Kushinda Kupitia Majaribu ya Shetani

26/01/2021

Na Chen Lu, China

Nilizaliwa miaka ya 1980 katika kijiji—tulikuwa tumekuwa familia ya wakulima kwa vizazi vingi. Nilijiingiza katika masomo yangu ili niweze kuhitimu kuingia katika chuo na kuepuka maisha ya kijijini ya umasikini na hali ya kuwa nyuma. Nilipoanza shule ya upili, nilikutana na Historia ya Sanaa ya Magharibi, na wakati nilipoona picha nyingi za kupendeza kama vile “Mwanzo,” “Bustani ya Edeni,” na “Mlo wa Mwisho,” ni hapo tu nilipojua kwamba kulikuwa na Mungu katika ulimwengu aliyeumba vitu vyote. Sikuweza kujizuia kuwa na moyo uliojaa hamu ya Mungu. Baada ya kuhitimu kutoka chuo, nilipata kazi nzuri kwa urahisi sana, na kisha nikampata patna mzuri. Hatimaye nilikuwa nimefanikisha matarajio yangu mwenyewe na yale ya mababu zangu. Nilikuwa nimeepuka nasaba ya mababu zangu ya kuuweka uso wangu chini na mgongo wangu kuangalia mbingu, na mwaka wa 2008, kuzaliwa kwa mtoto kuliongeza furaha zaidi kwa maisha yangu. Nikiangalia kila kitu nilichokuwa nacho katika maisha yangu, niliamini kuwa nilistahili niwe na maisha ya furaha, ya kustarehesha. Hata hivyo, wakati nilipokuwa nikifurahia maisha hayo ya kufanikiwa sana, mazuri, sikuweza kamwe kukatisha hisia zisizo yakini za utupu ndani ya moyo wangu. Hili lilinifanya kujihisi kuchanganyikiwa hasa na nisiyejiweza.

Mnamo Novemba ya mwaka wa 2008, familia yangu ilinizungumza kuhusu injili ya siku za mwisho ya Mwenyezi Mungu. Kupitia maneno ya Mungu hatimaye nilielewa kwamba Yeye ndiye chanzo cha maisha ya wanadamu, na kwamba maneno Yake ni msukumo na nguzo za maisha yetu. Tukiacha riziki na chakula cha Mungu kwa maisha yetu, roho zetu zitakuwa tupu na peke yake, na bila kujali ni furaha yakinifu gani tulizo nazo sisi hatutaweza kamwe kuyaridhisha mahitaji ya roho zetu. Kama vile tu Mwenyezi Mungu alivyosema: “Mwanadamu, hata hivyo, ni mwanadamu. Nafasi na maisha ya Mungu hayawezi kubadilishwa na mwanadamu yeyote. Mwanadamu hahitaji tu jamii iliyo na haki, ambapo kila mtu analishwa vyema na ana uhuru na usawa, lakini wokovu wa Mungu na Yeye kuwapa uhai. Wakati tu mwanadamu atapokea wokovu wa Mungu na kupatiwa uhai na Yeye ndipo mahitaji, hamu ya kuchunguza, na utupu wa kiroho wa mwanadamu utaweza kutatuliwa(Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Kiambatisho 2: Mungu Anaongoza Majaliwa ya Wanadamu Wote). Maneno Yake yaliathiri nafsi yangu ghafla kama chemchemi jangwani, na yaliondoa mchafuko ndani ya moyo wangu. Kuanzia wakati huo kwendelea, nilisoma maneno ya Mungu kwa njaa na kiu kubwa, na daima kulikuwa na hisia zisizoelezeka za utulivu moyoni mwangu kwamba roho yangu hatimaye ilikuwa imekuja nyumbani. Baada ya muda mfupi, kanisa liliwapangia ndugu fulani wa kiume na wa kike kukutana nami, na walifanya hivyo kwa uendelevu bila kujali jinsi hali ya hewa ilivyokuwa kali. Wakati huo, kulikuwa na vitu vingi ambavyo sikuvielewa na hawa ndugu wa kiume na wa kike waliwasiliana nami kwa uvumilivu. Hakukuwa na hata kiasi kidogo cha kuudhika au hata kufurahisha tamaa zangu, na kupitia hili nilihisi kwa kina uaminifu na upendo wa ndugu hawa wa kiume na wa kike. Nilipoelewa zaidi kuhusu ukweli, nilianza kuelewa hamu ya haraka ya Mungu ya kuwaokoa wanadamu, na niliona kuwa ndugu hawa wa kiume na wa kike walijitumia kwa hamu na kuhubiri injili kwa niaba ya Mungu. Nilitaka pia kutimiza wajibu wangu mwenyewe, lakini mtoto wangu alikuwa mdogo na sikuwa na mlezi mwingine, kwa hiyo nilimwomba tu Mungu anipe suluhisho. Baadaye, nilipata habari kwamba kulikuwa na dada mmoja aliyekuwa anasimamia shule ya malezi, hivyo nilimpeleka mtoto wangu kwake. Aliahidi kunisaidia kumtunza mtoto wangu bila kusita, na hata hangekubali karo au gharama za vyakula. Kuanzia wakati huo kwendelea, huyo dada alinisaidia tu kumtunza mtoto wangu wakati wa mchana, lakini wakati mwingine alisaidia usiku pia. Vitendo vya huyo dada vilinigusa kwa undani, na nilijua kuwa haya yote yalitoka kwa upendo wa Mungu. Ili kufidia upendo Wake, nilijiunga na safu ya wale waliohubiri injili bila kusita. Lakini wakati huo, ukandamizaji na kukamatwa kwa waumini na serikali ya CCP zilikuwa kali zaidi; kaka na dada wengi walikamatwa, na mimi mwenyewe sikuweza kuepuka hatima hii.

Kushinda Kupitia Majaribu ya Shetani

Hiyo ilikuwa asubuhi ya Desemba 21, mwaka wa 2012. Zaidi ya dazeni moja ya ndugu wa kiume na wa kike walikuwa wakikutana nyumbani mwa mwenyeji mmoja kulipokuwa ghafla na mshindo wa kubisha na kupiga kelele mlangoni: “Fungua mlango! Fungua mlango! Ukaguzi wa nyumba!” Dada mmoja alipokuwa akifungua mlango, polisi sita au saba waliokuwa wamebeba virungu walijilazimisha ndani. Kwa ukali walitumamanua na kisha wakaanza kupekua watoto wa meza. Dada mmoja kijana alikuja na kuwauliza: “Tunapanga kwa rafiki yetu na hatukuvunja sheria. Kwa nini mnapekua nyumba?” Polisi walijibu kwa ukali: “Shika adabu! Tukikuambia usimame hapo, simama hapo. Tusipokwambia uzungumze, funga kinywa chako!” Kisha wakamtupa kwa ukatili sakafuni, na wakasema kwa sauti kubwa ya ujeuri: “Ukitaka kubisha tutakupiga!” Ukucha wake wa kidole ulikuwa umevunjika na kidole chake kilikuwa kinavuja damu. Kuona nyuso mbovu za polisi, nilihisi chuki na hofu, kwa hiyo nikamwomba Mungu kimya kimya anipe nguvu na ujasiri, anilinde ili niwe shahidi. Baada ya kuomba, moyo wangu ulitulia sana. Polisi walichukua ngawira vifaa vingi vya kiinjilisti na mkusanyiko wa maneno ya Mungu, kisha wakatuingiza kwa magari ya polisi.

Mara tu tulipofika kituoni, walichukua ngawira kila kitu tulichokuwa tumebeba na kutuhoji ili kujua majina yetu, anwani, na viongozi wetu wa kanisa walikuwa akina nani. Sikusema chochote; dada mwingine hakusema chochote pia, kwa hiyo polisi walituona kama viongozi wa waasi na kutayarisha kusikiza kesi yetu mmoja kwa utenganisho. Niliogopa sana hapo—nilikuwa nimesikia kwamba polisi walikuwa hasa katili kwa watu ambao hawakuwa wenyeji, na nilikuwa nimelengwa kuhojiwa. Hilo bila shaka lingemaanisha ukatili zaidi, bahati kidogo. Nilivyokuwa tu katika hali ya kuogofya na kuishi katika hofu, nikamsikia dada yangu aliyekuwa karibu nami akisali: “Ee Mungu, Wewe ni mwamba wetu, kimbilio letu. Shetani yuko chini ya miguu Yako, na niko tayari kuishi kulingana na maneno Yako na kuwa shahidi ili kukuridhisha Wewe!” Baada ya kusikia hayo, moyo wangu ukachangamka. Niliwaza: Ni kweli—Mungu ni mwamba wetu, Shetani yuko chini ya miguu Yake, kwa hiyo ninaogopa nini? Alimradi ninategemea Mungu Shetani anaweza kushindwa! Ghafla sikuwa na hofu tena, lakini pia nilihisi aibu. Nilifikiria ukweli kwamba wakati huyo dada alipokabiliwa na hili, aliomba na kumtengemea Mungu na hakupoteza imani kwa Mungu, lakini nilikuwa mwepesi wa kutishwa na mwoga. Sikuwa na ujasiri hata kidogo wa mtu ambaye humwamini Mungu. Kwa sababu ya upendo wa Mungu na kupitia sala ya huyo dada ambavyo vilikuwa vimenipa motisha na kunisaidia, sikuwa tena na woga wa nguvu za udhalimu za polisi. Niliamua kwa utulivu: Ingawa nimekamatwa leo, nimedhamiria kuwa shahidi ili kumridhisha Mungu. Kabisa sitakuwa mwoga ambaye humsikitisha Mungu!

Takribani saa nne asubuhi, polisi wawili walinitia pingu na kunipeleka kwa chumba fulani ili kunihoji peke yangu. Mmoja wa wale polisi alinena nami kwa lugha ya mahali pale pale. Sikuelewa, na nilipomuuliza alichokuwa amesema, bila kutarajiwa swali hili liliwakasirisha. Mmoja wa polisi aliyekuwa amesimama karibu alizishika nywele zangu, akanirusha huku na huko. Nilikuwa na kizunguzungu na kutupwa pande zote, na ngozi ya kichwa changu ilihisi kama ilikuwa inaambuliwa na nywele zangu kung’olewa. Baada tu ya hayo, askari mwingine alinijia mbio na kusema kwa sauti kubwa: “Kwa hiyo tunapaswa kuwa wagumu? Sema! Ni nani aliyewafanya mhubiri injili?” Nilijaa hasira na nikajibu: “Kuhubiri injili ni wajibu wangu.” Niliposema hivi tu, yule polisi wa kwanza tena akanishika kwa nywele na kunipiga kofi usoni, kunigonga na kusema kwa sauti: “Nitakufanya uhubiri zaidi!” Nitakufanya uhubiri zaidi! Aliugonga uso wangu mpaka ukawa mwekundu kama kiazichekundu kwa maumivu, na ukaanza kuvimba. Alipochoka kunipiga, aliniacha niende, kisha wakachukua simu ya mkononi na kicheza kanda cha MP4 walivyopata nikiwa navyo na kuniuliza habari kuhusu kanisa. Nilitegemea hekima ili kushughulika nao. Kwa Ghafla, askari mmoja akauliza: “Wewe hujatoka hapa. Unazungumza Kimandarini vizuri sana—waziwazi wewe si mtu wastani. Sema ukweli! Kwa nini umekuja hapa? Nani aliyekutuma hapa? Ni nani kiongozi wako? Uliwasilianaje na kanisa hapa? Unaishi wapi?” Kusikia kwamba polisi hawa waliniona kama mtu muhimu na walisisitiza kukusanya taarifa juu ya kanisa kutoka kwangu, nilifadhaika na kumwomba Mungu anipe ujasiri na nguvu. Kupitia sala, moyo wangu polepole ulitulia, na nikajibu: “Sijui chochote.” Waliposikia nikisema hayo, waliponda meza kwa ukali na kupaaza sauti: “Wewe subiri tu, tutaona jinsi unavyohisi hivi punde!” Kisha wakachukua kicheza kanda changu cha MP4 na kukichezesha. Niliogopa mno. Sikujua wangetumia mbinu gani kunishughulikia, kwa hiyo kwa haraka nikatoa kilio kwa Mungu. Sikuwa nimewaza ya kwamba kile kilichochezwa kilikuwa ni kifungu cha maneno ya Mungu yaliyorekodiwa. “Sitawahurumia tena wale ambao hawakuwa waaminifu Kwangu kabisa wakati wa majonzi, kwa sababu huruma Yangu ina mipaka. Zaidi ya hayo, Simpendi yeyote yule ambaye amewahi kunisaliti Mimi, wala Sipendi kujihusisha na wale ambao hawawajali wenzao. Bila kujali huyo mtu ni nani, hii ndiyo tabia Yangu. Ni lazima Niwaambie hili: Yeyote atakayeuhuzunisha moyo Wangu hatapokea huruma kutoka Kwangu mara ya pili, na yeyote ambaye amekuwa mwaminifu Kwangu atadumu moyoni Mwangu milele(Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Tayarisha Matendo Mema ya Kutosha kwa ajili ya Hatima Yako) Niliposikia maneno ya mungu, nilihisi mchomo moyoni mwangu. Sikuweza kujizuia kufikiria kwamba wakati Bwana Yesu alipokuwa akifanya kazi, wale waliomfuata Yeye na kufurahia neema Yake walikuwa wengi, lakini wakati alipotundikwa msalabani na askari wa Kirumi walikuwa wakiwakamata Wakristo kutoka pande zote, watu wengi walikimbia kwa sababu ya hofu. Hili lilimletea Mungu uchungu mkubwa! Lakini basi, kuna tofauti gani kati yangu na wale watu wasio na shukrani? Wakati nilipofurahia neema na baraka za Mungu, nilikuwa na ujasiri mkubwa katika kumfuata Mungu, lakini nilipokabiliwa na taabu ambazo zilinihitaji kuteseka na kulipa gharama, nilikuwa mwepesi wa kutishwa na mwenye kuogopa. Je, hilo lingeufarijije moyo wa Mungu? Nilifikiria ukweli kwamba Mungu alijua wazi kwamba kuwa mwili nchini China, hii nchi iliyotawaliwa na wakana Mungu, kungedhihirisha hatari kubwa, lakini ili kutuokoa sisi watu wapotovu, bado Alikuja mahali hapa pa pepo bila kusita, akivumilia ufuatiliaji wao na lawama, na Yeye mwenyewe alituongoza kwenye njia ya ukimbizaji wa ukweli. Nikiona nia ya Mungu ya kujitolea kila kitu, kuacha kila kitu ili kutuokoa, ningekosaje, kama mtu aliyefurahia neema ya wokovu Wake, kulipa gharama ndogo kwa ajili Yake? Katika dhamiri yangu nilihisi kukemewa na nilichukia kwamba nilikuwa na ubinafsi sana, duni sana. Nilihisi sana kwamba Mungu alijaa tumaini kwangu na kunijali. Nilihisi kwamba Alijua vizuri kwamba nilikuwa mchanga kwa kimo na niliogopa mbele ya udhalimu wa Shetani; Aliniruhusu kulisikia hili kwa njia ya polisi kucheza maneno yaliyorekodiwa, akiniruhusu kuelewa mapenzi Yake, ili katikati ya dhiki na ukandamizaji ningeweza kuwa shahidi kwa Mungu na kumridhisha. Kwa muda mfupi, niliguswa sana na upendo wa Mungu kiasi kwamba machozi yalinitiririka usoni mwangu, na nikamwambia Mungu kimya kimya: “Ewe Mungu! Sitaki kukusaliti Bila kujali jinsi gani Shetani anavyonisumbua, nimeamua kuwa shahidi na kuufariji moyo Wako.”

Kisha kulikuwa na mshindo wa ghafla polisi alipozima kile kicheza kanda, kisha akakurupua kunielekea na kusema kwa chuki: “Kama hautatuambia, nitakutesa!” Kisha wakaniamuru nisimame sakafuni miguu mitupu na wakautia mkono wangu wa kulia pingu wakiuunganisha na uzingo wa chuma katikati ya kipande cha saruji. Ilinibidi kusimama kama nimeinama kwa sababu hicho kipande cha saruji kilikuwa kidogo sana. Hawakuniruhusu nichuchumae, wala hawakuniruhusu nitumie mkono wangu wa kushoto ili kuiegemeza miguu yangu. Sikuweza kuendelea kusimama baada ya muda na nilitaka kuchuchumaa, lakini polisi walinijia na kupiga kelele: “Hakuna kuchuchumaa! Ikiwa unataka kuteseka kidogo, fanya haraka na ukiri!” Yote niliyoweza kufanya ilikuwa ni kuyakereza meno yangu na kuvumilia. Sijui ni muda kiasi gani uliopita. Nyayo zangu zilikuwa kama barafu, miguu yangu ilikuwa inauma na yenye ganzi, na wakati kwa hakika sikuweza tena kukaa nimesimama, nilichuchumaa. Polisi waliniinua, wakaleta kikombe cha maji baridi, na wakayamimina kwa shingo yangu. Nilikuwa nahisi baridi sana kiasi kwamba nilianza kutetemeka. Kisha walizifungua pingu zangu, wakanisukuma kwa kiti cha mbao, wakaifunga mikono yangu pingu kwa miisho mkabala ya kiti kile, na kufungua madirisha na kuwasha kiyoyozi. Kulikuwa na dharuba ya ghafla ya upepo iliyonigonga na nilikuwa nikitetemeka kutokana na baridi. Sikuweza kujizuia kuwa na udhaifu katika moyo wangu, lakini katikati ya mateso haya nilikuwa nikisali bila kukoma, nikimwomba Mungu anipe ari na nguvu ya kuyahimili maumivu haya, kuniruhusu kuushinda udhaifu wa mwili. Wakati huo huo, maneno ya Mungu ukaniongoza kutoka ndani: “Hata wakati mwili wako unavumilia mateso, usichukue ushauri kutoka kwa Shetani. … Imani ni kama daraja moja la gogo la mti, wale ambao hushikilia maisha kwa unyonge watakuwa na ugumu katika kulivuka, lakini wale ambao wako tayari kujitolea wenyewe wanaweza kulivuka bila wasiwasi(Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Matamko ya Kristo Mwanzoni, Sura ya 6). Maneno ya Mungu yalinifanya nielewe kwamba Shetani alitaka kuutesa mwili wangu ili kunifanya nimsaliti Mungu, na kama ningeupuuza mwili ningeshikwa na udanganyifu wake. Nilizichunguza hizi sentensi mbili akilini mwangu, nikijiambia kuwa nilibidi kutahadhari dhidi ya udanganyifu wa Shetani na kuyakataa mawazo yake. Baadaye, polisi walichukua sufuria kubwa ya maji baridi na kuyamwaga yote kwa shingo yangu. Nguo zangu zote zilitota kabisa. Wakati huo nilihisi kama kwamba nilikuwa nimeanguka katika sanduku la barafu. Kuwaona hao polisi, wenye kustahili dharau sana, waovu sana, nilijaa chuki. Niliwaza: Hili kundi la pepo litatumia mbinu zozote ili nimsaliti Mungu—siwezi kuruhusu hila zao kufanikiwa! Wakiona nikitetemeka sana, hao polisi walishika konzi ya nywele zangu na wakakilazimisha kichwa changu kuangalia angani kupitia dirisha, kisha wakasema kwa mzaha: “Je, si wewe unahisi baridi? Basi, mwache Mungu aje akuokoe!” Waliona kwamba sikuwa naonyesha hisia, kwa hiyo polisi mara nyingine tena wakanimwagilia sufuria kubwa ya maji baridi na kuweka kiyoyozi kwenye hali yake ya baridi mno, kisha wakanipulizia moja kwa moja. Dharuba baada ya dharuba ya hewa kali baridi niliyopuliziwa ilinigonga pamoja na upepo baridi. Nilikuwa nahisi baridi sana kiasi kwamba nilikuwa nimejikunyata mithili ya mpira na nilikuwa nimeganda kama jiwe. Nilihisi kana kwamba damu imeganda ndani ya mishipa yangu. Sikuweza kujizuia kufikiri mawazo ya ujinga: Siku ya baridi hivi, lakini wananilowesha na maji baridi na kuwasha kiyoyozi. Je, wanajaribu kunigandisha nikiwa hai? Kama nitafia hapa, ndugu zangu hata hawatajua kulihusu. Nilipokuwa tu nikizama katika giza, nilifikiria ghafla mateso ambayo Yesu alivumilia alipokuwa akitundikwa msalabani ili kuwakomboa wanadamu. Na pia nilifikiria kuhusu maneno ya Mungu, “Upendo ambao umepitia usafishaji ni wa nguvu, na sio dhaifu. Haijalishi ni lini au vipi Mungu anakufanya upatwe na majaribu Yake, unaweza kutojali ikiwa unaishi au unaangamia, kuachana na kila kitu kwa furaha kwa ajili ya Mungu, na kuvumilia chochote kwa furaha kwa ajili ya Mungu—na hivyo upendo wako utakuwa safi, na imani yako halisi(Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Ni kwa Kupitia Usafishaji tu Ndiyo Mwanadamu Anaweza Kuwa na Upendo wa Kweli). Maneno haya kutoka kwa Mungu kwa kweli yaliniamsha—ndiyo! Siku hiyo kuweza kushuhudia kwa Mungu ilikuwa ni Yeye akiniinua—ningewezaje kuupuuza mwili? Hata kama ingemaanisha kupoteza maisha yangu, nilikuwa nimeamua kuwa mwaminifu kwa Mungu. Ghafla, kulikuwa na msisimko ndani ya moyo wangu na nikahisi kutiwa moyo sana. Kimya kimya niliomba kwa Mungu: “Ewe Mungu! Umenipa pumzi hii, afadhali nife kuliko kutenda kama msaliti kwako!” Polepole, sikuhisi hasa baridi tena, jambo ambalo liliniruhusu kwa kweli kuhisi urafiki wa Mungu na faraja. Kuanzia adhuhuri hadi takribani saa moja usiku, polisi waliendelea kunihoji. Waliona kwamba singefungua kinywa changu kabisa, kwa hiyo walinifungia katika chumba cha kuhojiwa na kwendelea kunipulizia hewa baridi.

Baada ya mlo mkuu wa siku, polisi waliongeza mkazo wa masaili yao. Walinitisha vikali, wakisema: “Tuambie! Ni nani kiongozi wa kanisa lako? Kama hutuambii, tuna njia zingine, tunaweza kukufanya unywe juisi ya pilipili kali, maji ya sabuni, kukufanya ule kinyesi, kukuvua nguo zote, kukutupa sehemu ya chini ya ardhi, na kukufanya ugande hadi kufa! Usipozungumza leo, tutakuuliza tena kesho. Tuna muda kwa upande wetu!” Polisi waliposema hivi, kwa kweli niliona kuwa hawakuwa watu kamwe, lakini walikuwa kundi la pepo katika mwili wa binadamu. Jinsi walivyozidi kunitisha kwa njia hiyo, ndivyo nilivyozidi kuwachukia moyoni mwangu, na ndivyo nilivyozidi kudhamiria kutokubali kamwe kushindwa nao. Walipoona singekubali kushindwa, walitafuta kitambaa cha mfuko, wakakilowesha maji, na kunigubika nacho kichwani mwangu. Walikibonyeza kwa kichwa changu na hawangeniruhusu kusogea, kisha wakakikaza. Sikuweza kusogea kabisa kwa sababu mikono yangu ilikuwa imefungiwa pingu kwa kiti. Kabla ya muda mrefu mno, nilikuwa karibu kunyongwa; Nilihisi kwamba mwili wangu mzima ulikwisha kuwa mgumu. Lakini hilo bado halikuwa la kutosha kuondoa chuki yao. Walichukua chungu cha maji baridi na kuyamimina ndani ya pua langu, wakinitisha, wakisema kwamba kama singezungumza, wangeninyonga. Mfuko uliolowa maji wenyewe haukupitisha hewa, na zaidi ya hayo maji yalikuwa yakimwagwa ndani ya pua langu. Kupumua kulikuwa kugumu sana, na ilihisi kana kwamba kifo kilikuwa kinakaribia. Niliomba kimya kimya kwa Mungu: “Ee Mungu, pumzi hii yangu nilipewa na Wewe, na leo ninastahili kuishi kwa ajili Yako. Bila kujali ni jinsi gani polisi wananitesa, sitakusaliti. Kama ukinihitaji nijitolee maisha yangu, niko tayari kutii madhumuni na mipango Yako bila malalamiko hata kidogo….” Bado waliendelea kunitesa. Nilipoanza tu kupoteza fahamu na nilikuwa karibu kuacha kupumua, ghafla wakatoa mikono yao. Sikuweza kujizuia kuendelea kumshukuru Mungu moyoni mwangu. Hata kama nilianguka mikononi mwa polisi, Mungu aliwaruhusu tu kuutesa mwili wangu lakini hakuwaruhusu kuyashikilia maisha yangu. Baada ya hayo, imani yangu ilikua.

Siku iliyofuata takribani saa sita mchana, polisi kadhaa walinichukua na dada mwingine ndani ya gari la polisi na kutupeleka kwa nyumba ya kizuizi. Mmoja wao akaniambia kwa kuniogofya: “Wewe hujatoka hapa. Tutakufungia kwa miezi sita, kisha tutakuhukumu miaka 3 hadi 5, kwa vyovyote akuna atakayejua.” “Kunihukumu?” Mara tu niliposikia kwamba ningehukumiwa, sikuweza kujizuia kuwa dhaifu. Nilihisi kwamba kama ningetumikia kifungo watu wengine wangeniangalia kwa dharau. Wale watu wengine katika seli nilimowekwa wote walikuwa dada ambao walimwamini Mwenyezi Mungu. Ingawa walikuwa katika hilo shimo la pepo, hawakuonyesha hofu hata kidogo. Walitiana moyo na kusaidiana, na walipoona kwamba nilikuwa hasi na dhaifu, walizungumza nami kuhusu uzoefu wao binafsi na kuwa na ushuhuda, wakinipa matumaini kwa Mungu. Pia waliniimbia wimbo wa uzoefu ili kunitia moyo: “Kwa unyenyekevu Mungu alipata mwili kuwaokoa wanadamu, akiongoza kila hatua, akitembea miongoni mwa makanisa, akionyesha ukweli, akijitahidi kumnyunyizia mwanadamu, akimtakasa na kumkamilisha. Ameyaona majira mengi ya kuchipua, ya joto, ya kupukutika na ya baridi, akiyachukua machungu na matamu. Anatoa yote bila kuwahi kujuta, Ametoa upendo Wake wote bila ubinafsi. Nimeonja uchungu wa majaribio na kupitia hukumu ya Mungu. Matamu yanafuata machungu, na upotovu wangu umetakaswa. Natoa moyo wangu, natoa mwili wangu kulipiza upendo wa Mungu, kulipiza upendo wa Mungu. Wapendwa wameniacha, wengine wamenikashifu. Lakini nitampenda Mungu bila kuyumbayumba hadi mwisho. Nimejitolea kabisa kufuata mapenzi ya Mungu. Ninavumilia mateso na taabu, nikipitia mema, nikipitia mabaya. Haijalishi kwamba navumilia haya maishani, haijalishi kwamba maisha yangu yamejaa machungu. Lazima nimfuate Mungu na kumshuhudia Yeye” (“Kulipiza Upendo wa Mungu na Kuwa Shahidi Wake” katika Mfuateni Mwanakondoo na Kuimba Nyimbo Mpya). Nikifikiri kuhusu wimbo huu, nilitiwa moyo pakubwa. Ulikuwa ni ukweli, tulikuwa tukifuata Mungu wa kweli na kutembea njia sawa ya uzima katika nchi chini ya utawala wa chama kikanacho Mungu ambacho kilimwona Mungu kama adui. Tulikuwa tumekusudiwa kupitia shida nyingi, lakini yote haya yalikuwa na maana, na hata kukaa gerezani lilikuwa jambo la utukufu kwa sababu tulikuwa tukiteswa kwa ajili ya kufuatilia ukweli na kuifuata njia ya Mungu. Ilikuwa tofauti kabisa na watu wa dunia kufungwa kwa kutenda makosa mabaya ya jinai. Nilifikiria kizazi baada ya kizazi cha watakatifu wengi ambao walipitia mateso na fedheha kwa sababu ya kushikilia njia ya kweli. Lakini sasa, nilikuwa nimepewa mengi sana kwa ukarimu ya neno la Mungu—nilielewa ukweli ambao vizazi vya watu havikuweza kuuelewa, nilijua siri ambazo vizazi havikuwa vimejua, hivyo ni kwa nini sikuweza kuvumilia mateso kidogo ili kumshuhudia Mungu? Wakati nilifikiria jambo hilo, nilijikokota tena kutoka kwa hali yangu ya udhaifu, moyo wangu ulijaa imani na nguvu, na nikaamua kumtegemea Mungu na kuyakabili mateso ya kesho na matakwa ya ungamo nikijivunia.

Siku kumi baadaye, polisi walinipeleka kwa kituo cha kizuizi peke yangu. Niliona kuwa watu wengine wote huko walizuiliwa kwa ulaghai, wizi, na biashara haramu. Mara tu nilipoingia, waliniambia: “Yeyote anayeingia hapa kwa kawaida huwa haitoki. Sote tunasubiri hukumu zetu, na baadhi yetu tumekuwa tukisubiri kwa miezi.” Nikiangalia watu hawa, nilikuwa na wasiwasi sana moyo wangu ulikaribia kupasuka. Niliogopa kwamba wangenitendea vibaya, na kisha nilipofikiri juu ya ukweli kwamba polisi wangenifungia nao, nilidhani kwamba huenda wangenipa hukumu ya mhalifu. Nilikuwa nimesikia kwamba baadhi ya ndugu wa kiume na wa kike walikuwa wamefungwa kwa muda mrefu kama miaka minane. Sikujua hukumu yangu ingekuwa urefu gani, na nilikuwa na umri wa miaka 29 tu! Haingewezekana ujana wangu kutumiwa kama nimefungiwa katika seli hii yenye giza? Siku zangu kutoka hapa kwendelea zingetumikaje? Wakati huo, ilionekana kwamba makazi yangu ya kudumu, wazazi, mume, na mtoto kwa ghafla walikuwa mbali sana na mimi. Ilikuwa ni kama kisu kikipinda ndani ya moyo wangu, na machozi yalijitunga machoni mwangu. Nilijua kwamba nilikuwa nimeanguka katika ulaghai wa Shetani, kwa hiyo nikamwita Mungu kwa hamasa, nikimtumainia Yeye aniongoze kuepuka mateso haya. Katikati ya sala yangu, nilihisi uongozi wazi ndani yangu: Unapokabiliana na hili, una ruhusa kutoka kwa Mungu. Kama vile tu Ayubu akijaribiwa, usilalamike. Kisha nikayafikiria Maneno ya Mungu: “Unafaa kujua, agano la kushinda Kwangu Shetani limo ndani ya uaminifu na utiifu wa binadamu, sawa tu na vile ilivyo katika agano la kumshinda kabisa binadamu. … Au afadhali unyenyekee katika kila mpangilio Wangu (uwe wa kifo au wa kuangamiza) au kutoroka hapo katikati ili kuepuka kuadibiwa?(Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Unajua Nini Kuhusu Imani?). Hukumu na kuadibu katika maneno ya Mungu kulinifanya niaibike. Niliona kwamba sikukaribia kuwa mwaminifu kwa Mungu, lakini nilisema kuwa nilitaka kuwa shahidi mzuri Kwake. Hata hivyo, nilipokabiliwa na hatari ya kufungwa, nilitaka tu kutoroka. Hakukuwa na uwezo wa utendaji wa kuteseka kwa ajili ya ukweli. Kufikiria nyuma wakati ule nilipokamatwa, Mungu alikuwa kwa upande wangu wakati wote. Yeye hakuniacha katika hatua yoyote ya njia kwa hofu kwamba ningepoteza njia yangu au kuanguka kwa njia. Upendo wa Mungu kwangu ulikuwa wa kweli kabisa na haukuwa mtupu kamwe. Lakini nilikuwa na ubinafsi na mchoyo, na wakati wote nilifikiria kuhusu faida na hasara zangu za kimwili. Sikuwa tayari kulipa gharama yoyote kwa ajili ya Mungu—ningewezaje kuwa na utu wowote? Dhamiri yoyote? S Nilipofikiria jambo hilo, nilijihisi kujaa majuto na madeni. Niliomba kimya kimya kwa Mungu na kutubu: Ee Mungu! Nilikosa. Siwezi tena kukuhudumia kwa maneno matupu na kukudanganya Wewe. Niko tayari kuishi kwa kudhihirisha ukweli ili kukuridhisha. Bila kujali hukumu yangu itakuwa nini, bila shaka nitakuwa shahidi Kwako—Wafungwa wengine hawakukosa kugombana nami tu, lakini kwa kweli walinitunza, wakinipa nguo, kunipa chakula cha ziada wakati wa chakula, na kugawana nami matunda na vitafunio walivyovinunua wenyewe, na pia walinisaidia na kazi yangu ya kila siku. Nilijua kwamba yote haya yalikuwa usanifu na mpango wa Mungu; ilikuwa huruma ya Mungu kwa asili yangu ya kama mtoto. Nikitazama upendo Wake na ulinzi Wake, niliweka azimio langu: Bila kujali jinsi hukumu yangu itakavyokuwa ndefu, nitakuwa shahidi kwa Mungu!

Katika kituo cha kizuizi, polisi wangenihoji mara moja kila siku mbili. Walipogundua kuwa kuchukua msimamo mkali hakungeniweza, walibadilisha na kuwa wapole. Polisi aliyekuwa akinihoji akawa na tabia za upole kwa makusudi na kuzungumza nami, akanipa chakula bora cha kula, na akasema angenisaidia kupata kazi nzuri. Nilijua kwamba huu ulikuwa ni udanganyifu wa Shetani, hivyo kila wakati aliponihoji niliomba tu kwa Mungu, nikimwomba Yeye kunilinda na kutoniruhusu niathiriwe na hila hizi. Wakati mmoja alipokuwa akinihoji, yule polisi hatimaye alifichua nia zao mbovu: “Hatuna neno nawe, tunataka tu kulichukulia hatua kali Kanisa la Mwenyezi Mungu. Tunatarajia unaweza kujiunga nasi.” Niliposikia maneno haya maovu, nilikuwa na hasira kubwa. Niliwaza: Mungu aliumba mwanadamu na ameendelea kutukimu na kutuongoza njia yote hadi sasa. Na sasa Amekuja kuwaokoa wale Aliowaumba na kutusaidia kutoroka kutoka kwa lindi letu kuu la mateso. Ni nini tena kilicho na kosa na hilo? Kwa nini linachukiwa sana, kukashifiwa sana na pepo hawa? Sisi ni viumbe wa Mungu. Kumfuata Mungu na kumwabudu Yeye ni sawa na sahihi, basi kwa nini Shetani atuzuie kwa njia hii, aondoe hata uhuru wa kumfuata Mungu? Sasa wanajaribu kunifanya kuwa kibaraka katika jitihada zao za kumwandama Mungu. Serikali ya CCP kwa kweli ni kundi la pepo walioamua kumkataa Mungu katakata. Wao ni wapinga maendeleo waovu kweli! Nilikuwa na hisia zisizoelezeka za maumivu ndani ya moyo wangu wakati huo, na yote niliyotaka ilikuwa ni kushuhudia Mungu na kuufariji moyo Wake. Wakati polisi walipoona kwamba bado singezungumza, walianza kutumia mbinu za kisaikolojia dhidi yangu. Walimpata mume wangu kupitia China Mobile na wakamleta yeye na mtoto wangu ili kunishawishi. Mume wangu mwanzoni alikuwa sawa na imani yangu kwa Mungu, lakini baada ya kudanganywa na polisi, aliniambia mara kwa mara: “Ninakusihi kuiacha imani yako. Angalau fikiria mtoto wetu kama si mimi. Kuwa na mama aliye gerezani kutakuwa na athari mbaya sana kwake. …” Wakati mume wangu alipoona kwamba maneno yake hayakuweza kugeuza mawazo yangu, alitupa maneno haya katili: “Wewe ni mkaidi na hautasikiliza—nitakutaliki tu, basi!” Neno hili, “taliki,” liliuchoma moyo wangu kwa kina. Lilinifanya niichukie serikali ya CCP hata kwa kina zaidi. Kulikuwa kukashifu huku kwayo na kuchonganisha kulikomfanya mume wangu aichukie kazi ya Mungu kwa njia hiyo na kusema maneno hayo yasiyo na huruma kwangu. Serikali ya CCP kwa kweli ndiyo mhalifu ambaye huwaambia watu wa kawaida kuikosea Mbinguni! Pia ilikuwa mhalifu katika kudhoofisha hisia zetu kama mume na mke! Kwa kufikiria haya, sikutaka kusema kitu chochote zaidi kwa mume wangu. Nilisema tu kwa utulivu: “Basi fanya haraka umrudishe mtoto wetu nyumbani.” Polisi walipoona kwamba mbinu hii haikuwa imefua dafu, walikuwa na hasira sana kiasi kwamba walienda dalji mbele na nyuma mbele ya dawati lao na kunipigia yowe, wakisema: “Tumefanya kazi kwa bidii sana na hatujapata jibu hata moja kutoka kwako! Kama utaendelea kukataa kuzungumza tutakupachika cheo cha mkuu wa mkoa huu, kama mfungwa wa kisiasa! Usipozungumza leo, hakutakuwa na fursa nyingine!” Lakini bila kujali jinsi walivyojitapa na kupayapaya, nilimwomba tu Mungu moyoni mwangu, nikimuuliza Yeye aimarishe imani yangu.

Wakati wa masaili yangu, kulikuwa na wimbo wa neno la Mungu ambao uliendelea kuniongoza kutoka ndani: “Katika hatua hii ya kazi sisi tunatakiwa kuwa na imani kuu na upendo mkuu. Huenda tukajikwaa kutokana na uzembe kidogo kabisa kwa sababu hatua hii ya kazi ni tofauti na zile zote za awali. Kile ambacho Mungu anakamilisha ni imani ya wanadamu—mtu hawezi kuiona au kuigusa. Kile ambacho Mungu anafanya ni kuyageuza maneno kuwa imani, kuwa upendo, na kuwa uzima. Watu lazima wafikie kiwango ambacho wamestahimili mamia ya kusafisha na wawe na imani iliyo kuu zaidi kuliko ya Ayubu. Wanatakiwa kustahimili taabu ya ajabu sana na aina zote za mateso bila kuondoka kwa Mungu wakati wowote. Wanapokuwa watiifu hadi kufa, na wawe na imani kuu katika Mungu, basi hatua hii ya kazi ya Mungu imetimizwa(“Kile ambacho Mungu anakamilisha ni imani ya wanadamu” katika Mfuateni Mwanakondoo na Kuimba Nyimbo Mpya). Kwa sababu ya imani na nguvu nilizopokea kutoka kwa maneno ya Mungu, wakati nilipokuwa nikihojiwa nilionekana madhubuti sana. Lakini niliporudi kwa seli yangu, sikuweza kujizuia kuwa dhaifu kidogo na kusononeka. Ilionekana kuwa mume wangu kwa kweli angenitaliki na singekuwa na nyumba tena. Pia sikujua hukumu yangu ingekuwa na urefu gani. Katikati ya maumivu haya, nilifikiria maneno haya kutoka kwa Mungu: “Sasa unafaa uweze kuona waziwazi njia iliyochukuliwa na Petro. Kama umeona hili waziwazi, basi utakuwa na hakika kuhusu kazi inayofanywa leo, kwa hiyo usingelalamika au kuwa kukaa tu, au kutamani chochote. Unafaa kupitia hali halisi aliyopitia Petro wakati huo: Alikumbwa na huzuni; hakuomba tena kuwa na mustakabali au baraka yoyote. Hakutafuta faida, furaha, umaarufu, au utajiri wa ulimwengu na alitafuta tu kuishi maisha yenye maana zaidi, ambayo yalikuwa ya kulipiza upendo wa Mungu na kujitolea kile alichokuwa nacho cha thamani kabisa kwa Mungu. Kisha angetosheka katika moyo wake(Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Namna Petro Alivyopata Kumjua Yesu). Niliguswa sana na matendo ya Petro, na hili pia liliyatikisa hiari yangu ya kukiacha kila kitu ili nimridhishe Mungu. Ilikuwa ni kweli. Petro alipofikia hatua yake ya kupatwa na majonzi, bado alikuwa anaweza kuhimili na kumridhisha Mungu. Haikuwa kwa matarajio yake mwenyewe au jaala, au faida yake mwenyewe, na mwishowe alipotundikwa juu chini kwa msalaba alitenda kama shahidi mzuri kwa Mungu. Lakini tena nilikuwa na bahati nzuri kumfuata Mungu mwenye mwili, kufurahia utoaji wa Mungu usio na mwisho kwa maisha yangu pamoja na neema na baraka Zake, lakini sikuwahi kulipa kamwe gharama yoyote halisi kwa Mungu. Halafu Aliponihitaji kuwa shahidi Kwake, sikuweza kumridhisha mara hiyo moja tu? Ukosaji wa fursa hii ungekuwa kitu ambacho ningejutia kwa maisha yote? Nilipofikiria hilo, niliamua hiari yangu mbele ya Mungu: Ee Mungu, niko tayari kufuata mfano wa Petro. Bila kujali matokeo yangu yatakuwa nini, hata kama ni lazima nitalikiwe au kutumikia kifungo jela, sitakusaliti Wewe! Baada ya kuomba, nilihisi wimbi la nguvu likiinuka ndani yangu. Singefikiria tena kama ningehukumiwa au la, au ni kwa muda gani hukumu hiyo ingekuwa, na singefikiria tena kama ningeweza kurudi nyumbani na kuungana tena na familia yangu au la. Ningefikiria tu kwamba siku nyingine katika pango hili la pepo ilikuwa siku nyingine ya kuwa shahidi kwa Mungu, na hata kama ningetumikia kifungo mpaka mwisho kabisa, singekubali kushindwa na Shetani. Nilipojitoa mwenyewe, kwa kweli nilikuwa na ladha ya upendo wa Mungu na huba. Siku chache baadaye wakati wa alasiri moja, mlinzi mmoja ghafla akaniambia: “Kusanya vitu vyako, unaweza kwenda nyumbani.” Sikuthubutu kuamini masikio yangu kabisa! Nilikuwa nimejawa na furaha. Mapigano haya katika vita vya kiroho yamepotezwa na Shetani na Mungu alitukuzwa mwishowe!

Baada ya kupitia siku 36 kizuizini na mateso na polisi wa Kichina, nilikuwa na ufahamu wa kweli wa udhalimu wa ukatili, na kiini cha uasi na cha kupinga maendeleo cha serikali ya CCP. Kuanzia wakati huo kwendelea nikawa na chuki kubwa kwayo. Najua kwamba wakati wa shida hizo, Mungu alikuwa nami daima, akanipa nuru, akiniongoza, na kuniruhusu niushinde ukatili wa Shetani na majaribio kila hatua ya njia. Hili lilinipa uzoefu wa ukweli kwamba maneno ya Mungu kwa kweli ni maisha ya wanadamu na nguvu zetu. Pia nilifahamu kwa kweli kwamba Mungu ni Bwana wetu na hutawala kila kitu, na bila kujali ni hila ngapi Shetani anazo, daima atashindwa na Mungu. Alijaribu kuutesa mwili wangu kunilazimisha kumsaliti Mungu, kumtelekeza Yeye, lakini mateso yake ya ukatili hayakukosa tu kunivunja, lakini yaliuimarisha uamuzi wangu na kuniruhusu kuona kabisa uso wake wenye uovu, kutambua upendo wa Mungu na wokovu. Ninamshukuru Mungu kutoka moyoni mwangu.

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Maudhui Yanayohusiana

Kutoroka Hatari

Mwenyezi Mungu anasema, “Mungu kamwe hajawahi kosa kwa moyo wa mwanadamu, na Anaishi miongoni mwa binadamu wakati wote. Amekuwa nguvu ya...

Upendo wa Mungu Hauna Mipaka

Na Zhou Qing, Mkoa wa ShandongNimepitia taabu ya maisha haya kikamilifu. Sikuwa nimeolewa kwa miaka mingi kabla ya mume wangu kufariki, na...

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp