Programu ya Kanisa la Mwenyezi Mungu

Sikiliza sauti ya Mungu na ukaribishe kurudi kwa Bwana Yesu!

Tunawakaribisha wote wanaotafuta ukweli wawasiliane nasi.

Mfuateni Mwanakondoo na Kuimba Nyimbo Mpya

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

(Ma)tokeo ya Kutafuta 0

Hakuna matokeo yaliyopatikana

Matamanio ya Dhati ya Kutubu

I

Kwa kuwa siku ya Mungu ya utukufu inakaribia,

moyo wangu umejaa huzuni na wasiwasi.

Uasi wangu wa Mungu naukumbuka kwa majuto,

mawazo ya wasiwasi huibuka juu ya deni langu kwake.

Mungu alinichagua, ili niweze kujiunga na karamu ya ufalme.

Mungu huonyesha njia tunayopaswa kufuatilia.

Ananisihi mara kwa mara, lakini sisikilizi.

Ninashindwa kupata ukweli, na sina ujasiri wa kumkabili Mungu.

Kumwamini Mungu lakini kutoweza

kumridhisha Yeye ni jambo la aibu.

Kushindwa kutimiza yote Mungu ameyafanya,

ninajua kwa kweli ni deni gani ninalowiwa Naye.

Nitakata shauri kutafuta ukweli,

kutumia maisha yangu yote kulipia neema yote ya Mungu.

Kipawa adimu namna gani kutoka kwa Mungu

kutenga saa zangu za mwisho Kwake.

II

Ninaziona kanuni kama ukweli wa uhalisi.

Ninatenda kazi ngumu badala ya ukweli,

hakuna bidii katika wajibu wangu, udanganyifu tu.

Ninapopogolewa, ninatetea na sitatii.

Mungu hupanga vitu vyote kunisaidia kupata ukweli.

Lakini mimi siitii au kutafuta ukweli.

Natembea kwa ukaidi kwa njia ya Mafarisayo, sitarudi nyuma.

Kuchukiwa na Mungu, maisha ni giza, baya zaidi kuliko kifo.

Kumwamini Mungu lakini kutoweza

kumridhisha Yeye ni jambo la aibu.

Kushindwa kutimiza yote Mungu ameyafanya,

ninajua kwa kweli ni deni gani ninalowiwa Naye.

Nitakata shauri kutafuta ukweli,

kutumia maisha yangu yote kulipia neema yote ya Mungu.

Kipawa adimu namna gani kutoka kwa Mungu

kutenga saa zangu za mwisho Kwake.

III

Maneno ya Mungu ya hukumu yanapitia moyo wangu kama mapanga,

yakiuacha kwa maumivu na mateso.

Hapo tu ndipo moyo wangu wenye ganzi na usiojua huanza kusisimka,

na ninachukia kukimbia kwangu kwa bidii kutoka kwa ukweli.

Yote ninayoishi kudhihirisha ni tabia ya Shetani,

Sina misimamo ya ukweli na ni mawazo yangu tu katika wajibu.

Na hakuna kitu kimoja ninachofanya kinachoweza kuitwa tendo jema.

Mimi sistahili kabisa kufurahia maneno ya Mungu.

Kumwamini Mungu lakini kutoweza

kumridhisha Yeye ni jambo la aibu.

Kushindwa kutimiza yote Mungu ameyafanya,

ninajua kwa kweli ni deni gani ninalowiwa Naye.

Nitakata shauri kutafuta ukweli,

kutumia maisha yangu yote kulipia neema yote ya Mungu.

Kipawa adimu namna gani kutoka kwa Mungu

kutenga saa zangu za mwisho Kwake,

kutenga saa zangu za mwisho Kwake.

Iliyotangulia:Neno la Mungu ni Nuru

Inayofuata:Njia za Mungu Haziwezi Kueleweka

Maudhui Yanayohusiana

 • Wewe Tu Unaweza Kuniokoa Mimi

  Ⅰ Mnyenyekevu na Uliyejificha, Wewe unaambatana na watu katika matatizo yao, Ukiwapa njia ya uzima wa milele. Unawapenda binadamu kama mwili Wako mwe…

 • Umuhumi wa Maombi

  I Maombi ni njia moja ya mwanadamu kishirikiana na Mungu, kuita Roho Wake na kuguswa na Mungu. Kadiri unavyoomba zaidi, ndivyo utakavyoguswa zaidi, ku…

 • Njia Yote Pamoja na Wewe

  I Nilikuwa kama mashua, ikielea baharini. Ulinichagua, na mahali pazuri Uliniongoza. Sasa katika familia Yako, nikipewa joto na upendo Wako, nina ama…

 • Jinsi Upendo wa Mungu kwa Mwanadamu Ulivyo Muhimu

  Mandhari iliyochorwa katika Biblia "Amri ya Mungu kwa Adamu" ni ya kugusa na yenye kutia moyo. Ingawa hiyo picha ina Mungu na mtu tu, uhusiano kati ya…