222 Rehema ya Mungu Ilinihuisha Tena

1 Nilikuwa nimemwamini Bwana kwa miaka mingi, lakini bado niliishi katika dhambi. Nilisema uongo na kudanganya mara nyingi, na sikuwa na moyo wa kumcha Mungu. Wokovu wa Mungu wa siku za mwisho ulinijia. Katika ujinga na upofu wangu, sikuitafuta au kuichunguza. Mungu alitumia maneno Yake kubisha kwenye mlango wa moyo wangu, lakini nilimhukumu na kumkana. Nilipoteza uwepo Wake na kuanguka gizani. Lawama za dhamiri yangu zilifanya kifo kiwe bora kuliko maisha. Wakati huo tu ndipo nilipogundua kwamba kuwa na dhamiri yenye amani ni furaha ya kweli. Isingekuwa huruma na wokovu wa Mungu, ningewezaje kumfuata Mungu hadi leo? Kulingana na matendo yangu, ningekufa zamani, na hata kifo kingekuwa kizuri sana kwangu. Kwa uvumilivu wa Mungu, navuta pumzi hii. Sistahili kabisa kufurahia upendo mkubwa wa Mungu.

2 Ingawa Mungu alinikuza nitekeleze wajibu wangu, sikufuatilia ukweli, na nilitamani baraka za hadhi siku zote. Huku nikijawa na mahitaji ya kupita kiasi, sikuwahi kufikiria mapenzi ya Mungu, na sikujua kwamba nilimkataa Mungu. Mungu amekuwa akiniruzuku na kunichunga kila siku, lakini sikuthamini jambo hilo sana. Niliepuka hukumu na kuadibiwa, na nikamwasi Mungu kwa ukaidi. Niliuumiza moyo wa Mungu. Nilikosa nafasi nyingi za kukamilishwa. Sikuridhisha kusudi zuri la Mungu. Hata kama ningetoa maisha yangu kwa ajili ya Mungu, ningewezaje kufidia maumivu ya moyo Wake? Ee Mwenyezi Mungu! Natamani kuwa mtu mpya na kuanza tena.

3. Maneno ya Mungu ya uzima yanashawishi moyo wangu. Ushawishi wa Mungu unanipa nguvu isiyo na kikomo, na unanifanya nisimame tena kutoka kwa kutofaulu na kuanguka. Sasa najua thamani ya maisha, na ninajua ni kwa nini niliumbwa. Ninapokabiliwa na matakwa ya Mungu, nawezaje kukimbia na kujificha tena? Natamani kulipa upendo wa Mungu kwa uaminifu na utiifu wangu. Nitatenda ukweli na kuishi kwa kufuata na neno la Mungu, kamwe sitamfanya Mungu awe na wasiwasi juu yangu. Iwe nimebarikiwa au nakutana na msiba, natafuta tu kumridhisha Mungu. Natamani kuutoa moyo wangu wa kweli kwa Mungu. Hata kama sina hatima, bado natamani kumhudumia Mungu maisha yangu yote. Nitafidia madeni yangu yote ya zamani na niufariji moyo wa Mungu.

Iliyotangulia: 221 Kutakaswa na Maneno ya Mungu

Inayofuata: 224 Napata Mengi Sana Kutoka kwa Hukumu na Kuadibu kwa Mungu

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?
Wasiliana Nasi
Wasiliana nasi kupitia WhatsApp

Maudhui Yanayohusiana

263 Njia Yote Pamoja na Wewe

1 Naelea na kuzurura katika dunia, nikihisi kupotea na mnyonge ndani. Ninapoamshwa na maneno Yako ya upole, naona kuonekana kwa mwanga....

115 Nimeuona Upendo wa Mungu

1 Mwenyezi Mungu, ni Wewe unayenipenda. Katika ulimwengu mchafu Umenichagua mimi! Hivyo nimekuja mbele Yako, naam, nimekuja mbele Yako,...

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki