanaiga kazi ya Bwana Yesu, wakionyesha ishara, kutenda miujiza, kuponya magonjwa na kufukuza pepo. Haya ndiyo maeneo ambayo Makristo wa uwongo ni ujanja na waovu zaidi, na ndizo sifa zao za msingi. Maneno ya Mwenyezi Mungu ni bayana zaidi na makali sana kuhusu udhihirisho na alama za Makristo wa uwongo. Mwenyezi Mungu alisema: ‘Kama, wakati wa zama hizi, kutatokea mtu mwenye uwezo wa kuonyesha ishara na maajabu, na kutoa mapepo, kuponya wagonjwa, na kufanya miujiza mingi, na kama mtu huyu anadai kwamba yeye ni Yesu ambaye amekuja, basi hii itakuwa ni ghushi ya roho wachafu, na kumuiga Yesu. Kumbuka hili! Mungu Harudii kazi ile ile. Hatua ya kazi ya Yesu tayari imekwisha kamilika, na Mungu Hataichukua tena hatua hiyo ya kazi. … Ikiwa, wakati wa siku za mwisho, Mungu bado Angeonyesha ishara na maajabu, na bado Angetoa mapepo na kuponya wagonjwa—kama Angefanya vilevile ambavyo Yesu Alifanya—basi Mungu Angekuwa Anarudia kazi ile ile, na kazi ya Yesu isingekuwa na maana au thamani yoyote. Hivyo, Mungu Anatekeleza hatua moja ya kazi katika kila enzi. Mara tu kila hatua ya kazi Yake inapokamilika, baada ya muda mfupi inaigizwa na roho wachafu, na baada ya Shetani kuanza kufuata nyayo za Mungu, Mungu Anabadilisha na kutumia mbinu nyingine. Mara Mungu Anapokamilisha hatua ya kazi Yake, inaigizwa na roho wachafu. Lazima muelewe vizuri hili(Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Kuijua Kazi ya Mungu Leo). Sote tunajua kuwa yote ambayo ni ya uwongo yanaweza tu kujishikilia kwenye mikia ya ya kile kilicho cha kweli na kukiiga. Makristo wa uwongo sio tofauti. Ni roho waovu na wanakosa kiini cha Kristo. Hawawezi kufanya kazi ya Kristo, hawana uwezo wa kuonyesha ukweli, na hawawezi kuonyesha tabia ya Mungu au yote ambayo Mungu anayo na kile Alicho. Hawawezi kumletea mwanadamu ukweli, njia, na uzima. Kwa hivyo, Makristo wa uwongo wanaweza tu kuiga kazi ambayo Bwana Yesu amefanya tayari; kila wanachoweza kufanya ni kutenda ishara na maajabu ili kuwadanganya watu wapumbavu na wajinga. Kuna watu wengine ambao wamepagawa na pepo wachafu, ambao kwa ufidhuli hutangaza kwamba wao ni Bwana Yesu aliyerejea, na kumwiga Bwana Yesu katika kufanya vitu kama vile kuponya magonjwa na kufukuza pepo, kufanya miujiza, na kuhubiri njia ya toba na msamaha. Hakuna hata chembe ya shaka kwamba wao ni Makristo wa uwongo wanaodanganya watu. Kazi ya Mungu ni mpya kila wakati na sio nzee kamwe, kila wakati inakua kwenda mbele. Kamwe Hatarudia kazi ya zamani ambayo Ameifanya hapo awali. Hii ni kama tu Bwana Yesu alipokuja kufanya kazi; Aliitamatisha Enzi ya Sheria na kufungua Enzi ya Neema. Hakurudia kazi ambayo Yehova Mungu alikuwa amefanya ya kutoa sheria ya kuwaongoza watu katika maisha yao, lakini badala yake, Alitekeleza kazi Yake ya ukombozi kwa msingi wa kazi ya Enzi ya Sheria. Bwana Yesu alimletea mwanadamu njia ya toba na msamaha; mradi tunakuja mbele Yake, tunakiri, na kutubu, Bwana atasamehe dhambi zetu na kusahau makosa yetu, na kutufanya tustahili kufurahia neema na baraka nyingi ambazo Bwana huwapa wanadamu. Kazi hiyo yote ilikuwa mpya, na isingeweza kufanywa na roho mbaya au na Shetani. Hii ni sawa kwa Bwana Yesu aliyerejea katika siku za mwisho—Mwenyezi Mungu alihitimisha Enzi ya Neema na kuanzisha Enzi ya Ufalme. Mwenyezi Mungu hakurudia kazi ya ukombozi ya Bwana Yesu—Yeye hafukuzi pepo, kuponya wagonjwa, au kuwafanyia watu miujiza. Badala yake, Anaonyesha ukweli na kutekeleza hatua ya kazi ya kumhukumu na kumtakasa mwanadamu kwa msingi wa kazi ya ukombozi. Anawaokoa wanadamu kabisa kutoka kwa umiliki wa Shetani na anatuleta katika ufalme wa Mungu. Hii yote ni kazi mpya kutoka kwa Mungu ambayo hajawahi kuifanya awali na haingeweza kutekelezwa na Kristo yeyote wa uwongo. Mradi tu tujue kuwa kazi ya Mungu ni mpya kila wakati na sio nzee kamwe, na tunaelewa kanuni za kumtambua Kristo wa kweli kutoka kwa Makristo wa uwongo, kwa kawaida tutatofautisha kati ya kuonekana na kazi ya Mungu na udanganyifu wa Makristo wa uwongo.”

Nilipata mengi sana kutoka kwa mawasiliano ya Ndugu Zhang; ushirika wake ulikuwa wazi sana. Makristo wa uwongo wanaweza kurudia tu na kuiga kazi zingine ambazo Mungu alifanya zamani, lakini hawawezi kamwe kufanya kazi yoyote mpya, wala hawawezi kumpa mwanadamu njia mpya. Kwa wakati huu, nilielewa maana ya kweli ya maneno ya Bwana Yesu: “Kwa kuwa wataibuka Makristo wasio wa kweli, na manabii wasio wa kweli, nao wataonyesha ishara kubwa na vioja; ili kwamba, ikiwezekana, watawadanganya walio wateule zaidi(Mathayo 24:24). Dada Yang pia alisema kwamba amevuna mavuno mengi kutoka katika hili, kwa hivyo tulifanya miadi na Ndugu Zhang jioni iliyofuata ili tuweze kuendelea kusikiliza ushirika wake.

Nilihisi kuwa kile ambacho Ndugu Zhang kutoka katika Kanisa la Mwenyezi Mungu alishiriki kilikuwa cha ajabu na cha kunijengea maadili kweli. Hata hivyo, nilipofikiria kuhusu uvumi wote huo uliokuwa mtandaoni nilikuwa bado naogopa kidogo. Baada ya kurudi kanisani kwangu, nilimuuliza mmoja wa akina ndugu wakubwa kama alijua chochote kuhusu Kanisa la Mwenyezi Mungu. Aliniambia kwamba mchungaji alikuwa amesema kwamba hatupaswi kuhusiana nao kwa vyovyote; pia aliniambia juu ya mambo kadhaa ambayo wachungaji kadhaa walikuwa wamesema, yakihukumu, kushambulia, na kumshutumu Mwenyezi Mungu. Wakati niliposikia haya nilisita kidogo. Sikupoteza muda kumjulisha Dada Yang kuhusu habari hii hasi na kupendekeza aache kuwasiliana na Kanisa la Mwenyezi Mungu. Hata hivyo, Dada Yang alionekana kuwa na nia ya kuchunguza kazi ya Mwenyezi Mungu ya siku za mwisho. Akaniambia, “Kila mahali ambapo nyayo za Mwanakondoo zinaniongoza, nitafuata. Hivi majuzi nimeelewa ukweli kadhaa kwa kusoma maneno ya Mwenyezi Mungu kwenye mtandao na kutazama video za kila aina na sinema za injili kutoka kwa Kanisa la Mwenyezi Mungu. Mkanganyiko na shida nyingi ambazo zilinisonga zamani zimesuluhishwa. Nahisi kuwa maneno ya Mwenyezi Mungu ni ukweli. Bila kujali jinsi wengine wanalishutumu Kanisa la Mwenyezi Mungu, nitalichunguza hadi nipate uwazi kamili.” Sikuweza kumshawishi Dada Yang, kwa hivyo nilimzuia yeye na Ndugu Zhang kwenye Facebook na sikuthubutu kuwasiliana nao tena.

Hata hivyo, hata siku mbili hazikuwa zimepita kabla ya mimi kuanza kuwa na ukavu kazini. Siku baada ya siku, sikuwa na chochote cha kufanya isipokuwa kutengeneza chakula nyumbani. Kwa vile sikuwa na cha kufanya, nilifungua YouTube kutazama sinema kadhaa, lakini cha kushangaza, kila wakati, sinema, video za muziki, na kwaya za Kanisa la Mwenyezi Mungu zingejitokeza. Nilianza kufikiria: “Video na sinema za Kanisa la Mwenyezi Mungu zinatolewa kwa haraka sana. Inashangaza! Chochote kinachotoka kwa Mungu bila shaka lazima kifanikiwe, kwa hivyo inaweza kuwa Kanisa la Mwenyezi Mungu linatoka kwa Mungu? Kila kitu ambacho Ndugu Zhang alizungumza kuhusu wakati uliopita kilikuwa sambamba na ukweli. Labda napaswa kujaribu kupata ufahamu wa Kanisa la Mwenyezi Mungu kwa mara nyingine tena. Siwezi kukataa kwa kupuuza kuchunguza kazi ya Mwenyezi Mungu ya siku za mwisho kwa sababu ya kile ambacho watu wengine wanasema.” Hata hivyo, mara tu nilipofikiria juu ya yale niliyoona mtandaoni yakimshutumu Mwenyezi Mungu pamoja na onyo la mchungaji wangu la kutowasiliana na Kanisa la Mwenyezi Mungu, nilifikiria labda sipaswi kuendelea zaidi. Kwa hivyo, niliamua kutafuta video zingine za kutazama kwenye YouTube. Hata hivyo, kila mahali nilipoangalia, kulikuwa na video kutoka kwa Kanisa la Mwenyezi Mungu na nilianza kuwa na hisia ya kutojiweza. Mwishowe, udadisi wangu ulichukua nafasi na nikawaza: “Haijalishi kama Kanisa la Mwenyezi Mungu ni nzuri au la. Nitaangalia video zao haraka tu, na ikiwa sio nzuri, basi litakuwa funzo la kupata utambuzi.” Kisha nilibofya kwenye video inayoitwa Utendaji wa 9 wa Kwaya ya Injili. Video hii ilivutia shauku yangu kwa sababu ilikuwa taswira halisi ya jamii ya kisasa ambayo nilifahamiana nayoa. Ilionyesha maisha ya binadamu kwa uwazi kabisa, kwa kweli, na kwa uhalisi. Nililia na kucheka ilipokuwa ikiendelea; moyo wangu uliguswa sana, na ulijawa na nguvu. Mara moja nilikuwa na hamu ya kutazama kila moja ya video iliyotolewa na Kanisa la Mwenyezi Mungu. Baada ya hapo nilianza kutazama video kutoka kwa Kanisa la Mwenyezi Mungu kila siku, na ndani ya wiki moja nilikuwa nimetazama matukio yote 17 ya video za kwaya za Kichina. Kadiri nilivyozitazama zaidi ndivyo nilivyohisimvuto kwazo zaidi. Kulionekana kuwa na nguvu ndani ya moyo wangu ikinihimiza kutazama na kuchunguza bila kuchelewa. Niliwaza: “Nimetazama video nyingi za Kanisa la Mwenyezi Mungu; kila moja yake imekuwa yenye faida kwangu, na pia hakujakuwa na neno hasi hata moja hasi kati yake: Yote ni mazuri. Mengine yayo hufunua giza la ulimwengu, mengine humshuhudia Mungu, na mengine yanamwongoza mwanadamu kurudi mbele za Mungu. Hakuna najisi ya mambo ya kimwili au ya kidunia. Kanisa la Mwenyezi Mungu limejaa kazi ya Roho Mtakatifu. Haliko kabisa kama vile uvumi unavyosema. Kazi ya Mwenyezi Mungu katika siku za mwisho hakika inafaa kuchunguzwa!”

Siku moja nilipokuwa nikivinjari kwenye Facebook, nilisoma uzoefu na ushuhuda wa mtu wenye kichwa “Nilipata Wokovu wa Siku za Mwisho kwenye Facebook.” Nilifungua na kuona kwamba dada huyu alikuwa na uzoefu kama wangu. Wakati aliwasiliana kwa mara ya kwanza na Kanisa la Mwenyezi Mungu, marafiki zake mtandaoni walimtumia uvumi kuhusu kanisa hilo ambao ulimzuia kweli. Nililiendelea kusoma kwa hamu, nikitamani kujua kilichotokea mwishoni. Niliona kuwa baada ya dada huyu kumwomba Bwana na kumwomba Amwongoze, alihisi kuwa hangeweza kuchagua kile alichochagua kusikiliza na kuamini, lakini ilimbidi achunguze Kanisa la Mwenyezi Mungu kwa njia ya vitendo ili agundue kama lilikuwa la kweli au la uongo. Kusikiliza uvumi bila kufikiria na kukataa kuchunguza kuja kwa Bwana mara ya pili hakutakuwa njia ya busara sana, kwa hivyo alihisi kwamba ilimlazimu apate ukweli kuhusu kurudi kwa Bwana. Maneno haya yalinigusa sana. Kurudi kwa Bwana ni jambo muhimu na lazima mtu alichukile kwa busara. Hatuwezi kufuata umati tu; hatuwezi kulikataa na kulipinga bila kufikiria. Niliendelea kusoma makala hiyo na kuona kwamba kile ambacho dada huyu alikuja kuelewa kuhusu Kanisa la Mwenyezi Mungu kilikuwa tofauti kabisa na kile ambacho marafiki wake wa mtandaoni walikuwa wakimwambia. Pia yeye binafsi alikuwa mwenyeji wa dada kadhaa wageni kutoka katika Kanisa la Mwenyezi Mungu ambao walishirikiana naye kuhusu maneno ya Mwenyezi Mungu, na walikuwa wenye msadaa na wenye kumjali. Uzoefu wa kweli wa dada huyu uliniambia kuwa singeendelea kudanganywa na uvumi huu, wala singeweza kudanganywa na uvumi, kukataa kuchunguza kazi ya Mwenyezi Mungu katika siku za mwisho. La sivyo, inawezekana ningepoteza wokovu wa Mungu wa siku za mwisho. Nilijua ilinilazimu niwasiliane na Kanisa la Mwenyezi Mungu kwa uchunguzi zaidi!

Usiku huo nilipokuwa nikigaagaa na kupindukapinduka kitandani bila kutulia, niliwaza, “Lazima nimtafute Dada Yang tena, hata ingawa nilimzuia. Nikiweza kumpata bila shaka nitaweza kumpata Ndugu Zhang kutoka katika Kanisa la Mwenyezi Mungu. Dada Yang ni muumini wa kweli na amekuwa akichunguza kazi ya Mwenyezi Mungu ya siku za mwisho wakati huu wote. Labda amepata ufahamu mwingi kufikia sasa. Ninahitaji sana kumuuliza jinsi uchunguzi wake unavyoendelea.” Haikuwa kazi rahisi, lakini kwa msaada wa marafiki kadhaa, niliipata akaunti ya Facebook ya Dada Yang siku kadhaa baadaye. Nilifurahi sana kwamba hakunikasirikia kwa sababu ya kumzuia. Nilipowasiliana naye, aliniambia kuwa tayari alikuwa amepata uwazi kupitia uchunguzi wake, na kwamba Mwenyezi Mungu ndiye kurudi kwa Bwana Yesu. Pia aliniunganisha na Ndugu Zhang kwa furaha. Wakati sote watatu tuliunganishwa mtandaoni, niliwaambia, “Kupitia uzoefu wangu wa hivi karibuni, naona kwamba Bwana ananiongoza. Mimi pia niko tayari kutafuta na kuichunguza kazi ya Mwenyezi Mungu katika siku za mwisho, lakini, nina maswali mengi sana kwenu wawili ambayo ningependa ushirika wenu kuyahusu. Jambo moja ambalo siwezi kuelewa kabisa ni kwamba Yesu alipata mwili kama mwanadamu kufanya kazi Yake, kwa hivyo ni vipi kwamba sasa Anarejea katika mwili kama mwanamke kufanya kazi Yake? Hii ni siri. Ndugu Zhang, unaweza kunielezea jambo hili?”

Kujibu swali langu, Ndugu Zhang alijibu, “Ndiyo. Kuna siri zilizomo ndani ya kupata mwili kwa Mungu—umuhimu ni mkubwa na wa kina, na vile vile kitu kisichoeleweka kwetu. Kwa hivyo, lazima tudumishe mioyo ya heshima kuhusu kurudi kwa Bwana. Hata kama kazi ya Mungu hailingani na fikira zetu hata kidogo, lazima tuchunge ndimi zetu. Hatupaswi kuihukumu bila kufikiria jambo hilo vizuri. Kwa kusema kweli, kuhukumu kiholela kazi ya Mungu ni kumkufuru Mungu, na dhambi ya kukufuru haiwezi kusamehewa katika maisha haya au yajayo. Mwenyezi Mungu wa siku za mwisho amekuja na kufungua siri zote. Hii inatimiza kabisa unabii wa Yesu: ‘Bado ningali nayo mengi ya kuwaambieni, lakini hivi sasa hamwezi kuyavumilia. Hata hivyo, wakati yeye, Roho wa ukweli, atakapokuja, atawaongoza hadi kwenye ukweli wote: kwa maana hatazungumza juu yake mwenyewe; bali chochote atakachosikia, atakinena: na atawaonyesha mambo yajayo(Yohana 16:12-13). Acha tusome maneno ya Mwenyezi Mungu kwa pamoja ili tuelewe kipengele hiki cha ukweli. Mwenyezi Mungu alisema: ‘Yesu alipokuja zamani, Alikuwa mwanaume, lakini Mungu anapokuja wakati huu Yeye ni mwanamke. Kutokana na hili, unaweza kuona kwamba Mungu aliwaumba mwanaume na mwanamke kwa ajili ya kazi Yake na Kwake hakuna tofauti ya jinsia. Roho Wake anapowasili, Anaweza kuchukua mwili wowote kwa matakwa Yake na mwili huo unaweza kumwakilisha Yeye. Uwe wa kiume au kike, unaweza kumwakilisha Mungu alimradi tu ni mwili Wake wa nyama. Kama Yesu angeonekana kama kike alipokuja, kwa maneno mengine, iwapo mtoto wa kike, sio wa kiume, angezaliwa kwa njia ya Roho Mtakatifu, hatua hiyo ya kazi ingekuwa imekamilika pia. Kama hali ingekuwa hivyo, basi hatua ya leo ya kazi ingelazimika kukamilishwa badala yake na mwanaume, lakini kazi ingekamilika pia. Kazi inayofanywa katika hatua hizi zote ni muhimu kwa kiwango sawa; hakuna hatua yoyote ya kazi inayojirudia au kupingana na nyingine. Wakati huo, Yesu alipokuwa akifanya kazi Yake aliitwa Mwana wa pekee, na “Mwana” inaashiria jinsia ya kiume. Basi kwa nini Mwana wa pekee halikutajwa katika hatua hii? Hii ni kwa sababu mahitaji ya kazi yamelazimisha badiliko la jinsia ambayo ni tofauti na ile ya Yesu. Kwa Mungu hakuna tofauti ya jinsia. Kazi Yake inafanywa kama Anavyotaka na katika kufanya kazi Yake hazuiliwi na kitu chochote kile, lakini hasa yupo huru. Hata hivyo, kila hatua ya kazi ina umuhimu wake mkubwa. Mungu alipata mwili mara mbili, na ni dhahiri kwamba kupata mwili Kwake katika siku za mwisho ni mara ya mwisho. Amekuja kufichua matendo Yake yote. Ikiwa katika hatua hii Hakupata mwili ili Yeye binafsi afanye kazi kwa ajili ya mwanadamu kushuhudia, mwanadamu milele angeshikilia fikra kwamba Mungu ni wa kuime tu, na si wa kike. … Hapo mwanzo, Yehova alipoumba wanadamu, Aliwaumba wanadamu wa aina mbili, mwanamume na mwanamke; na kwa hiyo, kuna mgawanyo wa kike na kiume katika miili Yake. Hakuamua juu ya kazi Yake kulingana na maneno aliyozungumza kwa Adamu na Hawa. Mara mbili Alipopata mwili kuliamuliwa kwa kuzingatia kabisa mawazo Yake alipowaumba wanadamu kwa mara ya kwanza, yaani, Alikamilisha kazi ya kupata Kwake mwili mara mbili, kwa msingi wa mwanamke na mwanamume kabla ya wao kupotoshwa(Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Kupata Mwili Mara Mbili Kunakamilisha Umuhimu wa Kupata Mwili). ‘Kijinsia, mmoja ni mwanamke na mwingine ni mwanamume; kwa hili, maana ya kupata mwili kwa Mungu imekamilishwa. Mawazo mabaya ya mwanadamu kumhusu Mungu yameondolewa: Mungu Anaweza kuwa mwanamke na mwanamume, na kimsingi Mungu mwenye mwili Hana jinsia. Alimuumba mwanamume na mwanamke, na Kwake, hakuna mgawanyiko wa jinsia(Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Kiini cha Mwili Ulio na Mungu).”

Baada ya kusoma maneno ya Mungu, Ndugu Zhang alishiriki ushirika huu, “Chochote afanyacho Mungu kina maana. Mungu hawezi kabisa kufanya kitu chochote kisicho na maana au thamani. Biblia inasema: ‘Kwa hivyo Mungu akamuumba mwanadamu kwa sura yake mwenyewe, kwa sura ya Mungu alimwumba; aliwaumba wa kiume na wa kike’ (Mwanzo 1:27). Tunaweza kuona kutoka kwa hili kwamba hapo mwanzo, Mungu alimuumba mwanamume na mwanamke kwa mfano Wake. Mungu anaweza kupata mwili kama mwanamume, na Anaweza kupata mwili kama mwanamke vile vile. Ndani ya Mungu, hakuna tofauti kati ya jinsia; ikiwa anakuwa mwanamume au mwanamke, Ana kiini cha Mungu na anaweza kufanya kazi ya Mungu mwenyewe. Mungu kuchukua jinsia mbili tofauti mara mbili ambazo Amepata mwili ni ili kukamilisha umuhimu wa kupata mwili Kwake na kuondoa imani isiyo ya kweli ya mwanadamu kwamba Mungu anaweza tu kuwa mwili kama mwanamume, kuwa Hawezi kupata mwili kama mwanamke. Hii inaruhusu wanadamu kutambua kuwa sio tu kwamba kupata mwili kwa Mungu kunaweza kuchukua utambulisho wa mwanamume, lakini pia kunaweza kuchukua utambulisho wa mwanamke. Hili linawaruhusu binadamu kuona kwamba Mungu kweli ni mwenye uweza, kwamba hatuwezi kumwelewa, na hatupaswi kumhukumu au kumwekea Mungu mipaka kiholelea. Kwa kuongezea, kiini cha Mungu ni cha roho, na hakuna tofauti ya jinsia katika roho. Jinsia inatumika kwa binadamu aliyeumbwa tu. Mungu amekuwa mwili mara mbili ili kuwaokoa na kuwakomboa wanadamu, kwa hivyo, jinsia ya mwili wa Mungu inategemea tu wakati ambao Yeye anafanya kazi Yake katika mwili. Mara tu kazi ya Mungu mwenye mwili ulimwenguni inapokamilika, Anarejea katika ulimwengu wa kiroho na wakati huo, hakuna tena tofauti yoyote kulingana na jinsia. Kwa hivyo, tukimwekea Mungu mipaka katika jinsia fulani, ni kufuru kubwa mno!”

Kusikiliza maneno ya Mwenyezi Mungu na ushirika wa Ndugu Zhang kulinipa mwale wa ghafla wa ufahamu. Mwishowe nilielewa ni kwa nini Mungu amechukua jinsia tofauti katika kila kupata mwili Kwake. Niligundua kuwa ndani ya hili kuna mapenzi ya Mungu kutoka Alipomuumba mwanadamu mwanzoni na nia Zake zenye fadhila. Kama Mungu angekuja kufanya kazi kama mwanaume katika kupata kupata mwili Kwake kuwili, tungeamini milele kwamba Mungu ni mwanamume na tungeamini kwa makosa kwamba jinsia ya kiume ni kubwa na ya hadhi ya juu kuliko jinsia ya kike. Mungu mwenye mwili wa siku za mwisho kufanya kazi kama mwanamke ni mfano wa usawa na haki ya Mungu, na kuliniruhusu nione umuhimu mkubwa wa Mungu kupata mwili na kufanya kazi kama mwanamke wakati huu! La sivyo, hatungekuwa na ufahamu kumhusu Mungu, na maoni yetu na kumwekea Mungu mipaka hakungeweza kuondolewa na aidha, hili lingeikosea tabia ya Mungu. Mara ya kwanza Mungu alipata mwili, Alionekana kama mwanadamu, na katika siku za mwisho, Ameonekana kama mwanamke. Huku kupata mwili kuwili kwa Mungu kunatuonyesha kweli umuhimu kamili wa kupata mwili wa Mungu; kumenipa ufahamu sahihi na wa kweli zaidi kumhusu Mungu. Shukrani ziwe kwa Mungu! Kazi ya Mungu ni ya busara kweli!

Baada ya Dada Yang na Ndugu Zhang kusikiliza ufahamu na ujuzi wangu wa maneno ya Mungu, walifurahi kwamba niliweza kuelewa mapenzi ya Mungu na kuondoa maoni yangu na na kumwelewa Mungu visivyo. Waliguswa sana hadi wakalia machozi na kazi ya wokovu ambayo Mungu alikuwa amefanya kwangu. Tuliungana pamoja katika ushirika mara tatu zaidi. Mshukuru Mungu kwa mwongozo Wake. Nilielewa ukweli zaidi na zaidi, nilijifunza siri ya kupata mwili kwa Mungu, na nilijifunza siri za hatua tatu za kazi za Mungu. Nilijifunza kuhusu tofauti kati ya kazi ya Mungu na kazi ya mwanadamu, tofauti kati ya kazi ya Roho Mtakatifu na kazi ya Shetani, na vipengele vingine vya ukweli. Nilihisi kweli kuwa Mwenyezi Mungu ni kurudi kwa Bwana Yesu na kwamba Yeye ndiye ukweli, njia na uzima. Jioni ya Jumamosihiyo, Dada Yang alinitumia video mpya ya muziki iitwayo Upendo wa Mungu Unauzingira Moyo Wangu, “Mapenzi ya Mungu yamefichuliwa kuwakamilisha wale wanaompenda kweli. Msio na hatia, mnaobubujikwa na uzima, toneni sifa zenu Kwake. Dansi ya furaha ni nzuri, rukeni na kucheza karibu na kiti cha enzi. Kutoka katika pembe nne za dunia, tunakuja, tukiitwa na sauti ya Mungu. Maneno Yake ya uzima tulipewa sisi, tunatakaswa na hukumu Yake. …” Wimbo huu ulinitia moyo sana kiasi kwamba nilitokwa na machozi. Nilipinga nambari ya simu ya Dada Yang, lakini nilikuwa nimezidiwa na hisia nyingi kiasi kwamba sikuweza kuzungumza. Nilichoweza kufanya kilikuwa tu kusema nikirudia, “Asante Mungu! Asante …”

Mara nguvu ya hisia zangu ilipopungua, usiku huo huo nilikuwa na mazungumzo ya moyoni sana na ndugu. Nilishukuru kwamba Mwenyezi Mungu hakukata tama kuhusu wokovu wangu wakati huo wote na kwamba hakuwa Amenishughulikia kulingana na uasi wangu na upinzani wangu. Badala yake, Yeye alikuwa pamoja nami kila wakati. Alitumia sinema za injili, video, na makala za ndugu juu ya uzoefu wao wao kuniongoza na kunisogeza kidogo kidogo, akinirudisha nyumbani Kwake, Akinileta mbele Yake. Kutoka katika kina cha moyo wangu, niliwaambia ndugu zangu: “Nimeshapitia upendo wa Mungu na pia ninaelewa ukweli wa kupata mwili kwa Mungu. Sitaamini tena uvumi na tetesi. Ninamkubali kabisa Mwenyezi Mungu kama Mwokozi wangu na kama Mungu wangu. Kwa maana tayari nimebaini kuwa Mwenyezi Mungu ndiye kurudi kwa Bwana Yesu—Yeye ndiye Mungu ambaye amenipa neema nyingi, na Yeye ndiye Mkombozi wa wanadamu.”

Ninapokumbuka nyuma kuhusu jinsi nilivyosikiliza uvumi zamani, jinsi nilivyokuwa na ugomvi kuhusu kazi ya Mungu katika siku za mwisho na hata nikasema maneno kadhaa ya hukumu dhidi ya Mungu, ya jinsi nilivyokuwa mwasi sana, ninahisi mdeni mkubwa kwa Mungu—nina huzuni na mwenye majuto mengi. Hata hivyo, Dada Yang aliniambia: “Wakati hatumjui Mungu, kama wanadamu tumo katika hatari ya kudanganywa na uwongo. Mradi tu tunatubu kwa kweli, Mungu hataweka rekodi. Neno la Mungu linasema, ‘Mungu hakuja wakati huu ili kuwaangusha watu, lakini badala yake kuwaokoa watu kwa kiwango kikubwa kiwezekanacho. Je, ni nani asiyefanya makosa kabisa? Je, kila mtu akiangushwa, basi unawezaje kuitwa wokovu? Makosa mengine hufanywa kimakusudi na makosa mengine kufanywa bila kupenda. Kwa mambo ya bila kupenda, unaweza kubadilika baada ya kuyatambua, hivyo Mungu angekugonga kabla hujabadilika? Je, hivi ndivyo Mungu huwaokoa watu? Si hivyo! Bila kujali iwapo unakosea bila kupenda ama kutokana na asili ya uasi, lazima ukumbuke: Harakisha na uuzindukie uhalisi. Endelea kwa bidii; bila kujali ni hali gani inayotokea, lazima uendelee kwa bidii. Mungu anafanya kazi ili kuwaokoa watu na Hatawagonga watu Anaotaka kuwaokoa bila taratibu(“Mapenzi ya Mungu ni Kuwaokoa Watu kwa Kiwango Kikubwa Sana Kinachowezekana” katika Kumbukumbu za Hotuba za Kristo).” Maneno ya Mungu yamenipa faraja kubwa na yameniruhusu nione kwamba Mungu ni mwingi wa rehema na msamaha. Upendo wa Mungu ni mkubwa sana! Siwezi kuzuia shukrani kwa Mungu ninayohisi ndani ya moyo wangu. Kwa kipindi cha muda kilichofuata, kupitia mwingiliano wangu na ndugu kutoka katika Kanisa la Mwenyezi Mungu, niliweza kuona kuwa kanisa haliko kabisa kama uvumi huo ulivyolidai kuwa. Kwa kweli, ni kinyume kabisa. Hapa ndipo pahali pa sisi kufuatilia ukweli na kumjua Mungu. Tunapokuwa na mikutano katika Kanisa la Mwenyezi Mungu, hakuna mtu anayeongea kuhusu kula, kunywa, na kufurahia; hakuna mtu anayeongea kuhusu magari, pesa au nyumba; hakuna mtu anayeongea kuhusu mambo machafu, najisi, maovu ulimwenguni. Sote tunasoma maneno ya Mwenyezi Mungu pamoja na tunashirikiana kuhusu uzoefu wetu na ufahamu wa maneno ya Mungu. Tunatenda na kufuata maneno ya Mwenyezi Mungu. Naweza kuona kuwa ndani ya Kanisa la Mwenyezi Mungu, maneno ya Mungu yana nguvu, ukweli unashikilia nguvu, na Kristo ana nguvu. Hapa ni mahali palipojaa usawa na haki. Ninahisi kama ninayeonja maisha mazuri katika mbingu na dunia mpya! Sasa ninapokumbuka uvumi huo, ninagundua kuwa yanawateka na kuwadhuru watu tu, na ilikuwa ni kwa sababu ya uvumi huo kwamba karibu nipoteze wokovu wa Mungu wa siku za mwisho. Kwa bahati nzuri, Mwenyezi Mungu aliniokoa na kuniruhusu nipate ufahamu fulani wa kazi ya Mungu. Roho yangu iligutushwa, nilipenya katika wavu uliofunganishwa wa uvumi wa Shetani, na nikaja mbele ya kiti cha enzi cha Mungu. Namshukuru Mungu kwa kuniokoa!

Iliyotangulia: 3. Kufichua Fumbo la Hukumu

Inayofuata: 5. Moyo Unaorandaranda Wakuja Nyumbani

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Maudhui Yanayohusiana

37. Mungu Yuko Kando Yangu

Na Guozi, MarekaniNilizaliwa katika familia ya Kikristo, na nilipokuwa na umri wa mwaka mmoja, mama yangu alikubali kazi mpya ya Bwana Yesu...

33. Bahati na Bahati Mbaya

Na Dujuan, JapaniNilizaliwa katika familia fukara katika kijiji cha mashambani. Tangu niwe mtoto, niliishi maisha magumu na nilidharauliwa...

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp