Jaribu la Foili

24/01/2021

Na Xingdao, Korea ya Kusini

Ee Mungu! Kama nina hadhi au la, sasa ninajielewa mwenyewe. Hadhi yangu ikiwa juu ni kwa sababu ya kuinuliwa na Wewe, na ikiwa iko chini ni kwa sababu ya mpango Wako. Kila kitu ki mikononi Mwako. Sina chaguzi zozote, wala malalamishi yoyote. Ulipanga kwamba ningezaliwa katika nchi hii na miongoni mwa watu hawa, na yote ninayopaswa kufanya ni kuwa mtiifu kabisa chini ya utawala Wako kwa sababu kila kitu ki ndani ya yale ambayo Umepanga. Sifikirii kuhusu hadhi; hata hivyo, mimi ni kiumbe tu. Ukiniweka kwenye shimo lisilo na mwisho, katika ziwa la moto wa jahanamu, mimi si chochote isipokuwa kiumbe. Ukinitumia, mimi ni kiumbe. Ukinikamilisha, mimi bado ni kiumbe. Usiponikamilisha, bado nitakupenda kwa sababu mimi si zaidi ya kiumbe. Mimi si chochote zaidi ya kiumbe mdogo sana aliyeumbwa na Bwana wa uumbaji, mmoja tu miongoni mwa wanadamu wote walioumbwa. Ni Wewe uliyeniumba, na sasa kwa mara nyingine tena Umeniweka katika mikono Yako ili unitumie Utakavyo. Niko tayari kuwa chombo Chako na foili Yako kwa sababu vyote ni vile Umepanga. Hakuna anayeweza kubadili jambo hilo. Vitu vyote na matukio yote yako katika mikono Yako(“Mimi ni Kiumbe Mdogo Sana tu Aliyeumbwa” katika Mfuateni Mwanakondoo na Kuimba Nyimbo Mpya). Ningependa kufanya ushirika juu ya jaribu langu mwenyewe kama foili.

Mwanzoni mwa 1993, nilikuwa na wajibu wa kuwanyunyizia waumini wapya kanisani. Tulikuwa katika hatari ya kukamatwa popote tulipoenda kwa sababu ya mateso makali na kukamakwa kwa Wakristo na serikali ya CCP. Licha ya mazingira magumu, sikuwahi kusita bali niling’ang’ania kufanya wajibu wangu. Nilisoma maneno haya ya Mungu, “Ni wale tu ambao wanampenda Mungu wanaweza kumshuhudia Mungu, ndio tu mashahidi wa Mungu, ndio tu wamebarikiwa na Mungu, na ndio tu wanaweza kupokea ahadi za Mungu(Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Wanaompenda Mungu Wataishi Milele Katika Mwangaza Wake). Kisha nikahisi kwamba nilijawa na imani ya kufuatilia kuwa mtu anayempenda Mungu. Nilidhani ufuatiliaji kama huo ungepata kibali cha Mungu na bila shaka ningeingia mbinguni na kuwa mmoja wa watu wa ufalme Wake.

Nilipokuwa tu nikijitumia kwa shauku huku nikiwa na hakika kwamba ningepelekwa katika ufalme wa Mungu, Mwenyezi Mungu alionyesha maneno ambayo yaliniingiza katika jaribu la foili. Siku moja mnamo Machi, ndugu zetu walilitumia kanisa letu matamshi mapya ya Mungu, “Ukweli wa Ndani wa Kazi ya Ushindi (1).” Nilisoma katika maneno ya Mungu: “Leo, Ninafanya kazi miongoni mwa watu wateule wa Mungu walio Uchina kufichua tabia zao zote za uasi na kuufunua ubaya wao wote, na hili linatia muktadha wa kusema kila Ninachotaka kusema. Baadaye Nitafanya hatua nyingine ya kazi ya kuushinda ulimwengu wote. Nitatumia hukumu Yangu kwenu kuhukumu udhalimu wa kila mtu duniani kote kwa sababu ninyi watu ndio wawakilishi wa waasi miongoni mwa wanadamu. Wasiojikakamua watakuwa foili[a] na vyombo vya kuhudumu tu, ila watakaojikakamua watatumika vizuri. Ni kwa nini Ninasema watakuwa foili? Ni kwa sababu maneno na kazi Yangu ya sasa vinalenga usuli wenu na kwa sababu mmekuwa wawakilishi na vielelezo vya uasi miongoni mwa wanadamu. Baadaye Nitapeleka maneno haya yanayowashinda kwa nchi za kigeni na kuyatumia kuwashinda watu wa huko, ila hutakuwa umeyafaidi. Je, hilo halitakufanya foili? Tabia potovu za wanadamu wote, matendo ya uasi wa mwanadamu, maumbile na sura mbaya za mwanadamu, zimeratibiwa zote katika maneno yanayotumiwa kuwashinda nyinyi. Baadaye Nitayatumia maneno haya kuwashinda watu wa kila taifa na kila dhehebu kwa sababu nyinyi ni mfano, kigezo. Hata hivyo, Sikupanga kuwaacha kwa makusudi; ukikosa kufanya vizuri katika utafutaji wako na kwa hivyo unathibitisha kuwa asiyeponyeka, hautakuwa tu chombo cha huduma na foili? Wakati mmoja Nilisema kwamba hekima Yangu hutumiwa kutegemea njama za Shetani. Kwa nini Nilisema hilo? Je, huo si ukweli unaounga mkono Ninachosema na kufanya wakati huu? Kama huwezi kuchukua hatua, kama hujakamilishwa lakini badala yake unaadhibiwa, je, hutakuwa foili? Labda umeteseka sana katika wakati wako, lakini sasa bado huelewi chochote; hujui kila kitu kuhusu uzima. Ingawa umeadhibiwa na kuhukumiwa, hujabadilika kamwe na ndani yako kabisa hujapata uzima. Wakati wa kutathmini kazi yako utakapofika, utapitia majaribio makali kama moto na hata majonzi makuu zaidi. Moto huu utageuza nafsi yako yote kuwa majivu. Kama mtu asiyekuwa na uzima, mtu asiye na aunsi ya dhahabu safi ndani yake, mtu ambaye bado amekatalia tabia potovu ya kale, na mtu asiyeweza hata kufanya kazi nzuri ya kuwa foili, ni jinsi gani hutaweza kuondoshwa?(Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Ukweli wa Ndani wa Kazi ya Ushindi (1)). Niliathirika sana nilipoona neno “foili” likitajwa mara kwa mara katika maneno ya Mungu. Niliwaza, “Foili? Mungu alitaja foili katika maneno Yake hapo awali, lakini, je, hilo halikuwa likihusu joka kubwa jekundu? Mimi hujitolea kwa ajili ya Mungu katika imani yangu na mimi hutafuta kumpenda. Napaswa kuwa mmoja wa watu wa ufalme Wake. Nawezaje kuwa foili?” Nilisoma maneno ya Mungu tena na kwa makini sana. Mungu alisema kwamba sisi Wachina ni watu waliopotoshwa sana, kwamba upinzani wetu kwa Mungu ni mbaya zaidi, na sisi ni wawakilishi wa uasi wote wa wanadamu. Wafuasi wa Mungu wasipoishia kubadilika, ikiwa hawajapata uzima, watahudumu kama foili kwa ajili ya kazi ya Mungu na wote wataondolewa na Mungu. Nilishtuka sana niliposoma haya na nikajiuliza, “Je, mimi ni foili? Hilo haliwezekani. Iwapo mimi kweli ni foili, bado naweza kuingia katika ufalme wa mbinguni?”

Muda mfupi baadaye, nilisoma ushirika huu kutoka kwa Mungu: “Kwa sababu nyinyi si waaminifu na ni wadanganyifu, na kwa sababu mnakosa ubora wa tabia na nyinyi ni wa hadhi ya chini, kamwe hamjawahi kuwa karibu na macho Yangu au katika moyo Wangu. Kazi Yangu inafanywa kwa kusudi la kuwahukumu tu; mkono Wangu kamwe haujawahi kuwa mbali nanyi, wala kuadibu Kwangu. Nimeendelea kuwahukumu na kuwalaani. Kwa sababu hamna ufahamu Wangu, ghadhabu Yangu daima imekuwa juu yenu. Ingawa daima Nimefanya kazi miongoni mwenu, mnapaswa kujua mtazamo Wangu kuwaelekea. Si chochote ila maudhi—hakuna mtazamo au maoni mengine. Ninataka tu mtende kama foili kwa ajili ya hekima Yangu na uwezo Wangu mkubwa. Nyinyi si kitu zaidi ya foili Wangu kwa sababu haki Yangu inafichuliwa kupitia uasi wenu. Ninawataka mtende kama foili kwa ajili ya kazi Yangu, kuwa viambatisho vya kazi Yangu….(Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Mbona Huna Hiari ya Kuwa Foili?). Niliona kwamba Mungu anasema waziwazi kuwa sisi ni foili, kwamba sisi ni viambatisho vya kazi Yake na Anahisi chuki na kinyongo kabisa juu yetu. Nilishtuka na kuhisi kwamba nilikuwa nimetelekezwa na Mungu. Nilitaabika sana na malalamiko yakaibuka ndani yangu. Niliwaza, “Nimeamini miaka hii yote, nimeacha familia na kazi yangu na nimeteseka sana huku nikijitumia kwa ajili ya Mungu. Nimepitia jaribu la kifo na jaribu la watendaji huduma. Sasa nimeanza kufuatilia kumpenda Mungu, nikifikiri kwamba bila shaka nitakuwa mtu wa ufalme. Sikuwahi kufikiria kwamba nitakuwa foili, kitu cha kutumikia na cha kuondolewa mara nitakapomaliza kuwa utumbuizo wa tabia ya Mungu yenye haki. Basi nimekuwa nikilipa gharama ya nini katika miaka hii yote? Je, jamaa na marafiki zangu watanionaje wakijua? Hakuweza kuelewa nilipoacha kazi na familia yangu kwa ajili ya imani yangu. Walinidhihaki. Nilitaka kuwa muumini mzuri ili mara kazi ya Mungu itakapomalizika na maafa makubwa yatakapokuja, nitapelekwa katika ufalme Wake. Wakati huo nitaweza kujiona na wote wataaibishwa. Je, nani angefikiri kwamba ningeishia kuwa duni sana kama vile foili? Foili hawana uzima. Wao hawana thamani na hata si wa maana kama watendaji huduma. Angalau watendaji huduma wanaweza kumhudumia Mungu kwa muda fulani na kufurahia neema na baraka Zake. Hata kuwa mtendaji huduma kungekuwa sawa. Kwa hali yoyote ile, kunaonekana bora kuliko kuwa foili.”

Neno “foili” liliendelea kujirudia akilini mwangu kwa siku chache zilizofuata, na sikuweza kuacha kujiuliza, “Je, nawezaje kuwa foili tu? Kwa nini nilizaliwa China? Joka kubwa jekundu lisingewapotosha Wachina mno, kamwe nisingekuwa foili! Nilidhani kwamba nilikuwa karibu kuingia katika ufalme wa Mungu na kuwa mmoja wa watu wa ufalme ili kufurahia ahadi za Mungu. Sikuwahi kufikiri kwamba nitaishia kuwa foili badala yake.” Kadiri nilivyozidi kufikiri juu ya hayo ndivyo nilivyozidi kufadhaika na sikuweza kuacha kulia. Niliona kwamba kwa kuwa hivyo ndivyo hali ilivyokuwa, sikuwa na budi kukubali kudura yangu bila kulalamika.

Baada ya hayo, hata ingawa niliendelea kuhudhuria mikutano na kufanya wajibu wangu, sikuwa na shauku. Sikuwa na lolote la kumwambia Mungu katika sala na sikuwa na shauku ya kuimba. Sikupata nuru yoyote kutoka katika maneno ya Mungu. Nilihisi kwamba kwa kuwa nilikuwa foili, hakukuwa na sababu ya kufuatilia zaidi kwa kuwa ningeishia kutupwa nje, kuondolewa na kutupwa ndani ya shimo lisilokuwa na mwisho. Nilikuwa hasi na nilifadhaika sana. Jioni moja nilipokuwa kitandani bila usingizi, nilitafakari maneno hayo yote yaliyotamkwa na Mungu katika kazi Yake katika siku za mwisho ambayo yalikuwa yakitunyunyizia na kuturuzuku, na majaribu na usafishaji ambao ulikuwa ukitutakasa. Nilitafakari sana jaribu la watendaji huduma. Wakati huo, ingawa Mungu aliondoa matarajio yetu ya mwili na kutuhukumu kwenda katika shimo lisilokuwa na mwisho, hilo lilikuwa jaribu la maneno na mambo haya kwa kweli yakutufika. Ilikuwa kupitia katika jaribu hilo ndiyo nilielewa kiasi kwamba motisha yangu ya kuamini ilikuwa kupokea baraka na nikapitia tabia kiasi ya Mungu yenye haki. Niliona kwamba bila kujali Mungu anafanya kazi gani, yote hufanywa ili kututakasa na kutuokoa. Nilikumbuka pia jinsi nilivyokuwa nimeamua mbele za Mungu kwamba nilifurahia kumhudumia. Nilijilaumu kidogo na nikapata motisha kiasi, na nikawaza, “Iwe kwamba mimi ni mtendaji huduma au foili, kufanya wajibu wangu kwa ajili ya Muumba ni sawa na sahihi, na bila kujali Mungu atapanga nini katika siku zijazo, hata nisipokuwa na matokeo mazuri baada ya huduma yangu, bado nitamhudumia mpaka mwisho.” Na kwa hivyo, niliendelea kutekeleza wajibu wangu. Lakini kwa kuwa sikuelewa mapenzi ya Mungu, kila nilipofikiri juu ya kuwa foili bila kupata uzima au matokeo mazuri, bado nilihisi vibaya na kufadhaika.

Mwanzoni mwa Aprili tulipokea matamshi mengine mapya ya Mungu. Nilisoma haya katika maneno ya Mungu: “Katika kutafuta kwenu, mna dhana, matumaini, na siku za baadaye nyingi sana za kibinafsi. Kazi ya sasa ni ili kushughulikia tamaa yenu ya hadhi na tamaa zenu badhirifu. Matumaini, hadhi, na dhana yote ni mifano bora kabisa ya tabia ya kishetani. Sababu ambayo vitu hivi vipo katika mioyo ya watu ni kwa sababu hasa sumu ya Shetani daima inaharibu fikira za watu, na daima watu hawawezi kuondoa vishawishi hivi vya Shetani. Wanaishi katikati ya dhambi ilhali hawaiamini kuwa dhambi, na bado wao huwaza: ‘Tunaamini katika Mungu, hivyo lazima Atupe baraka na kupanga kila kitu kwa ajili yetu ipasavyo. Tunaamini katika Mungu, hivyo lazima tuwe wa cheo cha juu kuliko wengine, na lazima tuwe na hadhi zaidi na maisha zaidi ya baadaye kuliko mtu mwingine yeyote. Kwa kuwa tunaamini katika Mungu, lazima Atupe baraka bila kikomo. Vinginevyo, hakungeitwa kuamini katika Mungu.’ Kwa miaka mingi, mawazo ambayo watu wametegemea kwa ajili ya kuendelea kuishi kwao yamekuwa yakiharibu mioyo yao hadi kiwango ambapo wamekuwa wadanganyifu, waoga, na wenye kustahili dharau. Hawakosi tu ushupavu na uamuzi, lakini pia wamekuwa walafi, wenye kiburi, na wa kudhamiria. Kabisa wanakosa uamuzi wowote upitao sana ubinafsi, na hata zaidi, hawana ujasiri hata kidogo wa kuondoa shutuma za ushawishi huu wa giza. Fikira na maisha ya watu ni mabovu sana kiasi kwamba mitazamo yao juu ya kuamini katika Mungu bado ni miovu kwa namna isiyovumilika, na hata watu wanaponena kuhusu mitazamo yao juu ya imani katika Mungu haivumiliki kabisa kusikia. Watu wote ni waoga, wasiojimudu, wenye kustahili dharau, na dhaifu. Hawahisi maudhi kwa nguvu za giza, na hawahisi upendo kwa nuru na ukweli; badala yake, wanafanya kila wanaloweza kuvifukuza(Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Mbona Huna Hiari ya Kuwa Foili?). Maneno ya Mungu yaliniumiza sana. Yalifunua kabisa tabia yangu ya kishetani na mawazo yangu mwenyewe ya kuendelea kuishi kwangu. Nilihisi aibu sana. Nilikumbuka jinsi ambavyo hapo mwanzoni, niliamini ili kupata baraka tu. Niliwaza, “Kwa kuwa tunaamini katika Mungu, lazima Atupe baraka bila kikomo. Vinginevyo, hakungeitwa kuamini katika Mungu.” Baada ya kupitia majaribu ya kifo na ya watendaji huduma, nilianza kuelewa nia zangu za kupata baraka na nikawa tayari kumtumikia Mungu, lakini ndani kabisa ya moyo wangu, tamaa hiyo ya baraka bado ilikuwa imekita mizizi na haikuwa imetakaswa kikamilifu. Hasa nilipoona ahadi ya Mungu ya baraka kwa wale wanaompenda, tamaa yangu ya baraka ilichochewa tena. Nilidhani kwamba, hakika nitaingia katika ufalme wa mbinguni wakati huu, kwa hivyo nilijitumia kwa ajili ya Mungu kwa ari hata zaidi. Lakini Mungu alipotufunua kama foili, kama viambatisho na walengwa wa chuki Yake, nilihisi kwamba matumaini yangu ya kupata baraka yalikuwa yamevunjwa na kwamba sikuwa na mategemeo au hadhi tena. Nilihisi kwamba nilikosewa sana na nilijawa na malalamiko. Nilichukulia kujitolea kwangu na kujitahidi kwangu kama mtaji ambao ningetumia kufanya mapatano na Mungu, ili kupata kibali cha bure kutoka kwa Mungu cha kuingia katika ufalme Wake, vinginevyo sikuwa tayari kuendelea kujitumia. Wakati huo tu ndipo nilipogundua jinsi shauku yangu ya hadhi na tamaa zangu za kupita kiasi zilivyokuwa kubwa. Sikumpenda wala kumtii Mungu hata kidogo. Yote niliyofanya yalikuwa tu mapatano ya kibiashara, uasi na udanganyifu. Nilipokabiliwa na ukweli huo, niliridhika kabisa. Niliona jinsi nilivyokuwa nimepotoshwa sana na Shetani. Nilikuwa fidhuli, mpotovu, mbinafsi na nilistahili dharau na sikuwa na dhamiri wala mantiki hata kidogo. Pia, niliiona tabia ya Mungu takatifu na yenye haki, ambayo haivumilii kosa lolote. Mtu mpotovu kama mimi, aliyetiwa doa na nia nyingi sana na tabia potovu ningekosaje kumchukiza Mungu? Jina lolote ambalo Mungu ataniita na vyoyote Atakavyonitendea ni haki.

Baadaye, nilisoma maneno haya ya Mungu katika mkutano mmoja: “Kumbuka yale ambayo umepitia katika kipindi hiki cha wakati, na angalia tena maneno ambayo Nimeonyesha katika wakati huu, na uyalinganishe na yale ambayo umefanya. Ni kweli kabisa kuwa wewe ni foili kabisa! Je, kiwango cha ufahamu wako ni kipi leo? Fikira zako, mawazo yako, tabia yako, maneno na matendo yako—si kila kitu unachoonyesha katika namna unavyoishi ni foili kwa haki na utakatifu wa Mungu? Si kile kinachofunuliwa katika maneno ya leo ni tabia potovu ya mwanadamu? Fikira zako, motisha yako—yote ambayo yamefunuliwa ndani yako yanaonyesha tabia ya Mungu yenye haki na utakatifu Wake. Mungu pia Alizaliwa katika nchi ya uchafu, lakini Anabaki kutopakwa matope na uchafu. Anaishi katika ulimwengu huo huo mchafu kama wewe, lakini Anayo mantiki na utambuzi, naye huchukia uchafu. Huenda usiweze hata kugundua kitu chochote kilicho kichafu katika maneno na vitendo vyako, lakini Yeye anaweza, na Yeye hukuonyesha kitu hicho. Mambo hayo yako ya zamani—ukosefu wako wa ukuzaji, utambuzi, na akili, na njia zako za kuishi za kuelekea nyuma—sasa vimedhihirishwa na ufunuo wa leo; ni kwa Mungu kuja duniani kufanya kazi tu ndipo watu wanaona utakatifu Wake na tabia Yake yenye haki(Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Jinsi Athari za Hatua ya Pili ya Kazi ya Ushindi Zinavyotimizwa). “Bila shaka, Mungu hawafanyi muwe foili bila sababu. Badala yake, ni wakati tu kazi hii inapozaa matunda ndipo inapodhihirika kwamba uasi wa mwanadamu ni foili kwa tabia ya Mungu yenye haki, na ni kwa sababu tu ninyi ni foili ndiyo mna fursa ya kujua onyesho asili la tabia ya Mungu yenye haki. Mnahukumiwa na kuadibiwa kwa sababu ya uasi wenu, lakini ni uasi wenu pia unaowafanya muwe foili, na ni kwa sababu ya uasi wenu ndiyo mnapokea neema kubwa ambayo Mungu huwapa. Uasi wenu ni foili kwa kudura na hekima ya Mungu, na pia ni kwa sababu ya uasi wenu ndiyo mmepata wokovu na baraka nyingi kama hizo. Ingawa mmehukumiwa nami mara kwa mara, mmepokea baraka nyingi sana ambazo hazijawahi kupokelewa na mwanadamu. Kazi hii ni ya muhimu sana kwenu. Kuwa ‘foili’ pia ni yenye thamani sana kwenu: Mmekombolewa na kuokolewa kwa sababu ninyi ni foili, kwa hiyo foili kama huyo si wa thamani kubwa sana? Je, si mwenye umuhimu mkubwa sana? Ni kwa sababu ninyi mnaishi katika ulimwengu uleule, nchi hiyo hiyo chafu, sawa na Mungu, kwamba ninyi ni foili na mnapokea wokovu mkubwa zaidi. Mungu asingekuwa mwili, ni nani angekuwa na huruma kwenu, na ni nani angewatunza, watu duni kama ninyi? Nani angewajali? Mungu asingekuwa mwili ili Afanye kazi miongoni mwenu, mngepokea lini wokovu huu ambao wale waliokuwa kabla yenu hawakuwahi kuupata? Nisingekuwa mwili ili Niwajali, Nihukumu dhambi zenu, je, si mngelikuwa mmeanguka kuzimu kitambo? Nisingekuwa mwili na kujinyenyekeza miongoni mwenu, mngewezaje kustahili kuwa foili kwa tabia ya Mungu yenye haki? … Ingawa Nimetumia ‘foili’ kuwashinda, mnapaswa kujua kwamba wokovu na baraka hii imetolewa ili kuwapata; ni kwa ajili ya ushindi, lakini pia ni ili Niweze kuwaokoa vyema zaidi. ‘Foili’ ni ukweli, lakini sababu ambayo ninyi ni foili ni kwa sababu ya uasi wenu, na ni kwa sababu ya jambo hili ndiyo mmepata baraka ambazo hakuna mtu amewahi kupata. Leo mnasababishwa kuona na kusikia; kesho mtapokea, na zaidi ya hayo, mtabarikiwa sana. Kwa hiyo, foili si wenye thamani kubwa sana?(Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Jinsi Athari za Hatua ya Pili ya Kazi ya Ushindi Zinavyotimizwa). Maneno ya Mungu yalinionyesha maana ya kuwa foili. Tulizaliwa nchini China, kwa hivyo tumeelimishwa, tumeshawishiwa na kupotoshwa na joka kubwa jekundu kwa miaka mingi. Tumejawa na falsafa za kishetani, imani kwamba hakuna Mungu, nadharia ya mageuko na dhana nyingine za uwongo. Mawazo yetu yote ni maovu na ni kinyume cha ukweli. Lakini hatutambui hayo, badala yake tunafikiri kwamba sisi ni watu wazuri na kwamba tunalingana na mapenzi ya Mungu. Mwenyezi Mungu hufunua vikali tabia zetu zote za kishetani kama vile kiburi, ujanja, ubinafsi, ulafi na uovu na kisha Yeye hutuaminisha kabisa kwa kufichua ukweli. Mungu anapoonyesha ukweli ili kuhukumu na kufunua upotovu wetu, tabia Yake yenye haki ya kuchukia dhambi na maovu hujionyesha kwa kawaida. Tunaona utakatifu Wake na tabia Yake yenye haki ambayo haivumilii kosa lolote, kisha upotovu na uovu wetu unakuwa foili ya tabia ya Mungu yenye haki. Niliona pia upendo na wokovu wa wanadamu katika maneno ya Mungu, hasa Aliposema, “Mungu asingekuwa mwili, ni nani angekuwa na huruma kwenu, na ni nani angewatunza, watu duni kama ninyi? Nani angewajali?” Maneno hayo yalinigusa sana. Nilipokuwa nikitafakari maneno ya Mungu, niligundua kwamba Mungu hajatutupa au kutuondoa kwa sababu ya uchafu na upotovu wetu, lakini badala yake, Ametuonea huruma sisi ambao tumepotoshwa na kuharibiwa sana na Shetani. Yeye binafsi Alipata mwili ili kutuokoa, Akapitia aibu kubwa zaidi ili kufanya kazi miongoni mwetu akionyesha ukweli ili kutunyunyizia na kuturuzuku, kutuhukumu na kutufunua. Hata ingawa Alitufunua kama foili, mapenzi Yake si kutuondoa, bali ni kutufanya tugundue tamaa yetu ya hadhi na matarajio yetu ya siku zijazo, tujue tabia zetu za kishetani za kiburi, ubinafsi na ulafi ili tuweze kufuatilia ukweli, kuondokana na upotovu na kuokolewa kikamilifu na Mungu. Huu ni upendo wa kweli na wokovu wa Mungu kwetu! Mara nilipofahamu mapenzi ya Mungu, nilikumbuka jinsi ambavyo nilikuwa nikimtendea Mungu na nilitaka ardhi inimeze. Nilikuwa kiumbe mdogo dhaifu, aliyepotoshwa sana na Shetani, mchafu na aliyeshushwa hadhi. Kuweza kutumika kama foili kwa ajili ya Mungu, Aliye juu zaidi na kupata nafasi ya kupitia kazi ya Mungu na kushuhudia haki na utakatifu Wake kulikuwa neema kubwa ya Mungu kwangu! Isingekuwa Mungu kupata mwili, kunena na kufanya kazi miongoni mwetu, je, ningepataje nafasi ya kuelewa ukweli mwingi sana? Je, ningepataje nafasi ya kujua tabia Yake yenye haki? Mbali na kutomshukuru Mungu, pia nilijaribu kubishana na Mungu juu ya kuitwa foili. Sikuwa na mantiki au ubinadamu wowote. Nilipogundua haya, nilihisi jinsi ambavyo nilikuwa nimepotoshwa sana na Shetani na jinsi nilivyokuwa na deni la Mungu. Nilitaka kutubu kwa Mungu na nilitaka kutii mipango ya Mungu bila kujali Anavyoniita, na bila kujali mustakabali na hatima yangu itakuwaje. Nilitaka kufuatilia ukweli na mabadiliko ya tabia.

Kwa kupitia jaribu la foili, nilipata ufahamu kiasi wa nia yangu ya kupata baraka na tabia yangu ya kishetani na nikagundua kwamba bila kujali iwapo nina hadhi ya juu au ya chini, mimi ni kiumbe mdogo tu na ninapaswa kutii yale ambayo Mungu hupanga wakati wote. Hata kama ninamtumikia Mungu kama foili, lazima nisifu haki Yake, nifuatilie ukweli vizuri na nifanye wajibu wangu kama kiumbe. Huo ndio ushuhuda ufaao ambao kiumbe anapaswa kushuhudia.

Tanbihi:

a. “Foili” Mtu/kitu kinachodhihirisha uzuri/ubora wa kingine kwa kuvilinganisha.

Iliyotangulia: Jaribu la Uzao wa Moabu

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Maudhui Yanayohusiana

Mbona Ujihusishe na Hila Unapomtumikia Mungu

Ee Mungu! Asante kwa kufunua asili yangu ya kiburi na majivuno. Kuanzia siku hii na kuendelea, hakika nitachukulia hili kama onyo na kuweka juhudi zaidi katika kujua asili yangu. Nitafanya kazi hasa kulingana na mipangilio ya kazi. Kwa kweli nitakuwa mtu mwenye mantiki, anayezingatia kanuni, na aliye na moyo wa uchaji Kwako.

Leave a Reply

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp