170 Ushuhuda wa Maisha

1

Siku moja huenda nikakamatwa kwa ajili ya kumshuhudia Mungu,

kuteseka huku ni kwa ajili ya haki,

ambayo najua moyoni mwangu.

Maisha yangu yakitoweka mara moja ghafla bin vu,

Bado nitakuwa na fahari kuwa naweza kumfuata Kristo na kumshuhudia katika maisha haya.

Ikiwa siwezi kuona tukio kuu la ukuaji wa injili ya ufalme,

bado nitatoa matarajio mazuri zaidi.

Ikiwa siwezi kuiona siku ambayo ufalme unafanikishwa,

lakini naweza kumwaibisha Shetani leo,

basi moyo wangu utajawa na furaha na amani.

Maneno ya Mungu yanaenea kote duniani,

mwanga umeonekana miongoni mwa binadamu.

Ufalme wa Kristo unainuka na unaanzishwa ndani ya dhiki.

Giza liko karibu kupita, alfajiri ya haki imewadia.

Wakati na uhalisi umemtolea Mungu ushuhuda.

2

Siku moja nikiwa mfia dini, na nisiweze tena kumtolea Mungu ushuhuda,

injili ya ufalme bado itaenezwa kama moto

wa nyikani na watakatifu wasiohesabika.

Ingawa sijui naweza

kuitembea njia hii yenye mabonde kwa umbali gani,

bado nitamshuhudia Mungu na nitautoa moyo wangu unaompenda Mungu.

Maneno ya Mungu yanaenea kote duniani,

mwanga umeonekana miongoni mwa binadamu.

Ufalme wa Kristo unainuka na unaanzishwa ndani ya dhiki.

Giza liko karibu kupita, alfajiri ya haki imewadia.

Wakati na uhalisi umemtolea Mungu ushuhuda.

3

Nina heshima kujitolea katika kumtangaza na kumshuhudia Kristo.

Kila ninachotaka kufanya ni kutekeleza mapenzi ya Mungu

na kushuhudia kuonekana na kazi ya Kristo.

Bila kutatizwa na dhiki,

kama dhahabu safi iliyotengeneza katika tanuu,

kutoka kwa ushawishi wa Shetani kunaibuka

kikundi cha askari washindi.

Maneno ya Mungu yanaenea kote duniani,

mwanga umeonekana miongoni mwa binadamu.

Ufalme wa Kristo unainuka na unaanzishwa ndani ya dhiki.

Giza liko karibu kupita, alfajiri ya haki imewadia.

Wakati na uhalisi umemtolea Mungu ushuhuda.

Iliyotangulia: 168 Chaguo Lisilo na Majuto

Inayofuata: 171 Wito wa Nafsi

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Maudhui Yanayohusiana

418 Umuhumi wa Maombi

Sala ni mojawapo ya njia ambazo mwanadamu hutumia kushirikiana na Mungu, ni njia ambayo mwanadamu hutumia kumwita Mungu, na ni mchakato...

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp