225 Ni Mungu Ambaye Ameniokoa

1 Kupata mwili na kuwa mwanadamu, kupitia upepo mwingi na mvua, Wewe ni mnyenyekevu na msiri kati ya wanadamu—hakuna mtu aliyewahi kukujua. Unahukumu na kufunua upotovu wa kina wa wanadamu; Unaadibu udhalimu na uasi wangu. Ingawa nimepitia mateso na usafishaji mwingi, tabia yangu potovu imetakaswa. Nilikuwa mwenye kiburi na mwenye kujidai na kufanya mabadilishano na Wewe—hilo lilikuwa jambo la ubinafsi sana na la kustahili dharau, kila wakati nikitaka kupata baraka za ufalme wa mbinguni kwa mbadala wa bidii na mateso yangu. Hiyo ni dhamiri na mantiki ya aina gani? Nilidhani kwamba kwa tabia nzuri kidogo naweza kulingana na mapenzi Yako, hata kuota ndoto ya kuingia kwenye ufalme wa mbinguni. Nimepotoka sana, nimejaa tabia za kishetani. Nisingekubali hukumu Yako, matokeo yangu yangekuwa nini?

2 Hukumu Yako imenitakasa; kazi Yako imenibadilisha, ikinipa maisha ya kweli. Ningekosaje kukushukuru kutoka moyoni mwangu? Ingawa bado nina uasi na udhalimu mwingi unaohitaji kutakaswa, nimeona jinsi unavyopendeza. Haijalishi majaribu yalivyo makubwa sitawahi kukuacha. Zamani nilijifanyia kila kitu, na sikuwahi kukupenda, nikikuumiza na kukuletea uchungu, ni nani anayejua machozi mangapi Ulilia. Nikifikiria juu ya upendo Wako kwangu, nachukia tabia hii yangu potovu. Natamani kufuatilia ukweli ili niufariji moyo Wako! Ni wewe Uliyeniokoa. Bila hukumu Yako, singekuwa hapa leo. Nimefurahia katika neema Yako ya ajabu—kwa kweli ni upendo na huruma Yako. Ee Mungu, ni Wewe ambaye Umeniokoa. Ninapoona kwamba tabia Yako ni yenye haki, nakupenda kutoka moyoni mwangu. Ee Mungu, ni Wewe ambaye Umeniokoa. Nitashukuru na kukusifu daima kwa ajili ya upendo Wako!

Iliyotangulia: 224 Napata Mengi Sana Kutoka kwa Hukumu na Kuadibu kwa Mungu

Inayofuata: 226 Nimeiona Haki ya Mungu

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?
Wasiliana Nasi
Wasiliana nasi kupitia WhatsApp

Maudhui Yanayohusiana

47 Furaha Katika Nchi ya Kanaani

1 Kurudi nyumbani kwa Mungu, nahisi furaha na msisimko. Nina bahati kuona hatimaye Mwenyezi Mungu wa vitendo. Maneno Yake huwaongoza watu...

84 Umuhumi wa Maombi

1 Maombi ni njia moja ya mwanadamu kishirikiana na Mungu, kuita Roho Wake na kuguswa na Mungu. Kadiri unavyoomba zaidi, ndivyo...

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki