213 Kufanya Upya Kiapo Changu cha Kumpenda Mungu

1

Nikishikilia maneno ya Mungu kwa mikono yote miwili, hisia zangu za majuto ni ngumu kuzungumzia.

Neno la Mungu ni ukweli, nachukia kwamba sikulifuatilia kwa dhati.

Niliwahi kuapa na kuahidi, nikisema moyo wangu umpendao Mungu hautawahi kubadilika.

Nilikuwa mjinga na mpumbavu, sikujua, na mambo hayakuwa kama nilivyofikiria.

Majaribu yalipofika, nilikufa moyo na kuelewa vibaya, nilishikilia mawazo ya mustakabali na majaliwa yangu.

Shauku yangu ya zamani ilipeperushwa na upepo, nikakata tamaa na kupoteza tumaini, na nikakubali kufa moyo.

Kwa kuona sura yangu mwenyewe dhoofu,

macho yangu yaliyokata tamaa, uso wangu usiofarijika,

ningewezaje kuanguka hivi?

2

Kwa kujilinganisha dhidi ya maneno ya Mungu na kujitafakari, moyo wangu hatimaye unatambua ukweli.

Nilisema nampenda Mungu lakini sikuutoa moyo wangu wa kweli Kwake, lakini badala yake nilifanya maafikiano na Mungu kila wakati.

Bila kujiondolea motisha ya kupata baraka, ningewezaje kujitolea moyo wangu kwa Mungu?

Niliona jinsi nilivypotoshwa sana, bila dhamiri au mantiki.

Sasa kiapo changu kimekuwa uwongo, alama ya aibu.

Nina aibu sana kuona uso wa Mungu na najichukia kwa kuumiza moyo wa Mungu.

Nimebaki na hatia na majuto ya milele.

Kumbukumbu nzito zimejificha, ziko kwa kina moyoni mwangu.

Natamani sana kuweza kufuta deni langu.

3

Mungu analipa gharama kamili kuonyesha ukweli ili kumruzuku mwanadamu.

Hukumu, kuadibu, majaribu na kufunua—Mungu afanya haya yote kumsafisha na kumwokoa mwanadamu tu.

Hajawahi kuuliza chochote kama malipo, Anatamani kuipata mioyo yetu.

Kwa kuona jinsi ninavyosikitisha, moyo wangu unawaka kwa wasiwasi.

Upendo safi na kamili wa Mungu unaupa joto moyo wangu.

Ikiwa singefuatilia ukweli bado, ningeona aibu kupokea upendo Wake.

Nawezaje kumwuliza Mungu aendelee kuningojea?

Nafanya upya kiapo changu cha kumpenda Mungu: Nautoa moyo na akili yangu Kwake,

nami nitakamilisha misheni yangu na kumshuhudia Mungu.

Iliyotangulia: 212 Toba ya Dhati

Inayofuata: 214 Ni Bahati Yetu Nzuri Kumhudumia Mungu

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Maudhui Yanayohusiana

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp