95 Kujitolea Kwa Upendo

1

Ee Mwenyezi Mungu! Wewe ni mtukufu, mzuri na Unayependeza!

Ulifuata mapenzi ya Baba kuja humu duniani,

Ukivalia mwili, kuonyesha ukweli na kuleta hukumu.

Wewe ni mwenye haki na mkuu, na huvumilii kosa lolote la mwanadamu.

Umevumilia kila kitu bila malalamiko ya kumwokoa binadamu.

Siku baada ya siku, mwaka baada ya mwaka,

Unavumilia kashfa nyingi, mateso, shida nyingi kutoka kwa watu wa ulimwengu huu.

Katika magonjwa na uchungu Unawakimu na kuwanyunyizia watu wateule wa Mungu,

Ukifanya ukweli na uzima ndani yetu.

Ee Mungu! Hii inafichua hisia Zako za kweli.

Ni utoaji wa maisha Yako, udhihirisho wa upendo Wako wote.

Upendo Wako ni mkubwa sana, tabia Yako ni yenye heshima sana isiyo na kifani.

Tunakosaje kucheza kwa furaha na kuimba sifa Zako?

2

Ee Mwenyezi Mungu! Wewe ni mtukufu, mzuri na Unayependeza!

Unatembea kati ya makanisa na kutamka maneno.

Maneno Yako yanatuongoza kila siku.

yakihukumu na kutakasa tabia zetu potovu.

Kupitia majaribu na usafishaji tunaona upendo Wako wa kweli.

Siku baada ya siku, mwaka baada ya mwaka,

Unavumilia upinzani, uasi, kuelewa vibaya, na malalamiko yetu.

Kwa uvumilivu usiochoka Unakimu mahitaji yetu.

Tumepata ukweli na tumekuwa na maisha mapya.

Ee Mungu! Tunapopitia kazi Yako, tunakuja kuujua upendo Wako.

Tumeona upendo, rehema, haki na utakatifu Wako.

Tuko tayari kukukabidhi mioyo yetu, kujitoa wenyewe kabisa.

Matamanio ya mioyo yetu ni kukupenda daima na kukushuhudia.

Iliyotangulia: 93 Mbona Upendo Wa Kweli Ni Mgumu Sana Kupatikana Duniani

Inayofuata: 96 Mungu Amelipa Gharama Kubwa Mno

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Maudhui Yanayohusiana

418 Umuhumi wa Maombi

Sala ni mojawapo ya njia ambazo mwanadamu hutumia kushirikiana na Mungu, ni njia ambayo mwanadamu hutumia kumwita Mungu, na ni mchakato...

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp