Bwana Yesu Amewakomboa Wanadamu, Hivyo Kwa Nini Afanye Kazi ya Hukumu Atakaporudi Katika Siku za Mwisho?

23/04/2023

Miaka 2,000 iliyopita, Bwana Yesu mwenye mwili alisulubishwa ili kuzikomboa dhambi za wanadamu, akifanyika sadaka ya dhambi na kukamilisha kazi Yake ya ukombozi. Aliahidi angerudi katika siku za mwisho, kwa hiyo waumini wote wamekuwa wakikesha wakingoja kwa uangalifu kuja kwa Bwana, na hufikiri kwamba kama waumini katika Bwana, dhambi zao zote zimesamehewa, na Yeye hawaoni tena kuwa wenye dhambi. Wanafikiri kwamba wako tayari kabisa, kwa hivyo wanahitaji tu kungojea kurudi kwa Bwana ili waweze kuchukuliwa hadi katika ufalme Wake. Hii ndiyo maana watu daima hutazama angani, wakisubiri siku Atakapotokea ghafla juu ya wingu na kuwachukua kwenda mbinguni ili kukutana na Yeye. Lakini linalowashangaza sana, wanatazama maafa makubwa yakianza lakini bado hawajamkaribisha Bwana. Hakuna anayejua kile kinachoendelea hasa. Ingawa hawajamwona Bwana akija juu ya wingu, wameona Umeme wa Mashariki likitoa ushuhuda thabiti kwamba Amerudi kama Mwenyezi Mungu mwenye mwili. Ameonyesha ukweli na anafanya kazi ya hukumu Akianza na nyumba ya Mungu. Kuonekana kwa Mwenyezi Mungu na kazi Yake vimeutikisa ulimwengu wote wa kidini na kuzindua upinzani mkubwa. Kazi ya hukumu ya Mungu mwenye mwili imepitana sana na fikira na mawazo ya watu. Wengi wanauliza: Bwana Yesu tayari alikamilisha kazi Yake kuu ya ukombozi, na Mungu ametuita wenye haki, kwa hivyo kwa nini Angehitaji kufanya kazi ya hukumu katika siku za mwisho? Wanahisi hilo haliwezekani. Jumuiya ya kidini hata inampinga na kumshutumu Mwenyezi Mungu, ikikataa kuichunguza kazi Yake, huku wakimngoja Bwana kwa hamu aje juu ya wingu ili kuwanyakua hadi katika ufalme, wakitumaini kuepuka maafa makubwa. Hata hivyo, kazi ya Mungu ni kubwa mno na yenye nguvu na hakuna anayeweza kuizuia. Mwenyezi Mungu amefanya kundi la washindi na majanga yameanza, huku ulimwengu wa kidini ukizama katika majanga, wakilia na kusaga meno. Kwa kuwa hawakunyakuliwa kabla ya majanga, wanatumaini kwamba wanyakuliwe wakati au baada ya majanga. Kwa nini hawakumkaribisha Bwana kabla ya majanga? Walikosea wapi? Je, Bwana Yesu alivunja ahadi Yake, na kushindwa kuwachukua waumini katika ufalme kabla ya majanga, na kuwavunjia matumaini kabisa? Au je, watu watu waliuelewa unabii wa Biblia visivyo, wakiamini fikira zao kwamba Bwana angekuja juu ya wingu, wakikataa kuisikia sauti ya Mungu, na hivyo kushindwa kumkaribisha Bwana na kushindwa na maafa? Kila mtu sasa anahisi aliyechanganyikiwa sana kuhusu kwa nini Bwana hajarudi juu ya wingu na kuwanyakua waumini kabla ya majanga. Leo, Nitashiriki ufahamu wangu wa kibinafsi wa kazi ya hukumu ya Mungu mwenye mwili katika siku za mwisho kama Mwana wa Adamu.

Kila mtu anayeifahamu Biblia anaelewa unabii mwingi wa Biblia unatabiri mambo mawili: Bwana atarudi, na Atafanya hukumu katika siku za mwisho. Hata hivyo, mambo haya mawili kwa kweli ni kitu kimoja, ambacho ni kwamba Mungu atakuja katika mwili katika siku za mwisho kufanya kazi Yake ya hukumu. Wengine wana hakika kuuliza ikiwa kuna msingi wa kibiblia wa kusema hivi. Bila shaka upo. Kuna unabii mwingi wa Biblia kuhusu mambo haya—200 au zaidi. Hebu tuangalie mfano mmoja, kama katika Agano la Kale: “Naye atahukumu miongoni mwa mataifa, na atawakemea watu wengi(Isaya 2:4). “Kwa kuwa anafika, kwa kuwa anafika kuihukumu dunia: ataihukumu dunia kwa haki, na watu kwa ukweli wake(Zab 96:13). Pia inasema katika Agano Jipya: “Kwa maana muda umekuja ambao lazima hukumu ianze katika nyumba ya Mungu(1 Petro 4:17). Bwana Yesu pia alitabiri Yeye mwenyewe kwamba Atarudi na afanye kazi ya hukumu katika siku za mwisho. Bwana Yesu alisema, “Iwapo mtu yeyote atayasikia maneno Yangu, na asiyaamini, Mimi sitamhukumu: kwa kuwa mimi sikuja ili niihukumu dunia, bali kuiokoa dunia. Yeye ambaye ananikataa Mimi, na hayakubali maneno Yangu, ana yule ambaye anamhukumu: neno hilo ambalo nimelisema, ndilo hilo ambalo litamhukumu katika siku ya mwisho(Yohana 12:47-48). “Kwa kuwa Baba hamhukumu mwanadamu yeyote, ila amekabidhi hukumu yote kwa Mwana(Yohana 5:22). “Na yeye amempa mamlaka ya kuhukumu pia, kwa kuwa yeye ni Mwana wa Adamu(Yohana 5:27). Ufunuo kinatabiri kwamba: “Akisema kwa sauti kuu, Mwogopeni Mungu, na kumpa utukufu; kwa kuwa saa ya hukumu yake imekuja(Ufunuo 14:7). Unabii huu uko dhahiri kabisa katika kusema kwamba Bwana atarudi kama Mwana wa Adamu na kufanya kazi ya hukumu katika siku za mwisho. Hakuna shaka kuhusu hili. Tunaweza kuona kwamba Bwana Yesu alitabiri waziwazi katika Enzi ya Neema kwamba Angerudi katika siku za mwisho kama Mwana wa Adamu kwa ajili ya kazi Yake ya hukumu. Ufunuo unatabiri waziwazi, “kwa kuwa saa ya hukumu yake imekuja.” Unabii huu unaonyesha kwamba Bwana anapata mwili kama Mwana wa Adamu katika siku za mwisho, akija kibinafsi miongoni mwetu kufanya kazi ya hukumu. Ni dhahiri kwamba hili lilipangwa zamani na Mungu, na hakuna anayeweza kukana hili. Mwenyezi Mungu ameonyesha ukweli kwa ajili ya kazi ya hukumu, Ametamka maneno mengi sana na kufanya kundi la washindi. Hili linaonyesha kwamba unabii huu umetimizwa kabisa. Sasa hebu tuangalie imani ya kawaida ya kidini kwamba Bwana amekamilisha kazi Yake ya ukombozi, kwa hivyo haiwezekani kwamba Atafanya kazi ya hukumu katika siku za mwisho. Je, kuna msingi wowote wa kibiblia kwa hili? Je, Bwana Yesu alisema haya? La hasha. Mawazo kama hayo ni fikira na dhana za binadamu tu—ni ndoto za mchana tu. Yanaenda kinyume kabisa na unabii wa Biblia, na hakuna neno lolote la Mungu linalowaunga mkono. Fikira ya aina hii ni ya kipumbavu kabisa! Kwa nini watu wasitafute maneno na unabii wa Bwana kwa bidii katika Biblia, lakini badala yake wanasisitiza kuihukumu na kuishutumu kazi ya Mungu ya siku za mwisho kwa sababu ya fikira zao wenyewe? Je, hilo si jambo la kiholela na kiburi? Biblia ina unabii mwingi sana kuhusu kuja kwa Mwana wa Adamu na hukumu katika siku za mwisho, hivyo kwa nini watu wasiyaone Maandiko yaliyo mbele ya macho yao? Kama tu vile Biblia inavyosema, “Kwa kusikia mtasikia, na hamtaelewa; na kutazama mtatazama, na hamtaona: Kwani mioyo ya hawa watu imekuwa mizito, na masikio yao hayasikii vizuri, na wameyafunga macho yao; wasije wakati wowote wakaona kwa macho yao, na kusikia kwa masikio yao, na kufahamu kwa mioyo yao, na wabadilishwe, na niwaponye(Mathayo 13:14-15). Wenye hekima wanapaswa kutafuta na kuchunguza kwa nini Mungu anafanya kazi ya hukumu katika siku za mwisho, kwa nini Mwana wa Adamu ndiye anayeonekana kufanya kazi. Tunapaswa kujibu maswali hayo kabla tuweze kuelewa kwa kweli unabii wa Biblia.

Sasa hebu tuchunguze kwa nini Bwana anapata mwili tena kwa ajili ya kazi ya hukumu baada ya kuwakomboa wanadamu. Mwenyezi Mungu tayari amelifunua fumbo hili. Hebu tuone maneno ya Mwenyezi Mungu yanasema nini kuhusu jambo hili. “Hata ingawa Yesu Alifanya kazi nyingi miongoni mwa wanadamu, Yeye Alimaliza tu ukombozi wa wanadamu wote na akawa sadaka ya dhambi ya mwanadamu, na Hakumwondolea mwanadamu tabia yake yote ya upotovu. Kumwokoa mwanadamu kikamilifu kutokana na ushawishi wa Shetani hakukumlazimu Yesu kuchukua dhambi zote za mwanadamu kama sadaka ya dhambi tu, lakini pia kulimlazimu Mungu kufanya kazi kubwa zaidi ili kumwondolea mwanadamu tabia yake kikamilifu, ambayo imepotoshwa na Shetani. Na kwa hivyo, baada ya mwanadamu kusamehewa dhambi zake, Mungu Amerudi katika mwili kumwongoza mwanadamu katika enzi mpya, na kuanza kazi ya kuadibu na hukumu, na kazi hii imemleta mwanadamu katika ulimwengu wa juu zaidi. Wote wanaonyenyekea chini ya utawala Wake watapata kufurahia ukweli wa juu na kupata baraka nyingi mno. Wataishi katika mwanga kwa kweli, na watapata ukweli, njia na uzima(Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Dibaji). “Ingawa mwanadamu amekombolewa na kusamehewa dhambi zake, inachukuliwa kuwa Mungu hakumbuki makosa ya mwanadamu na kutomtendea mwanadamu kulingana na makosa yake. Hata hivyo, mwanadamu anapoishi katika mwili na hajaachiliwa huru kutoka kwa dhambi, ataendelea tu kutenda dhambi, akiendelea kufunua tabia yake potovu ya kishetani. Haya ndiyo maisha ambayo mwanadamu anaishi, mzunguko usiokoma wa dhambi na msamaha. Wengi wa wanadamu wanatenda dhambi mchana kisha wanakiri jioni. Hivi, hata ingawa sadaka ya dhambi ni ya manufaa kwa binadamu milele, haitaweza kumwokoa mwanadamu kutoka kwenye dhambi. Ni nusu tu ya kazi ya wokovu ndiyo imemalizika, kwani mwanadamu bado yuko na tabia potovu. … Sio rahisi kwa mwanadamu kuzifahamu dhambi zake; mwanadamu hawezi kufahamu asili yake iliyokita mizizi. Ni kupitia tu katika hukumu na neno ndipo mabadiliko haya yatatokea. Hapo tu ndipo mwanadamu ataendelea kubadilika kutoka hatua hiyo kuendelea(Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Fumbo la Kupata Mwili (4)). Maneno ya Mwenyezi Mungu ni dhahiri kabisa, sivyo? Bwana Yesu aliwakomboa wanadamu katika Enzi ya Neema, kwa hivyo kwa nini Angerudi kwa ajili ya hukumu katika siku za mwisho? Ni kwa sababu Bwana Yesu alimaliza tu kazi ya ukombozi, akikamilisha tu nusu ya kazi ya Mungu ya wokovu. Hii ilitimiza ukombozi wa dhambi za mwanadamu, kwa hivyo tunastahili mbele ya Bwana kuomba na kushiriki na Yeye, na kufurahia neema na baraka Zake. Dhambi zetu zimesamehewa na tunafurahia amani na furaha inayotolewa na Roho Mtakatifu, lakini bado tunatenda dhambi wakati wote, tumekwama katika mzunguko wa dhambi, kuungama, na kutenda dhambi tena. Hakuna anayeweza kuepuka minyororo na vikwazo vya dhambi, lakini tunaishi tukipambana nayo. Ni chungu na hakuna namna ya kuwa huru. Hili linaonyesha kwamba ingawa Bwana alitusamehe dhambi zetu, asili yetu ya dhambi bado ipo; tabia yetu potovu bado ipo. Tuna uwezekano wa kuasi, kumpinga, na kumhukumu Mungu wakati wowote. Huu ni ukweli usiopingika. Haijalishi mtu amekuwa muumini kwa muda gani, hawezi kuepuka dhambi na kufikia utakatifu au kustahili kumkabili Mungu. Hili linatimiza kikamilifu unabii wa Bwana: “Siye kila mmoja ambaye aliniambia, Bwana, Bwana, ataingia ufalme wa mbinguni, ila yeye atendaye mapenzi ya Baba yangu ambaye yuko mbinguni. Wengi watasema kwangu siku hiyo, Bwana, Bwana, hatujatabiri kupitia jina lako? Na kutoa mapepo kupitia jina lako? Na kutenda miujiza mingi kupitia jina lako? Na hapo ndipo nitasema wazi kwao, Sikuwahi kuwajua: tokeni kwangu, ninyi ambao hutenda udhalimu(Mathayo 7:21-23). Na inasema katika Waebrania 12:14, “Bila utakatifu hakuna mwanadamu atakayemwona Bwana.” Tunaweza kuona hapa kwamba wale tu wanaofanya mapenzi ya Mungu ndio wanaoweza kuingia katika ufalme wa mbinguni. Lakini kwa nini Bwana alisema wale wanaohubiri na kutoa pepo kwa jina lake ni watenda maovu? Hili linaweza kuwa na utata kwa watu wengi. Hii ina maana kwamba wanatangaza imani yao, lakini wanaendelea kutenda dhambi na hawajatubu kikweli. Haijalishi wamehubiri au kutoa pepo katika jina la Bwana kiasi gani, ni miujiza mingapi waliyofanya, hawana kibali cha Bwana. Machoni pa Bwana, watu kama hao ni watenda maovu. Wanaweza kufanya mambo katika jina la Bwana, lakini hili ni dharau kwa Bwana ambalo analichukia. Je, watu hawa ambao dhambi zao zimesamehewa, wanastahili kuingia katika ufalme? La hasha. Bado wanaota kuhusu siku ambayo Bwana atakuja kuwachukua juu mbinguni. Hii ni ndoto ya binadamu. Ni dhahiri kwamba Bwana Yesu kutabiri kurudi Kwake hakukumaanisha Angewachukua watu moja kwa moja hadi angani ili kukutana na Yeye, bali kwamba Angetekeleza hukumu na kuwatakasa watu kutoka katika asili yao ya dhambi na upotovu, kwamba Angetuokoa kikamilifu kutoka dhambini na kutoka kwa nguvu za Shetani, na utupeleke kwenye hatima ya kupendeza. Hii ndiyo maana ya kazi ya hukumu ya Mungu katika siku za mwisho. Sasa nina uhakika sote tunaweza kuona kwamba kazi ya ukombozi katika Enzi ya Neema ilikuwa tu ya kutukomboa kutoka katika dhambi zetu, kwa hivyo dhambi zetu zimesamehewa. Hii ilikamilisha tu nusu ya kazi ya wokovu, na Mungu anafanya hatua kubwa zaidi ya kazi katika siku za mwisho. Juu ya msingi wa kazi ya ukombozi ya Bwana Yesu, Mwenyezi Mungu anaonyesha ukweli kwa ajili ya kazi ya hukumu ya siku za mwisho ili kuwasafisha kikamilifu na kuwaokoa wanadamu kutoka dhambini, ili kutuweka huru kutoka kwa nguvu za Shetani. Hapa tunaweza kuona kwamba ukombozi wa Bwana Yesu ulikuwa unatayarisha njia kabisa kwa ajili ya hukumu ya Mungu katika siku za mwisho. Ilikuwa kazi ya msingi. Na kazi ya Mwenyezi Mungu ya hukumu ndiyo hatua muhimu zaidi katika mpango wa usimamizi wa Mungu wa kuwaokoa binadamu na itahitimisha enzi hiyo. Kuikubali tu kazi ya ukombozi ya Bwana Yesu bila kukubali kazi ya hukumu ya Mwenyezi Mungu ya siku za mwisho kunamaanisha kuiachia katikati katika njia ya imani, na hatua ya mwisho ndiyo muhimu zaidi ambayo itaamua hatima na matokeo yetu. Kutochukua hatua hii kwa kweli ni kukata tamaa na ni kupoteza juhudi zote za awali. Nadhani kwamba kila mtu anaelewa kuwa sehemu ya mwisho ya safari mara nyingi huwa ngumu zaidi. Awamu hii ya mwisho katika njia yako ya imani ndiyo muhimu zaidi ambayo itaamua hatima yako. Kwa waumini, kinachoamua matokeo na hatima yetu ni kazi ya hukumu ya Mungu ya siku za mwisho. Ikiwa watu hawatakubali hili, wataondolewa na Mungu; huo hakina ni msiba. Kwa hivyo tunaweza kuwa na uhakika, haijalishi mtu amekuwa muumini kwa muda gani, ikiwa hatamkubali Mwenyezi Mungu, Mungu atamwondoa, na atakuwa bikira mpumbavu ambaye anaanguka katika janga akilia na kusaga meno yake. Wasioamini wengi waliotangulia wamekubali moja kwa moja kazi ya Mwenyezi Mungu na kupata wokovu wa Mungu wa siku za mwisho. Hawa ndio walio na bahati na wanafidia wale waumini wanaokataa kumkubali Mwenyezi Mungu na kuondolewa. Je, hayo hayatakuwa majuto makubwa zaidi kwa waumini? Baada ya miaka hiyo yote ya kumsubiri Bwana, wanaona Mwenyezi Mungu akifanya kazi ya hukumu na kuonyesha ukweli mwingi sana lakini wanakataa kukubali hilo, badala yake wakimsubiri kwa upumbavu Bwana aje akiwa juu ya wingu, wakiweka dau hili na Mungu. Hatimaye watapoteza nafasi yao ya wokovu. Je, hilo halitakuwa jambo la kuhuzunisha sana kwa muumini?

Wengine wanaweza kuuliza jinsi Mwenyezi Mungu anavyofanya kazi ya hukumu na utakaso ili kuwaokoa wanadamu kikamilifu. Kuna mengi sana ya kushiriki kuhusu ukweli unaohusiana na jambo hili, kwa hivyo leo tunaweza kugusia tu. Mwenyezi Mungu anasema, “Katika siku za mwisho, Kristo anatumia ukweli tofauti kumfunza mwanadamu, kufichua kiini cha mwanadamu, na kuchangua maneno na matendo yake. Maneno haya yanajumuisha ukweli mbalimbali, kama vile wajibu wa mwanadamu, jinsi mwanadamu anavyofaa kumtii Mungu, jinsi mwanadamu anavyopaswa kuwa mwaminifu kwa Mungu, jinsi mwanadamu anavyostahili kuishi kwa kudhihirisha ubinadamu wa kawaida, na pia hekima na tabia ya Mungu, na kadhalika. Maneno haya yote yanalenga nafsi ya mwanadamu na tabia yake potovu. Hasa, maneno hayo yanayofichua vile mwanadamu humkataa Mungu kwa dharau yanazungumzwa kuhusiana na vile mwanadamu alivyo mfano halisi wa Shetani na nguvu ya adui dhidi ya Mungu. Mungu anapofanya kazi Yake ya hukumu, Haiweki wazi asili ya mwanadamu kwa maneno machache tu; Anafunua, kushughulikia na kupogoa kwa muda mrefu. Mbinu hizi za ufunuo, kushughulika, na kupogoa haziwezi kubadilishwa na maneno ya kawaida, ila kwa ukweli ambao mwanadamu hana hata kidogo. Mbinu kama hizi pekee ndizo huchukuliwa kama hukumu; ni kwa kupitia kwa hukumu ya aina hii pekee ndio mwanadamu anaweza kutiishwa na kushawishiwa kabisa kujisalimisha kwa Mungu, na zaidi ya hayo kupata ufahamu kamili wa Mungu(Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Kristo Hufanya Kazi ya Hukumu kwa Ukweli). Maneno ya Mwenyezi Mungu ni dhahiri kabisa kwamba hukumu Yake katika siku za mwisho hasa ni kwa ajili ya kuhukumu asili potovu ya mwanadamu kwa kuonyesha ukweli, kufichua upotovu wetu ili tujitafakari na kujijua wenyewe, na tuone upotovu wetu wenyewe. Kisha tunahisi majuto, kujichukia, na kuichukia miili yetu, na kuishia kufanya toba ya kweli. Kazi hii ya hukumu haifanywi tu kwa kuonyesha ukweli kiasi ili watu waelewe, lakini Mungu anaonyesha vipengele vingi vya ukweli. Ukweli huu wote ni kwa ajili ya kuwahukumu, kuwafichua, kuwapogoa na kuwashughulikia wanadamu, na pia kutujaribu na kutusafisha. Hasa maneno ya Mungu ambayo huhukumu na kufunua kiini potovu cha mwanadamu kwa ukali hufichua tabia za kishetani za binadamu, asili na kiini chetu. Kusoma maneno haya ni jambo la kuhuzunisha sana, na yanaingia moja kwa moja mioyoni mwetu. Tunaona jinsi tulivyo wapotovu sana, kwamba hatustahili kuitwa binadamu. Hatuna pa kujificha, na tunataka kujificha kwenye nyufa za dunia ili kuepuka ghadhabu ya Mungu. Kupitia hukumu hii ndiyo njia pekee ya kuona ukweli wa upotovu wetu wenyewe, kisha tunajawa na majuto na kujua kwamba hatustahili baraka za Mungu za kuchukuliwa hadi katika ufalme Wake. Kwa kuwa wapotovu jinsi hiyo, hatustahili kumwona Mungu. Bila hukumu na kuadibu kwa Mungu, hatungeweza kujijua wenyewe kwa kweli, lakini tungesema tu maneno tusiyomaanisha kuungama dhambi zetu, bila kujua tunaishi kwa kufuata tabia za kishetani kabisa. Tungeendelea kumwasi na kumpinga Mungu, na bado tunadhani tunaweza kuingia mbinguni. Ni jambo la aibu na la kujidanga, ni kutojielewa kabisa. Wale kati yetu tunaopitia hukumu na utakaso wa Mwenyezi Mungu tuna ufahamu wa kweli kwamba maneno Yake ni ukweli, kwamba ni yenye thamani kubwa! Ni ukweli unaoonyeshwa na Mungu ndio unaoweza kutakasa upotovu wetu na kutuokoa kutoka dhambini. Kupitia tu hukumu ya maneno Yake kunaweza kutakasa na kubadilisha tabia zetu potovu, ili tuweze kuwa wale wanaofanya mapenzi ya Mungu, na tunaostahili kuingia katika ufalme. Kazi ya hukumu ya Mwenyezi Mungu ya siku za mwisho ndiyo inayotuletea njia, ukweli na uzima. Ni kupitia katika kazi ya Mwenyezi Mungu ndiyo tunaweza kupata ukweli na uzima na kuishi mbele za Mungu, ambayo ni baraka kuu kutoka kwa Mungu!

Katika hatua hii ya ushirika wetu, Nadhani kwamba wengi wetu tunaelewa kuwa kazi ya Mungu ya kuwaokoa wanadamu si rahisi kama tulivyofikiri. Haiishii tu katika kutukomboa na kuzisamehe dhambi zetu, lakini kazi Yake ya wokovu ni kwa ajili ya kutuokoa kikamilifu kutoka katika uovu na dhambi, kutuokoa kutoka katika mfumbato wa Shetani ili tuweze kumtii Mungu na kumwabudu. Kazi ya hukumu ndiyo njia pekee ya kufanikisha hili. Sasa Mwenyezi Mungu ameonyesha ukweli mwingi sana na Anafanya kazi ya hukumu. Hii kazi Yake ni kubwa kabisa, na isiyo na kifani! Maneno ya Mwenyezi Mungu yameitikisa dunia nzima na kuutikisa ulimwengu. Kila mtu anaiangalia kazi kuu ya Mungu katika siku za mwisho na imeitikisa dunia. Wote wanaopenda ukweli wanaichunguza kazi ya Mungu ya siku za mwisho, na ni wale tu wasiopenda ukweli ndio wanaoipa kisogo na kuipuuza kazi ya Mungu. Lakini kazi ya Mungu haitawahi kuathiriwa na ulimwengu wa kidini au wasioamini. Inasonga mbele bila kuzuiliwa. Kufumba na kufumbua, maafa makubwa yameanza na kazi ya Mungu ya hukumu katika siku za mwisho iko kwenye kilele chake. Kwa wafuasi Wake, ni hukumu inayoanza na nyumba ya Mungu, ikiwakamilisha baadhi yao na kuwaondoa wengi. Kwa wengine, ni kutumia maafa kuwashughulikia watenda maovu wanaompinga Mungu hatua kwa hatua, na kutamatisha enzi hii yenye uovu inayoongozwa na Shetani. Kisha tutaikaribisha na kuingia katika enzi mpya, ambamo ufalme wa Kristo utafanikishwa duniani. Wale ambao bado wanatamani Bwana aje juu ya wingu wataanguka katika maafa, wakilia na kusaga meno yao, wakitimiza unabii wa Ufunuo, “Tazama, anakuja na mawingu; nalo kila jicho litamwona yeye, na pia wale waliomdunga: na makabila yote ya ulimwengu yatalia kwa huzuni kwa sababu ya yeye(Ufunuo 1:7). Mwenyezi Mungu pia alisema, “Watu wengi wanaweza kukosa kujali kuhusu kile Ninachosema, lakini bado Nataka kumwambia kila anayedaiwa kuwa mtakatifu wa Mungu anayemfuata Yesu kwamba, mtakapoona Yesu Akishuka kutoka juu mbinguni juu ya wingu jeupe kwa macho yenu wenyewe, huu ndio utakuwa mwonekano wa umma wa Jua la haki. Pengine huo utakuwa wakati wa furaha kubwa kwako, ilhali lazima ujue kuwa wakati utakaposhuhudia Yesu Akishuka kutoka mbinguni ndio pia wakati ambapo utaenda chini kuzimu kuadhibiwa. Huo ndio utakuwa wakati wa mwisho wa mpango wa Mungu wa usimamizi na ndio utakuwa wakati ambapo Mungu atawatunukia wazuri na kuwaadhibu waovu. Kwani hukumu ya Mungu itakuwa imeisha kabla ya mwanadamu kuona ishara, wakati kuna onyesho la ukweli tu. Wale wanaokubali ukweli na hawatafuti ishara, na hivyo wametakaswa, watakuwa wamerudi mbele za kiti cha enzi cha Mungu na kuingia katika kumbatio la Muumba. Ni wale tu ambao wanashikilia imani kwamba ‘Yesu Asiyeshuka juu ya wingu jeupe ni Kristo wa uongo’ watakabiliwa na adhabu ya milele, kwani wanaamini tu katika Yesu ambaye Anaonyesha ishara, lakini hawamkubali Yesu Anayetangaza hukumu kali na Anatoa njia ya kweli ya uzima. Na hivyo itakuwa tu kuwa Yesu Atawashughulikia tu Atakaporejea wazi wazi juu ya wingu jeupe(Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Kufikia Utakapouona Mwili wa Kiroho wa Yesu, Mungu Atakuwa Ametengeneza Upya Mbingu na Dunia).

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Maudhui Yanayohusiana

Kunyakuliwa ni Nini Hasa?

Miaka 2,000 iliyopita, baada ya Bwana Yesu kusulubishwa na kukamilisha kazi Yake ya ukombozi, Aliahidi kwamba Atarudi. Tangu wakati huo,...

Leave a Reply

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp