Sura ya 56

Nimeanza kuchukua hatua kuadhibu wale ambao hufanya uovu, wale ambao hushika madaraka, na wale ambao hutesa wana wa Mungu. Kuanzia sasa kuendelea, mkono wa amri Zangu za utawala utakuwa daima juu ya wale wanaonipinga mioyoni mwao. Fahamu hili! Huu ndio mwanzo wa hukumu Yangu, na hakuna huruma itakayoonyeshwa kwa yeyote wala hakuna atakayesamehewa, kwani Mimi ni Mungu asiyependelea ambaye hutenda haki, na ingekuwa vyema kwenu nyote kutambua hili.

Si kwamba Nataka kuadhibu wale ambao hufanya uovu, badala yake ni adhabu inayoletwa kwao na uovu wao wenyewe. Mimi siwi na haraka ya kumwadhibu yeyote, wala Simtendei yeyote bila haki—Natenda haki kwa wote. Kwa hakika Napenda wana Wangu na hakika Nachukia wale waovu wasionitii; hii ndiyo kanuni ya matendo Yangu. Kila mmoja wenu anapaswa kuwa na umaizi wa amri Zangu za utawala. Iwapo sivyo, hamtakuwa na hofu hata kidogo na mtakuwa wazembe mbele Yangu, na hamtajua kile Ninachotaka kutimilisha, kile Ninachotaka kufanya kuwa kamili, kile Ninachotaka kupata ama ufalme Wangu unahitaji mtu wa aina gani.

Amri Zangu za utawala ni:

1. Haijalishi wewe ni nani, ukinipinga Mimi katika moyo wako, utahukumiwa.

2. Kwa wale ambao Nimechagua, watafundishwa nidhamu mara moja kwa sababu ya wazo lolote lisilo sahihi.

3. Nitawaweka wale wasioniamini kwa upande mmoja. Nitawaruhusu wazungumze na kutenda kwa uzembe hadi mwisho kabisa ambapo Nitawaadhibu kabisa na kupambana nao.

4. Kwa wale ambao wananiamini, Nitawatunza na kuwalinda nyakati zote. Nyakati zote Nitawapa uzima kwa kutumia njia ya wokovu. Watu hawa watakuwa na upendo Wangu na hakika hawataanguka ama kupoteza njia yao. Udhaifu wowote ambao wako nao utakuwa wa muda, na kwa hakika Sitaukumbuka.

5. Kwa wale ambao wanaonekana kuamini lakini ambao kwa kweli hawaamini—kumaanisha wale ambao wanaamini kuna Mungu lakini hawamtafuti Kristo, lakini ambao pia hawapingi—watu wa aina hizi ni wa kusikitisha zaidi, na kupitia vitendo Vyangu Nitawafanya waone kwa dhahiri. Kupitia matendo Yangu, Nitawaokoa watu wa aina hizi na kuwarudisha.

6. Wazaliwa wa kwanza ambao walikuwa wa kwanza kukubali jina Langu watabarikiwa! Hakika Nitawapa baraka bora zaidi na mtakuwa na furaha hadi kuridhika kwa mioyo yenu; hakuna atakayethubutu kuizuia. Kila kitu kimetayarishwa kabisa kwa ajili yenu, kwani hii ni amri Yangu ya utawala.

Katika vipengele vyote, mnapaswa kuweza kuona kile mkono Wangu hufanya na fikira ambazo Ninazo katika moyo Wangu—yote si kwa ajili Yenu? Ni nani kati yenu aliye upande Wangu? Je, mmechunguza fikira katika mioyo yenu ama maneno ambayo ninyi husema? Je, mmekaribia kwa uangalifu sana mambo haya? Wapumbavu! Wapotovu! Kutokubali vizuizi vya Roho Mtakatifu! Nimekuwa nikiiachilia sauti Yangu tena na tena ndani yako, lakini hakujakuwa na mjibizo wowote hata kidogo. Usiwe mpumbavu tena! Wajibu wako ni kuelewa mapenzi Yangu; aidha, ni njia unayopaswa kuingia. Umekanganyikiwa, huna umaizi, huoni kwa dhahiri kile Ninachotaka kutimiza ndani Yako, ama kile Ninachotaka kupata kutoka kwako! Ili kuelewa mapenzi Yangu lazima kwanza uanze kwa kunikaribia na kushiriki zaidi na Mimi. Daima unasema kwamba huwezi kuelewa mapenzi Yangu; tayari umejazwa na mambo yako mwenyewe, basi Nawezaje kufanya kazi kwako? Huji mbele Yangu kwa vitendo, lakini unasubiri tu kwa uhasi. Nasema wewe ni kama mnyoo, ilhali unahisi kukosewa na hulikubali. Wakati huu unapaswa kuinuka na kushirikiana na Mimi! Usiwe hasi! Hiyo itarudisha maisha yako nyuma. Kuwa wa vitendo huleta manufaa kwako, sio kwa wengine—bado hujatambua na kuelewa hili? Mapenzi yangu daima hufichuliwa kwako—hujayatambua? Mbona hujawahi kuyatilia maanani? Na mbona hujawahi kuweza kuelewa mapenzi Yangu? Je, kushika mapenzi Yangu hakukuletei manufaa?

Natumai unaweza kufikiria mapenzi Yangu kwa hali zote ili Niweze kuwa na njia ya kuendea na maskani ya kupumzikia ndani yako. Usinizuie tena, ni ukatili sana! Huna uelewa wa maneno Yangu na huyatolei hisia. Tazama na uone wakati ni upi sasa—hakuwezi kuwa na kusubiri zaidi! Usipofuata nyayo Zangu kwa ukaribu basi muda utakuwa umeisha, sembuse kuwepo njia yoyote ya wewe kuukomboa!

Iliyotangulia: Sura ya 55

Inayofuata: Sura ya 57

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp