52. Buriani, Mtu Mwenye Kujipendekeza

Na Li Fei, Uhispania

Kwa mintarafu ya watu ambao hujipendekeza, nilidhani kuwa walikua wazuri sana kabla ya kumwamini Mungu. Walikuwa na tabia za upole, hawakuwahi kubishana na mtu yeyote, kila mtu aliwapenda, na hawakuwahi kumkosea mtu yeyote. Nilitamani kuwa mtu wa aina hii. Ni kwa sababu tangu nilipokuwa mchanga, nilikuwa nimejazwa kupitia elimu yangu na jamii na vitu kama “Upatanifu ni kitu cha thamani, uvumilivu ni wema,” “Hata ukiona mabaya, ni bora kusema machache,” na “Kaa kimya ili ujilinde na utafute tu kuepuka lawama.” “Usichukulie jambo lolote kwa uzito sana kamwe,” “Kutojua ni hekima wakati mwingine.” “Kufumbia macho tabia njema za rafiki wa maana hudumisha urafiki.” Ni “Kufumbia macho dosari za rafiki wa maana hufanya urafiki kuwa wa muda mrefu na mzuri.” Niliyachukulia mawazo haya kama maneno yangu ya kuishi kwa kuyazingatia. Haikujalisha iwapo ilikiwa familia na marafiki au watu niliowafahamu, sikumkosea mtu yeyote, na kila wakati nilikubaliana na yale ambayo wengine walitaka. Kila mtu alinisifu kwa kuwa mwema kwa watu na kwa kuwa rahisi kuelewana naye. Pia nilihisi kwamba ili kuendelea kuishi katika jamii hii ya giza na mbaya kulihitaji kuunda uhusiano mzuri na wale walio karibu na wewe, kwa sababu hiyo ndiyo njia pekee ya kujipatia nafasi yako mwenyewe. Ilikuwa baadaye tu, baada ya kupokea kazi ya Mwenyezi Mungu ya siku za mwisho, kupitia hukumu na kuadibu kwa maneno ya Mungu, na kuelewa ukweli kiasi ndipo mwishowe niliona kwamba kanuni hizi za kuishi ni falsafa za kishetani na sumu za Shetani, na si kanuni ambazo watu wanapaswa kushikilia. Niliona kwamba, nilipoishi kwa njia hii, nilizidi kuwa mpotovu, mdanganyifu, mbinafsi, na anayestahili dharau, kwamba niliishi tu kwa kudhihirisha tabia za kishetani, na sikuwa na mfano mzuri wa binadamu. Mwishowe nilianza kujichukia, na nikatubu kwa Mungu.

Mnamo 2018, nilichaguliwa kuwa kiongozi wa wilaya. Mwanzoni, sikujua mengi juu ya kazi yote ya kanisa. Mwenzangu, Dada Liu, alikuwa amefanya wajibu huu kwa zaidi ya mwaka mmoja, na alielewa vipengele mbalimbali vya kazi ya kanisa, kwa hivyo nilimuuliza juu ya matatizo yoyote au shida nilizokuwa nazo, na alinisaidia sana. Ashukuriwe Mungu! Baadaye, nilimsikia Dada Liu akitaja mara kadhaa kwamba kiongozi wa kanisa alilowajibikia, Dada Zhang, alikuwa tu akifanya wajibu wake kwa namna isiyo ya dhati, bila kufanya kazi ya vitendo, akihubiri mambo ya kawaida na mafundisho katika mikutano, na alikuwa mwenye kiburi, mwenye kujidai, na alikataa kukubali maoni au msaada wa wengine. Wakati huo, nilifikiri kuwa mambo haya yote huenda yalikuwa udhihirisho wa kiongozi wa uwongo ambaye hafanyi kazi ya vitendo, na kwa kuwa Dada Liu alijua juu ya hilo, nilijiuliza ni kwa nini hakufanya mabadiliko kiasi na kumwachisha kazi Dada Zhang. Nilitaka kumwambia kitu, lakini ilinijia mawazoni kwamba nilikuwa nimeanza tu kutekeleza wajibu huu na sikumjua Dada Zhang vizuri sana. Iwapo ningesema kitu moja kwa moja, huenda Dada Liu angenikosoa kwa kutokuwa na subira na kutowatendea wengine kwa upendo. Kwa kuzingatia hili, nilishiriki mawazo yangu na Dada Liu kwa njia isiyo ya moja kwa moja, lakini hakujali hilo sana na akaniomba nimsaidie Dada Zhang kwa upendo. Niliwaza, “Dada Liu hakika anajua kanuni za kuwabadilisha viongozi, kwa hivyo nikimtajia jambo hili tena, si atafikiri kuwa ninasema kuwa hafanyi kazi ya vitendo? Na hakika atafikiri mimi husababisha matatizo mengi na kwamba ni vigumu kuelewana nami. Jambo hili likisababisha ugomvi kati yetu, tutafanyaje wajibu wetu kama wenzi katika siku zijazo?” Wakati huo, niliamua kutosema chochote zaidi.

Nilifanya ushirika na Dada Zhang mara kadhaa ili kufichua na kuchambua matatizo yake. Mbali na kuyakataa, alibishana nami. Baadaye kidogo, ndugu wengine walianza kuripoti kwamba Dada Zhang hakuwa akifanya kazi ya vitendo. Wakati huo ndipo nilipogundua tatizo la Dada Zhang lilikuwa kubwa, na iwapo singelishughulikia mapema, lingechelewesha kazi ya kanisa na kuingia katika maisha kwa ndugu zetu. Kwa hivyo, niliibua suala la kumwachisha kazi Dada Zhang kwa Dada Liu tena. Lakini Dada Liu alisema, “Ripoti hizi zimekabidhiwa wakuu wetu. Hebu tusubiri hadi wabaini chanzo cha tatizo hili kabla ya kumwachisha kazi.” Niliwaza, “Kupitia ripoti hizi na kwa kuchunguza hali hii, tunaweza kuona kuwa Dada Zhang hajafanya kazi ya vitendo, amefanya wajibu wake kwa njia isiyo ya dhati, na amezungumza tu juu ya mambo ya kawaida na mafundisho kwa muda mrefu. Tayari tunajua kuwa yeye ni kiongozi wa uwongo, kwa hivyo kulingana na kanuni, anapaswa kuachishwa kazi haraka iwezekanavyo.” “Sisi ni viongozi wa wilaya, na kiongozi wa uwongo amejitokeza kanisani, lakini badala ya kushughulikia jambo hilo mara moja, tunalikabidhi wakuu wetu. Je, huku si kuchelewesha majibu na kumruhusu kiongozi wa uwongo aendelee kuwadhuru ndugu zetu? Huku ni kumuunga Shetani mkono na kwenda kinyume na Mungu kabisa!” Hili ni tatizo kubwa sana! Nilitaka kuzungumza juu ya hilo tena na Dada Liu, lakini nikafikiri, mara ya mwisho nilipomtajia hili, hakutaka kumbadilisha Dada Zhang, na aliniambia nimchukulie kwa upendo. Niliona kwamba walipatana vizuri sana, kwa hivyo iwapo ningeibua suala la kumwachisha wajibu Dada Zhang tena, huenda Dada Liu angesema kuwa nilikuwa na kiburi sana. Watu wapya kazini hulazimika kuthibitisha ushupavu wao, kwa hivyo angefikiri kuwa nilikuwa nikijionyesha tu? Niliamua kutosema chochote. Angalau wakuu wetu walikuwa wakichunguza na kuangalia ukweli. Siku chache zaidi hazingedhuru. Na kwa hivyo, nilijizuia, maneno yakiwa kwenye ncha ya ulimi wangu. Siku chache baadaye baada ya wakuu wetu kuchunguza suala hilo, walitushughulikia kwa ajili ya kutomshughulikia kiongozi wa uongo, wakisema kwamba tulikatiza na kuvuruga kazi ya kanisa na kuchelewesha kuingia kwa ndugu zetu katika maisha. Walisema kuwa huku kulikuwa kutenda kama washiriki wa Shetani na kuwadhuru ndugu zetu. Niliposikia haya, nilihisi mwenye taabu. Niligundua kuwa sikuwa nimetenda ukweli ambao niliujua waziwazi, na sikuwa nimetetea kanuni. Kwa kweli nilikuwa nimemlinda kiongozi wa uwongo. Nilikuwa nikimficha. Kwa hivyo, nilimwachisha wajibu bila kupoteza muda. Lakini baadaye, nilijilaumu na kukerwa kidogo, na sikuchukua fursa hiyo kutafakari zaidi kujihusu. Baadaye niligundua kuwa Dada Liu kila daima alinena maneno ya kawaida na mafundisho mikutanoni, na kwamba hakuweza kutatua matatizo na shida za kina ndugu. Nilipoonyesha matatizo na kasoro zake kiasi, alikataa kuzikubali, na akajaribu kubishana na kujadili nami. Hakuna kilichofanikishwa katika kazi aliyowajibikia, na wakuu wetu walipompogoa na kumshughulikia, alikataa kukubali hilo. Alianza kuwa hasi na mzembe katika kazi yake, akitatizwa na malalamiko na suitafahamu. Wakati huo, nilitaka kufichua hali yake, lakini nikagundua kuwa kama mwenzi wake, pia niliwajibika iwapo hatungefanya kazi yetu vizuri, na iwapo ningechambua matatizo yake, angesema kuwa sikuelewa hisia za wengine, kwa hivyo sikuthubutu. Badala yake, nilijaribu kumfariji na kumhimiza asiwe hasi. Lakini baada ya hapo, niligundua kuwa Dada Liu bado hakuwa amebadilika hata kidogo. Hakujitambua hata kidogo! Iwapo mambo yangeendelea hivi, hilo lingechelewesha tu kazi ya kanisa na kuwadhuru ndugu zetu. Niligundua kwamba nilihitaji kuripoti mambo haya kwa wakuu wetu haraka iwezekanavyo. Ilitukia kuwa kanisa hilo lilikuwa likifanya uchunguzi wa maoni ya jumla, na wakuu wetu waliniomba niandike tathmini ya Dada Liu. Nilikuwa nikijiandaa kuiandika, lakini nikakumbuka kuwa ndugu wengi walikosa utambuzi juu yake na walimuunga mkono kabisa. Kwa hivyo, kama ningethubutu kuripoti juu matatizo ya Dada Liu, je, wangesema kuwa nilikuwa nikipanga njama na nilimtaka aondolewe, ili niweze kuwa na kauli katika kila kitu? Zaidi ya hayo, tulikuwa washirika katika wajibu wetu, na alikuwa amefanya mengi ili kunisaidia. Iwapo kwa kweli angeondolewa, je, si angenichukia? Niliwaza na kuwazua, na mwishowe nikaamua kwamba ningeficha maelezo ya yeye kutofanya kazi ya vitendo au kukubali ukweli. Lakini baada ya kuwasilisha tathmini yangu, sikuweza kuzima wasiwasi uliokuwa moyoni mwangu. Nilijua kuwa nilikuwa nikificha ukweli na kumdanganya Mungu, na nilihisi giza zaidi la kiroho. Nilisinzia kila mara niliposoma maneno ya Mungu, na sikupata nuru au mwangaza kutoka kwa ushirika katika mikutano. Sikuweza kugundua matatizo yoyote ambayo ndugu walikuwa nayo. Nilitenda wajibu kwa njia isiyo ya dhati kila siku bila nguvu hata kidogo, na nilihisi kuwa Mungu alikuwa ameniacha.

Wakuu wetu walichunguza mambo baadaye, na Dada Liu aliachishwa kazi kama kiongozi wa uwongo ambaye hakufanya kazi ya vitendo. Nilihisi aibu kubwa na nilijilaumu wakati huo, hasa nilipofikiria maneno ya Mungu, “Wale wote ambao hushikilia furaha ya kati ndio waovu zaidi. Wao hujaribu kutomkosea yeyote, ni watu wa kuwafurahisha watu, wanafuata mambo, na hakuna mtu anayeweza kuwaelewa. Mtu kama huyo ni Shetani aliye hai!(“Ni kwa Kuweka Ukweli Katika Vitendo Tu Ndipo Unaweza Kutupa Minyororo ya Tabia Potovu” katika Kumbukumbu za Hotuba za Kristo). Maneno ya Mungu yanaonyesha kuwa watu wenye kujipendekeza ni waovu na wajanja zaidi, kwamba wao ni mashetani walio hai. Niligundua kwamba hivyo ndivyo nilivyokuwa. Nilikuwa nimejua kwa muda mrefu kuwa Dada Liu alikuwa kiongozi wa uwongo, lakini ili kulinda uhusiano wangu na yeye, nilichagua kumkosea Mungu badala yake na sikutenda ukweli. Nilikuwa nimemficha kiongozi wa uwongo tena, nikaikosea tabia ya Mungu, na kufanya dhambi. Nilihisi kuwa nilikuwa nimegonga mwamba, kwamba Mungu hangemwokoa mtu kama mimi. Niliishi kwa taabu na uhasi kwa siku chache. Nilipoteza shauku ya kufanya chochote. Lakini baadaye, nilikumbuka maneno ya Mungu: “Haijalishi umefanya makosa gani, haijalishi umepotoka aje ama vile ulivyotenda dhambi, usiwache haya yawe mizigo ama vikorokoro ziada kubeba katika ufuataji wako wa kumwelewa Mungu: Endelea kutembea mbele. Nyakati zote, Mungu hushikilia wokovu wa mwanadamu moyoni Mwake; hili halibadiliki kamwe. Hii ni sehemu ya thamani sana ya kiini cha Mungu(Neno, Vol. 2. Kuhusu Kumjua Mungu. Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee VI). Nilitafakari maneno haya ya Mungu tena na tena, na nilihisi kuwa kila neno na kila mstari viliniletea rehema na tumaini. Hata ingawa uovu wangu ulikuwa umeikosea tabia ya Mungu, Mungu bado alitumia maneno Yake kunifariji na kunitia moyo, na kuniambia niendelee kusonga mbele. Nilishukuru sana, na nikajiambia kwamba singekuwa hasi tena. Kila niliposhindwa, ilibidi nijiinue. Ninapaswa kuwa na uwezo wa kutafakari, kuelewa matatizo yangu, na kutafuta ukweli ili kuyatatua.

Baadaye nilisoma kifungu kingine cha maneno ya Mungu: “Wote wamesema kwamba wangeweza kuudhukuru mzigo wa Mungu na kutetea ushuhuda wa kanisa. Ni nani ambaye kweli amefikiri kwa makini kuhusu mzigo wa Mungu? Jiulize: Je, wewe ni mtu ambaye ameonyesha nadhari kwa mzigo wa Mungu? Je, unaweza kutenda haki kwa ajili ya Mungu? Je, unaweza kusimama na kuzungumza kwa ajili Yangu? Je, unaweza bila kusita kuweka ukweli katika vitendo? Je, wewe ni jasiri vya kutosha kupambana dhidi ya matendo yote ya Shetani? Je, unaweza kuwa na uwezo wa kuweka hisia zako kando na kufichua Shetani kwa sababu ya ukweli Wangu? Je, unaweza kuyaruhusu mapenzi Yangu yatimizwe ndani yako? Je, umejitolea moyo wako wakati muhimu unapowadia? Je, wewe ni mtu ambaye hufanya mapenzi Yangu? Jiulize na kufikiri juu yake mara kwa mara(Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Matamko ya Kristo Mwanzoni, Sura ya 13). Baada ya kusoma maneno ya Mungu na mahubiri hayo, nilihisi uchungu ambao uliuchoma moyo wangu. Niliona kwamba nilikuwa tu mlaghai na mtu awapendezaye watu. Nilipokabiliwa na suala fulani, nilifanya juu chini ili kujilinda na sikuyadhukuru masilahi ya nyumba ya Mungu, na sikutambua jukumu au mzigo uliokuwa katika wajibu wangu. Ningeshughulikia jambo hilo mara tu viongozi wa uwongo walipojitokeza, lakini badala yake, ili kujilinda na kwa ajili ya kuogopa kumkosea Dada Liu, niliogopa sana kutenda ukweli au kulifichua na kuripoti jambo hilo. Nilificha ukweli kwa makusudi, na nikauficha ili kumlinda. Matokeo yalikuwa kwamba kila kipengele cha kazi ya kanisa kiliathiriwa na ndugu zangu walikosa maisha ya kanisa yanayofaa. Niliwaza, nyumba ya Mungu ilinikabidhi wajibu muhimu sana, lakini viongozi wa uwongo walipojitokeza kanisani, nilisaliti kanuni za ukweli ili kulinda masilahi yangu mwenyewe, nikimuunga mkono Shetani tena na tena na kuwalinda. Nilijua vyema kwamba kazi ya kanisa ingeathirika, lakini sikutenda ukweli au kutetea haki. Wakati wowote ambapo kulikuwa na uwezekano wa kumkosea mtu, niliacha kanuni za ukweli. Nilikuwa nikitenda kwa ubinafsi, kwa ajili ya manufaa yangu mwenyewe. Je, si kufanya mambo kwa njia hii kulikuwa kukatiza na kuvuruga kazi ya nyumba ya Mungu na kutenda kama mshiriki wa Shetani? Sikuweza kuthubutu kutenda ukweli au kuzitetea kanuni. Sikuwa mwenye haki hata kidogo. Nilistahili vipi kuwa kiongozi wa kanisa? Nilikuwa mbinafsi, mwenye kustahili dharau, mlanghai, mdanganyifu, na mwenye kujishughulisha na mambo madogo madogo! Nilisononeka sana nilipofikiria kwamba maneno ya Mungu yanasema Mungu huwachukia na kuwadharau watu wenye kujipendekeza, na hawaokoi, na mahubiri yanasema mara kwa mara kwamba nyumba ya Mungu inakataa kabisa kuwakubali watu wenye kujipendekeza wawe viongozi, kwa sababu wana mioyo yenye uovu, na wanaweza tu kuidhuru nyumba ya Mungu na ndugu zao. Kwa kuwalinda na kuwaficha viongozi wa uwongo, nilikuwa tayari nimemkosea Mungu na kuikosea tabia Yake, kwa hivyo nilienda mbele za Mungu na nikamwomba: “Mungu, nimekiuka mapenzi Yako mara kwa mara. Nilijua ukweli waziwazi lakini sikuutenda, na nikaidhuru kazi ya kanisa wakati huo. Niko tayari kukubali laana na adhabu Yako. Bila kujali Utakavyonitendea katika siku zijazo, niko tayari kutii na kutubu Kwako.”

Baada ya kuomba, nilianza kujiuliza ni kwa nini nilijaribu kuwapendeza watu na sikuweza kutenda ukweli mambo yaliponitokea. Ni nini kilichokuwa kikinitawala? Baadaye nilisoma kifungu cha maneno ya Mungu: “Shetani huwapotosha watu kwa kupitia masomo na ushawishi wa serikali za kitaifa na walio mashuhuri na wakuu. Upuuzi wao umekuwa uzima wa mwanadamu na asili. ‘Kila mtu kivyake na ibilisi achukue ya nyuma kabisa’ ni msemo wa kishetani unaojulikana sana ambao umeingizwa ndani ya kila mtu na umekuwa maisha ya watu. Kuna maneno mengine ya falsafa ya kuishi ambayo pia ni kama haya. Shetani hutumia utamaduni mzuri wa kila taifa kuwaelimisha watu, akisababisha wanadamu kuanguka ndani na kumezwa na lindi kuu lisilo na mipaka la uharibifu, na mwishowe watu wanaangamizwa na Mungu kwa sababu wanamtumikia Shetani na kumpinga Mungu. … Bado kuna sumu nyingi za kishetani maishani mwa watu, katika mienendo yao na shughuli zao na wengine; hawana ukweli wowote hata kidogo. Kwa mfano, falsafa zao za kuishi, njia zao za kufanya vitu, na kanuni zao zote zimejazwa sumu za joka kuu jekundu, na zote zinatoka kwa Shetani. Hivyo, vitu vyote vinavyopita katika mifupa na damu ya watu ni vitu vyote vya Shetani. Wale maafisa wote, wale wanaoshikilia mamlaka, na wale waliofaulu wana njia zao na siri za kufaulu. Je, si siri kama hizo ni uwakilishi mzuri zaidi wa asili yao? … Wanadamu wamepotoshwa kwa kina zaidi na Shetani. Sumu ya Shetani inabubujika kwa damu ya kila mtu, na inaweza kuonekana kwamba asili ya mwanadamu imepotoka, ni yenye uovu, na ya kupinga maendeleo, ikijawa na kuzamishwa katika falsafa za Shetani—kwa jumla ni asili inayomsaliti Mungu. Hii ndiyo maana watu humkataa Mungu na humpinga Mungu(“Jinsi ya Kujua Asili ya Mwanadamu” katika Kumbukumbu za Hotuba za Kristo). Baada ya kusoma neno la Mungu, nilipata chanzo kilichosababisha nitende kama mtu mwenye kujipendekeza. Ni kwa sababu tangu nilipokuwa mchanga, nilikuwa nimeelimishwa na CCP, na nilijazwa kila aina ya falsafa, mantiki, na sheria za dunia, kama vile “Mbingu huwaangamiza wale ambao hawajiwakilishi,” “Wanadamu si watakatifu, wanawezaje kukosa dosari?” “Ingawa unaona mabaya, ni bora kusema machache,” na pia “Kaa kimya ili kujilinda na utafute tu kuepuka lawama,” “Kufumbia macho dosari za rafiki wa maana hufanya urafiki kuwa wa muda mrefu na mzuri,” na kadhalika. Mambo haya yaliwekwa ndani kabisa ya moyo wangu, na niliishi kulingana nayo. Nilizidi kuwa mwenye kiburi, mwenye kujidai, mbinafsi, mwenye kustahili dharau, mlaghai, na mdanganyifu kila wakati. Nilifanya mambo haya yawe wito wa maisha yangu. Katika kupatana na watu nilichunguza kwa uangalifu kila neno na usemi wa wengine, na nilichukulia uhusiano wangu na kila mtu kwa makini sana. Nilikuwa mtu mwenye kujipendekeza, nilitembea kwenye njia ya hali duni, sikumkosea mtu yeyote, sikuthubutu kusema ukweli au kutetea haki, na niliishi bila hadhi hata kidogo. Viongozi wa uwongo walipojitokeza kanisani, kwa kuwa niliogopa kumkasirisha Dada Liu, niliacha kanuni zangu, nikachagua kuwa mwoga, na niliwaruhusu wawadhuru ndugu zangu na kuzuia kazi ya nyumba ya Mungu. Ningewezaje kujiita mtu mzuri? Nilikuwa na moyo mwovu, “mtu mzuri,” mtumwa wa Shetani anayestahili dharau. Sikuwa na ujasiri au haki. Ningalimchunguza na kumsaidia Dada Liu mapema, labda asingalifanya makosa mengi sana, kazi ya nyumba ya Mungu na kuingia katika maisha kwa ndugu labda kusingalizuiwa, na labda singalikosea tabia ya Mungu. Hivyo basi, mwishowe niliona kwamba kuishi kulingana na hizi falsafa za dunia za kishetani na kuwa mtu mwenye kujipendekeza kungewadhuru tu watu au kuwaangamiza, na kunifanyia vivyo hivyo. Kutokana na kilichofichuliwa na ukweli niliweza kuona hatimaye kwamba falsafa, mantiki, na sheria hizi za kishetani za dunia zinaweza tu kuwadanganya na kuwapotosha watu. Ni adui wa maneno ya Mungu na ukweli. Tunapoishi kulingana na falsafa hizi za kishetani, bila kujali tunaoneka kuwa wema, wapole, au wazuri jinsi gani, bado sisi tu walaghai, wadanganyifu, wenye kuleta hizaya, na tunasikitisha. Tusipotenda ukweli, kutubu, na kubadilika, bila shaka tutatelekezwa na kuondolewa na Mungu.

Baadaye nilisoma kifungu kingine cha neno la Mungu: “Mungu ana kiini cha uaminifu, na kwa hivyo neno Lake siku zote linaweza kuaminika. Aidha, matendo Yake hayana dosari wala hayajadiliwi. Hii ndiyo maana Mungu anawapenda wale walio waaminifu kabisa Kwake(Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Maonyo Matatu). “Kwamba Mungu huwataka watu wawe waaminifu inadhibitisha kwamba kwa kweli Anachukia wale ambao ni wadanganyifu, na kwamba Hawapendi watu wadanganyifu. Kwamba Mungu hawapendi watu wadanganyifu kunamaanisha kwamba Anachukia matendo, tabia na hata motisha zao; yaani, Yeye hapendi vile wanavyofanya vitu. Hivyo, ili kumfurahisha Mungu, lazima kwanza tubadili matendo yetu na jinsi tunavyoishi(“Vitendo vya Msingi Kabisa vya Kuwa Mtu Mwaminifu” katika Kumbukumbu za Hotuba za Kristo). “Punde unapoamini na kuwa na amini, unapokuja mbele ya Mungu lakini bado unaishi katika njia hiyo hiyo ya zamani, je, imani yako katika Mungu ni ya maana? Je, ni ya thamani? Malengo na kanuni za maisha yako na jinsi unavyoishi havijabadilika, na kitu cha pekee ambacho kinakuweka juu ya wasioamini ni kumkubali kwako Mungu. Unaonekana kuwa unamfuata Mungu, lakini tabia yako ya maisha bado haijabadilika hata kidogo. Mwishowe, hutaokolewa. Hali ikiwa hivyo, je, hii si imani tupu na furaha tupu?(“Ni kwa Kuweka Ukweli Katika Vitendo Tu Ndipo Unaweza Kutupa Minyororo ya Tabia Potovu” katika Kumbukumbu za Hotuba za Kristo). Baada ya kusoma neno la Mungu, niliona kwamba Mungu ni mwaminifu kimsingi. Mungu huwapenda watu waaminifu na kuwachukia wadanganyifu. Nilipoishi kulingana na falsafa hizi za kishetani, mtazamo wangu juu ya mambo na jinsi nilivyotenda hayakubadilika hata kidogo. Nilikuwa tu kama watu wasiomwamini Mungu. Bila kujali ningemwamini Mungu kwa njia hiyo kwa miaka mingapi, kamwe singepata ukweli au wokovu kamili. Ni wale tu wanaotenda ukweli, ambao ni watu waaminifu, ambao hawana udanganyifu katika mioyo yao, ambao wana ujasiri wa kufuata kanuni za ukweli, ambao wana haki, na wanaosimama upande wa Mungu katika vitu vyote na wanaojali mapenzi ya Mungu ndio Anaowapenda, na ndio wanaoweza kuokolewa na Yeye kikamilifu! Baada ya kuelewa anachohitaji Mungu, nilimwomba Mungu na kula kiapo kwamba ningetubu, ningetenda ukweli, na kuwa mtu mwaminifu.

Miezi michache baadaye, niligundua kuwa mwenzi wangu mpya Ndugu Li daima alizungumza mambo ya kawaida na mafundisho, na alijionyesha mikutanoni. Nilifanya ushirika naye kuhusu hilo mara kadhaa, lakini sikuona maendeleo yoyote, kwa hivyo niliwaambia wakubwa wetu kuhusu hilo. Lakini baadaye, waliniomba nichambue na kufichua tabia zake, na nikaanza kuhisi hofu. Nilichanganyikiwa kuhusiana na mambo haya, kwa sababu Ndugu Li alikuwa akitekeleza wajibu wake kule kwa muda mrefu zaidi kuliko mtu yeyote mwingine. Alionekana kama mzee, na alikuwa amenisaidia katika kazi yangu hapo zamani. Kama ningefichua hali yake, angefikiri vipi kunihusu? Je, angekasirika? Kisha, nikasoma kifungu hiki cha maneno ya Mungu: “Ikiwa una nia na mtazamo wa ‘mtu mzuri,’ kila wakati utaanguka chini na utashindwa katika mambo kama haya. Kwa hivyo basi, unapaswa kufanya nini katika hali kama hizi? Unapokabiliwa na vitu kama hivyo, lazima uombe kwa Mungu. Mwombe akupe nguvu na akuwezeshe ufuate kanuni, ufanye kile ambacho unapaswa kufanya, ushughulikie vitu kulingana na kanuni, uwe imara, na azuie madhara yoyote yafikie kazi ya nyumba ya Mungu. Ikiwa unaweza kutelekeza masilahi yako binafsi, hadhi, na mtazamo wa ‘mtu mzuri,’ na ukifanya kile unachopaswa kufanya kwa moyo mwaminifu, na kamili, basi utakuwa umemshinda Shetani, na utakuwa umepata kipengele hiki cha ukweli(“Ni Wakati Unapojijua Tu Ndipo Unaweza Kufuatilia Ukweli” katika Kumbukumbu za Hotuba za Kristo). Kusoma kifungu hiki cha neno la Mungu kulinipa ubayana wa ndani kwamba hili lilikuwa limenijia kwa sababu Mungu alikuwa Akinijaribu na kunipa nafasi ya kutubu. Mungu alitaka nione jinsi ambavyo ningeshughulikia suala hilo. Sikuweza kujiruhusu kulinda uhusiano wangu na wengine kama hapo awali. Nililazimika kuipa kipaumbele kazi ya kanisa, kutenda ukweli, na kudumisha haki. Kama Ndugu Li angekuwa mtu aliyefuatilia ukweli, angetumia ushirika na uchambuzi kutafakari juu yake mwenyewe na kujielewa, jambo ambalo lingesaidia kuingia kwake katika maisha, na kisha kuepuka kufanya dhambi nyingi zaidi. Na kwa hivyo, nilienda kumuona Ndugu Li, na nikafunua na kuchambua hali zake na tabia yake moja moja kwa kutumia maneno ya Mungu. Kilichonishangaza ni kwamba mbali na kutonichukia, alisema kwa kutubu, “Usingenifichua na kunihakiki kwa njia hii, nisingejua kuhusu matatizo yangu. Kwa kweli nahitaji kutafakari na kupata kuingia.” Kumsikia Ndugu Li akisema maneno hayo kulinigusa sana. Nilikuwa na wasiwasi kuwa kumfichua kungemfanya anichukie, lakini hayo yalikuwa mawazo yangu tu. Wakati huo, niliona kwa kweli kwamba kutenda ukweli na kuwa mtu mwaminifu huleta utulivu na amani ya mawazo, na hutuleta karibu zaidi na Mungu. Niliona pia kwa kweli kwamba njia pekee ya kulinda kazi ya nyumba ya Mungu ni kutenda ukweli na kushughulikia mambo kulingana na kanuni. Hii ndiyo njia ya pekee ya kuwasaidia ndugu zetu kwa kweli.

Kupitia hukumu na kuadibu kwa Mungu, maoni yangu mengine yenye makosa yalibadilishwa, na tabia yangu ya kishetani ya ulaghai, ujanja, ubinafsi, na ya kustahili dharau ilibadilishwa kidogo. Sasa, ninapoona ndugu zangu wakionyesha upotovu, au mambo yanaposhughulikiwa kwa njia zinazosaliti kanuni za ukweli, siwafichi, siwalindi, au kujaribu kulinda uhusiano wangu na watu tena. Naweza kutenda ukweli, kufanya ushirika, kusaidia, kuonyesha mambo, na kufichua mambo kwa makini. Hata ingawa wakati mwingine bado mimi husita na ninaogopa kuwakosea wengine, ninaweza kumwomba Mungu, kujinyima, kutenda kulingana na kanuni za ukweli, na kutoishi tena kulingana na falsafa za kishetani. Nikiwa na utendaji wa aina hii, nahisi utulivu na uthabiti zaidi. Ni jambo linalokomboa kabisa. Kutimiza mabadiliko haya na kupata haya yote kulikuwa tu matokeo ya hukumu na kuadibu kwa maneno ya Mungu.

Iliyotangulia: 45. Kuishi Mbele za Mungu

Inayofuata: 53. Kulegeza Uhusiano Unaowafunga Watu Pamoja

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Maudhui Yanayohusiana

13. Ukombozi wa Moyo

Na Zheng Xin, MarekaniMnamo Oktoba ya 2016, mimi na mume wangu tulikubali kazi ya Mungu katika siku za mwisho wakati tulikuwa ughaibuni....

2. Katikati ya Jaribu la Kifo

Na Xingdao, Korea ya KusiniMwenyezi Mungu anasema, “Mungu amekuja kufanya kazi ulimwenguni ili kumwokoa mwanadamu aliyepotoka—hakuna uongo...

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp