Tunawakaribisha wote wanaotafuta ukweli wawasiliane nasi.

Mfuateni Mwanakondoo na Kuimba Nyimbo Mpya

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

(Ma)tokeo ya Kutafuta 0

Hakuna matokeo yaliyopatikana

126 Fuata Mfano wa Petro na Utafute Kumpenda Mungu

1

Nilikuwa nikifikiria kuwa kuacha kila kitu na kumfanyia Mungu kazi kulimaanisha kuwa nilimpenda Mungu. Ingawa niliwindwa na CCP, sikurudi nyuma kamwe.

Familia yangu ilinikataa na dunia ikanikashifu, lakini nilikuwa tayari kutoa miaka yangu ya ujana kwa Mungu bila kulalamika au kujuta.

Mradi tu ningeinuliwa kuingia katika ufalme wa mbinguni na kuzawadiwa, ilikuwa inastahili kiwango chochote cha mateso na kiwango chochote cha machozi.

Majaribu yalipofika na kufichua uovu wangu, nikawa hasi na mnyonge, na nikalia machozi machungu.

Nikitafakari njia ambayo nilitembea katika imani yangu katika Mungu, hatimaye niligundua kuwa bila kufuatilia ukweli, ningeanguka mwishowe.

2

Maneno ya Mungu yalifichua kiini potovu cha binadamu, na ni hapo tu ndipo niliona kina cha upotovu wangu.

Nilisema nilimpenda Mungu, lakini ilikuwa tu ili nipate baraka na zawadi, na hata kazi yangu ngumu na juhudi ilifanywa ili kupata kitu kutoka kwa Mungu.

Kweli nilipoteza dhamiri, mantiki, ubinadamu wangu lakini Mungu bado alitumia maneno Yake kunihukumu na kunitakasa.

Naanguka mbele ya Mungu kwa majuto kuhusu yale niliyotenda, sistahili kabisa kupokea upendo wa Mungu.

Nimeamua kutafuta kumpenda Mungu na kumridhisha Mungu, sitafanya mipango ama kufikiria maisha yangu ya usoni ama majiliwa yangu tena.

3

Kupitia majaribu na taabu kunakamilisha imani yangu. Naona kwamba mwanzo wa majaribu kweli ni baraka ya Mungu.

Ingawa mwili unaweza kuteseka, naweza kuonja upendo wa Mungu. Kwa kutenda ukweli, tabia yangu potovu inabadilishwa.

Nitafuata mfano wa Petro, kumpenda Mungu kabisa, kumtii hadi kifo. Nimebarikiwa sana kuwa naweza kumpenda Mungu na kutoa ushahidi Kwake leo.

Nina hakika kuwa Kristo ndiye ukweli, njia, na uzima. Kuelewa ukweli na kumjua Mungu, maisha haya sio ya bure.

Kutii mipango ya Mungu hakuwezi kamwe kuwa makosa. Upendo na utiifu wa milele kwa Mungu ni wajibu wangu.

Iliyotangulia:Nimeamua Kumfuata Mungu

Inayofuata:Tunakamilisha Misheni Yetu

Maudhui Yanayohusiana

 • Upendo Safi Bila Dosari

  1 Upendo ni hisia safi sana, safi bila dosari. Tumia moyo wako, tumia moyo wako kupenda na kuhisi na kutunza. Upendo hauweki masharti au vizuizi au ba…

 • Upendo wa Kweli

  1 Namrudia Mungu na kuuona uso Wake upendezao, nikiwa huru kutokana na udhibiti wa kaida za dini. Neno Lake linanijaza na raha na furaha kutoka kwa ne…

 • Mradi tu Usimwache Mungu

  Upendo na huruma za Mungu hupenyeza katika kila sehemu ya kazi ya usimamizi Wake, na bila kujali kama watu wanaweza kuelewa nia njema za Mungu, bado …

 • Toa Akili na Mwili ili Kutimiza Agizo la Mungu

  I Kama washiriki wa jamii ya wanadamu, kama wafuasi wa Kristo wa dhati, ni wajibu wetu, jukumu letu kutoa akili zetu na miili yetu kwa kutimiza agizo …