Sura ya 58

Ukiielewa nia Yangu, utaweza kuufikiria mzigo Wangu na unaweza kupata mwanga na ufunuo, na kupata ufunguliwaji na uhuru, kuuridhisha moyo Wangu, kuyaruhusu mapenzi Yangu kwa ajili yako kutekelezwa, kuwaletea watakatifu wote ujenzi wa maadili, na kuufanya ufalme Wangu duniani kuwa imara na thabiti. Jambo la muhimu sasa ni kuelewa nia Yangu, hii ni njia mnayopaswa kuingia katika na hata zaidi ni wajibu wa kutimizwa na kila mtu.

Neno Langu ni dawa nzuri inayoponya kila aina ya maradhi. Alimradi uko tayari kuja mbele Yangu, Nitakuponya, na kukuruhusu kuona kuwepo kwa kudura Yangu, kuona matendo Yangu ya ajabu, kuona haki na uadhama Wangu na hata zaidi kuona upotovu wenu wenyewe na udhaifu wenu wenyewe. Naelewa kabisa kila hali ndani yako; daima unafanya vitu ndani ya moyo wako na hauonyeshi kwa nje. Niko wazi hata zaidi kuhusu kila kitu unachokifanya. Lakini unapaswa kujua ni vitu gani Ninavyovisifu, na ni vitu gani Nisivyovisifu; unapaswa kutofautisha kwa wazi hivi viwili na haupaswi kuchukulia hili kwa kawaida.

Unaunga mkono kwa maneno matupu tu, ukisema “Lazima tufikirie mzigo wa Mungu.” Lakini unapokabili ukweli, huufikiri vya kutosha ingawa unajua vizuri mzigo wa Mungu ni nini. Kweli umevurugwa kabisa, mjinga kwa kiwango fulani, na hata zaidi mshenzi kikamilifu. Hili linaeleza jinsi mwanadamu alivyo mgumu kushughulikia na yote anayofanya ni kuunga mkono kwa maneno matupu yanayosikika kuwa mazuri, akisema kitu kama “Siwezi kabisa kuielewa nia ya Mungu, lakini nikiielewa hakika ninatenda kulingana nayo.” Hii si hali yenu ya kweli? Ingawa nyote mnaijua nia ya Mungu, na mnajua chanzo cha ugonjwa wenu ni kipi, jambo la muhimu ni kwamba hamko tayari kutenda; huu ni ugumu mkubwa zaidi. Usipotatua hili mara moja, litakuwa kikwazo kikubwa zaidi kwa maisha yako mwenyewe.

Iliyotangulia: Sura ya 57

Inayofuata: Sura ya 59

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp