Upendo wa Mungu Hauna Mipaka

26/01/2021

Na Zhou Qing, Mkoa wa Shandong

Nimepitia taabu ya maisha haya kikamilifu. Sikuwa nimeolewa kwa miaka mingi kabla ya mume wangu kufariki, na tangu wakati huo mzigo mzito wa kutunza familia ulianguka mabegani mwangu. Kwa kuwa nilikuwa na mtoto mchanga, niliishi maisha magumu. Nilidhihakiwa na kudharauliwa na wengine kila mara; dhaifu na asiyejiweza, uso wangu ulijawa na machozi kila siku, nikihisi kana kwamba maisha katika ulimwengu huu yalikuwa magumu sana. Wakati tu nilikuwa nikizamia ndani kabisa ya kukosa rajua na kukata tamaa, dada alishiriki nami injili ya kazi ya Mwenyezi Mungu ya siku za mwisho. Moyo wangu ulijawa na ukunjufu niliposoma maneno haya kutoka kwa Mwenyezi Mungu: “Unapokuwa umechoka na unapoanza kuhisi huzuni kubwa ya ulimwengu huu, usipotoke, usilie. Mwenyezi Mungu, Mlinzi, atakaribisha kuwasili kwako wakati wowote(Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Kutanafusi kwa Mwenye Uweza). Mungu aliniita kama mama mwenye upendo na nilihisi kama kwamba nilikuwa mwishowe nimepata msaada wangu, na kupata mahali pa kupumzika pa roho yangu. Kuanzia wakati huo na kuendelea, nilisoma maneno ya Mungu kila siku, na nikapata habari kuwa Mungu ndiye chanzo cha maisha yote, kwamba Mungu hutawala hatima ya kila mtu, na kwamba Mwenyezi Mungu ni msaada na wokovu wa pekee wa wanadamu. Ili nipate kuelewa ukweli zaidi, nilihudhuria mikutano ya kanisa kwa bidii na, katika Kanisa la Mwenyezi Mungu, nilishuhudia ndugu wote wakiwa wanyofu na wazi kwa kila mmoja. Nilipokuwa nao nilihisi utulivu, nilihisi hisia kubwa ya uhuru moyoni mwangu, na nilikuwa na furaha na raha ambayo sikuwahi kuhisi kamwe ulimwenguni. Kwa hivyo, nilijawa na imani na matumaini ya maisha yangu ya baadaye. Nilianza kutekeleza wajibu wangu kanisani ili kulipa upendo wa Mungu. Hata hivyo, jambo la kushangaza ni kwamba, serikali ya CCP hairuhusu kabisa mtu yeyote kumwamini Mungu wa kweli au kufuata njia sahihi, na nilikamatwa mara kwa mara na kuteswa kikatili na kinyama na serikali ya CCP kwa sababu tu ya imani yangu.

Alasiri moja mnamo Desemba mwaka wa 2009, nilikuwa nikifanya kazi ya kufua nyumbani, wakati polisi watano au sita waliovalia nguo za raiya walipoingia kwa ghafla kwenye uwanja wangu. Mmoja wao alisema kwa sauti kuu, “Tumetoka katika Timu ya Polisi wa Jinai yenye jukumu maalum la kuwasaka waumini wa Mwenyezi Mungu!” Kabla ya kujituliza tena, walianza kufudikiza kila kitu nyumbani kwangu kama kundi la wanyang'anyi. Walichakura nyumba yangu, ndani na nje, na kuchukua ngawira vitu vingine vilivyohusu imani katika Mungu, kifaa cha kuchezesha DVD na cha kuchezesha CD ambavyo walivipata. Kisha walinisindikiza hadi kwenye gari la polisi na kunipeleka katika kituo cha polisi. Nilipokuwa njiani, nilifikiri juu ya jinsi ndugu walikuwa wameelezea kukamatwa na kuteswa kikatili na polisi waovu, na nikajawa na kiwewe; niliogopa sana. Katika dhiki kuu sana, nilimwomba Mungu kwa haraka: “Ee Mwenyezi Mungu! Ninahisi mnyonge sana hivi sasa. Mawazo kuhusu kuteswa yananiacha nikiwa na hofu sana. Tafadhali nipe imani na nguvu na Uondoe hofu yangu.” Baada ya kuomba, nilifikiria vifungu viwili vya maneno ya Mungu: “Kutoka kwa nje, wale walio na mamlaka wanaweza kuonekana kuwa waovu, lakini msiogope, kwa kuwa hii ni kwa sababu mna imani kidogo. Almuradi imani yenu ikue, hakuna kitu kitakachokuwa kigumu mno(Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Matamko ya Kristo Mwanzoni, Sura ya 75). “Katika mipango Yangu yote, joka kubwa jekundu ni foili[a] Yangu, adui Wangu, na pia mtumishi Wangu; kwa hivyo, Sijawahi kushusha ‘mahitaji’ Yangu kwake(Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Maneno ya Mungu kwa Ulimwengu Mzima, Sura ya 29). Nilipokuwa nikitafakari maneno ya Mungu, wazo lilinijia kwamba niliogopa mateso ya kikatili ya Shetani kwa sababu sikuwa na imani ya kweli katika Mungu. “Kwa kweli Shetani ni foili[a] ambayo humhudumia Mungu,” nilifikiria. “Bila kujali ni mkali na mkatili jinsi gani, yeye bado yuko mikononi mwa Mungu, na hana budi kutii mipangilio na mipango ya Mungu. Aidha, kadiri Shetani anavyozidi kuwa mkali na mkatili, ndivyo ninavyolazimika kutegemea imani yangu zaidi kutoa ushuhuda kwa Mungu. Wakati huu muhimu, siwezi kabisa kutishwa na mamlaka ya Shetani ya kidikteta, lakini badala yake lazima nitegemee imani na nguvu ambayo Mungu hunipa ili kumshinda Shetani.” Nilipokuwa nikifikiria hii, sikuogopa sana tena.

Tulipofika katika kituo cha polisi, polisi wawili walinitia pingu mikononi bila kusema neno lolote, na wakanipiga mateke na kunisukuma hadi kwenye ghorofa la pili na kisha kunikaripia, “Tuna mpango maalum kwa watu kama wewe kufurahia!” Nilijua moyoni mwangu kuwa “mpango huu maalum” ulimaanisha mateso. Wakati huo huo, niliendelea kumwomba Mungu moyoni mwangu, na sikuthubutu kumwacha Mungu hata kwa muda mfupi, nikihofia kwamba ningepoteza utunzaji na ulinzi Wake na kudanganywa na hila ya kijanja ya Shetani. Mara tu nilipoingia kwenye chumba cha mahojiano, mmoja wa polisi waovu aliniambia nipige magoti. Nilipokosa kufanya hivyo, alinigonga teke kali nyuma ya goti langu, na nikapiga magoti kwa kishindo pasipo kutaka. Kisha walinizingira na wakaanza kunichapa na kunipiga mateke mpaka kichwa changu kikazunguka na macho yangu yakawa na ukungu, na damu ilimwagika kutoka katika pua na mdomo wangu. Hata hivyo, bado hawakuwa wamemaliza, kwani waliniamuru nikae chini na wakaweka kiti mbele yangu. Mmoja wa polisi waovu kisha akaanza kunichapa mgongoni kwa nguvu, na uso na kichwa changu kiligonga kiti kila aliponichapa. Kichwa changu kilikuwa kiliwangwa, na uchungu haukuweza kuvumilika. Mmoja wa polisi alikenua kwa inda na kusema, “Kuna mtu ambaye tayari amekusaliti. Usipoanza kuzungumza, tutakupiga hadi ufe!” Baada ya kusema hivyo, alinipiga ngumi kifuani kikamilifu, ambayo iliniumiza vibaya kiasi kwamba sikuweza kupumua kwa muda mrefu. Polisi mwingine kisha akasema kwa sauti, “Unafikiria kwa kweli kuwa wewe ni Liu Hulan? Siku moja tutapiga hadi useme ukweli!” Genge la polisi waovu lilinitesa kwa kila njia, wakikoma tu wakati ambapo walichoka. Wakati tu nilipokuwa nikifikiria ningepewa muda fulani wa kupumzika, polisi mmoja aliyekuwa katika miaka yake ya hamisni alinijia na kujaribu kunihadaa kwa desturi yake ya askari mzuri “Mtu fulani ametwambia sasa kwamba wewe ni kiongozi wa kanisa. Unafikiri kuwa hatutaweza kushtaki kwa lolote usipozungumza? Tumekuwa tukikufuata kwa muda mrefu, na tulikukamata tu kwa sababu sasa tuna ushahidi wa kutosha. Kwa hivyo anza kuongea!” Nilishtuka kumsikia akisema hivi: “Yaweza kuwa kweli?” Niliwaza. “Ikiwa kwa kweli mtu amekuwa Yuda na kunisaliti, basi si tayari wangejua kila kitu kunihusu? Ninaweza kufanikiwa bila kuwaambia chochote? Nifanye nini?” Katika kukata tamaa kwangu, nilikumbuka maneno ya Mwenyezi Mungu: “Unafikiri kuhusu neema yote uliyoipata, maneno yote ambayo umeyasikia—je, unaweza kuyasikiliza bure? Haijalishi ni nani anakimbia, wewe huwezi. Watu wengine hawaamini, lakini lazima wewe uamini. Watu wengine wanamtelekeza Mungu, lakini lazima wewe umtetee Mungu na kushuhudia Kwake. Wengine humkashifu Mungu, lakini wewe huwezi. Haijalishi jinsi Mungu asivyo na huruma kwako, bado unapaswa kumtendea vyema. Unapaswa kuulipiza upendo Wake na lazima uwe na dhamiri, kwa sababu Mungu hana hatia. Kuja Kwake duniani kutoka mbinguni kufanya kazi miongoni mwa wanadamu kulikuwa aibu kubwa tayari. Yeye ni mtakatifu bila uchafu hata kidogo. Kuja kwenye nchi ya uchafu—ni fedheha kiasi gani ambayo Amevumilia? Kufanya kazi ndani yenu ni kwa ajili yenu(Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Umuhimu wa Kuukoa Uzao wa Moabu). Kila moja ya maneno ya Mungu liliugonga moyo wangu uliokufa ganzi. Nilifikiria juu ya jinsi nilivyomfuata Mwenyezi Mungu kwa miaka, jinsi ambavyo nilikuwa nimefurahia upendo na ukunjufu usiokuwa na mwisho kutoka kwa Mungu, nikapata riziki nyingi ya Mungu, nikaelewa ukweli ambao hakuna mtu yeyote katika historia aliyeweza kuuelewa, nikagundua maana na thamani ya maisha, na kujiepusha na maisha yangu ya zamani ya giza, maumivu, ukiwa na kukata tamaa. Mungu alikuwa amenipa upendo mkubwa kama huu —ningewezaje kusahau hayo? Ningewezaje kuchanganyikiwa na hata kuwa na mawazo ya kumsaliti Mungu wakati ambapo nilisikia kwamba kuna mtu mwingine aliyekuwa amemsaliti? Nilipofikiria mawazo haya, nililia na kulia, na nilijichukia kwa sababu ya kukosa dhamiri na ubinadamu. Wakati wowote mtu aliponionyesha wema, nilifikiria kila njia inayowezekana kulipa wema huo. Hata hivyo, Mungu alikuwa amenipa neema na baraka nyingi sana, na Alikuwa amenipa wokovu mkubwa sana, na bado dhamiri yangu ilibaki iliyokufa ganzi. Sio tu kwamba wazo la kumlipa Mungu halikunijia akilini, lakini badala yake nilipojikuta katika dhiki kubwa, nilikuwa hata nikifikiria kumsaliti Mungu. Nilikuwa nikiusababishia moyo wa Mungu huzuni nyingi wakati huo! Nilihisi majuto sana kwa sababu ya kuyumbayumba. Kama mtu mwingine alikuwa tu amemsaliti Mungu kwa kweli, basi Mungu angekuwa sasa anahisi kuumiana kuhuzunika sana, na ninapaswa sasa kujaribu kuufariji moyo wa Mungu kwa uaminifu wangu mwenyewe. Lakini nilikuwa mbinafsi sana na aliyestahili kudharauliwa kiasi kwamba sio tu kwamba sikuwa nimesimama upande wa Mungu, lakini pia nilikuwa na wazo la kumsaliti Mungu ili tu niweze kuendeleza maisha ya kusikitisha na ya aibu. Nilikuwa nimejifikiria mwenyewe tu, bila dhamiri yoyote au mantiki yoyote—nilikuwa nikiusababishia moyo wa Mungu huzuni mkuu sana na kumfanya Anichukie sana! Katika kujilaumu na kujuta kwangu, nilimwomba Mungu kimya kimya nikisema: “Ee Mwenyezi Mungu! Ninakosa dhamiri na ubinadamu! Yote ambayo umenipa ni upendo na baraka, lakini yote ambayo nimekupa ni maumivu na uchungu. Ee Mungu! Shukrani kwa mwongozo Wako kwa kuniruhusu nijue la kufanya. Sasa natamani kukuridhisha mara hii moja kwa tendo halisi. Bila kujali jinsi Shetani anavyoweza kunitesa, ni heri nife kuliko kushindwa kuwa shahidi Kwako, na sitawahi kukusailiti!” Polisi mwovu aliona jinsi nilivyokuwa nikilia na akadhani kwamba nilianza kukosa nguvu, kwa hivyo alinijia na akasema kwa upole wa kujisingizia, “Twambie kile tunachotaka kujua na utaweza kurudi nyumbani.” Nilimtazama na kumwambia kwa hasira, “Hakuna vile nitakayomsaliti Mungu daima!” Aliposikia nikisema hivi alikasirika kabisa; alianza kunizaba kofi usoni na kupiga kelele kwa jazba, “Kwa hivyo unapenda vitisho zaidi kuliko hongo, eh? Nilijaribu kukupa suluhisho la heshima kiasi lakini umeipoteza. Unafikiri kuwa hakuna kitu tunachoweza kukufanyia? Usipoanza kushika adabu na kukukiri, tutakufungia gerezani kwa miaka mitano na mtoto wako hataruhusiwa kwenda shuleni.” Nilijibu, “Ikiwa nitakaa gerezani kwa muda wa miaka mitano, basi hilo ni jambo tu ambalo nitalazimika kuvumilia. Unaweza kumzuia mwanangu kuenda shuleni, lakini majaliwa yake yatasalia kuwa majaliwa yake. Nitatii mamlaka ya Mungu.” Kundi lile la ibilisi lilikasirika hata zaidi, na mmoja wao alinishika kwa kola na kunikokota hadi kwenye jukwaa la saruji. Kisha walinifanya niketi sakafuni miguu yangu ikiwa imenyooka. Polisi mmoja alikanyaga mguu wangu mmoja, huku mwingine akishinikiza goti lake kwenye mgongo wangu, akivuta mikono yangu yote miwili kuelekea nyuma kwa ukali. Papo hapo mikono yangu ilipata maumivu yasiyoweza kuvumilika kana kwamba ilikuwa imebanwa yote miwili, na kichwa changu kilielemea upande wa mbele pasipo kutaka na kikagonga jukwaa la saruji na kusababisha uvimbe mkubwa kutokea papo hapo. Ilikuwa katikati ya msimu wa baridi wakati huo, upepo mkali sana ulikuwa ukivuma na kila tone la maji lilibadilika kuwa barafu, na bado polisi hawa waovu walikuwa wakinitesa hadi kufikia mahali ambapo nilikuwa nikitokwa na jasho jingi, likilowesha nguo zangu kabisa. Walipoona kwamba bado sikukubali kushindwa, walirarua koti langu la pedi ya pamba na kunifanya nilale chali kwenye sakafu iliyokuwa baridi sana nikiwa tu nimevalia nguo nyembamba za ndani, na waliendelea kunihoji. Wakati ambapo bado sikujibu maswali yao, walinipiga teke tena. Genge hili la ibilisi lilinitesa hadi kufikia jioni walikuwa wamechoka, lakini bado hawakuwa wamepata chochote kutoka kwangu. Walipokwenda kula mlo wao wa jioni, walinitishia, wakisema, “Ukiendelea kunyamaza usiku wa leo, tutakufungia kwenye benchi la mateso na kukuacha ugande hadi ufe!” Baada ya kusema hayo, waliondoka kwa hasira. Nilianza kuhisi hofu wakati huo huo, na nikajiwazia: “Polisi hawa waovu watanitesa kwa mateso mengine yapi? Nitaweza kuvumilia?” Hasa nilipofikiri juu ya sura zao katili na matukio ya wao kuninitesa, nilihisi mwenye kuhuzunika hata zaidi na asiye jiweza. Niliogopa kwamba singevumilia mateso ya kikatili na kwamba ningemsaliti Mungu, na kwa hivyo niliendelea kumwomba Mungu. Wakati huo, maneno ya Mungu yalinipa ukumbusho: “Kama mtu ana mawazo ya uoga na ya kuogofya, wao wanadanganywa na Shetani. Ina hofu kwamba tutavuka daraja la imani ili kuingia katika Mungu(Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Matamko ya Kristo Mwanzoni, Sura ya 6). Maneno ya Mungu yaliondoa wasiwasi akilini mwangu na nilijua wakati huo kwamba woga wangu ulikuwa kwa sababu Shetani alikuwa amenidanganya, na kwa hivyo nilikuwa nimepoteza imani yangu katika Mungu. Pia niligundua kuwa nilihitaji kupitia hali ya aina hii ili niweze kutulizwa na kuadilishwa, la sivyo singeweza kamwe kukuza imani ya kweli katika Mungu. Aidha, niligundua kuwa sikuwa nikipigana peke yangu kupitia shida hii, lakini kwamba nilikuwa na Mwenyezi Mungu kama msaada wangu thabiti. Kisha nilifikiria kuhusu wakati ambapo Waisraeli walitolewa Misri na walikuwa wakitafutwa na wanajeshi wa Misiri hadi kwenye Bahari ya Shamu. Kufikia wakati huo, hawangeweza kurudi nyuma, na walitii neno la Mungu na kutegemea imani yao kuvuka Bahari ya Sham. Jambo la kushangaza ni kwamba, Mungu aligawanya Bahari ya Shamu na kuibadilisha kuwa nchi kavu; walivuka kwa usalama na waliponyoka hatari, na hivyo kuepuka kufuatiliwa na kuuawa na askari wa Misri. Mimi kukabili mateso ya kikatili ya polisi wa CCP hivi sasa ilikuwa tu sawa na hayo. Mradi nilikuwa na imani na kumtegemea Mungu, hakika ningemshinda Shetani! Na kwa hivyo, nguvu ilirudi moyoni mwangu na sikuhisi tena woga na hofu. Nilimwomba Mungu moyoni mwangu: “Ee Mwenyezi Mungu! Natamani kupambana na Shetani huku nikikutegemea na kamwe nisitishwe tena na mamlaka ya kidikteta ya polisi waovu! Nitakuwa shahidi Kwako!” Wakati huu wa hatari, sio tu kwamba Mwenyezi Mungu alikuwa kama msaada wangu wenye nguvu, lakini pia Alionyesha huruma na upole kwa udhaifu wangu. Polisi hawakuja tena kunihoji jioni hiyo, na nilifikia mwisho wa usiku huo kwa usalama.

Alfajiri iliyofuata, polisi kadhaa wenye mtazamo wa kikatili machoni pao walikuja na kuanza kunitisha, wakisema, “Usiposhirikiana, utaadhibiwa! Tutakupa kionjo cha kifo! Mwenyezi Mungu wako hawezi kukuokoa sasa. Huwezi kulishinda hili hata kama ungekuwa Liu Hulan! Usipoanza kuzungumza, usitarajie kuibuka kutoka katika tatizo hili ukiwa hai.” Kisha walinilazimisha nilivue tena koti langu lililojazwa kwa pamba na kulala kwenye sakafu baridi sana walipokuwa wakinihoji. Nilipomwona kila mmoja wao akinikazia macho, yaliyojawa na uovu, nilichoweza kufanya tu ni kumwomba Mungu na kumsihi anifanye nisimame kidete katika ushuhuda wangu. Walipoona kwamba nilikuwa nimesalia kimya, walighadhibika kwa sababu ya aibu. Mmoja wa polisi alianza kunipiga vibaya kichwani na folda ya faili hadi nikahisi kizunguzungu na woga. Wakati alipokuwa akinipiga aliniita majina machafu na kunitishia, akisema, “Hebu kweli leo tumpe kionjo cha kiunzi cha miti cha kunyongwa. Je, mwanawe huenda shule ipi? Mjulishe mkuu wa shule na umlete mtoto wake hapa. Tutamfanya atamani angekuwa amekufa.” Kisha walinihoji kuhusu vitu walivyopata nyumbani kwangu, lakini kwa sababu hawakuridhishwa na majibu yangu, walianza kuigongesha folda ya faili mdomoni mwangu hadi damu ikachuruzika kutoka pembe za midomo yangu. Kisha walinipiga kikatili kwenye mwili wangu wote, wakikoma tu walipochoka. Wakati huo tu, polisi aliingia chumbani na kuona kwamba sikuwa nimekiri lolote, kisha wanne au watano wao walinijia na kufungua pingu zangu, kisha wakafunga mikono yangu pingu tena mgongoni wangu. Waliniketisha mbele ya dawati kubwa, kichwa changu kikiwa sawa na pembeni mwa dawati na miguu yangu ikiwa imenyooshwa sana. Walipodhani miguu yangu haikuwa imenyooka kiasi cha kutosha, wangeikanyaga na kuyagandamiza mabega yangu. Kwa muda mrefu, walishikilia mikono yangu na pingu zangu juu sana mgongoni mwangu na kunilazimisha nikae bila kusonga hata kidogo katika mkao ambao walikuwa wameniamuru. Ikiwa ningesonga mbele, ningekigongesha kichwa changu kwenye dawati, ikiwa ningesonga kushoto, kulia, au nyuma, ningeadhibiwa vikali. Mbinu hii yao yenye kustahili dharau iliniacha nikiwa katika maumivu makali sana kiasi kwamba nilitamani kufa tu na nilipiga unyende wa kutia hofu tena na tena. Ni wakati tu walipoona kwamba nilikuwa hali mahututi ndipo waliniachilia na kuniruhusu nilale kwa kujinyoosha sakafuni. Baada ya muda mfupi, genge hilo la ibilisi wakatili lilianza kunitesa na kuniumiza tena. Polisi wanne au watano waovu walisimama kwenye miguu na mikono yangu ili nisiweze kusonga, kisha wakashikilia pua yangu na kubana mashavu yangu ili nifungue mdomo wangu huku wakiumimina mtiririko wa maji baridi. Kwa ajili ya kukosa hewa, nilipambana sana, lakini bado hawakuniacha, nilipoteza fahamu polepole. Sijui nilikuwa nimezimia kwa muda gani, lakini ghafla niliamka, nikipaliwa na maji, na nilianza kukohoa kwa nguvu. Maji yalitoka kinywani mwangu, pua yangu na masikio yangu na kifua changu kilikuwa katika maumivu makubwa. Kitu pekee ambacho ningeweza kuhisi ni giza totoro lililonizunguka na nilihisi ni kama macho yangu yalikuwa yakitokeza kwenye mashimo yao. Nilipaliwa sana kiasi kwamba ningeweza tu kutoa pumzi na sio kuvuta pumzi. Macho yangu hayakuona, na nilihisi kana kwamba kifo kingenijia karibuni. Wakati tu maisha yangu yalipokuwa hatarini, ghafla nilishikwa na kikohozi kingine na msukosuko, na niliweza kutema maji kiasi. Nilipata afueni baada ya hapo. Mmoja wa polisi waovu kisha alinivuta kwa nywele hadi nikaketi na kuvuta pingu zangu kwa ukali. Kisha akamwamuru mmoja wa wadogo wake alete kirungu cha umeme cha kushtua ili akitumie kwangu. Kwa mshangao wangu, mdogo huyo aliporudi, alisema, “Niliweza kupata vinne tu. Viwili havifanyi kazi na vingine viwili vinahitaji kuchajiwa.” Aliposikia hivyo, afisa huyo alisema kwa sauti kubwa na kwa hasira, “Wewe ni mjinga sana kiasi kwamba huwezi kufanya kitu chochote! Leta maji ya pilipili!” Nilimwomba Mungu moyoni mwangu bila kukoma, nikimwomba Anilinde ili niweze kushinda mateso hayo yote ya kikatili niliyoteswa na polisi hao waovu. Wakati huo huo, kitu kisichotarajiwa kilitokea: Mmoja wa polisi kwa kweli alisema, “Hayo ni zaidi ya anayoweza kuvumilia. Tayari tumemtesa vibaya. Usifanye hivyo tena.” Polisi huyu aliposikia hivyo, alichoweza kufanya tu ni kupunguza hasira. Wakati huo nilitambua kwa kweli mamlaka na utawala wa Mungu juu ya vitu vyote, kwani ni Mungu aliyekuwa akinilinda na kunipa achilio la muda. Hata hivyo, polisi hawa waovu hawakuwa tayari kuniachilia bado. Walitia mikono yangu pingu mgongoni mwangu tena, wakasimama kwenye miguu yangu na kuivuta juu kwa nguvu zao zote mikono yangu iliyofungwa pingu. Nilichoweza kuhisi tu ni maumivu yasiyoweza kuvumilika kana kwamba mikono yangu ilikuwa ikivunjika, na nilipiga mayowe bila kukoma. Moyoni mwangu, niliendelea kumwomba Mwenyezi Mungu, na bila kujua nilisema, “Mwenye...” Lakini kisha mara moja nikapunguza sauti yangu na kusema, “Ninachojua ... nitakuambia yote ninayoyajua.” Genge hilo lilidhani kuwa nilitaka kuwaeleza kila kitu, na kwa hivyo waliniachilia na kusema kwa sauti kubwa, “Sisi sote ni wapelelezi mahiri wa kesi. Usithubutu hata kufikiria kutudanganya. Usipofanya vizuri na utueleze kila kitu sasa, usitarajie kuishi kwa muda mrefu zaidi au kuwahi kuondoka mahali hapa. Tutakupa muda kiasi wa kufikiria jambo hilo!” Niliteseka sana nilipokabiliwa na mateso na vitisho vyao, na nilijiwazia: “Sitaki kufia hapa, lakini sitaki kabisa kumsaliti Mungu wala kulisaliti kanisa. Nifanye nini? Je, itakuwaje nikiwaeleza kuhusu ndugu mmoja tu?” Lakini ghafla nikagundua kuwa singeweza kamwe kufanya hivi, na kwamba kuwaambia chochote kutakuwa kumsaliti Mungu, na kungenifanya niwe Yuda. Katika maumivu yangu, nilimwomba Mungu: “Ee Mungu! Nifanye nini? Tafadhali nipe nuru na uniongoze, na tafadhali nipe nguvu!” Baada ya kuomba nilifikiria maneno ya Mungu ambayo yanasema, “Kanisa ni moyo Wangu.” “Lazima mtoe kila kitu kulinda ushuhuda Wangu. Hili litakuwa lengo la matendo yenu, usisahau jambo hili(Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Matamko ya Kristo Mwanzoni, Sura ya 41). “Ndio,” niliwaza. “Kanisa ni moyo wa Mungu. Kumsaliti ndugu kutakuwa kuleta machafuko kanisani, na hicho ndicho kinachomsikitisha Mungu zaidi. Sharti nisifanye chochote kuliumiza kanisa. Mungu alikuja duniani kutoka mbinguni kufanya kazi ili atuokoe, na Shetani hulenga macho yake yenye tamaa kwetu sisi tulioteuliwa na Mungu, akitumai bila mafanikio kutushika sisi sote kwa njia moja na kuliangamiza kanisa la Mungu. Nikiwasaliti ndugu zangu, si nitakuwa nikiruhusu njama za Shetani zenye kudhuru kwa siri zifanikiwe? Mungu ni mzuri sana na kila kitu anachomfanyia mwanadamu Yeye hukifanya kwa ajili ya upendo. Sharti nisiusononeshe moyo wa Mungu. Siwezi kumfanyia Mungu chochote leo, kwa hivyo ninaomba tu niweze kuwa shahidi ili kulipa upendo wa Mungu—hiki ndicho kitu pekee ninachoweza kufanya.” Mara tu nilipofahamu mapenzi ya Mungu, nilimwomba Mungu: “Ee Mungu! Sijui ni mateso ya aina gani ambayo bado wameniandalia. Unajua kuwa mimi ni mtu wa kimo kidogo na kwamba mara nyingi nahisi woga na hofu. Lakini ninaamini ya kwamba Unashikilia kila kitu mikononi Mwako, na ningependa kuahidi mbele Yako kuwa shahidi Kwako, hata nikipoteza maisha yangu mwenyewe.” Wakati huo huo, mmoja wa polisi waovu alinifokea kwa hasira, “Umefikiria jambo hilo? Ikiwa hutakuwa na tabia na kutueleza kila kitu basi nitahakikisha utakufia hapa leo hii! Hata Mwenyezi Mungu hawezi kukuokoa!” Nilifumba macho yangu kabisa na, huku nikishikilia azimio langu la kuwa shahidi hata nikipoteza maisha yangu, sikusema neno. Polisi walikereza meno kwa hasira, wakanivamia, wakinidhalilisha na kunitesa bila kukoma kama walivyofanya hapo awali, kwa kunikanyaga na kunipiga. Walinipiga kikatili hadi nikapatwa na kizunguzungu. Sikuona chochote na kichwa changu kilihisi ni kama kimepasuka. Polepole nilianza kuhisi kuwa siwezi kusogeza macho yangu, mwili wangu hukuhisi maumivu, na singeweza kusikia chochote vizuri. Nilichoweza tu kutambua ni sauti zao ambazo zilionekana kuwa za kutoka mbali sana. Hata hivyo, ufahamu wangu ulikuwa mzuri mno, na niliendelea kurudia maneno haya kimya kimya: “Mimi si Yuda. Nitakufa kabla sijakuwa Yuda….” Sijui ni muda gani ulipita, lakini nilipoamka, niliona kuwa nilikuwa nimelowa maji, na polisi waovu wanne au watano walikuwa wakichutama kandokando yangu, kana kwamba walikuwa wakiangalia kama nilikuwa hai au nimekufa. Nilipolitazama genge hili la maafisa ambao hawakuwa bora kuliko wanyama, nilihisi hasira kubwa ikiibuka ndani yangu: Hawa ndio “Polisi wa Umma” ambao “waliwapenda watu kama watoto wao wenyewe”? Je, hawa ndio watekelezaji wa sheria ambao “walitetea haki, kuwaadhibu waovu na kusaidia wema”? Wote walikuwa pepo tu na madubwana ya kuzimu! Wakati huo, nilikumbuka kifungu kutoka katika Mahubiri na Ushirika: “Joka kubwa jekundu humpinga na kumshambulia Mungu kikatili sana na kwa hasira, na linawaumiza watu wa Mungu kwa udhalimu na vibaya sana—mambo haya ni ukweli. Joka kubwa jekundu huwatesa na kuwashurutisha watu wa Mungu wateule, na kusudi lake la kufanya hivyo ni nini? Linatamani kumaliza kabisa kazi ya Mungu ya siku za mwisho na kukomesha kurudi kwa Mungu. Huo ni uovu wa joka kubwa jekundu, na ni njama ya hila ya Shetani” (“Jinsi ya Kujua na Kutofautisha Asili na Sumu za Joka Kubwa Jekundu” katika Mahubiri na Ushirika Kuhusu Kuingia Katika Maisha III). Nilipoangalia ukweli ulionizunguka kwa kuzungatia maneno haya, niliona waziwazi kabisa kwamba serikali ya CCP ni mfano halisi wa Shetani na kwamba ni yule mwovu ambaye amempinga Mungu tangu mwanzo. Ni kwa sababu ibilisi Shetani pekee ndiye anayechukia ukweli na kuogopa nuru ya kweli, na anatamani kufutilia mbali ujio wa Mungu wa kweli, kwa sababu ni yeye tu anayeweza kuwaumiza kikatili na kuwatesa kinyama sana wale wanaomfuata Mungu na wanaotembea katika njia inayofaa. Mungu sasa amepata mwili na amekuja kufanya kazi ndani ya pango lake, na Alipanga hali kama hiyo nipitie ili mimi, licha ya kudanganywa sana nalo, niweze kugundua kuwa ni ibilisi Shetani anayewadhuru na kuwaangamiza watu, kwamba kuna nuru inayozidi utawala wake mwovu, na kwamba kuna Mungu wa kweli anayetulinda na kutukimu usiku na mchana. Ujio wa Mwenyezi Mungu umeniletea ukweli na mwanga, na umeniruhusu mwishowe nione uso wa shetani wa serikali ya CCP ambayo huringa kila siku kuwa “kubwa, ya heshima na haki,” hivyo kuamsha chuki kali dhidi ya serikali ya CCP ndani yangu. Ujio Wake pia umeniwezesha kutambua maana na thamani ya kufuatilia ukweli, na kuona njia ya nuru maishani. Kadiri nilivyozidi kutafakari kulihusu ndivyo nilivyozidi kuelewa jambo hili, na nilihisi nguvu ikiongezeka ndani yangu, ikinisaidia kukabiliana na mateso katili ya maafisa. Maumivu yangu ya mwili pia yalipungua, na nilijua moyoni kwamba Mungu ndiye aliyekuwa akinilinda na kunisaidia kushinda majaribio ya polisi ya kunitesa ili nikiri.

Mwishowe, polisi waliona kwamba hawangeweza kupata chochote kutoka kwangu, kwa hivyo walinishtaki kwa kosa la “kuvuruga usalama wa umma” na kunisindikiza hadi kizuizini. Serikali ya CCP huwashurutisha wafungwa kufanya kazi kama mashine katika sehemu hizo, ikiwalazimisha kufanya kazi bila kukoma siku nzima. Sikuweza hata kupata usingizi mdogo wa saa tano kila usiku, na kila siku nilichoka sana kiasi kwamba nilihisi ni kama mwili wangu wote ulikuwa ukivurugikiwa. Licha na haya, maafisa wa jela hawakuniruhusu kamwe nile hadi nishibe. Kwa kila mlo nilipewa tu maandazi mabili madogo yaliyopikwa kwa mvuke na mboga chache zisizo na hata tone la mafuta. Wakati ambao nilikuwa nimezuiliwa huko, polisi waovu walikuja kunihoji mara nyingi. Mara ya mwisho waliponihoji, walisema watanihukumu miaka miwili ya marekebisho kupitia kazi. Kwa ujasiri, niliwauliza, “Je, si sheria ya nchi imeruhusu uhuru wa dini? Kwa nini wanihukumu miaka miwili ya marekebisho kupitia kazi? Mimi ni mgonjwa. Ikiwa nitakufa, watoto na wazazi wazazi wangu watafanya nini? Pasi na mtu wa kuwatunza, wataona njaa.” Polisi mmoja katika miaka yake ya hamsini alisema kwa ukali, “Utahukumiwa kwa sababu umevunja sheria ya nchi, na ushahidi haukanushiki!” Nilijibu vikali, “Kumwamini Mungu ni jambo zuri. Siui, sichomi kwa makusudi, sifanyi chochote kibaya. Najitahidi tu kuwa mtu mzuri. Kwa hivyo kwa nini hamniruhusu niwe na imani yangu?” Walighadhibika kwa ajili ya aibu kutokana na jibu langu, na mmoja wao alinijia na kunizaba kofi, na kuniangusha sakafuni. Kisha walinilazimisha kulala nikiwa nimenyooka. Mmoja wao aligandamiza mabega yangu wakati mwingine alikuwa akigandamiza miguu yangu. Bado mwingine alinikanyaga kwa nguvu usoni mwangu kwa viatu vyake vya ngozi, na kusema bila aibu, “Imetokea kwa nasibu kwamba kuna soko leo. Tutakuvua nguo zote na kukutembeza kote sokoni!” Baada ya kusema hayo, aliikanyaga kwa nguvu sehemu ya chini ya mwili wangu na kwenye kifua changu. Alisimama juu ya kifua changu kwa mguu mmoja na kuuinua mguu huo mwingine kwa nguvu, na kisha akafanya hivyo tena na tena, wakati mwingine akikanyaga mapaja yangu. Suruali yangu ilikuwa imeraruka kutokana na kukanyagwa na pachipachi liliraruka vile vile. Nilifedheheshwa kiasi kwamba machozi yalibubujika bila kukoma kutoka machoni mwangu, na nilihisi kama nitavurugika kabisa. Singeweza tu kuvumilia kufedheheshwa na ibilisi hao kwa njia hii. Nilihisi kuwa ilikuwa vigumu sana kuishi hivyo, na kwamba afadhali kufa. Wakati tu nilipokuwa nikihisi uchungu huu mbaya, nilikumbuka maneno ya Mungu ambayo yanasema: “Wakati umewadia wa sisi kulipa upendo wa Mungu. Ingawa tutapata mara kwa mara dhihaka, kashfa, na mateso mengi sana kwa sababu tunafuata njia ya imani katika Mungu, Naamini hili ni jambo la maana. Ni jambo la utukufu, sio aibu, na lolote litokealo, baraka tunazofurahia si hafifu kamwe(Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Njia … (2)). “Wamebarikiwa wale wanaoteswa kwa sababu ya haki(Mathayo 5:10). Maneno ya Mungu yalichangamsha kumbukumbu yangu mara moja. “Ndiyo,” niliwaza. “Mateso na fedheha ambayo ninapata leo ni ya maana na dhamana kubwa sana. Ninapitia haya kwa sababu ninamwamini Mungu na kutembea kwa njia inayofaa, na yanapitiwa kwa ajili ya kupata ukweli na kupata uzima. Mateso haya sio ya aibu, lakini badala yake ni baraka kutoka kwa Mungu. Ni kwamba tu sielewi mapenzi ya Mungu, na ninapopata mateso haya na fedheha hii, ninataka kufa ili niyakomeshe, na siwezi kuona upendo wa Mungu au baraka Zake hata kidogo. Je, ningewezaje kukosa kumsikitisha Mungu?” Nilipofikiria mambo haya, nilihisi mwenye deni kwa Mungu, na nilifanya uamuzi kimoyomoyo: “Bila kujali ibilisi hawa watanidhalilisha na kunitesa namna gani, sitawahi kumsujudia Shetani. Hata kama nitakuwa katika kipindi cha mwisho kabla ya kufa, bado nitatumia wakati huo vizuri na kuwa shahidi kwa Mungu, na sitautamausha moyo Mungu hata kidogo.” Baada ya kunitesa kwa muda wa siku mbili usiku na mchana, bado hawakupata taarifa yoyote kutoka kwangu, na kwa hivyo walinipeleka kwenye kituo cha uzuiliaji cha manispaa.

Huko kizuizini, niliwaza kuhusu kila kitu nilichopitia katika siku chache zilizopita na, polepole, nilielewa kwamba kupitia mateso na shida kama hizo kulikuwa upendo mkubwa na wokovu wa Mungu kwangu. Mungu alitaka kutumia hali hii kuimarisha nia yangu na azimio langu la kuteseka na kuingiza imani ya kweli na upendo ndani yangu ili niweze kujifunza kuwa mtiifu katika matatizo mabaya hivi na kuweza kuwa shahidi Kwake. Katika upendo wa Mungu, nilikumbuka jinsi nilivyokuwa nimekuwa dhaifu na mwasi tena na tena wakati ambapo nilikuwa nikiteswa kikatili, na kwa hivyo nilikuja mbele za Mungu katika toba kubwa: “Ee Mwenyezi Mungu! Mimi ni kipofu na mjinga. Sikufahamu upendo Wako na baraka Zako, ila siku zote nilidhani kwamba mateso ya mwili ni jambo baya. Sasa ninaona kuwa kila kitu kinachonitokea sasa ni baraka Zako. Ijapokuwa baraka hii inakinzana na fikra zangu mwenyewe, na inaweza kuonekana kana kwamba mwili wangu unateseka na kufedheheshwa, kwa ukweli hii ni Wewe unanipa hazina ya thamani zaidi ya maisha kwangu, ni ushuhuda wa ushindi Wako dhidi ya Shetani, na zaidi, ni Wewe unanionyeshea upendo wa kweli na halisi zaidi. Ee Mungu! Sina chochote cha kukulipa kwa ajili ya upendo na wokovu Wako. Ninachoweza tu kukifanya ni kukupa moyo wangu na kupitia mateso haya na fedheha ili kuwa shahidi Kwako!”

Kilichojiri bila kutarajiwa ni kwamba, wakati tu nilipokuwa nimejiandaa kwenda gerezani na kuazimia kumridhisha Mungu, Mungu alinifungulia njia. Siku yangu ya 13 kizuizini, Mungu alimwinua shemeji yangu kuwaalika polisi matembezini na kuwapa zawadi kadhaa, zikimgharimu yuani 3,000. Pia aliwakabidhi polisi yuani 5,000 ili waniachilie kwa dhamana nikisubiri kesi. Nilipofika nyumbani, niligundua kuwa nyama kwenye miguu yangu ilikuwa na seli zilizokufa kutokana na jinsi ambavyo polisi waovu walikuwa wamenikanyaga sana. Ilikuwa imekuwa ngumu na nyeusi na ilinichukua muda wa miezi mitatu kupona. Mateso hayo niliyotendewa na polisi pia yalisababisha madhara makubwa kwenye ubongo na moyo wangu, na nimeachwa nikiwa na madhara. Bado ninavumilia mateso ya maumivu haya hadi leo. Isingekuwa ulinzi wa Mungu, labda ningekuwa nimepooza na mgonjwa kitandani, na ukweli kwamba sasa ninaweza kuishi maisha ya kawaida kikamilifu ni kwa ajili ya upendo mkubwa na ulinzi wa Mungu.

Baada ya kupitia mateso na shida hii, kwa kweli nilikuja kufahamu asili ya kumwasi Mungu na ya shetani ya serikali ya CCP. Pia nilikuja kufahamu waziwazi kuwa ni yule muovu na adui wa Mungu asiyeweza kupatanishwa. Ninayo chuki ya milele kwake moyoni mwangu. Wakati huo huo, pia nilikuja kupata ufahamu wa kina wa upendo wa Mungu kuliko nilivyokuwa hapo awali, na nilikuja kufahamu kwamba kazi zote ambazo Mungu hufanya kwa watu zinafanywa ili kuwaokoa na zinafanywa kutokana na wao kupendwa. Sio tu kwamba Mungu anaonyesha upendo Wake kwetu kupitia neema na baraka lakini, hata zaidi, Anaonyesha kupitia mateso na shida. Kuweza kusimama kidete kupitia mateso ya kikatili na matusi ambayo polisi walinilimbikizia, na kuweza kutoka katika tundu la pepo, nilikuja kutambua vyema ukweli kwamba haya yalifanyika ili maneno ya Mwenyezi Mungu yanipe imani na nguvu. Hata zaidi, ilikuwa kwa sababu nilitiwa moyo na upendo wa Mwenyezi Mungu, ambao uliniwezesha kumshinda Shetani polepole na kuwa huru kutoka kwa pango la pepo. Shukrani ziwe kwa Mungu kwa kunipenda na kuniokoa, na sifa na utukufu wote uwe kwa Mwenyezi Mungu!

Tanbihi:

a. Mtu/kitu kinachodhihirisha uzuri/ubora wa kingine kwa kuvilinganisha.

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Maudhui Yanayohusiana

Ujana Usio na Majuto Yoyote

Xiaowen Jijini Chongqing“‘Upendo,’ kama unavyoitwa, unaashiria hisia safi isiyo na dosari, ambapo unatumia moyo wako kupenda, kuhisi,...

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp