7. Jinsi Nilivyokaribia Kuwa Mwanamwali Mjinga

Na Li Fang, China

Katika majira ya kupukutika kwa majani ya mwaka wa 2002, Dada Zhao kutoka dhehebu langu, Kanisa la Kweli, alimleta mpwa wake wa kike, Dada Wang, nyumbani kwangu kuniambia habari njema kwamba Bwana amerudi. Baada ya siku chache za kusoma maneno ya Mwenyezi Mungu na kuusikiliza ushirika wa kina wa huyo dada, nilielewa kuwa tangu uumbaji wa ulimwengu hadi sasa Mungu ametekeleza hatua tatu za kazi ili kuwaokoa wanadamu. Ukweli mwingine ambao pia nilikuja kuujua ulikuwa ni Mungu kutwaa jina tofauti katika kila hatua ya kazi, umuhimu wa jina la Mungu kwa kila enzi, na fumbo la kupata mwili kwa Mungu, nk. Ukweli huu kwa kweli uliniruhusu kufungua macho yangu wazi kabisa na kuona maridhawa. Nikajiambia: “Yote yasikika kuwa dhahiri kabisa, na Mwenyezi Mungu huenda kabisa ni Bwana Yesu aliyerejea hivyo inanibidi kuhakikisha kuwa ninashika fursa hii na kusoma zaidi maneno ya Mwenyezi Mungu.” Kabla ya kuondoka, Dada Wang aliniachia vitabu fulani vya maneno ya Mungu. Kila nilipokuwa na nafasi wakati wa mchana, nilisoma maneno ya Mungu. Jinsi nilivyozidi kusoma ndivyo nilivyozidi kupenda kuyasoma na ndivyo nilivyozidi kuhisi kwamba yalikuwa maneno ya Mungu. Baada ya siku tatu nilikuwa na wasiwasi. Nilidhani: “Mwana wangu wa kiume, ambaye pia ni muumini, na ndugu wengi wa kiume na wa kike katika kanisa letu bado hawajui habari hii njema kuhusu kurudi kwa Bwana. Ni afadhali niharakishe na kuwaambia.”

Siku iliyofuata mapema asubuhi nilikwenda nyumbani kwa mwanangu wa kiume. Nikamwambia kwa furaha: “Hiki ni kitabu kikubwa sana. Unapaswa kukisoma haraka iwezekanavyo.” Mwanangu akanitupia jicho na kuuliza: “Kitabu gani? Unaonekana kufurahishwa sana. Kiweke tu hapo chini na nitakiangalia nikipata nafasi.” Nilidhani kwa kuwa waumini wote walikuwa wanatarajia kurudi kwa Bwana mwanangu angefurahi kupata habari kwamba Bwana tayari amerejea.

Singeweza kamwe katika miaka milioni moja kufikiria, hata hivyo, kwamba siku tatu baadaye mwanangu angekuja nyumbani kwangu akiwa ameandamana na viongozi sita wa kidini. Mmoja wao alikuwa Mchungaji Xia kutoka dhehebu langu, na wengine walikuwa wachungaji na wahubiri kutoka kwa dhehebu la mwanangu. Nilishtuka sana kuwaona, kwa maana sikuweza kuelewa ni nini kilichokuwa kikiendelea na ni kwa nini watu wengi sana walikuwa wamekuja kuniona. Mchungaji aliyeitwa kiukoo Li aliniangalia kwa karibu kwa muda mfupi na kwa mtazamo wa wasiwasi usoni mwake akasema: “Bibi, sisi sote ni waumini katika Bwana, familia moja kubwa. Mwanao ananiambia kuwa mtu fulani amekupa kitabu, lakini hupaswi kukisoma. Sasa ni siku za mwisho, na Bwana Yesu alisema: ‘Basi iwapo mtu yeyote atawaambia, Tazameni, Kristo yuko huku, au yuko pale; msiamini hili. Kwa kuwa wataibuka Makristo wasio wa kweli, na manabii wasio wa kweli, nao wataonyesha ishara kubwa na vioja; ili kwamba, ikiwezekana, watawadanganya walio wateule zaidi(Mathayo 24:23-24). Tunaamini kwamba maneno haya ya Bwana Yesu yanamaanisha kwamba mtu yeyote anayesema kuwa Bwana amerudi ni mdanganyifu ambaye tunapaswa kujilinda dhidi yake na kukataa kumsikiliza. Hivi sasa katika ulimwengu mzima kuna Umeme wa Mashariki tu ambalo linashuhudia kurudi kwa Bwana hadharani, kwa hiyo, chochote ufanyacho, usijihusishe nao. Wala usisome vitabu vyovyote vya Umeme wa Mashariki. Njia yao ni tofauti na imani yetu, hivyo usiwasikilize. Huielewi Biblia vizuri sana, na una kimo kidogo, kwa hiyo unadanganyika kwa urahisi. Tumekuwa tukihubiri kwa miaka mingi na tunaielewa vizuri Biblia. Tumetembea kote nchini China na tumeona mengi na maisha yetu ni makubwa. Tumekuja leo hasa kukuokoa, kwa hiyo unapaswa kutuamini na usijaribu kufanya mambo kivyako.” Niliposikia hayo niliwaza mwenyewe: “Mchungaji huyu anaonekana kujishughulisha nami na kile alichosema si kibaya. Mimi ni mzee na sijasoma sana, na sielewi Biblia vizuri sana. Bila shaka siwezi kutambua vyema kama wao.” Wakati huu Mchungaji Xia akasema: “Mimi ni mchungaji, na Bwana amenipa kondoo Wake kuwaongoza. Kwa hiyo ni jukumu langu kuhakikisha kwamba hupotei kutoka kwa njia ya kweli. Kama siwatunzi kondoo wa Bwana sitaweza kusuluhisha mambo yangu na Bwana. Dada, usijishughulishe sana na makundi mengine kama haya. Kama utaibwa kutoka kwetu na Umeme wa Mashariki basi miaka yote hii ambayo umemwamini Bwana itakuwa imepotea!” Kuangalia nyuso zao zenye fadhaa na kusikia sauti nzito ambazo walikuwa wakiniongeleshea vilinifanya nishtuke kidogo. Niliwaza: “Hilo ni kweli. Ikiwa nitaanza kuamini vibaya si basi hiyo miaka yote ya imani itapotea?” Lakini tena nikafikiria: “Maneno yaliyomo katika kitabu hicho yalionekana kuwa mema, yaliyo sawa sana. Hawa wachungaji na wahubiri hawajasoma maneno ya Mwenyezi Mungu, hivyo kwa nini wanaweza kusema kuwa si njia ya kweli?” Kwa hiyo nikawaambia: “Namna mnavyolisema mnalifanya lionekane kama kwa kweli ndivyo hivyo lakini kile nilichosikia kutoka kwao kinafanana kabisa na maneno ya Bwana katika Biblia!” Waliposikia nikisema hivyo wote walianza kuzungumza mara moja, wakisema vitu vingi kunitishia kiasi kwamba nilikuwa na kizunguzungu na kuchanganyikiwa na nikapitia mvurugiko mwingi wa akili. Niliketi pale, bila kuweza kusema jambo lolote. Kisha walitaka nisali pamoja nao na kutamka maapizo fulani, lakini sikukubaliana nalo hivyo wakaanza kunitishia tena. Hatimaye, mwanangu akasema: “Niacheni nishughulikie jambo hili la mamangu.” Kisha akachukua vitabu vile viwili vya nyimbo vilivyoitwa Mfuateni Mwanakondoo na Kuimba Nyimbo Mpya na kanda za nyimbo pamoja na kitabu cha maneno ya Mungu kiiitwacho Hukumu Yaanza na Nyumba ya Mungu kutoka kwa kabati na akampa mchungaji aondoke navyo.

Baada ya wao kuondoka nilikuwa na hasira sana kiasi kwamba sikuweza kula mlo mkuu wa siku, hivyo nikaenda mbele ya Bwana na kuomba: “Bwana Yesu, kile walichosema wale wachungaji ni kweli au la? Inaonekana kama wanayajali sana maisha yangu. Kama sitowasikiliza, nitaweka imani yangu mahali pabaya? Ee Bwana, kama kwa kweli umerudi kama Mwenyezi Mungu na mimi sikukubali Wewe si basi nitakuwa nikikufungia Wewe mlango? Si nitakuwa tu kama mmoja wa wale wanawali wajinga? Ee Bwana, kwa kusoma maneno ya Mwenyezi Mungu siku hizi chache zilizopita nimehisi kuwa nimepata ugavi mwingi wa kiroho. Kwa hakika na kwa uaminifu nimehisi hili, lakini ninaweza kuwa nimekosea? Sasa kwamba wamechukua vitabu vyangu na kanda zangu za nyimbo ninahisi huzuni. Tafadhali unionyeshe njia kwa kuwa sijui la kufanya….” Baada ya kuomba kwa ghafla nilikumbuka kuwa Dada Wang alikuwa amenipa kitabu kingine cha maneno ya Mwenyezi Mungu na nilikificha ndani kabisa ya kabati. Nilipogundua kwamba bado nilikuwa na kitabu hiki nilihisi vyema kidogo. Lakini tena nilifikiria kile wachungaji hao walichokuwa wamesema, na bado nilikuwa nimechanganyikiwa na sikujua la kufanya. Napaswa nikisome kitabu hicho au la? Usiku huo, sikulala kabisa, mawazo yangu yakiwa katika machafuko. Tena na tena ninakmwomba Mungu nikilia …

Mapema siku ya pili mwanangu alikuja kunipeleka kwa mkutano wa kanisa langu la zamani. Nilikuwa nimesitasita kabisa, lakini mwanangu alinipeleka shingo upande kwa eneo la mkutano na hata akamwambia mhubiri kwamba nilikuwa karibu kuibwa na Umeme wa Mashariki na akamwomba afanye juu chini kunishawishi nikae. Papo hapo, mhubiri na ndugu wote wa kiume na wa kike walinizunguka. Mhubiri aliushika mkono wangu, na kwa sauti ya upole akasema: “Bibi, chochote ufanyacho, usimsikilize mtu yeyote mwingine akihubiri. Ukiaanza kuamini vibaya, Bwana atakapokuja kuinyakua mikusanyiko ya waumini basi utaachwa nyuma, sivyo? Una kimo kidogo, hivyo kama mtu yeyote atakupa aina yoyote ya kitabu kusoma itakuwa bora kwako kutuuliza kwanza. Hebu tukupelelezee kitabu hiki….” Ndugu wote wa kiume na wa kike pia walikuwa wenye makini sana kunishawishi nipate kukaa, na niliguswa kiasi cha kutokwa na machozi kwa “upendo” wao. Walipoona jinsi nilivyokuwa nimeguswa walisizitiza hoja yao tena: “Kama mtu yeyote kutoka Umeme wa Mashariki atakuja kukutembelea tena, usimkaribishe. Usijishughulishe naye hata kidogo!” Niliamkia kwa kichwa kwa makubaliano.

Ilikuwa siku chache tu baadaye Dada Wang alipokuja kuniona tena. Nikamwambia: “Mchungaji alinisomea kifungu hiki kutoka Biblia: ‘Basi iwapo mtu yeyote atawaambia, Tazameni, Kristo yuko huku, au yuko pale; msiamini hili. Kwa kuwa wataibuka Makristo wasio wa kweli, na manabii wasio wa kweli, nao wataonyesha ishara kubwa na vioja; ili kwamba, ikiwezekana, watawadanganya walio wateule zaidi(Mathayo 24:23-24). Katika siku za mwisho, Makristo wa uongo wataonekana na mtu yeyote anayesema kuwa Bwana amerejea ni mdanganyifu. Sielewi Biblia, na kimo changu ni kidogo, kwa hiyo mimi hupotoshwa kwa urahisi. Sithubutu kuusikiliza ujumbe mwingine wowote, kwa hiyo sitakukaribisha. Usije tena.” Kwa uaminifu mkubwa Dada Wang akasema: “Bwana Yesu alisema hili ili kuhakikisha kwamba tutajilinda dhidi ya Makristo wa uongo wakati wa siku za mwisho lakini hakuwa na nia ya sisi pia kumkana Kristo. Kama kuna Makristo wa uongo ni kwa sababu Kristo wa kweli ameonekana tayari, kwa sababu bila ya Kristo wa kweli matapeli hawana chochote cha kuiga. Maneno hayo ya Bwana Yesu yanatuambia kwamba tunapaswa kujifunza kutambua; hayasemi kwamba tunapaswa kukataa kusikiliza injili ya kurudi kwa Bwana kwa sababu tu Makristo wa uongo watatokea wakati wa siku za mwisho. Vinginevyo, tutawezaje kukaribisha kurudi kwa Bwana? Kwa kweli, Bwana Yesu tayari ameelezea wazi tabia za Makristo wa uongo. Zile kuu ni pamoja na kuonyesha ishara, kufanya miujiza, kuponya wagonjwa na kuondoa pepo, na kuiga kazi ambayo Bwana Yesu alikuwa amefanya tayari ili kuwadanganya watu. Kwa hiyo wakati wa siku za mwisho mtu yeyote anayeiga Bwana Yesu kuhubiri njia ya kutubu na ambaye anaweza kuonyesha ishara chache rahisi au kuponya wagonjwa na kuondoa pepo ni Kristo wa uongo. Mwenyezi Mungu, ambaye ni Bwana Yesu aliyerudi katika mwili katika siku za mwisho, harudii kazi ambayo Bwana Yesu alikuwa amefanya tayari lakini anafanya kazi mpya kwa msingi wa kazi ya Bwana Yesu ya ukombozi. Mwenyezi Mungu amekamilisha Enzi ya Neema na amefungua Enzi ya Ufalme kwa kuonyesha ukweli ili kufanya hatua ya kazi ya kuhukumu na kuwatakasa wanadamu. Mwenyezi Mungu atawaokoa kabisa wale watu wote waliokombolewa lakini bado wanaishi katika dhambi kwa kuondoa pingu za asili yao ya dhambi na kuwaondoa kutoka kwa ushawishi wa giza wa Shetani. Wanadamu kwa hiyo watapelekwa kwa hatima yao ya ajabu ya mwisho. Ni Mungu Mwenyewe pekee anayeweza kufanya kazi hii; hakuna yeyote wa Makristo wa uongo anayeweza.” Ingawa kile dada alichokuwa akisema kilikuwa cha maana, mambo ambayo wachungaji walikuwa wameniambia bado yalikuwa yakizunguka upesi upesi kichwani mwangu. Mawazo yangu yalikuwa na wasiwasi na kutoweza kulenga na sikutaka kusikia ushirika wowote wake zaidi. Kwa hiyo nikamwambia kuwa nilikuwa na kitu cha kufanya kwa nyumba jirani, ambao ulikuwa ni uongo, ili kumwondokea. Dada Wang alirudi nyumbani kwangu mara nyingi baada ya hayo lakini daima nilimwepuka. Jirani yangu aliniambia: “Yeye haonekani kama mtu mbaya hivyo unaogopa nini?” Moyoni mwangu nilijua kwamba Dada Wang alikuwa mtu mzuri, lakini kama nilikuwa mdogo wa kimo niliogopa kupata imani yangu vibaya.

Baada ya kurudi kwa mkutano wa kanisa langu la zamani niliwasikia wahubiri bado wakisema mambo katika mahubiri ambayo walikuwa wamesema kabla. Walikuwa wakiongea daima kuhusu jinsi ya kulinda dhidi ya Umeme wa Mashariki, au kuchangia kanisa, au walirudia mambo mengi ya zamani ya kuchosha juu ya ni kiasi gani walichokuwa wamefanya kazi na kuteseka kwa ajili ya Bwana na ni kiasi gani cha neema ya Mungu walikuwa wamepata …. Hawakuweza kusema hata chembe ya kitu kipya na kichangamfu. Kwa haraka nilichoka kuwasikiliza, na nikaanza kusinzia. Katika tukio jingine, ndugu mmoja wa kiume kutoka kanisa jingine alikuja kutoa mahubiri, lakini yalikuwa mambo sawa tu juu ya jinsi alivyokuwa ametembea toka upande mmoja wa milima hadi mwingine kufanya kazi ya Bwana na ni kiasi gani alichoteseka, ni watu wangapi aliwaingiza kwa dini kupitia kueneza injili na idadi ya makanisa ambayo aliyaanzisha. Alitumia mahubiri hayo kujisifu. Kumsikiliza kulinifanya nijihisi kuwa na wasiwasi sana, na nikawa na wazo kwamba hakuwa na ushuhuda kwa ajili ya Bwana lakini alikuwa na ushuhuda tu kwa ajili yake mwenyewe. Siku nyingine, nilikuwa nimefika tu kwa mkutano wakati dada mmoja aliniambia: “Leo tuna msichana wa kike wa teolojia wa umri wa miaka 20 na kitu ambaye anatoa mahubiri.” Nilifurahi sana kusikia hilo na kujiambia kuwa ningekuwa na usikizi maalum kwa sababu kwa waziwazi angeweza kutoa mahubiri bora zaidi kuliko walivyofanya wahubiri wetu. Lakini yule mwanafunzi alianza mahubiri yake na jinsi ya kulinda dhidi ya Umeme wa Mashariki, kisha akaendelea kuzungumza juu ya jinsi alivyoacha masomo yake ya kawaida akiwa na umri wa miaka 16 ili kuingia seminari kujifunza teolojia, jinsi alivyofanya kazi na kuteseka nje licha ya mvua, ni mahali pangapi ambapo amekwenda …. Jinsi nilivyozidi kusikia, ndivyo nilivyozidi kuchoshwa. Nikajiwazia: “Hiyo yote ni divai ya kale tu katika viriba vipya! Kwa nini wao huendelea kutoa mambo yaleyale ya zamani yanayochosha? Hakuna chochote cha haya kinachohusiana na uzoefu wao au maarifa ya maneno ya Bwana, wala haituongozi katika kufuata njia ya Bwana au kutenda na kuingia katika maneno Yake.” Nilikuwa nimerejea kwa mikutano kwa zaidi ya mwezi mmoja lakini sikuwa nimepata kitu chochote kutoka kwao. Jinsi nilivyozidi kusikiliza ujumbe huu, ndivyo nilivyozidi kuwa mkavu katika roho yangu, na nilifikiri nitakufa kwa kiu cha kiroho kama ningeendelea kuamini jinsi hii. Jinsi nilivyozidi kulifikiria, ndivyo nilivyozidi kufadhaika.

Baada ya mkutano, nilienda nyumbani nikiwa na huzuni. Nilifikiria kitabu cha Hukumu Huanza na Nyumba ya Mungu ambayo Dada Wang alikuwa amenipa, ambayo ilisema kuwa watu hawapaswi kujigamba na hawapaswi kujisifu lakini wanapaswa kumheshimu Mungu kama mkuu na kumsifu Mungu. Lakini wahubiri hao wote walikuwa wakijishuhudia wenyewe, wakijitukuza zaidi ya kila kitu kingine, na kuwawafanya wengine kuwa na heshima kubwa kwao. Ilionekana kwangu kwamba kile kitabu kilichosema kilikuwa sahihi! Hivyo jioni wakati nilipokuwa peke yangu nilitoa nakala ya Hukumu Huanza na Nyumba ya Mungu na kusoma sehemu yake. Jinsi nilivyoendelea kusoma ndivyo moyo wangu ullivyozidi kufurahi, na kwa kweli nilihisi kuwa maneno haya yanaweza kuwa chakula kwa ajili ya maisha yangu. Nilishangaa ni kwa nini mchungaji wetu hangeniruhusu nisome kitabu kizuri kama hiki. Mchungaji wetu mara nyingi alisema kuwa alikuwa na wajibu kwa maisha yangu na bado alionekana tu kujua jinsi ya kujishuhudia katika mahubiri yake. Hakuwahi kuniambia kamwe jinsi ya kupata maisha. Nilikumbuka wakati fulani ambapo nilikuwa dhaifu sana na sikutaka kwenda kwa mikutano. Mchungaji hakuja kunitembelea au kutoa msaada. Lakini ilikuwaje mara tu nilipoanza kupata chakula cha kiroho kwa kusoma maneno ya Mwenyezi Mungu alionekana waziwazi ili kunilazimisha kuwasikiliza wakirudia mambo yale yale ya zamani? Huko si ni kuchukua wajibu kwa maisha yangu! Niligundua ghafla jinsi nilivyokuwa nimekosea, na nilijilauumu kwa uchungu: Maneno ya Mwenyezi Mungu yangeweza kutoa ugavi kwa maisha yangu, na labda yalikuja kutoka kwa Mungu. Ningeweza kuwa mjinga na kipofu jinsi gani kuamini kile mchungaji alichokuwa amekisema na kuacha kuchunguza njia kweli? Pia nilifikiria jinsi Dada Wang alikuwa amenipa msaada wa upendo mara nyingi, na alikuwa ameshuhudia kazi ya Mungu ya siku za mwisho kwangu ili nipate fursa ya kupata wokovu wa Mungu wa siku za mwisho. Lakini sikuwa mzuri sana kwa Dada Wang, na hata aliepuka kumwona mara kadhaa. Sikupaswa kumtendea kama adui. Nilipofikiria jambo hili nilihisi kusikitika mno. Kwa hiyo, nikaja mbele ya Bwana na kusema sala ya toba kwa machozi: “Bwana, nilimtendea huyo dada ambaye aliniletea kitabu cha maneno ya Mungu kama adui na kumkwepa. Hili si jambo la kumtelekeza mtu lakini kwa kweli ni jambo la kuukataa wokovu Wako. Bwana, sasa najua kwamba sikupaswa kuwasikiliza wale wachungaji na kuachana na kuchunguza kazi ya Mungu ya siku za mwisho. Nataka kutubu Kwako, lakini sijui jinsi ya kumpata Dada Wang. Tafadhali nisaidie kumpata.” Baada ya kuomba, nilikichukua tena hicho kitabu na kukisoma hadi usiku. Jinsi nilivyozidi kusoma ndivyo nilivyozidi kuhisi kuwa maudhui yalikuwa mazuri, na ndivyo nilivyokuja kuwadharau wale wachungaji kwa kunizuia kusoma maneno ya Mwenyezi Mungu.

Ninamshukuru Bwana sana kwa kusikiliza ombi langu! Siku ya pili adhuhuri, nilipokuwa nikila chakula cha mchana, Dada Wang alikuja nyumbani kwangu. Nilimwambia kuhusu kila kitu kilichokuwa kimetokea tangu nilipomwona mwisho. Aliposikia kwamba sikuweza kupata ugavi katika kanisa la kidini alinisomea kifungu cha maneno ya Mwenyezi Mungu: “Mungu atatimiza ukweli huu: Atawafanya watu wote ulimwengu mzima kuja mbele Yake, na kumwabudu Mungu duniani, na kazi Yake katika maeneo mengine itakoma, na watu watalazimishwa kutafuta njia ya kweli. Itakuwa kama Yusufu: Kila mtu alimwendea kwa ajili ya chakula, na kumsujudia, kwa sababu alikuwa na vyakula. Ili kuweza kuepuka njaa watu watalazimishwa kutafuta njia ya kweli. Jumuiya yote ya kidini itapitia njaa kubwa, na ni Mungu tu wa leo ndiye chemchemi ya maji ya uzima, akiwa na kisima chenye maji yasiyokauka kilichotolewa kwa ajili ya furaha ya mwanadamu, na watu watakuja na kumtegemea(Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Ufalme wa Milenia Umewasili). Kisha huyo dada alishiriki nami: “Mungu ni chemchemi ya maji yaliyo hai, na Mungu peke yake anayeweza kuleta uzima kwa watu. Watu wanapomwacha Mungu, watakuwa katika giza na kunyauka na kufa, kama tu tawi ambalo limevunjika kutoka kwa shina la mti. Katika imani yetu kwa Mungu, ni lazima tuzifuate kwa karibu hatua za Mwanakondoo, kuikubali kazi ya Mungu ya sasa, na kuja mbele ya Mungu ili tuweze kupata kazi ya Roho Mtakatifu na chakula na ruzuku ya maji yaliyo hai ya uzima ya Mungu. Kwa nini hatuwezi kupata riziki kutoka kwa kuwasikiliza wale wachungaji na wazee katika dini? Kuna sababu mbili za hili. Moja ni kwamba wale wachungaji na wazee hawazitii amri za Bwana na hawaweki maneno ya Bwana katika vitendo. Hawana uzoefu halisi wa maisha na hawana maarifa ya kweli ya Mungu na sembuse mioyo inayomwogopa Mungu, jambo linalodhihirika kwa njia ambayo hawamtukuzi Mungu kamwe au kumshuhudia Yeye katika kazi zao na kuhubiri. Wao hujisifu tu na kujishuhudia. Kwa kuchepuka kabisa kutoka kwa njia ya Bwana wamegeuka kuwa wachungaji wa uwongo wa mfano mmoja ambao huwadanganya watu. Hii ndio sababu wanachukiwa na kukataliwa na Roho Mtakatifu na kamwe hwapati nuru Yake na mwongozo. Na hii ndiyo sababu kuu ya jumuiya ya kidini imekuwa ya ukiwa. Sababu nyingine ni kwamba Bwana tayari amerejea kufanya kazi ya enzi mpya. Kazi ya Roho Mtakatifu kwa watu ya Enzi ya Neema tayari imeisha, na sasa inafanyika kwa kikundi cha watu ambao ni weledi kabisa wa kazi mpya ya Mungu. Lakini wachungaji na wazee wa kanisa hawachunguzi kamwe kazi mpya ya Mungu na hawafuati nyayo za Mungu na kukubali uongozi Wake. Yote wanayofanya ni kumpinga Mungu kwa bila kufikiria, kuihukumu kazi ya Mungu ya siku za mwisho, na kumkashifu na kumkufuru Mwenyezi Mungu, Kristo wa siku za mwisho. Wanafanya chochote wanachoweza ili kuwazuia waumini kuchunguza njia ya kweli na kurudi kwa Mungu, na hivyo wamekuwa tu kama Mafarisayo waliomtundika Bwana msalabani. Wao tayari wamehukumiwa na kuondoshwa na Mungu, kwa hiyo hakuna njia ambayo kwayo Roho Mtakatifu angeweza kuwafanyia kazi. Hivyo, ikiwa tunataka kupokea riziki ya uzima tunapaswa kujiunga na kazi ya sasa ya Roho Mtakatifu, kukubali mambo ambayo Mungu anayoyaonyesha kwa sasa, na kuukubali uongozi, ugavi na uchungaji wa Mwenyezi Mungu, Kristo wa siku za mwisho. Hii ndiyo njia ya pekee ya sisi kupata ukweli na uzima. Hili linathibitisha kile Bwana Yesu alichosema: ‘Mimi ndiye njia, ukweli na uhai(Yohana 14:6). ‘Ila yeyote akunywaye maji ambaye nitampa hatawahi kuwa na kiu; lakini maji hayo ambayo nitampa yatakuwa chemichemi ya maji ambayo yanachipuka katika uhai wa daima(Yohana 4:14).”

Baada ya kusikiliza ushirika wa Dada Wang juu ya maneno ya Mungu nilikuwa na ufahamu wa ghafla juu ya ni kwa nini wachungaji, wazee wa kanisa, na wanachuo wa teolojia hawakuwa na chochote cha thamani cha kuhubiri: Hawana ukweli! Wao humpinga Mungu, na ndiyo maana Roho Mtakatifu aliwaacha zamani za kale. Wanapohubiri wao huwa na ujuzi wa akili tu kutegemea, lakini hawana nuru ya Roho Mtakatifu na ndiyo maana mahubiri yao hayawasaidii watu. Lakini bado kulikuwa na kitu ambacho sikukielewa, hivyo nikamwuliza Dada Wang: “Wale wachungaji na wazee wote wa kanisa wanasema kwamba wana uzoefu mno wa Biblia, kwamba wamekwenda shule ya seminari na wana uzima mwingi. Siielewi Biblia vizuri na niliamini kuwa kwa kweli walikuwa wamekomaa zaidi kuniliko katika maisha, kwa hiyo ndiyo maana niliwasikiliza. Kwa hiyo sasa siwezi kuamua kwa kweli kama wana uzima mwingi au la. Dada, unafikiri kwamba kwa kweli wana uzima mwingi?” Dada Wang akajibu: “Hakuna mtu anayeweza kusema kuwa ana uzima. Haya yote huamuliwa kulingana na maneno ya Mungu. Ina maana gani kuwa na uzima? Je, mambo gani hasa yanayopaswa kudhihirishwa hasa? Bwana Yesu alisema: ‘Mimi ndiye njia, ukweli na uhai(Yohana 14:6). Na Mwenyezi Mungu alisema: ‘Ikiwa unaumiliki uhalisi au la haina msingi kwa kile unachokisema, badala yake, inatokana na kile unachoishi kwa kudhihirisha. Wakati maneno ya Mungu yanakuwa maisha yako na kujionyesha kwako kwa asili, hili tu ndilo linalochukuliwa kama uhalisi, na hili tu ndilo linachukuliwa kama wewe kumiliki uelewa na kimo cha kweli. Lazima uwe na uwezo wa kuhimili uchunguzi kwa muda mrefu, na lazima uwe na uwezo wa kuishi kwa kuidhihirisha sura ambayo inahitajika kwako na Mungu; isiwe mkao tu, lakini ni lazima ibubujike kwa kawaida kutoka ndani mwako. Hapo tu ndipo basi utakapokuwa na uhalisi kikweli, na ndipo tu basi utakapopata maisha(Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Kuuweka tu Ukweli Katika Matendo Ndiko Kuwa na Uhalisi). ‘Ni kwa nini inasemekana kuwa watu wengi hawana maisha? Ni kwa sababu hawamjui Mungu, na hivyo inasemekana kuwa hawana Mungu mioyoni mwao, na hawana uhai(Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Wale Wanaomjua Mungu Pekee Ndio Wanaoweza Kuwa na Ushuhuda Kwa Mungu). Kutoka kwa maneno ya Mungu tunaweza kuona kwamba Kristo ni ukweli, njia na uzima. Ukweli unaweza kutenda kama uzima wa watu, hivyo kupata ukweli ni sawa na kupata uzima, na kuwa na uzima huonyesha kwamba mtu amepata ukweli na kumjua Mungu. Mtu asiyeuelewa ukweli na hamjui Mungu hatakuwa na moyo unaomwogopa Mungu na hawezi kuishi kwa kudhihirisha maneno ya Mungu. Hili lina maana kwamba hana uzima. Kama mtu hana maneno ya Mungu kama uzima wake basi anaishi kwa sumu za Shetani. Yeye daima hudhihirisha tabia yake potovu—kiburi, majivuno, ubinafsi, wenye kustahili dharau, udanganyifu, hila, na kadhalika. Na hata kama wanamwamini Mungu bado wanashindwa kumcha Mungu na kukaa mbali na uovu. Daima wao husema uongo, kudanganya, kutenda dhambi, na kumpinga Mungu. Wanawezaje kamwe kuitwa watu walio na uzima? Kama wanasema wana uzima ni ule uzima mmoja wa kimwili tu, ule uzima wa shetani ambao umejaa tabia potovu ambazo zina upinzani kwa Mungu, na sio uzima mpya, utokao kwa kuyapitia maneno ya Mungu na kupata ukweli. Kwa hiyo ingawa wachungaji na wazee wa kanisa wanaweza kuwa na uzoefu wa Biblia, na kuwa na elimu ya Biblia na nadharia ya kidini, hiyo haimaanishi kwamba wanamjua Mungu na kumcha Mungu na kwamba wanauelewa ukweli na wana kazi ya Roho Mtakatifu. Na bila shaka haimaanishi kuwa wao hutenda maneno ya Bwana au kumtii Yeye. Badala yake, kile tunachokiona ni kwamba wao hujitukuza na kujishuhudia wenyewe, na kwa kawaida hujaribu kuwafanya waumini kuwaabudu. Kile wanachofichua ni mfano wa Shetani—kuwa na kiburi na majivuno, kukosa kumcha Mungu, na daima kujifanya kuwa wazuri ili kuwapumbaza watu. Si katika kazi zao wala katika kuhubiri kwao wanaweza kuzungumzia maarifa yoyote halisi ya maneno ya Bwana au uzoefu wowote wa vitendo ambao ni wa manufaa kwa watu wengine. Bila kujali ni miaka mingapi unayowasikiliza hutaweza kuelewa ukweli wowote na maisha yako hayatakua. Hawana maarifa yoyote ya Mungu au ya kazi Yake, na wakati Mungu amerudi kwa mwili katika siku za mwisho kuuonyesha ukweli na kufanya kazi Yake ya hukumu wao humpinga kwa mhemko, kumhukumu, na kumkufuru Yeye bila hata chembe ya hofu mioyoni mwao. Wana uzima wa aina gani? Wao kabisa wana uzima wa Shetani. Wao ni kama Mafarisayo ambao waliijua Biblia vizuri na walidhani kwamba walikuwa na imani ya kweli katika Mungu na walikuwa na uzima lakini hawakumjua Mungu na hata walimpinga na kumhukumu Bwana na kumtundika msalabani. Hili linatuambia kuwa kwa sababu tu kwamba mtu anaijua Biblia haimaanishi kwamba ana ukweli na uzima. Watu pekee walio na uzima ni wale wanaoufahamu na kuutenda ukweli na wanaomjua Mungu, wana moyo unaomcha Yeye, na wanaweza kuishi kwa maneno ya Mungu. Wale wachungaji na wazee wa kanisa wanasema kuwa wana uzima mwingi, na hili linawapumbaza waumini tu na kujidanganya.”

Baada ya kusikiliza maneno ya Mwenyezi Mungu na ushirika wa Dada Wang kila kitu kilikuwa wazi zaidi akilini mwangu: Kwa sababu tu kwamba mtu anaijua Biblia vizuri na anaweza kuelezea Biblia haimaanishi kwamba anaelewa ukweli, kumjua Mungu au kuwa na uzima. Nilikuwa nadhani kuwa watu walio katika vyeo vya juu au ambao walisoma teolojia au walikuwa na elimu ya Biblia wote walikuwa na uzima mwingi. Lakini sasa ninaona kuwa mtazamo wangu ulikuwa wa upuuzi kabisa. Inaonekana kwamba watu ambao hawana ukweli hawawezi kutambua, na hivyo hudanganywa kwa urahisi. Kwa hiyo basi nilimwuliza Dada Wang swali: “Mwenyezi Mungu huzungumza vizuri sana. Yote tunayopaswa kufanya ni kusoma maneno Yake kwa makini na tutaona kwamba haya ni maneno ya Mungu, sauti ya Mungu. Kwa hiyo ni kwa nini wachungaji na wazee wa kanisa hawakubali jambo hili na hata hufanya kila linalowezekana kumpinga na kumhukumu Yeye?” Dada Wang alijibu: “Katika siku za mwisho, Mwenyezi Mungu amekuja na kuonyesha ukweli wote ambao wanadamu wapotovu wanahitaji ili kutakaswa na kuokolewa. Ukweli huu ndio njia ya uzima wa milele ambao Mungu ametukirimu. Alimradi watu wanasoma maneno ya Mungu kwa makini watakubali kwamba maneno haya ni ukweli, uzima, na njia na ndiyo msingi na mwongozo wa maisha ya wanadamu. Huu ni ukweli. Ingawa wachungaji wengi na wazee wa kanisa hupinga na kuhukumu kazi ya Mungu ya siku za mwisho, na kujaribu kuwazuia watu wasisome maneno ya Mwenyezi Mungu, hili halimaanishi kwamba hawawezi kusikia mamlaka na nguvu ndani ya maneno hayo. Baadhi ya wachungaji na wazee wa kanisa hawawezi kuhubiri chochote muhimu kwa hiyo huiba maneno ya Mwenyezi Mungu na kuyahubiri kwa mikusanyiko yao ya waumini, wakidai kuwa ni nuru ambayo Roho Mtakatifu aliwatolea. Lakini kwa nini wao humpinga kwa mhemuko na kumhukumu Mwenyezi Mungu? Hili linahusiana na asili yao na kiini cha kuuchukia ukweli. Tukifikiria nyuma Bwana Yesu alipoanza kufanya kazi Yake kwanza, alionyesha miujiza mingi, hasa kumfufua Lazaron na kuwalisha watu elfu tano kwa mikate mitano na samaki wawili, vitendo ambavyo viliwastaajabisha zaidi watu kote nchini Uyahudi. Hivyo, watu wengi wa kawaida katika siku hizo walitambua kutoka kwa maneno ya Bwana na kazi kwamba Alikuwa ndiye Masihi aliyekuwa aje. Lakini viongozi wa Wayahudi hawakumkubali Bwana Yesu, na badala yake walimpinga na kumhukumu Yeye na mwishowe wakala njama na serikali ya Kirumi ili kumsulubisha Bwana. Kwa nini hili lilitokea? Ilikuwa ni kwa sababu hawakuweza kusikia mamlaka na nguvu katika maneno ya Bwana Yesu? Hapana! Ilikuwa ni kwa sababu waliona kwamba watu zaidi na zaidi walikuwa wakiikubali njia ya Bwana Yesu. Waliogopa kwamba kama watu wote wa kawaida wangemwamini Bwana Yesu basi hakuna yeyote angewafuata au kuwaabudu na wangepoteza hadhi yao na riziki yao. Kwa kweli walijua kwamba Bwana Yesu alikuwa Mungu na bado walimkataa kwa makusudi; hili lilifichua asili yao ya kupinga Kristo, ambayo ni kumpinga Mungu na chuki ya ukweli. Bwana Yesu aliwakemea kwa ukali Aliposema: ‘Lakini sasa mwataka kuniua, mtu aliyewaambia ukweli, ambao nimesikia kutoka kwake Mungu(Yohana 8:40). ‘Kwa nini hamwelewi nisemacho? hata kwa sababu hamwezi kusikia neno langu. Ninyi ni wa baba yenu ibilisi, na mtatimiliza tamaa za baba yenu. Alikuwa mwuaji tangu mwanzo, na hakudumu katika ukweli, kwa sababu ukweli haupo ndani yake(Yohana 8:43-44). Katika nyakati za sasa, maneno ya Mwenyezi Mungu yamefichua kwa uwazi kabisa asili na hali za viongozi wa sasa wa jumuiya ya kidini. Mwenyezi Mungu alisema: ‘Wale wanaosoma Biblia katika makanisa makubwa hukariri Biblia kila siku, lakini hakuna yeyote anayeelewa madhumuni ya kazi ya Mungu. Hakuna hata mmoja anayeweza kumwelewa Mungu; juu ya hayo, hakuna yeyote anayekubaliana na moyo wa Mungu. Wote hawana thamani, wanadamu waovu, kila mmoja akisimama juu kufundisha kuhusu Mungu. Ingawa wanalionyesha hadharani jina la Mungu, wanampinga kwa hiari. Ingawa wanajiita waumini wa Mungu, wao ni wale wanaokula mwili na kunywa damu ya mwanadamu. Wanadamu wote kama hao ni mashetani wanaoteketeza nafsi ya mwanadamu, pepo wakuu wanaowasumbua kimakusudi wanaojaribu kutembea katika njia iliyo sawa, na vizuizi vinavyozuia njia ya wanaomtafuta Mungu. Inagawa wao ni wenye “mwili imara,” wafuasi wao watajuaje kwamba wao ni wapinga Kristo wanaomwongoza mwanadamu katika upinzani kwa Mungu? Watajuaje kwamba hao ni mashetani hai wanaotafuta hasa nafsi za kuteketeza?(Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Watu Wote Wasiomjua Mungu Ni Watu Wanaompinga Mungu). Viongozi hawa wa jumuiya ya kidini leo ni kama Mafarisayo wa zamani: Ingawa wanajua Biblia vizuri hawajui kabisa juu ya kazi ya Mungu. Wao huona kwamba maneno ya Mwenyezi Mungu yanakubaliwa na watu zaidi na zaidi ambao wanatamani na kutafuta kuonekana kwa Mungu, na wanaogopa kwamba kama waumini wote wanamwamini Mwenyezi Mungu basi hakuna yeyote atakayewafuata tena au kuwachangia fedha. Kwa hiyo ili kulinda hadhi yao na riziki yao, kwa kisingizio cha kuwa waaminifu kwa Bwana na kuwalinda kondoo Wake wamebuni kila aina ya uvumi muovu ili kuipinga kwa mhemuko na kuihukumu kazi ya Mungu ya siku za mwisho na kufanya wawezavyo ili kuwazuia waumini kuitafuta na kuichunguza njia ya kweli. Kwa hiyo tunaweza kuona kwamba viongozi wa kidini kwa kweli ni Mafarisayo ambao hawaupendi na huuchukia ukweli. Ni pepo wanaoishi ambao huzila roho za watu; wao ni wapinga Kristo ambao wanafichuliwa na kazi ya Mungu ya siku za mwisho.”

Baada ya kusikiliza maneno ya Mungu na ushirika wa huyu dada nilikuwa na utambuzi wa ghafla na kukubali kwa kichwa changu mara chache na kusema: “Sasa ninaona ni kwa nini wale wachungaji na wazee wa kanisa, baada ya kusikia kwamba kuna watu wanaoshuhudia kurudi kwa Mungu, hawalitafuti au kulichunguza lakini badala yake humlaumu Yeye. Sasa ninaelewa ni kwa nini wale wachungaji na wazee wa kanisa wanapiga kelele kwamba wananilinda na wana wasiwasi juu ya maisha yangu ilhali kwa kweli wanafanya liwezekanalo kunisitisha na kunizuia kusoma maneno ya Mungu na kupata riziki kutoka kwa Mungu. Ni kwa sababu kila kitu wanachokifanya ni kuyalinda maslahi yao wenyewe. Wanaogopa kwamba kama watu wataanza kumfuata Mwenyezi Mungu hawatasikiliza mahubiri yao au kuwachangia pesa kwa hiyo ndiyo maana huwazuia watu kuchunguza njia ya kweli. Kwa kweli wanastahili dharau, na wamekuwa karibu sana kunifanya nipoteze fursa yangu ya wokovu. Sasa kwa kuwa ninajua jinsi ya kutambua vizuri nitakataa kuwa na uhusiano wowote nao. Bila kujali watakachokifanya ili kunisumbua, nitasimama imara na kumfuata Mwenyezi Mungu.” Baada ya hapo, sikwenda tena kamwe kwa mikutano ya kanisa langu lamwanzo.

Muda mfupi baadaye, wahubiri wawili kutoka kwa dhehebu langu la mwanzo. walikuja nyumbani kwangu. Mmoja wao, Mhubiri Zhang, aliniambia: “Bibi, kwa nini hujaja kwa mikutano? Umekuwa na mawasiliano na watu kutoka Umeme wa Mashariki tena? Chochote ufanyacho, usibadilishe kwa imani yao. Ukifuata imani yao utakuwa kwa shida!” Kwa sauti imara nilijibu: “Sikupata chochote kutoka kwa mikutano nanyi hivi karibuni na nilikuwa mjinga zaidi katika roho yangu na sikuweza kuhisi kuwepo kwa Bwana. Lakini tangu nilipoanza kusoma maneno ya Mwenyezi Mungu, roho yangu imeinuliwa na sasa ninaanza kuelewa ukweli na maisha yangu yamelishwa. Ninahisi kwamba Mungu yu pamoja nami na kwamba Roho Mtakatifu anaifanya kazi ndani yangu. Sasa nina hakika kwamba Mwenyezi Mungu ndiye Bwana aliyerejea na kwamba ukweli ulioonyeshwa na Mwenyezi Mungu ni maji yaliyo hai ya uzima. Ni maneno ya Mwenyezi Mungu pekee yanayoweza kunipa riziki, na popote ninapoweza kupata uzima ndipo nitakapokwenda.” Yule mwingine wao, Mhubiri Song, kisha akasema: “Tunaona wasiwasi juu yako. Tuna wasiwasi kwamba utachepuka kutoka kwa njia sahihi. Wewe ni mchanga katika maisha….” Nikamwambia: “Labda mimi ni mchanga katika maisha, lakini Mungu ataniongoza kwa vyovyote vile. Asante kwa kujali kwako, lakini mnapaswa kuyafikiria maisha yenu wenyewe. Maisha yangu yamo mikononi mwa Mungu….” Waliposikia kile nilichokisema waliondoka kwa hasira. Nilipowaangalia wakitokomea kwa mbali nilihisi nafuu kubwa sana kama ambayo kamwe sikuwahi kuihisi kabla. Baadaye, walirudi mara mbili zaidi, lakini walipoona kwamba sikuguswa kabisa na ushawishi wao hawakurudi tena kamwe. Ninamshukuru Mungu kwa kuniongoza na kuniruhusu kuziona nyuso za kweli na mioyo miovu ya viongozi hao wa kidini, kuziona hila za Shetani na kutafuta njia yangu kutoka kwa machafuko na kumrudia Mungu. Sasa ninapewa maji yaliyo hai ya uzima, na nitamfuata na kumwabudu Mwenyezi Mungu!

Iliyotangulia: 6. Sikiliza! Ni Nani Huyu Anenaye?

Inayofuata: 8. Mwenyezi Mungu alinielekeza kwenye Njia ya Kupata Utakaso

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Maudhui Yanayohusiana

43. Kupotea na Kurejea Tena

Na Xieli, MarekaniNilikuja Marekani kufanya kazi kwa bidii kama vile ningeweza kutafuta maisha yenye furaha na hali ya juu ya maisha....

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp