124 Mungu Huwabariki Wale Wampendao

Wale wampendao Mungu humtii,

wanaishi mbele Zake daima.

Kwa mwongozo wa maneno Yake,

wanapata amani na kufurahia.

Wale wampendao Mungu ni waaminifu,

wakitenda ukweli wanaelewa.

Daima wanayachukulia mapenzi ya Mungu kwa dhati,

wanatimiza wajibu wao ili kumridhisha.

Wale wampendao Mungu wana maadili.

kutumia ukweli katika maoni yao na matendo yao.

Hakuna sheria na hakuna pingu,

wameingia katika ulimwengu wa uhuru.

Mungu huwabariki wale wampendao,

Hukumu na kuadibu Kwake

daima huwa pamoja nao.

Wanatafuta ukweli na kupata nuru.

na upotovu wao umetakaswa.

Mungu hubariki wale wampendao,

Watakuwa na furaha kweli.

Kupitia hukumu wanapata wokovu.

Maneno ya Mungu huwa maisha yao,

Uso Wake huwaangazia.

Wale wampendao Mungu humcha,

wanakubali uchunguzi Wake.

Kutafuta mapenzi Yake katika majaribu,

wao huingia katika ukweli, wakishuhudia.

Wale wampendao Mungu ni waaminifu Kwake,

thabiti katika imani kupitia majaribu.

Wao huacha mustakabali na majaliwa,

kumpenda Mwenyezi Mungu kwa moyo wote.

Wale wampendao Mungu wana ukweli,

daima washuhudia na kumtukuza Mungu.

Wale wampendao Mungu, wamwabudu,

kusifu haki na utakatifu Wake.

Mungu huwabariki wale wampendao,

Hukumu na kuadibu Kwake

daima huwa pamoja nao.

Wanatafuta ukweli na kupata nuru.

na upotovu wao umetakaswa.

Mungu hubariki wale wampendao,

Watakuwa na furaha kweli.

Kupitia hukumu wanapata wokovu.

Maneno ya Mungu huwa maisha yao,

Uso Wake huwaangazia.

Iliyotangulia: 123 Wale Wanaompenda Mungu Wana Furaha Kweli

Inayofuata: 125 Nimeuona Upendo wa Mungu

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Maudhui Yanayohusiana

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp