263 Niliona Upendo wa Mungu katika Kuadibu na Hukumu

1

Ee Mungu! Ingawa nimevumilia mamia ya majaribio na mateso,

na hata nimekuwa karibu na kifo,

mateso hayo yameniruhusu kukujua Wewe

kwa kweli na kupata wokovu mkuu.

Kama adabu Yako, hukumu

na nidhamu vingeondoka kutoka kwangu,

basi ningeishi gizani,

chini ya himaya ya Shetani.

Ee Mungu! Ninakusihi,

nakuomba usichukue faraja yangu kubwa kutoka kwangu,

hata kama ni maneno machache tu ya uhakikisho.

Nimefurahia upendo wako,

na leo hii siwezi kuwa mbali na Wewe;

jinsi gani, Nieleze, singeweza kukupenda Wewe?

2

Mwili wa binadamu una faida gani?

Kama adabu Yako na hukumu ingeniwacha,

ingekuwa kana kwamba Roho Wako alikuwa ameniacha,

ni kama Wewe Haukuwa tena pamoja nami.

Kama Wewe utanipa ugonjwa, na kuchukua uhuru wangu,

naweza kuendelea kuishi,

lakini adabu Yako na hukumu vikiondoka kutoka kwangu,

sitakuwa na njia ya kuendelea kuishi.

Ee Mungu! Ninakusihi,

nakuomba usichukue faraja yangu kubwa kutoka kwangu,

hata kama ni maneno machache tu ya uhakikisho.

Nimefurahia upendo wako,

na leo hii siwezi kuwa mbali na Wewe;

jinsi gani, Nieleze, singeweza kukupenda Wewe?

3

Kama ningekuwa bila adabu Yako na hukumu,

ningepoteza upendo Wako,

upendo ambao ni mkuu sana mpaka

sina maneno ya kuueleza.

Bila Upendo wako, ningeishi chini ya himaya ya Shetani,

na singeweza kuuona uso wako mtukufu.

Jinsi gani, Nieleze, ningeweza kuendelea kuishi?

Giza kama hili, maisha kama haya, singeweza kuvumilia.

Mimi kuwa na wewe ni kama kukuona Wewe,

hivyo ni jinsi gani ningeweza kukuacha?

Ee Mungu! Ninakusihi,

nakuomba usichukue faraja yangu kubwa kutoka kwangu,

hata kama ni maneno machache tu ya uhakikisho.

Nimefurahia upendo wako,

na leo hii siwezi kuwa mbali na Wewe;

jinsi gani, Nieleze, singeweza kukupenda Wewe?

4

Nimemwaga machozi mengi ya huzuni kwa sababu ya upendo Wako,

ilhali daima nimehisi kuwa maisha kama haya ni ya maana zaidi,

yenye uwezo mwingi wa kuniimarisha, yenye uwezo zaidi wa kunibadilisha,

na yenye uwezo zaidi wa kunifanya nifikie ukweli ambao lazima viumbe wawe nao.

Ee Mungu! Ninakusihi,

nakuomba usichukue faraja yangu kubwa kutoka kwangu,

hata kama ni maneno machache tu ya uhakikisho.

Nimefurahia upendo wako,

na leo hii siwezi kuwa mbali na Wewe;

jinsi gani, Nieleze, singeweza kukupenda Wewe?

Iliyotangulia: 262 Napata Mengi Sana Kutoka kwa Hukumu na Kuadibu kwa Mungu

Inayofuata: 264 Siwezi Kumudu Bila Hukumu na Kuadibu kwa Mungu

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Maudhui Yanayohusiana

418 Umuhumi wa Maombi

Sala ni mojawapo ya njia ambazo mwanadamu hutumia kushirikiana na Mungu, ni njia ambayo mwanadamu hutumia kumwita Mungu, na ni mchakato...

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp