Programu ya Kanisa la Mwenyezi Mungu

Sikiliza sauti ya Mungu na ukaribishe kurudi kwa Bwana Yesu!

Tunawakaribisha wote wanaotafuta ukweli wawasiliane nasi.

Kwa nini Umeme wa Mashariki Hutapakaa Kwenda Mbele na Maendeleo Yasiyozuilika?

68

Kwa nini Umeme wa Mashariki Hutapakaa Kwenda Mbele na Maendeleo Yasiyozuilika?

Kristo wa siku za mwisho amekuwa akifanya kazi Yake nchini China kwa zaidi ya miaka 20, kazi ambayo imetetemesha makundi mbalimbali ya kidini kwa kina. Swali la kufadhaisha zaidi kwa jumuiya za kidini wakati huu limekuwa: Wachungaji wengi na wazee wa kanisa katika jumuiya ya kidini wamefanya liwezekanalo kuuhukumu na kuushambulia Umeme wa Mashariki kupitia njia mbalimbali kama vile kueneza uvumi kuhusu na kuukashifu Umeme wa Mashariki. Zaidi ya hayo, hata wamezingia makanisa yao na hata kuthubutu kushirikiana na serikali ya CCP kuwakamata na kuwatesa Wakristo katika Kanisa la Mwenyezi Mungu. Lakini wakiwa chini ya shutuma ya wayowayo, upinzani, na mateso kutoka kwa serikali CCP na ulimwengu wa kidini kutenda kama matawi mawili ya nguvu za shetani, kwa nini kuna waumini zaidi na zaidi kutoka madhehebu mbalimbali na makundi ya kidini wanaomkubali na kumfuata Mwenyezi Mungu? Ni kwa nini wale ambao wana ubinadamu mzuri na walikuwa na imani ya kweli katika Bwana hapo awali wako tayari kumfuata Mwenyezi Mungu hadi mwisho kabisa? Kwa nini wanaendelea kufanya hivyo licha ya kuvumilia shutuma isiyokuwa na mwisho, kashifa, shurutisho, na mateso kutoka kwa serikali CCP na ulimwengu wa kidini? CCP huwafunga jela na bado hawarudi nyuma. Ni vipi kuwa Umeme wa Mashariki hutapakaa kwenda mbele, bila kushindwa na bila kuvunjwa na nguvu za Shetani, kusitawi na neema mpya na ukuaji kila siku? Umeeneaje hadi sasa kwa mapana na marefu kwa kila pembe ya China ili kukubaliwa na kufuatwa na mamilioni? Kwa nini pia umeenea ulimwenguni kote kwa nchi na maeneo mengi tofauti?

Kwa kweli, watu wa kidini wanaoijua Biblia wamepuuza ukweli muhimu, ambao ni: Kitu chochote kitokacho kwa Mungu kitafanikiwa na kitu chochote kitokacho kwa mwanadamu kitaharibika kwa kweli. Fikiria hili kwa muda: Kama Umeme wa Mashariki haukuwa kuonekana na kazi ya Mungu mmoja na wa pekee wa kweli, ungeweza kuvunjilia mbali ngome ya kizuizi, upinzani, na mateso yaliyowekwa na ulimwengu wa kidini na serikali ya kumkana Mungu ya CCP na kuenea kwa haraka sana? Ikiwa haukuongozwa na kazi ya Roho Mtakatifu, ungekuwa na mamlaka na nguvu ya kuyafanya mataifa yote yafurike kwa mlima huu na kwa madhehebu yote kuwa moja? Kama Umeme wa Mashariki haukuwa kuonekana na kazi ya Mungu, ungekuwa umeleta ukweli unaowaruhusu watu kumwelewa Mungu? Je, ungekuwa umeonyesha njia ya wokovu? Je, ungeweza kuwahukumu na kuwashinda waumini wa kweli wa imani mbalimbali, wale kondoo wazuri na kondoo wa kuongoza, kutii na kufuata kwa mioyo thabiti? Wale katika madhehebu mbalimbali ya kidini hawakuwa na njia ya kutarajia kwamba Mwenyezi Mungu ambaye wana kujiamini na ujasiri wa kutosha kumshutumu, kumpinga, na kumtesa kwa kweli ni kurudi kwa Bwana na Mwokozi Yesu Kristo, ambaye walikuwa wamemsubiri kwa dukuduku na kung’ang’ania sana.

Kitabu cha Ufunuo kinasema kwamba ni Mwanakondoo pekee anayeweza kukifungua kitabu na kuivunja mihuri saba. Kristo wa siku za mwisho, Mwenyezi Mungu, ametoa maneno milioni nyingi ambayo sio tu kuwa yanafichua mafumbo yote ya mpango wa usimamizi wa miaka 6,000 wa Mungu, kufichua kusudi la Mungu katika hatua Zake tatu za kazi ili kuuokoa ubinadamu, na pia kutoa usuli, taarifa fiche, na kiini katika kila moja ya hatua katika kazi Yake, lakini aidha maneno Yake pia hutangaza kazi ya hukumu na kutakasa ambayo imeelekezwa kwa asili ya kishetani ya wanadamu na ukweli wa upotovu wao. Zaidi ya hayo, maneno Yake mengi yanahusu masomo mengi yanayohusiana na hadithi ya ndani ya Biblia, fumbo la Mungu kupata mwili, nia ya wazi ya Mungu na mahitaji maalum kwa mwanadamu, mfanyiko tendani wa maendeleo ya wanadamu na hatima ya wanadamu, nk. Hizi sio tu sherehe kwa macho ya wanadamu ili waweze kupanua upeo wao, lakini pia kuwaruhusu watu kuelewa kazi ya Mungu, tabia ya Mungu na asili. Zaidi ya hayo, maneno Yake hutuwezesha sisi wanadamu wapotovu kupata mabadiliko katika tabia na kutakaswa. Maneno Yake yana ukweli wote ambao sisi watu wapotovu tunahitaji ili kuokolewa na kukamilishwa. Kondoo wa Mungu huisikia sauti Yake na waumini ambao hutii kwa unyenyekevu wameshindwa kabisa na maneno ya Mungu wanapotafuta na kujifunza njia ya kweli; wameona kwa kweli na kwa dhahiri kwamba kazi halisi na maneno ya Mungu hayawezi kulinganishwa na hayawezi kubadilishwa na nadharia zozote au maarifa yaliyofanyizwa na wanadamu. Maneno na kazi Yake huthibitisha kwa wale ambao hukubali kwa unyenyekevu kwamba Mwenyezi Mungu kwa usahihi ni Mwana wa Adamu akirudi katika siku za mwisho na kuonekana kwa Mungu mmoja wa kweli. Wao huona kwamba ufalme umeshuka kwa milki ya mwanadamu na pia huona kwa dhahiri kwamba hatua tatu za kazi katika Enzi ya Sheria, Enzi ya Neema, na Enzi ya Ufalme ni kazi ya Mungu mmoja na kwamba ni kazi ya Mungu Mwenyewe, hakuna shaka kabisa juu ya hilo. Ni kama tu wamejizatiti na ukweli uliotolewa kutoka kwa Mwenyezi Mungu na uzoefu wa kazi ya Mungu ya siku za mwisho ambapo watamjua Mungu na kuingia katika njia sahihi ya imani ndani Yake ili kufanikisha wokovu. Kwa hiyo, wao husujudia mbele ya Mwenyezi Mungu na kukubali kwamba Yeye ni Mungu wao na wanarudi Kwake na kuahidi maisha yao Kwake. Ndiyo maana kuna watu wengi zaidi na zaidi waaminifu kwa hakika ambao hawaogopi tena yasiyojulikana na hufuata Umeme wa Mashariki kwa azimio lisilotikisika.

Kwa kweli, hakuna “sawa” au “baya” katika kazi ya Mungu, kuna “mpya” na “zee” au “mapema” na “baadaye” tu kwa sababu kanuni ya asili ya kazi ya Mungu ni kwamba daima ni mpya na kamwe si nzee na Hafuati kanuni zozote na hakuna tofauti kati ya kazi Yake mpya na nzee. Badala yake, kazi zenyewe husaidiana na kila hatua ikijenga juu ya ile hatua nyingine; kama viungo katika mnyororo vilivyounganishwa pamoja. Tukitafuta na kujifunza kwa moyo wa utulivu, kama tunaweza kuelewa hatua tatu za kazi katika mpango wote wa usimamizi wa miaka 6,000 ya Mungu, basi ni rahisi kuona kwamba kazi ya Kristo ya siku za mwisho– Mwenyezi Mungu–imejengwa juu ya msingi wa kazi ya Mungu iliyofanyika katika Enzi ya Neema na hutiririka kama moja na kazi ya Bwana Yesu; haijitegemei na si tofauti kwa njia yoyote. Aidha, tutaelewa kwa nini ni kazi ya Mwenyezi Mungu pekee ya siku za mwisho inaweza kuwatakasa na kuwabadilisha wanadamu, na pia kuwaruhusu kabisa wanadamu kuivunjilia mbali minyororo ya ushawishi wa giza wa Shetani ili kufanikisha wokovu wa Mungu.

Kuangalia nyuma kwa kipindi cha baadaye cha Enzi ya Sheria, wanadamu wote walijua dhambi ilikuwa ni nini, ingawa wao hawakutaka hivyo waliendelea kutenda dhambi daima, na hawakuweza kushika sheria na amri. Dhambi za wanadamu zilipoongezeka, dhabihu zao zikawa chache na chache na wakaanguka katika mtego usioweza kuepukika wa dhambi. Hatua kwa hatua, wanadamu walipoteza uchaji wa Mungu na wakathubutu kutoa dhabihu za mifugo vipofu na viwete katika madhabahu matakatifu ya Yehova Mungu. Kwa njia hii, walikabiliwa na kifo kwa sheria na laana ya Mungu. Ilikuwa kwa sababu hii ambapo kwa Mungu kumwokoa mwanadamu, hatua mpya ya kazi ilihitajika. Hii ni kwa sababu ni Mungu Mwenyewe tu–Muumba–angeweza kuwaokoa wanadamu waliopotoshwa na kuharibiwa tabia. Kwa sababu hii, Mungu alipata mwili na Akaonekana kwa mfano wa Bwana Yesu ili kuanza kazi ya Enzi ya Neema. Alichukua dhambi za wanadamu juu yake Mwenyewe na Alisulubiwa msalabani ili kukamilisha kazi ya ukombozi. Bwana Yesu aliwafundisha wafuasi wake kwamba wangetakiwa kusamehe na kuwa na subira, kuwapenda majirani zao kama wao wenyewe, na kuubeba msalaba kumfuata Yeye. Pia Aliwafundisha watu kuvunja mkate, kunywa divai, kuiosha miguu ya wengine na kuvifunika vichwa vyao. Aliwauliza watu kuweka ukweli zaidi katika matendo na Aliinua mahitaji ya wanadamu juu kuliko yalivyokuwa wakati Enzi ya Sheria. Bwana Yesu alimletea mwanadamu Enzi mpya na mwongozo mpya wa kusafiria na Akawapa watu njia ya kusafiria ili waweze kufurahia neema tele ya Mungu na kupata ukombozi Wake. Kazi ya Bwana Yesu katika Enzi ya Neema ilihitimisha Enzi ya Sheria iliyokuwa imeendelea kwa zaidi ya miaka 2,000 kwa namna ambayo ilitimiza sheria. Ni kazi mpya na ya juu iliyofanywa juu ya msingi wa kazi ya Yehova Mungu.

Bwana Yesu Kristo katika mwili huwaokoa wanadamu wote. Tukimwamini Bwana na kusamehewa dhambi zetu, basi tutatetewa na imani na kuokolewa. Ingawa tumesamehewa dhambi zetu, sababu ya msingi ya dhambi hizi, yaani asili ya kishetani iliyo ndani yetu ambayo humkataa na kumsaliti Mungu, haijawahi kutatuliwa kabisa. Kwa namna hii, hata kama Mungu akisahau dhambi zetu na hatutendei kwa kuzingatia dhambi zetu, hata hivyo sisi huishi katika mwili na hatuna njia ya kuvunja vifungo na udhibiti wa dhambi. Sisi tumekwama tu katika mzunguko unaoashiria mkwamo wa kutenda dhambi na ungamo na toba daima na hatujaepuka dhambi ili kuwa watu watakatifu. Katika hali nzuri, tabia yetu potovu ya kishetani itafichuliwa ingawa hatutataka; ambayo ni pamoja na kiburi, uroho, usaliti, udanganyifu, na dhambi zetu na makosa dhidi ya Bwana ambayo hatuwezi kudhibiti, ambayo ni kama tu Paulo anavyosema hapa: “kwa sababu kutaka kumo ndani yangu, lakini jinsi ya kutenda lililo jema sipati” (Warumi 7:18). Kwa dhahiri, “kuokolewa” hakumaanishi kuwa tumepatwa kikamilifu na Mungu. Kwa maneno mengine, tukiwa na ukombozi tu ambao tulipokea katika Enzi ya Neema, bado hatuwezi kushinda dhidi ya ushawishi wa Shetani ili kupatwa na Mungu kwa sababu Mungu hakujishughulisha na kazi ya kuifumua tabia yetu potovu ya kishetani inayoishi ndani ya mwanadamu katika Enzi ya Neema. Kama sisi hukawia tu katika hatua ya kazi iliyofanyika katika Enzi ya Neema na kushikilia mbinu zingine na matendo rahisi na yaliyopitwa na wakati, hata mpito wa miaka 1,000 haungezalisha mabadiliko ndani yetu; hatungefanikisha utakatifu, na pia hatungepata ufahamu mkubwa zaidi wa Mungu. Tumekwama tu katika utaratibu ule ule siku zote bila matumaini ya kukomaa maisha yetu kamwe. Tutachukuliwa hatua kwa hatua mbali na Mungu zaidi na zaidi na hatimaye kuishia katika mifumbato ya Shetani. Hivyo kwa wanadamu wapotovu kuokolewa kikamilifu kutoka kwa ushawishi wa Shetani, Mungu ni lazima atekeleze hatua nyingine ya kazi, moja ambayo ni ya kina zaidi na kamilifu, ili kuwaokoa wanadamu. Mungu huwapa wanadamu maneno ambayo wanahitaji kwa maisha ili wanadamu waweze: kuelewa kazi ya Mungu na usimamizi Wake; kujua uweza wa Mungu, hekima, kiini, tabia, na chote ambacho Anacho na alicho; kujua ukweli wote; na kuongozwa kwenye njia sahihi ya uzima. Kwa hivyo mawazo ya kale ya mwanadamu na tabia za kale zitabadilishwa, na asili ya dhambi ya mwanadamu itaondolewa kabisa, ambayo ni kusema, mwanadamu atatoroka kutoka kwa falsafa na sheria za kishetani na vile vile sumu za kishetani ambazo huishi ndani ya asili yake. Kisha mwanadamu anaweza kuwa mwenye huruma na mwenye ukweli na hivyo kuwa mtu anayemtii Mungu kweli. Wakati huu, kazi yote ya Mwenyezi Mungu ni hatua hii kamili ya kazi ambapo utakaso kamili na wokovu wa mwanadamu unafanyika. Mwenyezi Mungu haupi ubinadamu ukweli zaidi tu kwa kutegemeza msingi wa kazi ya Bwana Yesu katika Enzi ya Neema, lakini pia Anatangaza amri na maagizo ya utawala kwa Enzi ya Ufalme. Ameinua mahitaji yake kwa mwanadamu ili: Mwanadamu apaswe kuutafuta na kuelewa ukweli katika neno la Mungu; kujua tabia ya Mungu na chote Alicho nacho na alicho; na kujua asili ya mwanadamu mwenyewe ya kishetani ambayo humkaidi na kumpinga Mungu. Mwanadamu anapaswa kutenda ukweli na kuishi kwa neno la Mungu chini ya sharti la mwanzo la kuuelewa ukweli ili mwanadamu aweze kufikia mabadiliko ya tabia yake, kurejesha maisha ya kawaida ambapo yeye humwabudu Mungu, kuwa mtakatifu, na kuingia hatima ya ajabu ambayo Mungu amemtayarishia mwanadamu.

Biblia ina unabii juu ya wokovu wa Mungu katika siku za mwisho ambapo Waraka wa Kwanza wa Petro sura ya 1 mstari wa 5 inasema, “Mnaohifadhiwa na nguvu ya Mungu kupitia kwa imani hata mpate wokovu tayari kufichuliwa wakati wa mwisho.” Kipande hii cha maandiko kinatabiri kwa dhahiri: Kwetu tunaomfuata Bwana Yesu, Mungu ametuandalia wokovu katika siku za mwisho. Hivyo, wokovu huu katika siku za mwisho utakuwa nini kwa kweli? Biblia inasema: “Kwa maana wakati umefika ambao lazima hukumu ianze katika nyumba ya Mungu” (1 Petro 4:17). “Na alikuwa na nyota saba katika mkono wake wa kuume: na katika kinywa chake ulitoka upanga mkali wenye makali kuwili: na uso wake kama jua liking’aa kwa nguvu zake” (Ufunuo 1:16). “Na nikamwona malaika mwingine akiruka katikati ya mbingu, akiwa na injili ya milele kuwahubiria hao wanaoishi katika dunia, na kwa kila taifa, na kabila, na lugha, na watu, Akisema kwa sauti kuu, Mcheni Mungu, na kumpa utukufu; kwa maana saa ya hukumu yake imekuja: na mumsujudie yule aliyeziumba mbingu, na dunia, na bahari, na chemchemi za maji” (Ufunuo 14:6-7). Tunaweza kuona kutoka kwa maandiko kwamba injili ya milele inahusu kazi ya hukumu ya Mungu katika siku za mwisho, ambako Mungu hutumia maneno makali kama panga kumhukumu na kumtakasa mwanadamu. Hii ni hukumu hasa mbele ya kiti cheupe cha enzi kilichotajwa katika Kitabu cha Ufunuo, ambayo ni kazi itakayoamua matokeo ya mwanadamu na hatima yake. Mwenyezi Mungu anasema, “Ikifika kwa neno ‘hukumu,’ utawaza juu ya maneno yote ambayo Yehova alizungumza kila mahali na pia maneno ya kukaripia ambayo Yesu aliwaambia Mafarisayo. Ingawa maneno haya ni yenye ukali, sio hukumu ya Mungu kwa mwanadamu; maneno tu ambayo yamezungumzwa na Mungu katika mazingira tofauti, kumaanisha, mandhari tofauti, na ni tofauti kabisa na yale maneno anayonena Kristo wakati Anamhukumu mwanadamu siku za mwisho. Katika siku za mwisho, Kristo anatumia ukweli tofauti kumfunza mwanadamu, kufunua kiini cha mwanadamu, na kuchunguza maneno na matendo ya mwanadamu huyo. Maneno haya yanajumuisha kweli mbalimbali, kama vile wajibu wa mwanadamu, jinsi mwanadamu anavyopaswa kumtii Mungu, jinsi mwanadamu anavyopaswa kuwa mwaminifu kwa Mungu, jinsi mwanadamu anavyostahili kuishi kwa kudhihirisha ubinadamu wa kawaida, na pia hekima na tabia ya Mungu, na kadhalika. Maneno haya yanalenga nafsi na tabia potovu ya mwanadamu. Hasa, maneno hayo yanayofichua vile mwanadamu anavyomkataa Mungu kwa dharau yanazungumzwa kuhusiana na vile mwanadamu alivyo mfano halisi wa Shetani na nguvu za adui dhidi ya Mungu. Mungu anapofanya kazi Yake ya hukumu, Haiweki wazi asili ya mwanadamu kwa maneno machache tu; Anaifunua, na kuishughulikia na kuipogoa kwa muda mrefu. Mbinu hizi za ufunuo, kushughulika, na kupogoa haziwezi kubadilishwa na maneno ya kawaida, ila kwa ukweli ambao mwanadamu hana hata kidogo. Mbinu kama hizi pekee ndizo huchukuliwa kama hukumu; ni kwa kupitia kwa hukumu ya aina hii pekee ndio mwanadamu anaweza kutiishwa na kushawishiwa kabisa kujisalimisha kwa Mungu, na zaidi ya hayo kufaidi ufahamu kamili wa Mungu. Kile ambacho kazi ya hukumu humletea mwanadamu ni ufahamu wa uso halisi wa Mungu na ukweli kuhusu uasi wake mwenyewe. Kazi ya hukumu humruhusu mwanadamu kupata ufahamu zaidi wa mapenzi ya Mungu, wa makusudi ya kazi ya Mungu, na wa mafumbo yasiyoweza kueleweka kwa mwanadamu. Pia inamruhusu mwanadamu kutambua na kujua asili yake potovu na asili ya upotovu wake, na pia kugundua ubaya wa mwanadamu. Matokeo haya yote huletwa na kazi ya hukumu, kwa maana asili ya kazi ya aina hii hasa ni kazi ya kuweka wazi ukweli, njia, na uhai wa Mungu kwa wale wote walio na imani ndani Mwake. Kazi hii ni kazi ya hukumu inayofanywa na Mungu” (“Kristo Hufanya Kazi ya Hukumu kwa Ukweli” katika Neno Laonekana katika Mwili). Tunaweza kuelewa kutoka kwa maneno ya Mungu kwamba: Katika siku za mwisho, Mungu hutumia ukweli kufanya kazi Yake ya hukumu ili watu waweze kuelewa vyema mapenzi Yake, kuwa na maarifa ya kweli juu Yake, na kuelewa chanzo na kiini cha upotovu wa mtu kutoka kwa Shetani. Aidha, kazi ya hukumu pia huwaruhusu wanadamu kwa kweli kupata ukweli, njia, na uzima uliofadhiliwa na Kristo wa siku za mwisho ili waweze kabisa kupatwa na Mungu na kupata wokovu wake. Huu ndio wokovu mkamilifu zaidi uliojengwa juu ya msingi wa kazi ya ukombozi ya Bwana Yesu na pia ni hatua ya mwisho ya kazi katika mpango wa usimamizi wa miaka 6,000, ambayo ni kumshinda na kumkamilisha mwanadamu; huu ndio wokovu unaoonekana katika siku za mwisho.

Ndugu zangu, licha ya ukosefu wa ufahamu wa wanadamu juu ya kazi ambayo Mungu hufanya, na licha ya watu wengi kutoelewa yote ambayo Mungu hufanya na bila kujua nia Zake na kuwa wa kukwepa na kutotaka juu ya kazi mpya ya Mungu, hata hivyo, wafuasi wa kweli wa Mungu wana mahali Pake katika mioyo yao. Wao huweka kando mawazo yao na kutafuta na kujifunza njia ya kweli kwa moyo wa utulivu na kusikiliza sauti ya Mungu, na hivyo kupata nuru Yake na utambuzi halisi wa sauti ya Mungu. Wafuasi hawa wa kweli hutoka kwenye mawazo yao hadi kwa maarifa halisi kuhusu Mungu wa pili mwenye mwili. Waumini hawa wa kweli huhama kutoka kumpinga Mungu hadi kumtii Yeye, huhama kutoka kumtesa Mungu hadi kumkubali, na wanahama kutoka kumtelekeza Mungu hadi kumpenda. Hii ni sawa na siku za nyuma ambako wanafunzi wa Yesu na watu wengine wa kawaida wa Kiyahudi walitambua kuwa Bwana Yesu ndiye Mmoja wa mbinguni. Ingawa walikabiliwa na kizuizi kikubwa, kizuizi, kifungo, ukandamizaji na mateso na jumuiya ya kidini na utawala wa kishetani, walipofahamu njia ya kweli waliaminishwa kwa udhabiti na walijua bila shaka na wakamfuata Mungu kwa karibu. Hiyo ndiyo nguvu ya kutisha ya kazi ya Mungu wa kweli. Sasa, Injili ya ufalme ya Mwenyezi Mungu imekuwa ikienea kwa kasi ya mwako katika China Bara yote. Sasa inaongezeka kwa kila nchi na taifa; kwa hakika hutaki kupata ukweli kamili ambao Mungu huwafadhili wanadamu na kuishi katika mwanga? Umeelewa kweli yaliyomo na madhumuni ya makumbusho ya daima ya Bwana Yesu kwa wanadamu katika siku za mwisho ya kutazama? Je, huna wasiwasi juu ya kupoteza fursa hii kwa wokovu kamili kutoka kwa Mungu? Je, huhangaiki juu ya majuto yako ya kuhuzunisha sana? Inawezekana kuwa bado huelewi sababu ya maendeleo yasiyo na mipaka na yasiyozuilika ya Umeme wa Mashariki? Ikiwa unaelewa, basi unasubiri nini?