Programu ya Kanisa la Mwenyezi Mungu

Sikiliza sauti ya Mungu na ukaribishe kurudi kwa Bwana Yesu!

Tunawakaribisha wote wanaotafuta ukweli wawasiliane nasi.

Chanzo cha Mafanikio ya Umeme wa Mashariki

19

Chanzo cha Mafanikio ya Umeme wa Mashariki

Kila wakati Umeme wa Mashariki linapotajwa, ndugu wengi katika Bwana huhisi mafadhaiko: Ni kwa nini jumuiya ya kidini kwa ujumla huzidi kuhuzunika na kupotoka, wakati kila dhehebu linazidi kuwa na hadhari na kushikilia ukale katika kushutumu na kufukuza Umeme wa Mashariki, Umeme wa Mashariki halihuzuniki tu na kudhoofika, lakini linaendelea mbele kama mawimbi yasiyoweza kusimamishwa, likienea kote China Bara? Sasa kuwa hata limepanuka hata nje ya mipaka ya China hadi nchi za kigeni na maeneo, kama linavyokubaliwa na watu zaidi na zaidi duniani kote? Kama wamekabiliwa na ukweli huu, watu wa kidini wamefadhaika kabisa, huku kwa kweli sababu ni rahisi kabisa: Kile ambacho kila dhehebu la kidini linaita Umeme wa Mashariki ni Mwokozi Yesu aliyerudi wa siku za mwisho, akishuka kutoka mbinguni juu ya “wingu jeupe”; ni Mungu Mwenyewe ambaye alirejea kwa mwili na ni wa kweli na halisi! Kile Mwenyezi Mungu Kristo wa siku za mwisho huleta ni kazi ya hukumu ambayo hubadilisha tabia ya mwanadamu na kumtakasa, ili wanadamu waweze kufanikisha wokovu na kuwa wakamilifu. Mwenyezi Mungu huja na ukweli wote unaowatakasa, kuwaokoa, na kuwakamilisha wanadamu. Kwa sababu hii, hata kama kila dhehebu la kidini ulimwenguni kote humpinga, kumshambulia, kumtesa, kumkufuru, au kumshutumu Mungu mwenye mwili wa siku za mwisho au kazi Yake, hakuna yeyote wala nguvu yoyote ambayo inaweza kuzuia au kukomesha kamwe kile Anachotaka kufanikisha. Mamlaka ya Mungu, nguvu, na uweza Wake na hekima haviwezi kushindwa kwa nguvu yoyote ya Shetani.

Watu wengi huamini kuwa chochote kinachoshutumiwa na watu wengi hakiwezi kuwa njia ya kweli, lakini je, maoni haya yanapatana na ukweli? Fikiria nyuma wakati wa Enzi ya Neema wakati Mungu alipokuja katika mwili ili aanze kazi Yake mpya huko Uyahudi. Kuanzia mwanzo hadi mwisho Yeye aliteswa, akatukanwa, na kuhukumiwa na jumuiya ya kidini ya Kiyahudi. Walifanya kila kitu walichoweza ili kumwua Bwana Yesu. Hatimaye, walishirikiana na Roma ili kumfanya Bwana Yesu ashikwe na walimtundika Bwana Yesu mwenye rehema msalabani. Hata wakati wa ufufuo na kupaa mbinguni kwa Bwana Yesu, bado walibuni aina zote za uvumi na wakawasingizia na kuwashutumu Yohana, Paulo, na mitume wengine na wanafunzi, wakiwaita “Dhehebu la Wanazorayo” na “waasi na wanamadhehebu.” jumuiya ya kidini ya Wayahudi ilifanya kila lililowezekana kuwasaka na kuwatesa wafuasi wa Bwana Yesu. Lakini hekima ya Mungu daima hutumia na kujenga juu ya mbinu za Shetani; Je, kazi Yake ingewezaje kuzuiwa au kuangamizwa na Shetani? Ni kwa sababu ya mateso ya kitukutu ya Ufalme wa Kirumi na kufukuzwa ambapo wanafunzi walilazimika kukimbilia nchi mbalimbali na hivyo pia wokovu wa Bwana Yesu ulienea sehemu kubwa na kwa miisho ya dunia. Ndugu wa kiume na wa kike hebu tuzingatie: Kwa nini watu wengi walipinga Bwana Yesu na kuipinga njia Yake wakati huo? Inaweza kuwa ni kwa sababu Bwana Yesu hakuwa analeta njia ya kweli? Inaweza kuwa ni kwa sababu kile wanafunzi na mitume wa Bwana Yesu wa wakati huo walikuwa wakieneza hakikuwa wokovu wa Mungu? Inaweza kuwa kwamba kile ambacho watu walikitelekeza na kukipinga hakikuwa njia ya Mungu? Hakika hatuwezi kupima njia ya kweli kulingana na idadi ya watu wanaoiidhinisha? Usidhanie kitu kuwa ni njia ya uongo kwa sababu watu wengi huipinga. Almradi ni kazi ya Mungu, hata kama dunia nzima inaikataa na kuitelekeza, njia ya kweli iliyoletwa na Mungu haiwezi kukanwa; hakuna mambo ya pekee. Ikiwa tunamwamini Mungu na tumemfuata kwa miaka mingi lakini hatuijui kazi ya Mungu, ni rahisi kwetu kudanganywa na kufungwa na aina mbalimbali ya makosa ya kuhadaa na uvumi yanayoenezwa na Shetani. Kugeuka kutoka kwa muumini kuwa mfuasi wa Shetani, kumtumikia Mungu lakini pia kumpinga Yeye, si hili huleta huzuni na sikitiko kwa mtu? Watu wengi hawatafiti njia ya kweli kwa moyo mnyenyekevu na wa kutafuta, wao hufuata tu kundi na kufanya kile ambacho kila mtu mwingine hufanya. Bila kujali jinsi watu wengine wanavyomhukumu au kumshambulia Mungu na kazi Yake, wao hurudiarudia tu maneno hayo hayo na kufuata kwa upofu. Hili ni jambo hatari sana. Wakishikilia njia hii hatimaye watajikuta kwenye njia ya kikomo. Zamani za kale, wakati wafuasi wa Bwana Yesu walihubiri injili katika hekalu na walikumbana na upinzani kutoka kwa umma, mtu mmoja aitwaye Gamalieli, mwalimu wa sheria, aliwaonya Wayahudi, “Na sasa ninawaambia, Jiepusheni na hawa watu, achaneni nao: kwa kuwa kama ushauri huu ama kazi hii imetoka kwa wanadamu, itakuwa bure: Lakini kama imetoka kwa Mungu, hamuwezi kuiangamiza; ili msionekane kana kwamba labda hata mnapigana na Mungu” (Matendo 5: 38-39). Je, si hili pia lafaa kuwa kama onyo kwa waumini wa leo? Sasa, katika siku hizi za mwisho, Mungu amepata mwili tena nchini China–taifa ambako wakanamungu na wanamapinduzi wameshika madaraka na ni kiota hasa cha joka kubwa jekundu–kuanza kazi Yake ya hukumu ambayo inaanza kutoka kwa nyumba Yake. Mungu hutoa ukweli wa kuwahukumu na kuwatakasa wanadamu, kusudi likiwa ni kumwokoa mwanadamu kabisa kutoka kwa ushawishi mwovu wa Shetani. Hatimaye, wataletwa katika Ufalme Wake na Mungu na kupata hatima nzuri. Hata hivyo, msiba wa kihistoria wa upinzani wa Kiyahudi kwa Bwana Yesu umeonekana tena kwenye hatua. Kama Mungu anapofanya kazi Yake mpya ya siku za mwisho ambayo huchapa tena dhidi ya dhana za watu kutoka madhehebu mbalimbali ya kidini, watu hawa hawapokei kurudi kwa Bwana Yesu. Badala yake, hueneza kila aina ya mafundisho yaliyopotoka na uvumi wa udanganyifu. Wao humkashifu Mungu mwenye mwili na kazi Yake, wakiishutumu kazi ya Mungu mwenye mwili wa siku za mwisho kama “dhehebu bovu” au “usi.” Wao hufika kiasi cha kula njama na serikali ya Kikomunisti ya Kichina ili kumtesa na kumkamata Mungu mwenye mwili. Matendo yao si tofauti na yale ya jumuiya ya kidini ya Kiyahudi ambayo wakati mmoja ilimsingizia na kumtesa Bwana Yesu. Hata hivyo, njia ya kweli ni, hata hivyo, njia ya kweli. Kazi ya Mungu, hata hivyo, ni kazi ya Mungu. Bila kujali jinsi madhehebu mbalimbali ya kidini huipinga na kuishutumu kazi ya Mungu ya siku za mwisho, habari njema za ufalme Wake hata hivyo zimeenea kote nchini China, zikiitetemesha kabisa jamii ya kidini na ulimwengu wote.

Hivyo, kwa nini waumini wengi hupinga njia ya kweli? Kuna sababu mbili hasa kwa hili: 1.) Watu hawaelewi mwelekeo wa kazi ya Roho Mtakatifu na hawana ufahamu wa kirai, “Kazi ya Mungu daima inaenda mbele.” Si wafahamivu hata kidogo kwamba wanapaswa kutafuta kazi ya sasa ya Mungu; wao hupima tu kazi mpya ya Mungu kulingana na kile ambacho Mungu alifanya katika siku za nyuma. Iwapo hawakubaliani na kile wanachokiona, basi watadhania kazi mpya ya Mungu kuwa “uasi” au “dhehebu bovu.” 2.) Watu wana tabia za kujigamba na ya kujidai. Hawatafuti kabisa kazi mpya ya Mungu kwa moyo wa unyenyekevu. Badala yake, wao kwa ukaidi hushika mitazamo yao na kuamini kuwa maoni yao ni sawa na maoni ya Mungu na hawawezi kabisa kukubali ukweli. Kwa hiyo, wakati Mungu alipoanza enzi Yake mpya, sababu iliyofanya kazi Yake yote mpya ikabiliwe na upinzani kutoka kwa watu haikuwa kwa sababu ya hitilafu yoyote katika njia ya Mungu na haikuwa kutokana na kosa lolote katika kazi Yake mpya. Badala yake, ni kwa sababu watu hawaelewi kazi ya Mungu na ni kwa sababu hawawezi kutafuta ukweli kutokana na kiburi chao na hali yao ya kujidai. Itakuwa upuuzi na dhihaka ikiwa tutadhani kwamba hii sio njia ya kweli kwa sababu tu kuwa wengi wa waumini wameipinga na kuitelekeza kazi mpya ya Mungu. Hakika itakuwa ni kwa madhara yetu ya milele kama tutapoteza wokovu wa Mungu wa siku za mwisho kutokana na hili na bila mashaka litakuwa kosa lisilookoleka na la kifo.

Basi ni kwa jinsi gani hasa, tunatofautisha kati ya njia ya kweli na njia ya uongo? Neno la Mungu limetupa kanuni ambazo kwazo tunaweza kutofautisha. Mwenyezi Mungu anasema: “Kuijua kazi ya Mungu si kazi rahisi: Unapaswa kuwa na viwango na malengo katika utafutaji wako, unapaswa kujua jinsi ya kutafuta njia ya kweli, na jinsi ya kupima kujua kama ni njia ya kweli au si ya kweli, na kama ni kazi ya Mungu au kinyume chake. Kanuni ya msingi kabisa katika kuutafuta ukweli ni nini? Unapaswa kuangalia kama kuna kazi ya Roho Mtakatifu au la, iwapo maneno haya ni udhihirishaji wa ukweli, yanamshuhudia nani, na ni kitu gani yanaweza kukupatia. Kutofautisha kati ya njia ya kweli na hizi njia za uongo kunahitaji njia kadhaa za maarifa ya msingi, ya msingi kabisa kati ya zote ni kusema iwapo kuna Kazi ya Roho Mtakatifu au la. Maana kiini cha imani ya mwanadamu kwa Mungu ni imani katika Roho Mtakatifu. Hata imani yake kwa Mungu mwenye mwili ni kwa sababu mwili huu ni mfano halisi wa Roho wa Mungu, ikiwa na maana kwamba imani hiyo bado ni imani katika Roho. Kuna tofauti kati ya Roho na mwili, lakini kwa kuwa mwili unatokana na Roho, na ndio Neno linakuwa mwili, hivyo kile ambacho mwanadamu anaamini katika ni uungu halisi wa Mungu. Na hivyo, katika kutofautisha kama ni njia sahihi au la, zaidi ya yote unapaswa kuangalia kama kuna kazi ya Roho Mtakatifu, na baada ya hapo unapaswa kuangalia kama kuna ukweli katika njia hii. Ukweli huu ni silika ya maisha ya mwanadamu wa kawaida, ni sawa na kusema, kile ambacho Mungu alikitaka kwa mwanadamu alipomuumba hapo mwanzo, yaani, ubinadamu wote wa kawaida (ikiwa ni pamoja na hisia za kibinadamu, umaizi, hekima, na maarifa ya msingi ya kuwa mwanadamu). Yaani, unapaswa kuangalia iwapo njia hii inampeleka mwanadamu katika maisha ya mwanadamu wa kawaida au la, iwapo ukweli uliozungumzwa unahitajika kulingana na uhalisia wa ubinadamu wa kawaida au la, iwapo ukweli huu ni wa kiutendaji au hali, na iwapo ni wa wakati muafaka au la. Ikiwa kuna ukweli, basi unaweza kumpeleka mwanadamu katika uzoefu wa kawaida na halisi; aidha, mwanadamu anakuwa wa kawaida zaidi, hisia za kawaida za kibinadamu zinakuwa kamili zaidi, maisha ya mwanadamu katika mwili na maisha ya kiroho yanakuwa katika mpangilio mzuri zaidi, na mihemko ya mwanadamu inakuwa ya kawaida kabisa. Hii ni kanuni ya pili. Kuna kanuni nyingine moja zaidi, ambayo ni kama mwanadamu ana maarifa mengi juu ya Mungu, kama unapitia uzoefu wa kazi hiyo na ukweli unaweza kuchochea upendo wa Mungu ndani yake au la, na kumsogeza karibu zaidi na Mungu. Katika hili inaweza kupimwa kama ni njia sahihi au la. Kanuni ya msingi ni iwapo njia hii ni ya uhalisia badala ya kuwa ya kimiujiza, na iwapo inaweza kutoa maisha ya mwanadamu. Kama hukubaliana na kanuni hizi, hitimisho linaweza kuwekwa kwamba njia hii ni njia ya kweli” (“Ni Wale tu Wanaomjua Mungu na Kazi Yake ndio Wanaoweza Kumridhisha Mungu” katika Neno Laonekana katika Mwili). Kuna mambo matatu kutoka kwa maneno ya Mwenyezi Mungu ambayo tunapaswa kuzingatia ili tuweze kutofautisha kama kitu fulani ni njia ya kweli:

Kwanza, angalia kuona ikiwa kina kazi ya Roho Mtakatifu, ambalo ni jambo muhimu. Kwa sababu kama ni njia ya kweli, basi ni kazi ya Mungu Mwenyewe, kwa hivyo kwa hakika kina kazi ya Roho Mtakatifu na kitathibitishwa na Roho Mtakatifu. Sababu watu huamini katika Mungu mwenye mwili ni kwa sababu mwili huu ni mfano wa Roho wa Mungu, kwa hiyo yote ambayo Yeye hufanya ni kazi ya Roho Mtakatifu na ina thibitisho la Roho Mtakatifu. Kwa hiyo, watu humwamini Yeye na kumfuata Yeye. Hii ni kama wakati Bwana Yesu hufanya kazi Yake: Ingawa kwa juu juu inaweza kuonekana kwamba Yeye ni mtu wa kawaida na wa desturi, lakini kupitia neno Lake na kazi Yake mwanadamu huona kazi ya Roho Mtakatifu na matengenezo ya Roho Mtakatifu. Hii ni kwa sababu ubinadamu wote unaweza kuona kwamba neno na kazi ya Bwana Yesu zimejaa mamlaka na nguvu. Anaweza kumfanya kipofu aone, mtu aliyepooza atembee, na Aliwaponya wakoma. Anaweza kutumia mikate mitano na samaki wawili kulisha watu elfu tano na Anaweza hata kuwafufua wafu. Anaweza kuchunguza ndani ya mioyo ya wanaume kwa kina ili kufichua siri zao mbovu zaidi. Aidha, Anaweza kuwaambia wanadamu siri za mbinguni. Baada ya watu kumfuata, wao hupata amani na furaha katika mioyo yao. Sababu watu humfuata Bwana Yesu na kutambua kwamba Yeye ni Masihi ni kwa maana yote Anayofanya ni kazi ya Roho Mtakatifu. Tunaweza kuona kwamba almradi ndiyo njia ya kweli, itakuwa na kazi ya Roho Mtakatifu. Kwa hiyo, wakati wa kuangalia kama kitu ni njia ya kweli, tunapaswa kwanza kukiangalia ili kuona kama kina kazi ya Roho Mtakatifu.

Kipengele cha pili ambacho tunapaswa kupima wakati wa kuangalia kama kitu ni njia ya kweli ni kuona kama kina ukweli na ikiwa kinaweza kubadilisha tabia ya maisha ya mtu hatua ya kwa hatua ili kufanya ubinadamu uwe wa kawaida milele. Sote tunajua kwamba Mungu ni ukweli, njia, na uzima, na kwamba kila hatua ya kazi Yake mpya inategemea ukweli ambao Mungu hutoa kwa mtu, ambao huonyesha njia ya matendo katika enzi mpya. Mungu huhakikisha mtu ana ruzuku anazohitaji kwa maisha ili hatua kwa hatua aishi kwa kudhihirisha ubinadamu wa kawaida na ili hatua kwa hatua arudi kwa mfano wa asili wakati Mungu alipomuumba mwanadamu. Hii ni sifa bainifu dhahiri ya njia ya kweli. Ni kama tu wakati Bwana Yesu alipoanza kazi Yake katika Enzi ya Neema. Wakati huo, alitoa ukweli mwingi kwa watu ili wauweke katika matendo, na kuwafundisha kuwapenda wengine kama wanavyojipenda wenyewe, kuubeba msalaba, kujinyima, na kuwasamehe wengine mara saba mara sabini. Bwana Yesu aliwaambia watu kumwabudu Mungu katika roho na ukweli. Kila muumini wa kweli anaweza kuwa na mabadiliko fulani katika mwenendo wake wa nje kupitia mafundisho ya Bwana Yesu. Kwa njia ya Bwana Yesu anaweza kujiendesha kwa unyenyekevu na uvumilivu na kwa njia hiyo kumiliki mfano fulani wa mtu wa kawaida. Kwa hiyo, almradi ni njia ya kweli, basi kutakuwa na maonyesho ya ukweli. Hii inaweza kufanya akili ya binadamu ya mtu iwe ya kawaida zaidi na zaidi, na atafanana zaidi na jinsi mtu halisi anavyopaswa kuwa.

Kipengele cha tatu tunachopaswa kuangalia katika kutafakari njia ya kweli ni kuona kama njia inaweza kuwafanya watu wawe na ujuzi zaidi juu ya Mungu na kama inaweza kutia msukumo upendo wa Mungu ndani yao na kuwaleta karibu na Mungu. Sote tunajua kwamba kwa kuwa ni njia ya kweli, basi ni kazi ya Mungu Mwenyewe na kwamba kazi Yake huleta bila kuzuilika tabia Yake na chote kile Mungu alicho na alicho nacho. Wakati watu wanapopitia kazi ya Mungu, kwa kawaida wao hufikia ufahamu wa kweli wa Mungu, na kwa njia hiyo kuonyesha moyo wa upendo kwa Mungu ndani yao. Hii ni kama tu katika Enzi ya Sheria Yehova Mungu alipotoa sheria za kuyaongoza maisha ya watu duniani. Kutokana na uzoefu wao na kazi Yake, walitambua kuwa Yehova Mungu ni Mungu mmoja wa kweli. Aidha, walitambua uadhama na laana za Mungu na kwamba tabia Yake ni sharti isikosewe, ambayo ilisababisha ndani yao moyo wa kumchaji Mungu. Katika Enzi ya Neema, Mungu mwenye mwili alikuja duniani kufanya hatua ya kazi ya kuwakomboa wanadamu. Kupitia uzoefu wao na kazi ya Bwana Yesu, watu walitambua tabia ya Mungu ya upendo na huruma. Watu pia waliona kwamba Mungu alikuwa mara moja Roho lakini pia angeweza kuchukua mfano wa unyenyekevu wa binadamu, kwamba Angetenda miujiza, kuponya magonjwa na kuwatoa pepo…. Na kazi hii yote ambayo Bwana Yesu alifanya iliwafanya watu wawe na ufahamu mpya wa Mungu, ambao ulivutia kuabudu kwa Mungu ndani ya mioyo ya watu. Kwa hiyo, kama ni njia ya kweli itawafanya watu kuelewa zaidi kuhusu Mungu na kutia msukumo ufahamu mkubwa zaidi kuhusu tabia ya Mungu.

Ingawa kazi ya Mungu huenda mbele daima, almradi ni kazi ya Mungu Mwenyewe na njia ya kweli, hakika itamiliki na kuonyesha sifa tatu zilizojajwa. Hiyo ni kusema, njia ya kweli hakika itakuwa na kazi ya Roho Mtakatifu, itatoa ukweli, na itawafanya watu kupata ufahamu mkubwa zaidi wa Mungu na kuwaleta karibu zaidi na Yeye. Kwa hiyo, tukipambanua njia ya kweli kwa kupima viwango hivi vitatu, tutaweza kutofautisha yale ya kweli na ya uongo, hivyo tutaweza kwenda sambamba na kazi ya Mungu ya sasa kwa wakati wa kufaa, kupata ukweli, njia, na uzima, pamoja na kupata ahadi kubwa zaidi na baraka za Mungu.

Katika siku hizi za mwisho, Mungu anatekeleza kazi mpya tena, ambayo inahusisha kutoa maneno Yake ili kufanya kazi Yake ya hukumu na utakaso kwa wanadamu waliopotoka. Kazi hii inafanywa kulingana na mpango Wake na inategemea mahitaji halisi ya watu wa siku za mwisho. Ni kazi mpya, ya juu zaidi ilyotegemezwa kwa msingi wa kazi ya Bwana Yesu. Tukitafuta na kuchunguza kwa uangalifu na moyo wa utulivu, tunaweza kuona kwamba hatua hii ya kazi mpya ya Mungu haiwi na kazi ya Roho Mtakatifu tu, lakini pia hutoa ukweli na inaweza kuturuhusu kuwa na ufahamu zaidi wa kweli, mpana, na wa vitendo wa tabia ya Mungu na yote ambayo Mungu anayo na aliyo. Hapa chini, tutafanya ushirika kuhusu uzoefu wetu na ufahamu wa kazi ya Mungu katika siku za mwisho ukitegemezwa vipengele hivi vitatu vilivyojadiliwa vya kwanza kama viwango vya kuzingatia njia ya kweli.

Kwanza, njia ya kweli ina kazi ya Roho Mtakatifu. Mwenyezi Mungu amekuja na kuanzisha Enzi ya Ufalme, alitekeleza kazi mpya, akatoa neno Lake kuwahukumu na kuwatakasa watu, na Aliwaruzuku wanadamu ruzuku mpya za uhai. Waumini miongoni mwa kila kundi la dini na dhehebu, moja kwa moja, wamerudi kwa Mwenyezi Mungu chini ya jina Lake. Bila kujali upinzani, bila kujali ni vizuizi vipi vilivyoonekana, injili ya Mungu ya siku ya mwisho bado imeenda mbele kama mawimbi ya bahari na kuenea kote China bara. Watu wote wamekuwa wakimiminika kwa mlima mtakatifu katika eneo la furaha. Ingawa sote tulikuja kutoka kwa madhehebu tofauti, sisi bado tuna uwezo wa kuishi kwa umoja pamoja, kusaidiana. Hakuna magenge hapa na maisha ya kanisa yanafurika kwa uchangamfu. Ndugu wa kiume na wa kike hapa wanahisi kuwa mikutano yetu kamwe haitoshi, na kuna nyimbo za kuimba na kufurahia na sala zinazotunurisha. Kila wakati tunapokusanyika sisi wote tunaweza kupata ruzuku mpya kutoka kwa neno la Mwenyezi Mungu, tunaweza kutambua mapungufu yetu wenyewe, na kutoka kwa neno la Mungu sisi hupata njia ya kutenda. Ndugu zetu wa kiume na wa kike wanafurikwa na imani na wanaweza kuchukua agizo la Mungu kwa kujitoa. Tabia yetu potovu hubadilika kwa viwango tofauti, na tunaweza kuishi pamoja kwa kawaida na kupendana kwa mujibu wa neno la Mungu. Tunapokabiliwa na maoni tofauti, sote tunaweza kuweka kando maoni yetu wenyewe na kusikiliza kwa makini mawazo ya watu wengine, na kujitoa kwa mamlaka ya kweli katika neno la Mungu katika Kanisa. Hata kama katika hatua hii ya kazi Mungu harudii kazi Yake ya Enzi ya Neema ya kuponya wagonjwa na kutoa pepo, hata hivyo, tunaweza kuona kutokana na kazi ya Mwenyezi Mungu kwamba maneno yake ni yenye nguvu na hubeba mamlaka. Tukitii kazi na maneno ya Mwenyezi Mungu, basi tutaweza kupokea nuru na mwangaza kutoka kwa Roho Mtakatifu na tutaweza kujitenga kutoka hali zetu baridi na dhaifu, na kuweza kutekeleza wajibu wetu kiutendaji kama kiumbe aliyeumbwa kuwa wa kufikiria makusudi ya Mungu. Hivyo, ndugu zetu wa kiume na wa kike wanaweza kutelekeza anasa za mwili na kukimbilia kila mahali kwa ajili ya kazi ya kupanua injili ya ufalme ya Mungu kwa mioyo yetu yote. Bila kujali jinsi tunavyotendewa na madhehebu mbalimbali ya kidini, au kama tunakataliwa, au kuteswa, au kupigwa, au kulaaniwa, tuko tayari kuvumilia shida yoyote na tunaendelea kama kawaida kutekeleza mapenzi ya Mungu na kuihubiri injili ya Mwenyezi Mungu ya siku ya mwisho. Mtu anaweza kuona mamlaka na nguvu za Mwenyezi Mungu kutokana na tabia halisi ya ndugu zetu wa kiume na wa kike. Kazi ya Mwenyezi Mungu ina kazi ya Roho Mtakatifu na inathibitishwa na Roho Mtakatifu. Lakini kwa wale ambao hawajafuata kazi mpya wa Mungu, hayo madhehebu mbalimbali ya kidini yana wivu na ni yenye mkabala; wao hufanya kila kiwezekanacho kupiga maro dhidi ya wengine. Wao huishi katika mazingira ambamo huenda wao hufanya kazi ya aina moja, lakini sio kwa sababu sawa na yote haya yanatosha kuthibitisha kuwa jumuiya ya kidini tayari inakosa kazi ya Roho Mtakatifu. Kwa sababu Kanisa la Mwenyezi Mungu lina kazi ya Roho Mtakatifu, kwa hivyo huwa linaonekana likiwa na uchangamfu, wakati madhehebu mbalimbali ya kidini hayana mvuto, ni ya ukiwa, na yamepoteza kazi ya Roho Mtakatifu, yakiwa tofauti kabisa na Kanisa ya Mwenyezi Mungu. Kwa hiyo, ni dhahiri ni njia ipi iliyo ya kweli na ni ipi ambayo ni njia ya zamani.

Pili, njia ya kweli ina ukweli na inaweza kuashiria kwa watu njia ya matendo katika enzi mpya na inaweza kuwaruhusu watu kupata ruzuku mpya kwa ajili ya maisha. Tabia za maisha yao ya hupitia mabadiliko zaidi na zaidi na ubinadamu wao huwa wa kawaida zaidi na zaidi. Katika kazi Yake ya siku za mwisho, Mwenyezi Mungu hutoa ukweli mwingi katika nyanja mbalimbali. Hii ni pamoja na ukweli kuhusu kufahamu kazi ambayo Mungu hufanya na pia ukweli wa jinsi ya kutenda na kuingia katika enzi mpya. Kwa mfano hii ni pamoja na: Madhumuni ya usimamizi wa Mungu; kanuni ya Kazi Yake; ukweli wa ndani wa kazi ya Mungu kwenye Enzi ya Sheria na Enzi ya Neema, jinsi Mungu hufanya kazi Yake ya hukumu; umuhimu wa Mungu kupata mwili; jinsi wanadamu walikuja kuwa jinsi walivyo sasa; jinsi Shetani huwapotoa wanadamu; jinsi Mungu huwaokoa wanadamu; vile hatima ya wanadamu ya baadaye itakavyokuwa; vile mwisho utakavyokuwa kwa aina mbalimbali za watu; ni aina gani za maoni waumini wanapaswa kuwa nazo; kile imani yao katika Mungu kinapaswa kutafuta; kwa nini watu wanaoamini katika Mungu wanapaswa kujisalimisha Kwake; kwa nini kumpenda Mungu ndio njia pekee ya kuamini kwa kweli katika Mungu; na jinsi ya kumtumikia Mungu kwa njia ambayo huyaridhisha malengo Yake. Utoaji wa ukweli huu na Mwenyezi Mungu umeturuhusu kuwa na ufahamu bora zaidi wa nia za Mungu, na pia kuturuhusu kuwa na ufahamu bora juu ya asili yetu na tabia na ukweli wa upotovu wetu. Zaidi ya hayo, ukweli huu umeturuhusu kuona wazi barabara ya kubadilisha tabia zetu. Kupitia kwa kupata uzoefu wa kazi na neno la Mwenyezi Mungu, sisi hatimaye hukuja kuelewa mchanganyiko wa vipengele vya imani yetu ya zamani na hutambua kuwa hata kama tumepokea ukombozi wa Mungu na neema kubwa, hata hivyo bado sisi hutamani sana kupanga radhi zaidi za kimwili na baraka za mali kutoka kwa Mungu na jinsi ya kufanikisha ustawi wa ndoto zetu kupitia kwa Mungu. Zaidi ya hayo, hata kama sisi hushughulika tukifanya kazi kwa ajili ya Mungu, tunaifanya kwa ajili ya kubarikiwa na kupewa taji. Sisi hufanya hivyo kwa sababu ya umaarufu wa kibinafsi na kupata na sisi hukurupuka hapa na pale kwa faida yetu wenyewe. Huwa hatufanyi mambo haya ili kutimiza wajibu wetu kama kiumbe aliyeumbwa. Bila kujali ni kiasi gani cha neema au ni baraka ngapi sisi hupata kutoka kwa Mungu, kama chochote Mungu hufanya hukosa kwa njia fulani ndogo kuridhisha dhana zetu, mara moja sisi hupinga na kumlalamikia Mungu. Sisi hata huenda kwa kadiri ya kuwa wapinzani wa Mungu hadharani au hata kumtelekeza Mungu. Tulipoteza dhamiri zetu zamani sana na uwezo wa kuwa na fikira za kirazini mbele ya Mungu. Tulikuwa tumepotoshwa sana na Shetani kiasi kwamba tulipoteza kabisa umbo letu la ubinadamu. Ukweli uliotolewa na Mwenyezi Mungu unaturuhusu kuwa na ufahamu wa kweli wa upotovu wetu wenyewe na tunaweza kuona kuwa sisi ni wenye ubinafsi, wenye kustahili dharau, na tuliopungukiwa na ubinadamu. Wakati huo huo, tunaelewa umuhimu wa kazi ya wokovu ya Mungu ambayo tumefanyiwa, na tunaelewa wokovu wa Mungu wa binadamu ulikuwa umefikiriwa vizuri. Kwa njia hii, roho zetu zinaanza kuamka kidogo kidogo na dhamira yetu na uwezo wa kufikiri kirazini uaanza kurejeshwa siku baada ya siku. Hatutafuti tena kuiridhisha miili yetu wenyewe, tusimwelewe Mungu tena kwa njia ya kibiashara. Badala yake, twatafuta tu kutosheleza nia za Mungu na kutoa kwa Mungu kila kitu tulicho nacho. Kwa njia hii, sisi, kama viumbe walioumbwa, hatua kwa hatua tunarejesha uhusiano wa kawaida na Muumba. Tunakuwa wa kumpenda Mungu zaidi na zaidi, watiifu na watu wa kuabudu zaidi na zaidi, na hatimaye tunaanza kuonekana zaidi jinsi mtu ni lazima awe. Kwa kifupi, Mwenyezi Mungu hutupa, watu wa siku za mwisho, ukweli tunaouhitaji kwa dharura sana. Yeye hutuonyesha mwelekeo wa njia katika enzi mpya, Yeye hutukubalia kupata riziki halisi zaidi tunazohitaji kwa uhai. Haya yote yanathibitisha kuwa njia ya Mwenyezi Mungu ndiyo njia ya kweli.

Tatu, njia ya kweli humpa mwanadamu ufahamu mpya kuhusu Mungu. Ndugu zangu wa kiume na wa kike, kama mnaweza nyinyi binafsi kusoma maneno ya Mwenyezi Mungu na kwa kweli kuwasiliana na wale ambao wameipokea kazi ya Mwenyezi Mungu katika siku ya mwisho, si vigumu kugundua kwamba ndugu wa kiume na wa kike wa Kanisa la Mwenyezi Mungu wamepata maarifa mapya na ufahamu ulio na tofauti ndogo zaidi kumhusu Mungu kupitia namna ambavyo wao huutafuta ukweli wa Mwenyezi Mungu. Kwa njia ya kupitia kazi na maneno ya Mwenyezi Mungu, tunaelewa tabia ya haki ya Mungu na kuona kwamba tabia ya asili ya Mungu haina tu upendo na rehema, lakini pia uadhama na ghadhabu, na tabia Yake huwa haihimili kosa lolote lililotendwa na wanadamu. Kwa njia ya kupata uzoefu wa kazi na maneno ya Mwenyezi Mungu, tunaona jinsi Mungu humwokoa mwanadamu hatua kwa hatua, jinsi Mungu hutumia hekima Yake kumshinda Shetani, na hivyo tunapata elimu kiasi ya utendaji kuhusu uweza wa Mungu, hekima, shani na kutoeleweka. Zaidi ya hayo, tunapata pia ufahamu zaidi wa utendaji juu ya kusudi jema la Mungu kuwaokoa wanadamu, upendo Wake wa halisi kwa wanadamu na tabia Yake ya utakatifu na uzuri. Kupata uzoefu wa kazi na neno la Mwenyezi Mungu husaidia kutatua uelewa mwingi mbaya ambao tumekuwa nao kumhusu Mungu na hutusaidia kutambua kwamba Mungu si mali ya taifa lolote au kabila; Mungu ndiye Muumba, Mungu wa wanadamu wote. Tunaelewa pia kwamba kazi ya Mungu ni mpya daima na kamwe haizeeki na haijafungwa na kanuni zozote. Kutokana na haya inaweza kuonekana kuwa kazi na maneno ya Mwenyezi Mungu ya siku za mwisho yanaweza kumpa mtu ufahamu zaidi juu ya Mungu kuliko ilivyowezekana wakati wa Enzi ya Neema; ni ufahamu ambao ni wa utendaji zaidi na pia pana zaidi. Ni kazi ya Mungu mwenyewe tu inayoweza kuwa na athari hii na ni Mungu Mwenyewe tu anayeweza kutoa nje kwa watu tabia Yake na yote Aliyo na yote Aliyo nayo. Hakuna shaka yoyote kuwa njia ya Mwenyezi Mungu ndiyo njia ya kweli.

Kwa muhtasari, Umeme wa Mashariki, ambao umepingwa na kushutumiwa na jumuiya za kidini, ni Bwana Yesu ambaye amerejea kwa mwili katika siku za mwisho–ni Mungu Mwenyewe wa kipekee. Kwa hiyo, bila kujali jinsi madhehebu mbalimbali ya kidini yameupinga na kuushambuliwa na bila kujali ni kiasi gani umeshushiwa hadhi na kushutumiwa na majeshi ya Shetani, hayajaweza kuzuia hata kidogo upanuzi wa kazi ya Mungu katika siku za mwisho. Kwa takriban miaka kumi tu, injili ya ufalme ya Mwenyezi Mungu imeenea kotekote katika China bara nzima. Neno la Mungu na jina la Mungu yameeenea kote katika milioni mia nyingi za kaya. Miongoni mwa madhehebu mbalimbali, wale ambao huufuata ukweli na kwa kweli wanataka Mungu wamerudi mbele ya Mwenyezi Mungu. Watu milioni nyingi wanafurahia neno la Mungu, wakipokea hukumu ya Mungu, utakaso, wokovu na ukamilifu, na wakiyasifu matendo ya ajabu ya Mungu. Mungu ametengeneza kundi la washindi nchini China na amechuma kundi la watu ambao ni wa moyo mmoja na akili moja naye. Kazi ya Mungu hatimaye imehitimishwa kwa utukufu Wake na inaenda kwa kasi kutoka Mashariki–China hadi dunia ya magharibi na Kanisa la Mwenyezi Mungu limeanzisha matawi katika idadi kubwa ya nchi, ambalo ni utimizaji kamili wa unabii wa Bwana Yesu, “Kwa maana kama umeme utokavyo mashariki, na kumulika hata magharibi; hivyo ndivyo ujio wake Mwana wa Adamu utakavyokuwa” (Mathayo 24: 27). Wenzangu wa kiroho, wekeni chini kwa haraka dhana zenu za kufikiriwa na badala yake mtafute kusikia sauti ya Mungu, tafadhali njooni mbele ya Mungu kwa dhati: Mwenyezi Mungu anasubiri mrejeo yenu!