Kufunua Upotovu wa Wanadamu (I)

Maneno ya Mungu ya Kila Siku (Dondoo 300)

Baada ya miaka elfu kadhaa ya upotovu, mwanadamu amekuwa asiyehisi na mpumbavu, pepo anayempinga Mungu, kwa kiasi kwamba uasi wa mwanadamu kwa Mungu umeandikwa katika vitabu vya historia, na hata mwanadamu mwenyewe hana uwezo wa kutoa ripoti kamili ya tabia zake za uasi wake—kwa kuwa mwanadamu amepotoshwa sana na Shetani, na amehadaiwa na Shetani kiasi kwamba hajui ni wapi pa kugeukia. Hata wa leo, mwanadamu bado anamsaliti Mungu: Wakati mwanadamu anamwona Mungu, anamsaliti, na wakati yeye hawezi kumwona Mungu, bado anamsaliti. Kuna hata wale ambao, baada ya kushuhudia laana ya Mungu na ghadhabu ya Mungu, bado wanamsaliti. Na hivyo Nasema kwamba hisia ya mwanadamu imepoteza kazi yake ya awali, na kwamba dhamiri ya mwanadamu, pia, imepoteza kazi yake ya awali. Mwanadamu Ninayemtazamia ni mnyama katika mavazi ya binadamu, yeye ni nyoka mwenye sumu, haijalishi jinsi anavyojaribu kuonekana mwenye kuhurumiwa machoni Pangu, Sitawahi kamwe kuwa na huruma kwake, kwa kuwa mwanadamu hana ufahamu wa kutofautisha kati ya nyeusi na nyeupe, tofauti kati ya ukweli na yasiyo ya kweli. Hisia ya mwanadamu ni usiohisi chochote, ilhali bado anataka apate baraka; ubinadamu wake si wa kuheshimika lakini bado anataka kumiliki ukuu wa mfalme. Ataweza kuwa mfalme wa nani, na hisia kama hiyo? Jinsi gani yeye na ubinadamu kama huo ataweza kukaa kwenye kiti cha enzi? Mwanadamu kwa kweli hana aibu! Yeye ni mdhalili wa kujivuna tu! Kwa wale kati yenu mnaotaka kupokea baraka, Ninawashauri kwanza mtafute kioo na kuangalia picha zenu mbaya—je, una kile kinachohitajika kuwa mfalme? Je, una uso wa mwanadamu ambaye anaweza kupata baraka? Hakujawa mabadiliko hata madogo katika tabia yako na wewe hujaweka ukweli wowote katika vitendo, ilhali bado unatamani kuona siku ifuatayo ikiwa ya ajabu. Unajihadaa mwenyewe! Kwa sababu ya kuzaliwa katika nchi ya uchafu vile, mwanadamu ameangamizwa kabisa na jamii, amekuwa akishawishiwa na maadili ya kikabaila, na amefundisha katika “taasisi za elimu ya juu.” Fikra zilizo nyuma kimaendeleo, maadili potovu, mtazamo mbaya juu ya maisha, falsafa za kudharauliwa za kuishi, uwepo usio na thamani, na hali potovu za maisha na desturi—mambo yote haya yameuingilia moyo wa mwanadamu, na kudhoofisha na kushambuliwa dhamiri yake pakubwa. Matokeo yake, mwanadamu kamwe yuko mbali kutoka kwa Mungu, na kila mara anampinga. Tabia ya mwanadamu inakuwa matata zaidi kila siku, na hakuna hata mmoja ambaye kwa hiari yake atatoa chochote kwa ajili ya Mungu, hakuna hata mmoja ambaye kwa hiari atamtii Mungu, wala, zaidi ya hayo, mwanadamu mmoja ambaye kwa hiari yake atatafuta uso wa Mungu. Badala yake, chini ya umiliki wa shetani, mwanadamu hafanyi kitu ila kukimbiza anasa, kujitoa mwenyewe kwa upotovu wa mwili katika nchi ya matope. Hata wanaposikia ukweli, wale wanaoishi gizani hawafikiri kuuweka katika vitendo, na wala kuelekea kumtafuta Mungu hata kama wameuona mwonekano Wake. Jinsi gani wanadamu wapotovu kiasi hiki wawe na nafasi yoyote ya wokovu? Jinsi gani wanadamu waovu kiasi hiki kuishi katika mwanga?

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Kuwa na Tabia Isiyobadilika Ni Kuwa katika Uadui na Mungu

Maneno ya Mungu ya Kila Siku (Dondoo 301)

Tabia ya upotovu ya mwanadamu inatokana na hali yake ya kupewa sumu na kukanyagwa na Shetani, kutokana na madhara mabaya sana ambayo Shetani ameweka katika mawazo yake, maadili, ufahamu, na hisia. Ni hasa kwa sababu mambo ya msingi ya mwanadamu yamepotoshwa na Shetani, na ni tofauti kabisa na jinsi Mungu aliwaumba kwa asili, kwamba mwanadamu humpinga Mungu na haelewi ukweli. Hivyo, mabadiliko katika tabia za mwanadamu lazima yaanze na mabadiliko katika mawazo yake, ufahamu na hisia ambayo yatabadilisha maarifa yake ya Mungu na maarifa yake ya ukweli. Wale waliozaliwa katika nchi potovu zaidi ndio wasiojua zaidi kumhusu kile Mungu Alicho, au kunamaanisha nini kumwamini Mungu. Jinsi watu walivyo wapotovu zaidi, ndivyo wanavyokosa kujua kuwepo kwa Mungu na ndivyo hisia zao na utambuzi huwa duni. Chanzo cha upinzani wa mwanadamu na uasi dhidi ya Mungu ni kupotoshwa kwake na Shetani. Kwa sababu amepotoshwa na Shetani, dhamiri ya mwanadamu imekuwa bila hisia, yeye ni mwovu, mawazo yake yamepotoka, na ana mtazamo duni. Kabla ya kupotoshwa na Shetani, mwanadamu kawaida alimfuata Mungu na alitii maneno Yake baada ya kuyasikia. Alikuwa kawaida mwenye akili timamu na dhamiri, na wa ubinadamu wa kawaida. Baada ya kupotoshwa na Shetani, hali yake ya awali, dhamiri, na ubinadamu vilidhoofika sana na viliharibiwa na shetani. Hivyo, yeye amepoteza utii wake na upendo kwa Mungu. Akili ya mwanadamu imekuwa potovu, tabia yake imekuwa sawa na ile ya mnyama, na uasi wake kwa Mungu kabisa umekuwa wa mara kwa mara na wa kuhuzunisha zaidi. Hata hivyo mwanadamu bado hajui wala kutambua hili, na kwa upofu anapinga na kuasi. Ufunuo wa tabia ya mwanadamu ni udhihirisho wa hisia zake, utambuzi na dhamiri, na kwa sababu hisia yake na utambuzi si timamu, na dhamiri yake imezidi kuwa ndogo zaidi, hivyo tabia yake ni ya uasi dhidi ya Mungu. Kama hisia ya mwanadamu na utambuzi hauwezi kubadilika, basi mabadiliko katika tabia yake hayawezekani, sawa na kuwa baada ya moyo wa Mungu. Kama hisia ya mwanadamu sio timamu, basi hawezi kumhudumia Mungu na hafai kutumiwa na Mungu. “Hisia za Kawaida” inaashiria kutii na kuwa mwaminifu kwa Mungu, kuwa mwenye imani kamili kwa Mungu, na kwa kuwa na dhamiri kwa Mungu. Inamaanisha kuwa na moyo mmoja na akili kwa Mungu, na si kwa kumpinga Mungu kwa makusudi. Wale ambao ni wa akili potovu hawako hivi. Tangu mwanadamu aharibiwe na Shetani, ametunga dhana kuhusu Mungu, na yeye hajakuwa na uaminifu au kumtamani Mungu, pia hana dhamiri kwa Mungu. Mwanadamu kwa makusudi anapinga na huweka hukumu juu ya Mungu, na, zaidi ya hapo, anatupa shutuma Kwake nyuma Yake. Mwanadamu anajua vizuri kuwa Yeye ni Mungu, lakini bado humhukumu nyuma ya mgongo wake, hana nia ya kumtii, na hufanya madai ya kipofu na maombi kwa Mungu. Watu wa aina hii—watu walio na akili potovu—hawana uwezo wa kujua tabia zao za kudharauliwa au ya kujuta uasi wao. Kama watu wana uwezo wa kujijua wenyewe, basi wao wamerudisha kiasi kidogo cha akili zao; Zaidi ya vile watu wanavyomuasi Mungu lakini hawajui wenyewe, ndivyo walivyo zaidi wenye akili isiyo timamu.

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Kuwa na Tabia Isiyobadilika Ni Kuwa katika Uadui na Mungu

Maneno ya Mungu ya Kila Siku (Dondoo 302)

Chanzo cha ufunuo wa upotovu wa tabia ya mwanadamu ni dhamiri yake iliyofifia, asili yake mbovu na akili yake isiyo timamu; kama dhamiri ya mwanadamu na hisia vinaweza kurudi kawaida, basi atafaa kwa matumizi mbele ya Mungu. Ni kwa sababu tu kuwa dhamiri ya mwanadamu daima imekuwa isiyosikia, akili ya mwanadamu haijawahi kuwa timamu, na inazidi kuwa hafifu ndio mwanadamu amezidisha uasi wake kwa Mungu, hata akampiga Yesu misumari juu ya msalaba na kumkataa Mungu mwenye mwili wa siku za mwisho kuingia katika nyumba yake, na analaani mwili wa Mungu, na anaona mwili wa Mungu kuwa wa hali ya chini. Kama mwanadamu angekuwa na ubinadamu kidogo, hangekuwa mkatili kiasi hicho katika utendeaji wake wa mwili wa Mungu mwenye mwili; kama angekuwa na akili hata kidogo tu, hangekuwa hivyo katika utendeaji wake wa mwili wa Mungu mwenye mwili; kama angekuwa na dhamiri hata kidogo, hangekuwa mwenye “shukrani” kwa Mungu mwenye mwili kwa njia hii. Mwanadamu anaishi katika enzi ya Mungu kuwa katika mwili, lakini yeye hawezi kumshukuru Mungu kwa kumpatia nafasi nzuri kiasi hicho, na badala yake analaani kuja kwa Mungu, au kupuuza kabisa ukweli wa Mungu aliyepata mwili, na inaonekana anapinga hali hii na anachoshwa nayo. Haijalishi jinsi mwanadamu anachukua kuja kwa Mungu, Mungu, kwa ufupi, daima ameendeleza kazi yake kwa uvumilivu—hata kama mwanadamu hajawahi kumkaribisha, na bila kujua yeye hufanya maombi kwa Mungu. Tabia ya mwanadamu imekuwa mbaya zaidi, akili yake imekuwa hafifu zaidi, na dhamiri yake imekanyagwa kabisa na yule muovu na kwa muda mrefu imekoma kuwa dhamiri ya awali ya mwanadamu. Mwanadamu hajakosa tu shukrani kwa Mungu mwenye mwili kwa kukabidhi maisha na neema nyingi juu ya wanadamu, bali pia anachukia Mungu kwa kumpatia ukweli; ni kwa sababu mwanadamu hana haja ya kujua ukweli hata kidogo ndio maana anamchukia Mungu. Haitoshi kwamba mwanadamu hawezi kuutoa uhai wake kwa ajili ya Mungu mwenye mwili tu, lakini pia anajaribu kutoa neema kutoka kwa Mungu, na anafanya madai kwa Mungu yaliyo mara kadhaa kubwa kuliko kile mwanadamu ametoa kwa Mungu. Watu wa dhamiri na hisia kama hizo hufikiria kwamba hili si jambo kubwa, na bado wanaamini kuwa wao wamefanya mengi sana kwa ajili ya Mungu, na kwamba Mungu amewapa kidogo sana. Kuna watu ambao wamenipa bakuli la maji na kisha kunyosha mikono yao na kudai kwamba nilipie bakuli mbili za maziwa, au kunipa chumba kwa usiku mmoja lakini walijaribu kunilipisha mara nyingi zaidi katika ada ya makazi. Ukiwa na ubinadamu kama huo, na dhamiri ya aina hii, ni jinsi gani bado mnatarajia kupata uzima? Nyinyi ni fukara wa kudharauliwa mlioje! Ni kwa sababu ya ubinadamu huu na dhamiri ya mwanadamu ndio maana Mungu mwenye mwili anatembea katika ardhi yote, asipate mahali pa makazi. Wale ambao kwa kweli wanayo dhamiri na ubinadamu wanapaswa kumuabudu na kwa moyo wote kumhudumia Mungu mwenye mwili si kwa sababu ya kiasi cha kazi aliyofanya, lakini hata kama Yeye hangefanya kazi yoyote kamwe. Hili ndilo linafaa kufanywa na wale walio na akili timamu, na ndio wajibu wa mwanadamu. Watu wengi hata huzungumza juu ya masharti katika huduma yao kwa Mungu: Hawajali kama yeye ni Mungu au mwanadamu, na wao huzungumza juu ya masharti yao tu, na kutafuta kuridhisha tamaa zao wenyewe tu. Mnaponipikia, mnadai malipo ya huduma, wakati mnakimbia kwa ajili Yangu, mnadai pesa za mkimbiaji, mkinifanyia kazi mnadai ada ya kazi, mkifua nguo Zangu, mnadai ada ya kufua, wakati mnatoa kwa ajili ya kanisa mnadai malipo ya kurudisha nguvu, mkizungumza, mnadai malipo ya msemaji, mkipeana vitabu mnadai ada ya usambazaji, na wakati mnaandika mnadai malipo ya kuandika. Wale Nimehusiana nao hata hudai malipo kutoka Kwangu, na wale waliotumwa nyumbani hudai fidia kwa uharibifu wa majina yao; wale ambao hawajaoa au kuolewa hudai mahari, au fidia kwa ujana wao waliopoteza, wale wanaochinja kuku wanadai ada ya uchinjaji, wale wanaokaanga chakula wanadai ada ya kukaanga, na wale ambao hupika supu wanadai malipo pia…. Huu ndio ubinadamu wenu mkuu na wenye majivuno, na haya ndiyo matendo yanayoamrishwa na dhamiri yenu yenye joto. Hisia zenu ziko wapi? Ubinadamu wenu uko wapi? Wacha Niwaambie! Mkiendelea hivi Nitakoma kufanya kazi miongoni mwenu. Sitafanya kazi miongoni mwa wanyama waliovalia mavazi ya binadamu, Sitateseka hivyo kwa ajili ya kundi la watu ambao nyuso zao nzuri zimeficha nyoyo za uhasama, Sitavumilia kwa ajili ya kundi la wanyama ambao hawana uwezekano hata kidogo wa kuokolewa. Siku Nitakayowapa mgongo ndiyo siku mtakayokufa, ndiyo siku ambayo giza litakuja juu yenu, na ni siku mtakayoachwa na mwanga. Hebu Niwaambie! Sitakuwa mwema kamwe kwa kundi kama lenu, kundi ambalo liko chini ya hata wanyama! Kuna mipaka katika maneno na matendo Yangu, na vile ubinadamu wenu na dhamiri zilivyo, Sitafanya kazi zaidi, kwani mmekosa dhamiri, umenisababishia maumivu mengi sana, na tabia yenu ya kudharauliwa inanichukiza Mimi sana. Watu wanaokosa utu na dhamira kamwe hawatakuwa na nafasi ya wokovu; Mimi kamwe Sitawaokoa watu kama hao wasio na utu wala shukurani. Siku Yangu itakapofika, Nitanyesha mvua ya moto Wangu mkali milele juu ya wana waasi walioiamsha hasira na ghadhabu yangu kali hapo awali, Nitalazimisha adhabu yangu milele juu ya wanyama wale ambao wakati mmoja waliupa lugha chafu Kwangu na wakaniacha, Nitawachoma wakati wote kwa moto wa hasira Yangu wana wa uasi waliokula na kuishi pamoja Nami lakini hawakuniamini, na wakanitukana na kunisaliti. Nitawatia wote walionikasirisha kwa adhabu Yangu, Nitanyesha ghadhabu Yangu kwa ukamilifu juu ya wanyama hao waliotamani wakati mmoja kusimama kando Yangu kama visawe Vyangu ilhali hawakuniabudu wala kunitii, fimbo Ninayotumia kumgonga mwanadamu itaanguka juu ya wanyama hao waliofurahia utunzaji Wangu na siri Nilizonena, na waliojaribu kuchukua starehe ya mali ya dunia kutoka Kwangu. Sitamsamehe mtu yeyote anayejaribu kuchukua nafasi Yangu; Sitamsamehe yeyote anayejaribu kupokonya chakula na nguo kutoka Kwangu. Kwa sasa, mnabaki huru kutokana na madhara na kuendelea kujiharibia kwa kuzidi katika mahitaji mnayotaka kutoka Kwangu. Siku ya ghadhabu inapofika hamtafanya madai yoyote zaidi Kwangu; wakati huo, Nitawaruhusu “kujifurahia” hadi mtakaporidhika, Nitalazimisha nyuso zenu kuingia mchangani, na kamwe hamtaweza kuinuka tena! Wakati mmoja au mwingine, Ninaenda “kulipiza” madeni hayo kwenu na Natumaini mnasubiri kwa uvumilivu kuwasili kwa siku hii.

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Kuwa na Tabia Isiyobadilika Ni Kuwa katika Uadui na Mungu

Maneno ya Mungu ya Kila Siku (Dondoo 303)

Mwanadamu anashindwa kumpata Mungu sio kwa sababu Mungu ana hisia, au kwa sababu Mungu hataki kupatikana na mwanadamu, bali ni kwa sababu mwanadamu hataki kumpata Mungu, na kwa sababu mwanadamu hana haraka kumtafuta Mungu. Jinsi gani mmoja wa wale ambao kweli wanamtafuta Mungu alaaniwe na Mungu? Ni jinsi gani mwenye akili timamu na dhamiri nzuri anaweza laaniwa na Mungu? Ni vipi yule anayemwabudu kwa kweli na kumhudumia Mungu ataangamizwa na moto wa ghadhabu yake? Ni jinsi gani mwanadamu aliye na furaha ya kumtii Mungu kutupwa nje ya nyumba ya Mungu kwa mateke? Jinsi gani mwanadamu ambaye hawezi kumpenda Mungu vya kutosha aishi katika adhabu ya Mungu? Jinsi gani mwanadamu ambaye ana furaha ya kuacha kila kitu kwa ajili ya Mungu kuachwa bila chochote? Mwanadamu hana nia ya kumfuata Mungu, hana nia ya kutumia mali yake kwa Mungu, hana nia ya kutoa juhudi za milele kwa Mungu, na badala yake anasema kwamba Mungu amepita kiasi, kwamba mengi kuhusu Mungu yanakinzana na dhana za mwanadamu. Na ubinadamu kama huu, hata kama mngekuwa wakarimu katika juhudi zenu bado hamngeweza kupata kibali cha Mungu, bila kutaja kuwa hamumtafuti Mungu. Je, hamjui kwamba ninyi ni bidhaa mbovu za binadamu? Je, hamjui kwamba hakuna ubinadamu ulio mnyenyekevu zaidi kuliko wenu? Je, hamjui “cheo” chenu ni kipi? Wale ambao kweli wanampenda Mungu wanawaita baba wa mbweha, mama wa mbweha, mwanambweha, na mjukuu wa mbweha; nyinyi ni vizazi vya mbweha, watu wa mbweha, na mnapaswa kujua utambulisho wenu na kamwe msiwahi kuusahau. Msidhani kwamba nyinyi ni kiumbe mkubwa zaidi: Nyinyi ni kundi mojawapo la wasio-wanadamu wabaya zaidi miongoni mwa wanadamu. Je, hamjui lolote kuhusu haya? Je, mnajua ni kiasi gani cha hatari Nimechukua kwa kufanya kazi miongoni mwenu? Kama akili yenu haiwezi kurudi kawaida, na dhamiri yenu haiwezi kufanya kazi kwa kawaida, basi kamwe hamtawahi kuwa huru kutokana na jina “mbwa mwitu”, kamwe hamtaitoroka siku ya laana, kamwe hamtaitoroka siku ya adhabu yenu. Mlizaliwa mkiwa duni, kitu kisicho na thamani yoyote. Kwa hivyo nyinyi ni kundi la mbwa mwitu wenye njaa, rundo la uchafu na takataka, na, tofauti na nyinyi, Mimi Sifanyi kazi kwenu ili nipate chochote, lakini kwa sababu ya haja ya kazi. Mkiendelea kuwa waasi kwa njia hii, basi Nitakomesha kazi Yangu, na kamwe sitafanya kazi kwenu tena; badala yake, Nitahamisha Kazi yangu kwa kundi lingine linalonipendeza, na kwa njia hii kuondoka kwenu milele, kwa sababu Mimi sina nia ya kuwaangalia walio katika uadui na Mimi. Hivyo basi, je, mnataka kulingana na Mimi, au katika uadui dhidi Yangu?

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Kuwa na Tabia Isiyobadilika Ni Kuwa katika Uadui na Mungu

Maneno ya Mungu ya Kila Siku (Dondoo 304)

Watu wote wana tamaa ya kuona uso wa kweli wa Yesu na wote hutaka kuwa pamoja Naye. Naamini kuwa hakuna mmoja wa ndugu au dada anayeweza kusema kwamba yeye hana nia ya kumwona au kuwa pamoja na Yesu. Kabla ya nyinyi kumwona Yesu, yaani, kabla ya nyinyi kumwona Mungu Aliye kwenye mwili, mnaweza kuwa na mawazo mengi, kwa mfano, kuhusu sura ya Yesu, njia Yake ya kuzungumza, njia Yake ya maisha, na kadhalika. Hata hivyo, wakati mmemwona hasa, mawazo yenu yatabadilika haraka. Ni kwa nini? Je, mnataka kujua? Hata ingawa fikira za mwanadamu hakika haziwezi kupuuzwa, haikubaliki hata zaidi kwa mwanadamu kubadilisha kiini cha Kristo. Nyinyi mnamchukua Kristo kama asiyekufa au mhenga, lakini hakuna anayemchukulia kama mwanadamu wa kawaida mwenye kiini kitakatifu. Kwa hivyo, wengi wa wale ambao wanatamani usiku na mchana kumwona Mungu ni hasa maadui wa Mungu na hawapatani na Mungu. Je, haya si makosa kwa upande wa mwanadamu? Hata sasa bado mnadhani kwamba imani yenu na uaminifu umetosha kuwafanya mstahili kuona uso wa Kristo, lakini Mimi Nawasihi kujihami kwa mambo zaidi yaliyo na umuhimu! Hii ni kwa maana katika wakati uliopita, uliopo na ujao, wengi wa wale ambao hupatana na Kristo wameanguka au wataanguka; wao wote wamechukua jukumu la Mafarisayo. Sababu yenu ya kushindwa ni nini? Ni kwa sababu hasa katika fikra zenu kuna Mungu mkubwa, Atamanikaye. Lakini ukweli si kama vile mwanadamu atakavyo. Kristo si mkubwa tu, bali Yeye ni mdogo hasa; Yeye si mtu tu, bali ni mtu wa kawaida; Hana uwezo wa kupaa mbinguni tu, bali hana pia uhuru wa kuzunguka ardhini. Na kwa hivyo, watu humtendea kama mtu wa kawaida; wao humtendea kikawaida wanapokuwa pamoja naye, na kusema maneno kiholela Kwake, wakati huu wote wakingojea kurudi kwa “Kristo wa kweli.” Mnamchukua Kristo aliyekuja tayari kama mtu wa kawaida na neno Lake kama lile la mtu wa kawaida. Kwa hivyo, hamjapata chochote kutoka kwa Kristo na badala yake mmeonyesha ubaya wenu kwenye mwangaza kabisa.

Kabla ya kuwasiliana na Kristo, unaweza kuamini kwamba tabia yako imebadilishwa kabisa, kwamba wewe ni mfuasi mwaminifu wa Kristo, na kwamba wewe unastahili kupokea baraka za Kristo zaidi. Pia kwamba, kwa kuwa umesafiri njia nyingi, umefanya kazi nyingi, na kuleta matunda mengi, hivyo ni lazima utakuwa mtu anayepata taji mwishowe. Hata hivyo kuna ukweli ambao huenda hujui: Tabia potovu na uasi na upinzani wa mwanadamu huonekana wazi mara tu anapomwona Kristo, na uasi na upinzani unaoonekana wakati huu kwa hakika na kamilifu kuliko wakati mwingine wote. Ni kwa sababu Kristo ni Mwana wa Adamu—Mwana wa Adamu aliye na ubinadamu wa kawaida—kwamba mwanadamu hamwogopi wala kumheshimu. Ni kwa sababu Mungu anaishi katika mwili ndio maana uasi wa mwanadamu hufichuliwa kikamilifu na kwa uwazi sana. Kwa hivyo Nasema kwamba kuja kwake Kristo kumechimbua uasi wote wa wanadamu na kutupa asili ya mwanadamu katika afueni ya ghafla. Huku kunaitwa “kumvuta chui mkubwa kutoka mlimani” na “kumvuta mbwa mwitu kutoka pangoni pake.” Je, unathubutu kusema kwamba wewe ni mwaminifu kwa Mungu? Je, unathubutu kusema kwamba wewe huonyesha utiifu kamili kwa Mungu? Je, unathubutu kusema kwamba wewe si muasi? Wengine watasema: Kila wakati ambao Mungu ananiweka katika mazingira mapya, mimi daima hutii na silalamiki na aidha siweki fikra zozote juu ya Mungu. Wengine watasema: Kazi zozote nilizopewa na Mungu mimi hufanya kadri ya uwezo wangu na kamwe mimi si mvivu. Kama ndivyo hali, Nawauliza hivi: Je, mnaweza kulingana na Kristo wakati mnaishi pamoja naye? Na ni kwa muda gani nyinyi mnaweza kulingana na Yeye? Siku moja? Siku mbili? Saa moja? Saa mbili? Imani yenu inaweza kuwa ya kustahili sifa, lakini hamna uthabiti wa kutosha. Wakati unaishi na Kristo kwa kweli, kujidai kwako na kujigamba kwako kutawekwa wazi kwa maneno na matendo yako kidogo kidogo, na hivyo ndivyo tamaa yako ya kupindukia, na akili yako isiyotii na kutoridhika kwako kutafichuka kwa kawaida. Mwishowe, kiburi chako kitakuwa kikubwa zaidi, hadi wakati wewe utazozana sana na Kristo kama maji na moto, na basi asili yako itawekwa wazi kabisa. Wakati huo, fikra zako haziwezi kufichika tena, malalamiko yako, pia, yataonekana kwa ghafla, na ubinadamu wako duni utakuwa wazi kabisa. Hata hivyo, hata wakati huo, utaendelea kukana uasi wako mwenyewe, ukiamini kwamba badala yake kwamba Kristo kama huyu si rahisi kukubaliwa na mwanadamu, ni mwingi wa madai kwa binadamu, na ungetii kikamilifu kwake kama Yeye angekuwa tu Kristo mwenye huruma zaidi. Mnaamini kwamba daima kuna sababu ya haki ya uasi wenu, na kwamba nyinyi mnamwasi tu baada ya Kristo amewafikisha hatua fulani. Kamwe hamjawahi kufikiri kwamba mmekosa kumchukulia Kristo kama Mungu na katika nia ya kumtii. Badala yake, wewe kwa ukaidi unasisitiza Kristo afanye kazi Yake kulingana na matakwa yako, na punde ambapo kuna jambo lolote ambamo Hafanyi hivyo, basi unaamini kwamba Yeye si Mungu bali ni mwanadamu. Je, si kuna wengi kati yenu ambao wameridhika na Yeye katika hali hii? Ni nani huyo mnayemwamini hata hivyo? Na ni jinsi gani mnatafuta?

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Wale Ambao Hawalingani na Kristo Hakika Ni Wapinzani wa Mungu

Maneno ya Mungu ya Kila Siku (Dondoo 305)

Kila mara mnataka kumwona Kristo, lakini Nawasihi msijipandishe hadhi hivyo; kila mtu anaweza kumwona Kristo, lakini Nasema hakuna ambaye ni wa kufaa kumwona Kristo. Kwa sababu asili ya binadamu imejazwa na uovu, kiburi, na uasi, wakati unapomwona Kristo, asili yako itakuharibu na itakuhukumu hadi kufa. Ushirika wako na ndugu (au dada) huenda usionyeshe mengi kukuhusu wewe, lakini si rahisi hivyo unaposhiriki na Kristo. Wakati wowote, fikira zako zinaweza kukita mizizi, kiburi chako kianze kuchipuka, na uasi wako kuzaa mitini. Unawezaje kufaa kushiriki na Kristo na ubinadamu kama huo? Je, kweli unaweza kumchukua Yeye kama Mungu kila wakati wa kila siku? Je, kweli utakuwa na hali halisi ya utiifu kwa Mungu? Mnamuabudu Mungu mkubwa ndani ya mioyo yenu kama Yehova wakati mnamchukua Kristo anayeonekana kama mwanadamu. Hisia zenu ni duni mno na ubinadamu wenu ni wa hali ya chini! Hamwezi kumfikiria Kristo kama Mungu milele; ni mara chache tu, mnapotaka, ndio mnamshika na kumwabudu kama Mungu. Hii ndiyo sababu Ninasema nyinyi si waumini wa Mungu, ila kikundi cha washirika ambao wanaopigana dhidi ya Kristo. Hata watu ambao huonyesha wema kwa wengine hulipwa, lakini Kristo, ambaye amefanya kazi ya namna hiyo kati yenu, hajapokea upendo wa Mungu au fidia na utii wake. Je, hili si ni jambo la kusikitisha moyo?

Inaweza kuwa kwamba katika miaka yako yote ya imani katika Mungu, kamwe hujamlaani mtu yeyote wala kufanya tendo mbaya, lakini katika ushirika wako na Kristo, huwezi kusema ukweli, kutenda kwa uaminifu, au kutii neno la Kristo; basi, Ninasema kwamba wewe ndiye mtu mwovu zaidi na mwenye nia mbaya zaidi duniani. Unaweza kuwa mkunjufu na mwaminifu mno kwa jamaa zako, marafiki, mke (au mume), wanao na mabinti, na wazazi, na kamwe huwatumii wengine vibaya, lakini kama huwezi kulingana na kupatana na Kristo, basi hata ukitumia vitu vyako vyote kuwasaidia majirani zako au kulinda vizuri baba yako, mama, na wanakaya, Ningesema kwamba wewe bado ni mwovu, na zaidi ya hayo aliyejaa hila za ujanja. Usifikiri, kwamba wewe unalingana na Kristo kwa sababu tu unapatana na wengine au unafanya baadhi ya matendo mema. Je, unafikiri kwamba nia yako ya huruma inaweza kupata baraka kutoka Mbinguni kwa ujanja? Je, unafikiri kwamba matendo machache mema yanaweza kubadilishwa na utii wako? Hakuna hata mmoja wenu anaweza kukubali kushughulikiwa na kupogolewa, na wote wanaona vigumu kukubali ubinadamu wa kawaida wa Kristo, hata hivyo siku zote mnatangaza utiifu wenu kwa Mungu. Imani kama yenu italeta adhabu ya kufaa. Wacheni kujihusisha katika ndoto za ajabu na kutaka kumwona Kristo, kwa maana nyinyi ni wadogo sana katika kimo, kiasi kwamba nyinyi hata hamstahili kumwona. Wakati umeuwacha kabisa uasi wako na unaweza kupatana na Kristo, wakati huo Mungu Atakuonekania kwa kawaida. Iwapo utaenda kumwona Mungu kabla ya kupogolewa au kupitia hukumu, basi bila shaka utakuwa mpinzani wa Mungu na utakuwa katika njia ya kuangamizwa. Asili ya mwanadamu kwa kawaida ina uhasama kwa Mungu, kwa kuwa watu wote wamepotoshwa kabisa na shetani. Hakuna kizuri kinachoweza kupatikana kwa mtu kujaribu kushirikiana na Mungu kutokana na upotovu wake. vitendo na maneno yake kwa hakika vitafichua upotovu wake kila wakati; na katika kushirikiana na Mungu, uasi wake utafichuka katika vipengele vyote. Binadamu, kwa kutojua anakuja anampinga Kristo, kumdanganya Kristo, na kumtelekeza Kristo; hili litakapofanyika, mwanadamu atakuwa katika hali ya hatari zaidi na, hili likiendelea, atapata adhabu.

Baadhi ya watu wanaweza kuamini kwamba, kama kushirikiana na Mungu ni hatari sana, basi huenda likawa jambo la busara zaidi kukaa mbali na Mungu. Ni nini watu kama hawa wanaweza kupokea? Je, wanaweza kuwa waaminifu kwa Mungu? Hakika, kushirikiana na Mungu ni kugumu sana, lakini hiyo hasa ni kwa sababu mwanadamu amepotoka na si kwa sababu Mungu hawezi kushiriki naye. Ingekuwa bora kwenu kuweka juhudi zaidi kwa ukweli wa kuzijua nafsi zenu. Mbona hamjapata fadhili kwa Mungu? Kwa nini tabia zenu ni chukizo sana Kwake? Kwa nini maneno yenu yanachochea chuki Yake? Punde ambapo mmeonyesha uaminifu kidogo, nyinyi mnajisifu wenyewe, na mnadai malipo kwa ajili ya mchango mdogo; nyinyi huwadharau wengine wakati nyinyi mnaonyesha utiifu kidogo, na kumdharau Mungu baada ya kufanya kazi ndogo. Mnataka utajiri, zawadi na pongezi kwa ajili ya kumpokea Mungu. Nyoyo zenu huumwa wakati mnatoa sarafu moja au mbili; wakati mnatoa kumi, mnataka kubarikiwa na kutendewa kwa heshima. Ubinadamu kama wenu kweli ni wa kukera kuzungumziwa au kusikizwa. Kuna chochote kinachostahili sifa katika maneno na matendo yenu? Wale ambao wanatekeleza wajibu wao na wale wasiofanya; wale ambao huongoza na wale ambao hufuata; wale wanaompokea Mungu na wale wasiompokea; wale wanaotoa na wale wasiotoa; wale wanaohubiri na wale ambao hupokea neno, na kadhalika; watu wote kama hawa hujisifu wenyewe. Je, hamuoni hili likiwa la kuchekesha? Mkijua vyema kwamba mnamwamini Mungu, hata hivyo ninyi hamwezi kulingana na Mungu. Kweli mnajua vyema kwamba hamstahili hata kidogo. Je, hamhisi kuwa hisia yenu imepunguka kiasi kwamba hamwezi tena kujizuia? Na hisia kama hii, mnastahili vipi kushirikiana na Mungu? Je, kufikia hapa nyinyi hamjionei hofu? Tabia yenu tayari imepunguka kiasi kwamba hamwezi kulingana na Mungu. Hali ikiwa hivi, je, imani yenu si ya kuchekesha? Imani yenu si ya kipuuzi? Ni jinsi gani utashughulikia maisha yako ya baadaye? Ni jinsi gani utachagua njia ya kutembelea?

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Wale Ambao Hawalingani na Kristo Hakika Ni Wapinzani wa Mungu

Maneno ya Mungu ya Kila Siku (Dondoo 306)

Nimeeleza maneno mengi sana, na pia nimeeleza mapenzi Yangu na tabia, lakini hata hivyo, bado watu hawana uwezo wa kunijua Mimi na kuniamini. Au, inaweza kusemwa, bado hawana uwezo wa kunitii. Wale wanaoishi katika Biblia, wale wanaoishi katika sheria, wale wanaoishi juu ya msalaba, wale ambao wanaishi kwa mujibu wa mafundisho, wale wanaoishi miongoni mwa kazi Ninayofanya leo—yupi kati yao analingana na Mimi? Ninyi mnafikiria tu kupokea baraka na tuzo, na hamjawahi kamwe kufikiria jinsi ya kulingana na Mimi, au jinsi ya kujizuia wenyewe kutoka katika uadui na Mimi. Nimeaibishwa sana na nyinyi, kwa kuwa Nimewapa mengi sana, ilhali Mimi Nimepokea kidogo sana kutoka kwenu. Udanganyifu wenu, kiburi chenu, tamaa yenu, tamaa yenu yenye fujo, usaliti wenu, kuasi—lipi kati ya haya linaweza kujificha kutoka kwa macho Yangu? Ninyi mnanitendea hobela hobela, mnanidanganya Mimi, mnanitusi, mnanibembeleza, mnanilazimisha na kupata sadaka kutoka Kwangu kwa nguvu—ni jinsi gani tabia ya kudhuru kama hii itaepuka ghadhabu Yangu? Udhalimu wenu ni thibitisho la uadui wako Kwangu, na ni thibitisho la uwiano wenu na Mimi. Kila mmoja wenu anaamini mwenyewe akilingana na Mimi, lakini ikiwa ni hivyo, basi ni kwa nani ushahidi huu dhahiri unatumika? Mnaamini wenyewe kwamba mnao ukweli wa juu sana na uaminifu Kwangu. Mnafikiri kwamba nyinyi ni wema sana, wenye huruma sana, na mmetoa sana Kwangu. Mnafikiri kwamba mmefanya vya kutosha kwa ajili Yangu. Bado hamjawahi kulinganisha imani hizi dhidi ya tabia zenu wenyewe? Nasema mmejaa mengi ya kiburi, tamaa nyingi, wingi wa uzembe; hila mnayotumia kunidanganya ni janja sana, na mna mengi ya nia ya kudharau na mbinu ya kudharau. Uaminifu wenu pia ni mdogo, bidii yenu pia ni ndogo, na dhamiri yako hata haipo zaidi. Kuna mabaya mengi sana katika nyoyo zenu, na hakuna mtu anayeepuka kuathiriwa na hila yenu, hata Mimi mwenyewe. Mnanifungia nje kwa ajili ya watoto wenu, au waume wenu, au kwa ajili ya hifadhi zenu wenyewe. Badala ya kunijali, mnajali familia zenu, watoto wenu, hali yenu, maisha yenu ya baadaye, na kujitosheleza wenyewe. Ni lini mmewahi kuniwaza Mimi mnapozungumza au kutenda? Wakati hali ya hewa ni baridi, mawazo yenu hurejea kwa watoto wenu, waume wenu, wake wenu, au wazazi wenu. Wakati hali ya hewa ni ya joto, hata Siwezi kupata nafasi katika mawazo yenu pia. Unapotekeleza wajibu wako, wewe huwaza tu kuhusu maslahi yako mwenyewe, ya usalama wako mwenyewe binafsi, ya watu wa familia yako. Ni nini umewahi kufanya kwa ajili Yangu? Ni lini umeweza kuwaza kunihusu Mimi? Ni lini umewahi kujitoa mwenyewe, kwa gharama yoyote, kwa ajili Yangu na kazi Yangu? Uko wapi ushahidi wa uwiano wako na Mimi? Uko wapi ukweli wa uaminifu wako kwa ajili Yangu? Uko wapi ukweli wa utiifu wako Kwangu? Ni lini mujibu wako hujakuwa kwa sababu ya kupokea baraka Zangu? Mnanilaghai na kunidanganya Mimi, mnacheza na ukweli na kuficha kuwepo kwa kweli, na kuisaliti dutu ya ukweli, na mnajiweka wenyewe kwa uadui kama huu na Mimi. Basi, ni nini kinawangoja katika siku za usoni? Ninyi mnatafuta tu uwiano na Mungu asiye yakini, na kutafuta tu imani zisizo yakini ilhali ninyi hulingani na Kristo. Si uovu wenu utapata adhabu kama ile wanayostahili waovu? Wakati uo huo, mtagundua kuwa hakuna mtu yeyote asiyelingana na Kristo atakayeepuka siku ya ghadhabu, na mtagundua ni aina gani ya adhabu italetwa juu ya wale walio katika uadui na Kristo. Siku hiyo itakapofika, ndoto yenu ya kubarikiwa kwa imani yenu katika Mungu na kupata kuingia mbinguni, yote itakatizwa. Lakini, hata hivyo, si hivyo kwa wale ambao wanalingana na Kristo. Ingawa wao wamepoteza sana, ingawa wamekabiliwa na mengi ya ugumu wa maisha, watapokea urithi wote ambao Nimeutoa kwa ajili ya mwanadamu. Hatimaye, mtaelewa kwamba Mimi tu ndiye Mungu mwenye haki, na kwamba ni Mimi tu Niliye na uwezo wa kuwachukua binadamu mpaka kwenye hatima yao yenye kupendeza.

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Unapaswa Kutafuta Njia ya Uwiano na Kristo

Maneno ya Mungu ya Kila Siku (Dondoo 307)

Mungu amewaaminia wanadamu vitu vingi sana na Amezungumza bila kikomo juu ya kuingia kwao. Lakini kwa sababu ubora wa tabia ya watu ni duni mno, maneno mengi ya Mungu yameshindwa kuanza kustawi. Kuna sababu mbalimbali za huu ubora duni wa tabia, kama vile uharibifu wa mawazo na maadili ya binadamu, na kutokuwa na malezi mazuri; imani za usihiri zilizojaa moyoni mwa mwanadamu; mitindo ya maisha iliyopotoka ambayo imeweka maovu mengi katika sehemu ya ndani kabisa ya moyo wa mwanadamu; ufahamu wa juujuu wa utamaduni, na takribani asilimia tisini na nane ya watu ambao hawana elimu ya utamaduni na, aidha, watu wachache sana wanaopata viwango vya juu vya elimu ya utamaduni. Kwa hivyo, kimsingi watu hawajui ni nini maana ya Mungu au Roho, bali wana taswira hafifu ya Mungu na isiyoeleweka vizuri kama iliyopatikana kutoka kwa imani ya usihiri. Ushawishi wenye madhara ambao maelfu ya miaka ya “roho wa juu sana wa utaifa” umeacha ndani kabisa ya moyo wa mwanadamu pamoja na fikira za kikabaila ambazo watu wamefungwa nazo na kutiwa minyororo, bila uhuru wowote, na kusababisha watu kutokuwa na hamasa au ustahimilivu, hawana shauku ya kusonga mbele, lakini badala yake wanakuwa baridi na kurudi nyuma, wakiwa na akili ya utumwa ambayo ina nguvu sana, na kadhalika—sababu hizi zimetengeneza taswira chafu na mbaya kwa mitazamo ya njozi, mawazo, maadili, na tabia ya binadamu. Inaonekana, wanadamu wanaishi katika dunia ya giza la kutisha, na hakuna anayetafuta kusonga mbele miongoni mwao, hakuna anayefikiria kwenda katika ulimwengu ulio bora, badala yake, wanaridhika na waliyo nayo maishani, kutumia siku zao kuzaa na kuwalea watoto, wakikazana, wakitoka jasho, wakifanya kazi zao, wakiwa na njozi ya kuwa na familia ya raha na yenye furaha, ya upendo wa ndoa, ya watoto wenye upendo, ya maisha yenye furaha katika miaka yao ya uzeeni wanapoishi kwa kudhihirisha maisha yao kwa amani. … Kwa makumi, maelfu, makumi ya maelfu ya miaka hadi sasa, watu wamekuwa wakipoteza muda wao kwa njia hii, hakuna anayetengeneza maisha makamilifu, wanapigana tu wenyewe kwa wenyewe katika ulimwengu huu wa giza, wakipambana kupata umaarufu na utajiri, na kufanyiana njama wao kwa wao. Nani amewahi kutafuta mapenzi ya Mungu? Kuna mtu yeyote aliyewahi kutilia maanani kazi ya Mungu? Sehemu hizi zote za binadamu zinazomilikiwa na ushawishi wa giza zimekuwa asili ya mwanadamu tangu zamani, kwa hiyo ni vigumu sana kutekeleza kazi ya Mungu na hata watu hawana moyo wa kuzingatia kile ambacho Mungu amewaaminia leo. Vyovyote vile, Ninaamini kwamba watu hawatajali Ninapotamka maneno haya kwa vile kile Ninachokisema ni historia ya maelfu ya miaka. Kuzungumza juu ya historia kuna maana ya ukweli na, zaidi ya hayo, kashfa zinazojulikana kwa wote, sasa kuna maana gani kuzungumza kitu ambacho ni kinyume na ukweli? Lakini pia Naamini kwamba watu wenye akili, wanapoona maneno haya, wataamka na kujitahidi kwa ajili ya kuendelea mbele. Mungu hutumaini kwamba wanadamu wanaweza kuishi na kufanya kazi kwa amani na kuridhika huku wakati ule ule wakiweza kumpenda Mungu. Ni mapenzi ya Mungu kwamba binadamu wote waweze kuingia katika raha; zaidi ya hili, kuijaza nchi yote na utukufu wa Mungu ni shauku kubwa ya Mungu. Ni aibu tu kwamba wanadamu husalia katika hali ya kusahauliwa kabisa na wasiotambua mambo, waliopotoshwa vibaya sana na Shetani hivi kwamba leo hawafanani tena na binadamu. Kwa hiyo mawazo ya binadamu, uadilifu na elimu huunda kiungo muhimu, pamoja na mafunzo katika kujua kusoma na kuandika utamaduni yakiunda kiungo cha pili, bora zaidi ya kuinua ubora wa tabia wa utamaduni wa binadamu na kubadilisha mtazamo wao wa kiroho.

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Kazi na Kuingia (3)

Maneno ya Mungu ya Kila Siku (Dondoo 308)

Katika uzoefu wa watu katika maisha yao, mara nyingi wao hufikiria, nimetoa familia yangu na ajira yangu kwa Mungu, na Amenipa nini? Lazima niongezee na kuthibitisha haya—je, nimepokea baraka zozote hivi majuzi? Nimetoa mengi sana wakati huu, nimekimbia na kukimbia na kuteseka sana—je, Mungu amenipa ahadi zozote baada ya haya? Je, Amekumbuka matendo yangu mazuri? Mwisho wangu utakuwa vipi? Ninaweza kuzipokea baraka za Mungu? … Kila mtu kila wakati hufanya hesabu kama hizi ndani ya moyo wake, na yeye hutoa madai yake kwa Mungu yanayoonyesha motisha yake, malengo na mawazo ya mabadilishano. Hii ni kusema, ndani ya moyo wake mwanadamu siku zote humweka Mungu majaribuni, siku zote anaunda njama kumhusu Mungu, akijitetea kwa Mungu kila wakati kwa sababu ya mwisho wake binafsi na kujaribu kumfanya Mungu atoe kauli, aweze kuona kama Mungu anaweza kumpa kile anachotaka au la. Wakati huohuo akimfuata Mungu, binadamu hamchukulii Mungu kama Mungu. Siku zote mwanadamu amejaribu kufanya mipango na Mungu, akitoa madai bila kusita kwake Yeye na hata akimsukuma Yeye katika kila hatua, akijaribu kupiga hatua ya maili licha ya kupewa inchi moja. Wakati huohuo akijaribu kufanya mabadilishano na Mungu, binadamu pia anabishana na Yeye, na wapo hata watu ambao, wakati majaribu yanawapata au wanapojipata katika hali ya kuteketea, mara nyingi wanakuwa wanyonge, wananyamaza na kuzembea katika kazi yao, na wanajaa malalamiko kumhusu Mungu. Tangu wakati ambapo mwanadamu alianza kumwamini Mungu, amemchukulia Mungu kama alama ya pembe inayoonyesha wingi wa neema, kisu cha Kijeshi cha Uswisi, na amejichukulia yeye mwenyewe kuwa mdaiwa mkubwa zaidi wa Mungu, ni kana kwamba kujaribu kupata baraka na ahadi kutoka kwa Mungu ni haki na jukumu lake la asili, huku jukumu la Mungu likiwa ni kumlinda na kumtunza mwananadamu na kumruzuku. Huu ndio ufahamu wa kimsingi wa “imani katika Mungu” wa wale wote wanaomwamini Mungu, na ufahamu wao wa kina zaidi wa dhana ya imani katika Mungu. Kutoka katika kiini cha asili ya mwanadamu hadi katika ufuatiliaji wake wa kibinafsi, hakuna kitu chochote kinachohusiana na kumcha Mungu. Nia ya mwanadamu katika kumwamini Mungu huenda isiwe na uhusiano na kumwabudu Mungu. Hivi ni kusema kwamba, mwanadamu hajawahi kufikiria wala kuelewa kwamba imani katika Mungu inahitaji kumcha Mungu, na kumwabudu Mungu. Kwa mujibu wa haya yote, kiini cha mwanadamu kiko wazi. Kiini hiki ni kipi? Ni kwamba moyo wa mwanadamu ni mwovu, unaficha udanganyifu na ujanja, haupendi mambo ya kutopendelea na haki na kile kilicho chanya, nao ni wenye kustahili dharau na ulafi. Moyo wa mwanadamu umemfungia Mungu nje sana, hajampa Mungu moyo wake kabisa. Mungu hajawahi kuona moyo wa kweli wa mwanadamu, wala hajawahi kuabudiwa na mwanadamu. Haijalishi jinsi gharama ambayo Mungu amelipia ilivyo kubwa, au ni kiasi kipi cha kazi Anachofanya, au ni kiwango kipi Anachompa mwanadamu, mwanadamu anabakia yule asiyeona hayo yote, na hajali kuyahusu. Mwanadamu hajawahi kumpa Mungu moyo wake, anataka tu kuujali moyo wake yeye mwenyewe, kufanya uamuzi wake mwenyewe—sababu ikiwa kwamba mwanadamu hataki kufuata njia ya kumcha Mungu na kujiepusha na maovu, au kutii ukuu na mipangilio ya Mungu, wala hataki kumwabudu Mungu kama Mungu. Hivyo ndivyo hali ya mwanadamu ilivyo leo.

Neno, Vol. 2. Kuhusu Kumjua Mungu. Kazi ya Mungu, Tabia ya Mungu, na Mungu Mwenyewe II

Maneno ya Mungu ya Kila Siku (Dondoo 309)

Je, si watu wengi humpinga Mungu na kuzuia kazi ya Roho Mtakatifu kwa sababu hawajui kazi mbalimbali na tofautitofauti ya Mungu, na, zaidi ya hayo, kwa sababu wanamiliki maarifa na mafundisho duni ya kupima kazi ya Roho Mtakatifu? Ingawa uzoefu wa watu kama hawa ni wa juujuu tu, ni wenye majivuno na wadekezi katika asili yao, na wanatazama kazi ya Roho Mtakatifu kwa dharau, wanapuuza masomo ya Roho Mtakatifu na, hata zaidi, wanatumia hoja zao ndogo ndogo zee kudhibitisha kazi ya Roho Mtakatifu. Pia wanajifanya, na wanashawishika kabisa na elimu yao na maarifa yao, na kuwa wanaweza kusafiri duniani kote. Je, watu hawa si ni wale wanaochukiwa na kukataliwa na Roho Mtakatifu na je, si wataondolewa na enzi mpya? Je, si wale wanaokuja mbele ya Mungu na kumpinga waziwazi ni watu wadogo wasiojua na wasio na habari ya kutosha jinsi na wanajaribu kuonyesha walivyo werevu? Kwa maarifa haba ya Biblia, wanajaribu kupotosha “wasomi”; wa dunia, kwa mafundisho duni ya dini ili kuwafunza watu, wanajaribu kurudisha nyuma kazi ya Roho Mtakatifu, na kujaribu kuifanya ihusu mchakato wao wanavyofikiria, na kwa kuwa hawaoni mbali, wanajaribu kuona kwa mtazamo mmoja miaka 6,000 ya kazi ya Mungu. Watu hawa hawana mantiki yoyote hata kidogo! Kwa kweli, maarifa ya watu kumhusu Mungu yanavyozidi kuwa mengi, ndivyo wanavyokuwa wagumu wa kuhukumu kazi Yake. Zaidi ya hayo, wanazungumzia tu machache kuhusu maarifa yao ya kazi ya Mungu leo, lakini si wepesi wa kuhukumu. Kadri watu wanavyojua machache kumhusu Mungu, ndivyo wanavyozidi kuwa wenye majivuno na wenye kujiamini sana, na ndivyo wanavyozidi kutangaza nafsi ya Mungu kwa utundu—ilhali wanazungumzia tu nadharia, na wala hawapeani ushahidi wowote halisi. Watu kama hawa hawana thamani yoyote kabisa. Wale wanaoona kazi ya Roho Mtakatifu kama mchezo ni wenye upuzi! Wale wasio waangalifu wanapokumbana na kazi mpya ya Roho Mtakatifu, wanaopayuka, ni wepesi wa kuhukumu wanaoruhusu silika yao ya kiasili kukana haki ya kazi ya Roho Mtakatifu, na pia kuitusi na kuikufuru—je, watu hawa wasio na heshima si ni wale wasiojua kazi ya Roho Mtakatifu? Je, si wao ndio, zaidi ya hayo, wale wasiojua, wenye majivuno ya asili na wasioweza kutawalwa? Hata ikiwa siku itakuja ambapo watu hawa watakubali kazi mpya ya Roho Mtakatifu, bado Mungu hatawavumilia. Hawadharau tu wale wanaofanya kazi ya Mungu, bali pia wanamkufuru Mungu Mwenyewe. Watu kama hawa jasiri pasi na hadhari hawatasamehewa, katika enzi hii ama enzi itakayokuja na wataangamia kuzimuni milele! Watu kama hawa wasio na heshima, wenye kujifurahisha, wanajifanya kuwa wanamwamini Mungu, na kadiri wanavyozidi kufanya vile, ndivyo wanavyozidi kukosea amri za utawala wa Mungu. Je, si hao mafidhuli ambao kiasili hawazuiliki, na hawajawahi kumtii yeyote, wote hupitia njia hii? Je, si wao humpinga Mungu siku baada ya siku, Yeye ambaye daima huwa mpya na wala hazeeki?

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Kujua Hatua Tatu za Kazi ya Mungu Ndiyo Njia ya Kumjua Mungu

Maneno ya Mungu ya Kila Siku (Dondoo 310)

Maarifa ya utamaduni wa kale na historia ambayo imekuwepo kwa maelfu kadhaa ya miaka imefunga fikra na mawazo na akili yake mwanadamu kwa nguvu sana kiasi cha kuzifanya kutowezakana kupenyezwa na kutoweza kuoza.[1] Watu wanaishi katika duara la kumi na nane la kuzimu, kana kwamba wamefukuziwa chini na Mungu, wasiweze kuona mwanga tena. Fikra za kishirikina hivyo zimewakandamiza watu kiasi kwamba hawawezi kupumua na wana shida ya kupumua. Hawana nguvu hata kidogo ya kupinga, kimya kimya wanaendelea kuvumilia na kuvumilia... Hakuna hata mmoja aliyewahi kujaribu kupigana au kusimama kwa ajili ya uadilifu na haki; watu wanaishi maisha ambayo ni mabaya zaidi ya mnyama, chini ya kugongwa na unyanyasaji wa maadili ya kishirikina, siku baada ya siku na mwaka baada ya mwaka. Wanadamu hajawahi kufikiria kumtafuta huyu Mungu ili kufurahia furaha katika ulimwengu wa mwanadamu. Ni kana kwamba mwanadamu amepigwa, kama majani yaliyoanguka ya majira ya kupukutika, yaliyonyauka na kukauka kabisa. Mwanadamu amepoteza kumbukumbu na anaishi bila matumaini kuzimu kwa jina la ulimwengu wa kibinadamu, akisubiri ujio wa siku ya mwisho ili kwamba waweze kupotea pamoja na kuzimu, kana kwamba siku ya mwisho wanayoitamani sana ni siku watakayofurahia pumziko la amani. Maadili ya kishirikina yamempeleka mwanadamu “Kuzimu,” hivyo kudhoofisha zaidi uwezo wa mwanadamu wa kupinga. Ukandamizaji wa aina mbalimbali umemlazimisha mwanadamu taratibu kuzama chini kabisa Kuzimu na kutanga mbali kabisa na Mungu. Sasa, Mungu Amekuwa mgeni kabisa kwa mwanadamu, na mwanadamu bado anafanya haraka kumwepuka wanapokutana. Mwanadamu hamtilii maanani na anamtenga kana kwamba mwanadamu hajawahi kumwona hapo kabla. Bado Mungu amekuwa mwenye subira kwa mwanadamu wakati wote katika safari ndefu ya maisha ya binadamu, kamwe harushi ghadhabu Yake isiyoweza kusitishwa kwake, Amekuwa Akisubiri tu kimya tu, bila kunena lolote, kwa mwanadamu kutubu na kuanza upya. Mungu zamani alikuja kwenye ulimwengu wa binadamu na Huvumilia mateso hayo hayo kama mwanadamu. Ameishi na mwanadamu kwa miaka mingi na hakuna aliyegundua kuwepo Kwake. Mungu huvumilia tu kwa kimya taabu ya uchakavu katika ulimwengu wa binadamu huku Akifanya kazi Aliyoleta yeye mwenyewe. Anaendelea kuvumilia kwa ajili ya mapenzi ya Mungu Baba na kwa ajili ya mahitaji ya wanadamu, Amevumilia, Akipitia maumivu ambayo kamwe mwanadamu hajawahi kupitia. Mbele ya mwanadamu, Amewahudumia kimya kimya na kujinyenyekeza Mwenyewe, kwa ajili ya mapenzi ya Mungu Baba na mahitaji ya wanadamu. Maarifa ya utamaduni wa kale kwa taratibu yamemwondoa mwanadamu kutoka katika uwepo wa Mungu na kumweka mwanadamu kwa mfalme wa mashetani na wana wake. Vitabu Vinne na Maandiko Matano Bora[a] vimepeleka fikira za mwanadamu na mawazo yake katika enzi nyingine ya uasi, na kumfanya mwanadamu kuendelea kuwaabudu wale walioandika Vitabu hivyo na Maandiko ya Kiyunani, wakikuza zaidi mitazamo yao juu ya Mungu. Kwa ukosefu wa kujua wa mwanadamu, mfalme wa mashetani bila huruma alimtupa Mungu nje ya moyo wake na kuumiliki yeye mwenyewe kwa furaha ya ushindi tangu wakati huo, mwanadamu akawa na roho mbaya na ya uovu akiwa na uso wa mfalme wa mashetani. Chuki juu ya Mungu ilijaza kifua chao na sumu ya mfalme wa mashetani ikasambaa ndani ya mwanadamu hadi alipomalizwa kabisa. Mwanadamu hakuwa tena hata na chembe ya uhuru na hakuwa na njia ya kujikwamua kutokana na taabu za mfalme wa mashetani. Hakuwa na budi ila kuchukuliwa mateka papo hapo, kujisalimisha na kuanguka chini kwa kutii mbele yake. Hapo zamani, wakati moyo na nafsi ya mwanadamu vilikuwa vichanga, mfalme wa mashetani alipanda ndani yake mbegu ya saratani ya ukanaji Mungu ndani ya moyo mchanga wa mwanadamu, akimfundisha mwanadamu dhana za uongo kama vile, “kujifunza sayansi na teknolojia, kutambua Vipengele Vinne vya Usasa, hakuna Mungu duniani.” Si hivyo tu, ametangaza kwa kurudiarudia, “Hebu tujenge makazi mazuri sana kwa kufanya kazi kwa bidii,” akiwaomba wote kujiandaa toka wakiwa watoto kutumikia nchi yao. Mwanadamu amepelekwa mbele yake bila kujitambua, na bila kusita akajichukulia sifa (akimrejelea Mungu akiwa Ameshikilia binadamu mzima katika mikono Yake). Hajawahi kuwa na kuhisi aibu yoyote au kuwa na hisia yoyote ya aibu. Aidha, bila aibu amewanyakua watu wa Mungu na kuwaweka katika nyumba yake, wakati akirukaruka kama panya mezani na kumfanya mwanadamu amwabudu kama Mungu. Ni ujahili kabisa huu Anaropoka tuhuma hizo za kushtua, “Hakuna Mungu duniani. Upepo upo kwa ajili ya sheria za asili; mvua ni unyevunyevu unaoganda na kudondoka chini kama matone; tetemeko la ardhi ni mtikisiko wa uso wa ardhi kwa sababu ya mabadiliko ya jiolojia; ukame ni kwa sababu ya ukavu hewani kwa mwingiliano wa kinyuklia katika uso wa jua. Haya ni matukio ya asili. Ni sehemu gani ambayo ni tendo la Mungu?” Kuna wale hata wanaofoka kauli kama zifuatazo, kauli ambazo hazifai kutamkwa. “Mwanadamu alitoka kwa nyani katika nyakati zilizopita, na dunia leo inatoka kwa mfululizo wa jamii zizizostaarabika kuanzia takribani miaka mingi isiyohesabika. Iwapo nchi inaendelea au inaanguka inaamuliwa na mikono ya watu wake.” Kwa nyuma, inamfanya mwanadamu kuning’iniza kwenye ukuta au kuweka kwa meza ili kutoa heshima na kumtolea sadaka. Wakati huo huo anapiga kelele kwamba “Hakuna Mungu,” anajichukulia mwenyewe kuwa ni Mungu, na kumsukumia mbali Mungu nje ya mipaka ya dunia bila huruma. Anasimama katika sehemu ya Mungu na kutenda kama mfalme wa mashetani. Ni upuuzi mkubwa kiasi gani! Anamsababisha mtu kuteketezwa na chuki yenye sumu. Inaonekana kwamba Mungu ni adui wake mkubwa na Mungu Hapatani naye kabisa. Anafanya hila zake za kumfukuza Mungu wakati anabakia huru na hajapatikana.[2] Huyo kweli ni mfalme wa mashetani! Tunawezaje kuvumilia uwepo wake? Hatapumzika hadi awe ameisumbua kazi ya Mungu na kuiacha katika matambara na kuwa katika hali ya shaghalabaghala kabisa,[3] kana kwamba anataka kumpinga Mungu hadi mwisho, hadi mmoja kati yao awe ameangamia. Anampinga Mungu kwa makusudi na kusogea karibu zaidi. Sura yake ya kuchukiza imefunuliwa toka zamani na sasa imevilia damu na kugongwagongwa,[4] ipo katika hali mbaya sana, lakini bado hapunguzi hasira zake kwa Mungu, kana kwamba anatamani kummeza Mungu kabisa kwa mara moja ili kutuliza hasira moyoni mwake. Tunawezaje kumvumilia, huyu adui wa Mungu anayechukiwa! Ni kumalizwa kwake na kuondolewa kabisa ndiko kutaleta kutimia kwa matamanio yetu ya maisha. Anawezaje kuruhusiwa kuendelea kukimbia ovyoovyo? Amemharibu mwanadamu kwa kiwango kama hicho mwanadamu hajui ’mahali pa raha zote, na amekuja kuwa mfu na asiye na hisia. Mwanadamu amepoteza uwezo wa kawaida wa kufikiri wa kibinadamu. Kwa nini tusitoe nafsi zetu zote kumwangamiza yeye na kumchoma ili kuondoa kabisa hofu yote ya hatari ya siku zijazo na kuruhusu kazi ya Mungu kuufikia uzuri usiotarajiwa mapema? Genge hili la waovu limekuja katika dunia ya wanadamu na kusababisha hofu na shida kubwa. Wamewaleta wanadamu wote katika ukingo wa jabali, wakipanga kwa siri kuwasukumia chini wavunjike vipande vipande na kumeza maiti zao. Wana matumaini ya kuharibu mpango wa Mungu na kushindana na Mungu katika pambano ambalo ana nafasi ndogo sana ya kushinda.[5] Hiyo kwa vyovyote vile ni rahisi! Msalaba umeandaliwa, mahususi kwa ajili ya mfalme wa mashetani ambaye ni mwenye hatia ya makosa maovu sana. Mungu si wa msalaba tena na Amekwishamwachia Shetani. Mungu Aliibuka mshindi muda mrefu uliopita, Hahisi tena huzuni juu ya dhambi za binadamu. Ataleta wokovu kwa binadamu wote.

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Kazi na Kuingia (7)

Tanbihi:

1. “Kutoweza kuoza” imenuiwa kama tashtiti hapa, kumaanisha kwamba watu ni wagumu katika ufahamu, utamaduni na mitizamo yao ya kiroho.

2. “Huru na hajapatikana” inaonyesha kwamba shetani anapagawa na kucharuka.

3. “Hali ya shaghalabaghala kabisa” inahusu jinsi tabia ya shetani ya ukatili haivumiliki kuona.

4. “Imevilia damu na kugongwagongwa” inahusu sura mbaya ya kutisha ya mfalme wa pepo.

5. “Pambano ambalo ana nafasi ndogo sana ya kushinda” ni istiara ya mipango mibaya ya shetani yenye kudhuru kwa siri, ya uovu. Inatumiwa kwa dhihaka.

a. Vitabu Vinne na Maandiko Matano Boara ni vitabu vyenye mamlaka ya Ukonfushashi nchini China.

Maneno ya Mungu ya Kila Siku (Dondoo 311)

Kutoka juu hadi chini na kutoka mwanzo hadi mwisho, Shetani amekuwa akivuruga kazi ya Mungu na kutenda katika upinzani Kwake. Mazungumzo yote ya “urithi wa utamaduni wa kale,” “maarifa ya thamani ya utamaduni wa kale,” “mafundisho ya imani ya Tao na imani ya Confucius,” na “maandiko ya kale ya Confucius na ibada ya kishirikina” vimempeleka mwanadamu kuzimu. Sayansi na teknolojia ya kisasa, vilevile maendeleo ya viwanda, kilimo, na biashara havionekeni popote. Badala yake, anasisitiza ibada za kishirikina zilizoenezwa na “masokwe” wa kale kwa makusudi kabisa kuingilia, kupinga na kuharibu kazi ya Mungu. Sio tu amemtesa mwanadamu hadi leo hii, bali anataka kummaliza[1] mwanadamu kabisa. Mafundisho ya maadili ya kishirikina na kurithisha maarifa ya utamaduni wa kale vimemwambukiza mwanadamu kwa muda mrefu na kumbadilisha mwanadamu kuwa mashetani wakubwa na wadogo. Kuna wachache sana ambao wapo tayari kumpokea Mungu na kukaribisha kwa furaha ujio wa Mungu. Uso wa mwanadamu umejawa na mauaji, na katika sehemu zote, kifo kipo hewani. Wanatafuta kumwondoa Mungu katika nchi hii; wakiwa na visu na mapanga mikononi, wanajipanga katika pambano kumwangamiza Mungu. Sanamu zimetapakaa nchi nzima ya shetani ambapo mwanadamu anafundishwa kuwa hakuna Mungu. Juu ya nchi hii kunatoka harufu mbaya sana ya karatasi linaloungua na ubani, ni harufu nzito sana inayomaliza hewa. Inaonekana kuwa ni harufu ya uchafu unaopeperuka wakati joka anapojisogeza na kujizungusha, na ni harufu ambayo mwanadamu hawezi kuvumilia bali kutapika tu. Licha ya hiyo, kunaweza kusikika pepo waovu wakikariri maandiko. Sauti inaonekana kutoka mbali kuzimu, na mwanadamu hawezi kujizua kusikia baridi ikiteremka chini ya uti wake. Katika nchi hii sanamu zimetapakaa, zikiwa na rangi zote za upinde wa mvua, ambazo zinaibadilisha nchi kuwa ulimwengu ya furaha ya kutamanisha, wakati mfalme wa mashetani ameendelea kucheka vibaya, kana kwamba njama zake za kupotosha zimefanikiwa. Wakati huo mwanadamu hana habari naye, wala mwanadamu hajui kwamba shetani amekwishamharibu kwa kiwango ambacho amekuwa hawezi kuhisi na ameshindwa. Anatamani, kwa kishindo, kuangamiza kila kitu kuhusu Mungu, na kwa mara nyingine kuchafua na kumwangamiza; nia yake ni kubomoa na kuvunja kazi Yake. Anawezaje kumruhusu Mungu kuwa wa hadhi sawa? Anawezaje kumvumilia Mungu “akiingilia” na kazi yake miongoni mwa wanadamu ulimwenguni? Anawezaje kumruhusu Mungu kuufichua uso wake wa kutisha? Anawezaje kumruhusu Mungu kuingilia kazi yake? Inawezekanaje Shetani huyu anayevimba kwa ghadhabu, amruhusu Mungu kuwa na utawala juu ya mahakama yake ya kifalme duniani? Anawezaje kukubali kushindwa kwa urahisi? Sura yake ya chuki imefunuliwa wazi, hivyo mtu anajikuta hajui kama acheke au alie, na ni vigumu sana kuzungumzia hili. Hii si asili yake? Akiwa na roho mbaya, bado anaamini kwamba yeye ni mzuri kupita kiasi. Genge hili la washiriki jinai![2] Wanakuja miongoni mwa walio na mwili wa kufa na kuendeleza starehe na kuvuruga mpangilio. Usumbufu wao unaleta kigeugeu duniani na kusababisha hofu katika moyo wa mwanadamu, na wamemchezea mwanadamu sana kiasi kwamba mwonekano wake umekuwa ule wa mnyama wa mashambani, mbaya sana, na kutoka athari ya mwisho ya mwanadamu asilia imepotea. Aidha, wanatamani kuwa wa nguvu za ukuu duniani. Wanakwamisha kazi ya Mungu kiasi kwamba isiweze kusonga mbele kiasi kidogo na wanamfunga mwanadamu kwa mkazo kama wapo nyuma ya kuta za shaba na chuma cha pua. Baada ya kufanya dhambi mbaya sana na kusababisha majanga mengi sana, je, bado wanatarajia kitu tofauti na kuadibu? Mapepo na roho wa Shetani wamekuwa wakicharuka duniani na wamefunga mapenzi na jitihada za maumivu za Mungu, na kuwafanya wasiweze kupenyeka. Ni dhambi ya mauti kiasi gani! Inawezekanaje Mungu Asiwe na wasiwasi? Inawezekanaje Mungu Asiwe na ghadhabu? Wanasababisha vikwazo vya kusikitisha na upinzani kwa kazi ya Mungu. Uasi wa kutisha! Hata mapepo hao wadogo kwa wakubwa wanajivunia nguvu za Shetani mwenye nguvu zaidi na kuanza kufanya fujo. Kwa makusudi wanapinga ukweli licha ya kuuelewa vizuri. Wana wa uasi! Ni kana kwamba, sasa mfalme wao amepanda kwenda katika kiti cha enzi cha kifalme, wamekuwa wa kuridhika nafsi na kuwatendea wengine wote kwa dharau. Ni wangapi wanautafuta ukweli na kufuata haki? Wote ni wanyama kama tu nguruwe na mbwa, wakuongoza genge la nzi wanaonuka katika rundo la kinyesi na kuchomeka vichwa vyao na kuchochea vurugu.[3] Wanaamini kwamba mfalme wao wa kuzimu ni mkuu kuliko mfalme wa wote, kujua kidogo kwamba wao si zaidi ya nzi wenye uvundo. Na bado, wanatumia vibaya uwezo wa nguruwe na mbwa ambao ni wazaziwe ili kukashifu uwepo wa Mungu. Kama nzi wadogo, wanaamini wazazi wao ni wakubwa kama nyangumi wenye meno.[4] Hawatambui kwamba wao ni wadogo sana, ilihali wazazi wao ni nguruwe wachafu mara mamia ya mamilioni kuliko wao wenyewe kwa ukubwa? Hawatambui uduni wao, wanacharuka kwa misingi ya harufu iliyooza ya nguruwe na mbwa hao na wana mawazo ya udanganyifu ya kuzaa vizazi vijavyo. Huko ni kukosa aibu kabisa! Wakiwa na mbawa za kijani mgongoni mwao (hii inarejelea wao kudai kuwa wanamwamini Mungu), wanaanza kuwa na majivuno na kiburi juu ya uzuri wao na mvuto wao, kwa siri kabisa wanamtupia mwanadamu uchafu wao. Na hata ni wa kuridhika nafsi, kana kwamba jozi ya mbawa zenye rangi ya upinde wa mvua zingeweza kuficha uchafu wao, na kwa njia hizi wanaleta ukandamizaji kwa uwepo wa Mungu wa kweli (hii inarejelea yale yanayoendelea kwa nyuma katika ulimwengu wa kidini). Ni jinsi gani mwanadamu angejua kwamba, licha ya urembo mzuri wa mbawa za nzi, nzi mwenyewe ni kiumbe mdogo tu, aliye na tumbo iliyojaa uchafu na mwili uliojaa vijidudu? Kwa kutegemea uwezo wa nguruwe na mbwa wa wazazi wao, wanacharuka nchi nzima (hii inarejelea viongozi wa dini wanaomtesa Mungu kwa misingi ya uungwaji mkono mkubwa kutoka katika nchi inayomsaliti Mungu wa kweli na ukweli) kwa ukatili uliopitiliza. Ni kana kwamba mizimu ya Mafarisayo wa Kiyahudi wamerudi pamoja na Mungu katika nchi ya joka kuu jekundu, wamerudi katika kiota chao cha zamani. Wameanza tena mkondo mwingine wa usaliti, wakianzisha kazi yao yenye miaka maelfu kadhaa iliyopita. Kikundi hiki cha waliopotoka ni hakika kitaangamia duniani hatimaye! Inaonekana kwamba, baada ya milenia kadhaa, roho wachafu wamekuwa wenye hila na wadanganyifu sana. Muda wote wanafikiri juu ya njia za kuidhoofisha kazi ya Mungu kwa siri. Ni werevu sana na wajanja na wanatamani kurudia katika nchi yao kufanya majanga yaliyotokea maelfu kadhaa ya miaka iliyopita. Hii takribani imfanye Mungu kulia kwa sauti kuu, na Anajizuia sana kurudi katika mbingu ya tatu ili Awaangamize. Kwa mwanadamu kumpenda Mungu ni lazima aelewe mapenzi Yake na furaha Yake na huzuni, vilevile na kile Anachokichukia zaidi. Hii itakuza zaidi kuingia kwa mwanadamu. Kadiri mwanadamu anavyoingia kwa haraka, ndivyo moyo wa Mungu unavyoridhika zaidi; kadiri mwanadamu anavyomtambua kwa uwazi mfalme wa mashetani, ndivyo mwanadamu anavyosogea karibu zaidi na Mungu, ili kwamba matamanio Yake yaweze kutimia.

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Kazi na Kuingia (7)

Tanbihi:

1. “Kummaliza” inahusu tabia ya kidhalimu ya mfalme wa pepo, ambaye huwaangamiza watu wote.

2. “Washiriki jinai” ni wa namna moja na “kundi la majambazi.”

3. “Nyangumi wenye meno” inahusu jinsi watu ambao wana pepo husababisha ghasia, kuzuia na kuipinga kazi ya Mungu.

4. “Nyangumi mwenye meno” imetumiwa kwa dhihaka. Ni istiara ya jinsi nzi ni wadogo sana kiasi kwamba nguruwe na mbwa huonekana wakubwa kama nyangumi kwao.

Maneno ya Mungu ya Kila Siku (Dondoo 312)

Kwa maelfu ya miaka hii imekuwa ni nchi ya uchafu, ni chafu sana, shida zimejaa, mizimu wanakimbia kila mahali, wakihadaa na kudanganya, wakitoa tuhuma zisizokuwa na msingi,[1] wakiwa katili na waovu, wakikandamiza mji huu ulio mahame na kuuacha ukiwa umetapakaa maiti; harufu ya uozo inaijaza nchi na kuenea hewani, na inalindwa isivyo kawaida.[2] Nani awezaye kuuona ulimwengu kupita anga? Ibilisi anaufunga mwili wote wa mwanadamu, anafumba macho yake yote, na kufunga kinywa chake kwa nguvu. Mfalme wa pepo amefanya ghasia kwa maelfu kadhaa ya miaka, hadi leo hii, wakati bado anaangalia kwa karibu mji ulio mahame kana kwamba ulikuwa kasiri la pepo lisilopenyeka; kundi hili la walinzi, wakati uo huo, wakiangalia kwa macho yanayong’aa, wakiogopa sana kwamba Mungu atawakamata bila wao kujua na kuwafutilia wote mbali, Akiwaacha wakiwa hawana sehemu ya amani na furaha. Inawezekanaje watu wa mji wa mahame kama huu wawe wamewahi kumwona Mungu? Je, wamekwishawahi kufurahia uzuri na upendo wa Mungu? Wanathamini vipi masuala ya ulimwengu wa kibinadamu? Ni nani miongoni mwao anayeweza kuelewa matakwa ya kina ya Mungu? Haishangazi, basi, kwamba Mungu mwenye mwili abaki kuendelea kuwa Amefichwa: Katika jamii ya giza kama hii, ambapo pepo hawana huruma na ni katili, inawezekanaje mfalme wa pepo anayeua watu bila hisia yoyote, avumilie uwepo wa Mungu ambaye ni mwenye upendo, mpole, na mtakatifu? Anawezaje kushangilia na kufurahia ujio wa Mungu? Vikaragosi hawa! Wanalipa upole kwa chuki, wanamtweza Mungu kwa muda mrefu, wanamtukana Mungu, ni washenzi kupita kiasi, hawamjali Mungu hata kidogo, wanapora na kuteka nyara, wamepoteza dhamiri yote, wanaenda kinyume na dhamiri yote, na wanawajaribu watu wasiokuwa na hatia kuwa watu wasiokuwa na uwezo wa kuhisi. Wazazi wa kale? Viongozi Wapendwa? Wote wanampinga Mungu! Udukuzi wao umeacha wote walio chini ya mbingu katika hali ya giza na machafuko! Uhuru wa dini? Haki halali na matakwa ya wananchi? Zote hizo ni njama za kufunika dhambi! Nani ambaye ameikumbatia kazi ya Mungu? Nani ametoa maisha yake au kumwaga damu kwa ajili ya kazi ya Mungu? Kwa kizazi baada ya kizazi, kutoka kwa wazazi hadi watoto, mwanadamu aliyepo katika utumwa bila heshima amemfanya Mungu mtumwa—hii inawezaje kukosa kuamsha hasira? Maelfu ya miaka ya chuki ikiwa imejaa kifuani, milenia ya dhambi imeandikwa katika moyo—inawezekanaje hii isichochee chuki? Kumlipiza Mungu, kuuondoa kabisa uadui wake, usimwache kutangatanga tena, na usimruhusu kufanya fujo zaidi kama anavyotaka! Sasa ndio wakati: Mwanadamu ana muda mrefu tangu akusanye nguvu zake zote, amejitolea nguvu zake zote, amelipa kila gharama, kwa hili, kuchana uso uliojificha wa pepo hili na kuwafanya watu, ambao wamepofushwa na kuvumilia kila aina ya mateso na taabu, kuinuka kutoka katika maumivu na kurudi kwa ibilisi huyu wa zamani. Kwa nini uweke kikwazo hicho kisichopenyeka katika kazi ya Mungu? Kwa nini utumie hila mbalimbali kuwadanganya watu wa Mungu? Uhuru wa kweli na haki na matakwa halali vipo wapi? Usawa uko wapi? Faraja iko wapi? Wema upo wapi? Kwa nini utumie mbinu za hila kuwadanganya watu wa Mungu? Kwa nini utumie nguvu kukandamiza ujio wa Mungu? Kwa nini usimruhusu Mungu kuzunguka katika dunia ambayo Ameiumba? Kwa nini umsumbue Mungu hadi Anakosa sehemu ya kupumzisha kichwa Chake? Wema upo wapi miongoni mwa wanadamu? Ukarimu upo wapi miongoni mwa wanadamu? Kwa nini usababishe matamanio makubwa kiasi hicho kwa Mungu? Kwa nini umfanye Mungu kuita tena na tena? Kwa nini umlazimishe Mungu kuwa na wasiwasi kwa sababu ya Mwana Wake mpendwa? Katika jamii hii ya giza, kwa nini mbwa wao walinzi wasimruhusu Mungu kuja bila kizuizi na kuzunguka dunia ambayo Aliiumba? Kwa nini mwanadamu haelewi, mwanadamu anayeishi katika maumivu na mateso? Mungu amevumilia mateso makubwa kwa ajili yenu, kwa maumivu makubwa Amemtoa Mwanawe wa pekee, mwili wake na damu, kwa ajili yenu, sasa kwa nini bado mnakuwa vipofu? Katika mtazamo mzima wa kila mtu, mnakataa ujio wa Mungu, na mnakataa urafiki wa Mungu. Kwa nini mnakosa busara kiasi hicho? Mko tayari kuvumilia uonevu katika jamii ya giza kama hii? Kwa nini, badala ya kujaza tumbo lenu kwa milenia ya uadui, mnajidanganya wenyewe kwa “kinyesi” cha mfalme wa pepo?

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Kazi na Kuingia (8)

Tanbihi:

1. “Wakitoa tuhuma zisizokuwa na msingi” inahusu mbinu ambazo ibilisi hutumia huwadhuru watu.

2. “Inalindwa isivyo kawaida” inaonyesha kuwa mbinu ambazo ibilisi hutumia huwatesa watu ni mbovu hasa, na kuwadhibiti watu sana kiasi kwamba hawana nafasi ya kusogea.

Maneno ya Mungu ya Kila Siku (Dondoo 313)

Ikiwa watu wanaweza kweli kuiona vizuri njia sahihi ya maisha ya binadamu na vilevile kusudi la usimamizi wa Mungu wa binadamu, wasingeshikilia mategemeo yao ya baadaye na majaliwa yao binafsi kama hazina mioyoni mwao. Kisha wasingetataka tena kuwatumikia wazazi wao, ambao ni wabaya zaidi kuliko nguruwe na mbwa. Je, mustakabali na majaliwa ya mwanadamu si hasa wale wanaodaiwa kuwa “wazazi” wa Petro wa wakati wa sasa? Yamekuwa tu kama mwili na damu ya mwanadamu. Je, hatima na mustakabali wa mwili utakuwa upi hasa? Je, utakuwa kumwona Mungu wakati ukiwa ungali hai, au kwa roho kukutana na Mungu baada ya kifo? Je, kesho mwili utaishia katika tanuu kuu ya taabu, au katika moto mkubwa? Je, si maswali kama haya yanahusu iwapo mwili wa mwanadamu utahimili taabu au utavumilia habari kubwa sana ambayo kila mtu aliye katika mkondo huu wa sasa ambaye ana akili na ni mwenye busara anayahangaika? (Hapa, kuteseka kunarejelea kupokea baraka; kunamaanisha kwamba majaribu ya siku zijazo ni yenye manufaa kwa hatima ya mwanadamu. Taabu hurejelea kushindwa kusimama imara, au kudanganywa; au, kunamaanisha kwamba mtu atakumbana na hali za bahati mbaya na kupoteza maisha ya mtu katikati ya majanga, na kwamba hakuna hatima nzuri kwa roho wa mtu.) Ingawa wanadamu wana mantiki timamu, pengine kile wanachofikiri hakifanani kabisa na kile ambacho mantiki yao yanapaswa kuwa nacho. Hii ni kwa sababu wote ni waliochanganyikiwa na wao hufuata vitu bila kufikiri. Wote wanapaswa kuwa na ufahamu wa kina wa kile ambacho wanapaswa kuingia kwacho, na kwa mahususi wanapaswa kutatua kile wanachopaswa kuingia kwacho wakati wa mateso (yaani, wakati wa utakasaji katika tanuu), na vile vile kile wanachopaswa kujiandaa nacho wakati wa majaribu ya moto. Usiwatumikie wazazi wako siku zote (kumaanisha mwili) ambao ni sawa na nguruwe na mbwa na hata ni wabaya zaidi kuliko chungu na wadudu. Kuna haja gani ya kuteseka juu ya hilo, kufikiri sana, na kupiga bongo zako? Mwili si wako, bali upo katika mikono ya Mungu, ambaye kando na kukudhibiti wewe, pia Anamwamuru Shetani. (Hili linamaanisha kuwa kiasili mwili ni wa Shetani. Kwa kuwa Shetani pia yumo mikononi mwa Mungu, inaweza tu kusemwa hivi. Hii ni kwa sababu inashawishi zaidi kusema namna hiyo; inamaanisha kuwa wanadamu hawamilikiwi na Shetani kabisa, bali wamo mikononi mwa Mungu.) Unaishi chini ya mateso ya mwili, lakini, je, mwili ni wako? Uko chini ya udhibiti wako? Kwa nini upige bongo sana juu ya hilo? Kwa nini usumbuke sana kumsihi Mungu kwa ajili ya mwili wako uliooza ambao umeshahukumiwa zamani sana, kulaaniwa na vilevile kutiwa najisi na roho wachafu? Kuna haja gani ya kuwaweka washirika wa Shetani karibu sana na moyo wako? Huna wasiwasi kwamba mwili unaweza kuuharibu mustakabali wako halisi, matumaini yako mazuri, na hatima ya kweli ya maisha yako?

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Kusudi la Kuwasimamia Binadamu

Maneno ya Mungu ya Kila Siku (Dondoo 314)

Leo, kile ambacho mmepata kuelewa ni cha juu zaidi kuliko kile cha mtu yeyote kote katika historia ambaye hakufanywa mkamilifu. Iwe ni ufahamu wenu wa majaribu au imani katika Mungu, vyote ni vya juu zaidi kuliko ya muumini yeyote katika Mungu. Mambo mnayoyafahamu ni yale mnayokuja kujua kabla ya ninyi kupitia majaribu ya mazingira, lakini kimo chenu halisi hakipatani nayo. Kile mnachojua ni cha juu zaidi kuliko kile mnachotia katika vitendo. Ingawa mnasema kwamba watu wanaoamini katika Mungu wanapaswa kumpenda Mungu, na hawapaswi kupania baraka bali kuyaridhisha tu mapenzi ya Mungu, kinachoonekana katika maisha yenu ni tofauti kabisa na hili, na kimewekwa mawaa kabisa. Watu wengi huamini katika Mungu kwa ajili ya amani na manufaa mengine. Isipokuwa kwa manufaa yako, wewe huamini katika Mungu, na ikiwa huwezi kupokea neema za Mungu, wewe huanza kununa. Kile ambacho umesema kingekuwaje kimo chako halisi? Inapofikia matukio ya familia yasiyoepukika kama vile watoto kuwa wagonjwa, wapendwa kulazwa hospitalini, mazao mabaya ya mimea, na kuteswa na watu wa familia, hata mambo haya yanayotokea mara kwa mara, ya kila siku yanakuwa ya kukithiri kwako. Wakati ambapo mambo hayo hufanyika, wewe huingia katika hofu kubwa, hujui la kufanya—na wakati mwingi, wewe hulalamika kuhusu Mungu. Wewe hulalamika kwamba maneno ya Mungu yalikuhadaa, kwamba kazi ya Mungu yalikudhihaki. Je, ninyi hamna mawazo kama haya? Unadhani mambo kama haya hufanyika miongoni mwenu mara chache tu? Mnatumia kila siku kuishi katikati ya matukio kama haya. Hamfikirii hata kidogo sana kuhusu mafanikio ya imani yenu katika Mungu, na namna ya kuyaridhisha mapenzi ya Mungu. Kimo chenu halisi ni kidogo sana, hata kidogo zaidi kuliko cha kifaranga mdogo. Wakati ambapo biashara ya familia zenu hupoteza pesa ninyi hulalamika kuhusu Mungu, wakati ambapo ninyi hujikuta katika mazingira yasiyo na ulinzi wa Mungu ninyi bado hulalamika kuhusu Mungu, na ninyi hulalamika hata wakati ambapo mmoja wa vifaranga wenu hufa au ng’ombe mzee ndani ya zizi anapougua. Ninyi hulalamika kama ni wakati wa wana wenu kufunga ndoa lakini familia yenu haina pesa za kutosha; unataka kutekeleza kazi ya kanisa ya kuwa mwenyeji, lakini huwezi kuimudu, na kisha wewe hulalamika pia. Umejawa na malalamiko, na wakati mwingine huhudhurii mikutano au kula na kunywa maneno ya Mungu kwa sababu ya hili, wakati mwingine wewe huishia kuwa hasi kwa muda mrefu sana. Hakuna chochote kinachokufanyikia leo hii kilicho na uhusiano wowote na matazamio au majaliwa yako; mambo haya yangefanyika pia hata ikiwa hungeamini katika Mungu, ilhali leo hii unampitishia Mungu wajibu wa haya mambo, na kusisitiza kusema kwamba Mungu amekuondosha wewe. Na kuhusu imani yako katika Mungu, je? Umeyatoa maisha yako kwa kweli? Mngepitia majaribu sawa na yale ya Ayubu, hakuna hata mmoja miongoni mwenu anayemfuata Mungu leo hii angeweza kusimama imara, nyote mngeanguka chini. Na kunayo, kawaida kabisa, tofauti kubwa kati ya ninyi na Ayubu. Leo, kama nusu ya mali yenu ingetwaliwa mngethubutu kukana kuwepo kwa Mungu; kama mtoto wenu wa kiume au wa kike angechukuliwa kutoka kwenu, mngekimbia barabarani mkilalamika vikali; kama njia yako ya pekee kupata riziki ingegonga mwamba, ungejaribu kuanza kujadiliana mada hiyo na Mungu; ungeuliza kwa nini Nilisema maneno mengi sana hapo mwanzo kukutisha wewe. Hakuna kitu chochote ambacho hamngethubutu kufanya katika nyakati kama hizi. Hili linaonyesha kwamba hamjapata umaizi wowote wa kweli, na hamna kimo cha kweli. Hivyo, majaribu yaliyo ndani yenu ni makubwa mno, kwani ninyi mnajua mengi sana, lakini kile mnachoelewa kweli si hata sehemu moja kwa elfu ya kile mnachofahamu. Msikome tu kwa ufahamu na maarifa pekee; mngeona vyema kiasi gani mnachoweza kutia katika vitendo kwa kweli, kiasi gani cha nuru na mwangaza wa Roho Mtakatifu kilipatikana kupitia katika jasho la bidii yenu wenyewe, na katika matendo mangapi yenu mmetambua azimio lenu wenyewe. Unapaswa kuchukua kimo chako na kutenda kwa uzito. Katika imani yako kwa Mungu, hupaswi tu kujaribu kufanya mambo kwa namna isiyo ya dhati kwa ajili ya yeyote—kama unaweza hatimaye kupata ukweli na uzima au la hutegemea ufuatiliaji wako mwenyewe.

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Utendaji (3)

Maneno ya Mungu ya Kila Siku (Dondoo 315)

Wengine wanajivika mapambo mazuri, lakini ya juujuu: Kina dada wanajivika mapambo mazuri kama maua, na kina ndugu wanavalia kama wana wa wafalme ama wambuji wadogo matajiri. Wanajali tu kuhusu vitu vya nje, kama vitu wanavyokula na kuvalia; ndani yao, wao ni mafukara na hawamfahamu Mungu hata kidogo. Hili lina maana gani? Na kisha kuna wengine wanaovalia kama waombaji maskini—kweli wanaonekana kama watumwa wa Asia Mashariki! Je, kweli hamwelewi Ninachotaka kutoka kwenu? Shirikini kwa karibu: Mmepata nini kweli? Mmemwamini Mungu kwa miaka hii yote, lakini mmevuna hili tu—je, hamna aibu? Je, hamwoni haya? Mmekuwa mkifuatilia kwenye njia ya kweli kwa miaka hii yote, lakini leo kimo chenu bado ni cha chini kuliko cha jurawa! Watazame mabibi wadogo walio miongoni mwenu, warembo kama picha mkiwa mmevalia mavazi na vipodozi vyenu, mkijilinganisha kati yenu—na ni nini mnacholinganisha? Starehe zenu? Matakwa yenu? Je, mnadhani kwamba Nimekuja kuandikisha waonyesha mitindo? Hamna aibu! Maisha yenu yako wapi? Je, kile mnachokifuatilia si tamaa zilizopita kiasi tu? Unadhani kuwa wewe ni mrembo sana, lakini ingawa umevalia kila aina ya umaridadi, kwa kweli wewe si buu anayegaagaa, aliyezaliwa katika rundo la kinyesi? Leo, huna bahati ya kufurahia baraka hizi za mbinguni kwa ajili ya uso wako mrembo, ila kwa sababu Mungu anafanya jambo la kipekee kwa kukuinua. Je, bado huelewi ulikotoka? Maisha yanapotajwa, unafunga mdomo wako na husemi chochote, na unakimya kama sanamu, lakini bado una ujasiri wa kuvalia vizuri! Bado unataka kupaka uso wako rangi nyekundu na poda! Na watazame wambuji walio miongoni mwenu, wanaume waliopotoka wanaoshinda siku kutwa wakitembea huku na kule polepole, wakaidi, na wenye sura tepetevu usoni pao. Je, hivi ndivyo mtu anapaswa kutenda? Je, kila mmoja kati yenu, awe mwamamume ama mwanamke, anazingatia nini siku nzima? Je, mnajua mnamtegemea nani kujilisha? Tazama mavazi yako, tazama kile ulichovuna mikononi mwako, sugua kitambi chako—umefaidika nini kutoka kwa gharama ya damu na jasho ambayo umelipa katika miaka hii yote ya imani? Bado unafikiri kwenda kutalii sehemu maarufu, bado unafikiri kupamba mwili wako unukao—ufuatiliaji usio na maana! Unaombwa uwe mtu wa kawaida, lakini sasa wewe si mtu asiye wa kawaida tu, wewe ni mpotovu. Mtu kama wewe anawezaje kuwa na ujasiri wa kuja mbele Zangu? Ukiwa na ubinadamu kama huu, ukionyesha uzuri wako na kuringa kwa ajili ya mwili wako, ukiishi daima ndani ya tamaa za mwili—je, wewe si mzao wa mashetani wachafu na pepo waovu? Sitamruhusu shetani mchafu kama huyu aendelee kuishi kwa muda mrefu! Na usifikiri kwamba Sijui kile unachofikiri moyoni mwako. Unaweza kudhibiti vikali tamaa na mwili wako, lakini Nawezaje kukosa kujua fikira zilizo moyoni mwako? Nawezaje kukosa kujua tamaa zote za macho yako? Je, ninyi mabibi wadogo hamjirembeshi sana ili kuonyesha miili yenu? Wanaume wana faida gani kwenu? Je, kweli wanaweza kuwaokoa kutoka katika bahari ya mateso? Na kwa wambuji miongoni mwenu, nyote huvalia ili kujifanya muonekane waungwana na wa heshima, lakini, je, hii si hila iliyokusudiwa kuvuta macho kwa sura zenu changamfu? Mnafanya hili kwa sababu ya nani? Wanawake wana faida gani kwenu? Je, wao si chanzo cha dhambi yenu? Enyi wanaume na wanawake, Nimewaambia maneno mengi sana, lakini mmetii machache tu. Masikio yenu hayataki kusikia, macho yenu yamefifia, na mioyo yenu ni migumu kiasi kwamba kuna tamaa tu katika miili yenu, kiasi kwamba mmetegwa nayo, msiweze kutoroka. Ni nani anayetaka kuwakaribia ninyi mabuu, ninyi mnaojifurukuta katika uchafu na masizi? Msisahau kwamba ninyi tu ni wale Niliowatoa kutoka katika rundo la kinyesi, kwamba mwanzoni hamkuwa na ubinadamu wa kawaida. Ninachotaka kutoka kwenu ni ule ubinadamu wa kawaida ambao hamkuwa nao mwanzoni, si kwamba muonyeshe tamaa zenu ama muachilie miili yenu iliyooza, ambayo imeelekezwa na ibilisi kwa miaka mingi sana. Mnapojivisha nguo hivyo, je, hamwogopi kwamba mtategwa kwa kina zaidi? Je, hamjui kwamba mwanzoni mlikuwa wenye dhambi? Je, hamjui kwamba miili yenu imejaa tamaa sana kiasi kwamba hata inavuja kutoka kwa mavazi yenu, ikifichua hali zenu kama mashetani wabaya na wachafu kukithiri? Je, si kweli kwamba mnajua hili vyema zaidi kuliko yeyote mwingine? Mioyo yenu, macho yenu, midomo yenu—je, si vyote vimenajisiwa na mashetani wachafu? Je, hizi sehemu zenu si chafu? Je, unadhani kwamba alimradi hutendi, basi wewe ndiwe mtakatifu kabisa? Je, unadhani kwamba kuvalia mavazi mazuri kunaweza kuficha nafsi zenu duni? Hilo haliwezekani! Nawashauri muwe wenye uhalisi zaidi: Msiwe wadanganyifu na bandia, na msijigambe. Mnaonyeshana tamaa zenu, lakini yote mtakayopata kama malipo ni mateso ya milele na kurudiwa kikatili! Mna haja gani ya kupepeseana macho yenu na kujiingiza katika mapenzi? Je, hiki ndicho kipimo cha uaminifu wenu, kiasi cha uadilifu wenu? Nawachukia kabisa wale miongoni mwenu wanaojihusisha katika uganga na uchawi; Nawachukia sana wale wanaume na wanawake wadogo miongoni mwenu wanaopenda miili yao wenyewe. Ni vyema mjizuie, kwa sababu sasa mnahitajika kuwa na ubinadamu wa kawaida, na hamruhusiwi kuonyesha tamaa zenu—lakini mnachukua kila fursa muwezayo, kwani miili yenu imejaa sana, na tamaa zenu ni kubwa mno!

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Utendaji (7)

Maneno ya Mungu ya Kila Siku (Dondoo 316)

Sasa, iwapo ufuatiliaji wenu umekuwa wa kufaa au la linatathminiwa na kile mlicho nacho sasa. Hiki ndicho kinachotumiwa kuamua matokeo yenu; yaani, matokeo yenu yanafichuliwa katika kujitolea mlikofanya na mambo ambayo mmefanya. Matokeo yenu yatadhihirishwa na ufuatiliaji wenu, imani yenu na mambo ambayo mmefanya. Kati yenu nyote, kuna wengi ambao tayari hawawezi kuokolewa, kwani leo ndiyo siku ya kufichua matokeo ya watu, na Sitakanganyikiwa katika kazi Yangu; Sitawaongoza wale wasioweza kuokolewa kabisa katika enzi ifuatayo. Kutakuwa na wakati ambapo kazi Yangu itakuwa imekamilika. Sitafinyanga maiti hizo ambazo haziwezi kuokolewa hata kidogo; sasa ndizo siku za mwisho za wokovu wa mwanadamu, na Sitafanya kazi isiyo ya maana. Usishutumu Mbingu na dunia—mwisho wa dunia unakuja. Hauepukiki. Mambo yamefika hapa, na hakuna kitu ambacho wewe kama mwanadamu unaweza kufanya kuyasimamisha; huwezi kubadili vitu jinsi utakavyo. Jana, hukulipa gharama ya kufuatilia ukweli na hukuwa mwaminifu; leo, wakati umewadia, huwezi kuokolewa; na kesho, utaondolewa, na hakutakuwa na uhuru wa matendo kwa ajili ya wokovu wako. Hata ingawa moyo wangu ni mpole na Ninafanya kila Niwezalo kukuokoa, usipojitahidi wewe mwenyewe ama kujifikiria hata kidogo, hili linanihusu vipi? Wale wanaofikiria tu miili yao na wanaofurahia faraja, wale wanaoonekana kuamini lakini wasioamini kwa kweli; wale wanaojihusisha katika uganga na uchawi; wale ambao ni wazinzi, walio duni kabisa; wale wanaoiba sadaka za Yehova na mali Yake; wale wanaopenda hongo; wale walio na njozi za kupaa mbinguni; wale ambao ni wenye majivuno na fidhuli, wanaojitahidi tu kwa sababu ya umaarufu na utajiri wa kibinafsi; wale wanaoeneza maneno ya safihi; wale wanaomkufuru Mungu Mwenyewe; wale wanaotoa tu hukumu dhidi ya Mungu Mwenyewe na kumkashifu; wale wanaounda vikundi na kutafuta kujitegemea; wale wanaojitukuza juu ya Mungu, wale wanaume na wanawake wadogo, wa makamo na wakubwa ambao ni wapuuzi na wametegwa katika uasherati; wale wanaume na wanawake wanaofurahia umaarufu na utajiri wa kibinafsi na wanafuatilia hadhi ya kibinafsi miongoni mwa mengine; wale watu wasiotubu walionaswa katika dhambi—je, si wote hawawezi kuokolewa? Uasherati, kutenda dhambi, uganga, uchawi, matusi na maneno ya safihi yote yamejaa kwenu; na ukweli na maneno ya uzima yanakanyagwa miongoni mwenu, na lugha takatifu inachafuliwa miongoni mwenu. Ninyi Mataifa, mliojaa uchafu na uasi! Matokeo yenu ya mwisho yatakuwa yapi? Je, wale wanaopenda mwili, wanaotenda uchawi wa mwili, na waliotegwa katika dhambi ya uasherati wanawezaje kuwa na ujasiri wa kuendelea kuishi! Je, hujui kwamba watu kama ninyi ni mabuu wasioweza kuokolewa? Ni nini kinachowapa haki ya kudai hili na lile? Hadi leo, hakujakuwa na mabadiliko hata kidogo katika wale wasiopenda ukweli na wanapenda tu mwili—watu kama hawa wanawezaje kuokolewa? Wale wasiopenda njia ya uzima, wasiomtukuza Mungu ama kumshuhudia, wanaopanga njama kwa ajili ya hadhi yao wenyewe, wanaojisifu sana—je, si bado wao wako vivyo hivyo, hadi leo? Kuna thamani gani katika kuwaokoa? Iwapo unaweza kuokolewa hakutegemei ukubwa wako ama ni miaka mingapi umekuwa ukifanya kazi, sembuse sifa ambazo umeongeza. Badala yake, kunategemea iwapo ufuatiliaji wako umezaa matunda. Unapaswa kujua kwamba wale waliookolewa ni “miti” inayozaa matunda, siyo miti iliyo na majani yaliyositawi sana na maua mengi lakini ambayo hayazai matunda. Hata kama umeshinda miaka mingi ukizurura mitaani, hilo lina maana gani? Ushuhuda wako uko wapi? Uchaji wako wa Mungu ni kidogo sana kuliko upendo wako kwako mwenyewe na hamu zako zenye tamaa—je, si mtu kama huyu ni mpotovu? Anawezaje kuwa kielelezo na mfano wa wokovu? Asili yako ni isiyorekebishika, wewe ni mwasi sana, huwezi kuokolewa! Je, si watu kama hawa ni wale watakaoondolewa? Je, si wakati ambapo kazi Yangu inakamilika ni wakati wa kufika kwa siku yako ya mwisho? Nimefanya kazi nyingi sana na kuzungumza maneno mengi sana miongoni mwenu—kweli mmeyasikiliza kiasi kipi? Mmewahi kutii kiasi kipi? Kazi Yangu ikamilikapo, huo utakuwa wakati ambapo unakoma kunipinga, wakati ambapo unakoma kusimama dhidi Yangu. Nifanyapo kazi, mnanipinga bila kukoma; kamwe hamyatii maneno Yangu. Nafanya kazi Yangu na wewe unafanya “kazi” yako mwenyewe, ukitengeneza ufalme wako mdogo. Ninyi ni kundi la mbweha na mbwa tu, mnaofanya kila kitu kunipinga! Mnajaribu kila wakati kuwakumbatia wale wanaowapa upendo wao wa dhati—uchaji wenu uko wapi? Kila kitu mfanyacho ni kidanganyifu! Hamna utii wala uchaji, na kila kitu mfanyacho ni kidanganyifu na cha kukufuru! Je, watu kama hawa wanaweza kuokolewa? Wanadamu ambao ni waasherati na wakware daima hutaka kuwavutia makahaba wenye ubembe kwao kwa ajili ya raha zao wenyewe. Sitawaokoa mashetani wa kisherati kama hawa hata kidogo. Nawachukia ninyi mashetani wachafu, na ukware na ubembe wenu utawatumbukiza kuzimuni. Mna nini cha kusema kujihusu? Ninyi mashetani wachafu na pepo waovu ni wa kutia kinyaa! Mnachukiza! Watu ovyo kama ninyi mnawezaje kuokolewa? Je, wale waliotegwa katika dhambi wanaweza kuokolewa bado? Leo, ukweli huu, njia hii, na uzima huu hauwavutii; badala yake mnavutiwa na utendaji dhambi, fedha, hadhi, umaarufu na faida; mnavutiwa na raha za mwili; sura nzuri za wanaume na uzuri wa wanawake. Ni nini kinachowastahiki kuingia katika ufalme Wangu? Sura yenu hata ni ya juu zaidi kuliko ya Mungu, hadhi yenu hata ni ya juu kuliko ya Mungu sembuse fahari yenu kubwa miongoni mwa wanadamu—mmekuwa sanamu ambayo watu wanaabudu. Je, hujageuka kuwa malaika mkuu? Wakati matokeo ya watu yanafichuliwa, ambao pia ndio wakati kazi ya wokovu itakaribia kuisha, wengi kati yenu mtakuwa maiti msioweza kuokolewa na lazima muondolewe. Wakati wa kazi ya wokovu, Mimi ni mwenye huruma na mzuri kwa watu wote. Kazi inapokamilika, matokeo ya watu wa aina tofauti yatafichuliwa, na wakati huo, Sitakuwa mwenye huruma na mzuri tena, kwa kuwa matokeo ya watu yatakuwa yamefichuliwa, na kila mmoja atakuwa ameainishwa kulingana na aina yake, na hakutakuwa na haja ya kufanya kazi zaidi ya wokovu, kwa sababu enzi ya wokovu itakuwa imepita, na kwa sababu imepita, haitarudi.

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Utendaji (7)

Maneno ya Mungu ya Kila Siku (Dondoo 317)

Binadamu amekuwa akiishi katika funiko la ushawishi wa giza, huku akiwa amezuiliwa bila ya kuachiliwa na ushawishi wa Shetani. Nayo tabia ya binadamu, baada ya kutengenezwa na Shetani, inaendelea kuongezeka kuwa potovu. Mtu anaweza kusema kwamba binadamu huishi daima na tabia yake potovu ya kishetani, asiweze kumpenda Mungu kwa kweli. Kwa sababu ya hili, kama binadamu anataka kumpenda Mungu, lazima anyang'anywe kujidai kwake, kujigamba, kiburi, majivuno, na sifa nyingine kama hizo zinazomilikiwa na tabia ya Shetani. La sivyo, upendo wake si safi, ni upendo wa kishetani, na ule ambao hauwezi kabisa kupokea idhini ya Mungu. Kama binadamu hakamilishwi, kushughulikiwa, kuvunjwa, kupogolewa, kufundishwa nidhamu, kuadibiwa, au kusafishwa na Roho Mtakatifu moja kwa moja, hakuna yeyote anayeweza kumpenda Mungu kwa kweli. Ukisema kwamba sehemu ya tabia yako inamwakilisha Mungu na hivyo basi unaweza kumpenda Mungu kwa kweli, basi wewe ndiwe unayezungumza maneno ya kiburi na ni binadamu wa upuuzi. Binadamu kama hao ni malaika mkuu! Asili ya ndani ya binadamu haiwezi kumwakilisha Mungu kwa njia ya moja kwa moja. Lazima binadamu aiondoe asili yake ya ndani kupitia kwa ukamilifu wa Mungu, na kisha kupitia kutunza na kutosheleza mapenzi ya Mungu tu, na hata zaidi kupitia kwa kazi ya Roho Mtakatifu, ndipo kuishi kwa kudhihirishwa kwake kunaweza kuidhinishwa na Mungu. Hakuna anayeishi katika mwili anayeweza kumwakilisha Mungu kwa njia ya moja kwa moja isipokuwa kama yeye ni binadamu anayetumiwa na Roho Mtakatifu. Hata hivyo, hata kama huyu, tabia yake na kile anachoishi kwa kudhihirisha chote hakiwezi kuchukuliwa kwamba kinamwakilisha Mungu kabisa; inaweza kusemekana tu kwamba kile anachoishi kwa kudhihirishwa kinatawaliwa na Roho Mtakatifu. Tabia ya mtu kama huyo haiwezi kumwakilisha Mungu.

Ingawa tabia ya binadamu inaamrishwa na Mungu—hili halina shaka na linaweza kuchukuliwa kama jambo zuri—limetengenezwa na Shetani. Hiyo ndiyo maana tabia zote za binadamu kwa kweli ni tabia ya Shetani. Mtu anaweza kusema kuwa Mungu, katika tabia yake, ni mnyofu katika kutekeleza mambo, na kwamba yeye pia anatenda kwa njia hii; yeye pia an tabia kama hii, na hivyo basi anasema kwamba tabia yake inamwakilisha Mungu. Huyu ni binadamu wa aina gani? Je, tabia potovu ya kishetani inaweza kumwakilisha Mungu? Yeyote yule anayetangaza kwamba tabia yake ni wakilishi kwa Mungu, huyo mtu anamkufuru Mungu na kumtukana Roho Mtakatifu! Tukiangalia namna ambavyo Roho Mtakatifu hufanya kazi, kazi ambayo Mungu anafanya hapa ulimwenguni ni kwa ajili ya kushinda pekee. Hii ndiyo maana, nyingi ya tabia potovu za kishetani za binadamu bado hazijatakaswa, na ndiyo maana mienendo ya maisha ya binadamu bado ni taswira ya Shetani. Ndicho binadamu huamini kuwa chema a na kinawakilisha vitendo vya mwili wa binadamu au kwa usahihi zaidi, kinawakilisha Shetani na hakiwezi kumwakilisha Mungu kabisa. Hata kama binadamu tayari anampenda Mungu hadi kufikia kiwango ambacho anaweza kufurahia maisha ya mbinguni hapa ulimwenguni, anaweza kutamka kauli kama vile: “Eh Mungu! Siwezi kukupenda vya kutosha,” na kwamba amefikia eneo la juu zaidi, huwezi kusema kwamba anaishi kwa kumdhihirisha Mungu au kumwakilisha Mungu, kwani kiini cha binadamu ni tofauti na kile cha Mungu. Binadamu hawezi kamwe kuishi kwa kumdhihirisha Mungu, sembuse kuwa Mungu. Kile ambacho Roho Mtakatifu anamwelekeza binadamu kuishi kwa kudhihirisha ni kulingana tu na kile ambacho Mungu anahitaji kutoka kwa binadamu.

Vitendo vyote na matendo ya Shetani vinaonyeshwa kupitia kwa binadamu. Sasa vitendo vyote na matendo yote ya binadamu ni maonyesho ya Shetani na hivyo basi haviwezi kumwakilisha Mungu. Binadamu ni mfano halisi wa Shetani, na tabia ya mwanadamu haiwezi kuiwakilisha tabia ya Mungu. Baadhi ya wanadamu ni wenye tabia nzuri; Mungu anaweza kufanya baadhi ya kazi kupitia kwa tabia hiyo nayo kazi yao inatawaliwa na Roho Mtakatifu. Ilhali tabia yao haiwezi kumwakilisha Mungu. Kazi ambayo Mungu hufanya ndani yao ni kule tu kufanya kazi na pamoja na kupanua kile ambacho tayari kimo ndani yao. Wawe ni manabii au binadamu wanaotumiwa na Mungu kutoka kwa enzi zilizopita, hakuna yeyote anayeweza kumwakilisha Mungu moja kwa moja. Binadamu wote huja kumpenda Mungu kwa sababu tu ya shurutisho kutoka kwa mazingira yao, na hakuna kati yao ambaye hujitahidi kushiriki kwa hiari yake. Mambo mema ni yapi? Yote ambayo hutoka kwa njia ya moja kwa moja kutoka kwa Mungu ni mema. Hata hivyo, tabia ya binadamu imetengenezwa na Shetani na haiwezi kumwakilisha Mungu. Ni Mungu mwenye mwili tu—mapenzi Yake, nia Yake ya kuteseka, haki, utiifu, unyenyekevu na kujificha Kwake—hivi vyote humwakilisha Mungu moja kwa moja. Hii ni kwa sababu Alipokuja, Hakuwa na asili ya dhambi na alikuja moja kwa moja kutoka kwa Mungu bila ya kutengenezwa na Shetani. Yesu yumo tu katika mfano wa mwili wenye dhambi na hawakilishi dhambi; kwa hivyo, vitendo Vyake, matendo na maneno, mpaka wakati ule kabla ya mafanikio Yake ya kazi kupitia kwa kusulubishwa (pamoja na kusulubishwa) vyote ni viwakilishi vya moja kwa moja vya Mungu. Mfano wa Yesu unatosha kuthibitisha kwamba binadamu yeyote aliye na asili ya dhambi hawezi kumwakilisha Mungu, na kwamba dhambi ya binadamu inamwakilisha Shetani. Hiyo ni kusema kwamba dhambi haimwakilishi Mungu na Mungu hana dhambi. Hata kazi inayofanywa ndani ya binadamu na Roho Mtakatifu inaweza tu kuchukuliwa kuwa imetawaliwa na Roho Mtakatifu na haiwezi kusemwa kwamba ilifanywa na binadamu kwa niaba ya Mungu. Lakini kwa kadiri ambavyo binadamu anahusika, si dhambi yake wala tabia yake inamwakilisha Mungu. Kwa kuangalia kazi ambayo Roho Mtakatifu amefanya ndani kwa mwanadamu kutoka zamani hadi sasa, mtu anaona kwamba mwanadamu anacho kile anachoishi kwa kudhihirisha kwa sababu Roho Mtakatifu amefanya kazi juu yake. Ni wachache sana wanaoweza kuishi kwa kudhihirisha ukweli baada ya kushughulikiwa na kufundishwa nidhamu na Roho Mtakatifu. Ambayo ni kusema kwamba, kazi ya Roho Mtakatifu tu ndiyo iliyopo; ushirikiano kwa upande wa binadamu haupo. Je, unaliona suala hili kwa uwazi zaidi sasa? Kwa hiyo basi, ni nini unachofaa kufanya ili kufanya kazi kwa bidii pamoja na Yeye huku Roho Mtakatifu akiwa kazini na, kwa kufanya hivyo, kutimiza wajibu wako?

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Mwanadamu Mpotovu Hawezi Kumwakilisha Mungu

Maneno ya Mungu ya Kila Siku (Dondoo 318)

Imani yako kwa Mungu, ufuatiliaji wako wa ukweli, na vile unavyofanya mambo yote yanapaswa kujikita katika ukweli: Kila kitu unachokifanya kinapaswa kiwe kinatekelezeka, na hupaswi kufuatilia vitu vile ambavyo ni vya kinjozi tu. Hakuna maana yoyote katika kufanya vitu namna hii, na, aidha, maisha kama hayo hayana maana. Kwa sababu njia yako na maisha havijengwi katika kitu chochote kile isipokuwa uongo na ulaghai, na hufuati vitu ambavyo vina thamani na maana, kitu pekee unachopata ni fikira za kipuuzi tu na mafundisho ambayo hayana ukweli. Vitu kama hivyo havina uhusiano na maana na thamani ya uwepo wako, na vinaweza tu kukuleta katika ulimwengu ulio tupu. Kwa namna hii, maisha yako yote yatakuwa hayana maana au thamani—na kama hufuatilii maisha yenye maana, basi unaweza kuishi mamia ya miaka na yote hiyo inaweza kuwa haina maana yoyote. Hayo yanawezaje kuitwa maisha ya mwanadamu? Haya hakika si ni maisha ya mnyama? Kwa namna iyo hiyo, kama mtajaribu kufuata njia ya imani katika Mungu, na wala msijaribu kumfuata Mungu anayeweza kuonekana, na badala yake mumwabudu Mungu asiyeonekana na asiyeshikika, basi si kufuatilia kama huko ni bure? Mwisho wake, ufuatiliaji wako kutakuwa ni anguko kubwa. Kufuatilia kwa aina hiyo kuna manufaa gani kwako? Tatizo kubwa zaidi la mwanadamu ni kwamba anaweza kupenda tu vitu ambavyo hawezi kuviona au kuvigusa, vitu ambavyo ni vya siri kubwa na vya kushangaza, na kwamba haviwezi kufikiriwa na mwanadamu na haviwezi kufikiwa na mwanadamu. Kadiri vitu hivi vinavyokuwa si halisi, kadiri vinavyochambuliwa na mwanadamu, ambaye anavifuata bila kujali kitu chochote, na hujaribu kuvipata. Kadiri vinavyokuwa si halisi, ndivyo mwanadamu anavyozidi kuvichunguza na kuvichambua zaidi, hata kwenda kwa kiwango cha kufanya mawazo yake ya kina kuyahusu. Kinyume chake, jinsi vitu vinavyokuwa halisi zaidi, ndivyo mwanadamu anavyozidi kuvipuuza; huviangalia kwa dharau, na hata huvitweza. Huu hasa si mtazamo weni juu ya kazi halisi Ninayoifanya leo? Kadiri mambo hayo yanavyokuwa halisi, ndivyo unavyozidi kuyadharau. Wala hutengi muda kwa ajili ya kuyachunguza, bali unayapuuza; unayadharau mambo haya halisi yenye kiwango cha chini, yenye matakwa ya moja kwa moja, na hata unakuwa na fikira nyingi kuhusu Mungu huyu ambaye ni halisi sana, na huwezi tu kuukubali uhalisi na ukawaida Wake. Kwa njia hii, huamini katika hali isiyo dhahiri? Una imani thabiti katika Mungu asiye dhahiri wa wakati uliopita, na wala hupendi kumjua Mungu wa kweli wa leo. Hii si kwa sababu Mungu wa jana na Mungu wa leo wanatoka katika enzi tofauti? Si pia kwa sababu Mungu wa jana ni Mungu wa mbinguni aliyeinuliwa, wakati Mungu wa leo ni mwanadamu mdogo wa duniani? Aidha, si pia kwa sababu Mungu anayeabudiwa na mwanadamu ni yule aliyetokana na dhana zake, wakati Mungu wa leo ni mwili halisi uliotengenezwa duniani? Hata hivyo, si kwa sababu Mungu wa leo ni halisi sana kiasi kwamba mwanadamu hamfuatilii? Maana kile ambacho Mungu wa leo anamtaka mwanadamu afanye ni kile ambacho mwanadamu hayupo radhi kabisa kukifanya, na ambacho kinamfanya ahisi aibu. Huku sio kufanya mambo yawe magumu kwa mwanadamu? Je, hili halionyeshi makovu yake hapa? Kwa namna hii, wengi wao ambao hawafuati uhalisi wanakuwa maadui wa Mungu mwenye mwili, wanakuwa wapinga Kristo. Huu si ukweli dhahiri? Hapo zamani, wakati Mungu alikuwa hajawa mwili, inawezekana ulikuwa mtu wa dini, au msahilina. Baada ya Mungu kuwa mwili, wasahilina wengi kama hao waligeuka bila kujua na kuwa wapinga Kristo. Unajua ni nini kinachoendelea hapa? Katika imani yako kwa Mungu, hujikiti katika uhalisi au kuufuatilia ukweli, bali unashikilia sana uongo—je, si hiki ndicho chanzo wazi cha uadui wako na Mungu mwenye mwili? Mungu mwenye mwili anaitwa Kristo, hivyo sio kwamba wote ambao hawamwamini Mungu mwenye mwili ni wapinga Kristo? Je, yule unayemwamini na kumpenda ni huyu Mungu mwenye mwili kweli? Je, kweli ni huyu Mungu aliye hai ambaye ni wa halisi zaidi na ambaye ni wa kawaida kabisa? Malengo ya ufuatiliaji wako, zako ni yapi hasa? Yako mbinguni au duniani? Je, ni dhana au ni ukweli? Je, ni Mungu au ni kiumbe fulani asiyekuwa wa kawaida? Kwa kweli, ukweli ndio halisi zaidi katika methali zote za maisha, na ni mkuu kabisa kuliko methali hizo miongoni mwa wanadamu wote. Kwa sababu ni matakwa ambayo Mungu anayataka kwa mwanadamu, na ni kazi ambayo inafanywa na Mungu mwenyewe, hivyo inaitwa methali ya maisha. Sio methali iliyoundwa kutoka katika kitu fulani, wala si nukuu maarufu kutoka kwa mtu maarufu; badala yake, ni matamshi kwa mwanadamu kutoka kwa Bwana wa mbingu na nchi na vitu vyote, na sio maneno fulani yaliyotolewa na mwanadamu, bali ni maisha asili ya Mungu. Na hivyo unaitwa ni methali ya juu kabisa kupita methali zote za maisha. Ufuatiliaji wa mwanadamu wa kuweka ukweli katika matendo ni kufanya wajibu wake, yaani, ufuatiliaji wa kukidhi matakwa ya Mungu. Asili ya matakwa haya ni ukweli halisi, badala ya mafundisho yasiyokuwa na maana ambayo hayafikiwi na mwanadamu yeyote. Kama kufuatilia kwako ni mafundisho tu na bila uhalisi wowote, huoni unaasi dhidi ya ukweli? Wewe si mtu anayeushambulia ukweli? Mtu wa namna hiyo anawezaje kufuatilia kumpenda Mungu? Watu ambao hawana uhalisi ni wale ambao wanausaliti ukweli, na wote kwa asili ni waasi!

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Ni Wale tu Wanaomjua Mungu na Kazi Yake Ndio Wanaoweza Kumridhisha Mungu

Maneno ya Mungu ya Kila Siku (Dondoo 319)

Nyinyi nyote mna furaha kupokea tuzo mbele ya Mungu na kuwa walengwa wa fadhili Zake machoni Pake. Haya ni matakwa ya kila mtu baada ya yeye kuanza kuwa na imani kwa Mungu, kwani mwanadamu kwa moyo wake wote hujitahidi kupata mambo yaliyo juu na hakuna aliye tayari kubaki nyuma ya wengine. Hii ndiyo njia ya mwanadamu. Kwa sababu hii hasa, wengi kati yenu wanajaribu daima kujipendekeza kwa Mungu mbinguni, lakini kwa kweli, uaminifu wenu na uwazi kwa Mungu ni wa kiasi kidogo sana ukilinganishwa na uaminifu na uwazi wenu kwenu wenyewe. Mbona Nasema hivi? Kwa sababu Sikiri uaminifu wenu kwa Mungu kabisa, na zaidi Nakana kuwepo kwa Mungu aliye ndani ya mioyo yenu. Hiyo ni kusema, Mungu mnayemwabudu, Mungu asiye dhahiri mnayempenda, hayupo kabisa. Kinachonifanya niseme haya kwa uhakika ni kwamba mko mbali sana na Mungu wa kweli. Uaminifu mnaomiliki unatokana na kuwepo kwa sanamu mioyoni mwenu, na kunihusu Mimi, Mungu anayeonekana kama asiye mkubwa wala mdogo machoni penu, mnachofanya ni kunikiri kwa maneno tu. Ninaposema juu ya umbali wenu mkubwa kutoka kwa Mungu, Ninamaanisha jinsi mlivyo mbali sana na Mungu wa kweli, ilhali Mungu asiye dhahiri Anaonekana kuwa karibu. Nisemapo “asiye mkubwa,” inamaanisha jinsi Mungu mnayemwamini siku ya leo anaonekana tu kuwa mwanadamu asiye na uwezo mkubwa; mwanadamu asiye wa fahari sana. Na Nisemapo, “asiye mdogo,” inamaanisha kuwa ingawa mwanadamu huyu hawezi kuita upepo na kuamuru mvua, hata hivyo Anaweza kumwita Roho wa Mungu kufanya kazi inayotingisha mbingu na dunia, hivyo kumchanganya mwanadamu kabisa. Kwa nje, nyote mnaonekana kuwa watiifu sana kwa huyu Kristo aliye duniani, lakini kwa kiini hamna imani Kwake wala kumpenda. Ninachomaanisha ni kwamba yule mliye na imani kwake kwa kweli ni yule Mungu asiye dhahiri katika hisia zenu, na yule kweli mnayempenda ni Mungu mnayemtamani usiku na mchana, lakini bado hamjamwona kamwe kibinafsi. Na kuhusu huyu Kristo, imani yenu ni sehemu tu, na upendo wenu Kwake si kitu. Imani inamaanisha imani na kusadiki; upendo unamaanisha kusujudu na kusifu ndani ya mioyo yenu, bila kuondoka. Lakini imani yenu na upendo wenu kwa Kristo wa siku ya leo vimepunguka chini ya hili. Ikujapo kwa imani, mna imani Kwake jinsi gani? Ikujapo kwa upendo, mnampenda jinsi gani? Hamjui kabisa kuhusu tabia Yake, sembuse kiini Chake, hivyo ni jinsi gani kwamba mna imani Kwake? Uko wapi uhalisi wa imani yenu Kwake? Mnampenda jinsi gani? Uko wapi uhalisi wa upendo wenu Kwake?

Wengi wamenifuata bila kusita hadi leo, na katika miaka hii michache, nyote mmepitia uchovu mwingi. Nimefahamu vizuri tabia ya asili na mazoea ya kila mmoja wenu, na imekuwa vigumu sana kuingiliana nanyi. Cha kusikitisha ni kwamba ingawa nina maarifa nyingi kuwahusu, hamna ufahamu hata kidogo kunihusu. Sio ajabu wengine wanasema mlidanganywa na mwanadamu katika wakati wa mkanganyiko. Hakika, hamwelewi chochote kuhusu tabia Yangu, na hata zaidi hamwezi kufahamu yaliyo akilini Mwangu. Sasa ninyi kunielewa visivyo kunaongezeka haraka, na imani yenu Kwangu inabaki ile imani iliyokanganyika. Badala ya kusema kwamba mna imani na Mimi, ingekuwa bora kusema kwamba nyote mnajaribu kujipendekeza Kwangu na kunibembeleza. Nia zenu ni rahisi sana—yeyote anayeweza kunituza, nitamfuata, na yeyote anayeweza kuniwezesha kutoroka majanga makubwa, nitaamini kwake, awe Mungu ama Mungu fulani yeyote. Hakuna kati ya haya yanayonihusu. Kuna wanadamu wengi kama hao kati yenu, na hali hii ni nzito sana. Ikiwa siku moja, majaribio yatafanywa kuona ni wangapi kati yenu wanamwamini Kristo kwa sababu mna umaizi kuhusu kiini Chake, basi Nahofia kwamba hakuna mmoja wenu atakuwa na uwezo kufanya Ninavyotaka. Hivyo haitakuwa hoja kwa kila mmoja wenu kuzingatia swali hili: Mungu mliye na imani na Yeye ni tofauti sana na Mimi, na kwa hivyo, nini basi ni kiini cha imani yenu kwa Mungu? Kadri mnavyozidi kuamini katika mnayedai kuwa Mungu wenu, ndivyo mnavyozidi kupotea mbali sana nami. Basi, ni nini msingi wa suala hili? Nina uhakika hakuna mmoja wenu amewahi kufikiria suala hili, lakini mmefikiria uzito wake? Mmewaza kuhusu matokeo ya kuendelea na imani ya namna hii?

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Jinsi ya Kumjua Mungu Duniani

Maneno ya Mungu ya Kila Siku (Dondoo 320)

Nawathamini sana wale wasio na shaka kuhusu wengine na pia nawapenda sana wale wanaokubali ukweli kwa urahisi; kwa aina hizi mbili za wanadamu Ninaonyesha utunzaji mkubwa, kwani machoni Pangu wao ni waaminifu. Kama una udanganyifu mwingi, basi utakuwa na moyo wenye hadhari na mawazo ya shaka juu ya mambo yote na wanadamu wote. Kwa sababu hii, imani yako Kwangu inajengwa kwa msingi wa shaka. Imani kama hii ni moja ambayo kamwe Sitaitambua. Bila imani ya kweli, basi utakuwa mbali hata zaidi na upendo wa kweli. Na ikiwa unaweza kumshuku Mungu na kumkisia utakavyo, basi wewe bila shaka ni mdanganyifu zaidi kati ya wanadamu wengine. Mnakisia iwapo Mungu anaweza kuwa kama mwanadamu: mwenye dhambi isiyosameheka, mwenye tabia ndogondogo, anayependelea na asiye na mantiki, aliyekosa hisia ya haki, mwenye mbinu ovu, mdanganyifu na mjanja, na pia anayefurahishwa na uovu na giza, na kadhalika. Si sababu ambayo mwanadamu ana mawazo kama haya kwamba hana hata ufahamu mdogo wa Mungu? Imani kama hii ni sawa na dhambi! Zaidi ya hayo, kuna hata wale wanaoamini kwamba Sifurahishwi na yeyote isipokuwa wale wanaojirairai na kujipendekeza, na kwamba wale wasio na ujuzi huu hawatakaribishwa na watapoteza nafasi yao katika nyumba ya Mungu. Je, haya ndiyo maarifa ambayo mmepata kwa miaka hii yote mingi? Ni haya ndiyo mliyoyapata? Na ufahamu wenu kunihusu hauko kwa kutoelewa kama huku tu; mbaya hata zaidi ni kukufuru kwenu Roho wa Mungu na kuitukana Mbingu. Hii ndiyo maana Ninasema kwamba imani kama yenu itawasababisha tu kupotea mbali na Mimi na kukuwa na upinzani mkubwa dhidi Yangu. Kwa miaka mingi ya kazi, mmeona ukweli mwingi, lakini mnajua kile masikio Yangu yamesikia? Ni wangapi kati yenu walio tayari kukubali ukweli? Nyote mnaamini kwamba mko tayari kulipa gharama ya ukweli, lakini ni wangapi walioteseka kweli kwa ajili ya ukweli? Yote yaliyo ndani ya mioyo yenu ni uovu, na hivyo mnaamini kwamba yeyote, bila kujali ni nani, ni mjanja na asiye mwaminifu. Hata mnaamini kwamba Mungu mwenye mwili angekuwa bila moyo wa ukarimu na upendo wema kama tu binadamu wa kawaida. Zaidi ya hayo, mnaamini kwamba tabia ya adabu na asili yenye huruma na ukarimu ziko kwa Mungu wa mbinguni pekee. Na mnaamini kwamba mtakatifu kama huyu hayuko, na kwamba giza na uovu tu ndio unaotawala duniani, ilhali Mungu ni kitu ambacho mwanadamu huwekea matumaini yake ya mazuri na mema, na mtu maarufu aliyebuniwa na mwanadamu. Ndani ya akili zenu, Mungu aliye mbinguni ni mnyoofu sana, mwenye haki, na mkubwa, anayestahili ibada na upendezewaji, lakini Mungu huyu aliye duniani ni mbadala tu na chombo cha Mungu aliye mbinguni. Mnaamini Mungu huyu hawezi kuwa sawa na Mungu wa mbinguni, na hata zaidi hawezi kutajwa kwa pumzi moja na Yeye. Ifikapo kwa ukubwa na heshima ya Mungu, ni mali ya utukufu wa Mungu aliye mbinguni, lakini ifikapo kwa tabia na upotovu wa mwanadamu, vinahusishwa na Mungu aliye duniani. Mungu aliye mbinguni daima ni mkuu, ilhali Mungu wa duniani daima ni asiye na maana, mdhaifu na asiyejimudu. Mungu aliye mbinguni haathiriwi na hisia, kwa haki tu, ilhali Mungu aliye duniani ana motisha za kibinafsi tu na Hana haki na mantiki yoyote. Mungu aliye mbinguni hana udanganyifu hata kidogo na daima ni mwaminifu, ilhali Mungu wa duniani daima ana upande mdanganyifu. Mungu aliye mbinguni anampenda sana mwanadamu, ilhali Mungu wa duniani anamjali mwanadamu isivyotosha, hata kumpuuza kabisa. Ufahamu huu usio sahihi umewekwa kwa muda mrefu kwa mioyo yenu na unaweza pia kuendelezwa mbele katika siku za usoni. Mnachukulia matendo yote ya Kristo kwa msimamo wa wadhalimu na kuhukumu kazi Yake yote na utambulisho Wake na kiini Chake kwa mtazamo wa waovu. Mmefanya kosa kubwa sana na kufanya kile ambacho hakijawahi kufanywa na wale kabla yenu. Yaani, mnamtumikia tu Mungu mkuu aliye mbinguni na taji juu ya kichwa Chake na hammshughulikii kamwe Mungu mnayemchukulia kuwa asiye na maana kabisa kiasi cha kutoonekana kwenu. Hii siyo dhambi yenu? Huu sio mfano halisi wa kosa lenu dhidi ya tabia ya Mungu? Mnamwabudu sana Mungu aliye mbinguni. Mnapenda sana sura zilizo kuu na kuheshimu wanaojulikana kwa ajili ya umbuji wao. Mnaamrishwa kwa furaha na Mungu Anayejaza mikono yenu na utajiri, na mnatamani sana Mungu Anayeweza kutimiza tamaa zenu zote. Yule tu msiyemwabudu ni Mungu huyu asiye mkuu; Chombo chenu tu cha chuki ni ushirikiano na huyu Mungu ambaye hakuna mwanadamu anayeweza kumchukulia kuwa mkuu. Kitu pekee ambacho hamko tayari kufanya ni kumtumikia huyu Mungu ambaye hajawahi kuwapa senti hata moja, na Yule tu msiyemtamani ni huyu Mungu asiyependeza. Mungu kama huyu hawezi kuwawezesha kupanua upeo wenu wa macho, kuhisi kana kwamba mmepata hazina, sembuse kutimiza mnachotaka. Mbona, basi, mnamfuata? Je, mmefikiria kuhusu maswali kama haya? Kile ufanyacho hakimkosei huyu Kristo tu; cha muhimu hata zaidi, kinakosea Mungu aliye mbinguni. Nadhani kwamba, haya siyo madhumuni ya imani yenu kwa Mungu!

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Jinsi ya Kumjua Mungu Duniani

Maneno ya Mungu ya Kila Siku (Dondoo 321)

Mnatamani sana kwa Mungu kufurahishwa nanyi, lakini bado mko mbali sana na Mungu. Tatizo ni nini hapa? Mnakubali tu maneno Yake, lakini sio ushughulikiaji na upogoaji Wake; hata zaidi hamwezi kukubali mpangilio Wake wote, kuwa na imani kamilifu Kwake. Tatizo, basi, ni gani hapa? Kimsingi, imani yenu ni kaka tupu la yai lisiloweza kutoa kifaranga. Kwani imani yenu haijawaletea ukweli ama kuwapa maisha, na badala imewaletea hisia danganyifu ya tumaini na msaada. Madhumuni ya imani yenu kwa Mungu ni kwa ajili ya tumaini hili na msaada huu badala ya ukweli na maisha. Kwa hivyo, Nasema kwamba mkondo wa imani yenu kwa Mungu si mwingine bali ni kujaribu kujipendekeza kwa Mungu kupitia utumwa na kutokuwa na aibu, na hauwezi kuchukuliwa kuwa imani ya kweli hata kidogo. Kifaranga anaweza kujitokezaje kwa imani kama hii? Kwa maneno mengine, ni tunda lipi ambalo imani kama hii inaweza kuzalisha? Azma ya imani yenu kwa Mungu ni kutimiza nia zenu kupitia kumtumia Mungu. Huu sio ukweli zaidi unaoonyesha kosa lenu dhidi ya tabia ya Mungu? Mnaamini kuwepo kwa Mungu aliye mbinguni lakini mnakataa yule Mungu aliye duniani. Hata hivyo, Sikubaliani na maoni yenu. Nawapongeza tu wale wanadamu wanaosimama imara na kumtumikia Mungu wa duniani, kamwe sio wale wasiomkiri Kristo aliye duniani. Bila kujali jinsi wanadamu kama hawa walivyo waaminifu kwa Mungu aliye mbinguni, mwishowe, hawatauepuka mkono Wangu unaoadhibu waovu. Wanadamu kama hawa ni waovu; ni wale waovu wanaompinga Mungu na hawajawahi kumtii Kristo kwa furaha. Bila shaka, idadi yao inajumuisha wale wote wasiomjua na, zaidi, wasiomkiri Kristo. Unaamini kwamba unaweza kutenda utakavyo kwa Kristo alimradi wewe ni mwaminifu kwa Mungu aliye mbinguni? Makosa! Kutomjua Kristo kwako ni kutomjua Mungu aliye mbinguni. Bila kujali uaminifu wako kwa Mungu aliye mbinguni, ni maneno matupu tu na kujifanya, kwani Mungu aliye duniani si muhimu tu kwa mwanadamu kupokea ukweli na ufahamu mkubwa zaidi, lakini hata zaidi ni muhimu kwa lawama ya mwanadamu na baadaye kwa kuushika ukweli kuwaadhibu waovu. Umeelewa matokeo yenye faida na yanayodhuru hapa? Umepata kuyapitia? Ningependa siku moja hivi karibuni ninyi muelewe ukweli huu: Kumjua Mungu, mnapaswa kumjua sio tu Mungu wa mbinguni lakini, hata muhimu zaidi, Mungu aliye duniani. Msiyachanganye yaliyo kipaumbele ama kuruhusu yaliyo ya pili kuchukua nafasi ya yaliyo ya msingi. Ni kwa njia hii tu ndiyo unaweza kujenga uhusiano mzuri na Mungu, kuwa karibu na Mungu, na kupeleka moyo wako karibu na Yeye. Kama umekuwa wa imani kwa miaka nyingi na kushirikiana na Mimi kwa muda mrefu, lakini bado unabaki mbali na Mimi, basi Nasema kwamba ni lazima iwe kuwa mara nyingi unaikosea tabia ya Mungu, na mwisho wako utakuwa mgumu sana kufikiria. Kama miaka mingi ya ushirikiano na Mimi haijakubadilisha kuwa mwanadamu aliye na ubinadamu na ukweli, ila badala yake imeingiza njia zako ovu ndani ya asili yako, na huna maono maradufu ya uwongo kuhusu fahari kuliko awali pekee lakini kutonielewa kwako kumeongezeka pia, kiasi kwamba unakuja kunichukulia kuwa rafiki yako mdogo wa kando, basi Nasema kwamba mateso yako si ya juujuu tena, lakini yamepenya ndani kwa mifupa yako. Yote yaliyosalia ni wewe kusubiri matayarisho ya mazishi yako kufanywa. Huhitaji kunisihi basi Niwe Mungu wako, kwani umetenda dhambi inayostahili kifo, dhambi isiyosameheka. Hata kama Ningeweza kuwa na huruma nawe, Mungu aliye mbinguni Atasisitiza kuchukua maisha yako, kwani kosa lako dhidi ya tabia ya Mungu si shida ya kawaida, lakini lile lililo kubwa sana kiasili. Wakati utakapofika, usinilaumu kwa sababu ya kutokujulisha mbeleni. Yote yanarudia haya: Wakati unashirikiana na Kristo—Mungu aliye duniani—kama mwanadamu wa kawaida, yaani, unapoamini kwamba Mungu huyu si chochote ila ni mwanadamu, ni hapo basi ndipo utaangamia. Hili ndilo onyo Langu la pekee kwenu nyinyi nyote.

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Jinsi ya Kumjua Mungu Duniani

Maneno ya Mungu ya Kila Siku (Dondoo 322)

Ndani ya binadamu, kunalo neno lisilokuwa la uhakika, ilhali binadamu hajui imani inajumuisha nini, na vilevile hajui ni kwa nini anayo imani. Binadamu huelewa kidogo sana, na binadamu mwenyewe amepungukiwa sana; yeye anakuwa tu na imani ndani Yangu bila kujali na bila kujua. Ingawa hajui imani ni nini wala ni kwa nini anayo imani ndani Yangu, anaendelea kufanya hivyo kwa shauku mno. Kile Ninachomwomba binadamu, si tu yeye kuniita Mimi kwa shauku kwa njia hii au kuniamini Mimi kwa mtindo huu wa kukosa mwelekeo. Kwani kazi Ninayoifanya ni yake binadamu kunijia Mimi na kunijia Mimi, wala si kwa binadamu kuvutiwa na kuniangalia Mimi kwa njia mpya kwa sababu ya kazi Yangu. Awali Nilijionyesha katika ishara na maajabu mengi na kufanya miujiza mingi. Waisraeli wakati huo waliniangalia Mimi kwa tamanio kuu na walistahi pakubwa uwezo Wangu wa kipekee wa kuponya wagonjwa na kupunga mapepo. Wakati huo, Wayahudi walifikiri nguvu Zangu za uponyaji zilikuwa za kistadi na zisizo za kawaida. Kwa matendo Yangu mengi kama hayo, wote walinichukulia Mimi kwa heshima; waliweza kuhisi tamanio kuu katika nguvu Zangu zote. Kwa hiyo yeyote aliyeniona Mimi nikifanya miujiza alinifuatilia Mimi kwa karibu kiasi kwamba maelfu ya watu walinizunguka ili kunitazama nikiwaponya wagonjwa. Nilionyesha ishara na maajabu mengi, ilhali binadamu alinichukulia Mimi kama daktari stadi; Niliongea maneno mengi ya mafunzo kwa watu hao wakati huo, ilhali wote walinichukulia Mimi tu kama mwalimu aliyekuwa na mamlaka zaidi kwa wanafunzi wake! Hadi siku ya leo, baada ya binadamu kuona rekodi za kihistoria za kazi Yangu, ufasiri wao unaendelea kuwa kwamba Mimi ni daktari mkuu anayeponya wagonjwa na mwalimu kwa wasiojua. Na wameniita Mimi Bwana Yesu Kristo Mwenye huruma. Wale wanaofasiri maandiko huenda walizidi mbinu Zangu katika uponyaji, au huenda pengine wakawa wanafunzi ambao tayari wamempita mwalimu wao, ilhali binadamu kama hao wanaofahamika sana ambao majina yao yanajulikana kote ulimwenguni wananichukulia Mimi kwa kiwango cha chini sana cha kuwa daktari tu! Matendo Yangu ni mengi zaidi kwa kuhesabiwa kuliko chembechembe za changarawe kwenye ufuo na hekima Yangu kubwa zaidi kuliko ile ya watoto wote wa kiume wa Suleimani, ilhali binadamu wanafikiria kwamba Mimi ni daktari tu asiye na mengi kumhusu na mwalimu wa binadamu asiyejulikana! Ni wangapi wanaoniamini Mimi ili waweze tu kupata uponyaji? Ni wangapi wanaoniamini Mimi hili tu niweze kutumia nguvu Zangu kupunga roho chafu kutoka kwenye miili yao? Na ni wangapi wanaoniamini Mimi ili tu waweze kupokea amani na furaha kutoka Kwangu? Ni wangapi wanaoniamini Mimi ili kuhitaji kutoka Kwangu utajiri mwingi zaidi wa dunia, na ni wangapi wanaoniamini Mimi ili waweze kuishi maisha hayo kwa usalama na kuwa salama salimini katika maisha yajayo? Ni wangapi wanaoniamini Mimi ili waweze kuepuka tu mateso ya kuzimu na kupokea baraka za mbinguni? Ni wangapi wanaoniamini Mimi ili wapate tulizo lakini hawatafuti kupata chochote kutoka kwa ulimwengu ujao? Niliposhushia hasira Zangu binadamu na kuchukua furaha na amani yote aliyokuwa nayo mwanzo, binadamu akaanza kuwa na shaka. Nilipomkabidhi binadamu mateso ya kuzimu na kuchukua tena baraka za mbinguni, aibu ya binadamu iligeuka na kuwa hasira. Wakati binadamu aliponiomba Mimi kumponya, bado Sikumsikiza na aidha nilimchukia pakubwa, binadamu alienda mbali sana na Mimi na akatafuta njia za dawa ovu na uchawi. Nilipochukua kila kitu ambacho binadamu walitaka kutoka Kwangu, walitoweka bila kuonekana tena. Kwa hivyo, Ninasema kwamba mwnadamu ana imani Kwangu kwa sababu Nampa neema nyingi kupindukia, na mambo yapo mengi sana ya kupata. Wayahudi waliniamini Mimi kwa neema Yangu, na wakanifuata Mimi popote Nilipoenda. Binadamu hawa wasiojua wenye maarifa na uzoefu finyu walitafuta tu kuona ishara na maajabu ambayo nilionyesha. Walinichukulia Mimi kuwa mkuu wa nyumba ya Wayahudi ambaye angeweza kutekeleza miujiza mikubwa zaidi. Kwa hivyo, Nilipopunga mapepo kutoka kwa binadamu walijizungumzia miongoni mwao kwa mkanganyo mkubwa wakisema Mimi ni Eliya, kwamba Mimi ni Musa, kwamba Mimi ndimi nabii wa kale zaidi kati ya wote, kwamba Mimi ndimi daktari mkuu zaidi kuliko wote. Mbali na Mimi Mwenyewe kusema kwamba Mimi ndimi maisha, njia na ukweli, hakuna yeyote angejua uwepo Wangu au utambulisho Wangu. Mbali na Mimi Mwenyewe kusema kwamba mbingu ndipo ambapo Baba Yangu anapoishi, hakuna aliyejua kwamba Mimi ni Mwana wa Mungu, na tena Mungu Mwenyewe. Mbali na Mimi Mwenyewe kusema kwamba Nitaleta ukombozi kwa wanadamu wote na kulipia mwanadamu fidia, hakuna aliyejua Mimi ni Mkombozi wa mwanadamu; binadamu alinijua tu Mimi kama mtu mkarimu na mwenye huruma. Na mbali na Mimi Mwenyewe kuweza kufafanua kila kitu kuhusu Mimi, hakuna aliyeweza kunitambua Mimi, hakuna aliyeamini kwamba Mimi ni Mwana wa Mungu aliye hai. Binadamu pia anayo imani kama hii Kwangu Mimi, na ananidanganya Mimi kwa njia hii. Binadamu anawezaje kunitolea Mimi ushuhuda wakati anayo mitazamo kama hii kunihusu Mimi?

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Unajua Nini Kuhusu Imani?

Maneno ya Mungu ya Kila Siku (Dondoo 323)

Watu wamemwamini Mungu kwa muda mrefu, ilhali wengi wao hawaelewi maana ya neno hili “Mungu”. Wanafuata tu bila kufahamu vyema. Hawajui sababu ya ni kwa nini binadamu anafaa kumwamini Mungu ama Mungu ni nini hasa. Iwapo watu wanajua tu kumfuata na kuamini Mungu, na hawajui Mungu ni nini, wala hawamwelewi Mungu, si huo ni mzaha mkuu ulimwenguni? Ingawa watu wameshuhudia matukio ya kiajabu ya mbinguni wakati huu na wamepata kusikia kuhusu elimu kuu ambayo mwanadamu hajapata kuwa nayo awali, bado wako gizani kuhusu mambo mengi ya kawaida, na ambao ni ukweli ambao haujafikiriwa. Baadhi ya watu wanaweza kusema, “Tumemwamini Mungu kwa miaka mingi. Tutakosaje kujua kufahamu Mungu ni nini? Je, si hili linatudunisha?” Lakini ukweli ni kwamba, ingawa kila mtu ananifuata wakati huu, hakuna yeyote anao ufahamu kuhusu kazi hii yote ya sasa. Hawatilii maanani hata maswali ya kawaida na rahisi zaidi, sembuse yale magumu sana kama yanayomhusu Mungu. Mnapaswa kujua kwamba hayo maswali ambayo mnayachukulia kuwa ya kawaida na hamjayatambua ndiyo mnayopaswa kuyajua zaidi, kwa maana mnajua tu kuufuata umati, hamyatilii maanani wala kuyajali yale ambayo mnafaa kujihami nayo. Je, mnajua kwa uhakika ni kwa nini mnapaswa kuwa na imani kwa Mungu? Je, mnajua kwa uhakika Mungu ni nini? Je, mnajua kwa uhakika binadamu ni nini? Kama mwanadamu ambaye yuko na imani kwa Mungu, iwapo huelewi mambo haya, je, hupotezi hadhi ya mwumini wa Mungu? Kazi Yangu leo ni hii: kuwafanya watu waelewe umuhimu wao, kuelewa yote Ninayoyafanya, na kufahamu uso wa kweli wa Mungu. Hiki ndicho kitendo cha kufunga cha mpango Wangu wa usimamizi, hatua ya mwisho ya kazi Yangu. Ndiyo maana Nawaambia yote kuhusu mafumbo ya maisha mapema, ili nyote muweze kuyakubali kutoka Kwangu. Kwa kuwa hii ndiyo kazi ya nyakati za mwisho, lazima Niwaeleze ukweli wa maisha jinsi ilivyo kwa maana hamjawahi kuyakubali, hata ikiwa huwezi kuyakubali na kuyashika, kwa maana mmepungukiwa sana na hamna matayarisho ya kutosha. Ninataka kumalizia kazi Yangu, kukamilisha kazi yote Ninayopaswa kukamilisha, na kuwafahamisha kikamilifu kuhusu yale Ninayowatuma mfanye, msije mkapotoka tena na kuanguka katika mitego ya mwovu giza linapoingia. Kuna njia nyingi zaidi ya ufahamu wenu, maneno mengi msiyoelewa. Ninyi ni wapumbavu sana. Nazijua hali zenu na upungufu wenu vema. Kwa hivyo, ingawa kuna maneno mengi ambayo hamtaweza kuyaelewa, bado Ninataka kuwaambia ukweli huu wote ambao hamjawahi kuuchukua—kwa kuwa kila mara Ninahofu iwapo, katika hali yenu ya sasa, mtaweza kusimama na kutoa ushuhuda Kwangu. Sio kwamba Nawadhalilisha. Nyote mmekuwa wanyama ambao hawajapitia mafunzo Yangu ya rasmi, na hili ni jambo ambalo linaleta shauku kuhusu kiasi cha utukufu ulio ndani yenu. Ingawa Nimetumia nguvu nyingi kushughulika juu yenu, inaonekana kuwa vipengele vizuri ndani yenu havipo kabisa, ilhali dalili za uovu zinaweza kuhesabika kwa vidole na zinatumika tu kama shuhuda za kumwaibisha Shetani. Takriban kila kitu kingine ndani yenu ni sumu ya Shetani. Mnaonekana Kwangu ni kama ambao mmepita kiwango cha kuokolewa. Kama mambo yalivyo, Naziangalia baadhi ya maonyesho na mienendo yenu, na hatimaye, Najua vimo vyenu halisi. Hiyo ndiyo maana Nina wasiwasi kwa sababu yenu: Akiachwa kuishi maisha peke yake, je, mwanadamu atapata kuwa bora ikilinganishwa na hali ilivyo sasa? Je, hamna wasiwasi kuhusu hali zenu za kitoto? Mnaweza hakika kuwa kama watu wateule wa Uyahudi, kuwa waaminifu Kwangu pekee Yangu katika kila hali? Kile mnachodhihirisha sio mchezo wa watoto ambao wametangatanga kutoka wazazi wao, bali ni unyama unaoonekana katika wanyama ambao wako mbali na mjeledi wa mchungaji wao. Mnapaswa kujua hali yenu halisi, ambayo pia ni udhaifu mlio nao nyote, ambao ni ugonjwa mlio nao nyote. Kwa hivyo ombi Langu la pekee kwenu ni kwamba muwe na ushahidi Kwangu. Msije katika hali yoyote kuyaruhusu maradhi ya zamani kuchipuka tena. Jambo la muhimu zaidi ni kutoa ushuhuda. Hicho ndicho kiini cha kazi Yangu. Mnafaa kuyakubali maneno Yangu jinsi Maria alivyokubali ufunuo wa Yehova uliomjia kupitia kwenye ndoto, kuamini na kisha kutii. Hili pekee ndilo linakubalika kama kuwa mtakatifu. Kwa maana ni ninyi ndio mnasikia neno Langu zaidi, na ambao wamebarikiwa zaidi na Mimi. Ninawapa mali Yangu yote ya thamani, kuwakabidhi kila Nilicho nacho. Hali yenu na ile ya Wayahudi, hata hivyo, ni tofauti kabisa, ni kama nchi mbili tofauti. Lakini mkilinganishwa nao, mnapokea baraka nyingi zaidi yao. Huku wao wakisubiri kwa hamu ili kujitokeza Kwangu, muda mwingi Nimekuwa na ninyi, kutumia utajiri Wangu kwa pamoja. Kwa ulinganisho, ni nini kinachowapa haki ya kunifokea na kuzozana na Mimi na kudai sehemu za mali Yangu? Hampati vya kutosha? Ninawapa vingi sana, lakini Mnachonipa ni huzuni wa kuvunja moyo na dhiki na chuki isiyokomeshwa na kutoridhika. Mnakuwa wazushi sana, ilhali bado mnaiamsha huruma Yangu. Kwa hivyo sina la kufanya ila kuizima chuki Yangu yote na kunena kupinga Kwangu kwenu tena na tena. Katika hii miaka elfu kadhaa ya kazi Yangu, Sikuwa Nimewahi kuleta pingamizi kwa mwanadamu awali kwa kuwa Nilikuwa Nimegundua kwamba katika historia ya kukua kwa mwanadamu, wale waongo zaidi miongoni mwenu ndio wanaofahamika zaidi. Wao ni kama urithi wa thamani ambao umeachiwa wewe na “babu” maarufu wa zama za kale. Jinsi gani Ninavyochukia wale nguruwe na mbwa ambao wana upungufu wa ubinadamu. Hamna hisia kabisa! Tabia zenu ni zenye uovu sana! Mioyo yenu ni migumu mno! Iwapo Ningepeleka haya maneno Yangu na hii kazi Yangu kwa Wayahudi, Ningekuwa nimeshapata utukufu muda mrefu uliopita. Lakini sio hivyo miongoni mwenu. Miongoni mwenu kuna tu kutojali kwa kikatili, madharau yenu, na visingizio vyenu. Hamna hisia na hamna thamani yoyote kabisa!

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Ufahamu Wako Kumhusu Mungu Ni Upi?

Maneno ya Mungu ya Kila Siku (Dondoo 324)

Mnafaa nyote kufahamu sasa maana kamili ya kumwamini Mungu. Maana ya imani katika Mungu Niliyozungumzia awali inahusiana na kuingia kwenu kwa hali dhahiri. Lakini leo hii si juu ya hayo. Leo hii Ningependa kuchambua umuhimu wa imani yako katika Mungu. Bila shaka, lengo la jambo hili ni kuwaelekeza kutoka kwenye mabaya; Nisipofanya hivyo, basi hamtawahi kuifahamu sura yako kamili na utakuwa ukijisifu kila mara kuhusu kujitolea kwako na uaminifu wako. Kwa maneno mengine, Nisipoangazia uovu uliomo ndani ya mioyo yenu, basi kila mmoja wenu atajitwika taji kichwani na kujipa utukufu wote. Asili zenu za majivuno na kiburi huwaelekeza kusaliti dhamiri zenu wenyewe, kuasi na kumpinga Kristo, na kufichua uovu wenu, hivyo basi kuleta kwenye mwangaza fikra zenu, mawazo, tamaa nyingi na macho yaliyojaa ulafi. Ilhali mnaendelea kukiri kwamba mtajitolea maisha yenu kwa ajili ya kazi ya Kristo, na mnakariri tena na tena mambo ya kweli yaliyosemwa na Kristo zamani zile. Hii ndiyo “imani” yenu. Hii ndiyo “imani yenu isiyokuwa na doa”. Kwa muda huu wote, Nimemweka mwanadamu katika nidhamu ya hali ya juu. Iwapo uaminifu wako unakuja na nia na masharti, basi ni heri Nisijihusishe na huo mnaoita uaminifu wenu hata kidogo, kwa maana Ninachukia wale hunidanganya kupitia kwa nia zao na kunanihadaa na masharti. Natamani tu mwanadamu awe mwaminifu kabisa Kwangu, na afanye mambo yote kwa ajili ya, na kudhibitisha neno hilo moja: imani. Ninachukizwa na matumizi yenu ya maneno matamu ili Unifurahishe Mimi. Kwa maana daima Mimi napenda mtende pia kwa ukweli mtupu na uwazi na hivyo Ningependa pia mfanye matendo yenu Kwangu kwa imani ya kweli. Inapofika katika swala la imani, watu wengi hufikiri kwamba wanamfuata Mungu kwa sababu wako na imani, la sivyo hawangevumilia mateso hayo. Basi Nakuuliza hivi: Ni kwa nini humheshimu Mungu ilhali unaamini kuwepo Kwake? Ni kwa nini, basi, haumchi Mungu moyoni mwako iwapo unaamini kuwa Mungu Yupo? Unakubali kuwa Kristo ni kupata mwili kwa Mungu, basi ni kwa nini uwe na dharau Kwake? Kwa nini unatenda bila heshima Kwake? Ni kwa nini unamhukumu wazi wazi? Ni kwa nini siku zote unachunguza Yeye anakoenda? Mbona usijisalimishe katika mipango Yake? Ni kwa nini hutendi kulingana na neno Lake? Ni kwa nini unamhadaa na kumpokonya matoleo Yake? Ni kwa nini unazungumza katika nafasi ya Kristo? Ni kwa nini unatoa hukumu ya kubaini iwapo kazi Yake na neno Lake ni ya kweli? Mbona unathubutu kumkufuru Yeye kisiri? Ni mambo haya na mengine ndiyo yanayounda imani yenu?

Kila sehemu ya usemi na tabia zenu hufichua dalili za kutoamini katika Kristo ulizobeba ndani yako. Nia na malengo yenu kwa yale mnayoyafanya yamejaa kutoamini; hata hiyo hisi itokayo kwa macho yenu imetiwa doa na dalili hizi. Kwa maneno mengine, kila mmoja wenu, katika kila dakika ya kila siku, amebeba vipengele vyenu vya kutoamini. Hii ina maana kuwa kila wakati mko katika hatari ya kumsaliti Kristo, kwa maana damu iliyo ndani ya mishipa yenu imechanganyika na kutomwamini Mungu Aliyepata mwili. Kwa hivyo, Ninasema kwamba nyayo mnazoziwacha katika njia ya imani katika Mungu si nyingi. Safari yenu katika njia ya kumwamini Mungu haina msingi mzuri, na badala yake mnafanya kazi bila ya kujali matokeo yake. Nyinyi huwa na shaka na neno la Kristo na huwezi kulitia katika matendo mara moja. Hii ndio sababu ya nyinyi kutokuwa na imani katika Kristo, na daima kuwa na fikira kumhusu Kristo ndio sababu nyingine ya nyinyi kutoamini Kristo. Kuwa na shaka kila mara kuhusu kazi ya Kristo, kuacha neno Lake kuangukia sikio lisilosikia, kuwa na maoni kwa kila kazi inayofanywa na Kristo na kutoifahamu vizuri kazi hiyo, kuwa na ugumu wa kutupilia mbali fikira zako hata baada ya nyinyi kupewa sababu za kufanya vile, na kadhalika; hizi zote ni dalili za kutoamini zilizochanganyika ndani ya mioyo yenu. Ingawa mnafuata kazi ya Kristo na kamwe hubaki nyuma, kuna uasi mwingi uliochanganyika ndani ya mioyo yenu. Uasi huu ni doa la uchafu katika imani yenu kwa Mungu. Pengine hamkubaliani na haya, lakini iwapo huwezi kutambua nia yako kutoka kwayo, basi wewe ndiwe utakayeangamia. Kwa maana Mungu hustawisha wale wanaomwamini kwa kweli pekee, wala sio wale walio na shaka na hasa wale wanaomfuata shingo upande licha ya kutowahi kuamini kuwa Yeye ni Mungu.

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Je, Wewe Ni Muumini wa Kweli wa Mungu?

Maneno ya Mungu ya Kila Siku (Dondoo 325)

Watu wengi hawapati shangwe ndani ya ukweli, na vile vile katika hukumu. Badala yake, wao hupata furaha kwa nguvu na mali; watu kama hawa wanaitwa wanaotafuta mamlaka. Wanatafuta tu madhehebu yaliyo na ushawishi duniani na wahubiri na waalimu wanaotoka katika seminari. Hata ingawa wameikubali njia ya ukweli, bado wako na shaka ndani yao na hawawezi kujitolea kikamilifu. Wanazungumzia kujinyima kwa sababu ya Mungu, lakini macho yao yamelenga tu wahubiri wakuu na waalimu, na Kristo anasukumwa pembeni. Mioyo yao imejaa umaarufu, mali na utukufu. Hawaamini kamwe kuwa mtu wa kawaida tu anaweza kuwashinda wengi vile, kwamba mtu asiye wa kutambulika kwa macho tu anaweza kukamilisha watu. Hawaamini kuwa hawa watu wasio na sifa, walio kwenye vumbi na vilima vya samadi ni watu waliochaguliwa na Mungu. Wanaamini kuwa kama watu wale wangekuwa vyombo vya wokovu Wake Mungu, basi mbingu na ardhi zitageuzwa juu na chini na watu wote watacheka kupindukia. Wanaamini kuwa iwapo Mungu atawachagua watu wasio na sifa yoyote wafanywe viumbe kamili, basi wao walio na sifa watakuwa Mungu Mwenyewe. Maoni yao yamechafuliwa na kutoamini; hakika, mbali na kutoamini, wao ni wanyama wasio na maana. Kwa maana wao wanathamini tu nyadhifa, hadhi kuu na mamlaka; wanachokithamini sana ni makundi makuu na madhehebu makuu. Hawana heshima hata kidogo kwa wale wanaoongozwa na Kristo; wao ni wasaliti tu waliomgeuka Kristo, kuugeuka ukweli na uhai.

Unachopendezwa nacho sio unyenyekevu wa Kristo, ila ni wale wachungaji wa uongo wenye umaarufu. Hupendi maarifa au kupendeza kwa Kristo, bali unapenda wale watukutu wanaojihusisha na ulimwengu mchafu. Unauchekelea uchungu wa Kristo asiyekuwa na pahali pa kulaza kichwa Chake, na badala yake unatamani maiti zinazokamata sadaka na kuishi katika uasherati. Hauko tayari kupokea mateso pamoja na Kristo, lakini unakimbilia mikononi mwa wapinzani wa Kristo hata ingawa wanakupa nyama za mwili pekee, barua na udhibiti pekee. Hata sasa, moyo wako bado unawaendea wao, sifa zao, hadhi zao, na ushawishi wao. Ilhali unazidi kuchukua mtazamo ambapo unaona kazi ya Kristo kuwa ngumu sana kukubali na huko tayari kuikubali. Hii ndiyo maana Ninasema hauna imani ya kumkubali Kristo. Sababu iliyokufanya Umfuate mpaka leo hii ni kuwa hukuwa na chaguo jingine. Moyoni mwako milele mna picha nyingi refu; huwezi kusahau kila neno lao na matendo yao, au maneno yao ya ushawishi na mikono. Wao ni, katika moyo wenu, wakuu milele na tena mashujaa milele. Lakini hivi sivyo ilivyo na Kristo wa leo hii. Yeye moyoni mwako kamwe Hana umuhimu na kamwe Hastahili heshima. Kwa maana Yeye ni wa kawaida sana, mwenye ushawishi mdogo zaidi na Yuko mbali na ukuu.

Kwa vyovyote vile, Ninasema kuwa wote wale wasioenzi ukweli ni wasioamini na waasi wa ukweli. Watu kama hawa hawatawahi kuipokea idhini ya Kristo. Umeweza sasa kutambua kiasi cha kutoamini kilicho ndani yako? Na kiasi gani cha usaliti kwa Kristo? Kwa hivyo Nakuhimiza hivi; Kwa maana umeichagua njia ya ukweli, basi huna budi ila kujitolea na moyo wote; usiwe na kuchanganyikiwa au wa kusitasita. Unafaa kufahamu kuwa Mungu si wa ulimwengu huu au wa mtu yeyote, bali ni wa wale wote wanaoamini katika Mungu kwa kweli, wote wale wanaomwabudu, na wote wale waliojitolea na wanaoamini katika Mungu.

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Je, Wewe Ni Muumini wa Kweli wa Mungu?

Maneno ya Mungu ya Kila Siku (Dondoo 326)

Imani ya watu katika Mungu hutafuta kumfanya Mungu kuwapa hatima inayofaa, kuwapa neema yote chini ya jua, kumfanya Mungu mtumishi wao, kumfanya Mungu adumishe uhusiano wa amani, wa kirafiki pamoja nao, na ili kusiwe na mgogoro wowote kati yao. Yaani, imani yao kwa Mungu inahitaji Mungu kutoa ahadi ya kutimiza mahitaji yao yote, kuwapa chochote wanachoomba, kama ambavyo inasema katika Biblia “Nitazisikiliza sala zenu zote.” Wanahitaji Mungu kutomhukumu mtu yeyote au kushughulika na mtu yeyote, kwa kuwa Mungu daima ni Mwokozi Yesu mkarimu, ambaye huwa na uhusiano mzuri na watu wakati wote na mahali pote. Hivi ndivyo watu wanavyomwamini Mungu: Wao wanafanya madai kwa Mungu bila haya, wakiamini kwamba wawe ni waasi au watiifu, Atawapa tu kila kitu bila kufikiri. Wao daima “wanadai madeni” kutoka kwa Mungu, wakiamini kwamba lazima “Awalipe” bila upinzani wowote na, aidha, Alipe mara dufu; wanafikiri, Mungu awe amepata chochote kutoka kwao au la, Anaweza tu kuwa chini yao; Hawezi kuwapanga watu kiholela, sembuse Hawezi kuwafunulia watu hekima Yake ya kale ya siri na tabia ya haki kama Anavyotaka, bila ruhusa yao. Wao huungama tu dhambi zao kwa Mungu wakiamini kwamba Mungu atawasamehe tu, kwamba Hawezi kuchoshwa na kufanya hilo, na kwamba hili litaendelea milele. Wanamwamuru Mungu wapendavyo tu, wakiamini kwamba Yeye atawatii tu, kwa sababu imerekodiwa katika Biblia kwamba Mungu hakuja kutumikiwa na wanadamu, ila kuwatumikia, na kwamba Alikuja kuwa mtumishi wa mwanadamu. Je, si siku zote mmeamini kwa njia hii? Wakati ambapo hamuwezi kupata chochote kutoka kwa Mungu basi mnataka kukimbia. Na wakati ambapo hamuelewi kitu mnapata hasira, na hata kwenda mbali ili kutoa aina zote za matusi. Hamuwezi tu kumruhusu Mungu Mwenyewe kuonyesha kikamilifu hekima na shani Yake, lakini badala yake unataka tu kufurahia urahisi wa muda na faraja. Hadi sasa, mtazamo wenu katika imani yenu kwa Mungu umekuwa sawa na maoni ya zamani. Mungu akiwaonyesha utukufu mdogo tu mnakosa furaha; je, mnaona sasa jinsi kimo chenu kilivyo? Msifikiri kuwa ninyi nyote ni waaminifu kwa Mungu wakati kwa kweli maoni yenu ya zamani hayajabadilika. Wakati ambapo hakuna chochote kibaya kinachokuangukia, unafikiri kwamba kila kitu kinaelekea kwa urahisi na unampenda Mungu kwa vilele vya juu zaidi. Lakini kitu kidogo kinapokukumba, unakushuka kuzimuni. Je, huku ni wewe kuwa mwaminifu kwa Mungu?

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Mnapaswa Kuweka Pembeni Baraka za Hadhi na Kuelewa Mapenzi ya Mungu ya Kumletea Mwanadamu Wokovu

Maneno ya Mungu ya Kila Siku (Dondoo 327)

Katika kutafuta kwenu, mna dhana, matumaini, na siku za baadaye nyingi sana za kibinafsi. Kazi ya sasa ni ili kushughulikia tamaa yenu ya hadhi na tamaa zenu badhirifu. Matumaini, hadhi, na dhana yote ni mifano bora kabisa ya tabia ya kishetani. Sababu ambayo vitu hivi vipo katika mioyo ya watu ni kwa sababu hasa sumu ya Shetani daima inaharibu fikira za watu, na daima watu hawawezi kuondoa vishawishi hivi vya Shetani. Wanaishi katikati ya dhambi ilhali hawaiamini kuwa dhambi, na bado wao huwaza: “Tunaamini katika Mungu, hivyo lazima Atupe baraka na kupanga kila kitu kwa ajili yetu ipasavyo. Tunaamini katika Mungu, hivyo lazima tuwe wa cheo cha juu kuliko wengine, na lazima tuwe na hadhi zaidi na maisha zaidi ya baadaye kuliko mtu mwingine yeyote. Kwa kuwa tunaamini katika Mungu, lazima Atupe baraka bila kikomo. Vinginevyo, hakungeitwa kuamini katika Mungu.” Kwa miaka mingi, mawazo ambayo watu wametegemea kwa ajili ya kuendelea kuishi kwao yamekuwa yakiharibu mioyo yao hadi kiwango ambapo wamekuwa wadanganyifu, waoga, na wenye kustahili dharau. Hawakosi tu ushupavu na uamuzi, lakini pia wamekuwa walafi, wenye kiburi, na wa kudhamiria. Kabisa wanakosa uamuzi wowote upitao sana ubinafsi, na hata zaidi, hawana ujasiri hata kidogo wa kuondoa shutuma za ushawishi huu wa giza. Fikira na maisha ya watu ni mabovu sana kiasi kwamba mitazamo yao juu ya kuamini katika Mungu bado ni miovu kwa namna isiyovumilika, na hata watu wanaponena kuhusu mitazamo yao juu ya imani katika Mungu haivumiliki kabisa kusikia. Watu wote ni waoga, wasiojimudu, wenye kustahili dharau, na dhaifu. Hawahisi maudhi kwa nguvu za giza, na hawahisi upendo kwa nuru na ukweli; badala yake, wanafanya kila wanaloweza kuvifukuza. Je, si fikira na mitazamo yenu ya sasa iko hivi tu? “Kwa kuwa ninaamini katika Mungu ninapaswa tu kumiminiwa baraka na inapaswa kuhakikishwa kwamba hadhi yangu kamwe haitelezi na kwamba inabaki kuwa juu kuliko ile ya wasioamini.” Hamjakuwa mkihodhi mtazamo wa aina hiyo ndani yenu kwa mwaka mmoja au miaka miwili tu, lakini kwa miaka mingi. Kufikiria kwenu kwa kibiashara kumekua sana. Ingawa mmewasili kwenye hatua hii leo, bado hamjaacha hadhi lakini mnapambana bila kukoma kuuliza kuihusu, na mnaichunguza kila siku, kwa hofu kubwa kwamba siku moja hadhi yenu itapotea na jina lenu litaharibiwa. Watu hawajawahi kuweka kando tamaa yao ya starehe. Hivyo, Ninapowahukumu hivi leo, mtakuwa na kiwango kipi cha ufahamu mwishowe? Mtasema kwamba ingawa hadhi yenu haiko juu, mmefurahia kuinuliwa na Mungu. Kwa sababu mmezaliwa katika tabaka la chini, hamna hadhi, lakini mnapata hadhi kwa sababu Mungu anawainua—hiki ni kitu ambacho Aliwapa. Leo mna uwezo wa kibinafsi wa kupokea mafunzo ya Mungu, kuadibu Kwake, na hukumu Yake. Huku, hata zaidi, ni kuinuliwa na Yeye. Mnaweza kupokea utakaso na kuchomwa Kwake binafsi. Huu ni upendo mkuu wa Mungu. Kupitia enzi hakujakuwa hata mtu mmoja ambaye amepokea utakaso na kuchomwa Kwake, na hakuna hata mtu mmoja ambaye ameweza kukamilishwa kwa maneno Yake. Mungu sasa Ananena nanyi ana kwa ana, Akiwatakasa, Akifichua uasi wenu wa ndani—huu kweli ni kuinuliwa na Yeye. Watu wana uwezo upi? Kama wao ni wana wa Daudi au ni uzao wa Moabu, kwa jumla, watu ni viumbe ambao hawana chochote chenye kustahili kujigamba kuhusu. Kwa kuwa nyinyi ni viumbe wa Mungu, lazima mtekeleze wajibu wa kiumbe. Hakuna mahitaji mengine kwenu. Hivi ndivyo mnavyopaswa kuomba: “Ee Mungu! Kama nina hadhi au la, sasa ninajielewa mwenyewe. Hadhi yangu ikiwa juu ni kwa sababu ya kuinuliwa na Wewe, na ikiwa iko chini ni kwa sababu ya mpango Wako. Kila kitu ki mikononi Mwako. Sina chaguzi zozote, wala malalamishi yoyote. Ulipanga kwamba ningezaliwa katika nchi hii na miongoni mwa watu hawa, na yote ninayopaswa kufanya ni kuwa mtiifu kabisa chini ya utawala Wako kwa sababu kila kitu ki ndani ya yale ambayo Umepanga. Sifikirii kuhusu hadhi; hata hivyo, mimi ni kiumbe tu. Ukiniweka kwenye shimo lisilo na mwisho, katika ziwa la moto wa jahanamu, mimi si chochote isipokuwa kiumbe. Ukinitumia, mimi ni kiumbe. Ukinikamilisha, mimi bado ni kiumbe. Usiponikamilisha, bado nitakupenda kwa sababu mimi si zaidi ya kiumbe. Mimi si chochote zaidi ya kiumbe mdogo sana aliyeumbwa na Bwana wa uumbaji, mmoja tu miongoni mwa wanadamu wote walioumbwa. Ni Wewe uliyeniumba, na sasa kwa mara nyingine tena Umeniweka katika mikono Yako ili unitumie Utakavyo. Niko tayari kuwa chombo Chako na foili Yako kwa sababu vyote ni vile Umepanga. Hakuna anayeweza kubadili jambo hilo. Vitu vyote na matukio yote yako katika mikono Yako.” Wakati utakapofika ambapo hutafikiria tena hadhi, basi utaondokana na hilo. Hapo tu ndipo utaweza kwa kujiamini na kutafuta kwa ujasiri, na ni hapo tu ndipo moyo wako unaweza kuwa huru dhidi ya vikwazo vyovyote. Mara tu watu watakapokuwa wamenasuliwa kutoka katika mambo haya, basi hawatakuwa na shaka tena. Ni nini kinawahangaisha wengi wenu sasa hivi? Mnazuiwa daima na hadhi na mnashughulishwa daima na matarajio yenu wenyewe. Kila wakati mnayaangalia matamshi ya Mungu, mkitaka kusoma misemo inayohusu hatima ya wanadamu na kutaka kujua matarajio yenu ni yapi na hatima yenu itakuwa ipi. Mnajiuliza, “Kweli nina matarajio yoyote? Je, Mungu ameyaondoa? Mungu anasema tu kwamba mimi ni foili; basi matarajio yangu ni yapi?” Ni vigumu kwa ninyi kuweka kando matarajio na kudura yenu. Sasa nyinyi ni wafuasi, na mmepata ufahamu fulani wa hatua hii ya kazi. Hata hivyo, bado hamjaweka kando tamaa yenu ya hadhi. Wakati hadhi yenu iko juu mnatafuta vizuri, lakini wakati hadhi yenu iko chini hamtafuti tena. Baraka za hadhi daima ziko katika fikira zenu. Kwa nini watu wengi hawawezi kujiondoa katika uhasi? Je, si jibu bila shaka ni kwa sababu ya matarajio ya kuvunja moyo? Mara tu matamshi ya Mungu yanapotolewa nyinyi huharakisha kuona hadhi na utambulisho wenu kweli vikoje. Mnaipa hadhi na utambulisho kipaumbele, na kuyaweka maono katika nafasi ya pili. Katika nafasi ya tatu ni kitu mnachopaswa kuingia katika, na katika nafasi ya nne ni mapenzi ya Mungu ya sasa. Nyinyi huangalia kwanza iwapo jina la Mungu kwenu kama “foili” limebadilika au la. Mnasoma na kusoma, na mnapoona kwamba jina la “foili” limeondolewa, mnafurahi sana na kumshukuru Mungu kwa nguvu sana na kuisifu nguvu Yake kuu. Lakini mnapoona kwamba nyinyi bado ni foili, mnafadhaika na msukumo ulio mioyoni mwenu unatoweka mara moja. Kadiri unavyotafuta zaidi kwa njia hii, ndivyo utakavyovuna kidogo zaidi. Kadiri ilivyo kubwa zaidi tamaa ya mtu ya hadhi, ndivyo itabidi washughulikiwe kwa uzito zaidi na ndivyo watakavyozalimika kupitia usafishaji mkubwa. Watu kama hao hawana thamani kabisa! Lazima wshughulikiwe na wahukumiwe vya kutosha ili waachane na mambo haya kabisa. Mkifuatilia kwa njia hii mpaka mwisho, hamtavuna chochote. Wale ambao hawafuatilii uzima hawawezi kubadilishwa, na wale ambao hawana kiu ya ukweli hawawezi kupata ukweli. Hulengi kufuatilia mabadiliko ya kibinafsi na uingiaji, lakini badala yake unalenga tamaa badhirifu na vitu vinavyozuia upendo wako kwa Mungu na kukuzuia kumkaribia Yeye. Je, vitu hivyo vinaweza kukubadili? Je, vinaweza kukuleta katika ufalme? Ikiwa kusudi la kufuatilia kwako si kutafuta ukweli, basi afadhali utumie fursa hii na kurudi duniani ili kufanikiwa. Kupoteza muda wako hivi kwa kweli hakuna thamani—kwa nini ujitese? Je, si kweli kwamba unaweza kufurahia mambo ya aina yote katika dunia hii nzuri? Pesa, wanawake warembo, hadhi, majivuno, familia, watoto, na kadhalika—je, matokeo haya ya dunia siyo mambo mazuri zaidi ambayo ungeweza kufurahia? Kuna faida gani kuzurura zurura hapa ukitafuta mahali ambapo unaweza kuwa na furaha? Mwana wa Adamu hana pahali pa kulaza kichwa Chake, hivyo ungekuwaje na pahali pa utulivu? Angewezaje kukuumbia pahali pazuri pa utulivu? Hilo lawezekana? Kando na hukumu Yangu, leo unaweza kupokea tu mafundisho ya ukweli. Huwezi kupata faraja kutoka Kwangu na huwezi kupata kitanda cha starehe unachotamani sana usiku na mchana. Sitakupa utajiri wa duniani. Ukifuatilia kwa kweli, basi Niko tayari kukupa njia ya uzima yote, kukutaka uwe kama samaki aliyerudi majini. Usipofuatilia kwa kweli, Nitayafuta yote. Siko tayari kutoa maneno kutoka kwa kinywa Changu kwa wale ambao ni wenye tamaa ya faraja, ambao ni kama nguruwe na mbwa tu!

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Mbona Huna Hiari ya Kuwa Foili?

Maneno ya Mungu ya Kila Siku (Dondoo 328)

Jichunguzeni ili mwone kama mnatenda haki katika kila jambo mnalotenda, na iwapo matendo yenu yote yanachunguzwa na Mungu: Hii ndiyo kanuni ambayo kwayo wale wanaomwamini Mungu wanafanya shughuli zao. Mtaitwa wenye haki kwa sababu mnaweza kumridhisha Mungu, na kwa sababu mnakubali utunzaji na ulinzi wa Mungu. Machoni pa Mungu, wote wanaokubali utunzaji, ulinzi na ukamilishaji wa Mungu, na wale wanaopatwa na Yeye, ni wenye haki, na Yeye huwaona kuwa wenye thamani. Kadri mnavyozidi kuyakubali maneno ya sasa ya Mungu, ndivyo mtakavyozidi kuweza kupokea na kuelewa mapenzi ya Mungu, na ndivyo basi mtakavyoweza kuishi kwa kudhihirisha maneno ya Mungu na kuyakidhi mahitaji Yake zaidi. Hili ndilo agizo la Mungu kwenu na ndilo jambo ambalo nyote mnapaswa kuweza kufikia. Mkitumia fikira zenu wenyewe kumpima na kumwekea Mungu mipaka, kana kwamba Mungu ni sanamu ya udongo isiyobadilika, na mkimwekea Mungu mipaka kabisa katika vigezo vya Biblia na kumweka katika mawanda ya kazi yenye mipaka, basi hii inathibitisha kwamba mmemshutumu Mungu. Kwa sababu Wayahudi katika Agano la Kale walimchukulia Mungu kuwa sanamu yenye umbo lisilobadilika waliloshikilia mioyoni mwao, kana kwamba Mungu angeweza tu kuitwa Masihi, na Yeye aliyeitwa Masihi pekee ndiye Angeweza kuwa Mungu, na kwa sababu binadamu walimtumikia na kumwabudu Mungu kana kwamba Alikuwa sanamu ya udongo (isiyo na uhai), walimsulubisha Yesu wa wakati huo msalabani, wakimhukumu kifo—hivyo Yesu asiye na hatia Alihukumiwa kifo. Mungu hakuwa na kosa lolote, mwanadamu alikataa kumsamehe, naye alisisitiza kumhukumu afe na basi Yesu akasulubishwa. Kila wakati mwanadamu huamini kuwa Mungu habadiliki na humfafanua kwa msingi wa kitabu kimoja tu, Biblia, kana kwamba mwanadamu ana ufahamu wa kina kuhusu usimamizi wa Mungu, kana kwamba mwanadamu anavyo vitu vyote atendavyo Mungu katika kiganja cha mkono wake. Wanadamu ni wapumbavu kupita kiasi, wana kiburi kikubwa sana, na wote wana kipaji cha kutia chumvi sana wanapoelezea jambo. Bila kujali jinsi kiwango chako cha ufahamu kumhusu Mungu kilivyo, bado Nasema kwamba humfahamu Mungu, kwamba wewe ni mtu ambaye humpinga Mungu zaidi, na kwamba umemshutumu Mungu, kwa sababu huna uwezo kabisa wa kuiheshimu kazi ya Mungu na kutembea katika njia ya kufanywa kamilifu na Mungu. Kwa nini Mungu hatosheki kamwe na matendo ya mwanadamu? Kwa sababu mwanadamu hamjui Mungu, kwa sababu ana fikira nyingi sana, na kwa sababu maarifa yake kuhusu Mungu hayaafikiani na uhalisi hata kidogo, lakini badala yake hurudia tu mada ile ile bila mabadiliko na hutumia mwelekeo ule ule katika kila hali. Na hiyo, kwa kuwa Amekuja duniani leo, Mungu anasulubishwa kwa mara nyingine na mwanadamu. Wanadamu dhalimu! Kuwafumba watu macho na kula njama, kupokonyana na kunyang’anya mmoja kutoka kwa mwingine, kung’ang’ania umaarufu na mali, kuuana—haya yote yataisha lini? Licha ya mamia ya maelfu ya maneno ambayo Mungu amezungumza, hakuna hata mmoja ambaye ameacha kufanya upumbavu. Watu hutenda kwa ajili ya familia zao, watoto wao, kazi zao, matarajio yao ya baadaye, cheo, majivuno, na pesa, kwa sababu ya chakula, mavazi, na mwili. Lakini kuna yeyote ambaye matendo yake kwa kweli ni kwa ajili ya Mungu? Hata miongoni mwa wale ambao wanatenda kwa ajili ya Mungu, kunao wachache tu wanaomfahamu Mungu. Ni watu wangapi ambao hawatendi kwa ajili ya maslahi yao? Ni wangapi wasiowakandamiza na kuwatenga wengine ili kulinda vyeo vyao wenyewe? Na hivyo, Mungu amehukumiwa kifo mara nyingi kwa nguvu, na mahakimu wakatili wengi mno wamemhukumu Mungu na kumsulubisha msalabani tena. Wangapi wanaweza kuitwa wenye haki kwa sababu wanatenda mambo kwa ajili ya Mungu kwa kweli?

Je, ni rahisi sana kukamilishwa mbele ya Mungu kama mtakatifu au mtu mwenye haki? Ni kauli ya ukweli kwamba, “hakuna wenye haki katika dunia hii, wenye haki hawapo katika dunia hii.” Mnapokuja mbele za Mungu, fikirieni kile mnachovaa, tafakarini kila neno na kitendo chenu, juu ya kila fikira na wazo lenu na hata ndoto mnazoota kila siku—vyote ni kwa manufaa yenu wenyewe. Je, hivi sivyo hali halisi ilivyo? “Haki” haimaanishi kuwatolea wengine sadaka wala haimaanishi kumpenda jirani yako vile unavyojipenda na haimaanishi kuepukana na mizozo na ugomvi, au kunyang’anya na kuiba. Haki inamaanisha kuchukua agizo la Mungu kama wajibu wako na kuiheshimu mipango na utaratibu wa Mungu kama wito wako utokao mbinguni, bila kujali wakati ama mahali, kama tu yote ambayo Bwana Yesu aliyafanya. Hii ndiyo haki ambayo amezungumzia Mungu. Kwamba Lutu aliweza kuitwa mwenye haki ni kwa sababu aliwaokoa wale malaika wawili waliotumwa na Mungu bila kuzingatia faida ama hasara yake mwenyewe; inaweza kusemwa tu kwamba alichotenda wakati huo kinaweza kuitwa haki, lakini hawezi kuitwa mwanadamu mwenye haki. Ilikuwa tu ni kwa sababu Lutu alikuwa amemwona Mungu ndipo akawatoa wasichana wake wawili badala ya malaika, lakini tabia yake yote ya hapo awali haikuwakilisha haki. Na hivyo Nasema “hakuna wenye haki katika dunia hii.” Hata kati ya wale ambao wako katika mkondo wa urejesho, hakuna hata mmoja anayeweza kuitwa mwenye haki. Haijalishi matendo yako ni mazuri vipi, haijalishi jinsi unavyoonekana kulisifu jina la Mungu, si kuwapiga na kuwalaani wengine, wala kuwaibia na kuwapora wengine, bado huwezi kuitwa mwenye haki, kwa sababu haya ndiyo mtu wa kawaida ana uwezo wa kuwa nayo. Kilicho muhimu sasa ni kwamba wewe humfahamu Mungu. Inaweza tu kusemwa kwamba kwa sasa una kiasi kidogo cha ubinadamu wa kawaida, lakini hakuna vipengele vya haki viliyozungumziwa na Mungu, na hivyo hakuna chochote unachotenda ambacho kinaweza kuthibitisha kwamba unamfahamu Mungu.

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Waovu Hakika Wataadhibiwa

Maneno ya Mungu ya Kila Siku (Dondoo 329)

Hapo awali, Mungu alipokuwa mbinguni, mwanadamu alimtendea Mungu kwa namna ya udanganyifu. Leo, Mungu amekuwa miongoni mwa wanadamu—hakuna anayejua imekuwa ni kwa miaka mingapi—lakini katika kufanya mambo mwanadamu bado anatenda kwa namna isiyo ya dhati na anajaribu kumdanganya Yeye. Je, mwanadamu hayuko nyuma sana katika kufikiri kwake? Ndivyo ilivyokuwa na Yuda: Kabla Yesu aje, Yuda angesema uwongo ili kuwadanganya ndugu zake, na hata baada ya Yesu kuja, bado hakubadilika; hakumjua Yesu hata kidogo, na mwishowe alimsaliti Yesu. Je, hii haikuwa kwa sababu hakumfahamu Mungu? Kama leo bado hamumfahamu Mungu, basi kuna uwezekano kwamba mnaweza kuwa Yuda mwingine, na kufuatilia hili, msiba wa kusulubiwa kwa Yesu katika Enzi ya Neema maelfu ya miaka iliyopita unaweza kurudiwa tena. Je, hamwamini hili? Ni ukweli! Hivi sasa, watu wengi wako katika hali kama hiyo—Naweza kuwa Ninayasema haya mapema sana kiasi—na watu wa aina hii wote ni wahusika wanaochukua nafasi ya Yuda. Sizungumzi upuuzi, bali kwa msingi wa ukweli—na huna budi ila kuridhika. Ingawa watu wengi wanajifanya kuwa wanyenyekevu, katika mioyo yao hakuna kingine ila dimbwi la maji yaliyokufa, handaki la maji yanayonuka. Hivi sasa kuna wengi sana wa aina hii katika kanisa na mnafikiri Sina habari yoyote kuhusu hili. Leo, Roho Wangu huniamulia na kunishuhudia. Unafikiri kwamba Sijui lolote? Je, unafikiri Sielewi lolote kuhusu fikira za ujanja katika mioyo yenu, mambo mnavyoweka katika mioyo yenu? Je, ni rahisi hivyo kumdanganya Mungu? Je, unafikiri kwamba unaweza kumtendea kwa njia yoyote unayotaka? Hapo zamani, Nilikuwa na wasiwasi msije mkazuiwa, hivyo Niliendelea kuwapa uhuru, lakini binadamu hawakuweza kutambua kwamba Nilikuwa mzuri kwao, na Nilipowapa kidogo walitaka mengi. Ulizieni kati yenu: Sijawahi kumshughulikia yeyote, na Sijawahi kumkemea yeyote kijuujuu—na bado Sina tashwishi juu ya nia na fikira za mwanadamu. Je, unafikiri Mungu Mwenyewe, ambaye Mungu anamshuhudia, ni mjinga? Hivyo, Ninasema wewe ni kipofu sana! Sitakufunua, lakini hebu tuone tu jinsi unavyoweza kuwa mpotovu. Hebu tuone iwapo ujanja wako mdogo unaweza kukuokoa, ama iwapo kujaribu kadri uwezavyo kumpenda Mungu kutakuokoa. Leo, Sitakushutumu; hebu tungoje mpaka wakati wa Mungu tuone Atakavyokuadhibu. Sina wakati wa kupoteza kufanya maongezi madogo madogo na wewe sasa, na Sina nia ya kuchelewesha kazi Yangu kuu kwa ajili yako tu. Buu kama wewe hastahili muda utakaomchukua Mungu kukushughulikia—kwa hivyo hebu tuone tu jinsi unavyoweza kuwa mpotovu. Watu kama hawa hawafuatilii maarifa yaa Mungu hata kidogo, wala hawampendi Yeye hata kidogo, na bado wanataka Mungu awaite wenye haki—huu si utani? Kwa sababu idadi ndogo ya watu ni waaminifu kwa kweli, Nitalenga tu katika kuzidi kumpa mwanadamu uhai. Nitakamilisha tu kile Ninachohitaji kukamilisha leo, lakini katika siku zijazo Nitaleta adhabu kwa kila mmoja kulingana na kile ambacho amefanya. Nimesema yote yanayopaswa kusemwa, kwa sababu hii hasa ndiyo kazi Ninayoifanya. Ninafanya kile tu Ninachopaswa kufanya, na si kile Nisichopaswa kufanya. Hata hivyo, Natumai kwamba mtatumia muda zaidi katika kutafakari: Kiwango gani hasa cha ufahamu wako kuhusu Mungu ni cha kweli? Je, wewe ni mtu ambaye amemsulubisha Mungu kwa mara nyingine? Maneno Yangu ya mwisho ni haya: Ole wao wamsulubishao Mungu.

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Waovu Hakika Wataadhibiwa

Maneno ya Mungu ya Kila Siku (Dondoo 330)

Unapoitembea njia ya leo, ufuatiliaji unaofaa zaidi ni wa aina gani? Katika ufuatiliaji wako, unapaswa kujiona kama mtu wa aina gani? Unafaa kujua jinsi unavyopaswa kukabili yote yanayokukumba leo, yawe majaribu ama taabu, ama kuadibu na laana isiyo ya huruma. Unapaswa kuyazingatia kwa uangalifu katika hali zote. Mbona Nasema hili? Nasema hili kwa sababu yanayokukumba leo hata hivyo ni majaribu mafupi yanayotokea tena na tena; huenda huyaoni kuwa yanayosumbua sana kiakili, na hivyo unayaacha mambo yaende mrama, na huyachukulii kuwa rasilmali ya thamani katika ufuatiliaji wa maendeleo. Wewe ni asiyejali kweli! Sana kiasi kwamba unaifikiria rasilmali kana kwamba ni wingu linaloelea machoni pako, na huyathamini haya mapigo makali yanayokuja mara kwa mara—mapigo ambayo ni ya muda mfupi na yanayoonekana kuwa dhaifu kwako—ila unayatazama kwa utulivu, usiyafikirie kwa dhati na kuyachukulia tu kama mapigo ya mara moja. Wewe ni mfidhuli sana! Kwa mashambulio haya makali, mashambulio yaliyo kama dhoruba na yanayokuja mara kwa mara unaonyesha kupuuza kwa dharau; wakati mwingine hata unatabasamu bila hisia, ukifichua jinsi usivyojali—kwani hujawahi kujiwazia mbona unashinda ukipitia “misiba” kama hii. Je, Namtendea mwanadamu bila haki kwa kiasi kikubwa? Je, Natafuta makosa kwako? Ingawa shida zako za akili huenda zisiwe nzito jinsi Nilivyoeleza, kupitia utulivu wako wa nje, tangu zamani umebuni taswira nzuri sana ya dunia yako ya ndani. Hakuna maana ya Mimi kukuambia kwamba jambo la pekee lililofichika katika vina vya moyo wako ni matusi yasiyo adilifu na athari dhaifu ya huzuni ambayo wengine hawayaoni. Kwa sababu unahisi kwamba si haki hata kidogo kupitia majaribu kama haya, unatoa matusi; majaribu hayo hukufanya uhisi ukiwa wa dunia, na kwa sababu ya hili, unajawa na ghamu. Badala ya kutazama nidhamu na mapigo haya yanayorudiwa kama ulinzi bora kabisa, unayaona kuwa uchokozi wa Mbinguni usio na sababu, ama vinginevyo kama adhabu inayokufaa. Wewe ni mpumbavu sana! Unazifungia nyakati nzuri gizani bila huruma; mara kwa mara unaona nidhamu na mapigo mazuri kuwa mashambulio kutoka kwa adui zako. Huwezi kubadilika kulingana na mazingira yako sembuse kutaka kufanya hivyo kwani huna hiari ya kupata chochote kutoka kwa kuadibu huku kunakorudiwa na unakoona kuwa katili. Hufanyi juhudi yoyote kutafuta au kuchunguza, na, unajikabidhi tu kwa yale majaaliwayako, kwenda pahali popote itakapokuelekeza. Yanayoonekana kwako kuwa marudio makali hayajaubadili moyo wako wala hayajatwaa udhibiti wa moyo wako; badala yake, yanakuchoma moyoni. Unaona “kuadibu huku katili” kuwa adui wako katika maisha haya tu na hujapata chochote. Wewe unajidai sana! Ni mara chache ambapo unaamini kwamba unapitia majaribu kama haya kwa sababu wewe ni duni sana; badala yake, unajiona aliye na bahati mbaya sana, na kusema kwamba Mimi daima hutafuta makosa kwako. Kufikia leo, kwa kweli una kiasi kipi cha maarifa ya kile Ninachosema na kufanya? Usifikiri kwamba una kipaji cha asili, uliye chini kidogo ya mbingu lakini juu sana ya dunia. Wewe si mwerevu zaidi kuliko mtu mwingine yeyote—na hata inaweza kusemwa kwamba wewe ni mpumbavu zaidi kuliko watu wowote duniani walio na mantiki, kwani unajiona sana kuwa bora, na hujawahi kujiona kuwa mtu wa chini; inaonekana kwamba unayachunguza matendo Yangu kwa utondoti kabisa. Kwa kweli, wewe ni mtu ambaye kimsingi hana mantiki, kwa kuwa hufahamu kabisa Nitakachofanya sembuse kutambua Ninachofanya sasa. Kwa hivyo Nasema kwamba wewe hata hulingani na mkulima mzee anayefanya kazi kwa bidii shambani, mkulima ambaye hafahamu maisha ya binadamu hata kidogo na bado anategemeabaraka za Mbinguni wakati anapolima shamba. Huyafikirii maisha yako hata kidogo, hujui chochote chenye sifa sembuse kujijua. Wewe “una hadhi ya juu” sana!

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Wale Wasiojifunza na Wanaosalia Wajinga: Je, Wao Sio Wanyama?

Maneno ya Mungu ya Kila Siku (Dondoo 331)

Mmeyapuuza mafundisho Yangu yaliyorudiwa tangu zamani. Hata mnayachukulia kuwa vitu vya kuchezea wakati hamna shughuli, na daima mnayafikiria kuwa “hirizi yenu wenyewe ya kujilinda.” Mnaposhutumiwa na Shetani, mnaomba; wakati ninyi ni hasi, mnalala; wakati mna furaha, mnakwenda huku na huko; Ninapowashutumu, mnanyenyekea mno; na mnapotengana nami, mnacheka kwa shauku. Ukiwa katika umati, hakuna mwingine mwenye hadhi kubwa kukuliko, lakini kamwe hujioni kuwa fidhuli zaidi kuwaliko wote. Daima wewe ni mwenye kiburi, aliyeridhika na mwenye maringo kukithiri. Je, inawezekanaje “waungwana na wasichana wadogo” na “mabwana na mabibi” ambao hawajifunzi na wanabaki kuwa wajinga wanawezaje kuyachukulia maneno Yangu kuwa hazina ya thamani? Sasa Nitaendelea kukuhoji: Umejifunza nini hasa kutoka kwa maneno na kazi Yangu katika muda mrefu kama huu? Je, hujakuwa mjanja zaidi katika udanganyifu wako? Mstaarabu zaidi katika mwili wako? Wa kawaida zaidi katika mtazamo wako Kwangu? Nakwambia waziwazi: Nimefanya kazi nyingi sana, lakini imeongeza ujasiri wako, ujasiri ambao awali ulikuwa kama ule wa panya. Hofu yako Kwangu inapunguka kila siku, kwani Mimi ni mkarimu sana, na kamwe sijawatilia vkwazo kwa mwili wako kwa njia ya ukatili; Labda unavyoona, Mimi Nasema maneno makali—lakini kwa mara nyingi huwa Nakutolea tabasamu, na ni nadra ambapo Nakukaripia ana kwa ana. Aidha, Mimi husamehe udhaifu wako kila wakati, na ni kwa sababu ya hili tu ndiyo unanitendea jinsi nyoka humtendea mkulima mzuri. Napendezwa na kiwango chajuu cha ujuzi na ustadi kwa uwezo wa mwanadamu kuchunguza sana! Acha nikwambie ukweli mmoja: Leo haijalishi hata kidogo iwapo una moyo wa uchaji au la; Mimi sina wasiwasi wala wahaka kuhusu hilo. Lakini pia ni lazima Nikuambie hili: Wewe, huyu “mtu mwenye kipaji,” asiyejifunza na anasalia mjinga, hatimaye utaangamizwa na ujanja wako wenye kiburi na kujioenda—ni wewe utakayeteseka na kuadibiwa. Siwezi kuwa mjinga sana kiasi cha kukuandama unapoendelea kuteseka kuzimuni, kwani Mimi silingani na wewe. Usisahau kwamba wewe ni kiumbe aliyelaaniwa na Mimi, na bado aliyefunzwa na kuokolewa na Mimi. Huna chochote Ninachoweza kutotaka kutengana nacho. Kila Nifanyapo kazi, Sizuiliwi na watu, matukio ama vitu vyovyote. Mitazamo na maoni Yangu kuwahusu wanadamu daima yamebaki yale yale. Mimi si mwenye tabia njema kwako hasa, kwa kuwa wewe ni nyongeza kwa usimamizi Wangu na hauko bora sana kuliko kiumbe mwingine. Nakushauri hivi: Kila wakati, kumbuka kwamba wewe ni kiumbe wa Mungu tu! Unaweza kuishi nami, lakini unapaswa kujua utambulisho wako; usijione kuwa wa hadhi ya juu sana. Hata Nisipokushutumu, ama kukushughulikia, na Nakutazama kwa tabasamu, hili halithibitishi kwamba wewe unalingana na Mimi; unapaswa kujua kwamba wewe ni mmoja wa wale wanaofuatilia ukweli, sio ukweli wenyewe! Hupaswi kamwe kukoma kubadili kwa kuambatana na maneno Yangu. Huwezi kuepuka hili. Nakushauri ujaribu kujifunza jambo wakati huu muhimu, fursa hii adimu ikujapo. Usinipumbaze; Sikutaki utumie ubembelezaji kujaribu kunidanganya. Unaponitafuta, yote siyo kwa ajili Yangu, bali kwa ajili yako mwenyewe!

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Wale Wasiojifunza na Wanaosalia Wajinga: Je, Wao Sio Wanyama?

Maneno ya Mungu ya Kila Siku (Dondoo 332)

Kila siku mnayoiishi sasa ni ya maana sana na muhimu sana kwa hatima yenu na majaliwa yenu, kwa hivyo mnapaswa kufurahia kila mlicho nacho na kila dakika inayopita. Mnapaswa kutumia muda wenu vizuri ili muweze kujinufaisha, ili msije kuishi maisha haya bure. Pengine mnajihisi kukanganyikiwa mnaojiuliza ni kwa nini Ninazungumza maneno haya. Kwa kweli, Sijapendezwa na matendo ya yeyote kati yenu. Kwa maana matumaini ambayo Nimekuwa nayo juu yenu si vile tu mlivyo sasa. Kwa hivyo, Naweza kuelezea hivi: Nyinyi nyote mko hatarini kabisa. Vilio vyenu vya kwanza kwa ajili ya wokovu na matamanio yako ya kwanza ya kufuatilia ukweli na kutafuta nuru vinakaribia mwisho. Hivi ndivyo mtakavyonifidia mwishowe, ambacho ni kitu ambacho Sijawahi kutarajia. Sitamani kuzungumza kinyume cha ukweli, kwa maana mmenivunja moyo sana. Pengine hampendi kuiachia mada hapo na hutaki kuukabili ukweli, lakini ni lazima niwaulize swali hili: Kwa miaka hii yote, mioyo yenu imejawa na nini? Mioyo yenu inamwamini nani? Usiseme kwamba swali Langu limekuja ghafla sana, na usiniulize kwa nini Nauliza swali kama hilo. Mnapaswa kujua hili: Ni kwa sababu Ninawafahamu vizuri, ninawajali sana, na Ninajitolea moyo Wangu sana kwa kile mnachofanya, ndio maana Ninawauliza kwa kurudiarudia na kubeba taabu isiyoelezeka. Hata hivyo, malipo Yangu yamekuwa ni kupuuzwa na kukataliwa kusikostahimilika. Hivyo mmekuwa na ajizi sana juu Yangu; Ninawezaje kutojua kitu kuhusu hilo? Kama mnaamini kwamba hili linawezekana, inathibitisha ukweli zaidi kwamba hamnitendei wema kabisa. Kisha Ninawaambia kwamba mnajidanganya nyinyi wenyewe. Nyinyi nyote ni werevu sana kiasi kwamba hamjui kile mnachofanya; sasa mtatumia nini ili kunipatia ufafanuzi?

Swali muhimu sana kwangu ni mioyo yenu inamwamini nani. Pia Ningependa kila mmoja wenu afikiri vizuri na kisha ajiulize uaminifu wake uko kwa nani na anaishi kwa ajili ya nani? Pengine hamjawahi kuliangalia swali hili kwa makini, hivyo nitawapatia jibu lake.

Wale wenye kumbukumbu nzuri wataukubali ukweli huu: Mwanadamu anaishi kwa ajili yake mwenyewe na ni mwaminifu kwake mwenyewe. Siamini kwamba jibu lenu ni sahihi kabisa, kwa maana kila mmoja wenu anaishi maisha yake, kila mmoja wenu anapambana katika dhiki yake. Kwa hivyo, kile mnachokuwa waaminifu kwacho ni watu mnaowapenda, na vitu vinavyowapendeza, na wala nyinyi si waaminifu kwa nafsi zenu wenyewe. Kwa sababu kila mmoja wenu anaathiriwa na watu, matukio, na vitu vinavyowazunguka, kimsingi nyinyi si waaminifu kwa nafsi zenu. Nasema maneno haya siyo kwa sababu ya kuunga mkono ninyi kuwa waaminifu kwa nafsi zenu, bali kufichua uaminifu wenu kwa kitu chochote kile. Maana kwa miaka yote hii Sijawahi kupokea uaminifu kutoka kwa mtu yeyote kati yenu. Mmekuwa wafuasi Wangu kwa miaka mingi sana, lakini hamjawahi kunionesha hata chembe ya uaminifu. Badala yake mmekuwa mkizunguka kwa watu mnaowapenda na vitu vinavyowapendeza sana, na kuviweka karibu na mioyo yenu na havijawahi kuachwa, wakati wowote, mahali popote. Mnapokuwa na hamu ama shauku na kitu chochote kile Mnachokipenda, siku zote mnakuwa ni wakati ambapo mnanifuata, au hata wakati mnaposikiliza maneno Yangu. Hivyo nasema, mnatumia uaminifu ninaowataka muonyeshe, kuwa badala yake waaminifu na kufurahia “vipenzi” wenu. Ingawa mnaweza kutoa sadaka ya kitu kimoja au vitu viwili kwa ajili Yangu, hakuwakilishi vitu vyenu vyote, na haionyeshi kwamba ni Kwangu ambako uaminifu wako uko kwa kweli. Mnajiweka wenyewe katika shughuli ambazo mnazipenda: Wengine ni waaminifu kwa watoto, wengine kwa waume, wake, utajiri, kazi, wenye vyeo, umaarufu, au wanawake. Kwa maana kile ambacho mnakuwa waaminifu kwacho, hujawahi kuhisi kuchoshwa au kukerwa nacho, badala yake, mnatamani kuwa na kiasi kikubwa zaidi na ubora wa vitu ambavyo ninyi mu waaminifu kwavyo na hamjawahi kukata tamaa. Mimi mwenyewe na maneno Yangu daima hutupwa pembeni katika masuala ya vitu mnavyovipenda. Na hamna namna isipokuwa kuyaweka mwisho; wengi hata wanaondoka sehemu ya mwisho kwa ajili ya kuwa waaminifu kwa kitu ambacho hawajakigundua bado. Hawajawahi kuniweka mioyoni mwao kwa kiwango chochote kile. Pengine mtafikiri kwamba ninahitaji mambo mengi sana kutoka kwenu au Ninawahukumu kimakosa, lakini je, mmeshawahi kufikiri kuhusu ukweli huu kwamba mnapotumia muda kwa furaha pamoja na familia yenu, hujawahi kuwa mwaminifu kwangu hata mara moja? Wakati kama huu, hii haiwaumizi? Mioyo yenu inapojawa na furaha kwa kupokea malipo kwa kazi zenu, haiwavunji moyo kwamba hamjajitweka kwa ukweli wa kutosha? Ni lini mmewahi kulia kwa kukosa idhinisho langu? Mnaitesa akili yenu na kupata maumivu makubwa kwa ajili ya watoto wenu, lakini bado hamjaridhika, bado mnaamini kwamba hamjaweka jitihada za kutosha kwao, kwamba hamjatumia nguvu zenu zote. Lakini Kwangu, mmekuwa ajizi na wa kutojali, mkiniweka tu katika kumbukumbu zenu na wala Sidumu ndani ya mioyo yenu. Kujitolea Kwangu na jitihada zangu daima hupita bila nyinyi kuzihisi, na wala hamjawahi kuweka jitihada ili muweze kuelewa. Nyinyi hutafakari kidogo tu na kuamini kwamba hiyo itatosha. “Uaminifu” wa aina hii sio ule ambao Nimekuwa nikiutazamia, bali ni ule ambao umekuwa machukizo Kwangu kwa muda mrefu. Hata hivyo, licha ya kile Ninachokisema, mtaendelea kukubali kitu kimoja tu au vitu viwili na kushindwa kukikubali kwa ukamilifu, kwa maana nyote “mnajiamini” sana, na siku zote mnachagua kipi mtakachokikubali kutoka katika maneno Niliyoyasema. Kama bado mko hivi, Nina njia katika akiba za kukabiliana na kujiamini kwenu, na Nitazitumia ili muweze kuyatambua maneno Yangu yote kuwa ni kweli na sio upotoshaji wa ukweli.

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Wewe U Mwaminifu kwa Nani?

Maneno ya Mungu ya Kila Siku (Dondoo 333)

Kama sasa Ningeweka utajiri mbele yenu na kuwaambia kuwa mchague kwa uhuru, huku Nikijua kwamba[a] sitawahukumu, basi wengi wangechagua utajiri na kuacha ukweli. Wazuri miongoni mwenu wangeacha utajiri na kuchagua ukweli shingo upande, ilhali wale ambao wako katikati wangekumbatia utajiri kwa mkono mmoja na kwa mkono mwingine kuukumbatia ukweli. Kwa njia hii, je, rangi zenu halisi si zingejidhihirisha? Unapochagua ukweli kwa kulinganisha na kitu chochote ambacho u mwaminifu kwacho, wote mtafanya maamuzi kama hayo, na tabia yenu itabakia kuwa ile ile. Si ndivyo ilivyo? Je, hakuna watu wengi miongoni mwenu waliobadilika badilika katika kuchagua baina ya wema na ubaya? Katika mashindano kati ya mazuri na mabaya, nyeusi na nyeupe, mna uhakika na uchaguzi mlioufanya kati ya familia na Mungu, watoto na Mungu, amani na vurugu, utajiri na umasikini, hadhi na kuwa mtu wa kawaida, kusaidiwa na kutupiliwa mbali, na kadhalika. Kati ya familia yenye amani na familia iliyovunjika, nyinyi huchagua ya kwanza bila kusita; kati ya utajiri na wajibu, safari hii pia mnachagua ya kwanza, bila kuwa na nia ya kurudi ufuoni[b] kati ya starehe na umasikini, tena mlichagua ya kwanza; kati ya watoto, mke, mume na Mimi, mnachagua za kwanza; na kati ya dhana na ukweli, kwa mara nyingine tena mlichagua ya kwanza. Nikikabiliwa na kila namna ya matendo yenu maovu, karibu sana Nimepoteza imani Yangu kwenu. Ninashangazwa sana na kwamba mioyo yenu inapinga kulainishwa. Miaka mingi ya kujitolea na jitihada Yangu imeniletea kuvunjika moyo tu nanyi kupoteza imani Nami. Hata hivyo, matumaini Yangu juu yenu yanakua kila siku inayopita, kwa kuwa siku Yangu tayari imekwisha kuwekwa wazi kwa kila mtu. Lakini, bado mnaendelea kuyafuata yale ambayo ni ya giza na maovu, na mnakataa kulegeza mshiko wenu. Kwa kufanya hivyo, mtapata matokeo gani? Mmewahi kutafakari kwa makini kuhusu hili? Kama mngetakiwa kuchagua tena, msimamo wenu ungekuwa upi? Bado lingekuwa ni chaguo la kwanza? Je, yale ambayo mngenipatia bado yangekuwa maudhi na huzuni ya majuto? Je, mioyo yenu bado ingekuwa migumu? Je bado mngekuwa hamjui cha kufanya ili kuufariji moyo Wangu? Kwa wakati wa sasa, chaguo lenu ni nini? Mtayakubali maneno Yangu, au yatawachosha? Siku Yangu imewekwa wazi kabisa mbele ya macho yenu, na kile mnachokiona ni maisha mapya na mwanzo mpya. Hata hivyo, ni lazima niwaambie kwamba huu mwanzo mpya si mwanzo wa kazi mpya iliyopita, bali ni mwisho wa ya kale. Yaani, hili ni tendo la mwisho. Ninaamini nyote mtaelewa kitu ambacho si cha kawaida kuhusu mwanzo huu mpya. Lakini siku moja hivi karibuni, mtaelewa maana halisi ya huu mwanzo mpya, kwa hivyo hebu sote tuipite na kuikaribisha tamati inayofuata! Hata hivyo, kitu ambacho Ninaendelea kutofurahishwa nacho ni kwamba pale mnapokabiliwa na mambo ambayo si ya haki na mambo ya haki, daima mmekuwa mkichagua chaguo la kwanza. Lakini hayo yote yako katika maisha yenu ya zamani. Pia Ninatumai kuyasahau yale yote yaliyotokea katika maisha yenu ya zamani, kitu kimoja baada ya kingine, ingawa hili ni gumu sana kufanya. Lakini bado nina njia nzuri sana ya kulitimiza. Acha maisha ya baadaye yachukue nafasi ya maisha ya zamani na kuacha kivuli cha maisha yenu ya zamani kiondolewe badala ya utu wenu halisi wa leo. Hii ina maana kwamba nitawasumbua tena ili uweze kufanya maamuzi kwa mara nyingine tena na tutaona kabisa nyinyi ni waaminifu kwa nani.

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Wewe U Mwaminifu kwa Nani?

Tanbihi:

a. Matini ya asili haina kauli “kuelewa kwamba.”

b. Kurudi ufuoni: nahau ya Kichina, ikiwa na maana kwamba “mtu kuacha njia zake za uovu.”

Maneno ya Mungu ya Kila Siku (Dondoo 334)

Wakati wowote hatima inatajwa, muichukulie kwa uzito maalumu; nyinyi nyote ni mahususi hasa kuhusu jambo hili. Baadhi ya watu hawawezi kusubiri kumsujudia Mungu ili hatimaye kuwa na hatima nzuri. Naweza kutambua hamu yenu, ambayo haihitaji kuonyeshwa katika maneno. Kabisa hamtaki miili yenu ianguke katika maafa, na hata zaidi, hamtaki kushuka katika adhabu ya muda mrefu hapo baadaye. Mnatarajia tu kujiruhusu muishi kwa uhuru zaidi kidogo, kwa urahisi zaidi kidogo. Na hivyo unahisi mwenye wasiwasi hasa wakati wowote hatima inatajwa, ukiwa na hofu kubwa kwa undani kwamba, usipokuwa mwangalifu vya kutosha, unaweza kumkosea Mungu na hivyo upate adhabu unayostahili. Hamjasita kufanya maafikiano kwa ajili ya hatima zenu, na wengi wenu ambao wakati mmoja walikuwa wa kuzunguka na wapuuzi hata kwa ghafla wamegeuka hususa wapole na wa dhati; unyofu wenu hata una mzizimo. Pasipo kutilia maanani, nyinyi nyote mna mioyo “minyoofu”, na kutoka mwanzo hadi mwisho mmejifungua wazi Kwangu bila kuficha siri zozote katika mioyo yenu, yawe lawama, udanganyifu, au ibada. Kwa jumla, “mmekiri” kwa uwazi Kwangu yale mambo muhimu katika pahali pa siri yenye kina kwenu. Mambo kama yalivyo, Sijawahi kuepuka mambo kama haya, kwa sababu yamekuwa ya kawaida Kwangu. Afadhali muingie katika bahari la moto kwa hatima yenu ya mwisho kuliko kupoteza mlia mmoja wa nywele ili kupata kibali cha Mungu. Sio kwamba Ninakuwa wa kulazimishia imani kwenu; ni kwamba mioyo yenu ya ibada ni pungufu hasa kwa kukabiliana na kila kitu Ninachofanya. Hamuwezi kuelewa Ninachomaanisha, hivyo basi acheni Niwatolee maelezo rahisi: Mnachohitaji si ukweli na maisha; si kanuni za jinsi ya kutenda, na hasa siyo kazi Yangu yenye kujitahidi. Yote mnayohitaji ni yale ambayo mnamiliki katika mwili—mali, hadhi, familia, ndoa, nk. Ninyi mnatupilia mbali kabisa maneno na kazi Yangu, hivyo Naweza kujumlisha imani yako kwa neno moja: shingo upande. Mtafanya lolote ili kutimiza mambo ambayo bila shaka mmejitolea, lakini Nimegundua kwamba hampuuzi kila kitu kwa ajili ya mambo ya imani yenu katika Mungu. Badala yake, nyinyi ni waaminifu tu kiasi, na kiasi. Hiyo ndiyo sababu Nasema kwamba wale wanaokosa moyo wa usafi mkubwa ni washinde katika imani yao katika Mungu. Fikiria kwa uangalifu—je, kunao wengi washinde miongoni mwenu?

Mnapaswa kujua kwamba mafanikio katika kumwamini Mungu yanatimizwa kwa sababu ya matendo ya watu wenyewe; wakati watu hawafanikiwi lakini badala yake wanashindwa, hiyo pia ni kwa sababu ya matendo yao wenyewe, sio matokeo ya vipengele vingine. Ninaamini kwamba mngefanya kitu chochote kitachukua ili kupata kitu kufanyika ambacho ni kigumu zaidi na kinachohitaji mateso zaidi kuliko kumwamini Mungu, na kwamba mngekichukulia kwa makini sana. Hamngetaka hata kufanya makosa yoyote; hizi ni aina za juhudi zisizolegea ambazo nyote mmeweka katika maisha yenu wenyewe. Nyinyi hata mna uwezo wa kunidanganya Mimi katika mwili chini ya hali ambazo hamuwezi kudanganya yeyote wa familia yenu wenyewe. Hii ni tabia yenu thabiti na kanuni ambayo mnatumia katika maisha yenu. Je, si bado mnaendeleza picha ya uongo ili kunidanganya Mimi, kwa ajili ya hatima yenu, na kuwa na hatima nzuri na ya furaha? Nafahamu kwamba ibada yenu na unyofu wenu ni wa muda tu; je, matamanio yenu na gharama mnayolipa ni ya sasa tu na si ya baadaye? Mnataka tu kutumia nguvu moja ya mwisho ili kupata hatima nzuri. Azma yenu ni kubadilisha tu; siyo ili msiwe wenye deni kwa ukweli, na ni hasa msinilipe kwa ajili ya gharama Niliyolipa. Kwa neno, mko tu tayari kutumia ujanja wenu, lakini hamtaki kuipigania. Je, si haya ni matakwa yenu ya dhati? Sio lazima mjifiche, na hata zaidi, sio lazima mpige mbongo zenu juu ya hatima yenu hadi pale ambapo hamuwezi kula au kulala. Je, si ni kweli kwamba matokeo yenu yatakuwa yameamuliwa mwishowe? Mnapaswa kufanya wajibu wenu wenyewe kwa kadri ya uwezo wenu kwa mioyo iliyo wazi na wima, na muwe tayari kufanya chochote kitakachohitajika. Kama mlivyosema, wakati siku itakuja, Mungu hatakosa kumjali mtu yeyote ambaye aliteseka au kulipa gharama kwa ajili Yake. Aina hii ya imani ni yenye thamani kuishikilia, na hampaswi kuisahau kamwe. Ni tu kwa njia hii Ninaweza kutuliza akili Yangu kuwahusu. Vinginevyo, Sitakuwa na uwezo wa kutuliza akili Yangu kuwahusu, na milele mtakuwa malengo ya chuki Yangu. Kama nyote mnaweza kufuata dhamiri zenu na kutoa yote kwa ajili Yangu, msiwache jitihada zozote kwa ajili ya kazi Yangu, na kutenga maisha ya jitihada za kazi ya injili Yangu, basi si moyo Wangu mara kwa mara utaruka kwa furaha kwa ajili yenu? Si Mimi Nitakuwa na uwezo wa kutuliza akili Yangu kuwahusu? Ni aibu kwamba kile mnaweza kufanya ni cha kusikitisha sana na sehemu ndogo sana ya kile Ninachotarajia; hivi sasa, ni jinsi gani mna nyongo ya kutafuta kutoka Kwangu kile mnatumainia?

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Juu ya Hatima

Maneno ya Mungu ya Kila Siku (Dondoo 335)

Hatima yenu na majaliwa yenu ni muhimu sana kwenu—ni za matatizo makubwa. Mnaamini kuwa msipofanya mambo kwa uangalifu sana, itakuwa sawa na kutokuwa na hatima, na uharibifu wa majaliwa yenu. Lakini mmewahi kufikiri kwamba kama juhudi mtu hutumia ni kwa ajili ya hatima zao tu, hizo ni kazi tu zisizo na matunda? Juhudi za aina hiyo si halisi—ni bandia na danganyifu. Kama ni hivyo, wale ambao wanafanya kazi kwa ajili ya hatima yao watapokea maangamizo yao ya mwisho, kwa sababu kushindwa katika imani ya watu katika Mungu hutendeka kwa sababu ya udanganyifu. Hapo awali Nilisema kuwa Mimi Sipendi kusifiwa mno au kupendekezwa, au kuchukuliwa kwa shauku. Ninapenda watu waaminifu kukubali hali ilivyo kuhusu ukweli na matarajio Yangu. Hata zaidi, Ninapenda wakati watu wanaweza kuonyesha uangalifu mkubwa na kufikiria kwa ajili ya moyo Wangu, na wakati wanaweza hata salimisha kila kitu kwa ajili Yangu. Ni kwa njia hii tu ndipo Moyo wangu unaweza kuliwazwa. Sasa hivi, ni mambo mangapi yapo yanayowahusu ambayo Mimi Nachukia? Ni mambo mangapi yapo yanayowahusu ambayo Napenda? Je, hakuna kati yenu ambaye ametambua ubaya wote ambao mmeonyesha kwa ajili ya hatima zenu?

Katika moyo Wangu, Sitaki kuwa Mwenye kudhuru moyo wowote ambao ni chanya na wa motisha, na Mimi hasa Sitaki kupunguza bidii ya mtu yeyote ambaye anafanya wajibu wake kwa uaminifu; hata hivyo, ni lazima Niwakumbushe kila mmoja wenu juu ya upungufu wenu na roho chafu sana ndani ya mioyo yenu. Azma ya kufanya hivyo ni kutarajia kwamba mtaweza kutoa mioyo yenu ya kweli katika kukabiliana na maneno Yangu, kwa sababu kile Nachukia zaidi ni udanganyifu wa watu kuelekezwa Kwangu. Natarajia tu kuwa katika hatua ya mwisho ya kazi Yangu, mnaweza kutekeleza kwa kujitokeza, kujitoa kikamilifu, na wala sio shingo upande tena. Bila shaka, Natarajia pia kuwa nyote muwe na hatima nzuri. Hata hivyo, bado Nina mahitaji Yangu ambayo ni kwenu nyinyi mfanye uamuzi bora kabisa katika kujitoa Kwangu pekee na moyo wa ibada ya mwisho. Kama mtu hana moyo huo wa ibada pekee, mtu huyo hakika atakwenda kuwa thamani ya Shetani, na Mimi Sitaendelea kumtumia. Nitamtuma nyumbani akatunzwe na wazazi wake. Kazi yangu imekuwa ya msaada sana kwa ajili yenu; kile Natarajia kupata kutoka kwenu ni moyo ulio mwaminifu na unaotia msukumo kwenda juu, lakini hadi sasa mikono Yangu bado ni tupu. Fikiria kulihusu: Wakati siku moja bado Nitakuwa na kukwazika kusikoelezeka, mtazamo Wangu kuwaelekea utakuwa upi? Je, Mimi bado Nitakuwa mwema? Je, Moyo wangu utakuwa bado mtulivu? Je, mnaelewa hisia za mtu ambaye kwa kujitahidi amelima lakini hakuvuna hata nafaka moja? Je, mnaelewa ukubwa wa jeraha la mtu ambaye amepigwa kipigo kikubwa? Je, mnaweza kuonja uchungu wa mtu aliyejawa na matumaini ambaye anafaa kuachana na mtu kwa uhusiano mbaya? Je, mmeona hasira ya mtu ambaye amekasirishwa? Je, mnaweza kujua hisia ya kulipiza kisasi kwa haraka ya mtu ambaye amekuwa akichukuliwa kwa uadui na udanganyifu? Kama mnaelewa fikira za watu hawa, Nadhani haipaswi kuwa vigumu kwenu kuwaza mtazamo Mungu Atakuwa nao wakati ule wa adhabu Yake. Hatimaye, Natarajia nyote mnaweka jitihada kali kwa ajili ya hatima yenu wenyewe; hata hivyo, ni bora msitumie njia za udanganyifu katika juhudi zenu, au bado Nitasikitishwa nanyi katika moyo Wangu. Je, kusikitishwa kwa aina hii huelekea wapi? Je, hamjidanganyi wenyewe? Wale ambao hufikiria kuhusu hatima yao na bado wanaiharibu ni watu wenye uwezekano mdogo zaidi wa kuokolewa. Hata kama watu hawa watakerwa, ni nani atawahurumia? Kwa jumla, bado Niko tayari Kuwatakia muwe na hatima inayofaa na nzuri. Hata zaidi, Natarajia kwamba hakuna kati yenu atakayeanguka katika maafa.

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Juu ya Hatima

Iliyotangulia: Kufunua Upotovu wa Wanadamu

Inayofuata: Kufunua Upotovu wa Wanadamu (II)

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp