191 Maneno ya Mungu Yaliuzindua Moyo Wangu

1 Nilimwamini Mungu kwa miaka mingi, na ingawa nilihudhuria mikutano na kusoma maneno ya Mungu mara nyingi, kamwe sikukubali hukumu ya maneno ya Mungu ili kujichambua na kujichunguza. Nilikubali tu upotovu wangu na sikujua asili yangu au kiini changu. Nilipoelewa mafundisho kidogo, nilijisifu na nikadhani ni ukweli. Nilifanya kazi na kuhubiri lakini sikutilia maanani kutenda au kupitia maneno ya Mungu. Kama tu Paulo, nilijua tu jinsi ya kufanya kazi kwa ajili ya sifa na hadhi. Nilifurahia kuheshimiwa na kupendwa sana, na nilikuwa shupavu. Nilisisitiza kufuata njia yangu, lakini nilikuwa nimeridhika na sikuweza kujirudi.

2 Ni kwa kupitia tu kutofaulu na vizuizi ndipo niliona waziwazi kimo changu cha kweli. Nilipokabili hukumu na kuadibu kwa maneno ya Mungu, nilibishana na kujitetea. Nilijua vizuri kuwa ukweli ulikuwa na faida katika maisha ya watu, lakini sikuweza kukubali au kuutii. Nilitimiza wajibu wangu bila kanuni zozote za ukweli, na nikatenda kwa matamanio yangu. Nilipokabiliwa na kizuizi kidogo nilikuwa hasi na dhaifu, na nilijieleza kinaganaga. Kupitia majaribio niliona jinsi kimo changu kilivyokuwa kichanga, na kwamba nilikuwa mnyonge sana na mwenye kusikitisha. Kwa kukosa kujijua, nilijishaua, na hili lilikuwa jambo la aibu sana. Nilipokabiliwa na ukweli, nilihisi aibu na nikaacha kujivuna.

3 Baada ya kupitia hukumu, majaribio na ufunuo wa Mungu, sasa najijua. Ingawa naonekana kuwa na mwenendo mzuri, sina ucha Mungu moyoni mwangu. Bado ninashikilia fikira ya kazi ya Mungu moyoni mwangu, siwezi kunyenyekea kwa kweli. Nikiwa nimejawa na tabia ya kishetani, bado ninatenda kwa unafiki ili kumdanganya na kumpinga Mungu. Kutopata ukweli au uzima baada ya miaka hii yote ya imani ni aibu sana. Nimeelewa hatimaye kuwa kutofuatilia ukweli ni kupoteza wakati. Ni kwa msaada tu wa hukumu na kuadibu kwa Mungu ndiyo naweza kutubu kwa kweli. Natamani Mungu anihukumu, Aniadibu, Anijaribu na kunisafisha hata zaidi, ili tabia yangu ya kishetani iweze kutakaswa na niweze kuishi kwa kudhihirisha mfano wa binadamu ili kumtukuza Mungu.

Iliyotangulia: 190 Hukumu Iliuzindua Moyo Wangu

Inayofuata: 192 Hukumu ya Mungu Huniokoa Kutokana na Dhambi

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Maudhui Yanayohusiana

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp