Imani Isiyoweza Kuvujika

26/01/2021

Meng Yong, China

Mimi kwa asili ni mtu mwaminifu, ikiwa ndiyo maana nimekuwa nikidhulumiwa daima na watu wengine. Kwa sababu hiyo, nimeonja dharau ya ulimwengu wa mwanadamu na nilihisi maisha yangu yakiwa matupu na bila maana. Baada ya mimi kuanza kumwamini Mwenyezi Mungu, kupitia kusoma maneno ya Mungu na kuishi maisha ya kanisa, nilifurahia ari na shangwe katika moyo wangu ambazo sikuwahi kamwe kuzihisi kabla. Kuona ndugu wa kiume na wa kike wa Kanisa la Mwenyezi Mungu wakipendana wenyewe kwa wenyewe kama familia kulinifanya nitambue kwamba Mungu peke yake ndiye mwenye haki, na kwamba ni katika Kanisa la Mwenyezi Mungu tu kuliko na mwanga. Kupitia miaka kadhaa ya kupata binafsi uzoefu wa kazi ya Mwenyezi Mungu, nimekuja kufahamu kwa kweli kwamba maneno ya Mwenyezi Mungu yanaweza kuwabadilisha watu na kuwaokoa watu. Mwenyezi Mungu ni upendo, na ni wokovu. Ili watu wengi waweze kufurahia upendo wa Mungu na kupokea wokovu wa Mungu, ndugu zangu wa kiume na wa kike na mimi wote tulijitahidi kadri tulivyoweza kueneza injili, lakini hatukutazamia kukamatwa na kuteswa na Chama cha Kikomunisti.

Mnamo Desemba mwaka wa 2012, ndugu kadhaa wa kiume na wa kike nami tulifululiza kwa gari hadi mahali fulani ili kueneza injili, na tukaishia kuripotiwa na watu waovu. Muda mfupi baadaye, serikali ya wilaya iliwaagiza maafisa kutoka idara mbalimbali za kutekeleza sheria, kama vile kikosi cha kupambana na uovu, vikosi vya usalama wa kitaifa, kikosi cha kupambana na madawa ya kulevya, vikosi vya polisi wa silaha, na idara ya polisi ya mahali palepale, kuja hapo kwa magari zaidi ya 10ya polisi kutukamata. Wakati ndugu mmoja na mimi tulipokuwa tukiandaa kuondoka kwa gari, tuliona polisi saba au wanane wakitumia virungu kumpiga ndugu mwingine kwa ghadhabu. Wakati huo, maafisa wanne wa polisi walikimbia haraka na kulizuia gari letu. Mmoja wale maafisa waovu akachomoa vifunguo vya gari bila maelezo yoyote, na kutuamuru tuekae ndani ya gari bila kutoka. Wakati huo, niliona kuwa yule ndugu alikuwa tayari amepigwa kiasi kwamba alikuwa ameketi sakafuni, bila kusogea. Sikuweza kujizuia kujaa hasira za kudhulumiwa na kukimbia nje ya gari ili kuzuia vurugu yao, lakini wana polisi alinizuia Baadaye, walitupeleka kwa kituo cha polisi, na gari letu pia lilizuiliwa.

Baada ya saa tatu usiku huo, maafisa wawili wa polisi walikuja kunihoji. Walipoona kwamba hawakuweza kupata taarifa yoyote muhimu kutoka kwangu, walishikwa na wasiwasi na kughadhabika, walisaga meno yao kwa hasira wakiapiza: “Potelea mbali, tutakushughulikia baadaye!” Kisha wakanifungia katika chumba cha kusubiri. Saa tano u nusu usiku, maofisa wawili walinipeleka katika chumba kisichokuwa na kamera za upelelezi. Nilihisi kuwa wangetumia nguvu dhidi yangu, hivyo nikaanza kumwomba Mungu mara kwa mara moyoni mwangu, nikimwomba Mungu kunilinda. Wakati huu, afisa mmoja mwovu wa polisi aliyeitwa Jia kwa jina la ukoo alinijia kunihoji: “Je, umekuwa katika gari la Volkswagen Jetta katika siku kadhaa zilizopita?” Nikajibu hapana, na akapiga ukelele kwa ghadhabu: “Watu wengine tayari wamekuona, na bado unalikana?” Baada ya kusema hivyo, alinipiga kofi kwa ukali kwa uso. Yote niliyohisi yalikuwa ni maumivu makali kwa shavu langu. Kisha akanguruma kwa sauti kubwa: “Hebu tuone jinsi ulivyo mjeuri!” Alichukua ukanda mpana hali akiongea na kunichapa nao kwa uso wangu, sijui ni mara ngapi nilichapwa, lakini sikuweza kujizuia kupiga kelele kwa maumivu mara kwa mara. Walipoona jambo hili, waliuvuta ukanda kuziba kinywa changu. Maafisa wachache waovu wakati huo wakaufunika mwili wangu kwa blanketi kabla ya kunipiga kwa ghadhabu na virungu vyao, wakiacha tu walipochoka mno ili kupumua. Nilikuwa nimepigwa vibaya sana kiasi kwamba kichwa changu kilikuwa kikizunguka na mwili wangu uliumia kana kwamba kila mfupa ulikuwa umetawanywa. Wakati huo sikujua ni kwa nini walikuwa wakinitendea jinsi hii, lakini baadaye niligundua kwamba walinifunika kwa blanketi ili kuzuia pigo hilo kuacha alama mwilini mwangu. Kuniweka ndani ya chumba bila upelelezi, kukitia kinywa changu kifaa cha kuninyamazisha, na kunifunika kwa blanketi—yote ni kwa sababu waliogopa kwamba matendo yao maovu yangefichuka. Sikuwahi kufikiria kamwe kwamba “polisi wa watu” wenye heshima wangeweza kuwa wadanganyifu sana na waovu! Wale wanne walipochoka kutokana na kunipiga, walibadilisha utaratibu wa kunitesa: Maofisa wawili wa waovu waliupinda mkono mmoja wangu na kuuvuta juu kwa nguvu, wakati maafisa wengine wawili waovu waliuinua ule mkono wangu mwingine juu ya bega kwa nyuma na kuuvuta chini kwa nguvu. Lakini mikono yangu miwili haikuweza kuvutwa pamoja kwa vyovyote, kwa hiyo walidunga goti la nguvu kwa mkono wangu. Yote niliyosikia ilikuwa ni “klik,” na mikono yangu miwili ikahisi kama imeambuliwa. Liliumiza sana kiasi kwamba nilikaribia kufa. Waliita aina hii ya mateso “Kubeba Upanga Mgongoni,” ambayo watu wa kawaida hawangeweza kuvumilia kabisa. Haikunichukua muda mrefu kupoteza hisia katika mikono yangu yote miwili. Hili bado halikutosha kwao kuacha, kwa hiyo waliniamuru nipige magoti ili kuongeza maumivu yangu. Nilikuwa na maumivu mengi kiasi kwamba mwili wangu wote ulikuwa katika hali ya woga na wasiwasi, kichwa changu kilikuwa kinavuma, na fahamu zangu zilianza kuwa na kiwi kidogo. Niliwaza: Kwa miaka hiyo yote maishani mwangu sijawahi kuwa na hisia ya kutoweza kudhibiti fahamu zangu mwenyewe. Je, niko karibu kufa? Baadaye, kweli sikuweza kuvumilia tena, hivyo nilifikiria kutafuta faraja kwa njia ya kifo. Wakati huo, neno la Mungu lilinipa nuru kutoka ndani: “Leo, watu wengi sana hawana ufahamu huo. Wao huamini kwamba mateso hayana thamani…. Kuteseka kwa watu wengine hufikia kiwango fulani, na fikira zao hugeukia kifo. Huu si upendo wa kweli kwa Mungu; watu kama hao ni waoga, hawana ustahamilivu, wao ni wadhaifu na wasio na nguvu!(Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Ni kwa Kupitia tu Majaribio ya Kuumiza Ndiyo Mnaweza Kujua Kupendeza kwa Mungu). Maneno ya Mungu kwa ghafla yanifanya kuchangamka na kutambua kuwa njia yangu ya kufikiri haikulingana na nia za Mungu na ingeweza tu kumfanya Mungu ahuzunike na kusikitika. Kwa sababu katikati ya maumivu haya na mateso, kile ambacho Mungu anataka kuona siyo mimi kutafuta kifo, lakini kwamba ninaweza kuutegemea mwongozo wa Mungu kupambana na Shetani, kumshuhudia Mungu, na kumfanya Shetani aaibike na kushindwa. Kutafuta kifo kungekua kuanguka ndani ya mpango wa Shetani, kumaanisha nisingeweza kushuhudia na badala yake ningekuwa mfano wa aibu. Baada ya kuelewa nia za Mungu, nikamwomba Mungu kimya kimya: Ee Mungu! Uhalisi umeonyesha kuwa asili yangu ni dhaifu mno. Sina hiari na ujasiri wa kuteswa kwa ajili Yako na nilitaka kufa kwa sababu tu ya maumivu kidogo ya kimwili. Sasa kuepa na ni lazima niwe shahidi na kukuridhisha Wewe bila kujali ni shida gani ninayostahiki. Lakini wakati huu, mwili wangu wa kimwili una maumivu makubwa mno na ni dhaifu, na ninajua kuwa ni vigumu sana kushinda mapigo ya pepo hawa peke yangu. Tafadhali nipe ujasiri na nguvu zaidi ili niweze kukutegemea Wewe kumshinda Shetani. Naapa kwa maisha yangu kwamba sitakusaliti au kuwasaliti ndugu zangu wa kiume na wa kike. Nilipomwomba Mungu mara kwa mara, moyo wangu polepole ukawa mtulivu. Wale polisi waovu wakaona kwamba nilikuwa napumua kwa shida na waliogopa kwamba wangelazimika kuwajibika kama ningekufa, kwa hiyo walikuja kuzifungua pingu zangu. Lakini mikono yangu ilikuwa tayari imekauka, na pingu zilikuwa zimejikaza sana hivi kwamba zilikuwa ngumu sana kufungua. Ikiwa wangetumia nguvu zaidi mikono yangu ingevunjika. Wale polisi waovu wanne walichukua dakika kadhaa kufungua pingu kabla ya kuniburuta na kunirudisha kwa chumba cha kusubiri kuhojiwa.

Alasiri iliyofuata, wale polisi walinisingizia “kosa la jinai” kunirudisha kwa nyumba yangu ili kuivamia, na kisha wakanipeleka kwa kituo cha kizuizi. Mara tu nilipoingia kituo cha kizuizi, maafisa wanne wa magereza wakaninyang’anya jaketi langu la pamba, suruali, viatu, na saa, ikiwa ni pamoja na yuan1,300 taslimu nilizokuwa nimebeba. Wanilazimisha nivae sare ya gerezani ya kawaida na kunilazimisha kutumia yuan 200 kununulia blanketi kutoka kwao. Baadaye, hao maafisa wa magereza walinifungia pamoja na wanyang’anyi wenye silaha, wauaji, wabakanaji, na walanguzi wa madawa ya kulevya. Nilipoingia katika seli yangu, nikaona wafungwa kumi na wawili wenye vipara wakiniangalia kwa chuki. Mazingira yalikuwa mazito na ya kuogofya, na nikahisi wasiwasi kwa ghafla. Wawili wa viongozi wa seli wakanijia na kuniuliza: “Je, uko hapa kwa nini?” Nikasema: “Kueneza injili.” Bila neno jingine, mmoja wao akanichapa kofi kwa uso mara mbili, na kusema: “Wewe ni ‘Askofu,’ sivyo?” Wafungwa wengine wote wakaanza kucheka kishenzi na kunitania kwa kuuliza: “Kwa nini usimruhusu Mungu wako akuokoe kutoka hapa?” Katikati ya kuzomewa na kudhihakiwa, kiongozi wa seli akanichapa kofi kwa uso mara chache zaidi. Kutoka wakati huo kwendelea, wakanipa jina la utani “Askofu” na mara nyingi walinifedhehesha na kunidhihaki. Kiongozi mwingine wa seli akaona sapatu nilizokuwa nimevaa na akapiga ukelele kwa kujigamba: “Hujui thamani yako kabisa. Je, unastahili kuvaa viatu hivi? Vivue!” Alipokuwa akilisema, alinilazimisha kuvivua na kuvaa jozi ya sapatu zao kuukuu. Pia walipeana blanketi yangu kwa wafungwa wengine kutumia. Wale wafungwa walipigania blanketi yangu kwa fujo, na hatimaye nilisalia na blanketi kuukuu ambayo ilikuwa nyembamba, iliyopasuka, chafu, na yenye kunuka. Wakichochewa na hao maafisa wa magereza, wafungwa hawa walinipa shida za aina zote na mateso. Taa iliwaka daima katika seli usiku, lakini kiongozi mmoja wa seli kwa ghafula akaniambia kwa tabasamu la uovu: “Nizimie hiyo taa.” Kawa kuwa sikuweza kufanya hivyo (hata hakukuwa na swichi), walianza kunicheka na kunidhihaki tena. Siku iliyofuata, wafungwa vijana wachache walinilazimisha kusimama kwa kona moja na kukariri amri za gerezani, wakitishia: “Utakiona cha mtema kuni kama hutazikariri kwa siku mbili.” Sikuweza kujizuia kutishika, na nilivyozidi kufikiria yale niliyoyapitia siku chache zilizopita, ndivyo nilivyozidi kuogopa. Kwa hiyo, niliendelea kumwita Mungu nikimwomba anilinde ili niweze kulishinda jambo hili. Wakati huu, nilikufikiria wimbo wa maneno ya Mungu: “Majaribio yanapokuja, bado unaweza kumpenda Mungu; iwe unakabiliwa na kifungo, ugonjwa, dhihaka, au kashfa kutoka kwa wengine, au inaonekana huna suluhu, bado unaweza kumpenda Mungu. Hii inamaanisha kwamba moyo wako umemgeukia Mungu(“Moyo Wako Umemgeukia Mungu?” katika Mfuateni Mwanakondoo na Kuimba Nyimbo Mpya). Neno la Mungu lilinipa nguvu na kunionyesha njia kwangu kuitenda—kutafuta kumpenda Mungu na kutoa moyo wangu kwa Mungu! Katika wakati huo, ghafla ikawa dhahiri kabisa moyoni mwangu: Kwa Mungu kuruhusu mateso haya kunifika hakukuwa ni kunitia uchungu au kwa makusudi kunifanya kuteseka, lakini kunifundisha kuugeuza moyo wangu kwa Mungu katika mazingira kama hayo, ili niweze kuupinga udhibiti wa mvuto wa giza wa Shetani na hivyo moyo wangu bado unaweza kuwa karibu na Mungu na kumpenda Mungu, kamwe kutolalamika na daima kutii mipango na matayarisho ya Mungu. Nikiwa na hili katika akili yangu, sikuogopa tena. Bila kujali ni jinsi gani polisi na wafungwa watanitendea yote nitakayoshughulikia ni kuhusu kuipa nafsi yangu kwa Mungu sitaweza kujitoa kwa shetani.

Maisha gerezani kwa kweli ni ya. kuzimu duniani. Walinzi wa gerezani waliendelea kuja na njia za kuwatesa watu: Nilibanwa katikati ya wafungwa wengine kadhaa wakati wa kulala usiku. Hata kugeuka kitandani kulikuwa kugumu. Kwa kuwa nilikuwa wa mwisho kufika, hata nililazimika kulala karibu na choo. Baada ya kukamatwa, sikulala kwa siku kadhaa na nikawa mwenye usingizi kiasi kwamba sikuweza kuvumilia na ningesinzia. Wafungwa waliokuwa kwenye zamu ambao walikuwa wakilinda wangekuja kunibughudhi, kwa makusudi wakinipiga kidogo kichwani mpaka ningeamka kabla wao wangeondoka. Kuna mfungwa ambaye kimakusudi aliniamsha na kujaribu kuchukua chupi yangu ndefu. Baada ya kifungua kinywa, mkuu wa seli alifanya nisugue sakafu kila siku. Hizi ndizo zilizokuwa siku za baridi sana za mwaka na hakukuwa na maji moto, hivyo niliweza kutumia maji baridi tu kwa kitambaa cha kusafisha. Mkuu wa seli pia aliniamuru nisugue jinsi hii kila siku. Kisha, wanyang’anyi kadhaa wenye silaha walinilazimisha kukariri amri za gerezani. Kama sikuweza kuzikariri, wangenipiga ngumi na mateke; kupigwa makofi kwa uso kulikuwa hata kwa kawaida zaidi. Kukabiliana na mazingira kama hayo, nilijihisi mnyonge sana. Usiku, nilivuta blanketi yangu juu ya kichwa changu na kuomba kimya kimya: Ee Mungu, Uliyaruhusu mazingira haya kunifika, hivyo nia Zako njema zinapaswa kuwa ndani ya mazingira haya. Tafadhali nifichulie nia Zako. Wakati huo, maneno ya Mungu yalinipa nuru: “Mimi hustaajabia mayungiyungi yanayochanuka vilimani. Maua na nyasi zinanyooka toka upande mmoja hadi upande mwingine wa miteremko, lakini mayungiyungi yanaongeza mng’aro kwa utukufu Wangu duniani kabla ya kufika kwa majira ya kuchipua—je, mwanadamu anaweza kutimiza kiasi hiki? Je, angeweza kunishuhudia duniani kabla ya kurudi Kwangu? Je, angeweza kujitolea kwa ajili ya jina Langu katika nchi ya joka kubwa jekundu?(Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Maneno ya Mungu kwa Ulimwengu Mzima, Sura ya 34). Ndio, maua na nyasi na mimi vyote ni viumbe vya Mungu. Mungu alituumba ili tumdhihirishe Yeye, kumtukuza Yeye. Maua yanaweza kuongeza mng’aro kwa utukufu wa Mungu duniani kabla ya majira ya kuchipua kufika, kumaanisha yametimiza jukumu lake kama kiumbe cha Mungu. Kazi yangu leo ni kuyatii matayarisho ya Mungu na kumshuhudia Mungu mbele ya Shetani, Kuvumilia mateso haya yote na fedheha sasa si kwa sababu nimefanya kosa, lakini ni kwa ajili ya jina la Mungu. Kuvumilia mateso haya kunaleta sifa kuu. Jinsi Shetani anavyozidi kunifedhehesha, ndivyo ninavyopaswa kuzidi kusimama upande wa Mungu na kumpenda Mungu. Njia hiyo, Mungu anaweza kupata utukufu, na ningekuwa nimetimiza wajibu niliopaswa kuutimiza. Alimradi Mungu ana furaha na radhi, moyo wangu pia utapokea faraja. Niko tayari kuvumilia mateso ya mwisho ili kumridhisha Mungu na kuyaruhusu yote yatayarishwe na Mungu. Nilipoanza kufikiria jinsi hii, nilihisi kuguswa hasa moyoni mwangu, na kwa mara nyingine tena sikuweza kuyadhibiti machozi yangu: “Ee Mungu, Wewe unapendeza mno! Nimekufuata kwa miaka mingi sana, lakini sijawahi kamwe kuuhisi upendo wako wa huruma kama nilivyouhisi leo, au kuhisi kuwa karibu na Wewe kama nilivyohisi leo.” Nilisahau kabisa mateso yangu na nikazama katika hisia hii ya kusisimua kwa muda mrefu, muda mrefu …

Halijoto ilikuwa ya chini sana siku ya sita kizuizini. Kwa kuwa wale polisi waovu walikuwa wameninyang’anya koti langu la pamba, nilikuwa nimevaa chupi yangu ndefu tu na kuishia kushikwa na mafua. Nilishikwa na homa kali na pia sikuweza kuacha kukohoa. Usiku, nilijifunikia blanketi chakavu, nikivumilia maumivu ya ugonjwa huku pia nikifikiri juu ya uteswaji usio na mwisho wa wafungwa kwangu. Nilijihisi kuwa mwenye ukiwa sana na asiyejiweza. Taabu yangu ilipofikia kiwango fulani tu, maneno la Mungu yalirudia katika sikio langu: “Kama Wewe utanipa ugonjwa, na kuchukua uhuru wangu, naweza kuendelea kuishi, lakini adabu Yako na hukumu vikiondoka kutoka kwangu, sitakuwa na njia ya kuendelea kuishi. Kama ningekuwa bila adabu Yako na hukumu, ningepoteza upendo Wako, upendo ambao ni mkuu sana mpaka sina maneno ya kuueleza. Bila Upendo wako, ningeishi chini ya miliki ya Shetani, na singeweza kuuona uso wako mtukufu. Ningewezaje kuendelea kuishi?(“Matukio Aliyopitia Petro: Ufahamu Wake wa Adabu na Hukumu” katika Neno Limeonekana katika Mwili). Haya maneno yalinipa imani na nguvu. Petro hakufikiria chochote cha mateso ya mwili. Alichokidhamini, alichokishughulikia, kilikuwa ni hukumu adhabu za Mungu. Alichotafuta ni kupitia hukumu na adhabu za Mungu ili aweze kutakaswa na kutimia utii hata kifo, na upendo wa kweli wa Mungu. Nilijua kwamba nililazimika kufuata njia sawa kama ile ya Petro, kwamba Mungu alikuwa ameruhusu mimi niwekwe katika hali hiyo. Hata ingawa nilipitia mateso ya kimwili, ilikuwa upendo wa Mungu ukinijia. Mungu alitaka kukamilisha imani yangu na azimio langu katika mateso. Niliguswa sana mara tu nilipoelewa nia ya dhati ya Mungu na nilichukia jinsi nilivyokuwa dhaifu, jinsi nilivyokuwa mbinafsi. Nilijihisi mwenye deni kubwa kwa Mungu kwa kutoyajali mapenzi yake na nilihapa , bila kujali ya kwamba ,hata ingawa mateso yangu nimakubwa kiasi gani, nitasimama shahidi na kumridhisha Mungu. Siku iliyofuata, homa yangu kali ilipungua kimiujiza. Nilimshukuru Mungu moyoni mwangu.

Usiku mmoja, mchuuzi mmoja alikuja kwa dirisha na mkuu wa seli akanunua hemu nyingi sana, nyama ya mbwa, mapaja ya kuku, na kadhalika. Hatimaye, akaniamuru nilipe. Nilimwambia sikuwa na pesa, kwa hiyo akasema kwa ukali: “Ikiwa huna fedha nitakutesa polepole!” Siku iliyofuata, alinilazimisha nioshe shuka za kitanda, nguo, na soksi. Maafisa wa magereza katika kituo hicho cha kizuizi pia walinilazimisha niwaoshee soksi zao. Katika kituo hicho cha kizuizi, ilinibidi kuvumilia mapigo yao karibu kila siku. Wakati wowote ambapo sikuweza kuvumilia tena, nilikuwa nikifikiria maneno ya Mungu: “Lazima umfanyie Mungu wajibu wako wa mwisho wakati wa muda wako hapa duniani. Zamani, Petro alisulubiwa juu chini kwa ajili ya Mungu; hata hivyo, unapaswa kumridhisha Mungu mwishowe, na utumie nguvu zako zote kwa ajili ya Mungu. Kiumbe anaweza kumfanyia Mungu nini? Kwa hiyo unapaswa kujitolea kwa rehema ya Mungu mapema iwezekanavyo. Maadamu Mungu anafurahia na Anapendezwa, basi mwache Afanye chochote Atakacho. Wanadamu wana haki gani ya kulalamika?(Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Ufafanuzi wa Mafumbo ya “Maneno ya Mungu kwa Ulimwengu Mzima”, Sura ya 41). Maneno ya Mungu yalinipa nguvu. Ingawa mara kwa mara ningekuwa mwenye uelekeo wa mashambulizi, unyanyasaji, shutuma, na mapigo ya wafungwa, kwa uongozi wa maneno ya mungu, nilifarijika ndani na sikuhisi maumivu tena.

Siku moja afisa mmoja wa magereza alinipeleka kwa ofisi yake. Nilipofika huko, nikaona zaidi ya watu kumi na wawili wakinitazama kwa macho ya pekee. Mmoja wao alishikilia kamera ya video mbele yangu upande wangu wa kushoto, huku mwingine akinijia na mikrofoni, akiuliza: “Kwa nini unamwamini Mwenyezi Mungu?” Hapo ndipo nilipogundua kwamba haya yalikuwa ni mahojiano ya vyombo vya habari, kwa hivyo nilijibu kwa unyenyekevu wa kujivunia: “Tangu nilipokuwa mdogo, daima nimekuwa chini ya dhuluma ya watu na kutothaminiwa, na nimewaona watu wakidanganyana na kutumiana kwa manufaa ya wao kwa wao. Nilihisi kwamba jamii hii ilikuwa ya uovu mno, yenye hatari mno; watu walikuwa wakiishi maisha matupu na ya kutojiweza, bila matumaini na bila malengo ya maisha. Baadaye, wakati mtu fulani alinihubiria injili ya Mwenyezi Mungu, nilianza kuiamini. Baada ya kumwamini Mwenyezi Mungu, nimehisi waumini wengine wakinitendea kama familia. Hakuna mtu katika Kanisa la Mwenyezi Mungu anayenilia njama. Kila mtu anaelewana na mwenzake na ni wa upendo. Huwa wanatunzana, na hawana hofu ya kuzungumza kile kilicho akilini mwao. Katika neno la Mwenyezi Mungu nimepata kusudi na thamani ya maisha. Nadhani kumwamini Mungu ni kuzuri sana.” Mwandishi huyo kisha akauliza: “Unajua ni kwa nini uko hapa?” Nikajibu: “Baada ya kumwamini Mwenyezi Mungu, sijali sana kuhusu jina la kidunia na manufaa, na nahisi kwamba vitu hivi ni vitupu na visivyo na maana. Ni iwapo tu naweza kuwa mtu mzuri na kuchukua njia sahihi ndipo naweza kuishi kwa njia ya haki. Moyo wangu unageuka zaidi na zaidi kuelekea wema, na niko tayari zaidi na zaidi kuwa mtu mzuri. Kuona jinsi neno la Mwenyezi Mungu linaweza kwa hakika kuwageuza watu na kuwaongoza wachukue njia sahihi, nilifikiria kuwa kama watu wote wanaweza kumwamini Mungu, basi nchi yetu pia ingekuwa ya utaratibu zaidi na kiwango cha uhalifu pia kingeshuka. Kwa hivyo, niliamua kuwaambia watu wengine habari hii njema, lakini sikujua kamwe kwamba kazi nzuri kama hiyo ingekuwa imepigwa marufuku nchini China. Na hivyo nilikamatwa na kuletwa hapa.” Mwandishi huyo aliona kwamba majibu yangu hayakuwa na manufaa kwao, kwa hiyo mara moja akaacha mahojiano na akageuka na kwenda. Wakati huo, naibu mkuu wa Brigedi ya Usalama wa Taifa alikuwa na hasira kiasi kwamba alishinda akikanyaga kanyaga kwa nguvu. Alinitazama kwa ukali, akisaga meno na kunong’ona: “Wewe ngoja tu na uone!” Lakini sikuogopa maonyo yake au vitisho. Kinyume chake, nilihisi kuheshimiwa sana kwa kuweza kumshuhudia Mungu wakati kama huo, na aidha nilimpa Mungu utukufu kwa ajili ya kutukuzwa kwa jina la Mungu na kushindwa kwa Shetani. Asubuhi moja, afisa mmoja wa magereza aliwasilisha hasa karatasi moja ya gazeti. Wafungwa walitoa tabasamu la uovu na sura mbaya kwa sauti ya kudhihaki kusoma maneno kutoka kwa gazeti na kumkashifu na kumkufuru Mwenyezi Mungu. Nilikuwa na hasira sana ndani kiasi kwamba nilianza kusaga meno yangu. Wafungwa walikuja kuniuliza yote hayo yalikuwa ni nini, na nikasema kwa sauti kubwa: “Hii ni kampeni ya kuharibu jina na Chama cha Kikomunisti!” Kuwasikiliza wafungwa hawa wote wakifuata tu umati na kufifisha ukweli na kumkufuru Mungu kwa kuzungumza lugha moja na shetani, ilivyoonekana niliona kuja kwa mwisho wao. Kwa kuwa dhambi ya kumkufuru Mungu haitasamehewa kamwe, yeyote anayeikosea tabia ya Mungu atapata adhabu kali zaidi na malipo! Kwa kufanya hivi, Chama cha Kikomunisti kinawapeleka watu wote wa China kwa adhabu yao ya mwisho, kikiufichua kabisa tabia yake ya kweli kama pepo mla roho!

Baadaye polisi aliyehusika na kesi yangu alinihoji tena. Wakati huu, hakutumia mateso ili kujaribu kulazimisha ungamo, na badala yake akabadilika kwa kutumia uso “wenye huruma” kuniuliza: “Ni nani kiongozi wako? Nitakupa fursa nyingine. Ukituambia, utakuwa sawa. Nitakuonyesha huruma kubwa. Ulikuwa hauna hatia mwanzoni, lakini watu wengine walikusaliti. Kwa hiyo ni kwa nini unawaficha? Unaonekana kama mtu mwenye tabia nzuri. Kwa nini utoe maisha yako kwa ajili yao? Ukituambia, unaweza kwenda nyumbani. Kwa nini ukae hapa na kuteseka?” Hawa wanafiki waliona kwamba njia ya kuwa wagumu haikufua dafu, kwa hiyo waliamua kujaribu njia ya kuwa wapole. Wao kwa kweli wamejaa hila za ujanja na ni stadi wa zamani wa njama na hila! Kuona huo uso wake wa unafiki kuliujaza moyo wangu na chuki kwa kundi hili la pepo. Nikamwambia: “Nimekuambia kila kitu ninachokijua. Sijui chochote kingine.” Baada ya kuona mtazamo wangu thabiti, alijua kwamba hangeweza kupata chochote kutoka kwangu, kwa hiyo akaondoka kwa huzuni.

Baada ya kuzuiliwa kwa kituo cha kizuizi kwa nusu mwezi, niliachiliwa tu baada ya polisi kuiuliza familia yangu kulipa yuan 8,000 kama fedha za dhamana. Lakini walinionya nisiende mahali popote na kuwa ni lazima nikae nyumbani na kuhakikisha kuwa ningepatikana wakati wowote. Siku niliyoachiliwa, maafisa wa magereza hawakunipa chakula chochote cha kula kwa makusudi, huku wafungwa wakisema: “Mungu wako ni wa ajabu. Hatukukuwa wagonjwa, lakini sisi sote tukawa wagonjwa hapa. Ulikuja hapa kama umejaa magonjwa, lakini sasa unaondoka bila ugonjwa wowote. Hongera!” Katika wakati huu, moyo wangu ukawa na shukurani hata zaidi na kujaa sifa kwa Mungu! Mjomba wangu ni mlinzi wa jela. Aliendelea kushuku kuwa nimeachiliwa kwa sababu baba yangu alikuwa na uhusiano maalum na mtu fulani mwenye nguvu, ama sivyo hakuna jinsi ambavyo ningeweza kuachiliwa kutoka gereza la usalama wa juu katika kipindi cha nusu mwezi—angalau sana ingekuwa miezi mitatu. Familia yangu nzima ilijua vizuri sana kwamba hii ilikuwa imedhamiriwa na kudura ya Mungu na kwamba alikuwa ni Mungu akifichua kazi Yake nzuri kwangu. Niliona wazi kwamba haya yalikuwa mashindano kati ya Mungu na Shetani. Bila kujali jinsi Shetani alivyo katili na muovu, daima atashindwa na Mungu. Kuanzia wakati huo kwendelea, nikaamini kuwa kila kitu nilichokabiliwa nacho kilikuwa sehemu ya matayarisho ya Mungu. Baadaye, kwa mashtaka yasiyo na msingi, ya “kuvuruga utaratibu wa jamii,” Chama Cha Kikomunisti walifanya nihukumiwe kifungo cha mwaka mmoja kifungo cha muda uliyowekwa, kusimamishwa kwa miaka mbili.

Baada ya kupitia mateso haya na taabu, nilikuwa na ufahamu na niliweza kutambua asili ya uovu wa Chama cha kukana Mungu cha Kikomunisti cha China, na nikakuza chuki kubwa kwake. Yote kinayofanya ni kutumia mbinu za nguvu nyingi ili kudumisha hali yake ya kutawala, kushambulia na kukandamiza matendo yote ya haki na kuchukia sana ukweli kwa kuvuka mpaka. Ni adui mkuu mno wa Mungu. Ili kiweze kufanikisha lengo lake la kuwadhibiti watu kwa kudumu, huwa kiko tayari kufanya chochote kuizuia na kuivuruga kazi ya Mungu duniani, kwa ukali kikiwakandamiza na kuwatesa waumini wa Mungu, na tena ni adui wa sisi tunaoamini katika Mungu. Baada ya kupitia dhiki hili, naweza kuona kwamba ni neno la Mungu pekee linaloweza kuwaletea watu maisha. Wakati niliokuwa katika hali ya kukata tamaa kabisa au karibu kufa, ilikuwa ni neno la Mungu ambalo lilinipa imani na ujasiri na kuniruhusu kwa udhabiti kushikilia Maisha. Shukrani kwa Mungu kwa kunilinda, katika siku hizo za giza sana, ngumu mno. Upendo Wake kwangu ni, mkubwa mno!

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Maudhui Yanayohusiana

Leave a Reply

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp