Unasema kwamba Bwana Yesu amerudi, kwa nini hatujamwona? Kuona ni kuamini. Kama hatujamwona, basi hilo lazima limaanishe kuwa Yeye hajarudi bado; nitaamini hilo nitakapomwona. Unasema kwamba Bwana Yesu amerudi, kwa hiyo Yuko wapi sasa? Anafanya kazi gani? Bwana Amesema maneno gani? Nitaliamini ukishuhudia kwa dhahiri mambo haya.

07/06/2019

Jibu:

Kuonekana kwa Mungu na kazi katika siku za mwisho ni kama tu Bwana Yesu alivyotabiri. Kuna sehemu mbili—kuwasili Kwake kwa siri na kuwasili Kwake hadharani. Kuwasili kwa siri kunamaanisha Mungu kupata mwili miongoni mwa wanadamu kama Mwana wa Adamu ili kutamka maneno Yake, na kufanya kazi Yake ya siku za mwisho. Huku ni kuwasili Kwake kwa siri. Kuwasili hadharani ni Bwana kuja kwa wazi na mawingu, yaani, Bwana kuwasili na watakatifu wengi sana, akionekana kwa mataifa yote na watu wote. Tunaposhuhudia kazi ya Mungu ya siku za mwisho kwa sasa, watu wengi wana mashaka: “Mnasema kwamba Mungu ameonekana na anafanya kazi. Kwa nini hatujamwona? Mungu anasema maneno Yake lini na vipi? Je, kuna mtu ambaye amerekodi maneno ya Mungu anapoyasema, au Analeta maneno hayo moja kwa moja kwetu? Kwa nini Mungu anazungumza miongoni mwa ninyi wote? Kwa nini hatusikii sauti Yake au kumwona?” … Mungu ameonekana Uchina, Mashariki; Anaonyesha sauti Yake na kufanya kazi katika mfano wa Mwana wa Adamu mwenye mwili. Hakuna chochote cha mwujiza kabisa. Mungu anavaa mwili wa kawaida, sura Yake ni ile ya mtu wa kawaida, na Anazungumza na kufanya kazi miongoni mwetu. Hakuna kitu cha mwujiza. Watu wengine wanasema: “Ikiwa hiki si cha mwujiza hata kidogo, basi Yeye ni Mungu au la? Ikiwa Mungu anaonekana na kufanya kazi, basi kuonekana na kazi Yake yanapaswa kuwa ya mwujiza.” Hebu nikuulize, je, Bwana Yesu alikuwa wa mwujiza Alipofanya kazi? Alipokuwa akizungumza na Petro, je, watu katika mahali pengine wangeweza kuona hilo? Alipokuwa akionyesha miujiza na maajabu pahali pamoja, je, wale waliokuwa pahali pengine wangeweza kuona hilo? Bila shaka la. Bwana Yesu alikuwa Mwana wa Adamu mwenye mwili, na kazi Yake na maneno Yake hayakuwa ya mwujiza; kando na maonyesho Yake ya miujiza na maajabu, hakukuwa na vipengele vya mwujiza. Hiyo ndiyo maana watu katika mahali pengine hawangeweza kusikia maneno Yake au kuona kazi Yake—ni wale tu waliokuwa kando Yake ndio walioweza kuona, kusikia na kuyapitia. Huu ni upande wa utendaji na wa kawaida wa kazi ya Mungu. Kwa hiyo, dini zingine na madhehebu mengine hayajui kuhusu kazi ambayo Mungu amefanya kupitia Kanisa la Mwenyezi Mungu huko Uchina. Kwa nini hawayajui? Mungu hafanyi kazi kwa njia za mwujiza. Ni wale tu ambao Amefanya kazi miongoni mwao ndio wanaweza kuiona na kuisikia; wale ambao hajafanya kazi miongoni mwao hawawezi kusikia sauti Yake. Bwana Yesu alipotekeleza kazi Yake miongoni mwa watu wa Kiyahudi, je, sisi watu wa China, tuliweza kuiona au kuisikia? Je, Waingereza na Wamarekani huko Magharibi waliweza kuiona na kuisikia? Basi mbona watu wa Magharibi na Wachina huko Mashariki waliweza hatimaye kukubali kazi ya Bwana Yesu? Kwa sababu kulikuwa na watu walioshuhudia, walioeneza injili kwetu, na walitoa Biblia hii ambayo ilirekodi maneno na kazi ya Bwana Yesu kwetu. Tulipomwomba Bwana Yesu, Roho Mtakatifu alitekeleza kazi Yake na alikuwa nasi; Alitupa neema, kwa hiyo tulipata kuamini kwamba Bwana Yesu ni Mungu na Mwokozi. Hivi ndivyo jinsi tulipata kuamini. Watu wa Magharibi wanasema kwamba “Mungu ameonekana na kufanya kazi Uchina—kwa nini hatujajua hili? Kwa nini hatujaweza kuona na kusikia hili?” Je, swali hili ni rahisi kueleza?

Je, kuna unabii kutoka kwa Mungu katika Biblia kuhusu kazi ya siku za mwisho? Je, Bwana Yesu alisema nini kuhusu hili? “Kwa kuwa kama umeme unavyotokea mashariki, na kumulika pia magharibi; ujio wa Mwana wa Adamu utakawa hivyo pia(Mathayo 24:27). Hili linamaanisha nini? Linamaanisha kazi ya Mungu ya siku za mwisho ni kama umeme, utokao Mashariki. Mwana wa Adamu atafanya kazi Mashariki, akiwaruhusu watu wa Mashariki kuona mwonekano wa mwanga mkubwa kwanza, kuona mwonekano wa mwanga wa kweli, kuona mwonekano wa Mungu, na kisha punde sana baadaye, mwanga huu mkubwa utaangaza Magharibi kama tu umeme. Yaani, baada ya maneno ya Mwenyezi Mungu kutoka Mashariki, yatachapishwa mtandaoni na hivyo kuenea Magharibi. Maneno ya Mwenyezi Mungu yalichapishwa lini mtandaoni? Toleo la Kichina lilichapishwa mtandaoni, kwa kuchelewa kabla ya mwaka wa 2007, au mapema zaidi mwaka wa 2005. Toleo la Kiingereza huenda liliwekwa mtandaoni mwaka wa 2010. Maneno ya Mungu yamekuwa mtandaoni kwa miaka mingi sana, lakini ni watu wangapi kutoka kwa dunia ya dini ambao wameenda mtandaoni kuyachunguza? Sio wengi; wachache sana hufanya hivyo. Njia ya Mungu na maneno ambayo Ametamka yamekuwa mtandaoni kwa muda mrefu. Watu sasa wameona kwamba maneno ya Mwenyezi Mungu yako mtandaoni, kwa hiyo mbona wale wanaodaiwa kuwa waumini wa dhati wa Bwana Mungu hawayachunguzi? Suala ni lipi hapa? Ushuhuda wa njia ya Mungu tayari umepewa kwa watu kutoka mataifa yote na maeneo yote. Mwanadamu asipoyachunguza kamwe, hatimaye apitie mateso ya milele na kuangamizwa, hilo litakuwa jukumu la nani? Ni nani anayewajibikia kosa hili? Je, hili ni kosa la Mungu, au la mwanadamu? Ni la mwanadamu. Kwa nini tunasema hivyo? Kwa sababu Bwana Yesu alisema kitambo, “Kwa hiyo kesheni: kwa kuwa hamjui ni saa ipi ambayo Bwana wenu atakuja(Mathayo 24:42), “Na kukawa na kelele saa sita ya usiku, Tazama, anakuja bwana arusi; ondokeni nje ili kumkaribisha(Mathayo 25:6), “Kondoo wangu huisikia sauti yangu(Yohana 10:27). Bwana Yesu alisema mambo kama hayo mara nyingine nyingi: “Ombeni, na mtapatiwa; tafuteni, na mtapata; pigeni hodi, na mtafunguliwa(Mathayo 7:7). Hii ni ahadi ya Mungu, na Bwana Yesu alisema mambo ya aina hii mara nyingi sana. Kulingana na maneno ya Bwana Yesu, mwanadamu asipowahi kumtafuta Mungu, na asiwahi kuchunguza anapomsikia mtu fulani akishuhudia kuja kwa Mungu, badala ya kumshutumu bila kufikiri, kwa kusema mambo kama “Wale wote wanaoshuhudia kuja kwa Mungu ni wa uzushi na washiriki wenye kufuata imani tofauti,” basi watu hawa ambao hawajakubali kazi ya Mungu hata mwisho kabisa wataanguka katika misiba mikuu na watakufa katika maumivu makuu ya adhabu yao katika maafa. Nani anapaswa kulaumiwa? Watu wengi kutoka jamii za dini wana shaka kuhusu suala hili. “Kwa nini Mungu haonekani kwetu? Kwa nini Amefichwa kutoka kwetu? Kwa nini Asitujulishe?” Je, Mungu amewahi kusema, “Nitakapofika kwa siri kutekeleza kazi, Nitaonekana na kuwapa watu ufunuo”? Mungu alisema nini? “Iwapo basi hutakesha, nitakujia kama mwizi, na hutajua saa ambayo nitakuja kwako(Ufunuo 3:3). Hili lilitabiriwa katika Kitabu cha Ufunuo. Kwa hiyo, ikiwa sisi kama waumini wa Bwana tunasikia kwamba mtu fulani ameshuhudia kwamba “Bwana harusi amefika; Bwana amerudi,” lakini hatuchunguzi au kukubali kazi ya Mungu ya siku za mwisho kwa vitendo, tunapojipata katika msiba mkuu na kufa katika adhabu yetu, hatuwezi kumlaumu Mungu. Tunapaswa kuitafuta shida kutoka ndani yetu wenyewe kuona ni katika vipengele vipi hatujafanya vyema. Hili pekee ndilo la haki. Kuangalia nyuma, ulimkubali vipi Bwana Yesu? Je, Bwana Yesu alikujia? Je, Bwana Yesu alikuonekania? Hakufanya hayo mawili. Ulimkubali Bwana Yesu kwa sababu wengine walihubiri injili na kukutolea ushuhuda wa Bwana. Imani katika njia inatoka kwa kusikia kuhusu njia, wakati kusikia kuhusu njia kunatoka kwa maneno ya Mungu. Sasa kwa kuwa mtu fulani amekushuhudia kuhusu injili hii na ukweli kwamba Mungu amefika kutekeleza kazi, huu ni upendo, huruma, na hangaiko la Mungu kwako—je, hufai basi kulielewa? Hivi ndivyo jinsi mtu anayemcha Mungu anapaswa kuelewa hili. Kwa hiyo, usiwe mwenye majivuno mbele za Mungu, usijione kuwa mwenye hadhi ya juu, usifikirie tu “Mungu atakapokuja Anapaswa kwanza kunipa ufunuo. Anapaswa kwanza kulifichua kwangu. Akifika na kutolifichua kwangu, basi Yeye si Mungu, na sitamkiri.” Hawa ni watu wa aina gani? Wamefanya makosa yapi? Unathubutu kuhakikisha kwamba lazima Mungu akufichulie hilo Atakapofika? Una msingi upi wa hili? Je, Bwana alikuambia “Nitakufichulia kwanza Nitakapofika”? Amesema maneno kama hayo kwako? Unafikiri kwamba wewe uko bora kuliko kila mtu mwingine duniani, kwamba wewe ndiye muhimu zaidi, kwamba unampenda Mungu zaidi? Je, wewe ni bora kuliko kila mtu mwingine? Wewe ni kiumbe maalum aliyeumbwa? Je, mtu kama huyo anaweza kuokolewa kwa urahisi? Kwa nini Mungu anahitaji kutekeleza kazi ya hukumu katika siku za mwisho? Ni kwa sababu wanadamu wapotovu hawafai kumwona Mungu. Wanadamu wote wapotovu wana tabia ya Shetani; wote hasa ni wenye majivuno na wenye kujipenda, na wote wana tamaa za kupita kiasi kumhusu Mungu. Wanajiweka juu ya mengine yote, chini kidogo tu ya mbingu na juu sana kuliko wengine, kana kwamba wanapendelewa na Mbingu. Na tabia potovu ya aina hii, mtu yeyote ambaye hajakubali hukumu na kuadibu kwa Mungu hafai kumwona Mungu.

Kimetoholewa kutoka katika Mahubiri na Ushirika Kuhusu Kuingia Katika Maisha

Kuna watu wengi, wakiwemo watu wa dini, ambao wanasema: “Kama Mungu amekuja, kwa nini sijamwona? Kwa sababu sijamwona hilo linathibitisha kwamba Mungu hajaja.” Hilo linaonekanaje kwako? Linaonekana kuwa upuuzi na ujinga. Je, unaweza kuona kuja kwa Mungu? Kama ungeiona nafsi halisi ya Mungu ungekuwa umekufa! Hivyo, Mungu anakujaje? Yeye anakuwa mwili Mwenyewe katika umbo la Mwana wa Adamu, ambaye ananena ili kuwaokoa wanadamu. Je, ungeweza kumtambua Mungu mwenye mwili kama ungemwona Yeye? Hata kama ungemwona, hungemtambua. Hii ni kama tu wakati Bwana Yesu alikuja. Watu wengi walimwona Bwana Yesu, lakini ni wangapi wao walimtambua kama Kristo, Mwana wa Mungu? Ni mtu mmoja pekee: Petro, na hiyo ni kwa sababu Roho Mtakatifu alimpa nuru. Hili linathibitisha nini? Linathibitisha kwamba wanadamu wapotovu hawana nafasi ya kuuona mwili wa kiroho wa Mungu wakati Yeye yuko katika umbo la mwili. Kama inakupasa kuuona mwili wa kiroho wa Mungu ungekuwa umekufa—hutawahi kuona mwili Wake wa kiroho. Kuweza kuisikia sauti ya Mungu tayari ni upendeleo sana kwa wanadamu wapotovu. Mungu alipotenda kazi katika Enzi ya Sheria, ni watu wangapi wangeweza kuisikia sauti ya Mungu? Sio wengi. Tunajua kwamba Ayubu aliisikia sauti ya Mungu, lakini, je, aliuona uso wa Mungu? Hapana, alimsikia tu Yehova Mungu akimzungumzia kutoka katika kimbunga, hivyo tunaweza kusema kwamba kuisikia sauti ya Mungu ni sawa na kuuona uso Wake. Musa alimsikia Mungu akimwita, lakini, je, aliuona uso wa Mungu? Baadaye Musa aliuona mgongo wa Mungu, lakini si uso Wake. Hivyo ukimsikia mtu akisema: “Unashuhudia kwamba Mungu amekuja, lakini mbona sijamwona Yeye? Mbona hakujatangazwa kwenye runinga ya taifa au redioni?” Unafikiri nini kuhusu mazungumzo ya aina hii? Ni ya kitoto sana! Je, ni nani aliyeona kuja kwa Bwana Yesu? Ni Wayahudi wachache tu wa wakati huo walioona. Wale Wayahudi wa wakati huo ambao, katika neno la Bwana Yesu, waliisikia sauti ya Mungu na walisikia mamlaka na uwezo walimfuata Yeye. Lakini mwishowe, je, ni wangapi kweli walimwamini Bwana Yesu na kufuata Yeye kweli? Wachache sana. Hivyo Mungu mwenye mwili anapokuja katika siku za mwisho akiwa amevaa kama mtu wa kawaida, hatuhitaji kuuona uso wa mtu huyu ili tuweze kuuona uso wa Mungu. Badala yake, tunapoisikia sauti Yake na kuuona ukweli ambao Anauonyesha, tunapaswa kuuamini, kuutii, na kuuweka katika vitendo. Watu ambao wanatenda hili watapata ukweli na uzima, na wataupata wokovu wa Mungu. Je, ni jambo la kutetewa kwa kusema “Lazima niuone uso wa Kristo kabla ya kumkubali Yeye”? Je, mfano wa Mungu mwenye mwili unaweza kuuwakilisha mwili wa kiroho wa Mungu? Je, mfano wa Bwana Yesu unaweza kuuwakilisha mfano halisi wa Mungu? Hapana, hauwezi. Hivyo mfano ambao mwili wa nyama unapata ni wa muda, na unatosha kwamba watu waone kwamba Yeye ni mtu wa kawaida, wa desturi tu. La muhimu zaidi, watu lazima wakubali Mungu mwenye mwili wayasikilize maneno Yake na kuukubali ukweli wote ambao Anauonyesha. Hii ndio njia ya kuupata upendo na wokovu wa Mungu! Usipoyasikiliza maneno Yake na kuukubali ukweli wote ambao Anauonyesha basi hutakuwa na uhusiano na Mungu, hutaishinda sifa ya Mungu kamwe. Ukweli ambao Mungu anauonyesha katika siku za mwisho ni ukweli wote ambao unawatakasa na kuwaokoa watu, na kwa hivyo ndio ukweli muhimu zaidi. Watu ambao hawaukubali na kuuweka katika vitendo bila shaka hawataupata wokovu wa Mungu kamwe.

Kimetoholewa kutoka katika Ushirika kutoka kwa Aliye Juu

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp