85. Wakati wa mateso Ya Kikatili

Na Chen Hui, China

Nililelewa katika familia ya kawaida nchini China. Baba yangu alikuwa katika jeshi na kwa sababu nilikuwa nimeongozwa na kuathiriwa naye tangu utotoni, nilikuja kuamini kuwa wito wa askari na wajibu wake ulikuwa kuitumikia nchi yake, kufuata taratibu na kutumikia bila ubinafsi kwa niaba ya Chama cha Kikomunisti na kwa niaba ya watu. Pia mimi niliazimia kuwa mwanajeshi na kufuata katika nyayo za baba yangu. Hata hivyo, kadri muda ulivyoendelea na matukio fulani kubainika, mwendo wa maisha yangu na mwelekeo wa shughuli zangu vilibadilika pole pole. Mnamo mwaka wa 1983, niliisikia injili ya Bwana Yesu. Ulikuwa mwongozo maalum wa Roho Mtakatifu uliomwezesha mtu kama mimi, aliyekuwa amepotoshwa na imani kwamba hakuna Mungu na itikadi ya Kikomunisti ya Kichina tangu umri mdogo, hadi kuvutiwa sana na upendo wa Bwana Yesu. Baada ya kuisikia injili, niliingia katika maisha ya kumwamini Mungu—nikaanza kwenda kanisani, kusali, na kuimba nyimbo za kumsifu Bwana. Maisha haya mapya yaliniletea utulivu na amani kuu. Mnamo mwaka wa 1999, niliikubali injili ya siku za mwisho za Bwana Yesu aliyerejea—Mwenyezi Mungu. Kupitia kusoma neno la Mungu bila kukoma na kukutana na kushiriki na ndugu zangu, nilikuja kuelewa ukweli mwingi na kujifunza kuhusu kusudi la Mungu la haraka la kuwaokoa wanadamu. Nilihisi kuwa Mungu amempa kila mmoja wetu wito na wajibu mkubwa, na kwa hivyo nilianza kufanya kazi ya kueneza injili kwa bidii.

Hata hivyo, mateso ya kikatili ya serekali ya CCP yaliharibu kabisa maisha yangu matulivu na yenye furaha. Mnamo Agosti 2002, nilisafiri kwenda kaskazini magharibi pamoja na mume wangu ili kueneza injili kwa baadhi ya wafanyikazi wenzetu katika Kristo. Usiku mmoja, nilipokuwa nikikutana na ndugu wawili ambao hivi karibuni walikuwa wameikubali kazi ya Mungu katika siku za mwisho, ghafla nilisikia kishindo kikubwa na nikauona mlango ukipigwa teke na kuangushwa kwa nguvu na polisi sita au saba walioonekana katili na waliobeba virungu wakaingia. Mmoja wa polisi hao alinielekezea kidole na kunikaripia kwa ukali, “Mfunge pingu!” Polisi wawili walituamuru tusimame kando ya ukuta na tusisonge, huku wakianza kupekua masanduku na makasha ndani ya nyumba kama kundi la majambazi wa kuvamia. Walitafuta kwa makini chochote walichodhania kuwa kinaweza kutumiwa kuficha vitu na, baada ya muda mfupi, walikuwa wameifudikiza sehemu nzima. Mwishowe, mmoja wa polisi alipata kijitabu cha injili na kitabu cha neno la Mungu katika mkoba wa dada yangu na kunitazama kwa macho makali, akisema kwa sauti kubwa, “Ala, kwani unajaribu kujitafutia kuuawa? Unakuja hapa na kueneza injili yako. Je, hii ilitoka wapi?” Sikumjibu na kwa hivyo akanifokea akisema, “Hivyo hutoongea, au siyo? Tutakifungua hicho kinywa chako. Twende! Utazungumza kule tunakokwenda!” Aliposema hivyo aliniburuta kutoka nyumbani na kunitupa ndani ya gari la polisi. Wakati huo, niligundua kuwa hawakuwa wamewatuma polisi sita au saba tu—polisi spesheli waliobeba silaha walikuwa wamepiga foleni kwenye pande zote za barabara iliyokuwa nje. Nilipoona idadi ya askari waliotumia ili kutukamata, niliogopa sana na, bila kufikiria, nilianza kumwomba Mungu nikimwomba mwongozo na ulinzi Wake. Muda mfupi baadaye, kifungu cha neno la Mungu kilinijia akilini mwangu, “Unapaswa kujua kwamba vitu vyote vilivyo katika mazingira yanayo wazunguka vipo hapo kwa ruhusa Yangu, Mimi napanga yote. Oneni wazi na muridhishe moyo Wangu katika mazingira Niliyokupa. Msiogope, Mwenyezi Mungu wa majeshi hakika atakuwa pamoja nawe; Yeye anawasaidia na Yeye ni ngao yenu(Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Matamko ya Kristo Mwanzoni, Sura ya 26). “Hiyo ni kweli!” Niliwaza. “Mungu ndiye nguzo yangu; haijalishi ni aina gani ya hali ninayoweza kukabiliwa nayo, Mungu, Mtawala na Muumba wa vitu vyote, Yeye yuko kando yangu kila wakati. Ataniongoza kushinda hali yoyote ambayo ninaweza kuikabili. Yeye ni mwaminifu na Yeye ndiye Anayetawala na kupanga vitu vyote.” Nilipofikiria mambo haya, nilirudiwa tena na hali ya utulivu.

Ilikuwa mnamo saa kumi usiku huo nilipofikishwa kwenye Kitengo cha Upelelezi wa Jinai. Picha yangu ilichukuliwa, nami nikaongozwa katika chumba cha mahojiano. Jambo la kushangaza, tayari humo ndani kulikuwepo na majambazi wanne au watano walioonekana katili walionikazia macho nilipoingia. Mara tu nilipoingia ndani ya chumba hicho, walinizunguka kama kundi la mbwa mwitu wenye njaa wakionekana kuwa tayari kulishambulia windo. Nilikuwa na woga sana nami nikamwomba Mungu sana. Mwanzoni, polisi hawa jambazi hawakunigusa, lakini waliniamuru nisimame kwa muda wa saa tatu au nne. Nilisimama kwa muda mrefu kiasi kwamba miguu na nyayo zangu zilianza kuuma kwa maumivu na kufa ganzi, na mwili wangu wote ukachoka sana. Karibu saa saba au nane alfajiri, mkuu wa Kitengo cha Upelelezi wa Jinai aliingia kunihoji. Sikujizuia kutetemeka kwa wasiwasi. Alinikazia macho na kuanza kunihoji kwa ukali akisema, “Ongea! Unatoka wapi? Ni nani unayewasiliana naye hapa? Nani mkuu wako? Mmekuwa mkikutana wapi? Una watu wangapi wanaokufanyia kazi?” Nilipokosa kuongea, alikasirika, akaninyakua kwa nywele na kunipiga mangumi na mateke mengi. Mara tu nilipopigwa na kuanguka sakafuni, aliendelea kunipiga mateke hata zaidi. Masikio yangu yalianza kuwangwa mara moja kiasi kwamba sikuweza kusikia chochote, na kichwa changu kilihisi kana kwamba kitalipuka kwa maumivu ya kuchoma. Sikujizuia kulia kwa maumivu. Baada ya kupambana kwa muda mfupi, nililala sakafuni, nikashindwa kusonga. Yule mkuu alininyakua kwa nywele tena na kuniburuta ili nisimame, na ndipo majambazi hao katili wanne au watano wakanizunguka na kuanza kunipiga mateke na ngumi; nilianguka chini, mikono yangu ikikifunika kichwa changu, nikibingiria na kugaagaa kwa maumivu. Polisi hawa jambazi hawakuzuia chochote—kila teke na kila ngumi lilikuwa la nguvu nyingi. Walipokuwa wakinipiga, walisema kwa sauti, “Utaongea au la? Thubutu kutoongea! Ongea au ufe!” Yule mkuu alipoona kuwa bado sikuwa naongea, akanipiga teke kwa nguvu kwenye tindi ya mguu. Kila wakati aliponipiga teke, nilihisi kana kwamba mtu alikuwa amepigilia msumari ndani ya mifupa yangu, ilikuwa yenye maumivu makali sana. Baada ya hayo, waliendelea kunipiga mateke kila mahali hadi nikahisi kana kwamba walikuwa wamevunjika kila mfupa mwilini mwangu, na nilikuwa nikitetemeka na kugwaya mno kiasi kwamba nilishindwa kuvuta pumzi kwa ajili ya maumivu. Nililala sakafuni nikihema kwa shida na kulia machozi ya uchungu mtupu. Moyoni mwangu, nilimwomba Mungu nikisema, “Ee Mung! Siwezi kuendelea. Tafadhali nilinde kwani ninahofu kuwa nitakufa usiku huu. Ee Mungu, nipe nguvu. …” Sijui mateso hayo yaliendelea kwa muda gani. Nilihisi tu mwenye kizunguzungu sana nami nilikuwa katika maumivu makali mno kiasi kwamba nilihisi kana kwamba nilikuwa nimevamiwa vikali sana. Maumivu yalikuwa makali sana kiasi kwamba mwili wote ulikufa ganzi. Mmoja wa polisi hao jambazi alisema, “Inaonekana bado hujatosheka. Ah, utazungumza bila shaka!” Alipokuwa akiongea, alichukua kitu kilichoonekana kama nyundo ya umeme na kukigongesha kwenye paji la uso wangu. Nilihisi kila pigo kwa ndani kabisa, na kila wakati aliponipiga mwili wangu wote ulikufa ganzi, na kisha nililegea na kutetemeka bila kukoma. Wakati yule polisi jambazi ilipoona jinsi nilivyokuwa nikiteseka, alionekana kufurahishwa na kazi yake na kuanza kucheka kwa kelele. Katikati ya mateso yangu, kifungu cha neno la Mungu kilinipa mwongozo na nuru: “Lazima uvumilie mateso kwa ajili ya ukweli, lazima ujitoe kwa ajili ya ukweli, lazima uvumilie udhalilishaji kwa ajili ya ukweli, na kupata ukweli zaidi lazima upate mateso zaidi. Hili ndilo unalopaswa kufanya(Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Matukio Aliyopitia Petro: Ufahamu Wake wa Adabu na Hukumu). Neno la Mungu lilinipa nguvu ya ajabu sana, nami nikarudia kifungu hicho tena na tena akilini mwangu. Niliwaza: “Siwezi kushindwa na Shetani na kutomridhisha Mungu. Ili kuupata ukweli, ninaapa kuvumilia mateso yoyote, na hata kama itamaanisha mimi kufa, bado litakuwa jambo zuri na sitakuwa nimeishi bure!” Kundi hili la pepo lilinihoji usiku kucha hadi asubuhi iliyofuatia, lakini kwa kuwa nilikuwa na neno la Mungu likinitia moyo, niliweza kuhimili mateso yao! Mwishowe, walikuwa wametumia kila mkakati ambao wangeweza kufikiria na kusema kwa kukata tamaa, “Unaonekana kama mke wa kawaida afanyaye kazi za nyumbani asiye na talanta maalum, kwa hivyo Mungu wako alikupa vipi nguvu nyingi hivyo?” Nilijua kuwa polisi hawa majambazi hawakuwa wanakubali kushindwa nami, lakini badala yake Walikuwa wanajisalimisha chini ya mamlaka na nguvu ya Mungu. Nilishuhudia mimi binafsi kuwa neno la Mungu ni ukweli, kwamba linaweza kuwajaza watu nguvu nyingi, na kwamba kwa kutenda kulingana na neno la Mungu mtu anaweza kuishinda hofu yake ya kifo na kumshinda Shetani. Kutokana na haya yote, imani yangu katika Mungu ilikuwa thabiti hata zaidi.

Asubuhi ya siku ya pili takriban saa moja, mkuu huyo alikuja kunihoji tena. Alipoona kwamba sikuwa tayari kuzungumza, alijaribu kunishawishi kwa hila nyingine tena ya ujanja. Polisi mmoja mwenye kipara na aliyevalia nguo za kiraia aliingia, akanisaidia kuinuka, na kunipeleka kwenye kochi. Alilainisha nguo zangu, akanipapasa begani na, akijifanya kusikitika, alisema kwa tabasamu lisilokuwa na furaha, “Jitazame, hakuna haja ya kuteseka kwa njia hii. Ongea tu nasi halafu utaweza kwenda nyumbani. Kwa nini ukae hapa na kuvumilia mateso haya yote? Watoto wako wanakusubiri nyumbani. Je, unajua jinsi ninavyohuzunishwa kukuona ukiteseka hivi?” Niliposikia uongo wake wote na kuutazama uso huo wenye karaha na usio na haya, nilisaga meno yangu kwa hasira nami nikawaza, “Wewe ni pepo anayefoka kila aina ya uwongo ili kunidanganya tu. Usifikirie hata kidogo kuwa nitamsaliti Mungu. Hata usiote kuwa nitasema neno moja kuhusu kanisa!” Yule askari polisi alipoona kwamba sijashtuka, alinikodolea macho kwa mtazamo wa kiasherati nakuanza kunigusagusa kwa mkono wake. Nilisonga mbali naye upesi, lakini mshenzi huyo alinishika kwa mkono mmoja ili nisiweze kusonga na kisha akakikamata kifua changu kwa mkono wake mwingine. Nililia kwa uchungu na kuhisi chuki kubwa kwa ajili ya mtu huyu; nilikasirika sana hadi mwili wangu wote ukatetemeka na machozi yalitiririka mashavuni mwangu. Nilimtupia jicho lililojawa ghadhabu na, alipoiona sura yangu, akaniacha. Kupitia uzoefu huu wa kibinafsi, kwa kweli nilishuhudia hali mbaya, yenye kudharauliwa na katili ya serikali ya CCP. Niliona jinsi “Polisi wa Watu” wanaofanya kazi katika taasisi ya CCP walivyokuwa wenye kustahili dharau, majambazi wasio na aibu na watu wa hali ya chini bila dhamiri yoyote hata kidogo! Kwa sababu sikuwa nimekunywa hata tone la maji kwa muda wa saa 24, mwili wangu ulikuwa umechoka sana na kudhoofika nami sikuwa na hakika hasa kama ningeweza kuendelea tena. Ghafla nilipatwa na hisia ya huzuni nyingi kutokuwa na tumaini. Wakati huo, nilifikiria kuhusu wimbo wa kanisa: “Ingawa nimeteswa na kukamatwa na joka kubwa jekundu, nimeamua zaidi kumfuata Mungu. Ninaona jinsi joka kubwa jekundu lilivyo mbaya; inawezaje kumvumilia Mungu? Mungu amekuja katika mwili — ningewezaje kumfuata? Ninamuacha Shetani, na namfuata Mungu kwa mapenzi ya chuma. Popote ambapo shetani yuko madarakani, njia ya kumwamini Mungu ni ngumu. Shetani anashindana nami sana, hakuna mahali salama pa kukaa. Kumwamini na kumwabudu Mungu ni jambo sahihi kabisa. Baada ya kuchagua kumpenda Mungu, nitakuwa mwaminifu hadi mwisho. Ujanja wa shetani wa mfalme wa mashetani ni mkatili, mwovu, na wakudharauliwa kweli. Baada ya kupata maoni wazi ya uso wa Shetani, nampenda Kristo hata zaidi. Sitajisalimisha kwa Shetani kamwe, au kuishi maisha yasiyo na manufaa. Nitapata mateso yote, shida, na maumivu, na kuishi hadi usiku mweusi zaidi. Ili kumletea Mungu faraja, nitatoa ushuhuda wa ushindi na kumuaibisha Shetani” (“Kuinuka Katikati ya Giza na Dhuluma” katika Mfuateni Mwanakondoo na Kuimba Nyimbo Mpya). Wimbo huu wa kuvutia na wenye nguvu ulikuwa wenye motisha sana kwangu: Pepo hawa walikuwa wakiwatesa waumini wa Mungu kwa njia hii kwa sababu wanamchukia Mungu. Lengo lao bovu na onevu ni kutukomesha kumwamini na kumfuata Mungu na hivyo kuivuruga na kuiharibu kazi ya Mungu na kuharibu fursa ya wanadamu ya kuokolewa. Katika wakati huu muhimu wa vita hivi vya kiroho, singekata tamaa na kukubali kufanyiwa mzaha na Shetani. Kadri Shetani alivyonitesa, ndivyo nilivyozidi kuuona wazi uso wake mwovu waziwazi na ndivyo nilivyozidi kutaka kumwacha na kusimama upande wa Mungu. Ninaamini kuwa Mungu atashinda, na kuwa Shetani amehukumiwa kushindwa. Singekata tamaa, nami nilitamani kumtegemea Mungu na kuwa na ushuhuda wenye nguvu na mkubwa kwa ajili Yake.

Askari walipotambua kuwa hawatapata habari zozote zenye manufaa kutoka kwangu, walikata tamaa ya kunihoji na, jioni hiyo, walinisafirisha hadi kizuizini. Wakati huo, nilikuwa nimepigwa kiasi cha kutotambuliwa—uso wangu ulikuwa umevimba, sikuweza kufumbua macho yangu na midomo yangu ilikuwa imejaa vidonda. Watu walio katika kizuizi walinitazama na, walipoona kuwa nilikuwa nimepigwa hadi karibu kufa, hawakutaka kuwajibika kwa ajili ya yale yaliyotokea nao wakakataa kunipokea. Hata hivyo, baada ya majadiliano, hatimaye niliruhusiwa kuingia ikiwa takriban saa moja jioni nami nikasindikizwa hadi kwenye seli.

Usiku huo, nilikula mlo wangu wa kwanza tangu nilipokamatwa: andazi lililookwa kwa mvuke, gumu, jeusi, liliokuwa na mchanga ambalo lilikuwa gumu kutafuna na gumu kumeza, pamoja na bakuli la supu na mboga zilizonyauka, zikiwa na minyoo iliyokufa na safu ya uchafu chini ya bakuli. Yote hayo hayakunizuia kukila chakula hicho haraka iwezekanavyo. Kwa sababu nilikuwa muumini, katika siku zilizofuata, mara nyingi afisa wa marekebisho aliwachochea wafungwa wengine wayafanye maisha yangu yawe magumu. Wakati mmoja, mfungwa mkuu wa seli yetu alitoa amri na wadogo wake kwa cheo walinikamata kwa nywele na kukigongesha kichwa changu ukutani. Walikigongesha kichwa changu kwa nguvu sana kiasi kwamba nilihisi kizunguzungu na sikuweza kuona vizuri. Pia, usiku hawakaniruhusu nilale kitandani na kwa hivyo ilinibidi nilale kwenye sakafu ya saruji iliyokuwa baridi karibu na choo. Zaidi ya hayo, walinzi wa gereza walinilazimisha kukariri sheria za kizuizini na, ikiwa nilizikariri vibaya au kuzisahau, walinipiga kwa mkanda wa ngozi. Nikiwa nimekabiliwa na kuteswa kinyama na udhalilishaji nilidhoofika, na kuwaza kuwa ingekuwa bora kufa tu kuliko kuteseka kama mnyama aliyetiwa kizimbani siku baada ya siku. Mara nyingi, nilipokaribia tu kukigongesha kichwa changu ukutani nijiue, neno la Mungu kunielekeza, ikisema, “Hivyo, katika siku hizi za mwisho lazima uwe na ushuhuda kwa Mungu. Haijalishi mateso yenu ni makubwa vipi, mnapaswa kuendelea hadi mwisho kabisa, na hata wakati wa pumzi yenu ya mwisho, bado lazima muwe waaminifu kwa Mungu, na kudhibitiwa na Mungu; huku pekee ndiko kumpenda Mungu kweli, na huu pekee ndio ushuhuda thabiti na mkubwa sana(Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Ni kwa Kupitia tu Majaribio ya Kuumiza Ndiyo Mnaweza Kujua Kupendeza kwa Mungu). Maneno ya Mungu yalinitia moyo na kuuchangamsha moyo wangu. Nilipokuwa nikitafakari kuhusu maneno ya Mungu, machozi yalibubujika machoni mwangu. Nilifikiria jinsi wakati nilipokuwa nikipigwa kikatili na polisi hao wahuni, ilikuwa ni upendo wa Mungu ambao ulikuwa umenitunza wakati huo wote, Alikuwa amenielekeza kwa maneno Yake, na Alikuwa amenipa imani na nguvu, na kuniwezesha kuokoka kutokana na mateso hayo mabaya. Baada ya kudhulumiwa na kukandamizwa na mfungwa mkuu wa seli yetu na kuteswa na wafungwa wengine hadi kiwango ambacho nilikaribia kurukwa na akili na kufikiria kujiua, kwa mara nyingine maneno ya Mungu yalinipa imani na ujasiri wa kuinuka upya. Mungu asingekuwa kando yangu, Akinilinda, wale wahalifu katili wangekuwa washanitesa hadi kufa zamani sana. Licha ya upendo na huruma nyingi ya Mungu, singeweza tena kuupinga na kuuhuzunisha moyo wa Mungu. Ilinibidi kusimama imara pamoja na Mungu na kulipiza upendo wa Mungu kwa uaminifu. Bila kutarajia, mara tu nilipoirekebisha hali yangu ya kimawazo, Mungu akasababisha mfungwa mwingine ainuke na kupinga kwa niaba yangu, naye na mkuu wa wafungwa wakaanza kugombana vikali. Mwishowe, mfungwa mkuu akapunguza hasira na kuniruhusu kulala kwa kitanda. Mungu apewe shukrani. Laiti isingekuwa kwa ajili ya huruma ya Mungu, kulala kwa muda mrefu kwenye sakafu ya saruji iliyolowa maji na iliyo baridi kungesababisha nife au kuniacha nikiwa nimepooza, nikizingatia umbile langu dhaifu. Kwa njia hii, nilifanikiwa kupitia miezi miwili migumu sana huko kizuizini. Wakati huo, polisi hao jambazi walinihoji mara mbili zaidi kwa kutumia mkakati ule ule wa askari mzuri, askari mbaya. Lakini kwa ulinzi wa Mungu, niliweza kuitambua njama ya ujanja ya Shetani na kuuzuia mpango wao mwovu. Mwishowe, waliishiwa na mikakati na, baada ya mahojiano yao yote yaliyoshindwa, hatimaye walinihukumu kifungo cha miaka mitatu na kunipeleka katika Gereza la Pili la Wanawake ili kutumikia kifungo changu.

Kuanzia siku ya kwanza nilipofika gerezani, nililazimishwa kufanya kazi za sulubu. Ilinibidi kufanya kazi kwa zaidi ya masaa kumi kwa siku, na ilibidi nifume sweta moja, au kushona nguo thelathini hadi arobaini, au kupakia jozi elfu kumi za vijiti vya kulia kila siku. Ikiwa sikuweza kumaliza kazi hizi, kifungo changu kingeongezwa. Kana kwamba kazi hiyo ya sulubu haikuchosha vya kutosha, usiku tulilazimishwa kushiriki katika aina ya kasumba ya kisiasa iliyokusudiwa kuziponda roho zetu, ambapo tulilazimishwa kusoma amri za gereza, sheria, falsafa ya Umaksi-Ulenini, na Mawazo ya Mao Zedong. Kila niliposikia maafisa wa urekebishaji wakielezea kuhusu nadharia zao za kipuuzi za kumkana Mungu nilikuwa nikiona karaha na kuhisi chuki halisi kwa ajili ya njia zao zinazostahili dharau na za kufedhehesha. Wakati wote nilipokuwa gerezani, sikuwahi kuweza kulala vizuri usiku hata kidogo—mara nyingi tungegutushwa kutoka usingizini usiku wa manane kwa filimbi za walinzi wa gereza. Wangetulazimisha tuamke na kusimama ushorobani bila sababu yoyote au kutugawa kazi kama kuburuta viazi, mahindi na malisho. Kila begi lilikuwa na uzito zaidi ya kilo 50. Wakati wa usiku wa misimu ya baridi, tulilazimika kupambana na pepo zenye nguvu zilizotia baridi sana. Tungetembea polepole na kuchechemea, mguu baada ya mwingine, wakati mwingine hata tukianguka kutokana na uzito wa mizigo yetu. Mara nyingi, ningeukokota mwili wangu uliokuwa mchovu na kurudi kwenye seli yangu mnamo saa nane au tisa asubuhi, nikiwa nimechoka na macho yangu yakiwa yamejaa machozi. Katika usiku kama huo, mchanganyiko wa uchovu, baridi na hasira vilinizuia kupata usingizi. Wakati wowote nilifikiria kuhusu jinsi bado nilivyopaswa kuvumilia miaka mitatu mirefu ya kifungo, ningekata tamaa hata zaidi na mwili wangu wote ungehisi kupooza kwa uchovu. Mungu aliyafahamu vyema mateso yangu, na katika hali hizi zenye kusikitisha zaidi, Alinielekeza kukumbuka kifungu hiki cha maneno Yake, “Usivunjike moyo, usiwe dhaifu, Nitakufichulia. Njia ya kwenda kwa ufalme sio laini hivyo, hakuna kitu kilicho rahisi hivyo! Unataka baraka zije kwa urahisi rahisi, sivyo? Leo kila mtu atakuwa na majaribio machungu ya kukumbana nayo, vinginevyo moyo wa upendo ulio nao Kwangu hautakuwa wenye nguvu zaidi na hutakuwa na upendo wa kweli Kwangu(Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Matamko ya Kristo Mwanzoni, Sura ya 41). Maneno ya Mungu yalikuwa faraja kubwa kwa moyo wangu uliohuzunika na kuteseka nayo waliniwezesha kuelewa mapenzi Yake. Hali ambayo sasa nilijikuta nikiwa ndani ilikuwa jaribio halisi. Mungu alitaka kuona ikiwa ningebaki kuwa mwaminifu Kwake katikati ya mateso kama hayo na ikiwa ninampenda kweli au la. Ingawa miaka mitatu gerezani ulikuwa muda mrefu sana, nikiwa na neno la Mungu likiniongoza na upendo wa Mungu ukinisaidia, nilijua sikuwa pekee yangu. Ningemtegemea Mungu kuvumilia maumivu na mateso yote na kumshinda Shetani. Singeweza kukubali kuwa mwoga.

Uovu na ukatili wa CCP vilionekana wazi katika kila nyanja ya gereza hili ambalo ililisimamia, lakini upendo wa Mungu ulikuwa nami kila wakati. Wakati mmoja, mlinzi wa gereza aliniamuru nikokote begi la vijiti vya kulia hadi kwenye orofa ya tano. Kwa sababu ngazi ilikuwa imefunikwa kwa barafu, ilibidi nitembee polepole sana kutokana na uzito wa begi hilo. Hata hivyo, mlinzi aliendelea kuniambia niharakishe na, nikihofia kwamba ningepigwa vibaya ikiwa sikumaliza mgawo wangu, nilikuwa na wasiwasi na kuteleza nilipokuwa nikiharakisha, nikaanguka kwenye ngazi kuelekea chini na kuvunja mfupa wa kisigino changu. Nililala sakafuni nikiwa nimetandawaa, nikashindwa kuusongesha mguu wangu na nikiwa nimejawa jasho baridi kutokana na maumivu makali baada ya kuvunjika. Hata hivyo, mlinzi huyo hakujali hata kidogo. Alisema nilikuwa nikijisingizia na kuniamuru niinuke na kuendelea kufanya kazi, lakini sikuweza kusimama. Dada kutoka kanisani, ambaye alikuwa akitumikia kifungo chake katika gereza lile lile, aliona kilichotokea na mara moja akanibeba hadi kwenye kliniki ya gereza. Kule kliniki, daktari aliyehudumu pale aliufunga mguu wangu kwa bendeji tu, akanipa vidonge vichache vya dawa vya bei rahisi na kuniambia niende. Akiwa na hofu kwamba singeweza kukamilisha kiasi cha kazi niliyogawiwa, mlinzi wa gereza alikataa kuniruhusu nipate matibabu yoyote, kwa hivyo ilibidi niendelee kufanya kazi nikiwa na mguu uliovunjika. Dada huyo angenisaidia kufanya kazi yoyote ambayo tulikuwa tukiifanya. Kwa sababu upendo wa Mungu ulikuwa umefunganisha mioyo yetu, kila alipopata fursa, dada huyo angeshiriki kuhusu neno la Mungu nami ili kunitia moyo. Hii ilikuwa faraja kubwa kwangu katika katika wakati wangu mgumu na wenye changamoto zaidi. Katika kipindi hicho, sijui ni mara ngapi nilihisi uchungu sana na kuwa dhaifu kiasi kwamba singeweza kuinuka, nami sikuwa na nguvu ya kupumua, na mara nyingi ningejificha kwenye mfarishi nikimwomba Mungu huku nikitokwa na machozi, lakini nyimbo hizi mbili zilinitia moyo na kunifariji daima: “Kwamba wewe huweza kukubali hukumu, kuadibu, kuangamiza, na usafishaji wa maneno ya Mungu, na, aidha, unaweza kukubali maagizo ya Mungu, lilijaaliwa na Mungu mwanzoni mwa wakati, na hivyo lazima usihuzunishwe sana wakati ambapo wewe huadibiwa. Hakuna anayeweza kuondoa kazi ambayo imefanywa ndani yenu, na baraka ambazo zimetolewa ndani yenu, na hakuna anayeweza kuondoa yote ambayo mmepewa ninyi. Watu wa dini hawastahimili mlingano na ninyi. Ninyi hamna ubingwa mkuu katika Biblia, na hamjajizatiti na nadharia za kidini, lakini kwa sababu Mungu amefanya kazi ndani yenu, mmepata zaidi ya yeyote kotekote katika enzi—na kwa hiyo hii ni baraka yenu kuu zaidi(“Huwezi Kusikitisha Mapenzi ya Mungu” katika Mfuateni Mwanakondoo na Kuimba Nyimbo Mpya). “Njia ya ufalme ni yenye miamba ya milima na mabonde mengi. Kutoka kifo hadi uzimani katikati ya mateso na machozi mengi. Bila mwongozo na ulinzi wa Mungu, ni nani angeweza kufika leo? Mungu alitawala na kupanga kuzaliwa kwetu katika siku za mwisho, na tuna bahati kumfuata Kristo. Mungu hujinyenyekeza Mwenyewe kuwa Mwana wa Adamu, na Hupitia aibu kubwa sana. Mungu ameteseka sana, nawezaje kuitwa mtu kama simpendi Mungu? … Baada ya kuingia kwenye njia ya kumpenda Mungu, sitajuta kamwe kumfuata Yeye na kumshuhudia. Ingawa naweza kuwa dhaifu na hasi, kupitia machozi moyo wangu bado unampenda Mungu. Navumilia mateso na kutoa upendo wangu kwa Mungu, nisimsababishie huzuni tena kamwe. Kupitia ugumu katika dhiki ni vizuri kama dhahabu inavyojaribiwa kwa moto; ningekosaje kuutoa moyo wangu? Njia ya mbinguni ni ngumu na yenye miamba. Kutakuwa na machozi, lakini nitampenda Mungu kwa kina zaidi na sitakuwa na majuto” (“Wimbo wa Kumpenda Mungu Bila Majuto” katika Mfuateni Mwanakondoo na Kuimba Nyimbo Mpya). Maneno ya Mungu na upendo wa Mungu uliniokoa kutoka katika lindi la kutokuwa na tumaini na, mara kwa mara, yalinipa ujasiri wa kuendelea kuishi. Katika hali hii katili na mbovu ya mateso, nilishuhudia ukunjufu na uinzi wa upendo wa Mungu, nami niliazimia kuendelea kuishi ili niweze kuulipiza upendo wa Mungu. Haijalishi jinsi nilivyoteseka sana, ilibidi niendelee; hata kama ningekuwa na pumzi moja tu iliyobaki, ilibidi niendelee kuwa mwaminifu kwa Mungu. Katika miaka yangu mitatu gerezani, niliguswa sana wakati dada yangu aliponipa kurasa chache za neno la Mungu zilizoandikwa kwa mkono. Kwamba niliweza kusoma neno la Mungu nikiwa gerezani lililoendeshwa na pepo ambalo lililotiwa shinikizo zaidi kuliko Fort Knox kweli ulikuwa ushuhuda kwa upendo mkubwa na rehema ambazo Mungu alikuwa Akinionyesha. Ilikuwa ni maneno haya ya Mungu ambayo yalinitia moyo na kuniongoza, yakiniwezesha kuvumilia nyakati hizo ngumu zaidi.

Mnamo Septemba mwaka wa 2005, muda wangu wa kutumikia kifungo changu ulikamilika na mwishowe ningeweza kuzisahau siku za gerezani. Wakati nilipokuwa nikitoka gerezani, nilivuta pumzi nzito na kumshukuru Mungu kwa moyo wangu wote kwa ajili ya upendo na ulinzi Wake, ambao uliniwezesha kustahimili kifungo changu gerezani. Kwa sababu ya uzoefu wangu wa kibinafsi wa kukamatwa na kuteswa na serikali ya CCP, sasa najua kilicho chema na kilicho kibaya, kilicho kizuri na kilicho kiovu, kilicho cha kujenga na kilicho hasi. Nimetambua kile ambacho ninapaswa kuacha kila kitu ili nikifuatile na lile ambacho ninapaswa kukikataa kwa chuki na laana. Kupitia uzoefu huu, nilikuja kujua kwa hakika kuwa neno la Mungu ni maisha ya Mungu mwenyewe nalo limepewa nguvu zisizo za kawaida ambazo zinaweza kuwa motisha unaoyaendesha maisha ya mwanadamu. Maadamu mwanadamu anaishi kulingana na neno la Mungu, anaweza kuzishinda nguvu zote za Shetani na anaweza hata kushinda katika hali mbaya zaidi. Shukrani iwe kwa Mungu.

Iliyotangulia: 84. Imani Isiyoweza Kuvujika

Inayofuata: 86. Siku Baada Ya Nyingine Katika Jela Ya Chama Cha Kikomunisti

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Maudhui Yanayohusiana

68. Ulinzi wa Mungu

Mwenyezi Mungu anasema: “Watu hawawezi kubadilisha tabia yao wenyewe; lazima wapitie hukumu na kuadibu, mateso na usafishaji wa maneno ya...

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp