Programu ya Kanisa la Mwenyezi Mungu

Sikiliza sauti ya Mungu na ukaribishe kurudi kwa Bwana Yesu!

Tunawakaribisha wote wanaotafuta ukweli wawasiliane nasi.

Neno Laonekana katika Mwili

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

(Ma)tokeo ya Kutafuta 0

Hakuna matokeo yaliyopatikana

Sura ya 55

Ubinadamu wa kawaida ambao huzungumziwa si wa mwujiza sana kama watu wanavyofikiria, lakini unaweza kuvuka mipaka ya mafungo ya watu wote, matukio, na vitu, kupita mipaka ya nguvu za mazingira, na unaweza kunikaribia Mimi na kuwasiliana kwa karibu na Mimi mahali popote na katika mazingira yoyote. Ninyi daima hutafsiri vibaya nia Zangu. Ninaposema mnapaswa kuishi kwa kudhihirisha ubinadamu wa kawaida, mnajizuia na kudhibiti miili yenu. Lakini huzingatii kutafuta kwa makini ndani ya roho, ila kwa kile mnachovaa kwa nje pekee, ukikosa kuangalia ufunuo Wangu ndani yako, na kusisimua Kwangu ndani yako. Jinsi ulivyo mzembe! Mzembe sana! Inaweza kuwa kwamba kumaliza kile ambacho Nimekuaminia ni ufanisi mkubwa? Wewe ni mpumbavu! Huzingatii kukita mizizi kwa kina! “Usiwe jani kwa mti, ila uwe mzizi wa mti huo”—huo kweli ni wito wako? Hujali! Mzembe! Unaridhika unapofikiria kuwa una kitu kidogo. Jinsi unavyojali mapenzi Yangu kidogo sana! Kuanzia sasa kuendelea jihadhari. Usiwe baridi. Usiwe hasi! Unapohudumu, Nikaribie mara kwa mara na kuwasiliana kwa karibu na Mimi. Hii ndiyo njia yako ya pekee. Najua kwamba tayari umejinyima, unajua upungufu wako mwenyewe, unajua udhaifu wako mwenyewe. Lakini kujua tu hakutoshi. Unahitaji kushirikiana na Mimi na punde unapoelewa nia Zangu ziweke katika vitendo mara moja. Hii ndiyo njia bora kabisa ya kuonyesha kujali mzigo Wangu, njia bora kabisa ya kutii.

Bila kujali jinsi unavyonitendea, Nataka kutekeleza mapenzi Yangu kwako na watakatifu wote, na Nataka mapenzi Yangu yatekelezwe bila kuzuiwa katika nchi yote. Tambua hili kikamilifu! Hili linahusu amri Zangu za utawala! Huogopi hata kidogo? Hutetemeki kwa hofu kwa sababu ya vitendo vyako na mienendo yako? Miongoni mwa watakatifu wote karibu wote hawahisi nia Yangu. Hutaki kuwa wa kipekee kama mtu anayefikiria mapenzi Yangu kabisa? Je, wajua? Nia yangu ya dharura kwa sasa ni kutafuta kundi la watu wanaoweza kufikiria mapenzi Yangu kabisa. Hutaki kuwa mmoja wao? Hutaki kujitumia kwa ajili Yangu, kujitolea kwa ajili Yangu? Hutaki kulipa gharama hata kidogo, kutoa juhudi hata kidogo! Mambo yakiendelea kuwa hivyo, juhudi Yangu ya bidii itakuwa bure kwenu. Baada ya Mimi kukuonyesha hilo, bado hujaelewa uzito wa suala hili?

“Kwa wale ambao kweli wanatumia rasilmali kwa ajili Yangu, hakika Nitakubariki pakubwa.” Unaona! Nimekuambia hili mara kadhaa, lakini bado una mashaka mengi, ukiogopa mazingira ya jamii, ukiogopa mazingira ya nje. Kweli hujui kinachokufaa! Nawatumia tu watu waaminifu, wa kawaida, na wazi. Umekuwa na furaha na radhi kwa Mimi kukutumia, lakini kwa nini bado una wasiwasi sana? Inaweza kuwa kwamba maneno Yangu hayana athari hata kidogo kwako? Nimesema kuwa Nakutumia wewe, ilhali huwezi kuamini hilo kwa uthabiti. Kila mara unashuku, ukiogopa kwamba Nitakuacha. Dhana zako zimefungwa sana! Ninaposema kwamba Nakutumia hilo linamaanisha Nakutumia. Kwa nini una shaka sana kila mara? Je, ni kwamba Sijaongea kwa wazi vya kutosha? Kila neno ambalo Nimesema ni kweli. Hakuna tamko hata moja ambalo si la kweli. Mwanangu! Niamini. Jitolee nafsi kwa niaba Yangu, na hakika Nitajitolea nafsi kwako!

Iliyotangulia:Sura ya 54

Inayofuata:Sura ya 56

Maudhui Yanayohusiana

 • Mungu Ndiye Chanzo cha Uhai wa Mwanadamu

  Tangu unapoingia katika dunia hii ukilia, unaanza kutekeleza wajibu wako. Kwa kuchukua jukumu lako katika mpango wa Mungu na katika utaratibu Wake, u…

 • Kuhusu Biblia (3)

  Si kila kitu katika Biblia ni rekodi ya maneno aliyoyasema Mungu. Kimsingi Biblia inaandika hatua mbili za awali za kazi ya Mungu, ambapo sehemu moja…

 • Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee IX

  Mungu ni Chanzo cha Uhai kwa Vitu Vyote (III) Kwa kipindi hiki chote, tumezungumza juu ya mambo mengi yanayohusiana na kumjua Mungu na hivi karibuni t…

 • Maana ya Kuwa Mwanadamu Halisi

  Kumsimamia mwanadamu ndio Kazi Yangu, na ushindi Wangu dhidi yake ni kitu ambacho kilikuwa hata zaidi kimeshaamuliwa kabla Nilipoiumba dunia. Watu hue…