Mwokozi Anawaokoaje Wanadamu Anapokuja?

01/05/2023

Tunapozungumza kuhusu Mwokozi, waumini wote wanakubali kwamba katika siku za mwisho, hapana budi kwamba Atakuja duniani kuwaokoa wanadamu. Manabii wengi wamesema Mwokozi atakuja katika siku za mwisho. Hivyo Mwokozi ni nani? Madhehebu mbalimbali yana tafsiri tofauti, na dini tofauti husema mambo tofauti kumhusu. Mwokozi wa kweli ni nani? Mwokozi wa kweli ni Bwana aliyeumba mbingu na dunia na vitu vyote, na ndiye Mungu mmoja wa kweli, Muumba. Ni Bwana pekee aliyeumba kila kitu ndiye Mungu mmoja wa kweli, na ni Mungu pekee wa kweli katika mwili ndiye Mwokozi anayeweza kuwaokoa wanadamu. Ikiwa si Mungu wa kweli aliyeumba vitu vyote, basi mtu huyu si Muumba na hawezi kuwaokoa wanadamu. Hili ni jambo tunalopaswa kujua kwa dhahiri. Kumbuka! Kuna Mungu mmoja tu wa kweli, na ni Mungu mwenye mwili pekee ndiye Mwokozi. Ni Mungu wa kweli katika mwili pekee anayeweza kuonyesha ukweli na kuwaokoa wanadamu kikamilifu, na kutupeleka kwenye hatima nzuri. Kuna miungu wengi wa uongo, kwa hivyo hakuna haja ya kuwaorodhesha wote, lakini kuna Mwokozi mmoja tu wa kweli. Hivyo basi, huyu Mwokozi ni nani hasa? Miaka 2,000 iliyopita, Bwana Yesu alikuja na kusema, “Tubuni: kwa kuwa ufalme wa mbinguni u karibu(Mathayo 4:17). Kisha alisulubishwa ili kufidia dhambi za mwanadamu. Alikamilisha kazi ya ukombozi na kuanzisha Enzi ya Neema, Akawaruhusu watu kuja mbele za Mungu, kuomba, kuwasiliana na Mungu, na kumfuata Mungu hadi sasa. Hii ilikuwa kazi ya Bwana Yesu ya ukombozi. Bwana Yesu alikuwa Mwokozi, Aliyekuja miongoni mwa wanadamu na kufanya kazi. Kulingana na kile ambacho tumeona hadi sasa, Mwokozi ni nani? Ni Mungu katika mwili ambaye huja binafsi kuwaokoa wanadamu. Bwana Yesu alifanya kazi ya ukombozi, kusamehe dhambi za watu, lakini watu bado hutenda dhambi daima na hawawezi kufikia toba ya kweli. Wokovu wa Mungu ni wa kuwafanya watu watubu kwa kweli, sio tu kusamehe dhambi zetu na kukomea hapo. Ndiyo maana Bwana Yesu aliahidi kwamba atarudi katika siku za mwisho, kuwaokoa wanadamu kikamilifu. Mwokozi sasa amerudi na Yumo miongoni mwetu. Ameonyesha ukweli ili kumtakasa mwanadamu na kutuokoa kutokana na dhambi, ili tuweze kumgeukia Mungu kikamilifu na kupatwa na Yeye, kisha kuingia katika hatima nzuri Aliyotutayarishia—ufalme Wake. Sasa kuna watu duniani kote ambao wamesikia sauti ya Mungu na wameinuliwa mbele ya kiti Chake cha enzi. Wanahukumiwa na kutakaswa na Mungu na wana ushuhuda wa kupendeza. Ni washindi waliokamilishwa na Mungu. Cha kusikitisha ni kwamba, bado kuna watu wengi ambao hawajasikia sauti ya Mungu, ambao hawajaona kuonekana na kazi ya Mungu. Ndiyo maana tunatoa ushuhuda sasa hivi wa jinsi Mwokozi anavyowaokoa wanadamu.

Tunapozungumzia wokovu, watu wengine wana wazo hili lisilo dhahiri kwamba Mungu atashuka ghafla kutoka angani na kuwachukua waumini moja kwa moja, wakikwepa maafa na kwenda mbinguni. Hii ni fikira na njozi ya binadamu, lakini si halisi. Kuna tatizo lingine muhimu. Watu wote wamepotoshwa sana na Shetani na wana asili ya kishetani. Watu wote wanaishi katika dhambi, na wamejawa na uchafu na upotovu. Je, tunaweza kweli kunyakuliwa moja kwa moja? Je, tunastahili ufalme wa mbinguni? Watu wote wakimngoja Mwokozi ashuke, wakiwa wameshikilia wazo hili, bila shaka wataambulia patupu. Watatumbukia katika maafa, wakilia na kusaga meno. Basi, Mwokozi anawaokoa vipi wanadamu Anapokuja? Kwanza, Anatuokoa kutokana na dhambi. Bwana Yesu alifanya tu kazi ya ukombozi ili dhambi zetu zisamehewe, lakini licha ya msamaha huo, bado hatuwezi kujizuia kuendelea kutenda dhambi. Hatujaepuka minyororo ya dhambi. Huu ni ukweli usiopingika. Mungu ni mtakatifu na mwenye haki. Yeye hutokea mahali patakatifu na kujifichia nchi chafu. Kwa kuwa watu si watakatifu, hawawezi kumwona Bwana, kwa hivyo tunawezaje kustahili kuingia katika ufalme wa Mungu, iwapo tunaishi katika dhambi? Ndiyo maana Mungu amekuwa mwili tena katika siku za mwisho na Anaonyesha ukweli, na kufanya kazi ya hukumu na kuadibu ili kuwatakasa watu kikamilifu na kutuokoa kutokana na dhambi, na kutoka kwa Shetani. Ni kama tu Mwenyezi Mungu anavyosema: “Hata ingawa Yesu Alifanya kazi nyingi miongoni mwa wanadamu, Yeye Alimaliza tu ukombozi wa wanadamu wote na akawa sadaka ya dhambi ya mwanadamu, na Hakumwondolea mwanadamu tabia yake yote ya upotovu. Kumwokoa mwanadamu kikamilifu kutokana na ushawishi wa Shetani hakukumlazimu Yesu kuchukua dhambi zote za mwanadamu kama sadaka ya dhambi tu, lakini pia kulimlazimu Mungu kufanya kazi kubwa zaidi ili kumwondolea mwanadamu tabia yake kikamilifu, ambayo imepotoshwa na Shetani. Na kwa hivyo, baada ya mwanadamu kusamehewa dhambi zake, Mungu Amerudi katika mwili kumwongoza mwanadamu katika enzi mpya, na kuanza kazi ya kuadibu na hukumu, na kazi hii imemleta mwanadamu katika ulimwengu wa juu zaidi. Wote wanaonyenyekea chini ya utawala Wake watapata kufurahia ukweli wa juu na kupata baraka nyingi mno. Wataishi katika mwanga kwa kweli, na watapata ukweli, njia na uzima(Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Dibaji).

Mwokozi tayari amekuja. Bwana Yesu amerudi katika mwili kama Mwenyezi Mungu mwenye mwili. Mwenyezi Mungu ameonyesha ukweli wote unaowatakasa na kuwaokoa wanadamu, na kufanya kazi ya hukumu Akianza na nyumba ya Mungu. Hakuna mwingine isipokuwa Mungu katika mwili anayeweza kuonyesha ukweli na kuwaokoa wanadamu, bila kujali jinsi mtu alivyo mashuhuri au maarufu. Mungu mwenye mwili anayekuja duniani pekee ndiye Kristo, ndiye Mwokozi wetu. Je, “Kristo” ina maana gani? Inamaanisha Mwokozi. Hivyo basi, Mwenyezi Mungu, Kristo wa siku za mwisho, Anafanyaje kazi ya hukumu ili kuwatakasa na kuwaokoa wanadamu?

Mwenyezi Mungu anatuambia: “Katika siku za mwisho, Kristo anatumia ukweli tofauti kumfunza mwanadamu, kufichua kiini cha mwanadamu, na kuchangua maneno na matendo yake. Maneno haya yanajumuisha ukweli mbalimbali, kama vile wajibu wa mwanadamu, jinsi mwanadamu anavyofaa kumtii Mungu, jinsi mwanadamu anavyopaswa kuwa mwaminifu kwa Mungu, jinsi mwanadamu anavyostahili kuishi kwa kudhihirisha ubinadamu wa kawaida, na pia hekima na tabia ya Mungu, na kadhalika. Maneno haya yote yanalenga nafsi ya mwanadamu na tabia yake potovu. Hasa, maneno hayo yanayofichua vile mwanadamu humkataa Mungu kwa dharau yanazungumzwa kuhusiana na vile mwanadamu alivyo mfano halisi wa Shetani na nguvu ya adui dhidi ya Mungu. Mungu anapofanya kazi Yake ya hukumu, Haiweki wazi asili ya mwanadamu kwa maneno machache tu; Anafunua, kushughulikia na kupogoa kwa muda mrefu. Mbinu hizi za ufunuo, kushughulika, na kupogoa haziwezi kubadilishwa na maneno ya kawaida, ila kwa ukweli ambao mwanadamu hana hata kidogo. Mbinu kama hizi pekee ndizo huchukuliwa kama hukumu; ni kwa kupitia kwa hukumu ya aina hii pekee ndio mwanadamu anaweza kutiishwa na kushawishiwa kabisa kujisalimisha kwa Mungu, na zaidi ya hayo kupata ufahamu kamili wa Mungu. Kile ambacho kazi ya hukumu humletea mwanadamu ni ufahamu wa uso halisi wa Mungu na ukweli kuhusu uasi wake mwenyewe. Kazi ya hukumu humruhusu mwanadamu kupata ufahamu zaidi wa mapenzi ya Mungu, wa makusudi ya kazi ya Mungu, na wa mafumbo yasiyoweza kueleweka kwa mwanadamu. Pia inamruhusu mwanadamu kutambua na kujua asili yake potovu na asili ya upotovu wake, na pia kugundua ubaya wa mwanadamu. Matokeo haya yote huletwa na kazi ya hukumu, kwa maana asili ya kazi ya aina hii hasa ni kazi ya kuweka wazi ukweli, njia, na uhai wa Mungu kwa wale wote walio na imani ndani Mwake. Kazi hii ni kazi ya hukumu inayofanywa na Mungu(Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Kristo Hufanya Kazi ya Hukumu kwa Ukweli).

Katika siku za mwisho, Mungu anaokoa binadamu kwa kuonyesha ukweli ili kufichua asili yetu ya dhambi, ili tuweze kuona chanzo cha utenda dhambi wetu na ukweli wa kupotoshwa kwetu na Shetani. Mara mtu anapotambua hili, anaweza kuwa na majuto ya kweli, na kujidharau na kujichukia. Kisha ataweza kuanza kutubu kwa kweli, na kutamani tu kuelewa na kupata ukweli. Atakapoweza kutenda ukweli, atakuwa amejifunza jinsi ya kumtii Mungu. Ataelewa ukweli na kuishi kulingana na maneno ya Mungu na ukweli, hivyo tabia ya maisha yake itaanza kubadilika. Kwa kupitia hukumu ya maneno ya Mungu kila mara, hatimaye tabia yake potovu itatakaswa. Huyu ni mtu ambaye ameokolewa kikamilifu na kisha ataweza kuingia katika hatima nzuri ambayo Mungu amemtayarishia mwanadamu. Hii ndiyo sababu lazima tukubali hukumu na kuadibu kwa maneno ya Mwenyezi Mungu. Ni lazima tutubu kwa kweli, tubadilike kwa kweli, na kuwa watu wanaomtii na kumwabudu Mungu. Huu pekee ndio wokovu wa kweli, na huu pekee ndio utatufanya tustahili kuingia katika ufalme Wake.

Sasa kuna jambo moja ambalo ni dhahiri kwetu. Ni Mungu pekee, Muumba pekee anayeweza kuwaokoa wanadamu na kutuleta kwenye hatima hiyo nzuri. Mungu huyu, Muumba huyu amekuwa akizungumza na kufanya kazi ili kuwaongoza na kuwaokoa wanadamu wakati huu wote, hadi leo. Biblia nzima ni ushuhuda wa kuonekana kwa Mungu na kazi Yake. Inatoa ushuhuda kwamba mbingu na dunia, vitu vyote, viliumbwa na Mungu, na hutoa ushuhuda wa kuonekana kwa Muumba na kazi Yake. Huyu Mungu mmoja pekee wa kweli mwenye mwili anayekuja miongoni mwetu ndiye Mwokozi. Ni Yeye pekee Anayeweza kuwaokoa wanadamu. Mwokozi huyu lazima awe Mungu katika mwili na lazima Aonyeshe ukweli. Huyu pekee ndiye Mwokozi wa kweli. Yeyote anayedaiwa kuwa Mwokozi ambaye hawezi kuonyesha ukweli ni roho mbaya anayewadanganya watu. Kuna miungu wengi wa uongo, kama watu mashuhuri ambao husifiwa mno na kisha kutawazwa kuwa miungu na wafalme wakuu baada ya kufa kwao. Je, hii inaweza kuthibitishwa inapojaribiwa? Watu hao ni wanadamu wapotovu tu ambao huenda motoni wanapokufa, basi wanaweza kumwokoa nani? Hawawezi hata kujiokoa wenyewe, na Mungu huwaadhibu kwa ajili ya dhambi zao. Kwa hivyo wanaweza kuokoa binadamu? Wafalme hao wote walikufa zamani na wote wako motoni sasa. Miungu wa uongo waliowatawaza hakika hawawezi kuwaokoa wanadamu. Kwa vyovyote vile, usimwamini mungu wa uongo. Huo ni upumbavu na ujinga, na hakika utakuletea maangamizi. Kumbuka kwamba Mwokozi hana budi kuwa Mungu mwenye mwili, kwamba lazima Aonyeshe ukweli. Hili linaweza tu kutoka kwa Mungu. Mtu yeyote anayedaiwa kuwa Mwokozi ambaye hawezi kuonyesha ukweli ni wa uongo na anawapotosha watu. Yeyote ambaye si Mungu katika mwili lakini anadai kuwa Mungu ni Kristo wa uongo na roho mwovu. Watu hao si wakombozi na hawawezi kuwaokoa wanadamu. Shetani na pepo wote waovu hujifanya kuwa Mungu, lakini bado hawathubutu kudai kuwa Muumba wa vitu vyote, na hawathubutu hasa kudai walimuumba mwanadamu. Pia hawathubutu kudai kwamba wanaweza kuongoza hatima ya mwanadamu. Wao huonyesha tu ishara na miujiza fulani hapa na pale ili kuwapotosha watu, kupata utii wao. Miungu hawa wa uongo na pepo waovu wote ni mashetani, ibilisi wanaopotosha na kuwashawishi watu kutenda mabaya. Wao ni maadui wa Muumba, Mungu mmoja wa kweli, na wanajaribu kuwapokonywa wanadamu kutoka Kwake. Hii ndiyo sababu hawa mashetani na ibilisi waovu wote ni maadui wa Mungu wenye chuki, ndiyo sababu wanachukiwa na kulaaniwa naye. Wote wanaoheshimu na kuabudu mashetani na pepo waovu watahukumiwa kwenda motoni na kuangamizwa na Mungu. Mwenyezi Mungu anasema, “Ulimwengu wa kitambo ukiendelea kuwepo, Nitavurumisha hasira Yangu kwa mataifa yake, Nikieneza amri Zangu za utawala katika ulimwengu mzima, na kuleta kuadibu kwa yeyote anayezikiuka: Ninapougeuza uso Wangu kwa ulimwengu kuzungumza, binadamu wote wanasikia sauti Yangu, na hapo kuona kazi yote ambayo Nimefanya katika ulimwengu. Wale wanaoenda kinyume na mapenzi Yangu, hivyo ni kusema, wanaonipinga kwa matendo ya mwanadamu, watapitia kuadibu Kwangu. Nitachukua nyota nyingi mbinguni na kuzitengeneza upya, na kwa mujibu Wangu jua na mwezi vitafanywa upya—anga hazitakuwa tena jinsi zilivyokuwa hapo awali; vitu visivyohesabika duniani vitafanywa kuwa vipya. Yote yatakuwa kamili kupitia maneno Yangu. Mataifa mengi katika ulimwengu yatagawanishwa upya na kubadilishwa kuwa taifa Langu, ili kwamba mataifa yote yaliyomo duniani yatatoweka milele na kuwa taifa linaloniabudu Mimi; mataifa yote ya dunia yataangamizwa, na hayatakuwepo tena. Kati ya binadamu walio ulimwenguni, wale wote walio wa Shetani wataangamizwa; wale wote wanaomwabudu Shetani watalazwa chini na moto Wangu unaochoma—yaani, isipokuwa wale walio ndani ya mkondo, waliobaki watabadilishwa kuwa jivu. Nitakapoadibu watu wengi, wale walio katika dunia ya kidini, kwa kiasi tofauti, watarudi kwa ufalme Wangu, wakiwa wameshindwa na kazi Yangu, kwani watakuwa wameona kufika kwa Aliye Mtakatifu akiwa amebebwa juu ya wingu jeupe. Wanadamu wote watafuata aina yao, na watapokea kuadibu kunakotofautiana kulingana na kile walichofanya. Wale ambao wamesimama kinyume na Mimi wataangamia; na kwa wale ambao matendo yao duniani hayakunihusisha, kwa sababu ya vile wamejiweka huru wenyewe, wataendelea kuwa duniani chini ya uongozi wa wana Wangu na watu Wangu. Nitajionyesha kwa mataifa mengi yasiyohesabika, Nikipaza sauti Yangu kote duniani Nikitangaza kukamilika kwa kazi Yangu kuu ili wanadamu wote waone kwa macho yao(Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Maneno ya Mungu kwa Ulimwengu Mzima, Sura ya 26).

Inayofuata: Kupata Mwili Ni Nini?

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Maudhui Yanayohusiana

Leave a Reply

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp