Programu ya Kanisa la Mwenyezi Mungu

Sikiliza sauti ya Mungu na ukaribishe kurudi kwa Bwana Yesu!

Tunawakaribisha wote wanaotafuta ukweli wawasiliane nasi.

Mfuateni Mwanakondoo na Kuimba Nyimbo Mpya

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

(Ma)tokeo ya Kutafuta 0

Hakuna matokeo yaliyopatikana

Kumtamani Sana Mwenyezi Mungu

1 Ee Mungu, ee Mungu! Tunakutamani sana. Unakuwa mwili, Mwana wa Adamu, na kutembea kati ya makanisa. Maneno Yako yanatunyunyizia na kutukimu, Unatuongoza na kutusaidia kwa wakati unaofaa. Tunafurahia maneno Yako kila siku, tukiishi mbele Yako, mioyo yetu ni mitulivu na yenye amani. Ee Mungu, ee Mungu! Mwenyezi Mungu wetu mpendwa. Hukumu na ufunuo wa maneno Yako huturuhusu kuiona dunia wazi, tuepuke kudhuru kwa Shetani na kuingia katika njia sahihi maishani. Neema ya wokovu Wako haiwezi kusahaulika, imechongwa mioyoni mwetu. Tunakutamani sana!

2 Ee Mungu, ee Mungu! Tunakutamani sana. Unatamka maneno na kufanya kazi kati yetu kila siku. Unatumia maneno kutukumbusha na kutusihi, na kutuhukumu na kutufunua kwa ukali. Tumeona upotovu wetu ni wa kina sana, tunajuta sana na hatuna mahali pa kujificha, uchaji wetu Kwako unakua. Ee Mungu, ee Mungu! Mwenyezi Mungu wetu mpendwa. Ili tuweze kukua maishani, Umetamka kila neno linalowezekana na kufanya kazi kwa moyo wote. Unatuhukumu na kututakasa ili tuokolewe na kupata upendo Wako wote. Hii ni baraka kwetu, tunakua karibu na Wewe.

3 Ee Mungu, ee Mungu! Tunakutamani sana. Umekuwa nasi daima katika mateso ya CCP, maneno Yako hutuongoza kwa wakati unaofaa. Hatuogopi au kuhofu tena, tumeonja mamlaka na nguvu ya maneno Yako. Tunasimama imara na wenye nguvu katikati ya kuteseka kwetu, tunakushuhudia na kukutukuza. Ee Mungu, ee Mungu! Mwenyezi Mungu wetu mpendwa. Maneno Yako hutuongoza kumshinda adui Shetani. Katika shida na majaribu tunahisi upendo Wako, mioyo yetu inakuwa karibu na Wewe. Tunaona utakatifu na haki Yako, uweza na hekima Yako, tutakusifu milele.

4 Ee Mungu, ee Mungu! Tunakutamani sana. Umefanya kazi kwa miaka mingi, ukiishi pamoja nasi. Ulijawa na kicheko na furaha, ukiacha kumbukumbu nzuri sana. Hatuwezi kusahau upendo Wako wa kweli, mioyo yetu ilijawa na upendo Kwako zamani sana; tumeamua kuwa waaminifu Kwako milele. Ee Mungu, ee Mungu! Mwenyezi Mungu wetu mpendwa. Tunakumbuka kusihi Kwako, tunatenda maneno Yako, na tunatimiza kwa bidii wajibu wetu kukushuhudia na kukutukuza. Duniani tutakutii na kukuabudu milele. Daima tutapotana na Wewe, hatuwezi kamwe kutengana na Wewe.

Iliyotangulia:Hukumu Huninitakasa

Inayofuata:Naomba Niwe na Mungu Milele

Maudhui Yanayohusiana

 • Nitampenda Mungu Milele

  Ⅰ Ee Mungu! Maneno Yako yameniongoza kurudi Kwako. Nakubali kufundishwa katika ufalme Wako mchana na usiku. Majaribu mengi na uchungu, dhiki nyingi s…

 • Umuhumi wa Maombi

  I Maombi ni njia moja ya mwanadamu kishirikiana na Mungu, kuita Roho Wake na kuguswa na Mungu. Kadiri unavyoomba zaidi, ndivyo utakavyoguswa zaidi, ku…

 • Kusudi la Kazi ya Mungu la Usimamizi

  Ⅰ Mungu ana mpango wa usimamizi wa miaka 6,000, uliyogawanywa katika hatua tatu, kila moja inaitwa enzi. Kwanza ni Enzi ya Sheria, kisha Enzi ya Neema…

 • Wewe Tu Unaweza Kuniokoa Mimi

  Ⅰ Mnyenyekevu na Uliyejificha, Wewe unaambatana na watu katika matatizo yao, Ukiwapa njia ya uzima wa milele. Unawapenda binadamu kama mwili Wako mwe…