82. Mateso katika Chumba Cha Kuhojiwa

Na Xiao Min, China

Nilizaliwa katika sehemu maskini ya mashambani yenye maendeleo kidogo mno, nami niliishi maisha magumu na ya ufukara nilipokuwa mtoto. Ili nitimize maisha bora haraka iwezekanavyo, baada ya kufunga ndoa, nilianza kufanya kazi kana kwamba nilikuwa na kichaa. Hata hivyo, niliishia kuugua kutokana na kufanya kazi kupita kiasi, na hali yangu ilibadilika kutoka kuwa mwenye afya njema hadi kukumbwa magonjwa. Niliishi katika hali ya maumivu yaliyosababishwa na magonjwa yangu nami nilitafuta ushauri wa daktari na matibabu mahali popote ambapo ningeweza. Niliishia kutumia pesa nyingi, lakini sikupata nafuu kutokana na magonjwa yangu. Katika majira ya kuchipua ya mwaka wa 1999, dada wawili walinihubiria injili ya kazi ya Mwenyezi Mungu wa siku za mwisho. Kwa kuyasoma maneno ya Mwenyezi Mungu, nilifahamu mamlaka na uwezo wa maneno ya Mungu, nilijua kwamba hakuna mwanadamu yeyote ambaye angeweza kuyazungumza, na kwamba maneno ya Mwenyezi Mungu ni sauti ya Mungu kweli. Nilikuwa na hakika kabisa kuwa Mwenyezi Mungu ni Bwana Yesu aliyerudi, na kwamba Anaweza kutuokoa kutokana na maumivu yetu yote. Ninapoyasoma maneno ya Mungu zaidi na zaidi, nilikuja kuelewa ukweli fulani na mwishowe nilielewa kabisa mambo mengi ulimwenguni. Roho yangu iliyohuzunishwa na kusongwa ilihisi kukombolewa, nami nilianza kupata nafuu polepole kutokana na magonjwa yangu. Nilikuwa na shukrani nyingi mno kwa Mungu, nami nilianza kuhubiri injili kwa bidii na kushuhudia kazi ya Mungu ya siku za mwisho.

Hata hivyo, haikuchukua muda mrefu, nilikamatwa mara tatu mfululizo na serikali ya CCP kwa kuihubiri injili, na kila wakati nilipokamatwa, Mwenyezi Mungu alinielekeza kuyashinda mateso ya Shetani. Mnamo mwaka wa 2012, wakati wa kutekeleza jukumu langu kwa ajili ya kanisa, nilianguka tena katika tundu la jinamizi hilo nami nikateswa mikononi mwa ibilisi Shetani … Ilipoelekea jioni mnamo tarehe 13 Septemba, 2012, nilirudi nyumbani na jinsi nilivyokuwa nikifanya kila wakati, nikapakia skuta yangu nje na kubonyeza kengele ya mlango. Jambo la kushangaza, mara tu nilipofungua mlango watu wanne wenye miraba minne walinishambulia kama mbwa mwitu. Waliipopotoa mikono yangu nyuma ya mgongo wangu na kunitia pingu, kisha wakanisukuma ili niketi kwenye kiti na kunibana pale. Mara moja polisi kadhaa walianza kukagua begi langu…. Nikiwa nimekabiliwa na onyesho hili la ghafla na lenye nguvu, nilichanganyikiwa kwa woga, nami nilihisi kama mwana-kondoo mchanga wa kusikitisha aliyekamatwa na mbwa mwitu wabaya, bila nguvu yoyote ya kupinga chochote kile. Kisha wakanitoa nje na kuniweka nyuma ya gari dogo jeusi. Nilipokuwa ndani ya gari, mkuu wa polisi, aliyeonekana kama mtu mdogo wa kusikitisha aliyemelewa na mafanikio yake, alinigeukia na kutabasamu kitukutu, akisema, “Ha! Je, unajua jinsi tulivyokukamata?” Wakiogopa kwamba ningejaribu kukimbia, maafisa wa polisi walinishikilia pande zote, kana kwamba nilikuwa mhalifu hatari. Nilihisi hasira na hofu kwa wakati mmoja, nami singeweza kukisia jinsi polisi wangeniadhibu na kunitesa. Niliogopa sana kwamba singeweza kuhimili mateso yao nami ningekuwa Yuda na kumsaliti Mungu. Lakini baadaye niliyafikiria maneno ya Mungu: “Alimradi muombe na kusali zaidi mbele Yangu mara kwa mara, Nitawapa imani yote. Kutoka kwa nje, wale walio na mamlaka wanaweza kuonekana kuwa waovu, lakini msiogope, kwa kuwa hii ni kwa sababu mna imani kidogo. Almuradi imani yenu ikue, hakuna kitu kitakachokuwa kigumu mno(Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Matamko ya Kristo Mwanzoni, Sura ya 75). Maneno ya Mwenyezi Mungu yalinipa imani na nguvu na, polepole, yalinisaidia kutulia. “Ndio,” niliwaza. “Haijalishi jinsi polisi wale waovu walivyokuwa wakatili na wakali, wao ni vibaraka tu katika mikono ya Mungu nao wako katika mipango ya Mungu. Mradi niombe na kumwita Mungu kwa moyo wa kweli, basi Mungu atakuwa nami na hakuna haja ya kuwa na wasiwasi. Ikiwa polisi hawa waovu wananitesa na kunipiga kikatili, basi hiyo itakuwa tu ni Mungu akitaka kuijaribu imani yangu. Haijalishi jinsi wanavyoutesa mwili wangu, hawawezi kamwe kuuzuia moyo wangu kumtafuta Mungu na kumwomba Mungu. Hata wakiuua mwili wangu, hawawezi kuiua nafsi yangu, kwa kuwa kila kitu nilicho kiko mikononi mwa Mungu.” Nilipofikiria kuhusu jambo hili, sikumwogopa ibilisi Shetani tena nami niliazimia kumshuhudia Mungu. Kwa hivyo niliomba moyoni mwangu, “Ee Mungu Mwenyezi! Haijalishi watakavyonitendea leo, niko tayari kuyakabili yote. Ingawa mwili wangu ni dhaifu, ninatamani kuishi kwa kukutegemea na nisimpe Shetani nafasi hata moja ya kunitumia vibaya. Tafadhali nilinde, nisikusaliti, na nisiwe Yuda mwenye kuaibisha.” Tulipokuwa tukiendelea na safari, niliendelea kuimba akilini mwangu moja ya nyimbo za kanisa: “Kwa mpango Wake mtakatifu na enzi kuu, ninakabiliwa na majaribu yaliyokusudiwa kwangu. Ninawezaje kufa moyo au kujaribu kuficha? Kitu cha kwanza ni utukufu wa Mungu. Wakati wa shida, maneno ya Mungu yananiongoza na imani yangu inakamilishwa. Nimejitoa kabisa na kikamilifu, kujitoa kwa Mungu bila hofu ya kifo. Mapenzi Yake daima yako juu ya yote” (“Ninaomba tu Kwamba Mungu Aridhike” katika Mfuateni Mwanakondoo na Kuimba Nyimbo Mpya). Nilipokuwa nikiimba kimya kimya, moyo wangu ulijawa nguvu, nami niliamua kutegemea Mungu kutoa ushuhuda na kumdhalilisha shetani.

Mara tu walipokuwa wamenipeleka katika chumba cha kuhojiwa, nilishangaa kuona kwamba dada ambaye alifanya wajibu sawa nami, na kiongozi wa kanisa pia walikuwepo. Wote walikuwa wamekamatwa pia! Mmoja wa maafisa wa polisi aliniona nikiwatazama dada zangu wa kanisa naye akanikazia macho vikali na kunikemea, akisema, “Unakodolea macho nini? Ingia humo ndani!” Ili kutuzuia tusisemezane, polisi walituzuiliwa katika vyumba tofauti vya kuhojiwa. Walinichunguza kwa fujo, wakaufungua mkanda wangu na kunipapasa kila mahali. Ilikuwa ni kama tusi zito, nami nikaona jinsi hawa pepo wabaya wenye cheo cha chini wa serikali ya CCP walivyo waovu, wenye kustahili dharau na katili kweli! Nilihisi hasira, lakini ilinibidi niizuie hasira yangu, kwani hapakuwa na nafasi ya haki katika pango hili la majinamizi. Baada ya wao kuichukua skuta mpya iliyokuwa ya kanisa pamoja na zaidi ya yuani 600 nilizokuwa nazo, walianza kunihoji. “Jina lako ni nani? Cheo chako kanisani ni kipi? Kiongozi wako ni nani? Yuko wapi sasa?” Sikujibu, kwa hivyo polisi akaniambia kwa sauti kubwa, “Unafikiri hatutajua usipotuambia? Hujui ni nini tunachoweza kufanya! Unapaswa kujua kuwa tumewakamata viongozi wako wa ngazi ya juu pia!” Kisha wakaorodhesha majina machache na kuniuliza ikiwa nilimjua yeyote kati yao, nao waliendelea kunihoji. “Pesa zenu zote za kanisa lako huwekwa wapi? Tuambie!” Nilipuuza kila kitu walichosema, nikisema, “Simjui mtu yeyote! Sijui chochote!” Walipoona kwamba duru yao ya kwanza ya kuhoji ilikuwa imefeli, waliamua kutumia mbinu ambayo walitumai ingewapa matokeo, nao wakaanza kunihoji na kunitesa kwa zamu ili kujaribu kunichosha. Polisi walinihoji na kunitesa bila kukoma kwa siku tatu na usiku nne. Katika wakati huu mgumu, nilimwita Mungu kwa dhati, na maneno ya Mungu yaliniongoza: “Haupaswi kuwa na hofu ya hili na lile. Haidhuru wingi wa matatizo na hatari unazokabili, utabaki thabiti mbele Yangu; usizuiliwe na kitu chochote, ili mapenzi Yangu yaweze kufanyika. Huu utakuwa ni wajibu wako…. Usiwe na hofu; kwa msaada Wangu, ni nani angeweza daima kuzuia barabara? Kumbuka hiki! Kumbuka! Kila kitu ambacho hutokea ni kwa kusudi Langu njema na yote yako chini ya uangalifu Wangu(Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Matamko ya Kristo Mwanzoni, Sura ya 10). “Naam!” Niliwaza. “Mwenyezi Mungu ni ngome yangu imara, na nikiwa na Mwenyezi Mungu kama msaada wangu thabiti, siogopi chochote! Mradi ninayo imani ya kushirikiana na Mungu, basi ninaamini kuwa Mungu atanisaidia kuyashinda majaribu ya Shetani na kupitia wakati huu mgumu.” Kwa kuwa katika siku ya kwanza polisi hawakuwa wamepata habari waliyotaka kutoka kwangu, waliaibika hadi wakawa na hasira, na mkuu kati yao akaniambia kwa ukali, “Sitakubali kushindwa na ukaidi wake. Mteseni!” Nilipomsikia akisema hivi, roho yangu ilisita nami nikaanza kuogopa, na nilifadhaika kwani tayari nilikuwa ninavunjika kwa sababu ya mateso yao. Niliweza tu kumwita Mungu kwa dhati: “Ee Mungu Mwenyezi! Ninahisi dhaifu sana hivi sasa na sina nguvu kabisa. Lakini polisi wanataka kunitesa na sijui kabisa ikiwa ninaweza kuendelea kusimama imara. Tafadhali kuwa pamoja nami na Unipe nguvu.” Polisi waliichukua mikono yangu yenye pingu iliyokuwa bado nyuma ya mgongo wangu na kuining’iniza kwenye meza iliyovunjika, kisha wakanilazimisha nibaki nikiwa nimechuchumaa nusu na kusimama nusu. Walinitazama kwa uhasama na kunishinikiza kwa maswali. “Kiongozi wako yuko wapi? Fedha zote za kanisa ziko wapi?” Walikuwa wakitamani tu nivunjike kwa ajili ya shinikizo la mateso hayo na nijisalimishe kwao. Baada ya polisi hao waovu kuendelea na mateso haya kwa takriban nusu saa, miguu yangu ilianza kuuma na kutetemeka. Moyo wangu ulikuwa ukidunda kwa nguvu na mikono yangu pia ilikuwa inauma vibaya pia. Sikuweza kuvumilia tena nami nilihisi kana kwamba singeweza kudumu kwa muda mrefu, na kwa hivyo niliomba kwa dhati moyoni mwangu: “Ee Mungu Mwenyezi! Tafadhali niokoe. Siwezi kuvumilia tena. Sitaki kukusaliti kama Yuda. Tafadhali nipe nguvu” Wakati uo huo, maneno haya ya Mungu yalinijia akilini: “Kuna pingamizi la Shetani kwa Mungu katika kila hatua ambayo Mungu anatenda ndani yenu—katika kila kitu kuna vita. … Wakati Mungu na Shetani wanapigana katika milki ya kiroho, utamridhishaje Mungu, na utasimamaje imara katika ushuhuda wako Kwake? Unapaswa kujua kuwa kila kitu unachokipitia ni majaribu makubwa na ndipo Mungu hukuhitaji kuwa na ushuhuda(Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Kumpenda Mungu tu Ndiko Kumwamini Mungu Kweli). Maneno ya Mungu yalinizindua na kuniwezesha kugundua kuwa Shetani alikuwa akinitesa kwa njia hii ili anifanye nimsaliti Mungu na kuacha kuufuatilia ukweli. Hivi vilikuwa vita viliyokuwa vikipiganiwa katika ulimwengu wa kiroho: Shetani alikuwa akinijaribu, na pia ilikuwa njia ya Mungu ya kunijaribu. Huu ulikuwa wakati hasa ambao Mungu alinihitaji nishuhudie. Mungu alinitegemea na malaika wengi sana walikuwa wakinitazama hivi sasa, sawasawa na ibilisi Shetani, wote wakiningojea nitangaze msimamo wangu. Singeweza kukata tamaa na kusalimu amri hata kidogo na singeweza kujisalimisha kwa Shetani; nilijua lazima niiruhusu kazi ya Mungu ifanyike kupitia kwangu ili nitimize mapenzi ya Mungu. Kulingana na kanuni isiyoweza kubadilika, hili lilikuwa jukumu ambalo ninapaswa kutekeleza kama kiumbe aliyeumbwa—huu ulikuwa wito wangu. Katika wakati huu muhimu, mtazamo wangu na tabia yangu vilikuwa na athari ya moja kwa moja kwa uwezo wangu wa kuwa na ushuhuda wa ushindi kwa Mungu, na hata zaidi vilikuwa viathiri moja kwa moja uwezo wangu wa kuwa ushuhuda wa Mungu kumshinda Shetani na Yeye kupata utukufu. Nilijua singeweza kumsababishia Mungu huzuni au kumvunja moyo, na singeweza kuruhusu hila za Shetani ambazo zilinitesa kufanikiwa. Nilipokuwa nikifikiria kuhusu mawazo haya, nguvu iliibuka ghafla moyoni mwangu nami nikasema kwa uaminifu, “Mnaweza kunipiga hadi nife, lakini bado sijui chochote!” Wakati uo huo, afisa wa polisi wa kike akaingia chumbani. Aliniona na kusema, “Haraka, mteremshe. Mnajaribu kufanya nini, kumuua? Lolote likitendeka kwake ni juu yenu!” Nilijua moyoni mwangu kuwa Mwenyezi Mungu amesikia maombi yangu na Alikuwa amenilinda salama kutokana na madhara wakati huu wa hatari. Wakati polisi wabaya waliponiteremsha kutoka garini, mara nikaanguka chini. Sikuweza kusimama, na mikono na miguu yangu ilikuwa imekufa ganzi kabisa. Sikuwa na nguvu ya kupumua na sikuweza kuihisi mikono na miguu yangu hata kidogo. Nilihisi hofu sana wakati huo na machozi yalitiririka kwa mfululizo kutoka machoni mwangu. Nilifikiria: “Nitaishia kuwa kilema?” Licha ya hayo, hata hivyo, polisi wale waovu hawakuniachilia. Mmoja akiwa upande wangu na mwingine upande mwingine, waliishikilia mikono yangu na kunikokota kama maiti na kunikalisha katika kiti kilichovunjika, na kunisukuma nikikalie. Polisi mmoja kati yao alisema kwa ukali, “Ikiwa haiongei basi mning’inize kwa kamba!” Polisi huyo mwovu akatoa kamba nyembamba ya nailoni haraka sana na kuitumia kuining’iniza mikono yangu iliyotiwa pingu kwenye bomba la kupasha joto. Mikono yangu ilinyooshwa mara moja, na punde si punde mgongo na mabega yangu yakaanza kuhisi uchungu. Polisi wale waovu waliendelea kunihoji, wakiniuliza, “Je, utatueleza kile tunachotaka kujua?” Bado, sikujibu. Walikasirika sana hivi kwamba wakanimwagia kikombe cha maji usoni mwangu, wakisema ilikuwa ni kuniamsha. Kufikia wakati huu, nilikuwa tayari nimeshaumizwa vibaya kufikia kiwango ambacho sikuwa na nguvu hata kidogo, na macho yangu yalikuwa yamechoka kiasi kwamba sikuweza hata kuyafumbua. Mmoja kati ya polisi hao wabaya alipoona kwamba nimekaa kimya, aliyazimisha macho yangu kufunguka kwa mikono yake bila kuona haya ili kunifanyia mzaha. Baada ya kuhojiwa na kuteswa kwa masaa kadhaa, polisi hao waovu walikuwa wameshatumia kila hila walizojua, lakini kwa mara nyigine, jitihada zao za kunifanya niongee ziliambulia patupu.

Polisi wale waovu walipoona kwamba hawangeweza kupata chochote kutoka kwangu kwa kunihoji, waliamua kutumia mpango mwovu sana: Walimwita mtu kutoka jiji aliyejiita “mtaalam wa mahojiano” kuja kunishughulikia. Walinipeleka kwenye chumba kingine na kuniamuru niketi kwenye kiti cha chuma, kisha wakavifunga kwa kukaza vifundo vya miguu yangu kwenye matendegu ya kiti na mikono yangu kwenye mikono ya kiti. Muda mfupi baadaye, mtu mwenye miwani, aliyeonekana muungwana, akaingia akiwa amebeba mkoba. Alinipa tabasamu kubwa sana na, akijifanya kuwa mzuri, aliifungua minyororo iliyokuwa imeishikilia mikono na vifundo vya miguu yangu kwenye kiti na kuniruhusu kukaa kwenye kitanda kidogo katika upande mmoja wa chumba. Mara moja akinimiminia kikombe cha maji, kisha alikuwa akinipa peremende. Alinikaribia na kusema kwa urafiki wa kinafiki, “Mbona uteseke hivi? Umeteseka sana, lakini kwa kweli si neno. Tuambie tunachotaka kujua, na kila kitu kitakuwa sawa….” Nilipokabiliwa na hali hii mpya, sikujua jinsi gani nilivyopaswa kufanya, kwa hivyo nilimwomba Mungu moyoni mwangu kwa haraka na kumwomba Anipe nuru na kuniongoza. Wakati uo huo, nilifikiri kuhusu maneno ya Mwenyezi Mungu: “Lazima uvumilie majaribu yoyote, na kukubali yote yanayotoka kwa Mimi. Lazima ufuate chochote Roho Mtakatifu hufanya ili Akuongoze wewe. Lazima uwe na roho hodari na uwezo wa kutofautisha mambo. Ni lazima uelewe watu na usifuate wengine kwa upofu, weka macho yako ya kiroho nga’vu na umiliki elimu kamilifu ya mambo(Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Matamko ya Kristo Mwanzoni, Sura ya 18). Maneno ya Mungu yalinionyesha njia ya kutenda na kunisaidia kugundua kuwa pepo atakuwa pepo daima, na kwamba pepo hawezi kubadilisha asili yake ya kumpinga na kumchukia Mungu kamwe. Iwapo watatumia mbinu ya kikatili au mbinu ya huruma, lengo lao daima ni kunifanya nimsaliti Mungu na kuiacha na njia ya kweli. Kwa msaada wa onyo la maneno ya Mungu, nikipata utambuzi wa baadhi ya hila za kijanja za Shetani, akili yangu ilifunguka, nami nikaweza kuchukua msimamo thabiti. Kisha mhoji huyo akaniambia, “Serikali ya CCP inawakataza watu kumwamini Mungu. Ikiwa utaendelea kumwamini Mwenyezi Mungu, basi familia yako yote itaingia hatarini, na jambo hilo litaathiri hatima, matarajio ya ajira, na matarajio ya utumishi wa umma kwa watoto katika failia yako. Heri ufikirie kuhusu jambo hili kwa makini….” Baada ya kusema maneno haya, pambano lilianza kutawala ndani mwangu, nami nilihisi kusumbuka sana. Mara tu nilipokuwa nikihisi kupotea, ghafla nilifikiria kuhusu uzoefu wa Petro wakati alipokuwa shahidi mbele ya Shetani; siku zote Petro alijaribu kumwelewa Mungu alipokuwa akipitia kila hila ya ujanja ambayo Shetani alimtupia. Kwa hivyo, ndani ya moyo wangu, nilimwangalia Mungu na kumkabidhi kila kitu, nami nikatafuta mapenzi ya Mungu. Bila kujua, maneno ya Mwenyezi Mungu yalikuja akilini mwangu: “Mungu aliumba dunia hii, Aliumba mwanadamu huyu, na zaidi ya hayo Alikuwa muasisi wa utamaduni wa zamani wa Giriki na ustaarabu wa binadamu. Ni Mungu tu anayemfariji huyu mwanadamu, na ni Mungu tu anayemtunza mwanadamu huyu usiku na mchana. Ukuaji na maendeleo ya binadamu hayatengani na ukuu wa Mungu, na historia na mustakabali wa mwanadamu ni zisizochangulika kutoka kwa miundo ya Mungu. Kama wewe ni Mkristo wa kweli, basi hakika utaamini kwamba kupanda na kushuka kwa nchi ama taifa lolote hufanyika kulingana na miundo ya Mungu. Mungu pekee hujua majaliwa ya nchi ama taifa, na Mungu pekee hudhibiti mwendo wa huyu mwanadamu(Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Kiambatisho 2: Mungu Anaongoza Majaliwa ya Wanadamu Wote). Maneno ya Mungu yalinijaza nuru. “Ndio!” Niliwaza. “Mungu ndiye Muumbaji na hatima yetu kama wanadamu iko mikononi mwa Mungu. ibilisi Shetani ni wa namna ile ya kumpinga Mungu. Ikiwa hawawezi hata kubadilisha majaliwa yao wenyewe ya kuwahukumiwa kuzimu, basi wanawezaje kudhibiti hatima ya mwanadamu? Majaliwa ya mwanadamu yameamuliwa kabla na Mungu, na kazi yoyote ambayo watoto wangu wataweza kufanya katika siku za usoni na jinsi matarajio yao yatakavyokuwa ni juu ya Mungu—Shetani hana uwezo juu ya vitu hivi hata kidogo.” Nilipofikiria kuhusu jambo hili, niliweza kuona wazi kabisa jinsi Shetani na pepo wake walivyo wenye kustahili dharau na wasio na aibu. Ili kunilazimisha nimkane Mungu na kumkataa Mungu, alikuwa akitumia mbinu zenye kudhuru kwa siri na zilizo mbaya—hii “michezo ya kuitesa akili”—ili kunishawisi nidanganywe. Isingelikuwa kwa ajili ya nuru na mwongozo wa Mwenyezi Mungu kwa wakati ufaao, ningekuwa tayari nimeshindwa na kuchukuliwa mateka na Shetani. Sasa kwa kuwa nilijua jinsi Shetani alivyo mwenye kustahili dharau na mwovu, ujasiri wangu wa kuzikubali hila zake za kijanja uliimarika. Mwishowe, polisi huyo mwovu alishindwa na hakujua afanye nini tena, na kwa hivyo aliondoka kwa huzuni kubwa.

Siku ya tatu, mkuu wa polisi aliona kwamba hawakuwa wamepata habari yoyote kutoka kwangu naye akakasirika, akilalamika kuhusu jinsi maafisa wake wa cheo cha chini wasivyojiweza. Alikuja kwangu, na akiwa na tabasamu lisilokuwa na furaha usoni mwake, aliongea kwa kejeli, akisema, “kwanini bado hujakiri? Unafikiri wewe ni nani, Liu Hulan? Unafikiri tayari tumeshafanya mambo yote mabaya kwa hivyo huogopi, eeh? Mbona Mwenyezi Mungu wako haji kukuokoa? …” Alipokuwa akiongea, alinishtua kwa kupeperusha kidude kidogo chenye kuziraisha kwa umeme mbele ya macho yangu ambacho kilitoa sauti na kung'aa kwa taa ya rangi ya samawati, kisha akanionyesha kidude kikubwa chenye kuziraisha kwa umeme ambacho kilikuwa kikichaji na kunishtua, akisema, “Unaona hicho? Kidude hiki kidogo kitaisha chaji hivi punde. Baada ya muda mfupi, nitatumia kidude hicho kikubwa kilichojaa chaji kukupitishia shoti ya umeme, halafu tutaona ikiwa utaongea! Najua utaanza kuongea wakati huo!” Nilikiangalia kidude hicho kikubwa na sikujizuia kuanza kuwa na wasiwasi: “Polisi huyu mwovu ni mkali na katili sana. Je, ataishia kuniua? Nitaweza kuvumilia mateso haya? Je, nitapitishiwa shoti ya umeme hadi nife?” Katika wakati huo, udhaifu, woga, na uchungu na hali ya kutokuwa na msaada nilivyohisi vyote vilijaa akilini mwangu…. Kwa haraka nikamwita Mungu: “Ee Mungu, tafadhali nilinde na unipe imani na nguvu” Kisha, mistari kadhaa kutoka kwa wimbo wa maneno ya Mungu uliingia akilini mwangu: “Imani ni kama daraja moja la gogo la mti, wale ambao hushikilia maisha kwa unyonge watakuwa na ugumu katika kulivuka, lakini wale ambao wako tayari kujitolea wenyewe wanaweza kulivuka bila wasiwasi. Kama mtu ana mawazo ya uoga na ya kuogofya, wao wanadanganywa na Shetani. Ina hofu kwamba tutavuka daraja la imani ili kuingia katika Mungu(“Kuja kwa Magonjwa ni Upendo wa Mungu” katika Mfuateni Mwanakondoo na Kuimba Nyimbo Mpya). Maneno haya ya Bwana Yesu pia yalinijia akilini: “Msiwe na hofu ya wao wanaoua mwili, lakini hawana uwezo wa kuifisha roho: ila heri uwe na hofu ya yeye anayeweza kuiangamiza roho pamoja na mwili katika kuzimu(Mathayo 10:28). Maneno ya Mungu yalisababisha machozi kububujika—nilihisi kuguswa moyo sana. Nguvu iliyokuwa moyoni mwangu ilikuwa kama moto mkali. Nilifikiri, “Hata kama nitakufa leo,” “kuna nini cha kuogopa? Ni jambo la kupendeza kufa kwa ajili ya Mungu, na nitaacha kila kitu ili nipigane na Shetani hadi kufa!” Wakati uo huo, nilikumba mistari kadhaa kutoka katika wimbo mwingine wa maneno ya Mungu: “Alipokuwa njiani kuelekea Yerusalemu, Yesu alihisi maumivu makali, kama kwamba kisu kilikuwa kimedungwa ndani ya moyo Wake, ilhali hakuwa na nia yoyote ya kwenda kinyume cha Neno lake; kila mara kulikuwa na nguvu zenye uwezo mkuu zilizomvutia Yeye kuelekea mahali ambapo Angesulubiwa. Mwishowe, alipigiliwa misumari juu ya msalaba na akawa mfano wa mwili wenye dhambi, akiikamilisha kazi hiyo ya ukombozi wa wanadamu, na kufufuka kutoka kwa pingu za kifo na Kuzimu(“Muige Bwana Yesu” katika Mfuateni Mwanakondoo na Kuimba Nyimbo Mpya). Niliimba na kuimba moyoni mwangu, machozi yalitiririka kwenye mashavu yangu bila kukoma. Mandhari ya Bwana Yesu Kristo akisulubiwa yalionyeshwa mbele ya macho yangu mwenyewe: Bwana Yesu alidharauliwa, akatukanwa na kukashifiwa na Mafarisayo, chakari Wake alimchapa kwa mjeledi wa chuma mpaka Akajawa majeraha na michubuko, hadi mwishowe Akasulubishwa msalabani kikatili, na bado Yeye hakutoa sauti…. Kila kitu ambacho Bwana Yesu alipitia ilikuwa ni kwa ajili ya upendo Wake kwa wanadamu, na upendo huu ulishinda upendo Wake kwa maisha Yake mwenyewe. Wakati huo, moyo wangu ulichochewa na kusisimuliwa na upendo wa Mungu, nami nilijawa na nguvu kubwa na imani nyingi. Sikuwa na hofu ya kitu chochote, nami nilihisi kana kwamba ingependeza kufa kwa ajili ya Mungu, ilhali kuwa Yuda kungekuwa aibu kubwa. Jambo la kushangaza ni kuwa, nilipoamua kuwa shahidi kwa Mungu hata kwa gharama ya maisha yangu mwenyewe, polisi mwovu alikimbilia chumbani mwangu, akisema, “Kuna shida katika uwanja wa jiji, lazima tuhamasishe jeshi la polisi kuikomesha na kudumisha utulivu wa umma!” Polisi waovu wakaenda haraka. Kufikia wakati waliporudi, ilikuwa usiku sana, na hawakuwa na nguvu ya kunihoji tena. Waliniambia kwa ukali, “Kwa kuwa huwezi kuongea, tutakupeleka kizuizini!” Asubuhi ya siku ya nne, polisi waovu walichukua picha yangu na kupachika ishara kubwa ya mraba kwenye shingo langu iliyoandikwa jina langu juu yake kwa kutumia brashi. Nilikuwa kama mhalifu aliyeshutumiwa, nikidharauliwa na kudhihakiwa na wale polisi waovu. Nilihisi kana kwamba ninafedheheshwa vibaya sana, nami nilihisi dhaifu sana moyoni. Niligundua kuwa hali yangu ya akili haikuwa sawa, hata hivyo, na kwa hivyo kwa haraka sana nilimwita Mungu kimyakimya moyoni mwangu: “Ee Mungu! Tafadhali Ulinde moyo wangu na kuniwezesha kuelewa mapenzi Yako na nisinaswe katika mtego wa hila za kijanja za Shetani.” Baada ya kusali, kifungu cha maneno ya Mungu kilitokea akilini mwangu: “Wewe ni kiumbe aliyeumbwa—unapaswa bila shaka kumwabudu Mungu na kufuatilia maisha yenye maana. Usipomwabudu Mungu lakini unaishi ndani ya mwili wako mchafu, basi wewe si mnyama tu aliye ndani ya vazi la mwanadamu? Kwa kuwa wewe ni binadamu, unapaswa kujitumia kwa ajili ya Mungu na kuvumilia kila mateso! Unapaswa kukubali kwa furaha na kwa hakika mateso kidogo unayopitia leo na kuishi maisha yenye maana, kama Ayubu na Petro. … Usipoelewa maana ya maisha au kupata njia ya kweli, basi kuna umuhimu gani katika kuishi kwa namna hii? Ninyi ni watu mnaofuatilia njia sahihi, wale mnaotafuta maendeleo. Ninyi ni watu ambao huinuka katika nchi ya joka kuu jekundu, wale ambao Mungu huwaita wenye haki. Je, hayo si maisha yenye maana zaidi?(Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Utendaji (2)). Maneno ya Mungu yaliniwezesha kuelewa kwamba, kuweza kuufuatilia ukweli kama kiumbe aliyeumbwa, na kuishi ili kumwabudu Mungu na kumridhisha Mungu, kulikuwa maisha yenye kusudi na yenye maana zaidi. Kuweza kukamatwa leo na kuwekwa kizuizini kwa ajili ya imani yangu katika Mungu, kupitia aibu na maumivu haya yote, na kuweza kushiriki katika dhiki ya Kristo, halikuwa jambo la aibu, lakini la kupendeza. Shetani hamwabudu Mungu; badala yake, yeye hufanya yote awezayo kuingilia kati na kuizuia kazi ya Mungu, na hili ndilo jambo lenye kuaibisha na lenye kustahili dharau zaidi. Nilipokuwa nikifikiria mawazo haya, nilijazwa nguvu na furaha. Polisi wale wabaya waliona tabasamu usoni mwangu na kuniangalia kwa mshangao, na wakasema, “Unafurahia nini?” Nilijibu kwa haki na kwa nguvu, “Ni sawa kabisa kmwamini Mungu na kumwabudu Mungu. Hakuna chochote kibaya katika kufanya hivyo. Mbona nisifurahi?” Kusikia maneno haya, hawakusema chochote. Chini ya mwongozo wa maneno ya Mungu, niliweza tena kumtegemea Mungu ili nimshinde Shetani.

Kisha nikapelekwa kizuizini. Kila kitu mahali hapo kilikuwa cha kuhuzunisha na cha kutisha hata zaidi, nami nilihisi kana kwamba nimeingia katika kuzimu ya aina fulani. Kwa kila mlo, nilipewa kipande kidogo cheusi cha mkate uliookwa kwa mvuke na kabichi za Kichina zilizochemshwa kwenye bakuli la supu na majani machache ya mboga yaliyoelea juu. Nilikuwa na njaa sana siku nzima kila siku, tumbo langu lilikuwa likitoa sauti kwa sababu ya njaa. Licha ya haya, hata hivyo, bado ilibidi nifanye kazi kama mnyama wa kubeba mizigo, na ikiwa sikutimiza fungu la kazi nililogawiwa, nilipigwa au kulazimishwa kuwa mlinzi kama adhabu. Kwa sababu udhalilishaji huu wa kikatili uliendelea kwa siku nyingi, nilikuwa nimeumia na kujeruhiwa kutoka kichwani hadi vidoleni, na ikawa vigumu hata kutembea, lakini bado waangalizi walinilazimisha kubeba mizigo mizito ya nyaya za shaba. Kwa sababu ya kazi hii nzito, mgongo wangu uliokuwa umeumia ulikuwa na maumivu makali sana, mwishoni mwa kila siku niliweza tu kujikokota hadi kitandani mwangu. Lakini wakati wa usiku, polisi waovu wangenifanya niwalinde wafungwa pia, nami sikuweza kuvumilia kazi hii ya ziada na ya kuchosha. Usiku mmoja wakati nilipokuwa kwenye zamu ya ulinzi, nilichukua fursa ya kutokuwepo kwa polisi waovu na, kwa utulivu, nilijikunyata, nikitarajia kupumzika. Hata hivyo, ghafla, polisi mmoja mwovu aliniona kwenye kamera iliyo katika chumba cha upelelezi naye akanijia kwa nguvu akinguruma, “Nani alisema unaweza kuketi?” Mmoja wa wafungwa wengine alininong’onezea, “Harakisha umwombe msamaha, la sivyo atakulazimisha’ ‘ulale kwenye kitanda cha mbao.’” Kwa kusema hivi, alimaanisha mateso ambapo ubao wa mlango wa mbao unawekwa ndani ya seli ya mfungwa, miguu yake inafungwa kwenye ubao huo, na vifundo vya mikono yake vinafungwa kwenye ubao huo. Kisha mfungwa huyo anafungwa kwenye ubao huo, na hawaruhusiwi kusongaa tena kwa muda wa wiki mbili. Niliposikia hivi, nilijawa na hasira na chuki kwa wakati mmoja, lakini nilijua kuwa singeweza kuonyesha upinzani hata kidogo—niliizuia hasira yangu tu na kukaa kimya. Niliona vigumu kuvumilia unyanyasaji na mateso kama hayo. Usiku huo, nililala katika kitanda changu kilichokuwa baridi sana na kulia kuhusu ukosefu wa haki kwa ajili ya mambo yote hayo, moyo wangu ulijawa malalamiko na madai kwa Mungu, nikifikiri: “Haya yataisha lini? Siku moja tu katika mahali hapa pabaya mno ni siku nyingi sana.” Kisha nikawazia maneno ya Mungu: “Ikiwa unaelewa umuhimu wa maisha ya binadamu na umechukua njia inayofaas ya maisha ya mwanadamu na ikiwa katika siku za usoni utatii miundo Yake bila malalamiko yoyote au chaguo bila kujali jinsi Mungu anavyokushughulikia, na ikiwa hufanyi madai yoyote kwa Mungu, basi kwa njia hii wewe utakuwa mtu wa thamani(Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Jinsi Unavyopaswa Kuitembea Sehemu ya Mwisho ya Njia). Maneno ya Mungu yalinifanya nijionee aibu. Nilifikiria jinsi nilivyosema kila wakati kuwa nitatafuta kumtii Mungu kama Peter alivyofanya, maumivu au shida ziwe nyingi kiasi gani, na kwamba sitafanya maamuzi au madai kwa ajili yangu mwenyewe. Mateso na shida ziliponipata, hata hivyo, na ikanibidi kuteseka na kulipa gharama, nilijaribu kufikiria kuhusu namna ya kutoka. Sikuwa na utii hata kidogo! Ni wakati huo tu ndipo mwishowe nilipoelewa nia njema za Mungu: Mungu alikuwa Akiruhusu shida hii inipate ili aimarishe azimio langu la kuvumilia mateso, na kuniwezesha kujifunza jinsi ya kutii katika mateso yangu, ili niweze kuitii mipango ya Mungu na kuwa na sifa ya kupokea ahadi Yake. Kila kitu ambacho Mungu alikuwa Akinifanyia kilikuwa kikifanywa kwa upendo, na kilikuwa kikifanywa ili kuniokoa, Moyo wangu ulikombolewa baadaye, na sikuhisi tena au kuwa nimekosewa au kuumizwa. Nilitaka tu kutii mipango na utaratibu wa Mungu, kumtolea ushuhuda na kumdhalilisha shetani.

Mwezi mmoja baadaye, niliachiliwa. Hata hivyo, walinibandikia hatia ya “kuvuruga utekelezaji wa sheria na kushiriki katika shirika la Xie Jiao” ili kuzuia uhuru wangu wa kibinafsi. Kwa mwaka mmoja, sikuruhusiwa kutoka katika mkoa au manispaa, na ilibidi nitii amri wakati wowote polisi waliponihitaji. Ni baada tu ya kurudi nyumbani ndipo nilipogundua kuwa mali yote ambayo nilikuwa nimeiweka nyumbani ilikuwa imeibiwa na kuchukuliwa na polisi. Kando na hayo, polisi hao waovu walikuwa wameipekua nyumba yangu kama wanyang’anyi, na walikuwa wameitishia familia yangu, wakisema kwamba lazima watoe zaidi ya yuani 25,000 kabla ya kuniachilia. Mama-mkwe wangu hakuweza kustahimili hofu ya hayo yote na akapatwa na mshtuko wa moyo, na alipona tu baada ya kulazwa hospitalini na kupokea matibabu, kwa gharama ya zaidi ya yuani 2,000. Mwishowe, familia yangu ililazimika kumwomba kila mtu wanayemjua awape mkopo wa pesa ili waweze kukusanya kwa shida yuani 3,000 wawape polisi, na ni wakati huo tu ndipo tu nilipoachiliwa. Kwa sababu ya mateso ya kikatili niliyotendewa na hao polisi waovu, mwili wangu umebaki ukiteseka kwa ajili ya athari kali: Mara nyingi mikono na miguu yangu huvimba na kuuma kwa sababu ya dhiki kali iliyopitia wakati wa kifungo changu; Siwezi hata kuinua kilo mbili na nusu za mboga au kuosha nguo zangu, na nimepoteza kabisa uwezo wa kufanya kazi. Mateso ya kikatili yaliyosababishwa na serikali ya CCP yamenifanya nimchukie Shetani hata zaidi—namchukia huyu Shetani mpinga maendeleo, Shetani anayeidharau Mbingu.

Uzoefu huo wa kukamatwa na kuteswa ulinipa mtazamo wazi wa Chama cha Kikomunisti, kuhusu sura yake mbaya, ya kipepo ambayo huchukia ukweli na kumchukia Mungu. Iliongeza chuki yangu kwa Shetani na kwa chama cha mapepo, cha Kikomunisti cha Wachina ambacho kiko kinyume kabisa na Mbingu. Pia nilikuwa na uzoefu wa kweli, wa kibinafsi wa jinsi kazi ya Mungu ni ya vitendo na hekima. Kukamatwa na kuteswa na Chama cha Kikomunisti kuliendeleza utambuzi wangu; pia ilidhoofisha azimio langu na kukamilisha imani yangu, ikiniruhusu kujifunza jinsi ya kumtazama na kumtegemea Mungu. Pia nilipata ladha ya ukuu na mamlaka ya maneno ya Mungu, nikiona kuwa zinaweza kuwa chanzo cha msaada ambacho kila wakati ni pande zetu. Niliona kuwa ni Mungu tu anayempenda mwanadamu na ni Mungu tu ndiye anayeweza kumwokoa mwanadamu. Nilikua karibu na Mungu moyoni mwangu. Nilivuna thawabu hizi zote kutokana na kupitia shida na majaribu. Ninamshukuru Mungu!

Iliyotangulia: 81. Mateso na Majaribio Ni Baraka za Mungu

Inayofuata: 83. Kushinda Kupitia Majaribu ya Shetani

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Maudhui Yanayohusiana

1. Nimebahatika Kumhudumia Mungu

Na Gensui, Korea ya KusiniMwenyezi Mungu anasema, “Ni kupitia nini ndiyo ukamilishaji wa Mungu kwa mwanadamu hutimizwa? Kupitia tabia Yake...

31. Kushikilia Wajibu Wangu

Na Yangmu, Korea ya KusiniNilikuwa nikihisi wivu sana nilipowaona ndugu wakifanya maonyesho, wakiimba na kucheza kwa kumsifu Mungu....

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp