44. Nimerudi Nyumbani

Na Chu Keen Pong, Malasia

Nilimwamini Bwana kwa zaidi ya muongo mmoja na kuhudumu kanisani kwa miaka miwili, na kisha nikaliacha kanisa langu ili kwenda nje ya nchi kufanya kazi. Nilikwenda katika sehemu kadhaa, ikiwa ni pamoja na Singapore, na kuchuma pesa nzuri, lakini nikiishi katika maisha haya katika jamii ya kisasa ambapo mwenye nguvu ndiye mwadilifu, kila mtu akiunda njama dhidi ya mwenzake, na kukiwa na udanganyifu kila mahali. Licha ya kila aina ya maingiliano magumu kati ya watu, nilikuwa macho dhidi ya wengine kila mara. Pia wao walikuwa macho dhidi yangu kila mara, nikiachwa na hisia ndani yangu kiasi kwamba sikuweza kupata msingi wowote mzuri wa kusimama. Maisha ya aina hiyo yaliniacha nikiwa nimechoka katika mwili na roho. Kitu cha pekee kilichonipa faraja yoyote kilikuwa ni shajara niliyoibeba ambayo nilikuwa nimenakili vifungu kadhaa vya Maandiko. Wakati mwingine ningevisoma navyo viliujaza utupu uliokuwa katika nafsi yangu. Sikuwa nimeenda kwenye mkutano wa kanisa kwa miaka kadhaa lakini kwa mwaka uliopita nilikuwa na jambo moja tu akilini: kutafuta kanisa ambalo ningeweza kumtumikia Bwana kwa dhati. Baadaye nilitumia fursa ya muda wa ziada kwenda kwenye makanisa kadhaa nchini Malaysia, makubwa kwa madogo, lakini kila wakati niliingia nikiwa na furaha na kutoka nikiwa mwenye huzuni. Siku zote nilihisi kuwa kitu kilikuwa kinakosa kwa ndani, lakini sikuweza kueleza haswa kilikuwa nini. Nikiwa nimekabiliwa na mzozo huu niliingia katika hali mbaya zaidi, nikicheza tu video za michezo na kutazama sinema mtandaoni, wakati mwingine nikikesha nikicheza video hizo hadi alfajiri au kutazama sinema moja baada ya nyingine. Ratiba yangu ya kulala ilikuwa imevurugika. Nilipoanza kufanya hivi nilikuwa na utambuzi kidogo, nikihisi kuwa Bwana hatapendezwa, lakini polepole nikafa ganzi. Ilikuwa wakati huo ndipo nilipoipoteza simu yangu ya rununu. Wakati huo, nilihisi kuwa nimetaabishwa sana—simu yangu ya rununu ilikuwa imepotea na habari nyingi kupotea vilevile, zaidi ya hayo, sikuwa na njia ya kuingia kwenye mtandao wa Facebook. Kwa nje, hili lilikuwa jambo baya, lakini sikuwahi kutarajia kwamba lingekuwa jambo muhimu kwa maisha yangu. Ni kama msemo wa zamani, “bahati iliyojitokeza kwanza kwa sura ya balaa”.

Nilinunua simu mpya ya rununu mapema mwanzoni mwa mwaka wa 2017. Siku moja mwishoni mwa mwezi wa Februari, niliingia kwenye mtandao wa Facebook na kisha kwa bahati mbaya nikabonyeza kwenye mfululizo wa matukio wa lugha ya Kiingereza, na kuona kuwa kulikuwa na maandiko katika matangazo hayo. Niliona pia dondoo ambazo hazikuwa kutoka katika Biblia, lakini zilinitia moyo sana, na zilinishawishi kihisia. Niliiangalia kwa makini akaunti hiyo ya mtandao wa Facebook kwa siku chache zilizofuata, na hata nikatumia muda fulani kutafuta maneno kadhaa. Mwishowe, nilimaliza kusoma tangazo ambalo nilikuwa nimevutiwa nalo. Ni baada tu ya kulisoma ndipo nilipogundua kuwa maudhui ya tangazo hili yalikuwa tafsiri ya kifungu cha Maandiko ambamo Bwana Yesu anasema: “Siye kila mmoja ambaye aliniambia, Bwana, Bwana, ataingia ufalme wa mbinguni(Mathayo 7:21). Nilihisi kuwa tafsiri hii ilikuwa ya kipekee, na kwamba ilijaa msukumo na mwanga. Sikuwa nimemwongeza mtu huyo kama rafiki, kwa hiyo ingawa nilitaka kuona matangazo zaidi kwenye mfululizo wa matukio yake, sikuweza. Kile nilichoweza kuona kwenye mfululizo wa matukio yake, hata hivyo, ilikuwa kwamba mtumiaji huyu wa mtandao wa Facebook alitoka Korea Kusini na alikuwa dada anayeitwa Susan. Nilimtumia ombi la urafiki, lakini labda hakuwa mtandaoni wakati huo na kwa hiyo hakukubali ombi langu mara moja. Siku mbili baadaye, nilimwongezea mtu mwingine anayezungumza Kichina kwenye mtandao wa Facebook aliyeitwa Qi Fei, Mkristo mwingine kutoka Korea Kusini. Alizungumza nami kuhusu baadhi ya uzoefu wake katika imani yake, nami nilipenda sana kile alichosema. La kushangaza ni kuwa Dada Qi Fei pia alikuwa rafiki ya Dada Susan, kwa hivyo wakati huu tuliongezana kama marafiki. Kwa kusoma matangazo yao ya mtandao wa Facebook na kupitia mazungumzo yetu ya mara kwa mara, nilikuja kuhisi kuwa walielewa mengi kuhusu imani katika Mungu.

Baada ya muda fulani wa kuijadili Biblia na kuzungumza kuhusu mambo fulani katika maisha yetu, nilihisi kweli kwamba njia yao ya kunisaidia kushughulikia maudhi yangu kwa kweli ilikuwa ya kipekee, na kwamba kulikuwa na maana sana na utambuzi katika kile walichosema. Nilijionea mwenyewe kuwa walikuwa tofauti na watu wengine. Nilihisi kuwa mtulivu zaidi na mwenye amani moyoni mwangu kupitia kuwasiliana nao, na ingawa sikuwajua vizuri, punde si punde, nilikuwa nimeanza kuwachukulia kama marafiki wa karibu kwa sababu ya unyenyekevu na uaminifu wao. Nilitaka kufunua waziwazi kwao yaliyokuwa moyoni wangu. Polepole, nilianza kufanya mabadiliko fulani katika jinsi nilivyoishi maisha yangu.

Takriban wiki moja baadaye jioni ya Machi 11, niliingia kwenye mtandao wa Facebook na kuona kuwa Susan alikuwa kwenye mtandao. Nilizungumza naye kuhusu mambo fulani ya kazi kwanza, kisha nikamwambia kuhusu tamaa ya moyo wangu, kupata kanisa la kutumikia, na kwamba nilitaka kusikia maoni yake. Dada Susan alisema kuwa kila kitu kimepangwa na kutawaliwa na Mungu, na kwamba ninapaswa kumwomba Mungu zaidi na kushiriki katika kutafuta kuhusu suala hili. Alisema kuwa kila kitu kina wakati uliowekwa na Mungu, na sote tunapaswa kujifunza kusubiri na kutii. Kisha alitaja hali ya sasa katika makanisa mengi: Wahubiri hawana chochote kingine cha kuhubiri, katika makanisa mengine hakuna mtu yeyote anayehudhuria mikusanyiko, na katika makanisa mengine, hata kama kuna baadhi ya watu huko, wote wanazungumzia tu kuhusu kupata pesa, kuunda mahusiano ya kibiashara, na mambo mengine yasiyohusiana kabisa na imani. Alisema kuwa mambo haya yote ni dalili za makanisa kutokuwa na kazi ya Roho Mtakatifu, na yamekuwa ukiwa. Kwa kweli nilijihusisha na kila kitu alichokuwa akisema. Nilipokuwa nikihudumia kanisani hapo awali, wafanyakazi wenzangu walikuwa wakipigania kujipatia jina na kujipatia pesa, wakapanga njama dhidi ya kila mmoja, wakikashifiana, na kujaribu kutawala maeneo yao wenyewe yaliyo madogo. Hata kulikuwa na tabia fisadi. Nilipoona mambo haya yakitokea moja baada ya lingine, nilihisi kusikitika na mwenye hamaki kwa wakati mmoja. Wakati huo, nilimwuliza mchungaji pamoja na wafanyakazi wenzangu jinsi ninavyopaswa kutazama mambo haya yote, lakini hawakuweza kutoa maelezo ya wazi. Nilishangaa sana kwamba ilikuwa ni Dada Susan ambaye alitatua mchafuko huu ambao uliniudhi kwa muda mrefu sana. Nilihisi aina ya furaha isiyoelezeka moyoni mwangu.

Tulichungua pia mada ya misiba na vita kadhaa vilivyokuwa vikitokea wakati huo, na kulingana na ishara za misiba iliyokuwa ikitokea pande zote pamoja na vita vilivyokuwa karibu, unabii wa kibiblia wa kuja kwa Bwana mara ya pili ulikuwa umetimia kimsingi, na Bwana angerudi hivi karibuni. Jambo hilo lilinikumbusha kuhusu muumini ambaye nilikuwa nimekutana naye mtandaoni karibu saa sita mchana aliyesema kuwa Bwana alikuwa amerudi mnamo mwaka wa 1991, lakini kwa kweli nilikuwa na shaka kuhusu suala hilo. Ilibidi nimwulize Susan kuhusu jambo hili. Aliponiuliza nilifikiria nini kulihusu, nilisema: “Haiwezekani. Bwana atakaporudi hakika Atashuka juu ya wingu na Ataonekana na kila mtu. Lakini hatujamwona Bwana akishuka juu ya wingu, kwa hiyo mtu yeyote anawezaje kusema kuwa Bwana amesharudi?”

Susan alijibu, “Ndugu, unaielewa Biblia vizuri. Ukiyachunguza maneno ya Biblia kwa makini, nina hakika utapata jibu lako. Kwa kweli, kuna unabii mwingi tofauti kuhusu kuja kwa pili kwa Bwana. Sote tunaweza kuona kutoka kwa unabii wa kibiblia kwamba kimsingi uko katika makundi mawili. Moja ni jinsi ulivyoelezea, kutabiri kwamba Bwana atashuka waziwazi juu ya wingu na kuonekana na kila mtu. Aina nyingine inatabiri ujio wa siri wa Bwana, ambao kundi fulani tu la watu wataijua. Ni jinsi Bwana Yesu alivyosema:‘Tazama, mimi nakuja kama mwizi(Ufunuo 16:15). ‘Na kukawa na kelele saa sita ya usiku, Tazama, anakuja bwana arusi; ondokeni nje ili kumkaribisha(Mathayo 25:6). ‘Kama mwizi’ na ‘kukawa na kelele saa sita ya usiku’ inamaanisha kuwa itakuwa kimya na bila kusonga, isiyojulikana na mtu yeyote. Mbingu hazitasikika na dunia haitatikisika—hakitakuwa kitu ambacho kila mtu anaweza kuona. Kuna kikundi kidogo tu cha watu kinachoweza kusikia sauti ya Bwana, wanaoweza kumkaribisha. Huu ni unabii wa Bwana kuja kwa siri. Ikiwa tunashikilia tu unabii wa Bwana kushuka wazi juu ya wingu lakini tusizingatie unabii wa Bwana kuja kwa siri, hiyo ni sawa? Basi je, hatutashindwa kuisikia sauti ya Bwana, na kukosa nafasi yetu ya kumkaribisha Bwana na kuinuliwa hadi katika ufalme wa mbinguni?”

Niliduwazwa na swali la Susan. Nilisoma vifungu hivi viwili tena na tena, na kuwaza: “Je, kunaweza kuwa na utata katika Biblia? La hasha! Inawezekanaje? Lakini kwa kweli, kunayo makundi mawili tofauti ya unabii wa kibiblia kuhusu jinsi Bwana atakavyorudi! Jambo hili linaweza kuelezwaje?” Nikiwa nimechanganyikiwa, nilimsihi aendelee na ushirika wake. Susan alisema: “Tunaweza kuona kutokana na unabii katika Biblia kwamba kuja kwa Bwana kwa mara ya pili kutatokea katika njia mbili tofauti. Moja ni ujio wa siri, na nyingine ni kuonekana waziwazi. Katika siku za mwisho, Mungu atapata mwili ulimwenguni kama Mwana wa Adamu, na kwa nje Kristo ataonekana kuwa mtu wa kawaida kama Bwana Yesu katika mwili. Atamiliki ubinadamu, naye Atakula, kuvalia mavazi, kuishi, na kutenda kama mtu wa kawaida. Ataishi kati ya wanadamu, na kwa hiyo hii inachukuliwa kuwa siri kutoka kwa mtazamo wetu kwa sababu hakuna mtu atakayeona kuwa Yeye ndiye Mungu, na hakuna mtu atakayejua utambulisho Wake wa kweli. Mara tu Mwana wa Adamu atakapoanza kufanya kazi na kunena, wale wanaoweza kuisikia sauti ya Mungu wataona maonyesho ya tabia ya Mungu kupitia maneno na kazi ya Mwana wa Adamu. Wataona mamlaka na nguvu za Mungu, nao watatambua kuwa Bwana amekuja. Hii itatimiza unabii wa Bwana Yesu: ‘Kondoo wangu huisikia sauti yangu, na mimi Ninawajua, nao hunifuata(Yohana 10:27). Wale ambao hawawezi kuitambua sauti ya Mungu hakika watamchuklia Mungu mwenye mwili kama mtu wa kawaida kulingana na kuonekana Kwake kwa nje. Watamkana na kumkataa, na hata kumpinga, kumshutumu, na kumkufuru Kristo wa siku za mwisho. Hivi ni kama vile wakati Bwana Yesu alipokuja kufanya kazi Yake—kwa nje, Alionekana kama Mwana wa Adamu wa kawaida, ikawasababisha watu wengi kumkana, kumpinga na kumshutumu. Ni kikundi kidogo tu cha watu kilitambua kupitia maneno na kazi Yake kwamba Bwana Yesu alikuwa Kristo mwenye mwili, kwamba Alikuwa dhihirisho la Mungu, na kwa hiyo kilimfuata Bwana Yesu na kupata wokovu Wake.” Nilipousikia ushirika wa dada huyo, nilihisi kwamba ulikuwa wenye maana sana kwa sababu maneno haya yote yalikuwa ukweli—hivyo ndivyo ilivyokuwa kweli wakati Bwana Yesu alipokuja kutekeleza kazi Yake. Lakini nilifikiria kuhusu jambo hilo tena: Inasema katika Ufunuo kwamba Bwana atakaporudi Atashuka waziwazi juu ya wingu, na hivyo ndivyo wachungaji na wazee wote wanavyosema, pia. Kwa kuzingatia jambo hili, mara moja nikamwuliza Susan, kwa kusadiki kabisa: “Bwana Yesu mwenyewe Alisema kuwa kuja Kwake kwa mara ya pili kutakuwa juu ya wingu. Inawezaje kuwa kupata mwili? Unawezaje kukana maneno hayo ya Biblia?” Dada Susan alisema: “Unahitaji tu kuichunguza Biblia kwa uangalifu sana nawe utagundua kuwa kuna sehemu nyingi ambazo zinatabiri waziwazi kuwa Bwana atarudi Akiwa mwili.” Kwa kuzingatia kile alichosema Dada Susan, nilitafuta vifungu vya Maandiko na kuanza kuvisoma: “Na ninyi pia muwe tayari: maana katika saa kama hii msiyofikiria kuwa Mwana wa Adamu atakuja(Luka 12:40). “Kwani kama umeme, unavyomulika chini ya mbingu kutoka sehemu moja, huangaza hadi sehemu nyingine chini ya mbingu; vivyo ndivyo Mwana wa Adamu atakuwa katika siku yake. Bali kwanza lazima apitie mambo mengi, na akataliwe na kizazi hiki(Luka 17:24-25).

Baada ya kumaliza kusoma vifungu hivi vya Maandiko, Dada Susan alisema: “Unabii huu unataja ‘Mwana wa Adamu anakuja’ na ‘hivyo ndivyo Mwana wa Adamu atakavyokuwa pia.’ ‘Mwana wa Adamu’ amezaliwa na mwanadamu naye Anamiliki ubinadamu wa kawaida. Ikiwa Alijidhihirisha katika mwili wa kiroho, basi Asingeweza kutajwa kama Mwana wa Adamu, jinsi Yehova Mungu alivyo Roho na Hawezi kuitwa Mwana wa Adamu. Watu wameona malaika pia, ambao ni viumbe wa kiroho na kwa hiyo hawawezi kuitwa Mwana wa Adamu. Wote walio na umbo la kibinadamu lakini ni viumbe wa kiroho hawawezi kuitwa Mwana wa Adamu. Bwana Yesu aliyepata mwili huitwa Mwana wa Adamu na Kristo kwa sababu Yeye alikuwa kupata mwili kwa kimwili kwa Roho wa Mungu, na utambuzi wa Roho katika mwili. Alikuwa mtu wa kawaida, naye Aliishi kati ya wanadamu. Bwana Yesu alikuwa Mwana wa Adamu, kupata mwili kwa Mungu, kwa hiyo Bwana Yesu aliposema Atarudi tena kama Mwana wa Adamu, Alimaanisha kuwa Atarudi tena katika mwili kama Mwana wa Adamu, na sio katika umbo la kiroho. Kwa hiyo, Bwana Yesu aliposema Atarudi tena, Alimaanisha kwamba Atarudi katika umbo la kupata mwili. Zaidi ya hayo, Maandiko yanasema: ‘Bali kwanza lazima apitie mambo mengi, na akataliwe na kizazi hiki.’ Hii inathibitisha zaidi kwamba Bwana atakaporudi tena itakuwa kwa njia ya kupata mwili. Tafakari kuhusu jambo hilo: Ikiwa Bwana alitokea kwetu wakati wa kurudi Kwake akiwa katika mwili wa kiroho badala ya mwili, Asingeteseka sana, sembuse kukataliwa na kizazi hiki. Nani angethubutu kumkataa Roho wa Mungu? Ni nani angeweza kumfanya Roho wa Mungu ateseke? Kwa hiyo, ikiwa Bwana atarudi akiwa mwili au Aje katika mwili wa kiroho, hiyo si wazi?”

Nilishangaa niliposoma maneno “Mwana wa Adamu.” Nilikuwa nimewaza hapo zamani kuhusu swali la “Mwana wa Adamu,” lakini sikuwahi kuelewa. Maelezo ya Dada Susan yalitatua mashaka yangu yote kabisa, nami nilijawa na hisia nilipoyasikia. Usiku ulikuwa unaingia, kwa hivyo tuliagana na kutoka mtandaoni. Nilifurahi sana usiku huo kiasi kwamba sikuweza kulala hadi muda mrefu baadaye. Niliwaza jinsi nilivyokuwa nimemwamini Bwana kwa miaka mingi, lakini sikuwahi kusikia ushirika mzuri kama huo. Nilishtuka, na kulikuwa na aina ya uwazi wenye raha moyoni mwangu ambao sikuweza kuuelezea.

Siku iliyofuata, Machi 12, nilihisi aina ya tumaini lisilo dhahiri na msisimko usioelezeka. Hii ilikuwa ni kwa sababu mimi na Susan tulikuwa tumejadili sana kuhusu Mwana wa Adamu na kupata mwili usiku uliotangulia. Ingawa ningeweza kuona uhusiano kati ya Mwana wa Adamu na kupata mwili, nami nilijua katika nadharia kuwa Bwana Yesu si mwingine ila Kristo mwenye mwili, bado nilitaka kujua majibu ya maswali kama vile kupata mwili ni nini kwa hakika, Kristo ni nini, ni kwa msingi gani ambapo mtu anaweza kusema bila shaka kwamba Mungu amekuwa mwili, na kadhalika. Lakini kwa kuwa mimi na Susan tulikuwa na kazi wakati wa mchana nasi hatukuwa na kazi wakati wa jioni pekee, nilitumai tu kwamba muda ungesonga haraka zaidi.

Mwishowe, jioni ilifika na sote wawili tukaingia kwenye mtandao. Baada ya kuingia mtandaoni, swali la kwanza nililomwuliza Dada Susan lilikuwa kuhusu kupata mwili. Alinitumia vifungu kadhaa kutoka kwa maneno ya Mwenyezi Mungu, naye akanisihi nivisome. Na kwa hivyo nilianza kusoma: “Maana ya kupata mwili ni kwamba Mungu Anajionyesha katika mwili, na Anakuja kufanya kazi miongoni mwa wanadamu wa uumbaji Wake katika umbo la mwili. Hivyo, ili Mungu kuwa mwili, ni lazima kwanza Apate umbo la mwili, mwili wenye ubinadamu wa kawaida; hili ndilo hitaji la kimsingi zaidi. Kwa kweli, maana ya kupata mwili kwa Mungu ni kwamba Mungu Anaishi na kufanya kazi katika mwili, Mungu katika kiini Chake Anakuwa mwili, Anakuwa mwanadamu(Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Kiini cha Mwili Ulio na Mungu). “Mungu mwenye mwili Anaitwa Kristo, na Kristo ni mwili uliovishwa na Roho wa Mungu. Mwili huu ni tofauti na wa mwanadamu yeyote aliye wa nyama. Tofauti hii ni kwa sababu Kristo sio wa mwili na damu bali ni mwili wa Roho. Anao ubinadamu wa kawaida na uungu kamili. Uungu Wake haujamilikiwa na mwanadamu yeyote. Ubinadamu Wake wa kawaida unaendeleza shughuli Zake zote za kawaida katika mwili, wakati uungu Wake unafanya kazi ya Mungu Mwenyewe(Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Kiini Cha Kristo Ni Utiifu kwa Mapenzi ya Baba wa Mbinguni). “Yeye Aliye mwili wa Mungu Atakuwa na dutu ya Mungu, na Yule Aliye Mungu katika mwili Atakuwa na maonyesho ya Mungu. Kwa maana Mungu Hupata mwili, Ataleta mbele kazi Anayopaswa kufanya, na kwa maana Mungu Amepata mwili, Ataonyesha kile Alicho na Ataweza kuuleta ukweli kwa mwanadamu, kumpa mwanadamu uhai, na Amwonyeshe mwanadamu njia. Mwili usio na dutu ya Mungu kwa kweli sio Mungu mwenye mwili; kwa hili hakuna tashwishi. Kupeleleza kama kweli ni mwili wa Mungu mwenye Mwili, mwanadamu lazima aamue haya kutoka kwa tabia Yeye huonyesha na maneno Yeye hunena. Ambayo ni kusema, kama ni mwili wa Mungu mwenye mwili au la, na kama ni njia ya kweli au la, lazima iamuliwe kutokana na dutu Yake. Hivyo, katika kudadisi[a] iwapo ni mwili wa Mungu mwenye mwili, cha msingi ni kuwa makini kuhusu dutu Yake (Kazi Yake, maneno Yake, tabia Yake, na mengine mengi), bali sio hali ya sura Yake ya nje(Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Dibaji). Baada ya kumaliza kusoma, nilihisi kuwa maneno haya yalielezea waziwazi siri ya kupata mwili, hasa kuhusu ufafanuzi wa Kristo: “Mungu mwenye mwili Anaitwa Kristo.” Hii ilikuwa wazi, rahisi, na yenye fasaha kabisa! Ingawa nilikuwa nimemwamini Bwana kwa zaidi ya muongo mmoja na nilijua kuwa Yesu ndiye Kristo, sikuwa nimewahi kuelewa siri za ukweli kama vile mbona tunasema kwamba Bwana Yesu ndiye Kristo. Siku hiyo, nilijifunza kutoka kwa vifungu hivyo vya maneno ya Mungu ambayo Susan alikuwa amenitumia kwamba kwa hakika Mungu mwenye mwili ni Yule tunayemwita Kristo, na Kristo ndiye Yeye ambaye Mungu anakuwa mwili. Nilitafakari maneno haya kwa makini, na kadri nilivyoyatafakari, ndivyo moyo wangu ulivyong’aa zaidi.

Kisha Dada Susan aliniambia kuwa haya yalikuwa maneno ya Mwenyezi Mungu; Alisema pia kwamba neno la Mungu ni ukweli, na kwamba ni Mungu Mwenyewe pekee ndiye Anayeweza kuonyesha ukweli. Alipotaja maneno “Mwenyezi Mungu,” sikuweza kusema kwa muda, ingawa hayakunishangaza sana kwani nilikuwa nimeshadhani kuwa anaweza kuwa wa Kanisa la Mwenyezi Mungu. Pia nilikuwa nimesoma uvumi fulani kwenye mtandao kuhusu kanisa hili. Ni kwamba tu nilijifikiria kuwa Mkristo, na kwamba nilipaswa kuwa na moyo wa kumcha Mungu, kwa hivyo sikutaka kufikia maamuzi yoyote kwa kupuuza kabla ya kuelewa ukweli wa jambo hilo. Hii ilikuwa ni kwa ajili ya kuzuia kutenda dhambi kwa maneno yangu na kumkosea Mungu. Mbali na hayo, katika siku hizi chache za mwisho, nilikuwa nikifikiria: Dada Susan na mimi tulikuwa tumeongea mara nyingi, na ingawa sikuweza kuona ni nani niliyekuwa nikiongea naye, ukweli aliokuwa akishiriki nami bado ulikuwa unaweza kutatua mkanganyiko wangu. Kupitia mazungumzo yetu na kwa kusoma matangazo yake kwenye mfululizo wa matukio yake, nilihisi kuwa yeye na Qi Fei wote walikuwa watu waaminifu, wachangamfu, na wazuri. Maudhui ya ushirika wao yalikuwa yenye kujenga maadili na yenye faida kwangu. Imeandikwa katika Biblia kuwa unaweza kuujua mti kutoka kwa matunda yake; miti mizuri huzaa matunda mazuri, wakati miti mibaya huzaa matunda mabaya. Kwa hiyo, kupitia kwa mawasiliano yangu na Dada Susan na Qi Fei, polepole niliacha kuwa na mashaka na wasiwasi moyoni mwangu, nami nikamsihi Susan aendelee kushiriki.

Dada Susan alisema: “Kwa kuwa yeye ni Mungu mwenye mwili, Anayo maonyesho ya Mungu—yaani, Yeye hutamka maneno. Mungu mwenye mwili wa siku za mwisho Amekuja hasa kuuonyesha ukweli ili kuwahukumu, kuwatakasa, na kuwaokoa watu. Wote wanaoisikia sauti ya Bwana aliyerejea, na wanaoweza kuitafuta na kuikubali, ni mabikira wenye busara wanaoihudhuria karamu na Bwana, na hii inatimiza unabii uliotamkwa na Bwana Yesu: ‘Na kukawa na kelele saa sita ya usiku, Tazama, anakuja bwana arusi; ondokeni nje ili kumkaribisha(Mathayo 25:6). Mabikira wenye busara huisikia sauti ya Mungu na kwenda kumlaki. Bila kujua, wanainuliwa mbele ya kiti cha enzi cha Mungu ili kukutana uso kwa uso na Bwana; wanakubali hukumu na utakaso wa Mungu katika siku za mwisho. Kupitia hukumu ya maneno ya Mungu, tabia zao potovu zinabadilishwa na kutakaswa, na wanafanywa kuwa washindi na Mungu kabla ya majanga. Kwa sasa hii ni awamu ambayo kwayo Mwenyezi Mungu anafanya kazi kwa siri ili kumwokoa na kumkamilisha mwanadamu. Mara tu kikundi cha washindi kitakapoundwa, kazi ya Mungu iliyofichwa katika mwili Wake itakamilika, na majanga yataujia ulimwengu. Mungu ataanza kuwatuza wema na kuwaadhibu waovu, na kisha Atajitambulisha kwa nchi zote na watu wa ulimwengu. Wakati huo, unabii wa Bwana akishuka juu ya wingu katika Ufunuo 1:7 utatimizwa. ‘Tazama, anakuja na mawingu; nalo kila jicho litamwona yeye, na pia wale waliomdunga: na makabila yote ya ulimwengu yatalia kwa huzuni kwa sababu ya yeye.’ Mtu anaweza kusema kuwa watu wanapomwona Bwana akishuka juu ya wingu, Akijidhihirisha kwa watu wote, wote wanapaswa kufurahi sana. Lakini Maandiko yanasema kwamba jamaa yote ya dunia itaomboleza. Mbona iwe hivi? Ni kwa sababu wakati Mungu atakapojidhihirisha hadharani, kazi ya Mungu ya wokovu iliyofichwa katika mwili Wake itakuwa tayari imeisha naye Ataanza kazi ya kuwatuza wema na kuwaaadhibu waovu. Wakati huo, wote ambao waliikataa kazi ya Mungu iliyofichwa wataipoteza kabisa nafasi yao ya kupata wokovu, na wale wanaomwumiza—wale wanaompinga na kumshutumu Mwenyezi Mungu, Kristo wa siku za mwisho—wataona kuwa Mwenyezi Mungu, ambaye wamempinga na kumshutumu, si mwingine ila Bwana Yesu aliyerejea. Hebu fikiria kuhusu jambo hilo, wasingewezaje basi kusikitika, na kulia na kusaga meno? Huu ndio muktadha wa maneno ‘makabila yote ya ulimwengu yatalia kwa huzuni kwa sababu ya yeye.’”

Nilipousikia ushirika huo kutoka kwa Dada Susan, hisia hiyo niliyokuwa nayo ya ridhaa na furaha ilirudi. Kwa kweli sikuwa nimewahi kuelewa vifungu hivi wakati nilipokuwa mshiriki wa kanisa langu la zamani, lakini nilielewa tu maana yake halisi, nikifikiria kuwa kurudi kwa Bwana kutakuwa juu ya wingu na kujulikana na wote. Ni wakati huo tu ndipo mwishowe nilipofahamu kwamba kwanza Mungu huja kwa siri ili kufanya hatua ya kazi ya kumhukumu na kumwokoa mwanadamu. Mara tu kundi la washindi litakapoundwa, ni wakati huo tu ndipo Atakapojidhihirisha wazi kwa mataifa na watu wote wa ulimwengu. Ikiwa tutashikilia bila kufikiria wazo kwamba Bwana atashuka juu ya wingu wakati Atakaporudi, ikiwa tutakataa kuikubali kazi iliyofichwa ya Mungu katika mwili Wake na kungoja hadi Bwana atakaposhuka juu ya wingu, huo utakuwa wakati ambapo tutakwenda kuzimu moja kwa moja, kwa sababu kazi ya Mungu ya kuwaokoa wanadamu tayari imekwisha. Namshukuru Bwana kwa mwongozo Wake. Nilikuwa nimeelewa mengi katika muda huo mfupi ambao Dada Susan alikuwa akishiriki nami.

Kisha Dada Susan aliniuliza ikiwa nilitaka kumkubali Mwenyezi Mungu kama Mwokozi wangu. Aliponiuliza mara ya kwanza, sikujibu, na alipouliza tena, hisia isiyoelezeka ya msisimko ilibubujika ndani yangu, nami nilianza kutokwa na machozi. Nilijibu kwa dhati: “Nina … nataka … ku!” Mara tu nilipoyasema maneno haya, nilihisi kama mwana mpotevu aliyekuwa akitangatanga nyikani kwa muda mrefu, ambaye mwishowe alikuwa amerudi nyumbani kwenye upendo. Moyoni mwangu, nilihisi kujawa na furaha na raha.

Baada ya kuikubali kazi ya Mwenyezi Mungu ya siku za mwisho, nilitangaza tena baadhi ya matangazo ya Susan. Muda mfupi baadaye, marafiki watano au sita wa mtandao wa Facebook walinitumia ujumbe kuniambia “niamke” nao wakanitumia viungo kadhaa kuelekea kwenye tovuti ambazo zilikuwa zimejaa mashambulio, shutuma, na kashfa kwa Kanisa la Mwenyezi Mungu. Nilijua kuwa hii ilikuwa vurugu ya Shetani, nami sikuiruhusu inifikie. Siku iliyofuata, mchungaji fulani aliniona nikiwa mtandaoni, na baada ya kupiga porojo kwa muda, aliniuliza, “Je, unamwamini Mwenyezi Mungu kwa kweli? Kwa nini unataka kumwamini Mwenyezi Mungu?” Jambo hili lilinifadaisha sana, kwa hiyo nilimwuliza: “Kondoo wa Mungu huisikiza sauti ya Mungu. Nimegundua kutoka kwa maneno ya Mwenyezi Mungu kuwa kila kitu kilichoonyeshwa na Mwenyezi Mungu ni ukweli, kwamba ni sauti ya Mungu, kwa hiyo mbona nisimwamini Mwenyezi Mungu? Kwa nini?” Labda hakutazamia kwamba ningemwuliza swali kama hilo naye hakujibu kwa muda. Kwa hiyo, nilimwuliza tena, “Mchungaji, umeichunguza kazi ya Mwenyezi Mungu katika siku za mwisho? Je, umeyasoma maneno ya Mwenyezi Mungu? Kama mchungaji, unawezaje kukataa kutafuta na kuchunguza, lakini utoe tu hukumu na shutuma bila mpangilio?” Nilishangaa kwamba alizunguka na kusitasita katika kusema bila kutoa jibu halisi, kisha akaondoka mtandaoni ghafla. Nilipoona akiwa amehangaikahangaika sana, nilihisi furaha isiyoelezeka, nami nilihisi ridhaa kana kwamba nilikuwa nimeshinda moja ya majaribio ya Shetani. Kwa kweli, nilikuwa tu nimetumia baadhi ya maswali ambayo Dada Susan na Qi Fei walitaja mara nyingi katika majadiliano yetu; nilikuwanimesema tu jambo kutoka kwa kile nilichokuwa nimeelewa kutoka kwa maneno ya Mwenyezi Mungu. Sikuwa nimewahi kutarajia mchungaji wa kuheshimika kama huyo kutatizwa na maswali yangu. Uzoea huu mdogo ulinipa ujasiri sana. Namshukuru Mungu!

Kufumba na kufumbua, zaidi ya miezi mitano ilikuwa imepita. Kwa kuhudhuria mikutano na kusoma maneno ya Mungu, nilipata ufahamu kuhusu maana ya kupata mwili, ni watu wa aina gani wanaweza kuingia katika ufalme wa mbinguni, na vipengele vingine vya ukweli. Katika wakati huu wote, nilipitia usumbufu kutoka kwa kila aina ya uvumi ulioenezwa na wachungaji na wazee. Wakati mwingine nilikuwa hasi na dhaifu kwa sababu sikuweza kubaini ujanja wa Shetani, lakini Mungu hakuwahi kuniacha. Kupitia maneno ya Mungu waliyonisomea dada hao pamoja na ushirika wao mvumilivu kuhusu ukweli, niliweza kupata utambuzi fulani kuhusu asili ya wazee na asili ya kishetani ya wachungaji na kiini cha uhasama kuelekea ukweli, na upinzani kwa Mungu. Pia nilianza kuwa na utambuzi fulani kuhusu msukumo wao unaostahili dharau ili kufanya kila linalowezekana kuwazuia waumini wasiitafute na kuichunguza njia ya kweli. Sitawahi kupotoshwa tena au kudhibitiwa nao. Kuweza kuushinda ushawishi wa giza wa Shetani na kuinuliwa mbele ya kiti cha enzi cha Mungu ilikuwa neema na baraka ya Mungu kwa ajili yangu. Namshukuru Mwenyezi Mungu! Kuweza kumgeukia Mungu kuliamuliwa kabla na kupangwa na Mungu zamani. Nitamtegemea Mungu na kusonga mbele bila wasiwasi wowote! Nilipoingia ndani ya nyumba ya Mungu, wimbo wa kwanza ambao nilijifunza ulikuwa “Kutembea kwenye Njia Sahihi ya Maisha ya Binadamu”: “Maneno ya Mungu ni ukweli, kadiri niyasomavyo zaidi, ndivyo moyo wangu ung’aavyo zaidi. Maneno ya Mungu yanafichua siri ya maisha. Ghafla nauona mwanga. Yote niliyo nayo yanatoka kwa Mungu. Yote ni kwa neema ya Mungu. Namfuata Kristo, nafuatilia ukweli na uzima; natembea kwenye njia sahihi ya maisha ya binadamu” (Mfuateni Mwanakondoo na Kuimba Nyimbo Mpya). Na leo, ninaihubiri injili na kumshuhudia Mungu pamoja na ndugu zangu kanisani. Ninataka kujiingiza katika jukumu langu na kuulipiza upendo wa Mungu!

Tanbihi:

a. Nakala halisi ya mwanzo inasema “na kwa.”

Iliyotangulia: 43. Kupotea na Kurejea Tena

Inayofuata: 45. Kurejea Kutoka Ukingoni

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Maudhui Yanayohusiana

2. Njia ya Utakaso

Na Christopher, UfilipinoJina langu ni Christopher, na mimi ni mchungaji wa kanisa la nyumbani huko Ufilipino. Mnamo mwaka wa 1987,...

9. Upendo wa Aina Tofauti

Na Chengxin, BrazilNafasi ya bahati mnamo mwaka wa 2011 iliniruhusu nije Brazili kutoka China. Nilipokuwa nimewasili tu, nilizidiwa na...

4. Mwamko wa Roho Aliyedanganywa

Na Yuanzhi, BraziliNilizaliwa katika mji mdogo huko Kaskazini mwa China na mnamo 2010, nikafuata jamaa kwenda Brazili. Hapa nchini Brazili,...

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp