Ijue Kazi Mpya Kabisa ya Mungu na Ufuate Hatua Zake

Sasa, mnapaswa kufuatilia kuwa watu wa Mungu, na mtaanza kuingia kwenye njia sahihi katika mambo yote. Kuwa watu wa Mungu kunamaanisha kuingia katika Enzi ya Ufalme. Leo, mnaanza rasmi kuingia katika mafunzo ya ufalme, na maisha yenu ya baadaye yatakoma kuwa yaliyolegea na ya uzembe kama yalivyokuwa hapo awali; mkiishi kwa njia hiyo, haiwezekani kufikia viwango vinavyotakiwa na Mungu. Ikiwa huhisi haraka yoyote, basi hii inaonyesha kwamba huna hamu ya kufanya maendeleo, kwamba ufuatiliaji wako umekanganyika na hauna mpangilio, na hauwezi kuridhisha nia za Mungu. Kuingia katika mafunzo ya ufalme kunamaanisha kuanza maisha ya watu wa Mungu—je, uko tayari kukubali mafunzo kama hayo? Je, uko tayari kuwa na hisia ya haraka? Je, uko tayari kuishi chini ya adabu ya Mungu? Je, uko tayari kuishi chini ya kuadibu kwa Mungu? Maneno ya Mungu yanapokujia na kukujaribu, utatendaje? Na utafanya nini unapokabiliwa na kila aina ya ukweli wa mambo? Katika wakati uliopita, hamkuzingatia maisha; leo, lazima mzingatie kuingia katika uhalisi wa maisha, na mfuatilie mabadiliko katika tabia yenu ya maisha. Hiki ndicho kinachopaswa kufikiwa na watu wa ufalme. Wale wote ambao ni watu wa Mungu lazima wawe na uzima, lazima wakubali mafunzo ya ufalme, na wafuatilie mabadiliko katika tabia yao ya maisha. Hiki ndicho ambacho Mungu anahitaji kutoka kwa watu wa ufalme.

Mahitaji ya Mungu kwa watu wa ufalme ni kama yafuatavyo:

1. Lazima wakubali maagizo ya Mungu. Yaani, lazima wakubali maneno yote yaliyonenwa katika kazi ya Mungu ya siku za mwisho.

2. Lazima waingie katika mafunzo ya ufalme.

3. Lazima wafuatilie ili mioyo yao iguswe na Mungu. Moyo wako unapomgeukia Mungu kikamilifu, na una maisha ya kawaida ya kiroho, utaishi katika ulimwengu wa uhuru, jambo ambalo linamaanisha utaishi chini ya utunzaji na ulinzi wa upendo wa Mungu. Ni ikiwa tu unaishi chini ya utunzaji na ulinzi wa Mungu ndiyo wewe ni mtu ambaye amechaguliwa na Mungu.

4. Lazima wapatwe na Mungu.

5. Lazima wawe udhihirisho wa utukufu wa Mungu duniani.

Mambo haya matano ni maagizo Yangu kwenu. Maneno Yangu yananenwa kwa watu wa Mungu, na ikiwa hauko tayari kukubali maagizo haya, Sitakulazimisha—lakini ukiyakubali kwa kweli, basi utaweza kufuata mapenzi ya Mungu. Leo, mnaanza kukubali maagizo ya Mungu, na kufuatilia kuwa watu wa ufalme na kufikia viwango vinavyohitajika kuwa watu wa ufalme. Hii ndiyo hatua ya kwanza ya kuingia. Ikiwa unataka kufuata mapenzi ya Mungu kikamilifu, basi lazima ukubali maagizo haya matano, na ikiwa unaweza kuyafikia, utakuwa unalingana na nia za Mungu na hakika Mungu atakutumia kwa kiasi kikubwa. Jambo la muhimu leo ni kuingia katika mafunzo ya ufalme. Kuingia katika mafunzo ya ufalme kunahusisha maisha ya kiroho. Hapo awali, hakukuwa na mazungumzo kuhusu maisha ya kiroho, lakini leo, mnapoanza kuingia katika mafunzo ya ufalme, mnaingia rasmi katika maisha ya kiroho.

Maisha ya kiroho ni maisha ya aina gani? Maisha ya kiroho ni yale ambayo moyo wako umemgeukia Mungu kikamilifu, na unaweza kufikiria upendo wa Mungu. Ni yale ambayo unaishi katika maneno ya Mungu, na hakuna kingine kinachochukua nafasi moyoni mwako, na unaweza kushika nia za sasa za Mungu, na unaongozwa na nuru ya sasa ya Roho Mtakatifu ili kutekeleza wajibu wako. Maisha kama haya kati ya mwanadamu na Mungu ndiyo maisha ya kiroho. Ikiwa huwezi kufuata nuru ya sasa, basi uhusiano wako na Mungu utafifia—unaweza hata kufikia kikomo—nawe utakuwa bila maisha ya kawaida ya kiroho. Uhusiano wa kawaida na Mungu unajengwa juu ya msingi wa kukubali maneno ya sasa ya Mungu. Je, una maisha ya kawaida ya kiroho? Je, una uhusiano wa kawaida na Mungu? Je, wewe ni mtu anayefuata kazi ya Roho Mtakatifu? Ikiwa unaweza kufuata nuru ya sasa ya Roho Mtakatifu, na unaweza kushika nia za Mungu ndani ya maneno Yake, na unaingia katika maneno Yake, basi wewe ni mtu anayefuata mkondo wa Roho Mtakatifu. Ikiwa hufuati mkondo wa Roho Mtakatifu, basi bila shaka wewe ni mtu asiyefuatilia ukweli. Roho Mtakatifu hana nafasi ya kufanya kazi ndani ya wale ambao hawana matamanio ya kufanya maendeleo, na matokeo yake, watu kama hao hawawezi kamwe kukusanya nguvu zao, na daima ni hasi. Leo, je, unafuata mkondo wa Roho Mtakatifu? Je, uko katika mkondo wa Roho Mtakatifu? Je, umeibuka kutoka katika hali hasi? Wale wote wanaoamini katika maneno ya Mungu, wanaochukua kazi ya Mungu kama msingi, na kufuata nuru ya sasa ya Roho Mtakatifu—wote wako katika mkondo wa Roho Mtakatifu. Ikiwa unaamini kwamba maneno ya Mungu ni ya kweli na sahihi bila shaka yoyote, na ikiwa unaamini maneno ya Mungu bila kujali Anachosema, basi wewe ni mtu anayefuatilia kuingia katika kazi ya Mungu, na kwa njia hii unaridhisha nia za Mungu.

Ili kuingia katika mkondo wa Roho Mtakatifu, lazima uwe na uhusiano wa kawaida na Mungu, na lazima kwanza utupe mbali hali yako hasi. Watu wengine daima hufuata umati, na mioyo yao hupotoka mbali sana na Mungu; watu kama hao hawana hamu ya kufanya maendeleo, na viwango wanavyofuatilia ni vya chini sana. Ni ufuatiliaji wa kumpenda Mungu na kupatwa na Mungu tu ndio nia ya Mungu. Kuna watu wanaotumia dhamiri zao tu kulipa upendo wa Mungu, lakini hii haiwezi kufikia nia za Mungu; kadiri viwango unavyofuatilia vinavyokuwa vya juu, ndivyo vitakavyolingana zaidi na nia za Mungu. Kama watu wa kawaida, na kama watu wanaotafuta kumpenda Mungu, kuingia katika ufalme na kuwa watu wa Mungu ndio mustakabali wenu wa kweli, na maisha ambayo ni ya thamani na umuhimu mkubwa kabisa; hakuna aliyebarikiwa zaidi yenu. Kwa nini Ninasema hivi? Kwa sababu wale wasiomwamini Mungu wanaishi kwa ajili ya mwili, na wanaishi kwa ajili ya Shetani, lakini leo ninyi mnaishi kwa ajili ya Mungu, na mnaishi ili kufuata mapenzi ya Mungu. Hiyo ndiyo maana Ninasema maisha yenu ni yenye umuhimu mkubwa kabisa. Ni kundi hili tu la watu, ambao wamechaguliwa na Mungu, ndio wanaoweza kuishi kwa kudhihirisha maisha yenye umuhimu mkubwa kabisa: Hakuna mtu mwingine duniani anayeweza kuishi kwa kudhihirisha maisha ya thamani na maana kama yenu. Kwa sababu mmechaguliwa na Mungu, na mmeinuliwa na Mungu, na zaidi sana kwa sababu ya upendo wa Mungu, mmeshika maisha ya kweli, na mnajua jinsi ya kuishi kwa njia ambayo ni ya thamani kubwa kabisa. Hii si kwa sababu mnafuatilia vizuri, bali ni kwa sababu ya neema ya Mungu; ni Mungu aliyefumbua macho yenu ya kiroho, na ni Roho wa Mungu aliyegusa mioyo yenu, akiwapa bahati nzuri ya kuja mbele Yake. Roho wa Mungu asingewatia nuru, basi msingeweza kuona kile kinachopendeza kuhusu Mungu, wala isingewezekana kwenu kumpenda Mungu. Ni kwa sababu Roho wa Mungu amegusa mioyo ya watu kikamilifu ndiyo mioyo yao imemgeukia Mungu. Wakati mwingine, unapofurahia maneno ya Mungu, roho yako inaguswa, na unahisi kwamba lazima kabisa umpende Mungu, kwamba kuna nguvu kubwa ndani yako, na kwamba hakuna kitu ambacho huwezi kuweka kando. Ukihisi namna hii, basi umeguswa na Roho wa Mungu, na moyo wako umemgeukia Mungu kikamilifu, nawe utamwomba Mungu na kusema: “Mungu! Kwa kweli tumeamuliwa kabla na kuchaguliwa na Wewe. Utukufu Wako unanipa fahari, na ninahisi ni heshima kuwa mmoja wa watu Wako. Nitajitumia kwa chochote na kutoa chochote ili kufuata mapenzi Yako, na nitatoa miaka yangu yote, na nguvu zote nilizo nazo katika maisha haya, Kwako.” Unapoomba namna hii, kutakuwa na upendo usio na kikomo na utii wa kweli kwa Mungu moyoni mwako. Je, umewahi kuwa na uzoefu kama huu? Ikiwa watu mara nyingi wanaguswa na Roho wa Mungu, basi watatoa maombi ya kujitolea hasa kwa Mungu: “Mungu! Ninatamani kuona siku ambayo Unapata utukufu, na ninatamani kuishi kwa ajili Yako—hakuna kitu kinachostahili au chenye maana zaidi kuliko kuishi kwa ajili Yako, na sina hamu hata kidogo ya kuishi kwa ajili ya Shetani na mwili. Unaniinua kwa kuniwezesha niishi kwa ajili Yako leo.” Unapoomba kwa namna hii, utahisi kwamba lazima kabisa umpe Mungu moyo wako, kwamba lazima umpate Mungu, na kwamba ungechukia kufa bila kumpata Mungu ukiwa hai. Baada ya kuomba ombi kama hilo, nguvu huongezeka ndani yako isiyoisha, nawe hutajua inatoka wapi; moyoni mwako kutakuwa na nguvu isiyo na kikomo, na utakuwa na hisia kwamba Mungu ni mzuri sana, na kwamba Yeye anastahili kupendwa. Huu ndio wakati ambapo utakuwa umeguswa na Mungu. Wale wote ambao wamekuwa na uzoefu kama huo wameguswa na Mungu. Kwa wale ambao mara nyingi wanaguswa na Mungu, mabadiliko hutokea katika uzima wao, wanaweza kuazimia kumpata Mungu kikamilifu, mioyo yao impendayo Mungu ni yenye nguvu kiasi, na mioyo yao imemgeukia Mungu kikamilifu. Wanaondoa familia zao, ulimwengu, mambo yanayowatatiza, na matarajio yao kikamilifu kutoka mawazoni mwao, na wako tayari kutoa nguvu zote walizo nazo maishani kwa Mungu. Wale wote wanaoguswa na Roho wa Mungu ni watu wanaofuatilia ukweli, na ambao wana tumaini la kufanywa kuwa watimilifu na Mungu.

Je, umemgeukia Mungu moyoni mwako? Je, moyo wako umeguswa na Roho wa Mungu? Ikiwa hujawahi kuwa na upitiaji kama huo, na ikiwa hujawahi kuomba kwa namna hiyo, basi hili linaonyesha kwamba Mungu hana nafasi moyoni mwako. Wale wote wanaoongozwa na Roho wa Mungu na wanaoguswa na Roho wa Mungu wana kazi ya Mungu, jambo ambalo linaonyesha kwamba maneno ya Mungu na upendo wa Mungu vimekita mizizi ndani yao. Watu wengine husema: “Mimi si mwenye bidii kama wewe katika maombi yangu, wala siguswi sana na Mungu; wakati mwingine—ninapotafakari na kuomba—ninahisi kwamba Mungu ni mzuri, na moyo wangu unaguswa na Mungu.” Hakuna kitu kilicho muhimu zaidi ya moyo wa mwanadamu. Moyo wako unapomgeukia Mungu, nafsi yako yote itakuwa imemgeukia Mungu, na wakati huo moyo wako utakuwa umeguswa na Roho wa Mungu. Wengi kabisa miongoni mwenu wamekuwa na uzoefu kama huo—ni kwamba tu vina vya uzoefu wenu havilingani. Watu wengine husema: “Sisemi maneno mengi ya maombi, ninasikiliza tu ushirika wa wengine na nguvu huongezeka ndani yangu.” Hili linaonyesha kwamba umeguswa na Mungu kwa ndani. Watu wanaoguswa na Mungu kwa ndani hutiwa moyo wanaposikia ushirika wa wengine; moyo wa mtu ukibaki bila kuguswa kabisa anaposikia maneno ya kutia moyo, basi hili linathibitisha kwamba kazi ya Roho Mtakatifu haiko ndani yake. Hakuna shauku ndani yake, jambo ambalo linathibitisha kwamba hana azimio, na hivyo hana kazi ya Roho Mtakatifu. Ikiwa mtu ameguswa na Mungu, atakuwa na mjibizo anaposikia maneno ya Mungu. Ikiwa mtu hajaguswa na Mungu, hataweza kujihusisha na maneno ya Mungu; maneno ya Mungu hayatakuwa na uhusiano wowote naye, na hatapokea nuru yoyote. Wale ambao wamesikia maneno ya Mungu na hawakuwa na mjibizo wowote ni watu ambao hawajaguswa na Mungu—ni watu ambao hawana kazi ya Roho Mtakatifu. Wale wote wanaoweza kukubali nuru mpya wameguswa, na wana kazi ya Roho Mtakatifu.

Jipime:

Je, uko katikati ya kazi ya wakati wa sasa ya Roho Mtakatifu?

Je, moyo wako umemgeukia Mungu? Je, umeguswa na Mungu?

Je, maneno ya Mungu yamekita mizizi ndani yako?

Je, utendaji wako umejengwa juu ya msingi wa matakwa ya Mungu?

Je, unaishi chini ya mwongozo wa nuru ya wakati wa sasa ya Roho Mtakatifu?

Je, moyo wako unatawaliwa na dhana za zamani, au unatawaliwa na maneno ya sasa ya Mungu?

Mkisikia maneno haya, kuna mjibizo gani ndani yenu? Baada ya kuamini kwa miaka yote hii, je, mna maneno ya Mungu kama uzima wenu? Je, kumekuwa na mabadiliko katika tabia yako potovu ya hapo awali? Je, wewe, kulingana na maneno ya sasa ya Mungu, unajua maana ya kuwa na uzima, na maana ya kuwa bila uzima? Je, hili liko wazi kwenu? Jambo la muhimu kabisa katika kumfuata Mungu ni kwamba kila kitu kinapaswa kuwa kulingana na maneno ya sasa ya Mungu: Uwe unafuatilia kuingia katika uzima au kuridhisha nia za Mungu, kila kitu kinapaswa kujikita katika maneno ya sasa ya Mungu. Ikiwa kile unachoshiriki na kutafuta kuingia katika hakina kitovu chake katika maneno ya sasa ya Mungu, basi wewe ni mtu aliye nje ya maneno ya Mungu, na hakika huna kazi ya Roho Mtakatifu. Kile ambacho Mungu anataka ni watu wanaofuata hatua Zake. Haijalishi kile ulichoelewa hapo awali ni cha ajabu na safi kiasi gani, Mungu hakitaki, na ikiwa huwezi kuweka kando mambo kama hayo, basi yatakuwa kikwazo kikubwa kwa kuingia kwako katika siku za usoni. Wale wote wanaoweza kufuata nuru ya Roho Mtakatifu ya leo wamebarikiwa. Watu wa enzi na vizazi vilivyopita pia walifuata hatua za Mungu, lakini hawakuweza kuendelea kufuata hadi leo; hii ni baraka ya watu wa siku za mwisho. Wale wanaoweza kufuata kazi ya wakati wa sasa ya Roho Mtakatifu, na wanaoweza kufuata hatua za Mungu, wakimfuata Mungu popote Anapowaongoza—hawa ni watu ambao wamebarikiwa na Mungu. Wale wasiofuata kazi ya sasa ya Roho Mtakatifu hawajaingia katika kazi ya maneno ya Mungu, na haijalishi wanafanya kazi kiasi gani, au mateso yao ni makubwa kiasi gani, au wanazunguka huku na kule kiasi gani, hakuna hata moja kati ya hayo yenye maana yoyote kwa Mungu, na Yeye hatawakubali. Leo, wale wote wanaofuata maneno ya sasa ya Mungu wako katika mkondo wa Roho Mtakatifu; wale walio nje ya maneno ya sasa ya Mungu wako nje ya mkondo wa Roho Mtakatifu, na watu kama hao hawakubaliwi na Mungu. Huduma iliyo nje ya maneno ya sasa ya Roho Mtakatifu ni huduma ya mwili, na ya dhana, na haiwezekani iwe kulingana na nia za Mungu. Watu wakiishi katikati ya dhana za kidini, basi hawawezi kufanya chochote ambacho kinalingana na nia za Mungu, na hata wakimtumikia Mungu, wanatumikia katikati ya mawazo na dhana zao, na hawawezi kabisa kutumikia kulingana na nia za Mungu. Wale ambao hawawezi kufuata kazi ya Roho Mtakatifu hawaelewi nia za Mungu, na wale ambao hawaelewi nia za Mungu hawawezi kumtumikia Mungu. Mungu anataka huduma inayolingana na nia Zake; Hataki huduma ya dhana na ya mwili. Ikiwa watu hawawezi kufuata hatua za kazi ya Roho Mtakatifu, basi wanaishi katikati ya dhana. Huduma ya watu kama hao inavuruga na kusumbua, na huduma kama hiyo inakwenda kinyume na Mungu. Hivyo wale ambao hawawezi kufuata hatua za Mungu hawawezi kumtumikia Mungu; wale ambao hawawezi kufuata hatua za Mungu hakika wanampinga Mungu, na hakika hawawezi kulingana na Mungu. “Kufuata kazi ya Roho Mtakatifu” kunamaanisha kuelewa nia za sasa ya Mungu, na kuweza kutenda kulingana na mahitaji ya wakati wa sasa ya Mungu, kumtii na kumfuata Mungu wa wakati wa sasa, na kuingia kulingana na maneno mapya kabisa ya Mungu. Huyu tu ndiye mtu anayefuata kazi ya Roho Mtakatifu na yuko katika mkondo wa Roho Mtakatifu. Watu kama hao hawawezi tu kupokea kibali cha Mungu na kumwona Mungu, bali pia wanaweza kujua tabia ya Mungu kutokana na kazi mpya zaidi ya Mungu, na wanaweza kujua dhana na uasi wa mwanadamu, na asili na kiini cha mwanadamu, kutokana na kazi Yake mpya kabisa; zaidi ya hayo, wanaweza kufikia mabadiliko katika tabia yao hatua kwa hatua wakati wa huduma yao. Watu kama hawa tu ndio wanaoweza kumpata Mungu, na ambao wamepata njia ya kweli kwa dhati. Wale wanaoondoshwa na kazi ya Roho Mtakatifu ni watu ambao hawawezi kufuata kazi mpya kabisa ya Mungu, na ambao wanakuwa wahasama dhidi ya kazi mpya kabisa ya Mungu. Kwamba watu kama hao wanampinga Mungu waziwazi ni kwa sababu Mungu amefanya kazi mpya, na kwa sababu mfano wa Mungu si sawa na ule ulio katika dhana zao—kutokana na hili, wanampinga Mungu waziwazi na kumhukumu Mungu, jambo ambalo linasababisha Mungu kuwabeua. Kuwa na maarifa ya kazi mpya kabisa ya Mungu si jambo rahisi, lakini watu wakiweza kutii kazi ya Mungu kwa makusudi na watafute kazi ya Mungu, basi watakuwa na nafasi ya kumwona Mungu, na watakuwa na nafasi ya kupata mwongozo mpya kabisa wa Roho Mtakatifu. Wale wanaopinga kazi ya Mungu kwa makusudi hawawezi kupokea nuru ya Roho Mtakatifu au mwongozo wa Mungu. Hivyo, kama watu wanaweza kupokea kazi mpya kabisa ya Mungu au la kunategemea neema ya Mungu, pamoja na ufuatiliaji wao na nia zao.

Wote wanaoweza kutii maneno ya sasa ya Roho Mtakatifu wamebarikiwa. Haijalishi watu walikuwaje hapo awali, au jinsi Roho Mtakatifu alivyokuwa akifanya kazi ndani yao—wale wote ambao wamepata kazi mpya kabisa ya Mungu ndio waliobarikiwa kabisa, na wale wote ambao hawawezi kufuata kazi mpya kabisa katika wakati wa sasa wataondoshwa. Mungu anawataka wale wanaoweza kukubali nuru mpya, na Anawataka wale wanaokubali na kujua kazi Yake mpya kabisa. Kwa nini inasemwa kwamba lazima uwe bikira safi? Bikira safi anaweza kutafuta kazi ya Roho Mtakatifu na kuelewa mambo mapya, na zaidi ya hayo, anaweza kuweka kando dhana za zamani, na kutii kazi ya Mungu leo. Kundi hili la watu, wanaokubali kazi mpya kabisa ya leo, waliamuliwa kabla na Mungu kabla ya enzi, na ndio watu waliobarikiwa kabisa. Mnaisikia sauti ya Mungu moja kwa moja, na mnaona kuonekana kwa Mungu, na hivyo, katika mbingu na ardhi yote, na katika enzi na vizazi vyote, hakuna aliyebarikiwa zaidi ya nyinyi, kundi hili la watu. Haya yote ni kwa sababu ya kazi ya Mungu, kwa sababu ya uamuzi kabla na uteuzi wa Mungu, na kwa sababu ya neema ya Mungu; Mungu asingenena na kutamka maneno Yake, je, hali zenu zingeweza kuwa kama zilivyo leo? Hivyo, utukufu na sifa zote ziwe kwa Mungu, kwa maana haya yote ni kuinuliwa na Mungu. Ukiwa na mambo haya akilini, je, bado unaweza kuwa hasi? Je, nguvu zako bado zinaweza kushindwa kuongezeka?

Kwamba leo unaweza kukubali hukumu, kuadibu, kupiga, na usafishaji wa maneno ya Mungu, na zaidi sana kuweza kukubali maagizo ya Mungu, kuliamuliwa kabla na Mungu kabla ya enzi, na hivyo hupaswi kuhuzunika sana unapoadibiwa. Hakuna anayeweza kuondoa kazi ambayo imefanywa kwenu, na baraka ambazo mmepewa, na hakuna anayeweza kuondoa yote ambayo mmepewa. Watu wa dini hawawezi kustahimili kulinganishwa nanyi. Hamna maarifa mengi ya Biblia kama wao, na hamna mafundisho ya kidini waliyo nayo, lakini kwa sababu Mungu amefanya kazi kwenu, mmepata mengi zaidi kuliko mtu yeyote katika enzi zote—na hivyo hii ni baraka yenu kuu zaidi. Kwa sababu ya hili, lazima mjitoe zaidi kwa Mungu na muwe waaminifu kwa Mungu. Kwa sababu ya kuinuliwa na Mungu, lazima uongeze juhudi zako, na lazima uandae kimo chako ili kukubali maagizo ya Mungu. Kusimama imara katika nafasi uliyopewa na Mungu; kufuatilia kuwa mmoja wa watu wa Mungu; kukubali mafunzo ya ufalme; kupatwa na Mungu na hatimaye kuwa ushuhuda mtukufu kwa Mungu—je, una maazimio haya? Ikiwa una maazimio kama haya, basi hatimaye hakika utapatwa na Mungu, na utakuwa ushuhuda mtukufu kwa Mungu. Unapaswa kuelewa kwamba agizo kuu ni kupatwa na Mungu na kuwa ushuhuda mtukufu kwa Mungu. Hii ndiyo nia ya Mungu.

Maneno ya sasa ya Roho Mtakatifu ni elimumwendo ya kazi ya Roho Mtakatifu, na kuwatia nuru watu kwa kuendelea kwa Roho Mtakatifu katika kipindi hiki ni mwelekeo wa kazi ya Roho Mtakatifu. Na mwelekeo wa kazi ya Roho Mtakatifu leo ni upi? Ni kuwaongoza watu wa Mungu katika kazi ya sasa ya Mungu, na katika maisha ya kawaida ya kiroho. Kuna hatua kadhaa za kuingia katika uzima wa kawaida wa kiroho:

1. Kwanza, lazima uweke moyo wako katika maneno ya Mungu. Hupaswi kufuatilia maneno ambayo Mungu alizungumza hapo awali, na hupaswi kuyachunguza, sembuse kuyalinganisha na maneno ya leo. Badala yake, lazima uweke moyo wako kikamilifu katika maneno ya sasa ya Mungu. Ikiwa kuna watu ambao bado wangependa kusoma maneno ya Mungu, vitabu vya kiroho, au mahubiri mengine ya zamani, na ambao hawafuati maneno ya sasa ya Roho Mtakatifu, basi wao ni watu wapumbavu kabisa; Mungu anawachukia watu kama hao. Ikiwa uko tayari kukubali nuru ya sasa ya Roho Mtakatifu, basi weka moyo wako kikamilifu katika maneno ya sasa ya Mungu. Hili ndilo jambo la kwanza ambalo lazima ufikie.

2. Lazima uombe juu ya msingi wa maneno ya sasa yaliyonenwa na Mungu, uingie katika maneno ya Mungu na ushiriki na Mungu, na ufanye maazimio yako mbele za Mungu, ukiweka viwango unavyotaka kufikia katika ufuatiliaji wako.

3. Lazima ufuatilie kuingia kwa kina zaidi katika ukweli juu ya msingi wa kazi ya wakati wa sasa ya Roho Mtakatifu. Usishikilie misemo na mafundisho yaliyopitwa na wakati kutoka zamani.

4. Lazima utafute kuguswa na Roho Mtakatifu, na uingie katika maneno ya Mungu.

5. Lazima ufuatilie kuingia katika njia inayotebewa katika wakati wa sasa na Roho Mtakatifu.

Na unatafutaje kuguswa na Roho Mtakatifu? Jambo muhimu ni kuishi katika maneno ya sasa ya Mungu, na kuomba juu ya msingi wa matakwa ya Mungu. Baada ya kuomba kwa njia hii, hakika Roho Mtakatifu atakugusa. Ikiwa unajaribu kutafuta bila msingi katika maneno ya sasa yaliyonenwa na Mungu, basi hili halina matunda. Unapaswa kuomba, na kusema: “Mungu! Ninakupinga, na nina deni kubwa Kwako; mimi ni mwasi sana, na siwezi kamwe kukuridhisha. Mungu, ninatamani Uniokoe, ninatamani kutumika kwa ajili Yako hadi mwisho kabisa, ninatamani kufa kwa ajili Yako. Unanihukumu na kuniadibu, na sina malalamiko; Ninakupinga na ninastahili kufa, ili watu wote waweze kuona tabia Yako ya haki katika kifo changu.” Unapoomba kutoka ndani ya moyo wako kwa njia hii, Mungu atakusikia, na atakuelekeza; usipoomba juu ya msingi wa maneno ya sasa ya Roho Mtakatifu, basi hakuna uwezekano wa Roho Mtakatifu kukugusa. Tuseme kwamba unaomba kulingana na nia za Mungu, na kulingana na kile ambacho Mungu anataka kufanya leo. Unasema: “Mungu! Ningependa kukubali maagizo Yako na kujitolea kwa maagizo Yako, na niko tayari kujitolea maisha yangu yote kwa utukufu Wako, ili yote ninayofanya yaweze kufikia viwango vya watu wa Mungu, na ili moyo wangu uweze kuguswa na Wewe. Ningependa Roho Wako anitie nuru daima, ayafanye yote ninayofanya yamletee Shetani aibu, na kwamba hatimaye nipatwe na Wewe.” Ikiwa unaomba hivi, kitovu cha maombi kikiwa nia za Mungu, basi hakika Roho Mtakatifu atafanya kazi ndani yako. Haijalishi maneno ya maombi yako ni mangapi—jambo la muhimu ni kama unashika nia za Mungu au la. Huenda nyote mmekuwa na uzoefu ufuatao: Wakati mwingine, mnapoomba katika mkutano, mienendo ya kazi ya Roho Mtakatifu hufikia kilele chake, na kusababisha nguvu za kila mtu ziongezeke. Watu wengine hulia kwa uchungu na kutoa machozi wakati wakiomba, wakizidiwa na majuto mbele za Mungu, na watu wengine huonyesha azimio lao, na kuweka nadhiri. Hiyo ndiyo athari inayofikiwa na kazi ya Roho Mtakatifu. Leo, ni muhimu kwamba watu wote waweke mioyo yao kikamilifu katika maneno ya Mungu. Msizingatie maneno yaliyonenwa hapo awali; ikiwa bado unashikilia yale yaliyokuja kabla, basi Roho Mtakatifu hatafanya kazi ndani yako. Je, unaona jinsi hili lilivyo muhimu?

Je, mnajua njia inayotembewa katika wakati wa sasa na Roho Mtakatifu? Mambo kadhaa hapo juu ndiyo yatakayotimizwa na Roho Mtakatifu leo na katika siku za usoni; ndiyo njia inayochukuliwa na Roho Mtakatifu, na ndiyo ambayo watu wanapaswa kufuatilia kuingia ndani yake. Katika kuingia kwako katika uzima, angalau lazima uweke moyo wako katika maneno ya Mungu, na uweze kukubali hukumu na kuadibu kwa maneno ya Mungu; moyo wako lazima umtamani sana Mungu, lazima ufuatilie kuingia kwa kina zaidi katika ukweli, na malengo yanayotakiwa na Mungu. Unapokuwa na nguvu hii, basi inaonyesha kwamba umeguswa na Mungu, na moyo wako umeanza kumgeukia Mungu.

Hatua ya kwanza ya kuingia katika uzima ni kuweka moyo wako kikamilifu katika maneno ya Mungu, na hatua ya pili ni kukubali kuguswa na Roho Mtakatifu. Ni athari gani inayopaswa kufikiwa kwa kukubali kuguswa na Roho Mtakatifu? Ni kuweza kutamani, kutafuta, na kuchunguza ukweli wa kina zaidi, na kuweza kushirikiana na Mungu katika upande chanya wa mambo. Kushirikiana na Mungu leo kunamaanisha kuna lengo katika ufuatiliaji wako, katika maombi yako, na katika ushirika wako kuhusu maneno ya Mungu, na unatekeleza wajibu wako kulingana na matakwa ya Mungu—huku tu ndiko kushirikiana na Mungu. Ukizungumza tu kuhusu kumwacha Mungu atende, lakini huchukui hatua yoyote, huombi wala hutafuti, basi, je, huku kunaweza kuitwa ushirikiano? Ikiwa huna dalili yoyote ya ushirikiano ndani yako, na huna mafunzo ya kuingia ambayo yana lengo, basi hushirikiani. Watu wengine husema: “Kila kitu kinategemea amurisho la Mungu, yote yanafanywa na Mungu Mwenyewe; Mungu asingefanya, basi mwanadamu angewezaje?” Kazi ya Mungu ni ya kawaida, na si isiyo ya kawaida hata kidogo, na ni kupitia tu utafutaji wako wa vitendo ndiyo Roho Mtakatifu anafanya kazi, kwa maana Mungu hamlazimishi mwanadamu—lazima umpe Mungu nafasi ya kufanya kazi, na usiofuatilia wala kuingia, na ikiwa hakuna shauku hata kidogo moyoni mwako, basi Mungu hana nafasi ya kufanya kazi. Ni kwa njia gani ndiyo unaweza kutafuta kuguswa na Mungu? Kupitia maombi, na kumkaribia Mungu. Lakini muhimu zaidi, kumbuka, lazima iwe juu ya msingi wa maneno yaliyonenwa na Mungu. Unapoguswa mara nyingi na Mungu, huzuiwi na mwili: Mume, mke, watoto, na pesa—vyote haviwezi kukuzuia, nawe unataka tu kufuatilia ukweli na kuishi mbele za Mungu. Wakati huu, utakuwa mtu anayeishi katika ulimwengu wa uhuru.

Iliyotangulia: Ni Wale tu Wanaoijua Kazi ya Sasa ya Mungu Ndio Wanaoweza Kumtumikia Mungu

Inayofuata: Mungu Huwafanya Kuwa Watimilifu Wale Wanaolingana na Nia Zake

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp