Mungu Ni Nguvu Yangu Katika Maisha

26/01/2021

Na Xiaohe, Mkoa wa Henan

Katika kile kilichohisi kama kufumba na kufumbua, nimemfuata Mwenyezi Mungu kwa miaka 14. Katika miaka hii yote, nimepitia mema na mabaya, na njia imekuwa ya dhiki mara kwa mara, lakini kwa sababu nimekuwa na neno la Mungu, na vile vile upendo na huruma ya Mungu yakiandamana nami, nimehisi kukamilika hasa. Katika miaka hii 14, tukio la kukumbukwa zaidi lilikuwa kukamatwa kwangu mnamo Agosti mwaka wa 2003. Nilipokuwa rumande, niliteswa kikatili na polisi wa CCP, na karibu nilemazwe. Ilikuwa ni Mwenyezi Mungu ambaye alinichunga na kunilinda, na ambaye mara kwa mara Alitumia maneno Yake kuniongoza, jambo ambalo mwishowe lilinisababisha nishinde kuteswa na wale watu katili, nisimame imara, na kushuhudia. Wakati wa tukio hili, nilihisi sana nguvu ya ajabu ya maneno ya Mwenyezi Mungu na nguvu ya nishati uhai Yake, ambayo nilitumia kubaini kwamba Mwenyezi Mungu ndiye Mungu mmoja wa kweli ambaye ana mamlaka juu ya vyote na hutawala vyote. Hata zaidi, Yeye ndiye wokovu wangu wa pekee, Yule pekee ambaye ninaweza kumtegemea, na hakuna nguvu yoyote ya adui inayoweza kuniondoa kwa Mungu au kunizuia kufuata nyayo Zake.

Mungu Ni Nguvu Yangu Katika Maisha

Nakumbuka jioni hiyo ambapo mimi na dada zangu wawili tulikuwa tukikutana, wakati ambapo ghafla tulimsikia mbwa akibweka nje, na pia sauti ya watu wakija kupitia juu ya ukuta wa uwanja. Muda mfupi baadaye, tulimsikia mtu akisisitiza kubisha mlangoni kwa kishindo, akisema kwa sauti kuu, "Fungueni mlango! Mmezingirwa!” Tulikusanya vitu vyetu haraka na kuviondoa, lakini wakati huohuo, mlango ulianguka ndani kwa kishindo, na mng’ao mkali wa taa kadhaa ukatumulika moja kwa moja, ukitupofusha kiasi kwamba tulilazimika kuyafumba macho yetu. Mara moja, zaidi ya watu dazeni walikurupuka chumbani na kutusukuma kwa nguvu kuelekea ukutani huku wakisema kwa sauti kuu, "Msisogee! Shirikieni nasi” Baada ya hapo, walipekua nyumba, na kukurupuka humo kama majahili. Wakati huo huo, nilisikia mipigo miwili ya bunduki kutoka nje, ambayo ilifuatiwa na polisi mmoja aliyekuwa ndani akisema kwa sauti kuu, "Tumewakamata! Wote watatu!” Walitutia pingu, kisha wakatusukuma hadi kwenye gari la polisi kwa ukali. Kufikia wakati huu, akili zangu zilikuwa zimerudi, na nikagundua kuwa tulikuwa tumekamatwa na polisi. Mara tulipokuwa ndani ya gari lile, polisi mmoja, akiwa na kirungu cha umeme mkononi, alisema kwa sauti kuu, "Ninyi nyote, sikilizeni: Tulieni, kwa sababu nitamshtua kwa umeme yeyote atakayesogea, na hata ikiwa umeme utawaua, sitakuwa nikivunja sheria!” Njiani, polisi wawili waovu walikuwa wamenibana katikati ya kiti baina yao, na mmoja wao alishikilia miguu yangu kwenye paja lake na kunikumbatia mikononi mwake. Alisema kikware, "Nitakuwa nikipoteza nafasi yangu nisipojifurahisha nawe!" Alinishikilia kwa nguvu, hata ingawa nilipambana kwa nguvu yangu yote hadi polisi mwingine kati yao akasema, "Acha kucheza! Hebu tuharakishe na tumalize kazi hii maalumu ili tuweze kuachana nayo.” Ni wakati huo tu ndipo aliniachilia.

Walitupeleka kwenye kituo cha polisi na kutufungia katika chumba kidogo sana, na baada ya hapo walitufunga mmoja mmoja kwenye viti vya chuma. Mtu aliyepewa kazi ya kutulinda alituuliza vikali majina yetu na tulikoishi. Nilikuwa na wasiwasi na sikujua nilichopaswa kusema, kwa hivyo nilisali kwa Mungu kimyakimya, nikimwomba hekima na maneno yanayofaa ya kusema. Wakati huu ndipo maneno ya Mungu yalinipa nuru: “Kuzingatia masilahi ya familia ya Mungu kwanza katika mambo yote; kunamaanisha kukubali uchunguzi wa Mungu na kuitii mipango ya Mungu(Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Uhusiano Wako Na Mungu Ukoje?). Kweli! Nilihitaji kuyapa masilahi ya familia ya Mungu kipaumbele. Bila kujali wanavyoweza kunitesa au kuniumiza vibaya, singewasaliti ndugu zangu, wala singekuwa Yuda na kumsaliti Mungu. Nilihitaji kusimama kidete na kumshuhudia Mungu. Baada ya hapo, bila kujali jinsi alivyonihoji, nilimpuuza. Asubuhi iliyofuata, walipokuwa karibu kutupeleka kizuizini, yule afisa wa polisi mkware alisema, "Tuliwawekea jarife ili kuwakamata! Ilitubidi tuendelee kutafuta hadi tukawapata!” Alipokuwa akinitia pingu, aliyapapasa matiti yangu, jambo ambalo lilinikasirisha. Sikuwahi kufikiri kwamba Polisi wa Umma wangenisumbua jinsi hiyo peupe kabisa. Walikuwa tu majambazi na majahili! Jambo hilo lilichukiza kwa kweli!

Kule kizuizini, ili kunifanya niwaambie anwani ya nyumbani kwangu na habari kuhusu imani yangu katika Mungu, polisi walimtuma afisa wa kike kwanza ili anishawishi na kunibembeleza kwa kujifanya polisi mzuri. Walipogundua kuwa hiyo haikuwa ikifaulu, walinichukua video kwa nguvu, na kisha wakasema wangeipeleka video hiyo kwenye kituo cha runinga na kuharibu sifa yangu kwa kuitumia. Hata hivyo, nilijua kwamba nilikuwa muumini tu wa Mungu ambaye alifuatilia ukweli na kutembea kwenye njia sahihi katika maisha, na kwamba sikuwa nimefanya kitu chochote cha kufedhehesha, wala sikuwa nimefanya chochote kisicho halali au cha jinai, kwa hivyo kwa sauti ya kuonyesha kukosewa, nilimjibu, "Fanyeni lolote mpendalo!" Walipogundua kwamba mbinu yao haikuwa ikifaulu, polisi hawa waovu waliamua kunitesa vikali. Kana kwamba nilikuwa mhalifu sugu, walinitia pingu na silisili zilizokuwa za uzito wa kilo 5, na kisha wakanisindikiza kwenye gari ili kunipeleka nihojiwe. Kwa sababu silisili zilizokuwa kwenye miguu yangu zilikuwa nzito sana, nililazimika kuziburuta huku nikitembea. Kutembea kulikuwa kugumu sana, na baada ya hatua chache tu, ngozi kwenye miguu yangu ilisuguliwa hadi ikachunika na kupasuka. Punde tulipokuwa garini, walivisha kichwa changu mfuko mweusi mara moja, na nikabanwa kati ya maafisa wawili. Ghafla nilifikiri moyoni kwa mshtuko, "Polisi hawa waovu hawana ubinadamu kabisa, na huwezi kujua watafanya mambo gani maovu ili kunitesa. Ni nini kitatokea nisipoweza kuvumilia?" Kwa hiyo, nilimwomba Mungu upesi: "Mwenyezi Mungu! Mwili wangu ni dhaifu katika makabiliano na hali ambazo ninakaribia kustahimili. Tafadhali nilinde na Unipe imani. Bila kujali ni mateso gani yatakayonifika, natamani kusimama kidete katika ushuhuda wangu ili kukuridhisha, na ninakataa kabisa kukusaliti." Tuliingia ndani ya jengo fulani na wakaondoa mfuko ule kichwani pangu, kisha wakaniamuru nisimame siku nzima. Jioni hiyo, afisa wa polisi alikaa mbele yangu, akaketi kimarufaa, na kuniambia kwa sauti kali, "Jibu maswali yangu kwa ushirikiano, na utaachiliwa! Umemwamini Mungu kwa muda wa miaka ngapi? Ni nani aliyekuhubiria? Ni nani kiongozi wa kanisa lenu?” Nilipokosa kujibu, alipaza sauti kwa hasira, "Inaonekana hutajibu tusipofafanua njia mbadala!” Aliniamuru niyainue mikono yangu juu ya kichwa changu na nisiisogeze huku nikiendelea kusimama. Baada ya muda mfupi, mikono yangu ilianza kuuma, na sikuweza kuiinua juu ya kichwa changu, lakini hakuniruhusu niiweke chini. Ni wakati tu ambapo nilikuwa nikitokwa na jasho na kutetemeka kote na sikuweza kuiinua tena ndipo aliniruhusu niiweke mikono yangu chini, lakini bado hakuniruhusu niketi. Nilitakiwa nisimame hadi alfajiri, wakati ambapo miguu na nyayo zangu zilikuwa zimekufa ganzi na kuvimba.

Asubuhi ya siku ya pili, walianza kunihoji tena, lakini bado nilikataa kuwaambia lolote. Waliondoa upande mmoja wa pingu zangu (zenye minyororo), na kisha kiongozi wao akanigonga vikali sana nyuma ya magoti yangu kwa ufito wa mbao wenye upana wa sentimita 10 na urefu wa sentimita 70, akinilazimisha nipige magoti. Kisha akashindilia ufito ule ndani ya mwanya nyuma ya magoti yangu, kisha akavuta mikono yangu chini ya ufito huo na kunilazimisha nivalie pingu hizo tena. Papo hapo, kifua changu kilihisi kubanwa, ilikuwa vigumu kupumua, na kano mabegani mwangu zilihisi kunyoshwa hadi kufikia kiwango cha kuvunjika. Mashavu yangu ya miguu yalikazika sana kiasi kwamba yalikuwa tayari kukatika. Ilikuwa chungu sana kiasi kwamba nilitetemeka kote. Takribani dakika tatu baadaye, nilijaribu kurekebisha namna nilivyokuwa nimekaa, lakini sikuweza kujihimili, na nikaanguka nyuma kwa kishindo, uso wangu ukitazama juu. Mmoja wa polisi wale wanne katika chumba hicho aliwaelekeza wawili wengine waende pande zote mbili zangu na kuvuta ufito ule wa mbao kuelekea chini kwa mkono mmoja huku wakisukuma mabega yangu mbele wakitumia ule mwingine, na akaamuru yule wa tatu akishike kichwa changu mikononi mwake huku akipiga mgongo wangu teke kwa mguu wake, wakiniweka katika hali ya kuchutama, na kuniamuru nisalie katika ile hali. Lakini mwili wangu wote ulikuwa na maumivu yasiyovumilika, na baada ya muda mfupi nilianguka tena, wakati ambapo waliniweka tena katika hali ya kuchutama. Niliendelea kuangukia na kusukumwa wima katika hali ya kuchutama tena na tena, na mateso haya yakaendelea kwa takriban saa moja, hadi mwishowe, wote walipochoka na kutokwa na jasho, kiongozi wao akasema, "Tosha, tosha, nimechoshwa sana na hili!” Ni wakati huo tu ndipo waliondoa kifaa cha mateso. Nilihisi dhaifu kote, na nikalala sakafuni huku nikihema, bila nguvu kabisa. Kufikia wakati huu, pingu zilikiwa zimechuna na kuondoa ngozi kwenye vifundo vyangu vya mikono, na chini ya silisili vifundo vya miguu yangu vilijawa na damu. Nilihisi uchungu mno kiasi kwamba nilikuwa nikitokwa na jasho kote, na jasho yangu ilipokuwa ikipenya ndani ya vidonda vyangu, maumivu yalikuwa kama kukatwa kwa kisu. Katika taabu kama hii, sikuweza kujizuia kuendelea kulia moyoni mwangu, “Ee Mungu! Niokoe, siwezi kuvumilia haya kwa muda mrefu tena!” Na wakati huo huo, maneno ya Mungu yalinipa nuru: “Watu wanapokuwa tayari kuyatoa maisha yao, kila kitu huwa hafifu, na hakuna anayeweza kuwashinda. Ni nini kingekuwa muhimu zaidi kuliko uzima?(Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Ufafanuzi wa Mafumbo ya “Maneno ya Mungu kwa Ulimwengu Mzima”, Sura ya 36). Maneno ya Mungu yalinifunulia kila kitu mara moja. Shetani anajua kuwa watu wanathamini sana miili yao, na kwamba wanaogopa kifo hata zaidi, kwa hiyo alikuwa akitarajia kuumiza mwili wangu kikatili ili kunifanya niogope kifo, na kwa hiyo kunifanya nimsaliti Mungu. Hii ilikuwa njama yake, lakini Mungu pia alikuwa akitumia njama ya Shetani kujaribu imani yangu na uaminifu wangu Kwake. Mungu alitaka nimshuhudie mbele ya Shetani, na hivyo kumefedhehesha Shetani. Mara nilipofahamu mapenzi ya Mungu, nilipata tena imani na nguvu yangu, na pia azimio la kusimama kidete na kushuhudia kwa ajili ya Mungu hata nikifa. Mara nilipoapa kiapo cha kuhatarisha maisha yangu ili kumridhisha Mungu, maumivu yangu yalihisi kupunguka sana, na pia sikuhisi mwenye dhiki na taabu sana. Baada ya hapo, polisi aliniamuru nisimame, na akasema kwa hasira, "Nimekuambia usimame! Hebu tuone utadumu kwa muda gani!” Na kwa hiyo, walinilazimisha nisimame hapo hadi kulipokuwa giza. Jioni, nilipokwenda msalani, miguu yangu ilikuwa imevimba na kujaa damu iliyoganda kwa sababu ya silisili, kwa hivyo niliweza tu kuvuta miguu yangu kwenye sakafu umbali mfupi kwa wakati mmoja. Ilikuwa vigumu sana kusonga, kwani kila wakati niliposonga nilihisi maumivu makali kutoka miguuni pangu, na kwa kila hatua kulikuwa na mchirizo dhahiri wa damu mbichi. Ilinichukua karibu saa moja kutembea mita 30 kwenda chooni na kurudi. Usiku huo, sikuweza kujizuia kusugua miguu yangu iliyovimba kwa mikono yangu, na haikutulia bila kujali iwapo niliivuta karibu nami au kuinyosha. Nilihisi uchungu mno, lakini kilichonifariji ni kwamba, kwa sababu nilikuwa na ulinzi wa Mungu, sikuwa nimemsaliti Mungu.

Asubuhi ya siku ya tatu, polisi hawa waovu walitumia tena njia ile ile kunitesa. Kila wakati nilipoanguka, kiongozi wa polisi alicheka kiovu na kusema, "Huo ni mwanguko wa kupendeza! Hebu anguka tena!” Halafu wangeniinua, na ningeanguka tena, na angesema, “Ninakupenda ukiwa katika hali hiyo, inapendeza. Fanya hivyo tena!” Walinitesa mara kwa mara jinsi hii kwa takribani saa moja, hadi mwishowe wakaacha, wakitokwa na jasho kwenye mapaji yao na kuchoka kabisa. Nilianguka sakafuni, kichwa changu kikiangalia juu, nikihisi kana kwamba mbingu ilikuwa ikizunguka. Sikuweza kuacha kutetemeka, mimiminiko ya jasho yenye chumvi ilifanya kufungua macho yangu kusiwezekane, na tumbo langu lilikuwa likisokota vibaya sana kiasi kwamba nilitaka kutapika. Nilihisi kana kwamba nilikuwa karibu kufa. Wakati huu ndipo maneno ya Mungu yalinijia akilini mwangu ghafla: “‘Kwa kuwa huzuni yetu nyepesi, ambayo ni ya muda mdogo pekee, inatufanyia utukufu mkubwa na wa daima ambao unazidi kuwa mkuu kabisa.’ … Joka kuu jekundu humtesa Mungu na ni adui wa Mungu, kwa hiyo katika nchi hii, wanaomwamini Mungu wanateswa na kudhihakiwa. Ndiyo sababu maneno haya yatakuja kuwa kweli kwenu nyie kundi la watu(Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Je, Kazi ya Mungu Ni Rahisi Kama Vile Mwanadamu Anavyodhania?). Maneno ya Mungu yalinifanya nielewe kuwa humu China, taifa linalotawaliwa na pepo ambapo kumwamini Mungu na kumfuata Mungu kunahakikisha kuwa utapitia fedheha na madhara makuu, Mungu anakusudia kutumia mateso haya kufanyiza kundi la washindi na hivyo kumshinda Shetani, na hizi hasa ndizo nyakati ambazo tunapaswa kudhihirisha utukufu wa Mungu na kumshuhudia. Kwamba niliweza kutekeleza wajibu wangu kwa ajili ya utukufu wa Mungu ni heshima yangu. Huku nikiongozwa na maneno ya Mungu, sikugundua tu uwezo wenye nguvu, lakini pia nilimtangazia Shetani moyoni mwangu, "Pepo mbaya, nimejizatiti, na bila kujali jinsi unavyonitesa, sitakutii. Hata nikifa, naapa kusimama na Mungu.” Afisa mkuu alipoona kwamba bado sikuwa nikiyajibu maswali yao, aliondoa ufito ule kwa hasira, na kisha akasema kwa ghadhabu, “Haya, simama! Tutaona ukaidi wako utadumu kwa muda gani. Tutacheza ule mchezo mrefu na wewe. Nina hakika bado tutakufanya usalimu amri!” Sikuwa na lingine ila kusimama kwa maumivu makali, lakini miguu yangu ilikuwa imevimba na yenye maumivu sana kiasi kwamba sikuweza kusimama wima, na nililazimika kujiegemeza ukutani. Alasiri hiyo, afisa mkuu aliniambia, "Watu wengine 'wanapopanda bembea’ wote huzungumza mara ya kwanza. Unaweza kustahimili dhuluma kidogo! Angalia hali ya miguu yako, na bado hutaki kuzungumza. Sijui wewe hutoa wapi nguvu….” Baada ya hapo, alinitazama tena na kusema kwa sauti kuu, "Nimewafanya watu wengi sana wapasue mbarika, na wewe una ujasiri wa kushindana nami? Ah! Hata tusipoufungua mdomo wako, bado tunaweza kukuhukumu kifungo cha miaka 8 hadi 10, na tutawafanya wafungwa wakutukane na kukupiga kila siku! Tutakurekebisha!” Nilipomsikia akisema hivyo, nilifikiri, "Mungu yuko nami, kwa hivyo hata mkinihukumu kifungo cha miaka 8 hadi 10, siogopi." Wakati ambapo sikujibu, alipiga paja lake kofi kwa hasira, akagongesha mguu wake chini, na kusema, "Tumetumia siku nyingi kujaribu kukufanya usalimu amri. Kama kila mtu angekuwa kama wewe, ningewezaje kufanya kazi yangu?” Nilitabasamu kimoyomoyo nilipomsikia akisema hivyo, kwa sababu Shetani hakuwa na nguvu, akishindwa kabisa na mkono wa Mungu! Wakati huo, sikuweza kujizuia kufikiria maneno ya Mungu: “Nguvu za Mungu za maisha zinaweza kutawala juu ya nguvu zozote; zaidi ya hayo, inazidi mamlaka yoyote. Maisha Yake ni ya milele, nguvu zake za ajabu, na nguvu Zake za maisha haziwezi kuzidiwa na kiumbe yeyote au nguvu za adui(Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Ni Kristo wa Siku za Mwisho Pekee Ndiye Anayeweza Kumpa Mwanadamu Njia ya Uzima wa Milele). Kila neno la Mungu ni ukweli, na siku hiyo nilipitia hilo mimi binafsi. Sikuwa nimekula au kunywa chochote au kulala kwa siku tatu, na nilikuwa nimeteswa vibaya sana, na nilikuwa bado nikipinga, na hii ilikuwa tu kwa sababu ya nguvu niliyopewa na Mungu. Ilikuwa Mungu akinichunga na kunilinda. Bila Mungu kama msaada wangu thabiti, ningekuwa nimesalimu amri muda mrefu uliopita. Nishati uhai ya Mungu kwa kweli ina nguvu ya kipekee, na Mungu kweli ni mwenye uweza! Baada ya kushuhudia matendo ya Mungu, imani yangu ya kumshuhudia Mungu mbele ya Shetani iliimarika.

Asubuhi ya siku ya nne, wale polisi waovu walinilazimisha ninyoshe mikono yangu mbele na kuiweka sawa na mabega yangu na kukaa nikiwa nimechutama nusu, na baada ya hapo waliweka fimbo ya mbao nyuma ya mikono yangu. Haikunichukua muda mrefu kabla ya kutoweza kusalia nikichutama. Mikono yangu ilianguka, na ufito ukaangika sakafuni. Waliuchukua ule ufito na kuutumia kugonga viungo vya vidole vyangu na magoti yangu kwa nguvu, kila pigo likisababisha maumivu makali sana, na kisha wakanilazimisha niendelee kuchutama nusu. Baada ya siku kadhaa za mateso, miguu yangu ilikuwa tayari imevimba na yenye maumivu, kwa hiyo baada ya kuchutama kwa muda mfupi tu, miguu yangu haikuweza kuhimili uzito wangu, na nikaanguka sakafuni kwa kishindo. Waliniinua tena, lakini punde waliponiachilia nilianguka tena. Haya yaliendelea mara kadhaa. Makalio yangu yalikuwa tayari yamevilia sana kiasi kwamba hayakuweza kuvumilia kugongana na sakafu jinsi hii, na nilikuwa na uchungu sana kiasi kwamba nilianza kutokwa na jasho kotekote. Walinitesa kwa njia hii kwa karibu saa moja. Baadaye, waliniamuru niketi sakafuni, kisha wakaleta bakuli la maji mazito ya chumvi na wakaniambia niyanywe. Nilikataa, kwa hivyo mmoja wa polisi hao waovu alishika pande za uso wangu, huku mwingine akiweka mkono mmoja kwenye paji langu na kuufungua mdomo wangu na mwingine akayamwaga kooni mwangu. Maji yale ya chumvi yalihisi machungu na makali kwenye koo langu, tumbo langu lilihisi mara moja kana kwamba lilikuwa likichomeka, na hali hii haikuweza kuvumilika kiasi kwamba nilitaka kulia. Walipoona kusumbuka kwangu, walisema kwa ukatili, "Hutavuja damu kwa urahisi tutakapokupiga baada ya kunywa maji ya chumvi." Nilidhibiti hasira niliyohisi kwa shida niliposikia hivyo. Sikuwahi kufikiri polisi wa Umma wa China ambao wanadhaniwa kuwa waadilifu wangekuwa wabaya na waovu sana. Sio tu kwamba pepo hawa waovu walikusudia kuchezacheza nami na kuniumiza, lakini pia walinuia kunifedhehesha. Usiku huo, mmoja wa polisi hawa waovu alinijia, akachutama, na kugusa uso wangu kwa mkono wake huku akinizungumzia maneno machafu. Nilikasirika sana kiasi kwamba nilimtemea mate usoni pake moja kwa moja. Alikasirika na kunipiga kofi kali, akinifanya nione vimulimuli na masikio yangu kuwangwa. Kwa sauti ya kutisha akasema, "Bado hujapitia mbinu zetu nyingine za mahojiano. Ukikufa hapa, hakuna mtu atakayejua kamwe. Kiri, au kutakuwa na michezo zaidi ambayo tunaweza kucheza nawe!” Usiku huo, nililala sakafuni, pasipo kuweza kusonga hata kidogo. Nilitaka kwenda msalani, kwa hiyo waliniambia nisimame peke yangu. Huku nikitumia nguvu yangu yote, niliweza kusimama polepole, lakini nilianguka tena baada ya kupiga hatua moja tu. Sikuweza kusogea, kwa hiyo afisa wa kike alilazimika kunivuta hadi msalani, ambapo nilizimia tena. Nilipoamka, nilikuwa nimerudishwa kwenye chumba changu. Niliona kuwa miguu yangu ilikuwa imevimba sana kiasi kwamba ngozi iling’aa, pingu na silisili zilikuwa zimejitia ndani sana ya ngozi ya na vifundo vya mikono na miguu yangu, damu na usaha ulivuja kutoka kwenye vidonda, na ilikuwa chungu sana kuliko jinsi ambavyo ningeeleza. Nilifikiria juu ya mbinu nyingine za mateso zilizobaki ambazo afisa ambaye aligusa uso wangu alikuwa ametoka kusema kuwa wangetumia kwangu, na sikuweza kujizuia kuhisi dhaifu, kwa hiyo nilimwomba Mungu: “Mungu! Sijui pepo hawa waovu watafanya nini kunitesa, na siwezi kuvumilia kwa muda mrefu tena. Tafadhali niongoze, nipe imani, niridhie nguvu, na Uniruhusu nikushuhudie Wewe.” Baada ya kuomba, nilikumbuka mateso ambayo Mungu alivumilia nyakati mbili Alizokuja mwilini ili kuwaokoa wanadamu: Katika Enzi ya Neema, ili kuwakomboa wanadamu, Bwana Yesu alichezewachezewa, Akapigwa, na kutukanwa na askari na umati wa watu, Akalazimishwa kuvaa taji ya miiba, na mwishowe Akasulubishwa msalabani akiwa bado hai; leo, Mungu amefanya jambo la hatari kubwa zaidi kwa kuja mwilini ili kufanya kazi katika nchi imkanayo Mungu na, kimyakimya na bila malalamiko, Alivumilia kuteswa na kukamatwa na serikali ya CCP, pamoja na kuvumilia upinzani, kukataliwa, na shutuma kali ya ulimwengu wa dini. Nilikumbuka tena maneno ya Mungu: “E, mateso mnayokumbana nayo sasa si sawa kabisa na mateso ya Mungu? Mnateseka pamoja na Mungu, na Mungu yuko pamoja na watu katika mateso yao. Leo nyinyi nyote mna sehemu katika mateso ya Kristo, ufalme, na subira, na kisha, mwishowe mtapata utukufu. Aina hii ya mateso ina umuhimu. Kutokuwa na azimio hakutasaidia. Ni lazima uelewe umuhimu wa mateso ya leo na kwa nini lazima uteseke hivyo. Tafuta ukweli kidogo kutoka kwa hili na kuelewa nia chache za Mungu, na kisha utakuwa na azimio la kuvumilia mateso(“Ni Kwa Kufuatilia Ukweli Tu Ndiyo Unaweza Kupata Mabadiliko Katika Tabia Yako” katika Kumbukumbu za Hotuba za Kristo). Ni kweli, Mungu alivumilia mateso niliyokuwa nikiyapitia zamani sana. Mungu hakuwa na hatia, lakini ili kuwaokoa wanadamu wapotovu, Mungu alivumilia kila mateso na fedheha, wakati mateso niliyokuwa nikivumilia yalikuwa tu ili mimi mwenyewe nipate wokovu wa kweli. Kwa kuzingatia swali hilo kwa makini, niligundua kuwa mateso yangu mwenyewe hayakufaa kutajwa karibu na mateso ambayo Mungu alivumilia. Mwishowe nilielewa ukubwa wa mateso na fedheha ambayo Mungu alivumilia ili kutuokoa, na nikahisi kwamba upendo wa Mungu kwa wanadamu kwa kweli una nguvu na hauna ubinafsi! Moyoni mwangu, nilihisi kumtamani Mungu sana. Kupitia mateso yangu, Mungu aliniruhusu nione nguvu na mamlaka Yake zaidi, na kutambua kwamba maneno Yake ni nishati uhai ya mwanadamu, na yanaweza kuniongoza nishinde dhiki yoyote; kupitia mateso haya, Mungu pia alikuwa akiisafisha imani yangu, Akijaribu mapenzi yangu, na kuniruhusu nifidie kile nilichokosa na kukamilisha kasoro zangu mwenyewe. Nilielewa mapenzi ya Mungu, na nikagundua kwamba mateso niliyovumilia siku hiyo yalikuwa zawadi kubwa ya neema ya Mungu, na kwamba Mungu alikuwa pamoja nami, kwa hiyo sikuwa peke yangu. Sikuwa na budi kukumbuka wimbo wa kanisa: “Mungu ni msaada wangu, kuna nini cha kuhofu? Ninaahidi maisha yangu kupigana na Shetani mpaka mwisho. Mungu anatuinua, tunapaswa kuacha kila kitu nyuma na kupigana kuwa na ushuhuda kwa Kristo. Mungu atatekeleza mapenzi Yake duniani. Nitaandaa upendo wangu na uaminifu na kuvitoa kwa Mungu. Nitakaribisha kurudi kwa Mungu kwa shangwe atakaposhuka katika utukufu, na kukutana na Yeye tena ufalme wa Kristo utakapofanyika” (“Ufalme” katika Mfuateni Mwanakondoo na Kuimba Nyimbo Mpya).

Siku ya tano, polisi hawa waovu waliendelea kunifanya nichutame nusu. Miguu na nyayo zangu tayari zilikuwa zimevimba sana kiasi kwamba sikuweza kusimama hata kidogo, kwa hiyo polisi walinizingira na kunisukuma kutoka kwa mmoja hadi kwa mwingine. Baadhi yao pia walitumia fursa ya hali yangu kunipapasa. Niliweza tu kuwaacha wacheze nami kama mwanasesere bila kujali. Nilikuwa tayari nimeumizwa vibaya hadi kufikia kiwango ambacho kichwa changu kilikuwa kikizunguka na macho yangu yalikuwa na ukungu. Lakini wakati tu ambapo sikuweza kuvumilia tena, ghafla nikasikia nyayo nje ya mlango, jambo ambalo lilifuatiwa na wao kukimbia mlangoni, kuufunga, na kuacha mchezo wao katili. Nilijua kuwa huyu alikuwa Mungu akinionyesha huruma, na kwamba Alikuwa akipunguza maumivu yangu. Usiku huo, mmoja wa polisi waovu alinijia, akavua kiatu chake, na kuweka mguu wake ulionuka mbele ya uso wangu huku akisema kikware, “Unafikiri kuhusu nini unapokaa hapo? Ni kuhusu wanaume? Haya, unaonaje hili? Unapenda uvundo wa mguu wangu? Nafikiri kuwa uvundo wa mguu wangu ndio hasa kile ambacho umekuwa ukikosa!” Lugha yake chafu ilinighadhabisha. Nilimkazia macho kwa hasira, na nilipoangalia uso wake usio na aibu na wa kuchukiza, nilikumbuka jinsi ambavyo nilikuwa nimeteswa na kufedheheshwa tena na tena. Walikosa ubinadamu kabisa, walikuwa wabaya zaidi kuliko wanyama, walikuwa tu genge la pepo ambao hawakuwa na mantiki hata kidogo, na nilichukia pepo hawa kwa dhati! Kupitia uzoefu wangu wa binafsi katika siku kadhaa zilizopita, niliona kuwa Polisi wa Umma ambao nilikuwa nimewachukulia kama mifano halisi ya unyofu hapo zamani walikuwa tu wahalifu wasio na haya, na hii ilinipa azimio la kumuacha Shetani na kusimama kidete na kushuhudia ili kumridhisha Mungu.

Kufikia siku ya sita, nilianza kulala bila kujua. Afisa mkuu alitangaza kwa majivuno, "Hatimaye umeanza kulala! Unataka usingizi? Haiwezekenai! Tutakunyima usingizi hadi tukufanye usalimu amri! Hebu tuone utadumu muda gani!" Walinilinda kwa zamu, na pindi tu nilipofunga macho yangu au kusinzia, waliugonga meza kwa mijeledi yao, au kutumia fimbo nyembamba ya mbao kugonga miguu yangu, ambayo ilikuwa imevimba sana kiasi kwamba ngozi iling’aa, au walivuta nywele zangu kwa nguvu au kukanyaga mguu wangu, na kila wakati niligutushwa. Wakati mwingine walipiga silisili zangu teke, na silisili zangu zilipogusa vidonda vyangu vilivyotunga usaha, maumivu yalitosha kunigutusha. Mwishowe, kichwa changu kiliuma sana kiasi kwamba nilihisi kana kwamba kingelipuka, nilihisi kana kwamba chumba kilikuwa kikizunguka, na nikaanguka sakafuni kichwa kwanza na kuzimia…. Kupitia hali yangu ya kuchanganyikiwa, nilimsikia daktari akisema, "Hamjamruhusu ale au kulala kwa siku kadhaa? Ninyi ni wakali sana. Na silisili hizi tayari zimeng’ata kwenye nyama. Hapaswi kuzivaa tena.” Baada ya daktari kuondoka, polisi walinitia pingu zenye uzito wa kilo 2.5 na wakanipaka dawa, na hapo tu ndipo nilipata fahamu. Nilijua kuwa nilikuwa nimenusurika kwa sababu tu ya kudura ya Mungu, na kwa sababu Mungu alikuwa akinilinda sirini, Akipunguza maumivu yangu na kupunguza mateso yangu kwa kunena kupitia daktari huyo. Nilikuwa na imani zaidi katika Mungu kuliko hapo zamani, na nikapata azimio la kupambana na Shetani hadi mwisho. Mungu alikuwa msaada wangu thabiti na kimbilio langu. Nilijua kuwa bila idhini ya Mungu, bila kujali jinsi Shetani alivyonitesa, hangeweza kuniua.

Asubuhi ya siku ya saba, nilikuwa nimechoka sana kiasi kwamba sikuweza kuvumilia tena, na nilishinda nikisinzia. Polisi mmoja mwovu aliona hali yangu na alikanyaga vidole vyangu vya mguu mara kwa mara, akafinya nyuma ya mikono yangu, na kunipiga kofi usoni. Adhuhuri hiyo, wale polisi waovu waliniuliza tena habari kuhusu kanisa. Nilimwomba Mungu upesi, "Ee Mungu! Nimenyimwa usingizi sana kiasi kwamba siwezi kufikiri vizuri. Tafadhali nilinde na Unipe akili safi, ili niweze kukushuhudia nyakati zote.” Kwa msaada wa ulinzi wa Mungu, licha ya kuwa macho kwa siku saba na usiku sita, bila chakula, maji, au usingizi, akili yangu ilikuwa wazi kabisa, na bila kujali jinsi walivyonijaribu, bado sikuwaambia chochote. Baada ya hapo, afisa mkuu wa polisi alitoa orodha ya wafanyakazi wa mishonari ambao nilikuwa nimewaandika, kisha akajaribu kunilazimisha nifumbue majina mengine. Lakini baada ya kupitia ukatili uliotoloewa na pepo hawa, sikuwa tayari kumwacha ndugu yangu yeyote atumbukie mikononi mwao, kwa hivyo nilimwomba Mungu anipe nguvu, na wakati ambapo afisa wa polisi hakuwa makini, nilisogea mbele, nikachukua orodha ya majina, nikaijaza kinywani mwangu, na nikaimeza. Polisi wawili waovu walinitukana kwa hasira walipokuwa wakikurupuka kwenda mbele na wakajaribu kuufungua mdomo wangu na kunigonga usoni vikali. Mapigo yalisababisha damu itiririke kutoka katika pembe za kinywa changu, na kusababisha kichwa changu kizunguke, na yakafanya uso wangu uvimbe.

Baada ya raundi kadhaa za mahojiano yasiyo na maana, hawakuwa na chaguo ila kusalimu amri, kwa hivyo walinirudisha kizuizini. Polisi kule kizuizini waliona jinsi nilivyoumizwa vibaya, na waliogopa kuwajibika iwapo ningefia pale, kwa hiyo walikataa kunipokea. Katika hali ya kukata tamaa, mahojaji waovu walilazimika kunipeleka hospitalini kwa ajili ya kutiwa tubu za oksijeni. Baadaye, walinirudisha kizuizini, na nilikuwa katika hali ya kuzimia kwa siku nne. Baada ya wafungwa wengine kuniamsha, nilizimia tena mara mbili zaidi. Mwishowe, serikali ya CCP ilinihukumu kifungo cha mwaka mmoja na miezi tisa ya marekebisho kupitia kazi kwa kosa la "kujiunga na shirika la xie jiao." Hata hivyo, kwa sababu nilikuwa nimeteswa vibaya sana, nilikuwa nimepooza na sikuweza kutembea, na kambi ya kazi haingenipokea, kwa hiyo polisi walichapisha video yangu kwenye runinga. Miezi mitatu baadaye, mume wangu hatimaye alipata habari kuhusu kile kilichokuwa kimenifika na akatumia yuani 12,000 kama dhamana ya kunitoa gerezani ili niachiliwe huru lakini bado nikisimamiwa. Mume wangu alipokuja kunichukua, nilikuwa nimeumia vibaya sana kiasi kwamba singeweza kutembea, kwa hiyo alilazimika kunibeba hadi garini. Baada ya kurudi nyumbani, madaktari walionifanyia uchunguzi walibaini kuwa nilikuwa na gegedu mbili za uti ambazo zilikuwa zimetenguka, kwamba singejitunza katika siku zijazo, na kwamba nimepooza maisha yangu yote. Nilidhani kuwa ningeshinda maisha yangu yote nikiwa nimelala kitandani, lakini kwa msaada wa huruma za Mungu na mfululizo wa matibabu, mwaka mmoja baadaye, mwili wangu ulianza kupona tena polepole. Kwa kweli nilishuhudia nguvu za Mungu zenye kudura, na vile vile upendo Wake kwangu. Kwa msaada wa Mungu, niliweza kuendelea kutekeleza wajibu wangu kama kiumbe aliyeumbwa!

Kupitia mateso na shida hizi, hata ingawa nilionja maumivu kikamilifu, nilipata pia utajiri wa uzima. Sikuona tu asili ya pepo ya serikali ya CCP waziwazi lakini, la muhimu zaidi, niliona matendo ya kushangaza ya Mungu, niliona mamlaka na nguvu ya maneno ya Mungu, na nilihisi umaalumu na wingi wa nishati uhai ya Mungu: Katika hali yangu ya udhaifu na kutojiweza kabisa, ni maneno ya Mungu ambayo yalinipa nguvu na ujasiri, na ambayo yalinipa imani ya kuachana na nguvu za giza za Shetani; wakati ambapo mwili wangu haukuweza kuvumilia mateso na maumivu makali tena, Mungu alipanga watu, mambo, na vitu ili kupunguza mzigo wangu; nilipoteswa na pepo hadi nikakosa fahamu, kazi ya ajabu ya Mungu ilifungua njia na kuniokoa kutoka hatarini kwa salama…. Baada ya kupitia mambo haya, niliona kwamba Mungu alikuwa karibu nami kila wakati, Akinichunga, Akinilinda, na kutembea nami. Upendo wa Mungu kwangu kweli ni mkubwa! Mungu ni nguvu yangu maishani, muawana na msaada wangu wakati wowote ninapouhitaji, na ninatamani kujitoa mwili na roho kwa Mungu, kutafuta kumjua Mungu, na kuishi kwa kudhihirisha maisha yenye maana!

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Maudhui Yanayohusiana

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp