212 Toba ya Dhati

1

Katika usiku usio na usingizi kumbukumbu nyingi zaja akilini.

Kwa miaka mingi sana ya kumwamini Bwana, bado nilifuata mwenendo wa ulimwengu.

Nilisamehewa dhambi zangu, lakini bado nilikubali kutawaliwa na tamaa za mwili.

Nilidhani kwamba ningetia bidii, singekataliwa na Bwana.

Nilisikia sauti ya Mungu, na kutambua kuwa Bwana alikuwa ameonekana.

Na kwa hivyo nilifikiria kwamba ningeinuliwa mbele za Mungu na kuwa na sehemu yangu katika ufalme wa mbinguni.

Kamwe sikukubali hukumu na kufunuliwa kwa maneno ya Mungu na kutafakari kujihusu.

Nilifuata matamanio yangu na kutenda kwa makusudi, nikachukulia maneno ya Mungu kwa bezo.

Niliposhiriki juu ya maneno ya Mungu nilizungumza tu kuhusu mafundisho na kuhusu kuwa nilifanya vizuri.

Nilipopogolewa na kushughulikiwa nilipinga na kutoa udhuru.

Nilipokabiliwa na majaribio, nilitaka daima kukimbia; sikujua wokovu wa Mungu.

Sasa, naona kwamba sikufuatilia ukweli hata kidogo.

Nimepotea mbali toka kwa maneno ya Mungu, nimeingia katika giza lisilo na mipaka.

Nikishindwa kuhisi uwepo wa Mungu, kuna hofu na wasiwasi moyoni mwangu.

Nikihofu na kutetemeka, napiga magoti mbele ya Mungu, nikiogopa kumpoteza.

Nilisoma maneno ya Mungu na kumwomba Mungu, nikitamani kubadilika kwa msimamo Wake.

2

Ee Mungu! Unaweza kuusikia moyo wangu ukilia kwa toba?

Kupoteza uwepo Wako ni giza na chungu kama nini!

Hakuna nuru bila maneno Yako moyoni mwangu.

Naishi ndani ya tabia potovu na Shetani hunichezeachezea.

Ee Mungu! Natamani kutubu, kuanza upya.

Ningependa Unihukumu na kuniadibu zaidi.

Hata majaribio na usafishaji mkali zaidi vikija,

almradi naweza kuishi mbele Yako naweza kuvumilia chochote.

Nimepotoshwa sana, siwezi kutakaswa bila hukumu Yako.

Hukumu tu ndiyo inayoweza kuniokoa kutoka kwa Shetani.

Ee Mungu ! Nimeonja kwamba hukumu na kuadibu ni upendo.

Maneno yako ni ukweli, njia na uzima.

Nitafuata nyayo Zako kwa makini hadi mwisho.

Bila kujali jinsi barabara iliyo mbele ilivyo na milima na mabonde,

naamua kukufuata na kukutumikia kwa uthabiti siku zangu zote!

Iliyotangulia: 211 Kuna Maumivu Ndani ya Moyo Wangu

Inayofuata: 213 Kufanya Upya Kiapo Changu cha Kumpenda Mungu

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Maudhui Yanayohusiana

418 Umuhumi wa Maombi

Sala ni mojawapo ya njia ambazo mwanadamu hutumia kushirikiana na Mungu, ni njia ambayo mwanadamu hutumia kumwita Mungu, na ni mchakato...

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp