Mungu Mmoja wa Kweli Ni Nani?

23/04/2023

Siku hizi, watu wengi wana imani na wanaamini kwamba kuna Mungu. Wanaamini katika Mungu aliye mioyoni mwao. Kwa hivyo baada ya muda, katika sehemu mbalimbali, watu wamepata kuamini miungu wengi sana mbalimbali, mamia au pengine hata maelfu. Je, kunaweza kuwa na miungu wengi hivyo? La, hasha. Basi kuna wangapi, na Mungu wa kweli ni nani? Hakuna mtu maarufu au mashuhuri anayeweza kujibu hili kwa wazi, kwa sababu hakuna mwanadamu anayeweza kumwona Mungu au kuwasiliana na Yeye moja kwa moja. Kila mtu ana maisha mafupi, na yale anayopitia na kushuhudia ni machache mno, hivyo ni nani anayeweza kutoa ushuhuda wa wazi juu ya Mungu? Wale wanaoweza ni wachache na ni mara chache. Tunaijua Biblia kuwa kitabu maarufu sana na chenye mamlaka kinachomshuhudia Mungu. Ina ushuhuda kwamba Mungu aliumba kila kitu, na tangu kumuumba mwanadamu, Hajaacha kamwe kuongoza maisha ya mwanadamu duniani. Alimpa mwanadamu sheria na amri, na pia inatoa ushuhuda wa Mungu katika mwili, kwamba Bwana Yesu alikuja kuwakomboa wanadamu. Inatabiri kurudi kwa Mungu katika siku za mwisho kufanya kazi ya hukumu ili kuwaokoa wanadamu kikamilifu na kumpeleka mwanadamu kwenye hatima nzuri. Kwa hivyo ni wazi kwamba Mungu ambaye Biblia inashuhudia ni Muumba, Mungu mmoja wa kweli. Jambo hili lina msingi imara. Wengine huuliza, “Mungu huyu ambaye Biblia inamshuhudia ni nani hasa? Jina Lake ni nani? Tutamwitaje?” Aliitwa Yehova, kisha baadaye katika mwili Akaitwa Bwana Yesu, na kisha kitabu cha Ufunuo kinatabiri kuja kwa Mwenyezi katika siku za mwisho—Mwenyezi Mungu. Mungu huyu ndiye aliyeumba mbingu, dunia, vitu vyote na wanadamu. Yeye ndiye Mungu mmoja wa kweli ambaye amekuwa Akiwaongoza na kuwaokoa wanadamu siku zote. Yeye ni wa milele, Ana mamlaka juu ya kila kitu, na Hutawala kila kitu. Kwa hivyo yeyote kando na Muumba na Mungu huyu mmoja wa kweli ni mungu wa uongo. Shetani ni mungu wa uongo, na wale malaika waasi waliomfuata, wote wanajifanya kuwa miungu ili kuwadanganya watu. Kwa mfano, Budha, Guanyin, na Mfalme Jade wa dini ya Tao, wote ni miungu wa uongo. Kuna miungu wengine wengi wa uongo, kama wale waliotawazwa na wafalme wa zamani, na hakuna haja ya kuanza kuzungumzia miungu wa dini nyingine. Hivyo kwa nini tunasema kwamba wao ni miungu wa uongo? Kwa sababu hawakuumba kila kitu mbinguni na duniani, au kuwaumba wanadamu. Huu ni ushahidi wenye mantiki zaidi. Wale wote ambao hawana uwezo wa kuumba vitu vyote, na wa kutawala kila kitu, ni miungu wa uongo. Je, unafikiri kuwa mungu wa uongo anaweza kuthubutu kudai kwamba vitu vyote viliumbwa naye? Hapana. Na wanadamu, je? Hawezi kuthubutu. Je, anaweza kuthubutu kudai kuwa anaweza kuwaokoa wanadamu kutoka kwa Shetani? Bila shaka hawezi. Maafa yatakapokuja kwa kweli, ukimwomba mungu wa uongo, ataonekana? Hataweza—atajificha, siyo? Kwa hivyo tunaweza kuona kwamba miungu wa uongo hawawezi kuwaokoa wanadamu, na kuwaamini ni bure. Kuwaamini kutakuwa kujitia kitanzi, na unaweza tu kuishia kutumbukia katika maangamizo. Hii ndiyo sababu, umuhimu wa kupambanua Mungu halisi, Bwana aliyeumba kila kitu ni nani, unasisitizwa mno.

Hebu tuangalie kitabu cha Mwanzo 1:1 kinavyosema, “Hapo mwanzo Mungu aliziumba mbingu na nchi.” Huu ni mstari wa kwanza kabisa katika Biblia. Sentensi hii ina mamlaka na ni ya maana mno. Inaeleza siri ya Mungu kuumba mbingu, dunia, na vitu vyote na wanadamu. Mwanzo pia ni kumbukumbu ya Mungu kuumba nuru na hewa kwa maneno Yake, pamoja na wanyama wote, mimea, na kadhalika, na kumuumba mwanadamu kwa mikono Yake mwenyewe. Mungu aliumba kila kitu, na Yeye huhimili na kustawisha kila kitu. Yeye hutupa kila kitu kwa ajili ya kuishi kwetu. Wanadamu na viumbe vyote huendelea kuishi chini ya sheria zilizowekwa na Mungu. Huu ni uwezo na mamlaka ya kipekee ya Muumba, na ni kitu ambacho hakuna mwanadamu, malaika, au roho mwovu wa Shetani anayeweza kumiliki au kufikia. Tunaweza kusema kwa hakika kwamba Yule pekee Anayeweza kuumba vitu vyote na wanadamu wote ni Muumba, Mungu mmoja wa kweli.

Mungu aliumba vitu vyote na Aliwaumba wanadamu; Yeye hutawala kila kitu. Kwa sasa, Anawaongoza na kuwaokoa wanadamu wote. Hebu tuone kile ambacho Biblia inasema. Hapo mwanzo, Mungu aliwaumba wanadamu, na baada ya Adamu na Hawa kujaribiwa na Shetani, mwanadamu aliishi katika dhambi. Wazawa wa Adamu na Hawa waliongezeka duniani, lakini hawakujua jinsi ya kuishi au kumwabudu Mungu wa kweli. Kulingana na mpango Wake wa usimamizi, Mungu alianza kazi Yake ya Enzi ya Sheria, Akatoa sheria na amri, Akawafundisha wanadamu dhambi ilikuwa nini, walichopaswa kufanya na ambacho hawakupaswa kufanya, hivyo walijua jinsi ya kuishi na jinsi ya kumwabudu Yehova Mungu. Hivi ndivyo Mungu alivyowaongoza wanadamu kwenye njia sahihi ya maisha. Mwishoni mwa Enzi ya Sheria, wanadamu walipotoshwa sana na Shetani hivi kwamba hawakuweza kufuata sheria na walikuwa wakitenda dhambi zaidi na zaidi. Hata hakukuwa na sadaka za dhambi za kutosha za kutoa. Iwapo hilo lingeendelea, wanadamu wote wangehukumiwa na kuuawa chini ya sheria. Ili kuwaokoa wanadamu, Mungu alifanyika mwili kama Bwana Yesu. Yeye binafsi Alisulubishwa kwa ajili ya wanadamu kama sadaka yetu ya dhambi, na Akachukua dhambi za mwanadamu. Baada ya hapo, hakuna mtu aliyehitaji kutoa sadaka za dhambi kwa ajili ya dhambi zake. Ilimradi aliamini, kuungama, na kutubu kwa Bwana, dhambi zake zilisamehewa, na angeweza kuja mbele za Mungu kufurahia kila alichowapa. Bila sadaka ya dhambi ya Bwana Yesu, kila mtu angehukumiwa na kuuawa chini ya sheria, na tusingekuwa hapa leo. Kwa hivyo tunajua kwamba Bwana Yesu ndiye Mkombozi wa wanadamu wote, na kuonekana kwa Mungu mmoja wa kweli. Roho Wake ni Roho wa Yehova Mungu. Yeye ndiye kuonekana kwa Yehova Mungu katika mwili. Kwa kauli ya kawaida zaidi, Yehova Mungu alikuja ulimwenguni kama mwanadamu ili kuwakomboa wanadamu, na Yeye ndiye Mungu wa pekee wa kweli.

Katika Enzi ya Neema, Bwana Yesu alifanya kazi ya ukombozi, na kila mtu aliyemwamini Bwana alisamehewa dhambi zake. Licha ya kufurahia amani na furaha ya msamaha wa dhambi na neema yote ambayo Mungu humpa mwanadamu, wanadamu hawajawahi kuacha kutenda dhambi. Watu huishi katika mzunguko wa kutenda dhambi, kutubu, na kutenda dhambi tena. Hawajafikia utakatifu au kustahili kuingia katika ufalme wa Mungu. Bwana Yesu aliahidi kuja tena katika siku za mwisho ili kumwokoa mwanadamu kikamilifu kutokana na dhambi na kuwatakasa, ili kuwapeleka katika ufalme Wake. Kama Alivyoahidi, sasa Mungu amekuja binafsi duniani katika mwili. Yeye ni Mwenyezi Mungu anayeonyesha ukweli na kufanya kazi Yake ya hukumu ya siku za mwisho. Mwenyezi Mungu ametamka mamilioni ya maneno, Akifichua mafumbo ya mpango wa usimamizi wa miaka 6,000 wa Mungu, na kuwaambia wanadamu yote kuhusu chanzo cha utenda dhambi na upinzani wa mwanadamu dhidi ya Mungu, jinsi Shetani anavyompotosha mwanadamu, jinsi Mungu anavyofanya kazi hatua kwa hatua ili kumwokoa mwanadamu, jinsi ya kutenda imani ili kutakaswa na kuingia katika ufalme Wake, jinsi ya kupata utiifu na upendo kwa Mungu, pamoja na matokeo na hatima ya mwisho ya watu wa kila aina. Kuna mambo ya aina nyingi sana katika ukweli uliotamkwa na Mwenyezi Mungu—hakuna kitu kinachokosa. Tunapoona ni ukweli kiasi gani ambao Mwenyezi Mungu ameonyesha, tunaweza kuthibitisha kwamba Yeye ndiye Bwana Yesu aliyerudi, kwa sababu Bwana alitabiri, “Wakati Yeye, Roho wa ukweli, atakapokuja, Atawaongoza hadi kwenye ukweli wote(Yohana 16:13). Je, Mwenyezi Mungu kufichua ukweli hakutimizi unabii wa Bwana Yesu? Je, hili halithibitishi kwamba Yeye ni Roho wa Bwana Yesu aliyerudi kufanya kazi katika mwili? Na kwa hivyo, Mwenyezi Mungu na Bwana Yesu ni wa Roho mmoja, na Mwenyezi Mungu ndiye Mwokozi aliyekuja duniani kuwaokoa wanadamu kikamilifu. Ni Mungu Mwenyewe pekee anayeweza kuonyesha ukweli. Kando na Mungu, hakuna mwanadamu awezaye kufanya hivi. Katika historia nzima ya wanadamu, hakuna mwanadamu ambaye ameweza kuonyesha ukweli. Mambo yaliyosemwa na watu hao wote maarufu na mashuhuri, na hao ibilisi na pepo wote waovu wanaojifanya kuwa miungu ni dhana yenye makosa na uongo wa kupotosha, na hayana hata neno moja la ukweli. Ni Mungu Mwenyewe pekee anayeweza kuonyesha ukweli na kuwaokoa wanadamu. Hapana shaka kuhusu hilo.

Mungu aliumba mbingu, dunia, vitu vyote, na Akawaumba wanadamu. Amekuwa akizungumza na kufanya kazi ili kuwaongoza na kuwaokoa wanadamu wakati huu wote. Tunaweza kusema kwa hakika kwamba Muumba pekee anayeweza kuumba mbingu, dunia, na vitu vyote, na kuwa na mamlaka juu ya hatima ya wanadamu ndiye Mungu mmoja wa kweli. Mungu alimuumba mwanadamu, na ni Mungu pekee anayejishughulisha na hatima na maendeleo ya mwanadamu. Tangu kumaliza kazi ya kuumba ulimwengu, Mungu amekuwa Akiwalenga wanadamu, Akituchunga na kutupa kila kitu tunachohitaji, na kutupa mengi hata zaidi. Hakutuacha wala kutupuuza baada ya kutuumba. Binadamu alipoanza kuishi rasmi duniani, Mungu alianza kazi Yake ya Enzi ya Sheria, Akitoa amri za kuyaongoza maisha ya mwanadamu duniani. Mwanadamu alipopotoshwa sana na Shetani kiasi cha kutoweza kufuata sheria, kila mtu alikuwa akikabiliwa na hukumu chini ya sheria na alikuwa katika hali ya kutoweza kurejeshwa nyuma tena, kwa hivyo Mungu alifanyika mwili kama Bwana Yesu na akakamilisha kazi ya ukombozi ili kuwasamehe wanadamu dhambi zao, na kuwaruhusu kufurahia neema na baraka zinazotolewa na Mungu. Enzi hiyo ilipoisha, Mungu alipata mwili tena, wakati huu akiwa Mwenyezi Mungu, kwa ajili ya kufanya kazi ya hukumu katika siku za mwisho ili kuwaokoa wanadamu kikamilifu kutoka dhambini na kutoka kwa nguvu za Shetani, na kuwaongoza wanadamu hadi kwenye hatima nzuri. Ingawa kila enzi ya kazi ya Mungu ina jina tofauti na Amekamilisha kazi tofauti, yote hufanywa na Mungu mmoja. Yeye ana Roho mmoja tu, na Yeye ndiye Mungu mmoja wa kweli. Hili ni dhahiri. Kama Mwenyezi Mungu asemavyo, “Kazi mzima ya mpangilio wa usimamizi wa Mungu inafanywa binafsi na Mungu mwenyewe. Awamu ya kwanza—uumbaji wa ulimwengu—ilifanywa binafsi na Mungu Mwenyewe, na kama haikuwa hivyo, basi hakuna yeyote ambaye angekuwa na uwezo wa kumuumba mwanadamu; awamu ya pili ilikuwa ukombozi wa wanadamu wote, na pia ilifanywa binafsi na Mungu Mwenyewe, awamu ya tatu inaenda bila kusemwa: Kuna haja kuu zaidi ya mwisho wa kazi ya Mungu kufanywa na Mungu Mwenyewe. Kazi ya ukombozi, ushindi, kumpata, na kumkamilisha wanadamu wote inafanywa binafsi na Mungu Mwenyewe. Kama hangefanya kazi hii Yeye binafsi, basi utambulisho wake hauwezi kuwakilishwa na mwanadamu, au kazi kufanywa na mwanadamu. Ili kumshinda Shetani, ili kumpata mwanadamu, na ili kumpa mwanadamu maisha ya kawaida duniani, Yeye binafsi humwongoza mwanadamu na hufanya kazi binafsi miongoni mwa wanadamu; kwa ajili ya mpangilio mzima wa usimamizi, na kwa kazi yake yote, ni lazima Yeye binafsi afanye kazi hii(Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Kurejesha Maisha ya Kawaida ya Mwanadamu na Kumpeleka Kwenye Hatima ya Ajabu). “Hatua tatu za kazi ambazo zilifanywa tangu mwanzo hadi leo zote zilitekelezwa na Mungu Mwenyewe, na zilitekelezwa na Mungu mmoja. Ukweli wa hatua tatu za kazi ni ukweli wa uongozi wa Mungu kwa wanadamu wote, ukweli ambao hakuna anayeweza kuupinga. Mwishoni mwa hatua tatu za kazi, vitu vyote vitaainishwa kulingana na aina na kurejea chini ya utawala wa Mungu, kwa kuwa duniani kote kuna Mungu mmoja tu, na hakuna dini nyingine. Yule asiyeweza kuiumba dunia hataweza kuiangamiza, ilhali Yule aliyeumba dunia hakika ataiangamiza, na kwa hivyo, kama mtu hana uwezo wa kutamatisha enzi na ni wa kumsaidia mwanadamu kukuza akili zake tu, basi hakika hatakuwa Mungu, na hakika hatakuwa Bwana wa mwanadamu. Hataweza kufanya kazi kuu kama hii; kuna mmoja tu anayeweza kufanya kazi kama hii, na wote wasioweza kufanya hii kazi hakika ni adui wala si Mungu. Dini zote ovu hazilingani na Mungu, na kwa sababu hawalingani na Mungu, wao ni adui za Mungu. Kazi yote inafanywa na huyu Mungu mmoja wa kweli, na ulimwengu mzima unatawaliwa na huyu Mungu mmoja. Bila kujali kama Anafanya kazi Uchina ama Israeli, bila kujali kama kazi inafanywa na Roho ama mwili, yote hufanywa na Mungu Mwenyewe, na haiwezi kufanywa na mwingine yeyote. Ni kabisa kwa sababu Yeye ni Mungu wa wanadamu wote ndiyo kwamba Yeye hufanya kazi kwa njia ya uhuru, pasipo kuwekewa masharti yoyote—na haya ndiyo maono makuu zaidi(Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Kujua Hatua Tatu za Kazi ya Mungu Ndiyo Njia ya Kumjua Mungu). Tunaweza kuona kutoka katika maneno ya Mungu kwamba kuna Mungu mmoja tu, Muumba mmoja tu, ni Mungu Mwenyewe pekee anayeweza kuumba vitu vyote, kuathiri majaliwa yote ya wanadamu, kuongoza maisha ya mwanadamu duniani, kumwokoa mwanadamu, na kumwongoza mwanadamu kuingia katika hatima nzuri. Kama kitabu cha Ufunuo kinavyosema, “Mimi ndiye Alfa na Omega, Mwanzo na tena mwisho, wa awali na wa mwisho(Ufunuo 22:13). Miungu wa uongo hawawezi kuumba vitu vyote, sembuse kuwaokoa wanadamu au kutamatisha enzi. Mungu wa uongo kamwe hawezi kufanya kazi ambayo Mungu wa kweli hufanya. Mungu wa uongo anaweza tu kuonyesha miujiza kadhaa, au kueneza uzushi na uongo ili kuwapotosha na kuwaongoza watu kutenda mabaya. Anaweza kuwapa watu ufadhili kidogo ili kuwavuta, na kuwafanya watu wawafukizie uvumba na kuwaabudu kama Mungu. Lakini miungu wa uongo hawawezi kusamehe dhambi au kuonyesha ukweli ili kutakasa upotovu wa watu. Hawawezi kuwaokoa wanadamu kutoka kwa nguvu za Shetani. Miungu wa uongo kuthubutu kumwiga Mungu wa kweli kunaonyesha kuwa wao ni waovu na hawana aibu hata kidogo, na mwishowe watafungwa na kutupwa na Mungu katika shimo lisilo na mwisho—wataadhibiwa. Wote wanaokwenda kinyume na Mungu wataondolewa kabisa na Yeye mwishoni.

Kwa hivyo, ili kumtafuta Mungu wa kweli, ni lazima umtafute Yule aliyeumba vitu vyote, Anayetawala vitu vyote, Yule anayeweza kuonyesha ukweli na kufanya kazi ya kuwaokoa wanadamu. Jambo hili ni muhimu. Unaweza tu kukombolewa kutoka dhambini, kupokea wokovu wa Mungu, na kuingia katika hatima nzuri kwa kumwamini na kumwabudu huyu Mungu mmoja wa kweli, kukubali ukweli Anaouonyesha, na kupata ukweli kama maisha yako. Iwapo humjui Mungu wa kweli ni nani, unahitaji kutafuta na kuchunguza. Hatuwezi kudhania miungu wa uongo kuwa Mungu wa kweli kwa sababu tu wanaonyesha miujiza fulani au kuponya magonjwa fulani. Huu utakuwa mwiko, kwa sababu wao si Mungu wa kweli. Kuabudu mungu wa uongo ni kufuru, ni kwenda kinyume na Mungu na ni sawa na kumsaliti Mungu wa kweli. Tabia ya Mungu haitavumilia kosa la binadamu, kwa hivyo wote wanaomwamini mungu wa uongo watahukumiwa kwenda motoni na kuangamizwa na Mungu. Mwenyezi Mungu anasema, “Ulimwengu wa kitambo ukiendelea kuwepo, Nitavurumisha hasira Yangu kwa mataifa yake, Nikieneza amri Zangu za utawala katika ulimwengu mzima, na kuleta kuadibu kwa yeyote anayezikiuka: Ninapougeuza uso Wangu kwa ulimwengu kuzungumza, binadamu wote wanasikia sauti Yangu, na hapo kuona kazi yote ambayo Nimefanya katika ulimwengu. Wale wanaoenda kinyume na mapenzi Yangu, hivyo ni kusema, wanaonipinga kwa matendo ya mwanadamu, watapitia kuadibu Kwangu. Nitachukua nyota nyingi mbinguni na kuzitengeneza upya, na kwa mujibu Wangu jua na mwezi vitafanywa upya—anga hazitakuwa tena jinsi zilivyokuwa hapo awali; vitu visivyohesabika duniani vitafanywa kuwa vipya. Yote yatakuwa kamili kupitia maneno Yangu. Mataifa mengi katika ulimwengu yatagawanishwa upya na kubadilishwa kuwa taifa Langu, ili kwamba mataifa yote yaliyomo duniani yatatoweka milele na kuwa taifa linaloniabudu Mimi; mataifa yote ya dunia yataangamizwa, na hayatakuwepo tena. Kati ya binadamu walio ulimwenguni, wale wote walio wa Shetani wataangamizwa; wale wote wanaomwabudu Shetani watalazwa chini na moto Wangu unaochoma—yaani, isipokuwa wale walio ndani ya mkondo, waliobaki watabadilishwa kuwa jivu. Nitakapoadibu watu wengi, wale walio katika dunia ya kidini, kwa kiasi tofauti, watarudi kwa ufalme Wangu, wakiwa wameshindwa na kazi Yangu, kwani watakuwa wameona kufika kwa Aliye Mtakatifu akiwa amebebwa juu ya wingu jeupe. Wanadamu wote watafuata aina yao, na watapokea kuadibu kunakotofautiana kulingana na kile walichofanya. Wale ambao wamesimama kinyume na Mimi wataangamia; na kwa wale ambao matendo yao duniani hayakunihusisha, kwa sababu ya vile wamejiweka huru wenyewe, wataendelea kuwa duniani chini ya uongozi wa wana Wangu na watu Wangu. Nitajionyesha kwa mataifa mengi yasiyohesabika, Nikipaza sauti Yangu kote duniani Nikitangaza kukamilika kwa kazi Yangu kuu ili wanadamu wote waone kwa macho yao(Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Maneno ya Mungu kwa Ulimwengu Mzima, Sura ya 26).

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Maudhui Yanayohusiana

Kupata Mwili Ni Nini?

Sote tunajua kwamba miaka elfu mbili iliyopita, Mungu alikuja mwilini katika ulimwengu wa mwanadamu kama Bwana Yesu ili kuwakomboa...

Je, Umesikia Sauti ya Mungu?

Hamjambo ndugu. Tumebahatika sana kukusanyika pamoja—mshukuruni Bwana! Sisi sote ni watu tunaopenda kusikiliza maneno ya Mungu na...

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp