Programu ya Kanisa la Mwenyezi Mungu

Sikiliza sauti ya Mungu na ukaribishe kurudi kwa Bwana Yesu!

Tunawakaribisha wote wanaotafuta ukweli wawasiliane nasi.

Mfuateni Mwanakondoo na Kuimba Nyimbo Mpya

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

(Ma)tokeo ya Kutafuta 0

Hakuna matokeo yaliyopatikana

197 Elewa Ukweli na Uwe Huru

1

Katika miaka mingi ya kumwamini Bwana, nilizungumza tu maneno na mafundisho, nikashikilia sheria, na kufanya utaratibu wa kidini.

Kila ombi langu lilikuwa majivuno tupu, sikuwahi kumwambia Mungu maneno ya moyoni mwangu.

Wala sikutafuta ukweli niliposoma maneno ya Mungu; sikuweza kutafakari mapenzi ya Mungu.

Nilidhani kwamba kukariri vifungu maarufu na misemo ya Biblia kulimaanisha kuwa nilikuwa na uhalisi wa ukweli.

Nililenga tu kujizuia kudanganya, na hivyo nilijiona mwaminifu.

Nilijitahidi kwa bidii na kwa furaha kwa miaka ili niingie katika ufalme wa mbinguni na kutunukiwa.

Bahati iliyoje kwamba maneno ya Mwenyezi Mungu yaliniita; niliisikia sauti ya Mungu na nikamrudia Mungu.

Nimeelewa ukweli mwingi kutoka kwa maneno ya Mungu, nimeona kuonekana na kazi ya Mungu.

2

Hukumu ya maneno ya Mungu iliniamsha ghafla; kufuatilia ukweli kunaupendeza moyo wa Mungu kabisa.

Nikimwamini Mungu lakini nisipitie kuadibu na hukumu ya Mungu, tabia yangu potovu haiwezi kubadilika.

Kama simjui Mungu, na simwogopi Mungu, basi tabia yangu nzuri ni ulaghai tu.

Tabia ya Mungu yenye haki haiwezi kukosewa na mwanadamu, tamaa ya mwanadamu mdanganyafu ya kuingia katika ufalme ni ndoto tu.

Nimeamua kutenda na kupitia maneno ya Mungu, kuupata ukweli na kuondoa upotovu wangu.

Katika vitu vyote, natafuta ukweli na kutenda ukweli; moyoni mwangu, nahisi niliyepumzika na mwenye amani.

Natekeleza wajibu wangu kwa uaminifu, na kumtumikia Mungu kwa furaha; siombi baraka, bali kwamba nimpende Mungu tu.

Kwa kuwa sasa naelewa ukweli, sishikilii tena sheria; nikiishi mbele za Mungu, nimewekwa huru.

Iliyotangulia:Eh Mungu! Sistahili Upendo Wako Kweli

Inayofuata:Kukubali Ukweli ni Kuwa Mwanamwali Mwenye Busara

Maudhui Yanayohusiana

 • Mradi tu Usimwache Mungu

  Upendo na huruma za Mungu hupenyeza katika kila sehemu ya kazi ya usimamizi Wake, na bila kujali kama watu wanaweza kuelewa nia njema za Mungu, bado …

 • Nimeuona Upendo wa Mungu

  1 Mwenyezi Mungu, ni Wewe unayenipenda. Katika ulimwengu mchafu Umenichagua mimi! Hivyo nimekuja mbele Yako, naam, nimekuja mbele Yako, nikiishi maish…

 • Nitampenda Mungu Milele

  1 Ee Mungu! Maneno Yako yananiita nirudi Kwako. Nakubali kufundishwa katika ufalme Wako mchana na usiku. Mara nyingi sana nilikuwa dhaifu na hasi, m…

 • Upendo Safi Bila Dosari

  1 Upendo ni hisia safi sana, safi bila dosari. Tumia moyo wako, tumia moyo wako kupenda na kuhisi na kutunza. Upendo hauweki masharti au vizuizi au ba…