Programu ya Kanisa la Mwenyezi Mungu

Sikiliza sauti ya Mungu na ukaribishe kurudi kwa Bwana Yesu!

Tunawakaribisha wote wanaotafuta ukweli wawasiliane nasi.

Mfuateni Mwanakondoo na Kuimba Nyimbo Mpya

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

(Ma)tokeo ya Kutafuta 0

Hakuna matokeo yaliyopatikana

Natamani Kuiona Siku ya Utukufu wa Mungu

1

Leo nakubali hukumu na utakaso wa Mungu, kesho nitapokea baraka Zake.

Niko radhi kutoa ujana wangu na kutoa maisha yangu ili kuona siku ya utukufu wa Mungu.

Eh, upendo wa Mungu umeufurahisha moyo wangu.

Anafanya kazi na kuonyesha ukweli, Akinipa maisha mapya.

Niko radhi kunywa kikombe cha dhiki na kuteseka ili kupata ukweli.

Nitastahimili fedheha bila malalamiko, natamani kuishi maisha yangu nikilipiza wema wa Mungu.

2

Nitatoa upendo na uaminifu wangu kwa Mungu na kukamilisha misheni yangu ya kumtukuza Mungu.

Nimedhamiria kusimama imara katika ushuhuda kwa Mungu, wala kamwe sitashindwa na Shetani.

Eh, kichwa changu kinaweza kupasuka na damu itiririke, lakini ujasiri wa watu wa Mungu hauwezi kupotea.

Ushawishi wa Mungu umo moyoni, naamua kumwaibisha Shetani Ibilisi.

Maumivu na shida vimeamuliwa kabla na Mungu, nitastahimili aibu ili kuwa mwaminifu Kwake.

Kamwe sitamsababisha Mungu alie au kusumbuka.

3

Maneno ya Mungu hunipa imani na nguvu, nitamfuata Mungu kwa uthabiti hadi mwisho.

Nitatangaza na kushuhudia injili ya Mungu siku zote hadi nife.

Eh, nitamsifu Mungu kwa furaha, na kumwimbia wimbo na dansi mpya.

Nazungumza waziwazi kwa dhati, natoa uaminifu wangu kwa Mungu.

Moyo wangu utakuwa na Mungu daima. Siku ya utukufu wa Mungu itakapokuja,

tutakusanyika kando ya kiti cha enzi na kucheza kwa furaha, tutafurahia mapumziko ya milele katika mbingu mpya na nchi mpya.

Iliyotangulia:Kutembea kwenye Njia ya Kumpenda Mungu

Inayofuata:Nimeona Uzuri wa Mungu

Maudhui Yanayohusiana