Sura ya 48

Mimi nina wasiwasi, lakini wangapi kati yenu wanaweza kuwa na nia moja na mawazo sawa na Mimi? Ninyi hamyasikilizi tu maneno Yangu, mkipuuza kabisa na kushindwa kuyatilia maanani, badala yake mkizingatia tu mambo yenu wenyewe ya juu juu. Mnachukulia kujali Kwangu kwa bidii na juhudi kama jitihada za bure; je, dhamiri yenu haiwahukumu? Ninyi ni wajinga na hamna mantiki; ninyi ni wapumbavu, na hamwezi kuniridhisha kabisa. Niko upande wenu kabisa—ninyi mnaweza kuwa upande Wangu kiasi gani? Mmeelewa visivyo nia Yangu, na hakika huu ni upofu wenu na kutoweza kuona mambo, daima mkinifanya Niwe na wasiwasi kuwahusu na kutumia muda kwenu. Sasa, ni kiasi gani cha muda wenu ambao mnaweza kuutumia na kutenga kwa ajili Yangu? Mnapaswa kujiuliza zaidi.

Nia Yangu yote ni kwa sababu yenu—je, mnaelewa hili kweli? Kama kweli mngeelewa, mngekuwa mmekwisha kufahamu nia Yangu na kuufikiria mzigo Wangu. Msiwe wazembe tena, la sivyo Roho Mtakatifu hatafanya kazi ndani yenu, jambo ambalo litazifanya roho zenu zife and kuanguka kuzimuni. Je, hilo si jambo baya sana kwako? Hakuna haja ya Mimi kuwakumbusha tena. Mnapaswa kuchunguza dhamiri zenu na kujiuliza: Je, ni kwamba Ninawahurumia sana, au kwamba ninyi mna madeni Yangu mengi sana? Msichanganye mema na mabaya na muwe bila akili! Sasa si wakati wa kupigania nguvu na faida au kushiriki katika kula njama, badala yake lazima muweke kando kwa haraka mambo haya ambayo ni yenye kuleta madhara kwa maisha na kutafuta kuingia ndani ya ukweli. Ninyi ni wazembe sana! Hamwezi kuuelewa moyo Wangu au kutambua nia Yangu. Kuna mambo mengi ambayo Sikupaswa kuyasema, lakini ninyi ni watu mliochanganyikiwa sana ambao hamwelewi, imenibidi Niyaseme mara kwa mara, na hata hivyo, ninyi bado hamjauridhisha moyo Wangu.

Nikiwahesabu mmoja mmoja, ni wangapi wanaoweza kuufikiria moyo Wangu kwa hakika?

Iliyotangulia: Sura ya 47

Inayofuata: Sura ya 49

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp