Kuwatambua Makristo wa Uongo Kutoka kwa Kristo wa Kweli

23/04/2023

Leo ningependa kuzungumzia jinsi ya kuwatambua Makristo wa uongo kutoka kwa Kristo wa kweli. Huenda wengine wakauliza hilo linahusiana nini na imani yetu katika Mungu. Linahusiana na mengi sana. Je, kila mtu anajua Kristo ni nani? Ikiwa unajua kwamba Kristo ndiye Mwokozi aliyekuja duniani, sasa kwa kuwa maafa yanakuja na siku za mwisho zimewadia, je, unafikiri kwamba unahitaji Mwokozi? Ikiwa unahitaji Mwokozi, unajua ni yupi unayehitaji akuokoe? Je, unajua jinsi ya kumkaribisha Mwokozi? Je, unafikiri kwamba hili ni jambo muhimu na linalokufaa? Kwa mfano, miaka 2,000 iliyopita, Mwokozi wetu Yesu alikuja kuwakomboa wanadamu, na akaonyesha ukweli mwingi. Watu wa Kiyahudi wakati huo walijua kwamba maneno Yake yalikuwa na mamlaka, yenye nguvu, na yote yalikuwa ukweli. Lakini kwa sababu hakuitwa Masihi na hakuwaokoa kutoka kwa utawala wa Kirumi kama walivyowazia, hawakumkubali Bwana Yesu kama Kristo. Walimhukumu na kumshutumu kama mtu anayewadanganya watu na mwishowe wakamfanya atundikwe msalabani akiwa hai. Matokeo yalikuwa yapi? Je, Mungu mwenye mwili kusulubishwa na watu wa Kiyahudi lilikuwa jambo rahisi? Hakika ililaaniwa na Mungu. Tunajua kwamba miaka 60 baadaye, taifa la Israeli liliangamizwa na Tito wa Roma. Israeli lilikuwa taifa lililoharibika kwa muda gani? Kwa takribani miaka 2,000! Kwa sababu walimsulubisha Mwokozi, Waisraeli walilipa gharama kubwa sana. Kwa hivyo basi, je, kumkaribisha Mwokozi ni jambo muhimu? Ni nani anayeweza kuthubutu kumkosea Mwokozi duniani? Ikiwa humjui au kumkubali, lakini hata umpinge na kumshutumu, wewe umeangamia—umeangamia kabisa, na una uhakika wa kufa. Ikiwa unataka kuokolewa na kunusurika majanga, lazima umkubali Mwokozi! Mwenyezi Mungu yuko hapa sasa, na Yeye ndiye Mwokozi aliyeshuka, akionyesha ukweli na kufanya kazi ya hukumu ya siku za mwisho ili kuwaokoa binadamu kutoka katika dhambi na kutoka katika majanga. Lakini ungemtambua? Je, ungemkubali? Ingawa wengi wanakiri kwamba maneno ya Mwenyezi Mungu yana nguvu na mamlaka, wanapoona kwamba Hakuja juu ya wingu na Yeye haitwi Bwana Yesu, wanakataa kwa uthabiti kumkubali Mwenyezi Mungu. Wanakubaliana hata na ulimwengu wa kidini, wakimshutumu na kumkufuru, wakisema kwamba Bwana akija katika mwili ni Kristo wa uongo, kwamba huu ni udanganyifu. Na majeshi ya wapinga Kristo wa kidini wanakubaliana na mapepo ya Chama cha Kikomunisti, wakimwinda Kristo kwa wazimu, wakijaribu kumwangamiza. Wanawatesa wale wanaoshiriki injili ya ufalme wa Mungu na wanataka sana kuliharibu kabisa Kanisa la Mwenyezi Mungu na kumfukuza Mungu kutoka katika ubinadamu. Huku ni kufanya dhambi kuu ya kumsulubisha Mungu tena, na hakika watalaaniwa na kuadhibiwa na Mungu. Kama vile Mwenyezi Mungu asemavyo, “Ole wao wamsulubishao Mungu(Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Waovu Hakika Wataadhibiwa). “Po pote ambapo Aliyepata mwili huonekana, adui anaangamiziwa mahali hapo. Uchina ni ya kwanza kuangamizwa, kuharibiwa kabisa kwa mkono wa Mungu. Mungu haipi Uchina upande wowote kabisa(Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Ufafanuzi wa Mafumbo ya “Maneno ya Mungu kwa Ulimwengu Mzima”, Sura ya 10). Kwa hivyo, mtazamo wa watu kwa Mwokozi huamua kama watanusurika au wataangamizwa.

Sasa kila mtu anajua kwamba kuweza kumkaribisha Mwokozi kunahusiana na mafanikio au kushindwa kwa mtu katika imani, na kunahusiana na matokeo na hatima yake ya mwisho! Kwa hiyo, tukiendelea, hebu tuzungumze kuhusu jinsi Mwokozi anavyorudi katika siku za mwisho. Kulingana na mawazo ya kawaida yanayoshikiliwa na ulimwengu wa kidini, ni hakika kwamba Bwana atakuja juu ya wingu na kuwachukua waumini juu angani ili wakutane na Yeye. Hili ni wazo la makosa kabisa. Hili ni wazo la binadamu tu na haliambatani na maneno ya Bwana. Bwana Yesu alitabiri binafsi “atakapokuja Mwana wa Adamu” “Mwana wa Adamu atafunuliwa” “atakapokuja Mwana wa Adamu” na “ndivyo Mwana wa Adamu atakuwa katika siku yake.” Alisisitiza kwa kurudia “mwana wa Adamu,” ambayo inaonyesha kwamba Bwana anakaporudi, Anapata mwili kama Mwana wa Adamu tena, na huku ndiko kuonekana kwa Kristo kwa binadamu. Hakuna uwezekano wa namna nyingine. Wengine wanaweza kuuliza, “Ikiwa ni Mwana wa Adamu mwenye mwili, je, si Yeye ni sawa na Bwana Yesu? Lazima aonekane kama mtu wa kawaida. Kuna watu ulimwenguni kote wanaodai kuwa Kristo aliyerudi. Wengine husema mtu fulani ni Kristo, wengine husema mwingine ni Kristo. Kwa hivyo ni yupi aliye wa kweli, na yupi ni wa uwongo? Je, tunawezaje kumkaribisha Mwokozi?” Hapa ndipo watu wengi hukwama wanapokuwa wakitafuta njia ya kweli. Kwa kweli, hili sio swali gumu. Mradi tunatafakari kwa dhati unabii wa Bwana Yesu, tutapata njia. Bwana Yesu alisema, “Bado ningali nayo mengi ya kuwaambieni, lakini hivi sasa hamwezi kuyavumilia. Hata hivyo, wakati Yeye, Roho wa ukweli, atakapokuja, Atawaongoza hadi kwenye ukweli wote(Yohana 16:12-13). “Na kukawa na kelele saa sita ya usiku, Tazama, anakuja bwana arusi; ondokeni nje ili kumkaribisha(Mathayo 25:6). “Kondoo wangu huisikia sauti yangu, na mimi Ninawajua, nao hunifuata(Yohana 10:27). “Tazama, nimesimama mlangoni, na kupiga hodi: mtu yeyote akisikia sauti Yangu, na aufungue mlango, Mimi nitaingia kwake, na nitakula na yeye, na yeye na Mimi(Ufunuo 3:20). “Basi iwapo mtu yeyote atawaambia, Tazameni, Kristo yuko huku, au yuko pale; msiamini hili. Kwa kuwa wataibuka Makristo wasio wa kweli, na manabii wasio wa kweli, nao wataonyesha ishara kubwa na vioja; ili kwamba, ikiwezekana, watawadanganya walio wateule zaidi(Mathayo 24:23-24). Bwana alizungumza kwa uwazi kabisa. Bwana Yesu atakaporudi katika siku za mwisho, Atatamka maneno mengi zaidi na kumwongoza mwanadamu kuelewa na kuingia katika ukweli wote. Kwa hiyo aliwakumbusha watu tena na tena kwamba ufunguo wa kumkaribisha Bwana ni kuisikia sauti ya Mungu. Na tukimsikia mtu fulani akitoa ushahidi kwamba “anakuja bwana arusi” tunapaswa kuwa mabikira wenye busara, na kutafuta na kuisikiliza sauti ya Mungu. Hiyo ndiyo njia pekee ya kumlaki Bwana. Ndiyo njia pekee ya kukaribisha kurudi Kwake. Kristo amekuja katika siku za mwisho, kwa hivyo bila shaka Anaonyesha ukweli zaidi kwa ajili ya wokovu wa wanadamu, lakini Makristo wa uongo wanategemea tu kuonyesha baadhi ya ishara na maajabu ili kuwapotosha watu. Hii ni kanuni muhimu ambayo Bwana Yesu alituambia ya kuwatambua makristo wa uongo kutoka kwa Kristo wa kweli. Kulingana na kanuni hii, tunaweza kujua kama ni Kristo wa kweli au wa uongo kulingana na iwapo anaonyesha ukweli. Kama anaweza, lazima ni Kristo. Wale wasioweza kuonyesha ukweli lazima wawe makristo wa uongo. Ikiwa mtu anadai kuwa Kristo lakini hawezi kuonyesha ukweli wowote, badala yake anategemea ishara na maajabu, bila shaka ni sura ya pepo mchafu, Kristo wa uongo anayekuja kuwapotosha watu. Tunapofuata maneno ya Bwana Yesu ili kutambua Kristo wa kweli kutoka kwa wale wa waongo, ni rahisi sana, sivyo? Lakini kwa bahati mbaya, wafuasi wa dini hawatafuti ukweli au kutafuta sauti ya Mungu kulingana na maneno ya Bwana. Kwa hivyo wakiogopa kupotoshwa na Kristo wa uwongo, wao hawatatafuta hata kuonekana na kazi ya Bwana. Je, huko sio kukata pua lako ili kuudhihaki uso wako, kuwe mwenye busara kuhusu mambo madogo lakini mjinga kuhusu mambo makubwa? Wanashikilia kwa upofu Maandiko kuhusu Bwana kuja juu ya wingu, wakilaani na kukataa kazi ya Kristo wa siku za mwisho. Matokeo yake, wanapoteza nafasi yao ya kumkaribisha Mwokozi na kuanguka katika majanga. Je, hayo si matokeo ya upumbavu na ujinga wao? Hili linatimiza mistari hii ya Biblia: “Wapumbavu hukufa kwa ajili ya ukosefu wa busara” (Mithali 10:21). “Watu wangu wanateketezwa kwa ajili ya ukosefu wa maarifa(Hosea 4:6).

Kuhusu jinsi ya kumjua Kristo wa kweli kutoka kwa wale wa uongo, hebu tuingie kwa undani juu ya mada hiyo kulingana na maneno ya Mwenyezi Mungu. Mwenyezi Mungu anasema, “Mungu mwenye mwili Anaitwa Kristo, na Kristo ni mwili uliovishwa na Roho wa Mungu. Mwili huu ni tofauti na wa mwanadamu yeyote aliye wa nyama. Tofauti hii ni kwa sababu Kristo sio wa mwili na damu bali ni mwili wa Roho. Anao ubinadamu wa kawaida na uungu kamili. Uungu Wake haujamilikiwa na mwanadamu yeyote. Ubinadamu Wake wa kawaida unaendeleza shughuli Zake zote za kawaida katika mwili, wakati uungu Wake unafanya kazi ya Mungu Mwenyewe(Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Kiini Cha Kristo Ni Utiifu kwa Mapenzi ya Baba wa Mbinguni).

Mungu aliyepata mwili anaitwa Kristo, na hivyo Kristo ambaye anaweza kuwapa binadamu ukweli anaitwa Mungu. Hakuna kitu kilichozidi kuliko hiki, kwa kuwa Anacho kiini cha Mungu, na ana tabia za Mungu, na busara katika kazi Yake, ambavyo haviwezi kufikiwa na mwanadamu. Wale wanaojiita Kristo, walakini hawawezi kufanya kazi ya Mungu, ni matapeli. Kristo wa kweli sio tu udhihirisho wa Mungu duniani, bali pia, mwili hasa uliochukuliwa na Mungu kufanya na kutimiza kazi Yake kati ya wanadamu. Mwili huu si ule unaoweza kubadilishwa na mtu yeyote tu, lakini ambao unaweza kutosha kufanya kazi ya Mungu duniani, na kuonyesha tabia ya Mungu, na pia kumwakilisha Mungu vizuri, na kumpa binadamu uzima. Hivi karibuni au baadaye, wale wanaojifanya kuwa Kristo wataanguka wote, kwani ingawa wanadai kuwa Kristo, hawana chochote kinachohusiana na kiini cha Kristo. Na hivyo Mimi nasema kwamba uhalali wa Kristo hauwezi kuelezwa na mwanadamu, bali unajibiwa na kuamuliwa na Mungu Mwenyewe(Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Ni Kristo wa Siku za Mwisho Pekee Ndiye Anayeweza Kumpa Mwanadamu Njia ya Uzima wa Milele).

Yeye Aliye mwili wa Mungu Atakuwa na dutu ya Mungu, na Yule Aliye Mungu katika mwili Atakuwa na maonyesho ya Mungu. Kwa maana Mungu Hupata mwili, Ataleta mbele kazi Anayopaswa kufanya, na kwa maana Mungu Amepata mwili, Ataonyesha kile Alicho na Ataweza kuuleta ukweli kwa mwanadamu, kumpa mwanadamu uhai, na Amwonyeshe mwanadamu njia. Mwili usio na dutu ya Mungu kwa kweli sio Mungu mwenye mwili; kwa hili hakuna tashwishi. Kupeleleza kama kweli ni mwili wa Mungu mwenye Mwili, mwanadamu lazima aamue haya kutoka kwa tabia Yeye huonyesha na maneno Yeye hunena. Ambayo ni kusema, kama ni mwili wa Mungu mwenye mwili au la, na kama ni njia ya kweli au la, lazima iamuliwe kutokana na dutu Yake. Hivyo, katika kudadisi iwapo ni mwili wa Mungu mwenye mwili, cha msingi ni kuwa makini kuhusu dutu Yake (Kazi Yake, maneno Yake, tabia Yake, na mengine mengi), bali sio hali ya sura Yake ya nje. Mwanadamu akiona tu sura Yake ya nje, na aipuuze dutu Yake, basi hilo linaonyesha upumbavu na ujinga wa mwanadamu(Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Dibaji).

Kuna wengine ambao wamepagawa na roho wachafu na wanalia kwa kusisitiza wakisema, ‘Mimi ni Mungu!’ Lakini mwishowe, hufichuliwa, kwani wanafanya kazi kwa niaba ya kiumbe asiyefaa. Wanawakilisha Shetani na Roho Mtakatifu hajali kuwahusu hata kidogo. Hata ujiinue vipi, ama kwa nguvu kivipi, wewe bado ni kiumbe aliyeumbwa na wewe unamilikiwa na Shetani. … Huwezi kuleta njia mpya ama kumwakilisha Roho. Huwezi kueleza kazi ya Roho ama maneno Anenayo. Huwezi kufanya kazi ya Mungu Mwenyewe ama ile ya Roho. Huwezi kuelezea busara, ajabu na mambo ya Mungu yasiyoeleweka, ama tabia yote ambayo Mungu humwadibu mwanadamu kupitia kwayo. Kwa hivyo madai yako ya kila mara ya kusema kuwa wewe ni Mungu hayajalishi; unalo tu jina lakini huna dutu. Mungu Mwenyewe Amekuja, lakini hakuna anayemtambua, ilhali Anaendelea na kazi Yake na Anafanya hivyo kwa uwakilishi wa Roho. Haijalishi unamwita mwanadamu ama Mungu, Bwana ama Kristo, ama umwite dada, yote ni sawa. Lakini kazi Afanyayo ni ile ya Roho na Anawakilisha kazi ya Mungu Mwenyewe. Hajali ni jina gani mwanadamu anamwita. Je, jina hilo linaweza kuamua kazi Yake? Bila kujali unachomwita, kutoka kwa mtazamo wa Mungu, Yeye ni kupata mwili kwa Roho wa Mungu; Anawakilisha Roho na amekubaliwa na Yeye. Huwezi kutengeneza njia ya enzi mpya, na huwezi kuhitimisha enzi nzee na huwezi kukaribisha enzi mpya ama kufanya kazi mpya. Kwa hivyo, huwezi kuitwa Mungu!(Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Fumbo la Kupata Mwili (1)).

Kama, wakati wa zama hizi, kutatokea mtu mwenye uwezo wa kuonyesha ishara na maajabu, na kutoa mapepo, kuponya wagonjwa, na kufanya miujiza mingi, na kama mtu huyu anadai kwamba yeye ni Yesu ambaye amekuja, basi hii itakuwa ni ghushi ya roho wachafu, na kumuiga Yesu. Kumbuka hili! Mungu Harudii kazi ile ile. Hatua ya kazi ya Yesu tayari imekwisha kamilika, na Mungu Hataichukua tena hatua hiyo ya kazi. Kazi ya Mungu haipatani na dhana za mwanadamu; kwa mfano, Agano la Kale lilitabiri juu ya ujio wa Masihi, lakini ilikuwa dhahiri kwamba Yesu Alikuja, hivyo itakuwa makosa kwa Masihi mwingine kuja tena. Yesu tayari Amekwishakuja mara moja, na yatakuwa ni makosa ikiwa Yesu Atakuja tena wakati huu. Kuna jina moja kwa kila enzi, na kila jina linaeleza sifa ya enzi. Katika dhana za mwanadamu, Mungu ni lazima siku zote Aonyeshe ishara na maajabu, ni lazima siku zote Aponye wagonjwa na kutoa mapepo, na siku zote ni lazima Awe tu kama Yesu, lakini Mungu wakati huu Hayupo kama hivyo kabisa. Ikiwa, wakati wa siku za mwisho, Mungu bado Angeonyesha ishara na maajabu, na bado Angetoa mapepo na kuponya wagonjwa—kama Angefanya vilevile ambavyo Yesu Alifanya—basi Mungu Angekuwa Anarudia kazi ile ile, na kazi ya Yesu isingekuwa na maana au thamani yoyote. Hivyo, Mungu Anatekeleza hatua moja ya kazi katika kila enzi. Mara tu kila hatua ya kazi Yake inapokamilika, baada ya muda mfupi inaigizwa na roho wachafu, na baada ya Shetani kuanza kufuata nyayo za Mungu, Mungu Anabadilisha na kutumia mbinu nyingine. Mara Mungu Anapokamilisha hatua ya kazi Yake, inaigizwa na roho wachafu. Lazima muelewe vizuri hili(Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Kuijua Kazi ya Mungu Leo).

Baada ya kusoma haya, je, si sisi sote tunaelewa vyema zaidi kuhusu Kristo ni nini, na jinsi ya kumtofautisha Kristo wa kweli na wale waongo? Kristo ni Mungu mwenye mwili, Roho wa Mungu aliyevikwa mwili kama Mwana wa Adamu. Kutoka nje, Kristo ni mtu wa kawaida tu. Lakini kiini Chake ni tofauti kabisa na kile cha mtu wa kawaida. Kristo ana Roho wa Mungu ndani Yake, Yeye ni mfano halisi wa Roho wa Mungu, kwa hivyo ana asili ya kiungu. Kimsingi, Kristo ndiye Mungu mmoja wa kweli, Bwana wa uumbaji! Kristo anaweza kuonyesha ukweli, na tabia ya Mungu na kile Alichonacho na alicho mahali popote, wakati wowote. Anaweza kufanya kazi ya ukombozi wa mwanadamu na vilevile kazi ya hukumu na utakaso wa mwanadamu. Kando na Kristo, hakuna mwanadamu aliyeumbwa, malaika, au roho mwovu wa kishetani ambaye anaweza kuonyesha ukweli, sembuse kuwaokoa binadamu. Hakuna shaka kuhusu hili. Kwa hivyo, cha msingi katika kumtambua Kristo wa kweli kutoka kwa waongo ni hasa kuona kama anaonyesha ukweli, kama anaweza kufanya kazi ya wokovu wa mwanadamu. Hii ndiyo kanuni muhimu na ya msingi zaidi. Sote tunajua kwamba Bwana Yesu alionyesha ukweli mwingi na kuhubiri njia ya toba, na Alifanya ishara nyingi na maajabu, akikamilisha kazi ya ukombozi wa mwanadamu. Alianzisha Enzi ya Neema na kuitamatisha Enzi ya Sheria. Maneno ya Bwana yalikuwa na nguvu na mamlaka mengi na yalijawa na tabia ya Mungu, na kile Alicho nacho na alicho. Tunajua mioyoni mwetu kwamba Bwana Yesu alikuwa Kristo katika mwili, kuonekana kwa Mungu. Mwenyezi Mungu amekuja katika siku za mwisho, Akionyesha mamilioni ya maneno ya ukweli, na kufanya kazi ya hukumu akianza na nyumba ya Mungu. Maneno Yake hayakufunua tu mafumbo yaliyo katika Biblia, lakini pia yale ya mpango wa Mungu wa usimamizi wa miaka 6,000. Hii inajumuisha malengo ya mpango wa usimamizi wa Mungu, ukweli wa ndani wa hatua Zake tatu za kazi, jinsi Shetani anavyowapotosha wanadamu, jinsi Mungu anavyofanya kazi hatua kwa hatua ili kuwaokoa wanadamu, mafumbo ya kupata mwili, ukweli wa ndani wa Biblia, matokeo ya mtu wa kila aina, jinsi ufalme wa Kristo unavyotimizwa duniani, na zaidi. Mafumbo haya yote yamefunguliwa. Mwenyezi Mungu pia huhukumu na kufunua asili ya mwanadamu ya dhambi, ya kumpinga Mungu na tabia potovu. Anatoa njia ya kutupilia mbali upotovu na kutakaswa, na kadhalika. Maneno ya Mwenyezi Mungu ni mengi sana, na yote ni mafumbo na ukweli ambao watu hawajawahi kusikia hapo awali. Ni yenye kuzindua na kutimiza, na yeyote anayeyasoma lazima akubali kwamba kweli ni ya ukweli. Watu wateule wa Mungu hupitia hukumu ya maneno Yake na kuelewa ukweli mwingi; wanasafishwa hatua kwa hatua kutoka kwa upotovu, wakitoa ushahidi mkubwa wa kutupilia mbali dhambi na kumshinda Shetani. Hili linatimiza unabii wa Bwana Yesu: “Bado ningali nayo mengi ya kuwaambieni, lakini hivi sasa hamwezi kuyavumilia. Hata hivyo, wakati Yeye, Roho wa ukweli, atakapokuja, Atawaongoza hadi kwenye ukweli wote: kwa maana Hatazungumza juu Yake Mwenyewe; bali chochote Atakachosikia, Atakinena: na Atawaonyesha mambo yajayo(Yohana 16:12-13). Hili linathibitisha kwamba Mwenyezi Mungu ni “Roho wa ukweli.” Yeye ndiye kuonekana kwa Kristo wa siku za mwisho, Mwokozi aliyekuja duniani.

Sasa nadhani kila mtu anapaswa kuelewa bayana kwamba Mwenyezi Mungu ni Kristo, Mwokozi. Haya si mazungumzo tu, bali yanathibitishwa kulingana na ukweli Anaoonyesha na kazi Anayoifanya. Vipi kuhusu makristo wa uwongo? Wao hupiga kelele mara kwa mara, “Mimi ndiye Kristo.” Unaweza kuwauliza, “Je, mnaweza kuonyesha ukweli? Je, unaweza kufichua ukweli wa upotovu wa mwanadamu? Je, unaweza kuwaokoa wanadamu kutoka katika dhambi?” Hawawezi kufanya hata moja kati ya haya. Wanapigwa na butwaa wanapokabiliwa na maswali haya. Makristo wa uwongo ni bandia za Shetani au pepo wabaya tu, wanaokosa kabisa uzima na kiini cha Mungu. Kwa hivyo, hawawezi kamwe kuonyesha ukweli au kufanya kazi ya kutakasa na kuwaokoa wanadamu. Wanachoweza kufanya ni kueneza mafundisho ya uwongo ambayo yanaonekana kuwa ya kweli au kuonyesha ishara na maajabu kiasi ili kuwapumbaza watu. Baadhi ya makristo wa uongo wana vipaji fulani, na wanaweza kuandika vitabu vyao wenyewe, na wanaweza kufafanua ujuzi wa kina wa Biblia. Lakini vitu vyote wanavyoshiriki ni mawazo na nadharia za binadamu, na haijalishi jinsi yanavyoonekana mazuri kwa mwanadamu, hayo si ukweli. Hawawezi kamwe kutoa riziki kwa maisha ya mwanadamu au kuwasaidia watu kumjua Mungu na ukweli, na hasa hawawezi kutuokoa kutoka dhambini ili tuweze kutakaswa. Huu ni ukweli ulio wazi. Kristo wa uwongo hana ukweli kabisa, lakini ana shauku nyingi mno, na anataka watu wamwabudu kama Mungu. Kwa hiyo wanafanya nini? Wanaiga kazi ya zamani ya Mungu, wakionyesha baadhi ya ishara na maajabu rahisi ili wajifanye kuwa Kristo, na kuwapotosha wengine kwa upendeleo fulani mdogo. Ikiwa muumini hapendi ukweli, lakini anataka tu kula ashibe na kufurahia neema kiasi, na kufanya ishara na maajabu ndicho kipimo cha pekee cha kujua kama mtu fulani ni Mungu, basi ni rahisi kwake kupotoshwa. Kwa kweli, hila za Kristo za uwongo zinaweza tu kuwapumbaza watu wasio na akili na wajinga. Kondoo wa Mungu, mabikira wenye busara, hawatachukuliwa kamwe na Kristo wa uwongo, kwa sababu wanapenda ukweli na wanaisikiliza sauti ya Mungu. Wanaposikia sauti ya Mungu, wanaikubali na kuifuata. Mungu aliamua hili zamani sana. Kama tu Bwana Yesu alivyosema, “Kondoo wangu huisikia sauti yangu, na mimi Ninawajua, nao hunifuata(Yohana 10:27). “Baba yangu ambaye alinikabidhi wao, ni mkubwa kuliko wote; na hakuna mwanadamu anayeweza kuwanyakua kutoka mkononi mwa Baba yangu(Yohana 10:29).

Sasa nadhani sote tunaelewa zaidi juu ya jinsi ya kumtambua Kristo wa kweli kutoka kwa Makristo wa uongo. Kristo ni Mungu katika mwili, ukweli, njia na uzima. Kiini cha uungu cha Kristo kinadhihirishwa hasa katika uwezo Wake wa kuonyesha ukweli na kufanya kazi ya Mungu mwenyewe. Haijalishi jinsi Anavyoweza kuonekana asiyestaajabisha, na haijalishi Anavyoweza kuwa mwenye mamlaka na hadhi ya chini, Awe anakubaliwa au kukataliwa na wanadamu, mradi Anaweza kuonyesha ukweli, tabia ya Mungu, na kile ambacho Mungu Anacho na Alicho, na Anaweza kufanya kazi ya wokovu, basi Yeye ni mwonekano wa Mungu. Hakuna shaka kuhusu hili. Ukweli ulioonyeshwa na Mwenyezi Mungu, kazi Yake ya kuhukumu na kuwatakasa wanadamu kabisa inathibitisha kwamba Yeye ni Mungu katika mwili, kwamba Yeye ni kuonekana kwa Kristo. Lazima tumkubali na kumfuata Kristo wa siku za mwisho, Mwenyezi Mungu, ili tupate ukweli, kuokolewa kikamilifu, na kuingia katika ufalme wa Mungu. Lakini sasa watu wengi wanawaona wachungaji na viongozi wa kidini na utawala wa kishetani wa Chama cha Kikomunisti wakimpinga na kumhukumu Mwenyezi Mungu kwa wazimu, hivyo wanafikiri kwamba kazi ya Mwenyezi Mungu si njia ya kweli. Mawazo yao ni: Kama hii ingekuwa kazi ya Mungu, yote ingekuwa ya mwendo shwari, na kila mtu angesadikishwa kabisa. Kulichukulia jambo hili kwa njia hii ni upumbavu wa ajabu! Huku ni kukosa kuona kwamba mwanadamu amepotoshwa sana hadi kufikia kiwango cha kuwa adui wa Mungu na kukosa nafasi kwa Mungu. Je, watu walimkaribisha Bwana Yesu alipokuja? Je, watu wa Kiyahudi hawakuungana na serikali ya Kirumi ili kumsulubisha? Je, unaweza kusema kwamba kazi ya Bwana Yesu haikuwa njia ya kweli? Na watu wanamtendeaje Mwenyezi Mungu, saas kwa kuwa Amekuja katika siku za mwisho? Majeshi ya wapinga Kristo ya ulimwengu wa kidini yanafanya kila kitu kumpinga na kumhukumu, utawala wa kishetani wa CCP unamwinda kwa wazimu, ukitumia kila mbinu kufuta kuonekana kwa Mungu na kazi Yake. Hii inatimiza kile ambacho Bwana Yesu alitabiri: “Kwani kama umeme, unavyomulika chini ya mbingu kutoka sehemu moja, huangaza hadi sehemu nyingine chini ya mbingu; vivyo ndivyo Mwana wa Adamu atakuwa katika siku yake. Bali kwanza lazima apitie mambo mengi, na akataliwe na kizazi hiki(Luka 17:24-25). Hii ina maana gani? Njia ya kweli imekandamizwa kila wakati! Kristo huonyesha ukweli ili kumwokoa mwanadamu, kwa hivyo ni jambo lisiloepukika kwamba Atapingwa, kushutumiwa, na kufuatiliwa na nguvu za uovu za Shetani. Ikiwa kuna madai kwamba mtu fulani ni Kristo, lakini haonyeshi ukweli na hajakataliwa na kizazi hiki, ikiwa hajashutumiwa kwa fujo na kushambuliwa na majeshi ya Shetani, hiyo inathibitisha kwamba yeye si Kristo. Zaidi ya chochote, Shetani anachukia kuonekana kwa Mungu na kazi Yake, na anachukia ujio wa Mwokozi. Shetani anajua kwamba Mwokozi anapokuja, watu wanakuwa na nafasi ya kupata wokovu, kuelewa ukweli na kubaini hila za Shetani. Kisha wanaweza kupata utambuzi, kumkataa, kumgeukia Mungu kikamilifu na kupatwa na Mungu. Kisha Shetani anashindwa kabisa, na siku yake ya mwisho iko karibu kufika. Je, unafikiri kwamba Shetani atakubali hilo bila kufanya chochote? Bila kuelewa hili, lakini kung'ang'ania tu mawazo yako mwenyewe na kushindwa kuichunguza kazi ya Mwenyezi Mungu, au hata kukubaliana na nguvu za wapinga Kristo wa ulimwengu wa kidini, ukimlaani na kumpinga Mwenyezi Mungu, kutasababisha matokeo ya kutisha. Hebu tuone kile ambacho Mungu Mwenyezi Anasema. “Wale ambao wanataka kupata uzima bila kutegemea ukweli wa neno la Kristo ni watu wafidhuli mno duniani, na wale ambao hawawezi kukubali njia ya maisha inayoletwa na Kristo wamepotea ndotoni. Na hivyo nasema kwamba watu ambao hawakubali Kristo wa siku za mwisho watadharauliwa milele na Mungu. Kristo ni lango la binadamu kwa ufalme katika siku za mwisho, ambayo hakuna anayeweza kupita bila Yeye. Hakuna anayeweza kukamilishwa na Mungu ila kwa njia ya Kristo. Unaamini katika Mungu, na hivyo ni lazima ukubali neno Lake na kutii njia Yake. Lazima usifikiri juu ya kupata baraka tu bila kupokea ukweli, au kukubali utoaji wa maisha. Kristo Anakuja katika siku za mwisho ili wale wote ambao kweli wanaamini katika Yeye waweze kupata maisha. Kazi Yake ni kwa ajili ya kuhitimisha enzi ya zamani na kuingia enzi mpya, na ni njia ambayo lazima ichukuliwe na wale wote ambao wataingia enzi mpya. Kama huna uwezo wa kumtambua Yeye, na badala yake kumhukumu, kulikufuru jina Lake au hata kumtesa Yeye, basi wewe umefungwa kuchomwa milele, na kamwe hutaingia katika ufalme wa Mungu. Kwa maana Kristo Mwenyewe ni onyesho la Roho Mtakatifu, onyesho la Mungu, Yule ambaye Mungu amemkabidhi kufanya kazi Yake hapa duniani. Na hivyo nasema kwamba kama huwezi kukubali yote yanayofanywa na Kristo wa siku za mwisho, basi unakufuru Roho Mtakatifu. Adhabu ambayo lazima ishuhudiwe na wale ambao wanakufuru Roho Mtakatifu ni hasa dhahiri kwa wote. Nawaambia tena kwamba kama mtampinga Kristo wa siku za mwisho, na kumkanusha, basi hakuna mtu ambaye anaweza kubeba matokeo ya hilo kwa niaba yako. Aidha, tangu siku hii na kuendelea huwezi kuwa na nafasi nyingine ya kupata kibali cha Mungu; hata kama utajaribu kujikomboa mwenyewe, kamwe tena hutautazama uso wa Mungu. Kwa kuwa unachopinga si binadamu, unachokataa si jambo dogo, bali ni Kristo. Je, unafahamu ghadhabu ya matokeo haya? Wewe hujafanya makosa madogo, bali umetenda uhalifu wa kutisha. Na hivyo Nashauri kila mtu kutoweka wazi meno yenu mbele ya ukweli, au kufanya shutuma bila ya kujali, kwa kuwa ni ukweli tu unaoweza kukuletea maisha, na hakuna kitu isipokuwa ukweli kinachoweza kukuruhusu kuzaliwa upya na kutazama uso wa Mungu(Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Ni Kristo wa Siku za Mwisho Pekee Ndiye Anayeweza Kumpa Mwanadamu Njia ya Uzima wa Milele).

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Maudhui Yanayohusiana

Leave a Reply

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp