Tunawakaribisha wote wanaotafuta ukweli wawasiliane nasi.

Mfuateni Mwanakondoo na Kuimba Nyimbo Mpya

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

(Ma)tokeo ya Kutafuta 0

Hakuna matokeo yaliyopatikana

273 Ee Mungu, Nakukosa

1

Kwa kimya, bila neno nakutamani sana, ninasoma maneno Yako na kuhisi majuto zaidi.

Macho yangu yamejaa machozi, natumaini kuwa na Wewe tena hivi karibuni.

Moyo wangu mgumu umekukosea mara nyingi, makosa mengi yasiyoweza kurekebishwa.

Moyo wangu huumia nisipoweza kuuona uso Wako, nakungojea Wewe,

katika majira ya kuchipua, ya joto, ya kupukutika kwa majani na ya baridi.

Mchana na usiku zinapita zikiwa zimejaa kujilaumu.

Machozi ya hatia yanatiririka chini usoni mwangu, nimejawa na majuto.

Natamani sana kuondoa makosa ya zamani, natamani kuufungua moyo wangu Kwako.

2

Nimejaa kumbukumbu ya siku hizo za furaha, mara nyingi mimi hufikiria kuhusu uso Wako na tabasamu Yako.

Sauti ya kicheko Chako kinasikika masikioni mwangu, siwezi kusahau haya katika maisha yangu yote.

Miaka hii mingi imeniletea mateso, upweke wangu na kuyumbayumba hakuvumiliki.

Ninaota kuhusu kuurejesha wakati nyuma, ninatamani sana kuwa na Wewe.

Uko wapi, mpendwa wangu?

Moyo wangu una hamu kubwa ya kuuona uso Wako, kuingia katika kumbatio Lako.

Moyo wangu daima utakuwa katika mapatano na Wako, na kujenga wimbo mzuri wa upendo.

Iliyotangulia:Kujitolea Kwa Upendo

Inayofuata:Mungu Anatupenda Sana

Maudhui Yanayohusiana