Pambano la Kuwa Mtu Mwaminifu

25/08/2020

Mwenyezi Mungu anasema, “Ufalme Wangu unawahitaji wale ambao ni waaminifu, wasio wanafiki, na wasio wadanganyifu. Je, si watu wenye moyo safi na waaminifu duniani hawapendwi na watu? Mimi ni kinyume kabisa cha jinsi ilivyo. Inakubalika kwa watu waaminifu kuja Kwangu; Nafurahia mtu wa aina hii, pia Ninamhitaji mtu wa aina hii. Hii ni haki Yangu hasa(Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Matamko ya Kristo Mwanzoni, Sura ya 33). “Mnastahili kujua kwamba Mungu hupenda binadamu mwaminifu. Mungu ana kiini cha uaminifu, na kwa hivyo neno Lake siku zote linaweza kuaminika. Aidha, matendo Yake hayana dosari wala hayajadiliwi. Hii ndiyo maana Mungu anawapenda wale walio waaminifu kabisa Kwake. Uaminifu unamaanisha kumpa Mungu moyo wako; kutomdanganya katu katika kitu chochote; kuwa wazi Kwake katika mambo yote, kutowahi kuficha ukweli; kutowahi kufanya kile kinachowadanganya wale walio juu na kuwafumba macho wale walio chini; na kutowahi kufanya kile ambacho kinakupendekeza kwa Mungu. Kwa ufupi, kuwa waaminifu ni kujizuia dhidi ya uchafu katika matendo na maneno yenu, na kutomdanganya Mungu wala binadamu(Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Maonyo Matatu). Kusoma maneno ya Mungu kunanikumbusha jinsi nilivyokuwa nikichuma pesa kwa njia zisizo aminifu katika biashara yangu. Niliishi bila hata chembe ya mfano wa binadamu. Baada ya kukubali kazi ya Mwenyezi Mungu na kuhukumiwa na kuadibiwa na maneno Yake, hatimaye nilielewa machache kuhusu tabia zangu za kishetani za ubinafsi na udanganyifu. Kulikuwa na mabadiliko katika mtazamo wangu na nilianza kutenda ukweli na kuwa mtu mwaminifu.

Miaka michache iliyopita, nilifungua duka la kutengeneza vifaa. Nilitaka kuwa mfanyabiashara mwaminifu na kuchuma pesa kidogo tu ili familia yangu iwe na kiasi cha kutosha. Lakini baada ya kuwa na shughuli nyingi kila wakati kwa muda fulani, niliona kwamba nilikuwa nimechuma pesa za kutosha familia kuishi, na kuweka akiba hakukuwezekana. Wakati mwingine mapato yangu ya kila mwezi yalikuwa madogo zaidi kuliko ya mfanyakazi wa kiwango cha chini kabisa. Mke wangu alikuwa akinilalamikia kila mara kuhusu hilo, akisema kuwa nilikuwa mwaminifu sana na sikujua jinsi ya kufanya biashara. Shemeji yangu pia aliingilia kati. Alisema, “Tunaishi katika enzi ya pesa, na bila kujali unafanyaje, lazima uwafanye watu wakupe pesa zao ili uonekane hodari.” Alisema pia mambo kama vile “Hakuna mali ipatikanayo bila ujanja” na “Pesa ni muhimu sana ulimwenguni” ili kunizindua na kunifanya nifuate mwenendo, nifanye biashara kama wengine na nisiwe mkaidi sana. Nilidhani kwamba walichosema kilileta maana, lakini sikuweza kabisa kuwadanganya wateja wangu. Nilihisi kwamba dhamiri yangu haikuweza kukubaliana na hilo kabisa.

Baadaye niliona kwamba Bw. Qian, mmiliki wa duka la kukarabati vifaa lililokuwa karibu na duka langu, alikuwa na ujuzi kidogo sana wa kiufundi. Aliweza tu kufanya marekebisho madogo madogo, lakini alikuwa na ubao mkubwa ulioning’inia mbele ya duka lake ambao ulisema “Marekebisho Bora kwa Vifaa Vyote.” Alivutia wateja wengi kwa njia hiyo. Alikubali kazi na kurekebisha kifaa iwapo kilikuwa rahisi kurekebisha. Vinginevyo, alituma kifaa kile mahali pengine pa marekebisho na kuchukua sehemu ya malipo. Alipata pesa nyingi kiasi kwa njia hiyo. Wakati mmoja tulipokuwa tukiongea, aliniambia jinsi alivyopata pesa zake. Alisema kwamba sehemu ndogo katika kifaa inapovunja, unaweza tu kubadilisha sehemu zote ili uweze kutoza fedha zaidi. Wateja hawajui lolote. Alisema kwamba tunaishi katika jamii inayothamini pesa, na “Haijalishi kama paka ni mweupe ama mweusi, mradi amkamate panya.” Alisema pia kuwa kuweza kuchuma pesa kunamaanisha kuwa una uwezo, vinginevyo, haijalishi wewe ni mtu mzuri kiasi gani, utadharauliwa. Baada ya kusikia “umaizi mzuri sana” wa mtu huyu, niliwaza, “Hii ndiyo enzi tunamoishi. Watu wengine wanaweza kufanya lolote kwa ajili ya fedha na uaminifu haupo kabisa, kwa hivyo kuna faida gani ikiwa mimi pekee ndiye mwaminifu? Aidha, kufanya biashara yangu kwa uaminifu hakujanipa mafanikio. Mtu huyu hutengeneza vitu kama mimi tu na anaishi maisha mazuri. Familia yake yote inaishi vizuri, lakini mimi nachuma tu fedha za kutosha kuishi. Inaonekana kwamba nimekuwa mkaidi sana. Napaswa kutafuta njia za kuchuma pesa nyingi zaidi ili familia yangu iwe na maisha mazuri zaidi.” Baada ya hapo, nilianza kujifunza kutoka kwa “mafanikio” ya wenzangu na kutumia njia za hila kuwalaghai wateja wangu. Nilifadhaika, lakini sikufikiria sana juu ya hilo ili niweze kuchuma fedha nyingi zaidi.

Mteja mmoja alikuja kurekebishiwa kifaa siku moja. Nilipokuwa nikitoa sehemu iliyokuwa imeharibika niliondoa sehemu zilizokuwa sawa kabisa ili afikirie kwamba sehemu nyingi zilikuwa zimeharibika, na asijue wakati ambapo ningemtoza fedha nyingi zaidi. Msemo huo wa zamani, “Mwenye hatia kama mwizi,” ni kweli kabisa. Mara ya kwanza nilifadhaika sana na moyo wangu ulikuwa ukipapa, nikiogopa kwamba angenibaini na kunikaripia papo hapo. Hilo lingeniabisha. Lakini nilijifanya kuwa mtulivu na nikabadilisha sehemu zote hizo. Ilipofika wakati wa kulipa, bila aibu, nilimtoza 50% zaidi ya kiwango nilichotaja awali. Niliinamisha kichwa changu wakati wote, na sikuthubutu kumtazama machoni, lakini kwa mshangao wangu, alilipa bila kusema lolote. Mwishowe nilishusha pumzi baada ya yeye kuondoka. Uso na mgongo wangu vilijawa na jasho na nilihisi hali ya ajabu ya wasiwasi. Lakini nilipoona fedha zile za ziada nilizokuwa nimepata, hisia ile ilitoweka kwa haraka.

Kuanzia wakati huo nilianza kufikiria mbinu za kila aina za kuwatoza wateja fedha zaidi. Nilikuwa na dhamiri yenye hatia hapo mwanzoni, lakini nilijihimiza kimyakimya ili niweze kuendelea kuchuma mapato ya ziada. “Sifai kuwa mpole sana—‘Kwa vile akili ndogo haimfanyi mtu kuwa muungwana, mwanamume mwenye thamani hakosi sumu.’ Lazima niwe mjanja iwapo ningependa kuchuma fedha. Aidha, kila mtu hufanya hivyo, si mimi tu.” Baada ya muda hisia hiyo ya hatia iliisha na nikawa stadi na mstaarabu zaidi katika “umahiri” wangu wa kuchuma pesa. Nilijifunza pia kutambua mawazo ya watu na kuwapima, na kuwatendea watu tofauti kwa njia tofauti. Nilijifunza mbinu nyingi zaidi. Wateja wakwasi walipokuja, niliwashawishi huku nikisema kile walichotaka kusikia na kuwafurahisha ili iwe rahisi kwangu kuwatoza fedha nyingi zaidi. Nilipokuwa na mteja aliyekuwa na wasiwasi sana, nilijifanyanya kwamba ukarabati ulikuwa mgumu na mtatanishi sana, na kisha nilichukua muda zaidi kwa makusudi. Kwa njia hiyo alinipa pesa zaidi. Wateja wengine walikuwa werevu, kwa hivyo nilifikiria sababu ya kuwafanya waniachie vifaa vyao na wavichukue siku nyingine, na waliporudi nilisema kwamba nilikuwa nimepata matatizo mengine. Nilikuwa nikichuma fedha zaidi, na sikuwa na wasiwasi nilipokuwa peke yangu. Na kwa hivyo, nilifikiria kila wakati jinsi ya kuwatoza wateja fedha nyingi zaidi. Nilikuwa nikichuma pesa nyingi zaidi na kuishi maisha mazuri zaidi, lakini sikuhisi raha au furaha yoyote moyoni mwangu. Badala yake, kila nilipofikiria mambo niliyoyafanya yaliyostahili dharau na yasiyo ya maadali nilihisi hofu na wasiwasi. Wakati mwingine niliwaza, “Napaswa kuacha. Sifai kufanya biashara hii ya hila tena. Kama inavyosemekana, ‘Mema hulipwa kwa mema, na maovu kwa maovu.’ Nitapata kile ninachostahili.” Lakini baadaye nilipofikiria kupata pesa hizo zote, sikuweza kabisa kukusudia kuacha.

Nilipokuwa tu nikizidi kutumbukia katika upotovu na kutojali, dadangu alishiriki nami injili ya ufalme wa Mwenyezi Mungu. Baada ya kukubali kazi ya Mungu, nilianza kukusanyika pamoja na kina ndugu na kusoma maneno ya Mungu mara kwa mara. Nilisoma maneno haya kutoka kwa Mwenyezi Mungu katika mkutano mmoja: “Mwanadamu ametembea katika enzi hizi tofauti pamoja na Mungu, lakini bado hafahamu kwamba Mungu huongoza hatima ya mambo yote na viumbe hai au jinsi Mungu hupanga na kuelekeza mambo yote. Hili ni jambo ambalo limekwepa ufahamu wa binadamu tangu enzi za kale mpaka leo. Kuhusu sababu, siyo kwa sababu matendo ya Mungu hayafahamiki, au kwa sababu mpango wa Mungu bado haujakamilika, lakini ni kwa sababu moyo na roho ya mwanadamu viko mbali sana na Mungu, kiasi ya kwamba, mwanadamu anabaki katika huduma ya Shetani wakati ule ule anapomfuata Mungu—na hata halitambui hili. Hakuna anayetafuta nyayo za Mungu kwa vitendo au kuonekana Anakoonyesha, na hakuna aliye na hiari ya kuwepo katika huduma na utunzaji wa Mungu. Badala yake, wao wako tayari kutegemea upotoshaji wa Shetani, yule mwovu, ili kurekebishwa kufuatana na dunia hii na kanuni za kuwepo ambazo watu waovu hufuata. Wakati huu, moyo na roho za mwanadamu hutolewa ushuru kwa shetani na kuwa riziki ya Shetani. Hata zaidi, moyo wa binadamu na roho yake zimekuwa mahali ambapo Shetani anaweza kuishi na uwanja wake wa kuchezea unaofaa. Kwa njia hii, mwanadamu kwa kutojua hupoteza ufahamu wake wa kanuni za kuwa binadamu, na wa thamani na maana ya kuwepo kwa binadamu. Sheria za Mungu na agano kati ya Mungu na mwanadamu huangamia hatua kwa hatua kutoka katika moyo wa mwanadamu, na yeye huacha kumtafuta na kumsikiza Mungu. Wakati upitavyo, mwanadamu haelewi tena kwa nini Mungu alimuumba, wala haelewi maneno yanayotoka katika kinywa cha Mungu na yote yanayotoka kwa Mungu. Mwanadamu kisha huanza kupinga sheria na amri za Mungu na moyo na roho zake hufishwa…. Mungu humpoteza mwanadamu ambaye Alimuumba mwanzoni, na mwanadamu hupoteza mzizi wa mwanzo wake: Hii ndiyo huzuni ya hii jamii ya wanadamu(Neno Laonekana katika Mwili). Maneno ya Mungu yanaakisi uhalisi. Hata ingawa nilikuwa nimepata pesa nyingi ulimwenguni na starehe zangu za mwili zilikuwa bora kuliko hapo awali, nilikuwa mtupu na niliumia moyoni, na ilikuwa tu kwa sababu nilikuwa nimejitenga na Mungu, nimeenda kinyume na matakwa Yake kwa mwanadamu, na kuishi kulingana na sheria za Shetani za kuishi. Nilipofungua duka lile kwa mara ya kwanza, nilichuma pesa kwa moyo safi, na hata ingawa sikuchuma pesa nyingi, nilikuwa na amani. Lakini baadaye nilishawishiwa na mazingira yangu, na kuwaona wengine wakitajirika kwa njia za hila. Nilianza pia kukubali, “Hakuna mali ipatikanayo bila ujanja,” “Pesa ni muhimu sana ulimwenguni.” na “Pesa siyo kila kitu, lakini bila hiyo, huwezi kufanya chochote,” na sheria nyingine kama hizi za kuishi zitokazo kwa Shetani. Nilifuata mwenendo mbaya na niliacha kanuni zangu za msingi ili kuchuma pesa, nikipuuza dhamiri yangu niwalaghai wateja ili walipe pesa nyingi zaidi. Pesa zilikuwa mikononi mwangu, lakini zote zilikuwa zimepatikana kwa wizi. Kila nilipofikiria mambo hayo maovu na ya kustahili dharau niliyokuwa nimeyafanya, nilihisi vibaya sana na sikuweza kupata amani yoyote. Niliishi kwa kuhofia siku ambayo mtu fulani angenifunua, wakati ambapo ningeshutumiwa. Hali mbaya zaidi ikiwa kwamba hata ningeripotiwa kwa polisi. Nilikuwa na wasiwasi kila wakati. Ilikuwa njia chungu ya kuishi. Lakini siku hiyo nilielewa kwamba ni kwa sababu nilikuwa nikiishi kulingana na falsafa ya kishetani. Hayo yalikuwa matokeo ya kufungwa na kudanganywa na sheria za Shetani. Bila mwongozo wa maneno ya Mungu, singewahi kuona uhalisi wa jinsi Shetani alivyokuwa akinidhuru.

Dada mmoja kisha alinisomea vifungu kadhaa vya maneno ya Mungu: “Mnastahili kujua kwamba Mungu hupenda binadamu mwaminifu. Mungu ana kiini cha uaminifu, na kwa hivyo neno Lake siku zote linaweza kuaminika. Aidha, matendo Yake hayana dosari wala hayajadiliwi. Hii ndiyo maana Mungu anawapenda wale walio waaminifu kabisa Kwake. Uaminifu unamaanisha kumpa Mungu moyo wako; kutomdanganya katu katika kitu chochote; kuwa wazi Kwake katika mambo yote, kutowahi kuficha ukweli; kutowahi kufanya kile kinachowadanganya wale walio juu na kuwafumba macho wale walio chini; na kutowahi kufanya kile ambacho kinakupendekeza kwa Mungu. Kwa ufupi, kuwa waaminifu ni kujizuia dhidi ya uchafu katika matendo na maneno yenu, na kutomdanganya Mungu wala binadamu.” “Ufalme Wangu unawahitaji wale ambao ni waaminifu, wasio wanafiki, na wasio wadanganyifu. Je, si watu wenye moyo safi na waaminifu duniani hawapendwi na watu? Mimi ni kinyume kabisa cha jinsi ilivyo. Inakubalika kwa watu waaminifu kuja Kwangu; Nafurahia mtu wa aina hii, pia Ninamhitaji mtu wa aina hii. Hii ni haki Yangu hasa(Neno Laonekana katika Mwili). Kisha alishiriki ushirika huu: “Mungu ni mwaminifu kimsingi. Anawapenda na kuwabariki wale ambao ni waaminifu. Tunapojihusisha na wengine ulimwenguni, tunaishi kulingana na sheria ya Shetani, ‘Usiwahi kumsaidia mtu bila kupewa thawabu.’ Maneno na matendo yetu yote ni kwa ajili ya faida ya kibinafsi, na tunalaghai na kudanganya bila aibu. Hatujui kuwa mtu mzuri kunamaanisha nini.” “Lakini imani katika Mungu ni tofauti leo. Anahitaji tuwe watu waaminifu, tuseme ukweli, na kuwa wanyofu. Anataka tukubali uchunguzi Wake wa makini katika kila neno na kila tendo, kwamba tuwe wazi na waaminifu, na tusijaribu kumhadaa au kumdanganya Mungu au mwanadamu. Ni watu waaminifu pekee ndio walio na mfano wa kweli wa kibinadamu, na ni wao tu wanaoweza kumshuhudia na kumtukuza Mungu.” Nilijifunza kutoka kwa maneno ya Mungu kwamba Anapenda watu waaminifu na nilipaswa kutenda kulingana na mahitaji Yake. Nilianza kujizoeza kuwaambia ukweli kina ndugu, na kutowadanganya, lakini bado nilikuwa na wasiwasi nilipofanya biashara. Nilihisi kwamba ilikuwa rahisi kutenda kuwa mtu mwaminifu kwa kina ndugu, lakini kama ningefanya hivyo katika biashara yangu, ningepata fedha kidogo sana na huenda ningelazimika kufunga biashara. Lakini kama ningeendelea kuwahadaa na kuwadanganya watu kama hapo awali, je, si huko kungekuwa kinyume na mapenzi ya Mungu? Kwa hivyo, utendaji wangu ulipaswa kuwa upi? Niliwaza na kuwazua na nilipata suluhu: Nilikuwa mtu mwaminifu kanisani, lakini niliendelea na biashara kama kawaida dukani kwangu.

Siku moja mzee fulani alileta runinga yake, akisema kwamba picha hazikuonekana vizuri. Niliangalia na nikaona kwamba nyaya za rangi zilikuwa zimechakaa na zilifaa kubadilishwa, lakini sikumwambia ukweli. Niliongeza tu volteji ya nyaya za ndani ili aitumie kwa muda kidogo zaidi, kisha nizibadilishe tatizo litakapotokea tena. Kwa njia hiyo ningepata pesa zaidi ya yuani 30 ya matengenezo. Wiki mbili baadaye, runinga ile kweli ilipata tatizo na yule mzee aliniomba niitengeneze tena, akisema kwamba sikuwa nimefanya kazi nzuri. Nilimwambia kwamba nyaya za rangi zilikuwa kuukuu na zilihitaji kubadilishwa. Kwa mshangao wangu, alibaini ujanja wangu. Alikatalia ada ya marekebisho ya yuani 30 na kusema kwa kushutumu, “Kijana, kufanya biashara kunahitaji uaminifu. Usiwe mlafi sana!” Nilihisi aibu sana wakati huo lakini sikujali wala kufikiria hilo zaidi. Ajuza mmoja baadaye alileta wimbi maikro iliyokuwa imevunjika, na nilipata sehemu moja ndogo iliyokuwa imevunjika ndani yake. Nilifikiri kwamba ningeirekebisha na kisha kutoza ada inayofaa. Lakini baadaye nilifikiri kuhusu jinsi alivyokuwa tajiri, kwa hivyo kumtoza zaidi hakukuwa tatizo. Lazima uchukue unachoweza kupata. Lakini alirudi dukani siku chache baadaye na kusema, “Ulinitoza fedha nyingi zaidi kwa ajili ya wimbi maikro hiyo. Kuwa na dhamiri. Mungu huona tunayoyafanya!” Nilihisi vibaya sana baada ya kukaripiwa naye na nilifikiria tena alichokuwa amesema mtu yule. Nilifadhaika sana. Nilitambua pia kwamba Mungu alikuwa Akitumia vitu vinavyonizingira kunionya ili nitafakari juu yangu na kujijua.

Baadaye, nilisoma haya katika maneno ya Mungu: “Bila kujali unachokifanya, jambo ni kubwa au dogo kiasi gani, na kama unalifanya ili kutimiza wajibu wako katika familia ya Mungu au kwa ajili ya sababu zako za faragha, lazima ufikirie kama kile unachofanya kinalingana na mapenzi ya Mungu, na vile vile kama ni kitu ambacho mtu ambaye ana ubinadamu anapaswa kufanya. Ukitafuta ukweli kwa namna hiyo katika kila kitu unachofanya, basi wewe ni mtu anayemwamini Mungu kwa kweli. Ukishughulikia kwa moyo wote kila jambo na kila ukweli kwa njia hii, basi utaweza kufanikisha mabadiliko katika tabia yako. Watu wengine hufikiri kwamba wanapokuwa wakifanya kitu cha kibinafsi, wanaweza tu kupuuza ukweli, wakifanye watakavyo, na wakifanye kwa njia yoyote inayowafurahisha na kwa namna yoyote ile iliyo na faida kwao. Hawafikirii hata kidogo jinsi inavyoweza kuathiri familia ya Mungu, wala hawafikirii kama kile wanachofanya kinastahili umakini wa kitakatifu. Hatimaye, punde wanapomalizana na jambo hili, wanakuwa waovu ndani yao na kuhisi wasiwasi, ingawa hawajui ni kwa nini. Je, si hii ni adhabu inayowafaa? Ukifanya vitu ambavyo havijaidhinishwa na Mungu basi umemkosea Mungu. Ikiwa mtu hapendi ukweli, na mara nyingi nafanya vitu kulingana na mapenzi yake, basi atamkosea Mungu mara kwa mara. Watu kama hao kwa kawaida hawakubaliwi na Mungu katika yale wayatendayo, na wasipotubu, basi adhabu haitakuwa mbali sana nao.” “Mpaka watu wawe wamepitia kazi ya Mungu na kupata ukweli, ni asili ya Shetani inayotwaa madaraka na kuwatawala kwa ndani. Ni nini, hasa, kilicho ndani ya asili hiyo? Kwa mfano, kwa nini wewe ni mchoyo? Kwa nini wewe hulinda nafasi yako mwenyewe? Kwa nini una hisia kali sana namna hiyo? Kwa nini unafurahia hivyo vitu visivyo vya haki? Kwa nini unapenda maovu hayo? Msingi wa kupenda kwako vitu hivi ni upi? Mambo haya hutoka wapi? Kwa nini unafurahia sana kuyakubali? Kufikia sasa, nyote mmekuja kuelewa kwamba sababu kuu ya mambo haya yote ni kwamba sumu ya Shetani iko ndani yenu. Kuhusu sumu ya Shetani ni nini, inaweza kuelezwa kwa ukamilifu kwa maneno. Kwa mfano, ukiwauliza baadhi ya watenda maovu kwa nini walitenda jinsi walivyotenda, watajibu, ‘Kwa sababu kila mwamba ngoma huvutia upande wake.’ Msemo huu mmoja unaonyesha asili ya shida. Mantiki ya Shetani imekuwa maisha ya watu. Wanaweza kutenda mambo kwa ajili ya madhumuni fulani au mengine, lakini wanajifanyia tu. Kila mtu hudhani kwamba kwa kuwa ni kila mwamba ngoma huvutia upande wake, watu wanafaa kuishi kwa sababu yake mwenyewe tu, na kufanya kila awezalo kupata wadhifa mzuri kwa ajili ya chakula na mavayi mazuri. ‘Kila mwamba ngoma huvutia upande wake’—haya ndiyo maisha na falsafa ya mwanadamu, na pia inawakilisha asili ya binadamu. Maneno haya ya Shetani ni sumu ya Shetani hasa, na watu wanapopoiweka moyoni, inakuwa asili yao. Asili ya Shetani hufunuliwa kupitia maneno haya; yanamwakilisha yeye kabisa. Sumu hii inakuwa maisha ya watu pamoja na msingi wa kuwepo kwao; na wanadamu waliopotoshwa wametawaliwa kwa uthabiti na sumu hii kwa maelfu ya miaka(Kumbukumbu za Hotuba za Kristo). Nilipokuwa nikisoma haya, niliweza kuona kabisa kwamba Roho wa Mungu huona yote. Sikuwa nimewahi kushiriki hisia zangu za ndani na mtu yeyote, lakini zilifichuliwa kikamilifu katika maneno ya Mungu. Nilielewa kutoka kwa maneno ya Mungu kwamba Anataka tumpe mioyo yetu. Iwe tunafanya wajibu wetu katika nyumba ya Mungu au kushughulikia masuala yetu, lazima tutende maneno Yake. Lakini nilikuwa nikitenda ukweli katika maisha yangu wakati mwingine. Niliona kwamba Mungu na kina ndugu walipenda nilipotia kuwa mwaminifu katika vitendo kanisani, hivyo nilikuwa tayari kufanya hivyo. Lakini katika biashara yangu, nilidhani kwamba nitapoteza pesa na kufanya hivyo hakutafaidi masilahi yangu, kwa hivyo sikufanya hivyo. Niliona kwamba nilikuwa nimezingatia tu masilahi yangu ya kibinafsi, na kwamba nilikuwa nikiyatelekeza maneno ya Mungu na mahitaji Yake. Nilijua kwamba kuwa mdanganyifu hakukulingana na mapenzi ya Mungu, lakini bado nilifanya chochote nilichotaka, na chochote kilichofaidi masilahi yangu. Je, huko kulikuwaje kuwa mtu wa imani? Nilianza kwa kweli kufahamu wakati huo. “Kila mwamba ngoma huvutia upande wake” na “Mwanadamu atafanya chochote ili atajirike” ni sheria za kishetani za kuendelea kuishi ambazo zilikuwa zimenitawala na kuwa maisha yangu. Nilikuwa nimefikiri kwamba nisingeishi kulingana nazo, nisingefaulu. Lakini kwa kweli, kwa kuishi kwa njia hiyo, nilipata tu faida ya kibinafsi na starehe ya vitu vya mwili. Lakini ilikuwa njia mbaya ya kuishi, na isiyo na hadhi yoyote. Watu walinichukia na kunikataa kwa dharau, na Mungu alizidi kunichukia na kunidharau. Nilifikiria yale ambayo Bwana Yesu alisema: “Naye akasema, Kweli nawaambia, Ila msipobadilishwa, na kugeuka kama wana wadogo, hamtaingia ndani ya ufalme wa mbinguni(Mathayo 18:3). Na Mwenyezi Mungu asema: “… kwa sababu Siwezi kuwaleta katika ufalme Wangu maadui Wangu na watu waliojawa na maovu kwa mfano wa Shetani, katika enzi ijayo(Neno Laonekana katika Mwili). Mungu ni mtakatifu na mwenye haki, na Anataka kuwapata watu waaminifu. Wale ambao daima husema uongo na kudanganya, wale wenye tabia za kishetani, ambao humpinga Mungu kwa asili na kukataa kutubu wataangamizwa na Mungu. Hawataingia kamwe katika ufalme Wake. Kama singetubu, bali niendelee kuishi kulingana na falsafa na sheria za Shetani, na kuwa mpotovu na kutenda udhalimu, ningeishia kuondolewa. Nilipofikiria hayo nilimwomba Mungu haraka. “Mwenyezi Mungu! Nakuamini, lakini Wewe hujakuwa na nafasi moyoni mwangu. Bado nimekuwa nikiishi kulingana na sheria za Shetani. Sitaki kuwa mdanganyifu tena. Nataka kutubu na kuwa mtu mwaminifu.”

Wakati mmoja baadaye, vijana kadhaa walileta runinga katika duka langu ili ikarabatiwe. Nilipokuwa nikiirekebisha, niliwasikia wakizungumza kule nje kwa utulivu: “Tungalijua mahali hapo si pazuri, tungaliokoa hizo siku mbili. Hebu tuone kama huyu jamaa ataweza kuirekebisha.” Niliposikia haya, niliwaza “Kama wamiliki wengine wa maduka wangesikia hayo, wangewatoza fedha nyingi, kwa hivyo naweza kuwatoza yuani 20 au 30 zaidi kwa urahisi. Litakuwa jambo la kusikitisha kutokuchukua pesa zinazonijia kwa ghafla. Naweza kuwa mtu mwaminifu wakati ujao. Mungu hatalalamika kwa sababu sitendi ukweli mara hii moja tu.” Lakini baadaye nilikumbuka nilichokuwa nimeamua mbele za Mungu, na nilikumbuka maneno ya Mungu: “Ikiwa mtu hapendi ukweli, na mara nyingi nafanya vitu kulingana na mapenzi yake, basi atamkosea Mungu mara kwa mara. Watu kama hao kwa kawaida hawakubaliwi na Mungu katika yale wayatendayo, na wasipotubu, basi adhabu haitakuwa mbali sana nao(Kumbukumbu za Hotuba za Kristo). Nilihisi kwamba ni Mungu aliyekuwa Akinionya. Sikustahili kuendelea kutenda maovu kwa makusudi. Ilinibidi nitubu na kuwa mtu mwaminifu. Na kwa hivyo, nilitoza tu ada ya kawaida baada ya kuirekebisha. Nilipoona tabasamu za furaha kwenye nyuso za wateja wale nilihisi kwamba kuwa wazi na kutoficha chochote kulikuwa kuishi kwa uhuru.

Wakati mwingine nilipotengeneza runinga ya mwanamke fulani, ada ya kutengeneza ilikuwa yuani 50, lakini alinipa 100 na hakutaka chenji. Nilikataa, hata hivyo, nilikanganyikiwa. Kwa nini alikuwa mkarimu sana? Kisha akaniambia, “Mtu wa kwanza niliyemwendea alisema kwamba bodimama ilikuwa imeharibika na yuani 400 zilihitajika ili kuibadilisha, lakini sikubadilisha. Mtu mmoja ninayemjua alikusifia baadaye, akisema kwamba ulikuwa mwaminifu na hukuwatoza wateja pesa nyingi zaidi. Sasa naona kwamba huo ni ukweli kabisa.” Nilipomsikia akisema hivi, niliwaza, “Si kwamba mimi ni mtu mzuri hata kidogo, ni kwamba maneno ya Mungu yalinibadilisha ili niweze kuishi kwa kudhihirisha mfano wa binadamu.”

Mtazamo wangu kwa mambo pia ulibadilika kutokana na kusoma maneno ya Mungu na kutenda kuwa mtu mwaminifu. Nilikuwa nikifikiri kwamba kuwa mfanyabiashara mwaminifu hakuwezekani, kwamba huwezi kuchuma pesa, kwamba utapata hasara na utalazimika kuifunga. Lakini baada ya kuanza kuwa mwaminifu kulingana na maneno ya Mungu, mbali na kutopata hasara, pia nilipata wateja zaidi kila siku. Wengine hata walitoka mbali sana, wote wakisema kwamba walikuwa wameshauriwa na mtu fulani. Sikuwa nimefanya matangazo ya kibiashara kwa njia yoyote au kuwaomba wengine waitangaze biashara yangu. Ni kwa sababu tu nilitenda maneno ya Mungu, kwa sababu nilikuwa mwaminifu na nilikuwa mwadilifu kama Mungu anavyotaka, na nilipata tu pesa kwa njia ya uaminifu, wateja waliniamini. Kwa kweli ilikuwa baraka ya Mungu iliyotokana na kutenda ukweli. Hii inanikumbusha kifungu kingine cha maneno ya Mungu. Mwenyezi Mungu anasema, “Wakati watu wanaishi katika dunia hii chini cha ushawishi wa Shetani, haiwezekani kwa wao kuwa waaminifu; wanaweza kuwa wadanganyifu zaidi tu. Hata hivyo, tunaweza au hatuwezi kuishi katika ulimwengu huu ikiwa tutakuwa waaminifu? Je, tutatengwa na wengine? Hapana; tutaishi kama zamani. Hii ni kwa sababu hatutegemei ujanja kula au kupumua. Badala yake, tunaishi kwa kutegemea pumzi na uzima tuliopewa na Mungu. Ni kwamba tu tumekubali ukweli wa maneno ya Mungu na tuna sheria mpya za jinsi ya kuishi, na malengo mapya ya maisha, ambavyo vitasababisha mabadiliko katika msingi wa maisha yetu; ni kwamba tunabadilisha njia na namna ambavyo tunaishi ili tuweze kumridhisha Mungu na tutafute wokovu. Hili halihusiani kabisa na kile tunachokula kimwili, kile tunachovaa, au kule tunakoishi; hili ni hitaji letu la kiroho(Kumbukumbu za Hotuba za Kristo). Shukrani kwa Mungu!

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Maudhui Yanayohusiana

Uzinduzi wa Kiroho wa Mkristo

Na Lingwu, Japani Mimi ni mtoto wa miaka ya themanini, na nilizaliwa katika kaya ya kawaida ya mkulima. Kakangu mkubwa alikuwa mgonjwa na...

Kuinuka licha ya kushindwa

Na Fenqi, Korea ya Kusini Kabla ya kumwamini Mungu, nilifundishwa na CCP, na sikufikiria chochote ila jinsi ya kufaulu kutokana na juhudi...

Leave a Reply

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp