Programu ya Kanisa la Mwenyezi Mungu

Sikiliza sauti ya Mungu na ukaribishe kurudi kwa Bwana Yesu!

Tunawakaribisha wote wanaotafuta ukweli wawasiliane nasi.

Mfuateni Mwanakondoo na Kuimba Nyimbo Mpya

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

(Ma)tokeo ya Kutafuta 0

Hakuna matokeo yaliyopatikana

Kuna Maumivu Ndani ya Moyo Wangu

1

Kuna maumivu ndani kabisa ya moyo wangu. Kila ninapofikiria kuhusu zamani ni kama kisu kilipinda moyoni mwangu.

Wakati mmoja nilimpinga na kumkufuru Kristo. Nilimwamini Mungu lakini sikumjua, na nikampinga.

Nilimshuhudia Kristo akionyesha ukweli lakini bado nilimkana, mimi si tofauti na Mafarisayo.

Sitasahau kamwe somo hili lililoandikwa kwa damu. Nimeachwa na toba na majuto ya milele.

2

Nilimwamini Bwana kwa miaka mingi lakini sikufuatilia ukweli. Nilijizatiti kwa maarifa ya kibiblia ili kuringa.

Nilizungumza juu ya nadharia za teolojia ili kuwafanya wengine waniabudu na kuniheshimu. Nilijitahidi kwa ajili ya baraka na thawabu.

Nilikuwa mbinafsi na mwovu, bila kujali kamwe mapenzi ya Mungu. Nilipiga kelele nyingi juu ya kumpendeza Mungu lakini sikutenda ukweli.

Niliapa kuwa mwaminifu kwa Mungu kwa maneno lakini sikutekeleza wajibu wangu. Nilikuwa mcha Mungu kwa nje lakini sikumtii Mungu.

3

Hukumu na kuadibu kwa Mungu vinanifanya nisujudu. Natetemeka kwa hofu ninapoona tabia ya Mungu ya haki.

Nachukia upotovu wangu wa kina na ukatili. Nimetenda dhambi nyingi sana na nimeuvunja moyo wa Mungu.

Kwa yote niliyoyafanya ningeangamizwa na Mungu muda mrefu uliopita. Lakini Mungu ni mvumilivu na mstahimilivu kwangu, Akanipa nafasi ya kutubu.

Kuona wokovu wa Mungu kunaujaza moyo wangu majuto. Nimeamua kutenda ukweli na kuishi kwa kudhihirisha mfano wa binadamu.

Niko tayari kutumia maisha yangu kwa ajili ya Mungu na kulipa mapenzi ya Mungu. Nitamtii Mungu na kumwabudu Mungu milele.

Iliyotangulia:Upendo wa Kweli wa Mungu

Inayofuata:Tambua Kuwa Kristo Ni Ukweli Milele

Maudhui Yanayohusiana