20. Kwa Nini Nimetembea Njia ya Mafarisayo

Suxing Mkoa wa Shanxi

Mimi ni mtu mwenye kiburi na majivuno, na cheo kimekuwa udhaifu wangu. Kwa miaka mingi katika imani yangu, nimefungwa na sifa na cheo na sijaweza kujiweka huru kutoka kwazo. Mara kwa mara nimepandishwa cheo na kubadilishwa na mtu mwingine; nimekuwa na vizuizi vingi katika cheo changu na nimekumbwa na matuta mengi njiani. Baada ya miaka mingi ya kushughulikiwa na kusafishwa, nilihisi kwamba sikuwa nachukulia cheo changu kwa uzito. Sikutaka kuwa kama nilivyokuwa katika nyakati zilizopita nikifikiri kwamba mradi nilikuwa kiongozi ningeweza kukamilishwa na Mungu na kwamba iwapo sikuwa kiongozi, basi sikuwa na matumaini. Nilielewa kwamba pasipo kujali jukumu ambalo nilikuwa natimiza, nilihitaji tu kutafuta ukweli na ningefanywa kamili na Mungu; kufuatilia sifa na cheo ni njia ya yule anayempinga Kristo. Sasa ninahisi kwamba pasipo kujali jukumu ambalo ninatimiza, naweza kubali kutokuwa na cheo. Ni sheria ya mbingu na dunia kwamba uumbaji utimize wajibu wake. Haijalishi pale unapowekwa, unapaswa kukubali mipango ya Mungu. Wakati upotovu wa umaarufu na cheo unafichuliwa, unaweza kutatuliwa kwa kuutafuta ukweli. Haijalishi ninachokabiliwa nacho wakati ninatimiza wajibu wangu, mradi ninauelewa ukweli nitakuwa tayari kulipia gharama. Kwa kuzingatia haya, nilifikiri kuwa nilikuwa tayari nimetembea njia ya kutafuta ukweli. Nilifikiri kwamba nimepata tena utu na mantiki. Mungu hupekua moyo na kuchunguza akili. Alijua kwamba nilikuwa mwenye najisi katika kutafuta kwangu ukweli, na kwamba sikuwa kweli natembea njia ya kuutafuta ukweli. Mungu alijua mbinu ya kutumia ili kunitakasa na kuniokoa.

Mwishoni mwa Juni mwaka wa 2013, kiongozi wa hapa alibadilishwa. Baadaye, ndugu walinichagua kuwa kiongozi mpya. Familia ya Mungu iliniruhusu kuinuka na kufanya kazi hiyo. Niliposikia kwamba ningekuwa nachukua jukumu kubwa kama hilo, nilihisi kwamba sikuwa na uhalisi wa ukweli na kwamba singeweza kuitenda kazi hiyo. Mawanda yalikuwa makubwa sana na kulikuwa na ndugu wengi sana. Ningewezaje kuwaongoza? Kulikuwa na watu wengi mno ambao walikuwa na sifa nyingi zaidi za ndani kuliko nilizokuwa nazo ambao walibadilishwa. Ningewezaje kutenda vyema zaidi? Si hili litanifichua? Sikuwa tayari kupitia milima na mabonde. Mradi ningeweza kutimiza wajibu wangu, ningetenda kile niwezacho popote ambapo kazi ingehitaji. Kwa hivyo, nilikataa papo hapo: “La, sina ustadi wa kufanya kazi hii. ...” Nilitoa aina zote za sababu na visingizio. Niliamini kikamilifu kwamba nilikuwa na urazini katika kufanya hili na kwamba ulikuwa ukweli. Baadaye, niliweza kutambua kupitia ushirika wa ndugu zangu kwamba nilikuwa nimeshikilia sumu ya lile joka kuu jekundu ndani yangu; yaani, “Kadiri walivyo wakubwa, ndiyo wanavyoanguka kwa kishindo zaidi” na “Kuna upweke sana kwenye upeo.” Sikutaka kusumbuliwa na cheo tena. Hata ingawa kwa kuwaza nilijua kwamba sababu ya watu hao kutolewa ilikuwa kwamba hawakutafuta ukweli na asili zao zilikuwa ovu sana na walitenda aina zote za maovu; hata hivyo, akilini mwangu niliamini kwamba nisingekuwa kiongozi mzuri kabisa, basi hakungekuwa na nafasi ya kutenda uovu; ilikuwa kinga kwangu. Kisha nilifikiri kwamba kwa sababu ya imani yangu ya sasa na kuhubiri injili, nilikuwa nawindwa na CCP na singeweza kurudi nyumbani. Sikuwa na suluhisho. Iwapo ningebadilika kuwa kiongozi mkubwa, na mwishowe nikosee tabia ya Mungu na nifukuzwe kwa sababu sikuwa na ukweli, basi kwa kweli singekuwa na uwezo wa kuendelea kuishi. Kwa sababu nilikuwa nimefungwa na fikira na sumu hizi, niliishi kwa giza na mateso. Katika uchungu wangu nililazimishwa kumlilia Mungu: “Ee Mungu, katika kukabiliana na jukumu hili, najua kwamba Umenipandisha cheo. Najua kwamba kukataa jukumu hili ni kumsaliti Mungu. Lakini sasa hivi ninaishi nikiwa nimefungwa na sumu ya Shetani na siwezi kujitoa kwayo. Naogopa sana kuchukua jukumu hili kubwa, naogopa kwamba asili yangu ni hatari, kwamba sina ukweli na kwamba nitaadhibiwa kwa kutenda ovu kubwa. Ee Mungu, nina uchungu na nimekanganyiwa sana. Sijui jinsi ya kumtii Mungu. Ninakuomba Ewe Mungu unisaidie na kuniokoa.” Wakati wa maombi, Mungu alinipa nuru kufikiria kuhusu kifungu cha maneno ya Mungu: “Na ufahamu wenu kunihusu hauko kwa kutoelewa kama huku tu; mbaya hata zaidi ni kukufuru kwenu Roho wa Mungu na kuitukana Mbingu. Hii ndiyo maana Ninasema kwamba imani kama yenu itawasababisha tu kupotea mbali na Mimi na kukuwa na upinzani mkubwa dhidi Yangu. Kwa miaka mingi ya kazi, mmeona ukweli mwingi, lakini mnajua kile masikio Yangu yamesikia? Ni wangapi kati yenu walio tayari kukubali ukweli? Nyote mnaamini kwamba mko tayari kulipa gharama ya ukweli, lakini ni wangapi walioteseka kweli kwa ajili ya ukweli? Yote yaliyo ndani ya mioyo yenu ni uovu, na hivyo mnaamini kwamba yeyote, bila kujali ni nani, ni mjanja na asiye mwaminifu(Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Jinsi ya Kumjua Mungu Duniani). Maneno ya hukumu ya Mungu yalibadilisha kukanganyikiwa kwangu na uchungu kuwa hofu na mashaka mengi. Hasa, “kukufuru kwenu Roho wa Mungu na kuitukana Mbingu,” na “Yote yaliyo ndani ya mioyo yenu ni uovu,” maneno haya yalikuwa kama upanga unaodunga moyo wangu, kunifanya nihisi haki, uadhama na ghadhabu ya tabia ya Mungu Niliona kwamba hali yangu ya sasa ilikuwa inampinga Mungu kweli na kumkufuru Mungu na kwamba ilikuwa ya kuhuzunisha mno! Kwa sababu ya hili moyo wangu wa uasi uliweza kubadilika na nilinyenyekea mbele ya Mungu ili kutafuta kumtii Yeye. Nilichunguza kile kilichokuwa kumefichuliwa kunihusu. Sijui ni mara ngapi nilikuwa nimepitia hukumu na kuadibu kwa Mungu kwa miaka iliyopita, lakini sikujua upendo na wokovu wa Mungu tu, kwa kweli nilimwelewa visivyo na kujikinga kutokana naye, hivyo kuifanya hali iwe mbaya zaidi. Nilimlaumu Mungu kwa kila kitu kilichokuwa si chenye haki kana kwamba kazi ya Mungu ilikuwa ya kuchosha sana kwa mwanadamu. Baada ya miaka mingi ya kupitia kazi ya Mungu, uhusiano wangu na Mungu haukuwa umekuwa wa karibu zaidi wala wa kawaida; bali, nilikuwa ninatenganishwa na Mungu zaidi na mbali naye. Kulikuwa na shimo kubwa baina yangu na Mungu ambalo singeweza kuvuka. Je, hili ndilo nimevuna baada miaka hii yote? Wakati huu, niliweza kugundua kwamba asili yangu choyo na ya kusikitikia ilikuwa inanipeleka kusaliti dhamiri yangu. Nilikuwa nimesahau gharama aliyolipa Mungu kwa ajili yangu; nilikuwa nimesahau wokovu Wake na ukuzaji Wake kwangu. Wakati huu, nilimwomba Mungu tena: “Ee Mungu, sitaishi kwa sumu ya Shetani tena, sitaumiza moyo Wako tena. Niko tayari kukubali hukumu na adabu ya Mungu, na kugeuka kutoka kwa mitazamo yangu iliyokosea.” Kwa hivyo nilisoma mahubiri yaliyotolewa Juni 15, 2013 kutoka kwa wale wa juu: “Kila asiyempenda Mungu yuko kwenye njia ya anayempinga Kristo na mwishowe atawekwa wazi na kuondoshwa. Kazi ya Mungu ya siku za mwisho ni kuwaokoa na kuwafanya kamili watu na kila mtu mwovu ambaye hajaokoka atawekwa wazi na kuondoshwa. Kwa hivyo, kila mtu atafuata aina yake mwenyewe. Mbona watu wengi sana wanawekwa wazi wakitenda maovu ya kila aina na vyeo vyao na mamlaka yao? Sio kwa sababu cheo chao kinawaumiza. Shida ya kimsingi ni kiini cha asili ya mwanadamu. Cheo hakika kinaweza kuwaweka watu wazi, lakini iwapo mtu mwema ana cheo cha juu, hatatenda maovu mbalimbali. Watu wengine hawatatenda maovu kama hawana cheo, wanaonekana kuwa watu wa zuri kwa juu, lakini mara wakipata cheo watatenda aina zote za maovu” (“Lazima Mpitie na Kuingia Katika Uhalisi wa Ukweli wa Neno la Mungu Ili Kupata Ukamilisho wa Mungu” katika Mkusanyiko wa Mahubiri—Ruzuku ya Maisha). Kupitia ushirika huu, niliweza kuona jinsi dhamiri zilizokuwa moyoni mwangu zilikuwa za kipumbavu na bila maana. Iwapo watu wote wanaweza kutembea katika njia ya kutafuta ukweli au la haina msingi kwa ikiwa wana cheo au la, na sio kwamba kuwa na cheo kunaifanya iwe vigumu kutembea kwenye njia ya kutafuta ukweli. Cha muhimu ni iwapo asili ya mwanadamu inapenda ukweli au la na iwapo mwanadamu anampenda Mungu au la. Nilifikiri kwamba kupitia kwa miaka yangu mingi ya “kujiimarisha,” nilikuchukulia cheo changu bila uzito na nilidhani nilikuwa kama nyasi ambayo haingeweza kutafuta kuwa mti mkuu na kwamba niliweza kuwa mwaminifu katika kutafuta ukweli na kutimiza wajibu wangu. Singekuwa kama awali nikihisi uchungu, udhaifu, ubaya na kufa moyo nilipoiona familia ya Mungu ikipandisha cheo watu wengine badala ya mimi. Kwa sababu ya maonyesho haya, niliamini kwamba tabia yangu ilikuwa imebadilishwa kwa kiwango fulani na kwamba nilikuwa tayari ninatembea katika njia ya Petro. Leo, kwa kuzingatia mambo ya hakika na ukweli, niliweza kuona kwa dhahiri tabia zangu halisi: Sikuwa kweli naachilia cheo changu, ila nilikuwa nakuwa mwerevu na mjanja zaidi. Baada ya kushughulika na hili mara nyingi, sikuwa nampa Mungu moyo wangu na kutafuta kumpenda Mungu kwa uaminifu. Badala yake, nilikuwa najihifadhi. Siku zote nilikuwa na matarajio yangu ya wakati wa baadaye akilini mwangu. Nilikuwa nimeweka wazo pumbavu moyoni mwangu kwamba “Vyeo vya juu si salama.” Je, nilikuwa naonyesha vipi upendo kwa Mungu na kutembelea njia ya Petro?

Kuhusu mitazamo yangu ambayo haikuwa sahihi, nilisoma “Kanuni za Kuamua Wajibu wa Mtu na Nafasi” na vilevile “Kanuni za Kutumia kwa Ajili ya Mungu” katika “Matendo na Mazoezi kwa Tabia yenye Maadili”. Miongoni mwa kanuni hizi kulikuwa na maneno ya maombi ya Petro: “Unajua kile ninachoweza kufanya, na unajua zaidi wajibu ninaoweza kutekeleza. Nitafanya lolote utakalo na nitajitolea kila kitu nilichonacho Kwako. Wewe tu ndiwe unayejua kile ninachoweza kukufanyia Wewe. Ingawa Shetani alinidanganya sana na nikakuasi Wewe, ninaamini kwamba Hunikumbuki mimi kwa ajili ya dhambi hizo, kwamba hunichukulii mimi kutokana na hizo dhambi. Ningependa kuyatoa maisha yangu yote kwa ajili Yako wewe. Siombi chochote, na wala sina matumaini au mipango mingine; ningependa tu kuchukua hatua kulingana na nia Zako na kutimiza mapenzi Yako. Nitakunywa kutoka kwenye kikombe Chako kichungu, na mimi ni Wako wa kuamuru(Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Namna Petro Alivyopata Kumjua Yesu). “Hakuna uhusiano kati ya wajibu wa mwanadamu na endapo amebarikiwa au amelaaniwa. Wajibu ni kile ambacho mwanadamu anapaswa kutimiza; ni wajibu wake na hautegemei fidia, masharti, au sababu. Hapo tu ndipo huko kutakuwa kufanya wajibu wake. Mwanadamu aliyebarikiwa hufurahia wema baada ya kufanywa mkamilifu baada ya hukumu. Mwanadamu aliyelaaniwa hupokea adhabu tabia yake isipobadilika hata baada ya kutiwa adabu na kuhukumiwa, yaani, hajakamilishwa. Kama kiumbe, mwanadamu anapaswa kutimiza wajibu wake, afanye anachopaswa kufanya, na afanye anachoweza kufanya, bila kujali kama atabarikiwa au kulaaniwa. Hili ndilo sharti la msingi kwa mwanadamu, kama anayemtafuta Mungu. Usifanye wajibu wako ili ubarikiwe tu, na usikatae kutenda kwa kuogopa kupata laana. Acha Niwaambie hiki kitu kimoja: Ikiwa mwanadamu anaweza kufanya wajibu wake, inamaanisha kuwa anafanya anachopaswa kufanya. Ikiwa mwanadamu hawezi kufanya wajibu wake, inaonyesha uasi wake(Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Tofauti Kati ya Huduma ya Mungu Mwenye Mwili na Wajibu wa Mwanadamu). Kutoka kwa maneno ya Mungu inaweza kuonekana kwamba Petro alitafuta kuweza kweli kumpenda Mungu maisha yake yote na kwamba alitii mipangilio ya Mungu katika kila jambo; hakufanya chaguo au mahitaji yake mwenyewe. Pasipo kujali jinsi Mungu alipanga vitu, yeye siku zote alitii. Mwishowe, alifanya wajibu wake kama kiumbe na alimpa Mungu maisha yake na upendo wake mkuu kwake Yeye. Sababu ya Petro kufanikiwa katika imani yake kwa Mungu haikuwa kwa sababu ya wajibu aliotimiza. Kwa msingi wa mtazamo wangu mwenyewe, Petro ndiye aliyekuwa mfuasi mkuu kati ya wale kumi na wawili, nakatika nafasi ya juu kama ile ilikuwa rahisi kwake kufanya maovu na alikuwa katika hatari ya kuwekwa wazi na kuondolewa. Lakini Petro alifuata njia sahihi na Bwana Yesu alimpa agizo kuu la kuchunga makanisa. Hakuwa anafanya kazi katika cheo chake kama mtume, alikuwa haonekani na hajulikani, alikuwa mwenye bidii na mwangalifu sana katika kutimiza wajibu wake kama kiumbe, kumpenda Mungu kwa kweli, na kumtii. Alipata ridhaa ya Mungu kwa kufanya kadiri ya uwezo wake katika kutimiza wajibu wake. Hii ndiyo ilikuwa siri ya kufanikiwa kwake. Baada ya kutofautiana na maombi ya Petro na hukumu na adabu ya neno la Mungu, nilihisi aibu kubwa. Neno la Mungu liliugonga moyo wangu na kuniruhusu kuona kwamba sikuwa mtiifu na nilimpinga Mungu. Katika kumwamini Mungu, daima nilidumisha matumaini na mipango yangu mwenyewe. Miaka hii yote nilikuwa nashughulika kukurupuka huku na kule nikitafuta hatima ya mwisho, matazamio yangu ya baadaye, umaarufu, faida na cheo. Wakati nilitimiza tu baadhi ya majukumu yangu, nilijaribu kuweka mpango na Mungu na kumwacha Mungu autilie muhuri Wake wa kukubali ili kuhakikisha kwamba ningeokolewa. Mahitaji yangu kwa Mungu kunifanyia hili yanafichua kwamba asili ya Shetani ndani yangu ilikuwa ya ubinafsi sana, ya kusikitikia sana na ovu. Sikuwa na kiwango kidogo cha mantiki na dhamiri ambacho kiumbe anafaa kuwa nacho. Nililikataa agizo kwa sababu ya asili yangu isiyo aminifu. Niliukataa wito wa Mungu ili kujihifadhi mwenyewe; kinyume chake, nilitumia hoja zisizo za maana na kutafuta visingizio. Nilijadili na Mungu. Nilikuwa bila mantiki. Wakati huu, nilisoma neno la Mungu, “Ikiwa mwanadamu anaweza kufanya wajibu wake, inamaanisha kuwa anafanya anachopaswa kufanya. Ikiwa mwanadamu hawezi kufanya wajibu wake, inaonyesha uasi wake.” Dhamiri yangu ilihisi kujilaumu pakubwa; niliwaza kuhusu jinsi kila kitu nilichokuwa nacho kilipewa na Mungu, na chochote nilichoweza kufanya, chochote ambacho ningepitia, Mungu alipanga kila kitu. Mara baada ya nyingine, hukumu na adabu ya Mungu zilinishukia ili nipate tena mantiki na dhamiri yangu na kunifanya niweze kwa kweli kutekeleza majukumu yangu kama kiumbe. Pasipo kujali jinsi Mungu alihitaji kutoka kwangu, ningepaswa kujitolea na kulipiza upendo wa Mungu. La sivyo ingekuwa uhaini na ninapaswa kuadhibiwa! Leo, hoja si iwapo agizo la Mungu lilipangwa na yeyote, bali ni Mungu kujaribu ile njia niliyotembelea miaka hii yote na kile ambacho nimetafuta miaka hii yote. Leo, sina uhalisi wa ukweli na mimi ni mdogo kwa kimo. Mungu hakunipa jukumu hili kwa sababu nina uhodari kwa sasa; bali, linanuiwa kuniruhusu kuendeleza kutafuta ukweli na kukubali mafunzo. Linanilazimu kujitolea kikamilifu kwa Mungu na kuingia katika uhalisi wa kumpenda Mungu na moyo, roho, nguvu na akili yangu yote. Zamani, nilikuwa naishi na mawazo ya kipumbavu. Niliamini kwamba nilikuwa na uhakika na wajibu wangu na cheo changu. Huku nikitekeleza majukumu yangu na mtazamo na usuli huu, sikuwa napokea usafishaji mwingi wala shinikizo nyingi. Hata hivyo, lilifichua tabia yangu potovu kupitia ridhaa na kuridhishwa kwangu na hali yangu ya sasa. Lilifichua maoni yangu ya ubinafsi na ya kusikitisha: Nilikuwa natafuta kutimiza wajibu wangu na imani katika Mungu bila kufanya yote niliyoweza kumridhisha na kumpenda Mungu. Wakati huo, niliweza kuzinduka: Baada ya hii miaka yote, nilidhani tayari nilikuwa natembea kwenye njia ya Petro nikitafuta ukweli. Lakini leo, ukweli unafichua kwamba niliweka umuhimu mkubwa zaidi kwa matazamio yangu ya baadaye. Sikuwa na kiwango hata kidogo cha upendo kwa Mungu na sikuwa tayari kubeba mzigo mzito wala kujitolea kikamilifu kwa Mungu. Je, hili lililingana vipi na kile Petro alikuwa anatafuta?

Katika kutafuta kwangu, nilisoma maneno ya Mungu: “Kama kiumbe wa Mungu, mwanadamu anapaswa kutafuta kutekeleza wajibu wa kiumbe wa Mungu, na kutafuta kumpenda Mungu bila kufanya chaguo lingine kwa kuwa Mungu anastahiki upendo wa mwanadamu. Wale ambao wanatafuta kumpenda Mungu hawapaswi kutafuta faida zozote za kibinafsi au lile ambalo wanatamani binafsi; hii ndiyo njia sahihi kabisa ya ufuatiliaji. Kama kile ambacho unatafuta ni ukweli, kile ambacho unatenda ni ukweli, na kile ambacho unafikia ni badiliko katika tabia yako, basi njia unayopitia ni sahihi. Iwapo utafutacho ni baraka za mwili, na kile unachoweka katika vitendo ni ukweli wa dhana zako mwenyewe, na iwapo hakuna mabadiliko katika tabia yako, na wewe si mtiifu kabisa kwa Mungu katika mwili, na bado unaishi kwenye mashaka, basi unachotafuta bila shaka kitakupeleka kuzimu, kwa kuwa njia ambayo unatembea ni njia ya kushindwa. Iwapo utafanywa mkamilifu ama utatolewa katika mashindano inategemea na harakati yako mwenyewe, ambayo pia ni kusema kuwa mafanikio au kushindwa kunategemea njia ambayo mwanadamu anapitia(Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Mafanikio au Kushindwa Kunategemea Njia Ambayo Mwanadamu Hutembea). Neno la Mungu ni ukweli, njia, na uzima, na wakati huu niliunganisha hali yangu halisi na vifungu viwili vya maneno ya Mungu tena. Niligundua kwamba neno la Mungu tayari lilikuwa limefichua njia ya kuelekea kwa mafanikio ya Petro pamoja na maonyesho ya njia inayoelekea kwa mafanikio. Njia ya Petro iliyoelekea kwa mafanikio hairejelei kutotafuta cheo au kuchukua na kuchagua wajibu. Haikuwa tu juu ya kushindwa katika vipengele vibaya, la muhimu zaidi ilirejelea kutafuta kwa wema kumpenda Mungu na kutimiza wajibu wako wa kiumbe. Isitoshe, kutembea kwenye njia sahihi kutaleta matokeo mengi mazuri na halisi kama vile kumjua Mungu vizuri zaidi, kuzidi kuwa mnyenyekevu zaidi kupitia kwa kutafuta ukweli na kuutia katika vitendo, na kutokuwa na mahitaji, matumaini na najisi zako mwenyewe tena; tabia yako itabadilishwa, na la muhimu zaidi, watu wataingia vizuri zaidi katika ukweli na kuzidi kuwa na upendo wa kweli kwa Mungu ili wajitolee kwa Mungu kikamilifu bila maombi mengine na ni wenye bidii kumpenda Mungu maisha yao yote. Nilidhani kuwa nilitembea kwenye njia sahihi na kwamba nilikuwa tayari nimeingia katika uhalisi wa ukweli fulani. Lakini katika ukweli uliofichuliwa, maonyesho yangu ya kupata ukweli na kubadilisha tabia yangu yalikuwa wapi? Maonyesho yangu ya kumpenda Mungu kweli yalikuwa wapi? Kama kweli nilikuwa nimeingia ndani, basi ningeweza kujaribiwa. Pasipo kujali mipango ambayo Mungu huweka, ningeweza kunyenyekea. Ikiwa kweli nilikuwa nimeingia ndani, basi ningeweza kubaini kiini cha asili ya Shetani ndani yangu na ningeona wokovu wa Mungu kwa kweli. Ningekuwa tayari zaidi kujitolea kwa Mungu na kulipiza mapenzi Yake. Na ukweli hizi pamoja na hukumu na adabu ya neno la Mungu, niliweza kuona kwamba nilikuwa natembea katika njia isiyo sahihi. Sikuwa natembea katika njia ya kutimiza wajibu wangu kama kiumbe wala kutafuta kumpenda Mungu. Badala yake, nilikuwa kwenye njia ya kutafuta maslahi yangu na matumaini yangu binafsi; ilikuwa njia ya kumdanganya Mungu kwa kulazimishwa kufuata na kulipia gharama finyu ili kujihifadhi na kuhakikisha kwamba ningepata hatima ya mwisho. Siku zote nimefuatilia matamanio ya mwili. Ili kukidhi raha ya muda mfupi, sikuwa tayari kukubali hukumu na adabu ya Mungu na kupata ukweli; sikuwa tayari kutafuta kumpenda Mungu, kumtolea Mungu kila kitu, wala kugharimia kila kitu kwa ajili ya Mungu kupitia hukumu Yake na adabu, na majaribio Yake na usafishaji Wake. Maoni yangu kutoka kwa kina cha moyo wangu yakikuwa: Tafuta tu kutimiza wajibu kwa amani, usikosee tabia ya Mungu. Mwishowe, nitapata hatima nzuri na hiyo itatosha. Neno la Mungu limeonyesha tena na tena kwamba kiini cha kushindwa kwa Petro kiko katika shughuli zake na Mungu. Alifanya kazi kwa ajili ya thawabu yake ya baadaye na taji lake na hakuwa na unyenyekevu na upendo hata kidogo kwake Bwana wa Uumbaji. Mwishowe ilisababisha yeye kushindwa na kupokea adhabu ya Mungu. Neno la Mungu linatuonya kwa dhahiri: “… wale ambao wanafanya kazi kwa ajili ya hatima yao watapokea maangamizo yao ya mwisho, kwa sababu kushindwa katika imani ya watu katika Mungu hutendeka kwa sababu ya udanganyifu(“Juu ya Hatima” katika Neno Laonekana Katika Mwili). Aina hii ya uwekezaji haufanywi kwa uaminifu; una sura ya uwongo na unadanganya. Nilikuwa na kiburi kweli na nilihepa hukumu ya maneno ya Mungu kwa kutembea njia yangu mwenyewe. Nikiwa nimetawaliwa na asili yangu, siku zote nilikuwa nikitembelea njia nikifuata watu ambao walikuwa wameshindwa. Wakati kazi ya Mungu ya wokovu ilinijia, sikuwa na uwezo wa kutofautisha mabaya na mazuri na nilinyea kambi. Yote niliyokuwa ninampa Mungu yalikuwa kuelewa visivyo, upinzani na usaliti. Wakati huu, niliweza kuona kwa dhahiri jinsi asili yangu ilikuwa ya ubinafsi na ya kusikitikia. Nilimwamini Mungu miaka hii yote na kufurahishwa naye ilhali bado nilipanga njama dhidi ya Mungu, daima nikingoja kufanya biashara na Mungu. Sikuwa na upendo kwa Mungu hata kidogo moyoni mwangu. Hii hasa ndiyo sababu mbona nilikuwa nikitembea katika njia isiyo sahihi na hasa kile Mungu alichokuwa akizungumzia: “Kwa sababu mwanadamu si hodari kwa kujitolea mwenyewe kwa Mungu kabisa, kwa sababu mwanadamu hayuko tayari kutekeleza wajibu wake kwa Muumba, kwa sababu mwanadamu ameona ukweli lakini anauepuka na kutembea katika njia yake mwenyewe, kwa sababu mwanadamu daima anatafuta kwa kufuata njia ya wale walioshindwa, kwa sababu mwanadamu daima anaasi Mbingu, hivyo, mwanadamu daima hushindwa, huchukuliwa na hila za Shetani, na anakamatwa kwa hila na wavu wake(Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Mafanikio au Kushindwa Kunategemea Njia Ambayo Mwanadamu Hutembea).

Baadaye, nilisoma ushirika kutoka kwa wale wa juu, ambacho kilisema: “Kuna watu ambao wana hofu hizi bila kuepukika: ‘Ninatekeleza wajibu wangu, lakini naogopa kutembea njia ya yule anayempinga Kristo; naogopa kutenda kitu kibaya na kumpinga Mungu.’ Je kuna watu wengi na hofu kama hizi? Hasa wale wanaohudumu kama wafanyikazi na viongozi, wameona kwamba mtu fulani na fulani ambaye alitafuta kwa bidii zamani, alikuwa na vipawa, alikuwa na akili nzuri, na kisha alianguka. Mtu fulani na fulani alikuwa na ujuzi kabisa katika kuhubiri, lakini mwishowe, alianguka pia, bila kutarajia. Wanasema: “Nikifanya vitu hivyo, je, nitaishia kama wao na kuanguka pia?” Kama ungekuwa mtu anayempenda Mungu ungekuwa bado na uoga wa vitu hivi? Kama ungekuwa na upendo wa kweli kwa Mungu, ungetawaliwa na hofu yako bado? Watu wanaompenda Mungu daima hufikiria mapenzi Yake na hawatafanya kitu kibaya. … Kama una utambuzi juu ya kutembea njia ya anayempinga Kristo ni nini na kutembea katika njia ya kufuatilia ukweli na kukamilishwa ni nini, basi mbona unaogopa kufuata njia ya mpinga Kristo? Woga huo hauthibitishi kwamba bado unataka kutembea kwayo na kwamba huko tayari kuiacha njia mbaya? Hili silo shida?” (“Jinsi ya Kutafuta Kumpenda Mungu na Kumshuhudia Mungu” katika Ushirika na Mahubiri Kuhusu Kuingia Maisha IX). Kupitia ufunuo wa ushirika kutoka kwa wale wa juu, niliweza kuona kwa dhahiri zaidi kwamba watu wasiompenda Mungu wako kwenye njia ya anayempinga Kristo; kwamba watu hawampendi Mungu ndiyo asili ya kushindwa; pia niliona kwa dhahiri zaidi sababu na visingizio ambavyo nilikuwa navyo kutoka kwa Shetani vilivyojificha ndani yangu; niliweza kubaini hila za Shetani. Kwamba sikuwa tayari kukubali majukumu makubwa zaidi na niliogopa kutembea njia ya kushindwa ilifichua kwamba asili yangu ilikuwa yenye ubinafsi, ya kusikitikia na ovu. Ilifichua kwamba nilijipenda mimi na Shetani sana na kwamba sikudharau njia ya yule anayempinga Kristo, ambayo ilikuwa kutafuta cheo na umaarufu pamoja na matazamio na hatima ya siku za baadaye. Sikuthamini ukweli wala kuwa na upendo hata kidogo kwa Mungu. Niliweza pia kuelewa kwa kweli kwamba kile ambacho wale wa juu walisema kuhusu watu waliomwamini Mungu kwa miaka mingi na bado hawakuwa na upendo wowote kwa Mungu hawakuwa na asili ya binadamu; ungeweza kusema kwamba wote walikuwa na asili fulani ovu; wote walikuwa watu binafsi, wa kusikitikia na waovu. Hivyo nilikuwa na ufahamu wa kweli kuhusu kiini cha asili yangu mwenyewe. Kwa wakati uo huo, ilinisababisha pia kugeuza mitazamo yangu iliyokuwa na makosa na kuwachiliwa na kuwa na mwelekeo sahihi na njia ya kutenda ili nisiishi tena kwa ubinafsi na kwa namna ya kusikitikia; kila kitu kinapangwa na Mungu na ninahitaji tu kutafuta ukweli kwa hakika na kutenda upendo kwa Mungu wakati ninatimiza wajibu wangu.

Msifu Mungu kwa ajili ya hukumu Yake na adabu Yake ambazo ziligeuza lengo la kutafuta kwangu huku na kule na kunirudisha kutoka njia ya makosa. Iliniruhusu pia kutambua kweli kiini cha asili ya Shetani iliyokuwa ndani yangu na kupata chanzo cha kushindwa kwangu. Nilimwamini Mungu miaka hii yote na sikuwahi kumpenda Mungu. Nilihisi aibu na kujilaumu. Nilimsikitisha Mungu kweli na kumwumiza Mungu mno. Moyo wangu unatamani sana kukuza upendo wa kweli kwa Mungu. Petro alikamilishwa kwa sababu alimpenda Mungu kweli na kwa sababu alikuwa na hiari na uvumilivu wa kutafuta ukweli. Ingawa niko mbali na hilo, sitaishi kwa namna ya kuchukiza na isiyovutia tena ili kujihifadhi; niko tayari kufanya kumpenda Mungu kuwa lengo langu katika kutafuta na nitatumia juhudi zote na kulipa gharama katika kutimiza wajibu wangu. Kweli nitaubeba mzigo wa majukumu yangu na kutia ukweli katika vitendo wakati ninatimiza wajibu na kuingia katika uhalisi wa kumpenda Mungu.

Iliyotangulia: 19. Ubora Duni wa Tabia Sio Kisingizio

Inayofuata: 21. Nimejifunza Jinsi ya Kuwatendea Watu Vizuri

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Maudhui Yanayohusiana

1. Nimebahatika Kumhudumia Mungu

Na Gensui, Korea ya KusiniMwenyezi Mungu anasema, “Ni kupitia nini ndiyo ukamilishaji wa Mungu kwa mwanadamu hutimizwa? Kupitia tabia Yake...

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp