Programu ya Kanisa la Mwenyezi Mungu

Sikiliza sauti ya Mungu na ukaribishe kurudi kwa Bwana Yesu!

Tunawakaribisha wote wanaotafuta ukweli wawasiliane nasi.

Neno Laonekana katika Mwili

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

(Ma)tokeo ya Kutafuta 0

Hakuna matokeo yaliyopatikana

Kujadili Maisha ya Kanisa na Maisha Halisi

Watu huhisi kuwa wao wanaweza tu kubadilika katika maisha yao ya kanisani, na kuwa iwapo hawaishi ndani ya kanisa, mbadiliko hauwezekani, kuwa hawawezi kutimiza mbadiliko katika maisha yao halisi. Mwaweza kutambua suala hili ni lipi? Nimeongea juu ya kumleta Mungu katika maisha halisi, na hii ndiyo njia kwa wale wanaomwamini Mungu kuingia katika uhalisi wa maneno ya Mungu. Kwa kweli, maisha ya kanisa ni njia ndogo tu ya kuwakamilisha watu. Mazingira ya msingi ya kuwakamilisha wanadamu bado ni maisha halisi. Hiki ndicho kitendo halisi na mafunzo halisi Niliyozungumzia, yanayowaruhusu wanadamu kutimiza maisha ya ubinadamu wa kawaida na kuishi kwa kudhihirisha mfano wa mtu wa kweli katika maisha ya kila siku. Kipengele kimoja ni kwamba mtu lazima aelimike ili kuinua kiwango chake mwenyewe cha elimu, aweze kuelewa maneno ya Mungu, na kutimiza uwezo wa kuelewa. Kipengele kingine ni kwamba mtu lazima ajiandae na ujuzi wa msingi unaohitajika kuishi kama mwanadamu ili kutimiza ufahamu na busara ya ubinadamu wa kawaida, kwa sababu wanadamu wamepungukiwa sana katika sehemu hii takriban kwa ukamilifu. Aidha, mtu lazima pia aje kufurahia maneno ya Mungu kupitia kwa maisha ya kanisa, na polepole kupata ufahamu dhahiri wa ukweli.

Kwa nini husemwa kuwa katika kumwamini Mungu, mtu sharti amlete Mungu katika maisha halisi? Maisha ya kanisa hayawezi tu kumbadilisha mwanadamu, lakini muhimu zaidi, mwanadamu anapaswa kuingia katika uhalisi wa maisha halisi. Mlikuwa daima mkizungumzia hali yenu ya kiroho na masuala ya kiroho huku mkipuuza mafunzo katika mambo mengi katika maisha halisi, na pia kupuuza kuingia kwenu ndani yao. Mliandika kila siku, mkasikiliza kila siku, na mkasoma kila siku. Mliomba mlipokuwa mnapika: “Ee Mungu! Na uwe maisha yangu ndani yangu. Niipite siku hii namna gani? Tafadhali nibariki, nipe nuru. Lolote utakalonipa nuru kuhusu leo, tafadhali niruhusu kulielewa kwa wakati huu, ili maneno Yako yawe kama maisha yangu.” Ninyi pia mliomba mlipokuwa mnakula chajio: “Ee Mungu! Umetupatia sisi chakula hiki. Utubariki sisi. Amina! Tafadhali turuhusu kukutumainia Wewe kwa ajili ya maisha yetu. Uwe nasi. Amina!” Baada ya kumaliza chajio chako na huku ukisafisha vyombo ukaanza kuparaganya tena: “Ee Mungu, mimi ni bakuli hii. Tumepotoshwa na Shetani na tuko tu kama mabakuli ambayo yametumika na ni lazima yaoshwe kwa maji. Wewe ndiwe maji, maneno Yako ndiyo maji yaliyo hai yanayotoa kwa maisha yangu.” Kufumba kufumbua, ilikuwa wakati wa kulala, na ulianza kuparaganya tena: “Ee Mungu!” Umenibariki mimi na kuniongoza siku nzima. Ninakushukuru kwa dhati....” Hivi ndivyo ulitamatisha siku yako na kuingia kwenye usingizi. Watu wengi sana waliishi namna hii kila siku, na hata mpaka sasa, hawajazingatia kuingia halisi, ila wanasisitiza tu maneno matupu kwenye maombi yao. Haya ndiyo maisha ya awali ya mwanadamu—haya ndiyo maisha yao ya kale. Watu wengi sana wako hivi, wamekosa mafundisho yoyote halisi, na wana mabadiliko halisi machache sana. Wanatoa tu maneno matupu katika maombi yao, wakimwendea Mungu kwa maneno yao lakini wanakosa uketo katika ufahamu wao. Hebu tuchukue mfano rahisi zaidi—kusafisha nyumba yako. Unaona kuwa nyumba yako ni chafu, kwa hiyo unakaa hapo na kuomba: “Ee Mungu! Tazama upotovu ambao Shetani amegusisha kwangu. Mimi ni mchafu tu kama nyumba hii. Ee Mungu! Nakusifu na kukushukuru Wewe. Bila wokovu na nuru Yako, singetambua jambo hili.” Unakaa hapo tu na kuparaganya, ukiomba kwa muda mrefu, na kisha unajifanya kuwa hakuna kilichotendeka, ukitenda kama mwanamke mzee mwenye kusemasema ovyo. Unapitisha maisha yako ya kiroho hivi bila kuingia kokote kwa kweli katika uhalisi kabisa, na vitendo vingi sana vya kujipurukusha! Katika mafunzo ya kuingia kwenye uhalisi, yanahusu maisha halisi ya watu na kuhusisha matatizo yao ya utendaji—hili tu ndilo linaweza kuwabadilisha. Pasipo maisha halisi, wanadamu hawawezi kubadilishwa. Kuna haja gani kutumia maneno matupu kwenye maombi yao? Bila kuelewa asili ya wanadamu, kila kitu ni kupoteza muda, na pasipo njia ya kutenda, kila kitu ni kupoteza juhudi! Maombi sahihi yanaweza kudumisha hali sahihi kati ya watu, lakini hayawezi kuwabadilisha kikamilifu. Kujua kujidai, kiburi, majisifu, kujiona na tabia potovu ya binadamu—ujuzi wa mambo haya hauji kwa maombi, bali hutambulika kwa kufurahia maneno ya Mungu, na unajulikana kwa kupewa nuru na Roho Mtakatifu katika maisha halisi. Watu siku hizi wote huweza kuongea vizuri, na wamesikiza mahubiri ya juu sana, yaliyo juu sana kuliko mengine yoyote katika enzi, lakini ni kidogo mno yanayotekelezwa katika maisha yao halisi. Hivyo ni kusema, katika maisha halisi ya watu hakuna Mungu, na wanakosa maisha ya mtu mpya baada ya kubadilishwa. Hakuna kuishi kwa kudhihirisha ukweli katika maisha halisi, na hakuna kumleta Mungu katika maisha halisi. Maisha ya watu yanaendelezwa kana kwamba wao ni wana wa jehanamu. Je, huku si kupotoka dhahiri?

Ili kurudisha mfanano wa mtu wa kawaida, yaani, kutimiza kuwa na ubinadamu wa kawaida, watu hawawezi tu kumpendeza Mungu kwa maneno yao. Wanajiumiza wenyewe kwa kufanya hivyo, na haileti faida yoyote kwa kuingia na kubadili kwao. Kwa hivyo, ili kufikia mbadiliko, watu lazima watende kidogo kidogo, waingie taratibu, watafute na kuchunguza kidogo kidogo, waingie ndani kutoka kwa halisi, na kuishi maisha ya utendaji wa ukweli, maisha ya watakatifu. Tangu sasa kuendelea, inahusisha mambo halisi, vitu halisi, na mazingira halisi, kuwaruhusu watu kuwa na mafunzo ya utendaji. Haiwahitaji hao kutoa maneno matupu; badala yake, inahitaji mafunzo katika mazingira halisi. Watu huja kutambua kuwa wao ni wenye ubora duni wa tabia , na kisha wana kula na kunywa halisii kwa maneno ya Mungu halisi, kuingia halisi, na utandaji halisi, hivi ndivyo wanavyopokea uhalisi na hivi ndivyo kuingia kunaweza kufanyika hata haraka zaidi. Ili kuwabadili watu, lazima kuwe na utendaji, lazima wafanye mazoezi na mambo halisi, vitu halisi, na mazingira halisi. Kwa kutegemea tu maisha ya kanisa, inawezekana kutimiza mafunzo ya kweli? Je, mwanadamu angeingia katika uhalisi? La. Iwapo mwanadamu hawezi kuingia katika maisha halisi, basi yeye hawezi kubadili njia zake za zamani za kufanya mambo na kuishi maisha. Sio tu kwa sababu ya uvivu wa mwanadamu au utegemezi wake wa nguvu, bali ni kwa sababu mwanadamu hana uwezo wa kuishi, na zaidi, hana uelewa wa kiwango cha mfanano wa mwanadamu wa kawaida ambacho Mungu anahitaji. Hapo kale, watu walikuwa daima wakiongea, wakinena, wakiwa na ushirika, hata wakawa “wanenaji hodari”; lakini hakuna yeyote kati yao alitafuta mabadiliko katika tabia ya maisha; walishikilia tu kutafuta nadharia za kina. Kwa hivyo, leo inapasa mbadili maisha haya ya kidini ya kumwamini Mungu. Lazima muingie ndani na kutenda kwa kulenga kitu kimoja, jambo moja, mtu mmoja. Lazima mfanye mambo na malengo—hapo tu ndio mtafikia matokeo. Ili kuwabadili watu, lazima kuanze na kiini chao. Kazi lazima ilenge kiini cha watu, maisha yao, uvivu, utegemezi, na utumwa wa watu, na kwa njia hii tu ndio wanaweza kubadilishwa.

Ijapokuwa maisha ya kanisa yanaweza kuleta matokeo katika sehemu nyingine, msingi bado ni kuwa maisha halisi yanaweza kuwabadilisha watu, na hali yao ya kale haiwezi kubadilika bila maisha halisi. Hebu tuchukue kazi ya Yesu katika Enzi ya Neema. Yesu alipoharamisha sheria za awali na kuanzisha amri za enzi mpya, Alinena kupitia mifano ya maisha halisi. Wakati Yesu Alipowaongoza wanafunzi wake kupita katika shamba la ngano siku ya Sabato, wanafunzi walipohisi njaa na wakatunda na kula masuke ya nafaka, Mafarisayo walipoona hivi walisema kuwa hawakuitii Sabato. Pia walisema kuwa watu hawakuruhusiwa kuwaokoa ndama walioanguka shimoni katika siku ya Sabato, wakisema kuwa hakuna kazi ingepaswa kufanywa wakati wa Sabato. Yesu alitumia matukio haya ili kutangaza rasmi amri za enzi mpya hatua kwa hatua. Wakati huo, Alitumia mambo mengi ya kiutendaji ili watu waelewe na kubadilika. Hii ndiyo kanuni ambayo kwayo Roho Mtakatifu hutekeleza kazi Yake, na ni njia hii pekee inayoweza kubadili watu. Wanapokosa mambo ya kiutendaji, watu wanaweza tu kupata ufahamu katika nadharia na wanaweza kuelewa tu mambo kiakili—hii si njia ya kufaa kubadili watu. Tukiongea juu ya kupata busara na ufahamu kupitia mafundisho, hili lingetimizwaje? Je, mwanadamu angeweza kupata busara na ufahamu kwa kusikiza, kusoma na kukuza ujuzi wake tu? Je, hili linasababishaje kupata busara na ufahamu? Mtu lazima afanye bidii kuelewa na kuwa na uzoefu kupitia maisha halisi. Kwa hivyo, mafunzo hayawezi kukosa na mtu hawezi kuacha maisha halisi. Mtu lazima azingatie hali tofauti na aingie kwa hali mbalimbali: kiwango cha elimu, ufafanuzi, uwezo wa kuona mambo, utambuzi, uwezo wa kuelewa maneno ya Mungu, maarifa ya kawaida na kanuni za ubinadamu, na vitu vingine vinavyohusiana na ubinadamu ambavyo mtu lazima awe navyo. Baada ya ufahamu kufikiwa, mtu lazima alenge kuingia, na hapo tu ndio mabadiliko yanaweza kufikiwa. Iwapo mwanadamu amefikia ufahamu lakini anakaidi utendaji, mabadiliko yanawezaje kutokea? Sasa, mwanadamu amefahamu mengi, lakini haishi kwa kudhihirisha uhalisi, hivyo basi anaweza kuwa tu na ufahamu halisi kidogo wa maneno ya Mungu. Umepata nuru kwa kiasi kidogo, umepokea mwangaza kidogo kutoka kwa Roho Mtakatifu, lakini huna kuingia katika maisha halisi, au hata huenda hujali juu ya kuingia, hivyo basi utakuwa na mabadiliko kidogo tu. Baada ya muda mrefu hivyo, watu wameelewa mengi na wanaweza kusema mengi juu ya ujuzi wao wa nadharia, lakini tabia yao ya nje husalia ile ile, na ubora wa tabia yao wa asili hudumu bila upandaji hadhi hata kidogo. Iwapo mambo yako hivi, mtaingia lini humo hatimaye?

Maisha ya kanisa ni aina ya maisha tu ambapo watu hukutana kufurahia maneno ya Mungu, na huchukua tu kipande kidogo cha maisha ya mtu. Iwapo maisha halisi ya mtu yangekuwa kama maisha yake ya kanisani, yakijumuisha maisha sahihi ya kiroho, kufurahia maneno ya Mungu kwa usahihi, kuomba na kuwa karibu na Mungu kwa usahihi, kuishi maisha halisi ambapo kila kitu kinatekelezwa kwa mujibu wa mapenzi ya Mungu, kuishi maisha halisi ambapo kila kitu kinatekelezwa kwa mujibu wa ukweli, kuishi maisha halisi ya kutekeleza maombi na kuwa kimya mbele ya Mungu, ya kutekeleza kuimba nyimbo za kidini na kucheza, maisha kama haya tu yangemleta mtu katika maisha ya maneno ya Mungu. Watu wengi sana hulenga tu masaa kadhaa ya maisha yao ya kanisa bila “kutunza” maisha yao nje ya masaa hayo, kana kwamba hayahusiki nao. Pia kunao watu wengi ambao huingia tu katika maisha ya watakatifu wanapokula na kunywa maneno ya Mungu, wakiimba nyimbo za kidini au wakiomba, kisha hurejelea nafsi zao za kale nje ya nyakati hizo. Maisha kama hayo hayawezi kubadili watu, na hayatawaruhusu kumjua Mungu. Katika kumwamini Mungu, iwapo mwanadamu anataka mabadiliko kwa tabia yake mwenyewe, basi lazima asijitenge na maisha halisi. Katika maisha halisi, lazima ujijue mwenyewe, ujitelekeze mwenyewe, utende ukweli, na vilevile kujifunza kanuni, maarifa ya kawaida na masharti ya kujiendesha katika mambo yote kabla ya wewe kuweza kutimiza mabadiliko ya polepole. Iwapo utalenga tu ujuzi katika nadharia na kuishi tu katika sherehe za dini bila ya kuingia ndani ya uhalisi, bila kuingia kwenye maisha halisi, basi hutaweza kamwe kuingia katika uhalisi, hutaweza kujijua mwenyewe, kuujua ukweli, au kumjua Mungu, na daima utakuwa kipofu na mjinga. Kusudi la Mungu kumfinyanga mtu sio kumruhusu kuwa na maisha sahihi ya binadamu kwa masaa kadhaa tu katika siku nzima huku akiishi katika mwili muda uliosalia. Na sio kubadili ujuzi wa nadharia wa mtu. Badala yake ni kubadili tabia yake ya kale, kubadili maisha yake yote ya kale, kubadili fikira zake zote zilizopitwa na wakati na mtazamo wake wa kiakili. Kulenga tu maisha ya kanisa pekee hakuwezi kubadili mazoea ya kale ya mtu au kubadili njia za kale alizoishi kwa muda mrefu. Lolote litokealo, mtu hapaswi kujitenga na maisha halisi. Mungu anauliza kwamba watu waishi kwa kudhihirisha ubinadamu wa kawaida katika maisha halisi, sio tu katika maisha ya kanisani; kwamba waishi kwa kudhihirisha ukweli katika maisha halisi, sio tu katika maisha ya kanisani; kwamba watimize majukumu yao katika maisha halisi, sio tu katika maisha ya kanisani. Ili kuingia katika uhalisi, mtu lazima apindue vitu vyote kuelekea maisha halisi. Iwapo waumini katika Mungu hawawezi kuingia katika maisha halisi na kujijua wenyewe au kuishi kwa kudhihirisha ubinadamu wa kawaida katika maisha halisi, watashindwa. Wale wanaomkaidi Mungu wote ni watu ambao hawawezi kuingia katika maisha halisi. Wote ni watu wanaozungumza kuhusu ubinadamu lakini wanaishi kwa kudhihirisha asili ya pepo mbaya. Wote ni watu wanaozungumza kuhusu ukweli lakini wanaishi kwa kudhihirisha kanuni badala yake. Wale wasioweza kuishi kwa kudhihirisha ukweli katika maisha halisi ni wale wanaoamini katika Mungu lakini wanachukiwa na kukataliwa na Yeye. Lazima ufanye mazoezi ya kuingia kwako katika maisha halisi, ujue upungufu wako mwenyewe, ukaidi na upumbavu, na ujue ubinadamu wako usio wa kawaida na udhaifu. Kwa njia hiyo, ufahamu wako wote utaambatanishwa ndani ya hali yako halisi na ugumu. Ni aina hii ya ufahamu pekee ndiyo ya kweli na inaweza kukufanya ushike kwa hakika hali yako mwenyewe na ufanikishe mabadiliko ya tabia yako.

Sasa kwa vile kukamilishwa kwa mwanadamu kumeanza rasmi, mtu lazima aingie katika maisha halisi. Kwa hivyo, ili kutimiza mabadiliko, lazima mtu aanzie kwa kuingia katika maisha halisi, na kubadilika kidogo kidogo. Ukihepa maisha ya mtu ya kawaida na kuongea tu kuhusu mambo ya kiroho, basi mambo hugeuka makavu na bapa, hugeuka yasiyo ya uhalisi, na mtu angebadilika vipi? Sasa unaambiwa uingie katika maisha halisi kufanya mazoezi, ili uweze kuweka msingi wa kuingia katika uzoefu wa kweli. Hii ni mojawapo ya mambo ambayo mtu anapaswa kufanya. Kazi ya Roho Mtakatifu hasa ni kuongoza, ilhali iliyosalia hutegemea utendaji wa watu na kuingia. Kila mmoja anaweza kufikia kuingia katika maisha halisi kwa njia mbalimbali, kiasi kwamba wanaweza kumleta Mungu katika maisha halisi, na kuishi kwa kudhihirisha ubinadamu wa kawaida halisi. Haya tu ndiyo maisha yenye maana!

Iliyotangulia:Kuhusu Maisha ya Kawaida ya Kiroho

Inayofuata:Kuhusu Kila Mmoja Kutekeleza Wajibu Wake

Maudhui Yanayohusiana

 • Je, Kazi ya Mungu Ni Rahisi Jinsi Mwanadamu Anavyodhania?

  Kama mtu anayemwamini Mungu, inakupasa kuelewa kuwa, leo, katika kupokea kazi ya Mungu nyakati za mwisho na kazi yote ya mpango wa Mungu ndani yako, …

 • Kazi na Kuingia (4)

  Ikiwa mwanadamu anaweza kuingia kabisa kulingana na kazi ya Roho Mtakatifu, maisha yake yatachipuka haraka kama mmea wa mwanzi baada ya mvua ya majira…

 • Ufalme wa Milenia Umewasili

  Je, mmeona kazi ambayo Mungu ataikamilisha katika kundi hili la watu? Mungu alisema, hata katika Ufalme wa Milenia watu ni lazima waendelee kufuata ma…

 • Njia … (5)

  Ilikuwa kwamba hakuna aliyejua Roho Mtakatifu, na hasa hawakujua njia ya Roho Mtakatifu ilikuwa gani. Ndio maana watu kila mara walifanya upumbavu mb…