6. Sikiliza! Ni Nani Huyu Anenaye?

Na Zhou Li, China

Kama mhubiri wa kanisa, hakuna jambo linaloumiza zaidi kama udhaifu wa kiroho na kutokuwa na lolote la kuhubiri. Nilihisi kutojiweza nilipoona ndugu wachache zaidi wakija mikutanoni, na nilikuja mbele za Bwana mara nyingi kuomba kwa dhati na kumsihi Bwana aimarishe imani ya ndugu. Lakini hali ya ukiwa ya kanisa haikutengemaa hata kidogo na hata niliishi kwa udhaifu na uhasi …

Nilikuwa nikifanya kazi nyumbani siku moja wakati Ndugu Wang na Ndugu Lin walipotokea ghafla, na nikawakaribisha kwa furaha. Baada ya kutaniana, Ndugu Wang alisema, “Dada Zhou, roho yako i hali gani kwa sasa?” Nilitanafusi na kusema, “Si kitu. Mimi ni dhaifu katika roho na sina jambo la kuhubiri katika mahubiri yangu! Ndugu wote ni hasi na dhaifu pia. Kuna watu wachache tu kanisani.” Ndugu Lin aliuliza, “Dada Zhou, unajua ni kwa nini huna jambo la kuhubiri katika mahubiri na kwa nini kuna watu wachache kanisani?” Mara alipoongea, nilifikiri: Hili ndilo hasa ninalotaka kujua. Je, wanaweza kweli kujua sababu? Niliuliza kwa haraka, “Kwa nini?” Ndugu Wang alisema, “Ni kwa sababu Bwana amerudi tayari. Amekuwa mwili kwa mara ya pili na ananena maneno Yake na kutekeleza kazi mpya. Ndugu wengi tayari wamekubali kazi ya Mungu katika Enzi ya Ufalme na wanaishi ndani ya mkondo wa kazi ya sasa ya Roho Mtakatifu. Hali zao zinaendelea kuwa nzuri zaidi. Wale ambao hajaenda sambamba na kazi mpya ya Mungu wamepoteza kazi ya Roho Mtakatifu, na kwa hivyo hawana maneno ya kuhubiri na ni hasi na dhaifu. Lazima tufanye hima ili tunede sambamba na nyayo za Mungu!” Niliposikia hili, nilikumbuka ghafla maneno ya mfanyakazi mwezangu mwandamizi: “Mtu akisema kwamba Mungu amekuja kufanya kazi mpya na kwamba amenena maneno mapya, basi huko ni kupotoka kutoka kwenye Biblia, na kupotoka kutoka kwenye Biblia si kumwamini Bwana; ni uasi wa dini.” Nilipofikiri kuhusu hili, nilisema bila utani: “Je, si wafanyakazi wenzetu waandamizi mara nyingi hutuambia kuwa kupotoka kutoka kwenye Biblia si kuamini katika Bwana?” Mnapaswa nyote kujua hili, kwamba kupotoka kutoka kwenye Biblia ni kupotoka kutoka kwenye njia ya Bwana. Mnathubutu vipi kunihubiria hivi!” Nilisimama kwa hasira nilipokuwa nikisema hivi. Ndugu Lin alisema, “Dada Zhou, usighadhabike. Tunajua kuwa unamwamini Mungu kwa kweli na u mwenye raghba, na ndiyo sababu tunakwambia kuhusu kazi mpya ya Mungu. Tumemwamini Bwana kwa miaka mingi sana. Je, si tumekuwa kila wakati tukingoja kwa hamu kurudi kwa Bwana? Sasa Bwana amerudi na anatenda kazi ya hukumu ya siku za mwisho. Hii ni habari nzuri sana. Ni lazima tutafute na kuchunguza kwa bidii na tusikose nafasi ya kumkaribisha Bwana!” Bila kungojea Ndugu Lin akamilishe, niliuchukua mkono wangu juu na kumkatiza kwa sauti, “Nymaza, nymaza, nymaza! Usizungumze tena. Sitaamini kile kilichopotoka kutoka kwenye Biblia. Hamfuati njia ya Bwana, lakini sharti niifuate.” Waliona kuwa kwa kweli sikuwa nikisikiliza na kwa hivyo hawakuwa na budi kuondoka. Baadaye, walikuja tena mara nyingine chache, lakini niliwapuuza tu.

Baadaye, Ndugu Wang na Ndugu Lin walikuja nyumbani kwangu na dada wawili kunihubiria injili. Siku hiyo, nilikuwa nikichagua maharagwe nyumbani huku mume wangu alikuwa nje akifanya kazi. Aliwaona wakija na akawakaribisha ndani ya nyumba. Mara nilipowaona, moyo wangu ulianza kupiga kwa haraka: Kwa nini walikuwa wamerudi tena na wakaleta msaada wa watu wawili? Wanne hao waliingia katika nyumba na kuniamkua na kisha wakaanza kufanya ushirika na mume wangu. Nilihisi wasiwasi hata zaidi na nikajiwazia: “Wanachokihubiri kinapotoka kutoka kwenye Biblia kwa hivyo ni sharti nimlinde mume wangu na nisimruhusu akubali chochote!” Nilitaka kuwafukuza, lakini niliogopa kuwa mume wangu angefadhaishwa name. Nilichoweza kufanya ni kukaa kimya tu, ingawa sikusikiliza kwa makini neno lolote walilolisema. Lakini mume wangu aliwasikiliza na akaamkia kwa kichwa na hangejizuilia kusema, “Naam! Hilo ni kweli! Ndiyo! Hivyo ndivyo ilivyo. Unaeleza vizuri sana!” Nilipoona mume wangu alivyoshawishiwa sana, ghafla nilihisi mwenye hasira na nikamnyooshea kidole mume wangu na kumkaripia: “Ni nini ambacho ni kweli? Umesoma Biblia kwa kiasi gani? Umemwamini Mungu kwa muda gani? Umemwomba Bwana? Unasema, ‘Kweli, kweli, kweli,’ lakini unaelewa kiasi gani?” Nilipopiga kelele sana, kimya kilijaa chumbani ghafla na wote wakaangaliana. Mume wangu aliniambia kwa haraka, “Usipige kelele. Sikiliza kwanza. Ni vizuri kwetu. Usiposikiliza, utajuaje kama ni sahihi ama si sahihi?” Nilipoona kuwa singeweza kumkomesha kuwasikiliza, nilisukuma maharagwe mbele na nyuma kwa mikono yote miwili na kwa hasira, nikipiga kelele kubwa kimakusudi, na nikafikiria, “Nikuruhusu usikilize? Sitakuruhusu usikie chochote. Nitakomesha jambo hili!” Lakini kupiga kelele sana kwa kutumia maharagwe hakukumzuia mume wangu kusikiliza ushirika wao. Kinyume na hivyo, aliongea na kucheka na wanne hao na ushirika wao ulikuwa patanifu kuridhisha sana. Baada ya kitambo kidogo, mume wangu aliniambia kwa furaha: “Ah, Li! Bwana kwa kweli amerudi. Maneno ya kitabu hiki ni matamshi binafsi ya Mungu! Ni jambo zuri sana! Li, nenda utupikie chakula.” Nilimtupia jicho na sikujibu. Baadaye, Ndugu Lin alimwachia mume wangu tepu kadhaa, kitabu cha nyimbo na nakala ya Neno Laonekana katika Mwili na kisha wakaenda. Singeweza kuvumilia tena na nikamwambia mume wangu, “Je, wafanyakazi wenzetu waandamizi wametuambia mara ngapi kwamba ili kumwamini Mungu, hatupaswi kupotoka kutoka kwenye Biblia, na kwamba kupotoka kutoka kwenye si kumwamini Mungu. Umesahau? Kwa nini huwezi kuchukua msimamo katika suala hili?” Mume wangu alisema bila kusita: “Wanachokisema hakipotoki kutoka kwenye Biblia lakini ni cha juu na cha kina zaidi kuliko Biblia. Aidha, kazi mpya ya Mungu wanayoeneza inatimiza neno la Bwana na unabii wa Kitabu cha Ufunuo. Baada ya kusikiliza ushirika wao, naelewa na nina hakika kuhusu mambo mengi ambayo yamo kwenye Biblia na ambayo sikuwa nimeyaelewa hapo awali. Injili ya Mwenyezi Mungu wanayoshuhudia ni njia ya kweli. Fungua macho yako na utazame. Kuna watu tu wachache waliosalia katika kanisa letu. Kanisa limekuwa mahame. Na bado huachi maneno ya wafanyakazi wenza waandamizi. Je, si huu ni upumbavu mtupu? Ni vyema uharakishe na uchunguze suala hili.” Niliposikia akisema hivi, nilisema kwa hasira, “Unajua nini? Kupotoka kutoka kwenye Biblia ni kumsaliti Bwana. Kama hutafuata Biblia, mimi nitafanya hivyo!”

Baada ya hili, kila siku mara mume wangu alipopata wakati, alisoma kitabu ambacho Ndugu Lin alikiacha, Neno Laonekana katika Mwili. Siku moja, mume wangu aliamka kabla ya mapambazuko kusoma kitabu hicho. Kwa bumbuwazi, nilisikia mume wangu akisoma: “Huenda ikawa umesahau…? Umesahau…?(“Namna Petro Alivyopata Kumjua Yesu”). Niliposikia akisoma kwa sauti, nilihisi mwenye hasira kidogo na nikafikiri: Mapema sana asubuhi na hawaachi watu walale! Baada ya kitambo kidogo, nilisikia kwa sauti hafifu. “Kwa sababu kabla ya Yesu kusulubishwa alikuwa amemwambia: ‘Mimi si wa ulimwengu huu, na wewe pia si wa ulimwengu huu.’(“Namna Petro Alivyopata Kumjua Yesu”). Ni jambo la ajabu! Kwa nini Bwana Yesu ametajwa katika kitabu hiki? Yawezekana kuwa nimesikia vibaya? Kisha nikasikia waziwazi: “Huenda ikawa umesahau…? Umesahau…?” Niliposikia hili, moyo wangu ulisisimuka kidogo na sikuweza kulala tena. Nilijisemea: “Ni nani aliyezungumza maneno haya? Ee Mungu! Ni Wewe unayeniuliza swali hili? Ni kama kwamba Unaninenea maneno haya. Ni yenye huruma sana! Ni sharti niamke haraka na kuandaa kiamsha kinywa. Baada ya kiamsha kinywa nitaona kinachosemwa katika kitabu hicho hatimaye, nione kama kimepotoka kutoka kwenye Biblia au la, na iwapo haya ni maneno ya Mungu au la.”

Baada ya kiamsha kinywa, mume wangu alienda kusoma kitabu hicho tena. Nilijiwazia: Kwa nini hakunialika nisome kitabu hicho pamoja naye? Nilisimama mlangoni kwa muda mrefu, lakini mume wangu alizamisha kichwa chake katika kitabu hicho na hakunitilia maanani. Kwa hivyo nilienda na kurudi jikoni. Nilihisi wasiwasi sana. Nilitaka sana kusoma kilichokuwa kimeandikwa katika kitabu hicho. Kwa hivyo nilisukumiza kichwa changu chumbani na nikaona mume wangu bado alikuwa amezamisha kichwa chake katika kitabu hicho. Nilitaka kwenda kukisoma pia, lakini nilipofikiri kuhusu mara nyingi ambazo ndugu walikuwa wamekuja kunihubiria na jinsi ambavyo nilikuwa nimekataa kila mara, nilijiuliza iwapo mume wangu angenikosoa iwapo ningeanza kukisoma mwenyewe. Iwapo angenikosoa, ningehisi kufedheheka! Nilipofikiria hili, niliacha kufanya hivyo. Nilipokuwa nikienda na kurudi kule nje, nilikumbuka maneno ambayo mume wangu alikuwa ameyasoma kwa sauti asubuhi na nikawa na wasiwasi hata zaidi. Nilifikiria: Hili halitasaidia. Ni sharti niingie na nione kitabu hicho kinahusu nini. Lakini nilirudi nyuma tena nilipofika mlangoni. Kama paka aliyekuwa kwenye matofali moto, sikujua nifanye nini. Hatimaye, niliamua: Ah! Mungu anataka niseme kwa sauti! Ni nani aliyeniambia nizungumze namna hiyo na nisisikize ushauri wa mume wangu? Kwa hivyo, nilijikaza na nikaingia chumbani na, huku nikijipa moyo, nilisema kwa fedheha, “Je, ninaweza kukisoma na wewe?” Aliniangalia kidogo na akaonekana kushangaa sana, kisha akasema kwa furaha, “Njoo, njoo! Hebu tusome pamoja.” Wakati huu, niliguswa sana! Mume wangu hakunikosoa kama nilivyokuwa nimedhania! Moyo wangu uliokuwa na wasiwasi hatimaye ulitulia na nikasoma kitabu hicho pamoja na mume wangu kwa furaha. Hata hivyo, maneno niliyosoma katika kitabu hicho hayakuwa yale niliyoyasikia hapo saa za mapema asubuhi! Mara moja, mume wangu alitoka nje, na nikafungua kurasa za kitabu hicho kwa haraka. Ghafla, niliona kile nilichokuwa nikitafuta, na nikasoma kwa furaha na kwa sauti: “Petro alihimizwa pakubwa na maneno yake Yesu, kwa sababu kabla ya Yesu kusulubishwa alikuwa amemwambia: ‘Mimi si wa ulimwengu huu, na wewe pia si wa ulimwengu huu.’ Baadaye, wakati Petro alipofikia hali ya maumivu makali, Yesu alimkumbusha: ‘Petro, je, umesahau? Mimi si wa ulimwengu huu, na ni kwa ajili tu ya kazi Yangu ndipo Niliondoka mapema. Wewe pia si wa ulimwengu huu, umesahau? Nimekuambia mara mbili, kwani hukumbuki?’ Petro alimsikia na kumwambia: ‘Sijasahau!’ Yesu naye akasema: ‘Uliwahi kuwa na wakati mzuri ukiwa umekusanyika pamoja na Mimi kule mbinguni na kwa kipindi fulani kando Yangu mimi. Unanidata Mimi, na Mimi ninakudata. Ingawa viumbe hawa hawastahili kutajwa machoni Pangu, ninawezaje kukosa kupenda yule ambaye hana hatia na anapendeka? Je, umesahau ahadi Yangu? Lazima ulikubali agizo Langu hapa ulimwenguni, lazima utimize kazi Niliyokuaminia. Bila shaka siku moja Nitakuongoza kuwa kando Yangu’(Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Namna Petro Alivyopata Kumjua Yesu). Nilikisoma mara kadhaa na kadiri nilivyozidi kukisoma ndivyo nilivyozidi kuhisi kuwa maneno haya hayakupotoka kutoka kwenye Biblia. Yalikuwa tu yakini zaidi na bayana zaidi kuliko Biblia. Lakini wafanyakazi wenzangu waandamizi walikuwa wamesema, “Yeyote anayeeneza ujumbe wa Mungu kuja kufanya kazi mpya na Mungu kunena maneno mapya anapotoka kutoka kwenye Biblia, na kupotoka kutoka kwenye Biblia ni kupotoka kutoka kwenye njia ya Bwana.” Lakini walichokuwa wamekisema hakikulingana na ukweli, siyo? Niliomba katika moyo wangu: “Ee Mungu! Haya yote yanamaanisha nini? Na Unipe nuru na kuniongoza ili nifahamu mapenzi Yako. …”

Baadaye, niliona kuwa maneno ya Mwenyezi Mungu yalisema: “Kwa miaka mingi, imani ya watu ya kitamaduni (hiyo ya Ukristo, moja ya dini kuu tatu za dunia) imekuwa ni kusoma Biblia; kujitenga na Biblia sio imani kwa Bwana, kujitenga na Biblia ni kufuata imani tofauti tofauti na uzushi, na hata pale watu wanaposoma vitabu vingine, msingi wa vitabu hivi ni lazima uwe ni ufafanuzi wa Biblia. Ni kusema kwamba, kama unasema unamwamini Bwana, basi ni lazima usome Biblia, unapaswa kula na kunywa Biblia, na nje ya Biblia hupaswi kuabudu kitabu kingine ambacho hakihusishi Biblia. Ikiwa utafanya hivyo, basi unamsaliti Mungu. Kuanzia kipindi ambapo kulikuwa na Biblia, imani ya watu kwa Bwana imekuwa imani katika Biblia. Badala ya kusema watu wanamwamini Bwana, ni bora kusema kwamba wanaamini Biblia; badala ya kusema wameanza kusoma Biblia, ni bora kusema wameanza kuamini Biblia; na badala ya kusema wamerudi mbele ya Bwana, ingekuwa vyema kusema wamerudi mbele ya Biblia. Kwa njia hii, watu wanaiabudu Biblia kana kwamba ni Mungu, kana kwamba ni damu yao ya uzima na kuipoteza itakuwa ni sawa na kupoteza maisha yao. Watu wanaitazama Biblia kuwa ni kuu kama Mungu, na hata kuna wale wanaoiona kuwa ni kuu kuliko Mungu. Kama watu hawatakuwa na kazi ya Roho Mtakatifu, ikiwa hawawezi kuhisi Mungu, wanaweza kuendelea kuishi—lakini punde tu watakapoipoteza Biblia, au kupoteza sura na maneno maarufu sana kutoka katika Biblia, basi inakuwa ni kana kwamba wamepoteza maisha yao(Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Kuhusu Biblia (1)). Maneno ya Mungu yaliugusa moyo wangu sana. Je, si hili lilisema kunihusu kwa kweli? Nilipokumbuka wakati ambapo nilianza kumwamini Bwana, hivi ndivyo nilivyotetea imani yangu. Nilichukulia Biblia kama kitu kinachonitia nguvu. Nililazimika kuiweka juu kila wakati baada ya kuisoma, kwa kuogopa kuwa watoto wangeigusa. Nilikuwa nimechukulia Biblia kama iliyozidi vitu vingine vyote na hata nilikuwa nimefikiria kupotoka kutoka kwenye Biblia kulikuwa kumsaliti Bwana. Je, nilikuwa nimekosea kufanya hivi? Kwa moyo wa kutafuta, niliendelea kusoma, kuanzia “Kuhusu Biblia (1)” hadi “Kuhusu Biblia (4).” Kadiri nilivyozidi kusoma ndivyo nilivyozidi kuhisi kunurishwa. Maneno ya Mwenyezi Mungu yalinifanya nielewe kikamilifu. Ilitokea kuwa Biblia ilikuwa rekodi tu ya historia ya kazi ya Mungu na ushuhuda wa hatua mbili za kwanza za kazi ya Mungu. Kama tu jinsi ambavyo Agano la Kale linarekodi kazi iliyofanywa na Yehova Mungu kuanzia uumbaji wa dunia hadi mwisho wa Enzi ya Sheria, Agano Jipya linarekodi kazi ya Bwana Yesu katika Enzi ya Neema. Kazi ya Mungu ni mpya kila wakati, haizeeki na husonga mbele kila wakati. Sasa Mungu amefanya kazi mpya nje ya Biblia—kazi ya Enzi ya Ufalme. Hatua hii ya kazi ni hatua ya mwisho ya kazi ya wokovu ya Mungu kwa wanadamu. Kuanzia Enzi ya Sheria, hadi Enzi ya Neema na kisha Enzi ya Ufalme katika nyakati za mwisho, hatua zote tatu zinafanywa na Mungu mmoja. Kusoma maneno ya Mwenyezi Mungu kulikuwa kambo kuu la kunizindua, na nilifurahisha macho yangu kwa kuyaangalia yale maneno! Ndiyo, Mungu ni mwenye uweza sana na hekima, Angewezaje kufanya kazi chache iliyorekodiwa kwenye Biblia? Na kutokana na maneno ya Mwenyezi Mungu, niliona kwa kweli kuwa maneno na kazi ya Mungu ya siku za mwisho havikukana Biblia. Badala yake, viliinua na kuzidisha kazi ya Enzi ya Sheria na Enzi ya Neema kama ilivyoandikwa katika Biblia, na kila kitu ambacho Mungu anafanya sasa kinakubaliana zaidi na mahitaji ya sasa ya watu. Kifungu kimoja cha maneno ya Mungu chasema: “Unapaswa kuelewa ni kwa nini leo unaambiwa usisome Biblia, kwa nini kuna kazi nyingine ambayo inajitenga na Biblia, kwa nini Mungu haonekani mpya na wa kina zaidi katika Biblia, kwa nini badala yake kuna kazi kubwa zaidi nje ya Biblia. Haya ndiyo yote mnayopaswa kuelewa. Unapaswa kuelewa tofauti kati ya kazi ya zamani na kazi mpya, na hata kama hausomi Biblia, unapaswa kuitenganisha; kama hautaweza, bado utakuwa unaiabudu Biblia, na itakuwa ni vigumu sana kwako kuingia katika kazi mpya na kupitia mabadiliko mapya. Kwa kuwa kuna njia ya juu, kwa nini mjifunze hiyo ya chini, njia ya kale? Kwa kuwa kuna matamshi mapya, na kazi mpya, kwa nini uishi katikati ya rekodi za kale za kihistoria? Matamshi mapya yanaweza kukupa, ambayo yanathibitisha kwamba hii ni kazi mpya; rekodi za kale haziwezi kukushibisha, au kutosheleza mahitaji yako ya sasa, kitu ambacho kinathibitisha kwamba ni historia, na sio kazi ya hapa na sasa. Njia ya juu zaidi ni njia mpya zaidi, na kazi mpya, bila kujali njia ya zamani ni ya juu kiasi gani, bado ni historia ya kumbukumbu ya watu, na haijalishi ina thamani kiasi gani kama rejeleo, bado ni njia ya kale. Ingawa imerekodiwa katika ‘kitabu kitakatifu,’ njia ya kale ni historia; ingawa hakuna rekodi yake katika ‘kitabu kitakatifu,’ njia mpya ni ya hapa na sasa. Kwa njia hii inaweza kukuokoa, na kwa njia hii inaweza kukubadilisha, maana hii ni kazi ya Roho Mtakatifu(Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Kuhusu Biblia (1)). Wakati huu, niliona nuru ghafla, na nikatambua ni kwa nini nilitetea Biblia siku zote lakini roho yangu ilizidi kuwa hasi sana kiasi kwamba nilikuwa nimekosa mambo ya kuhubiri; nilitambua ndugu pia waliendelea kuwa dhaifu zaidi na zaidi, hadi kufikia kiwango ambacho hata hawakuhudhuria mikutano, wakati ambapo wale ndugu ambao walikuwa wamekubali injili ya ufalme ya Mwenyezi Mungu walikuwa wamejaa imani. Bila kujali nilivyowatendea, hawakuwahi kuwa hasi wala kukata tamaa, na bado walikuja tena na tena kunihubiria injili. Sababu ya hili ni kwamba nilichokuwa nikishikilia ni kazi ya Mungu iliyopita. Ilikuwa njia ya kale, ambayo ilikuwa imepoteza kazi ya Roho Mtakatifu zamani. Hata hivyo, ndugu wa Kanisa la Mwenyezi Mungu walikuwa wamekubali uongozi wa kazi mpya ya Mungu, walikuwa wamepokea ruzuku ya maneno ya Mungu ya wakati huu na kupata kazi ya Roho Mtakatifu. Hii ndiyo ilikuwa tofauti kati ya njia mpya na njia ya kale! Hii ndiyo iliyokuwa sababu kuu ya ulimwengu wa dini kudidimia, na Kanisa la Mwenyezi Mungu kuendelea kusitawi zaidi na zaidi! “Bwana” niliomba. “Sasa hatimaye naelewa kwamba Umerudi kwa kweli, na Umetupa njia mpya, ruzuku mpya ya uzima. Nakushukuru!”

Wakati huu, hisia zangu zilipata shida ya kuchagua kati ya furaha na kuhisi vibaya. Nilifurahia kwamba Mungu hakuwa ameniacha, licha ya mimi kuwa mwasi na asiye tii, na kwamba Alikuwa ametumia njia hii maalum ya mume wangu kusoma maneno ya Mungu kwa sauti ili kunifanya nisikie sauti ya Mungu. Huu kweli ulikuwa upendo wa Mungu kwangu na wokovu Wake kwangu! Nilihisi vibaya kwa sababu nilikuwa nimesubiri kwa hamu kurudi kwa Bwana kwa miaka mingi, na sikuwahi kufikiria uwezekano wa kumkana Bwana wakati ambapo angerudi na kubisha mlangoni pangu. Ndugu hao walikuja tena na tena kueneza injili kwangu, lakini nilichokifanya ni kuwapuuza. Walishiriki na mume wangu lakini niliwadhihaki na nikawasumbua kwa makusudi…. Nilipofikira hili, moyo wangu ulihisi huzuni na singezuia machozi kutiririka kutoka machoni pangu. Nilipiga magoti mbele za Mungu na nikamwomba: “Mwenyezi Mungu! Nilikuwa nimekosea. Kwa miaka mingi sana nilishikilia Biblia kila wakati na nikafikiri kuwa kupotoka kutoka kwenye na Biblia si kumwamini Mungu. Nilichukulia Biblia kama Mungu na nikakataa ujio Wako. Nilikuwa kipofu sana! Sasa niko radhi kuweka kando Biblia, kufuata kazi Yako mpya na kusikiliza maneno Yako ya enzi mpya. Sitakuwa kamwe mwenye uhasama Kwako na siko radhi kukubali maisha yangu yote yaharibiwe na mawazo na fikira zangu. Ee Mungu! Natamani kufanya azimio, kushirikiana na Wewe na kuwarudisha wale walioko kanisani ambao wanakuamini kwa kweli katika familia Yako ili nifidie kile Unachonidai.”

Iliyotangulia: 5. Moyo Unaorandaranda Wakuja Nyumbani

Inayofuata: 7. Jinsi Nilivyokaribia Kuwa Mwanamwali Mjinga

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Maudhui Yanayohusiana

2. Njia ya Utakaso

Na Christopher, UfilipinoJina langu ni Christopher, na mimi ni mchungaji wa kanisa la nyumbani huko Ufilipino. Mnamo mwaka wa 1987,...

38. Wokovu wa Aina Tofauti

Na Huang Lin, ChinaNilikuwa mwumini wa kawaida katika Ukristo wa Kipaji, na tangu nianze kuamini katika Bwana sikuwahi kukosa ibada....

40. Kuja Nyumbani

Na Muyi, Korea ya Kusini“Upendo mwingi wa Mungu amepewa binadamu kwa ukarimu, unamzunguka binadamu; binadamu ni mnyofu na asiye na hatia,...

23. Kuwa katika Hatari Kubwa

Nilikubali kazi ya Mwenyezi Mungu ya siku za mwisho zaidi ya mwezi mmoja uliopita. Mchungaji na wazee hawajaacha kunisumbua na kuwashawishi...

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp