Nahisi Nikiwa Mwepesi Zaidi Baada Ya Kutupilia Mbali Minyororo ya Hadhi

18/10/2019

Na Liang Zhi, Mkoa wa Anhui

Jina langu ni Liang Zhi nami niliukubali wokovu wa Mungu wa siku za mwisho miaka sita iliyopita. Wakati mmoja, wakati wa uchaguzi wa kidemokrasia katika kanisa letu, nilichaguliwa kuwa kiongozi wa kanisa, na nikaiona habari hii kama isiyotarajiwa na ya kufurahisha. Niliwaza moyoni: “Kuchaguliwa kama kiongozi wa kanisa kati ya ndugu wote na kuwajibika kwa kazi zote za kanisa inaonyesha kuwa mimi ni bora kuliko kila mtu mwingine!” Wakati nilipofikiria juu ya jambo hili, hisia ya kujihisi bora ilianza kukita mizizi vilindini mwa moyo wangu, nilianza kutembea huku kichwa changu kikiwa kimeinuliwa na nilijawa na nguvu katika mikutano nikiwa pamoja na ndugu. Baada ya muda, hata hivyo, niligundua kuwa yule dada ambaye nilitekeleza wajibu wangu pamoja naye alikuwa na ubora mzuri wa tabia na alishiriki juu ya ukweli kwa njia yenye kuelewa haraka. Aliweza kufahamu chanzo cha shida yoyote ambayo ndugu waliibua na angeweza kushiriki nao juu ya jinsi ya kuisuluhisha na kuwaonyesha njia ya kutenda. Ndugu wote walitaka kumsikia akifanya ushirika, na nilipoona hali hii ikijitokeza, nilianza kumwonea wivu na kumwonea kijicho. Sikutaka kukubali kuwa nilikuwa nimeshindwa na kwa hivyo, kabla ya kila mkutano, nilikuwa nikifanya maandalizi ya uangalifu kuhusianana na hali na shida za ndugu, na nilikuwa nikipiga bongo juu ya jinsi ya kushiriki kwa njia inayoweza kufahamika zaidi, yenye kutoa nuru zaidi kumliko dada yangu. Baada ya kutoa ushirika na kuwaona ndugu wote wakitikisa vichwa vyao kwa kukubali, ningehisi raha na kuridhika sana. Kama ningewaona ndugu zangu wanajibiza kwa njia yenye kuvuvuwaa, ningehisi mwenye kuvunjika moyo na kufadhaika. Baadaye, niligundua kwamba ndugu ambaye nilitekeleza wajibu wangu pamoja na yeye alijua mengi sana juu ya kutengeneza filamu na kwamba alikuwa mzuri katika kutumia kompyuta. Wakati nilipoona kuwa ndugu walikuwa wanamtafuta ili kujadili shida za kitaalamu walizokumbana nazo wakati wa kutengeneza sinema, licha ya kuwa niliyesimamia kanisa letu, nilihisi kama singeweza kusema hata neno moja—sikuhisi nikiwa sehemu ya kikundi hicho. Nilihisi ukosefu wa utulivu na sikuwa na furaha hata kidogo, na niliwaza: “Ndugu humtafuta kila wakati wanapokuwa na shida, kwa hivyo wanafikiri yeye ni bora kuniliko? Ingekuwa vema kama ningeelewa ustadi wa uandaaji wa filamu pia, kwa kuwa ndugu wangekuwa wananitafuta badala yake wakati wowote wanapokuwa na shida.” Na kwa hivyo, kila siku tangu alfajiri hadi machweo nilitafuta habari zinazohusiana na uundaji filamu nami nilisoma kila kitu kuhusu jinsi ya kutengeneza sinema. Wakati tu nilipokuwa nikijitahidi kwa shauku na bidii kwa ajili ya hadhi, shida ziliibuka moja baada ya nyingine katika kazi ya kila kikundi kanisani, na haijalishi jinsi nilivyofanya mikutano au kufanya ushirika, sikufanikiwa. Nilihisi nikiwa na shinikizo kubwa nisiweze kupumua, na moyo wangu uliteseka. Niliwaza: “Ndugu zangu watafikiria nini juu yangu? Je, watafikiria kuwa, licha ya kuwa kiongozi, sina talanta ya kufanya kazi na kwamba sina sifa za kutekeleza wajibu huu hata kidogo? Inaonekana kana kwamba sitaweza kuushikilia wadhifa wa kiongozi kwa muda mrefu zaidi.” Kadiri nilivyofikiria zaidi juu ya jambo hilo, ndivyo nilivyokuwa hasi zaidi na nafsi yangu yote ilihisi kama mpira ulioisha pumzi: nguvu nilizohisi hapo awali zilikuwa zimekwisha. Hatimaye, kwa sababu nilikuwa naishi katika hali ya uhasi wakati wote na nilikuwa nimekuwa mzembe katika kazi yangu, nilikuwa nimeipoteza kazi ya Roho Mtakatifu na sikuwa nimepata chochote halisi katika utendaji wa wajibu wangu, na kwa hivyo nilibadilishwa. Wakati huo, nilihisi kana kwamba nilikuwa nimepoteza sifa zangu zote na nilitaka ardhi inimeze. Wakati huo huo, niliwaza: “Je, ndugu zangu watazungumza watanisengenya na kusema kwamba mimi ni kiongozi wa uwongo, kwamba najitahidi tu kupata umaarufu na faida na kwamba sifanyi kazi yoyote halisi?” Kadiri nilivyofikiria juu ya jambo hili, ndivyo nilivyozidi kuhisi maumivu yakiufunika moyo wangu, kana kwamba sauti nyingi za shutuma zilikuwa zikisikika masikioni mwangu …

Jioni hiyo, nililala juu ya kitanda changu, nikigeuka huku na kule na sikuweza kulala hata chembe. Nilichoweza tu kufanya kilikuwa ni kuomba tena na tena, nikimwita Mungu aniongoze na kunielekeza … Baadaye, niliyaona maneno haya ya Mungu ambayo yanasema: “Katika kutafuta kwenu, mna dhana, matumaini, na siku za baadaye nyingi sana za kibinafsi. Kazi ya sasa ni ili kushughulikia tamaa yenu ya hadhi na tamaa zenu badhirifu. Matumaini, hadhi, na dhana yote ni mifano bora kabisa ya tabia ya kishetani. Sababu ambayo vitu hivi vipo katika mioyo ya watu ni kwa sababu hasa sumu ya Shetani daima inaharibu fikira za watu, na daima watu hawawezi kuondoa vishawishi hivi vya Shetani. Wanaishi katikati ya dhambi ilhali hawaiamini kuwa dhambi, na bado wao huwaza: ‘Tunaamini katika Mungu, hivyo lazima Atupe baraka na kupanga kila kitu kwa ajili yetu ipasavyo. Tunaamini katika Mungu, hivyo lazima tuwe wa cheo cha juu kuliko wengine, na lazima tuwe na hadhi zaidi na maisha zaidi ya baadaye kuliko mtu mwingine yeyote. Kwa kuwa tunaamini katika Mungu, lazima Atupe baraka bila kikomo. Vinginevyo, hakungeitwa kuamini katika Mungu.’ … Sasa nyinyi ni wafuasi, na mmepata ufahamu fulani wa hatua hii ya kazi. Hata hivyo, bado hamjaweka kando tamaa yenu ya hadhi. Wakati hadhi yenu iko juu mnatafuta vizuri, lakini wakati hadhi yenu iko chini hamtafuti tena. Baraka za hadhi daima ziko katika fikira zenu. … Kadiri unavyotafuta zaidi kwa njia hii, ndivyo utakavyovuna kidogo zaidi. Kadiri ilivyo kubwa zaidi tamaa ya mtu ya hadhi, ndivyo itabidi washughulikiwe kwa uzito zaidi na ndivyo watakavyozalimika kupitia usafishaji mkubwa. Watu kama hao hawana thamani kabisa! Lazima wshughulikiwe na wahukumiwe vya kutosha ili waachane na mambo haya kabisa. Mkifuatilia kwa njia hii mpaka mwisho, hamtavuna chochote. Wale ambao hawafuatilii uzima hawawezi kubadilishwa, na wale ambao hawana kiu ya ukweli hawawezi kupata ukweli. Hulengi kufuatilia mabadiliko ya kibinafsi na uingiaji, lakini badala yake unalenga tamaa badhirifu na vitu vinavyozuia upendo wako kwa Mungu na kukuzuia kumkaribia Yeye. Je, vitu hivyo vinaweza kukubadili? Je, vinaweza kukuleta katika ufalme?(Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Mbona Huna Hiari ya Kuwa Foili?).” “Watu wengine daima wana hofu kwamba wengine wataiba maarufu wao na kuwashinda, wakipata utambuzi ilhali wao wenyewe wanatelekezwa. Hili huwasababisha kuwashambulia na kuwatenga wengine. Je, huku si kuwaonea wivu wale walio na talanta? Je, huku si kuwa wabinafsi na wachoyo? Je, mwenendo kama huu si wa binafsi na wa kudharauliwa? Hii ni tabia ya aina gani? Ni ovu! Kujifikiria tu, kuridhisha tu tamaa zako mwenyewe, kutofikiria wajibu wa wengine, na kufikiria tu kuhusu maslahi yako mwenyewe na sio maslahi ya nyumba ya Mungu—watu kama hawa wana tabia mbaya, na Mungu hawapendi. Ikiwa kweli unaweza kufikiria mapenzi ya Mungu, basi utaweza kuwatendea wengine kwa haki. Ukimpa mtu pendekezo lako, na mtu huyo akuzwe kuwa mtu wa kipaji, na hivyo kuleta mtu mmoja mwingine mwenye kipaji katika nyumba ya Mungu, je, hutakuwa umefanya kazi yako vizuri? Je, basi hutakuwa mwaminifu katika kutimiza wajibu wako? Hili ni tendo jema mbele za Mungu, na ndiyo aina ya dhamiri na mantiki ambazo watu wanapaswa kuwa nazo(“Mpe Mungu Moyo Wako wa Kweli, Na Unaweza Kupata Ukweli” katika Kumbukumbu za Hotuba za Kristo). Maneno ya Mungu yalifunua kiini changu cha ndani ambacho kilikuwa katika ufuatiliaji wa hadhi, umaarufu na faida, na nilihisi kusikitishwa sana. Tangu nilipoanza kutekeleza wajibu wa kiongozi wa kanisa, daima nilikuwa nimejitolea kwa shauku na kwa hivyo nilijiamini kuwa mtu ambaye alikuwa katika ufuatiliaji wa ukweli. Lakini sasa kwa kuwa ukweli ulikuwa umefunuliwa kwangu, nikiwa nimekabiliwa na hukumu na kuadibu kwa maneno ya Mungu mwishowe niliona uchafu katika imani yangu katika Mungu. Nilitafakari juu ya jinsi, kila wakati nilipokutana na ndugu zangu ili kushiriki kuhusu maneno ya Mungu, sikufanya hivyo ili kumtukuza Mungu au kumtolea Mungu ushuhuda ili kila mtu aelewe ukweli katika maneno ya Mungu, aelewe mapenzi ya Mungu na ajue jinsi ya kutenda ili aingie katika ukweli wa maneno ya Mungu. Badala yake, nilitumia nguvu zangu zote kufikiria jinsi ya kuwa bora kuliko dada yangu na jinsi ya kuwafanya ndugu wakubaliane nami na kuniheshimu, katika jitihada ya kukuza taswira yangu mwenyewe mioyoni mwao na kuimarisha nafasi yangu zaidi. Nilipoona kwamba ndugu yangu alikuwa na uwezo zaidi kuniliko kitaaluma na kwamba ndugu wote walimtafuta ili wapate ushauri na kushiriki pamoja naye walipokuwa na shida, na sikupata fursa ya kufanya hivyo, basi ningemwonea wivu na kumtenga. Niliogopa kwamba angeiba umaarufu wangu na kuniacha nikiwa bila nguvu yoyote, na kwa hivyo nilijitahidi kujiandaa na maarifa ya kitaalam ili kuimarisha cheo changu. Wakati kanisa lilikuwa na shida ambayo singeweza kusuluhisha, sikuja mbele za Mungu kuomba, sikumtegemea Mungu au kumtazamia Mungu, na sikuutafuta ukweli pamoja na ndugu zangu ili kusuluhisha shida hiyo, lakini badala yake nilishinda kila siku nikihangaishwa na mawazo ya faida na hasara kwa hadhi yangu, nikihofu kwamba kama singefanya kazi vizuri basi ningeshindwa kushikilia cheo changu kama kiongozi. Niliona kwamba sikuwa nikitekeleza wajibu wangu ili kuufuatilia ukweli na kuyaridhisha mapenzi ya Mungu, na sikuwa nikitafuta mabadiliko katika tabia yangu nikiwa natekeleza wajibu wangu. Badala yake, nilikuwa nikiuchukulia wajibu wangu kana kwamba ulikuwa ni kazi na kuuona kama kifaa ambacho ningeweza kukitumia ili kuonekana tofauti na watu wengine na kujitengenezea sifa. Kile nilichowahi kufikiria kuhusu kilikuwa jinsi ya kujionyesha na kujithibitisha, ili nipate heshima na uthamini kutoka kwa kila mtu na kuridhisha maazimio na tamaa yangu ya kuinuka zaidi ya kila mtu mwingine yeyote. Sikuwa nahifadhi matendo mema katika utendaji wa wajibu wangu hata kidogo, lakini badala yake nilikuwa naishi kabisa kwa ajili ya umaarufu, faida na hadhi!

Kisha nilisoma maneno ya Mungu yanayosema: “Ninaamua hatima ya kila mtu si kwa kuzingatia umri, ukubwa, kiwango cha mateso, sembuse kiwango ambacho kwacho anataka huruma, bali kulingana na ikiwa anao ukweli. Hakuna chaguo lingine ila hili. Sharti mtambue kwamba wale wote ambao hawafuati mapenzi ya Mungu wataadhibiwa pia. Huu ni ukweli usiobadilika(Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Tayarisha Matendo Mema ya Kutosha kwa ajili ya Hatima Yako). Baada ya kusoma maneno ya Mungu, nilielewa mapenzi Yake. Mungu anapoamua mwisho wa mtu, Hafanyi hivyo kulingana na jinsi hadhi yake ilivyo ya juu au ya chini, jinsi cheo chake kilivyo kikubwa, amemfanyia Mungu kazi kiasi gani au ameteseka kiasi gani. Badala yake, Mungu huamua mwisho wa mtu kulingana na kama anaufuatilia ukweli na kuupata ukweli au la, na kama maisha yake yamebadilika au la. Nilikuwa nimemwamini Mungu kwa miaka kadhaa lakini sikuwa nimewahi kufanya juhudi yoyote katika kuufuatilia ukweli au kuyafuata maneno ya Mungu. Kinyume na hilo, nilikuwa nikiufuatilia umaarufu, faida na hadhi bila kukoma, na mitazamo niliyoshikilia juu ya kile cha kufuatilia ilikinzana kabisa na kile ambacho Mungu alitaka. Matokeo ya haya yote ni kwamba, ingawa nilikuwa namemwamini Mungu kwa miaka, sikuwa nimeingia katika uhalisi wa ukweli kwa vyovyote na tabia ya maisha yangu haikuwa imebadilika hata kidogo. Katika mikutano, sikuweza kuzungumza juu ya uzoefu wowote au ujuzi wa maneno ya Mungu, lakini mara nyingi nilikuwa nimehubiri tu baadhi ya nyaraka na mafundisho ili kuwadanganya watu. Kwa hivyo nilikuwa nimeipoteza kazi ya Roho Mtakatifu na sikuwa nimefanikisha chochote katika utendaji wa wajibu wangu. Kama ningeendelea kufuata njia mbaya, basi mwishowe ningewekwa wazi na kuondolewa na Mungu, na ningepoteza nafasi yangu ya kuupata wokovu wa Mungu. Ninapofikiria juu ya jambo hilo sasa, niligundua kuwa kubadilishwa ilikuwa hukumu na kuadibu kwa haki kwa Mungu. Mungu alikuwa Amelifanya ili kushughulikia na kutakasa lengo na tamanio ndani yangu ya kujitahidi kwa ajili ya umaarufu na faida, na Alikuwa akinielekeza kwenye njia sahihi ya kuufuatilia ukweli—Mungu alikuwa Ananiokoa! Wakati huo, nilijawa na shukrani kwa Mungu na singejizuia ila kuja mbele ya Mungu kuomba: “Ee Mungu, nakushukuru kwa hukumu na kuadibu Kwako, kwa kuniruhusu nitambue kuwa nilikuwa nikiifuata njia isiyo sahihi na kuona athari hatari za kufuatilia umaarufu, faida na hadhi. Ee Mungu, ninatamani kurudi Kwako, kuacha sifa, faida na hadhi, nami nachagua kuifuata njia ya kuufuatilia ukweli ili niufariji moyo Wako.”

Kwa kipindi cha ibada za kiroho na kutafakari, hali yangu iliimarika polepole na kiongozi wa kanisa akanipangia niwanyunyizie waumini wapya. Nilimshukuru sana Mungu kwa kunipa nafasi ya kutekeleza wajibu wangu, na nikafanya azimio kimya kimya: “Lazima nithamini nafasi hii ya kutekeleza wajibu wangu. Siwezi kufanya makosa yaleyale tena na kufuata njia ya kufuatilia umaarufu, faida na hadhi!” Katika wajibu wangu baada ya hapo, kila nilipokumbana na suala, ningelijadili zaidi na ndugu zangu nami ningewasikiliza na kuchukua maoni yao. Wakati wowote nilipoanza kufichua tabia yangu potovu ya kujitahidi kwa ajili ya umaarufu na faida, ningemwomba Mungu, na kwa makusudi ningeenda kusoma maneno ya Mungu zaidi ambayo yalihusiana na hukumu Yake ya kiini potovu cha mwanadamu, na kisha ningetenda kulingana na maneno Yake. Baada ya kupitia haya kwa kipindi, niliweza kisha kuuacha umaarufu, kupata na hadhi kwa kiasi fulani. Hata hivyo, asili yangu ya kishetani ambayo ilipigania umaarufu na faida na ambayo ilitafuta kuinuka zaidi ya wengine haingeweza kutatuliwa mara moja kwa kuwa na ufahamu kidogo tu. Bado nilihitaji kupitia hukumu na kuadibu zaidi kabla ya kutakaswa na kubadilishwa hatimaye.

Miezi kadhaa baadaye, Mungu alipanga tena mazingira ili kunifunua na kuniokoa. Kwa sababu watu wengi zaidi walikuwa wakiichunguza na kuikubali kazi ya Mungu ya siku za mwisho, na kazi ya kuwanyunyizia na kuwasaidia waumini wapya ilikuwa inazidi kuwa nyingi zaidi na zaidi, kiongozi wetu wa kanisa alisema tulihitajika kuchagua kiongozi wa kikundi atakayewajibikia kupanga kazi hiyo. Niliposikia jambo hili, nilianza kufikiria kwa makini uwezekano huo akilini mwangu: “Kati yetu sote saba katika kikundi hiki, Ndugu Zhang labda ndiye ana uwezo mkubwa wa kufanya kazi. Yeye pia ana hali ya haki, yeye hushiriki juu ya ukweli katika njia ya vitendo na ana uwezo wa kuilinda kazi ya kanisa kwa bidii. Inawezekana kwamba yeye atachaguliwa kuwa kiongozi wa kikundi.” Lakini basi nilifikiri jinsi hapo awali nilivyokuwa kiongozi wa kanisa na jinsi siku zote mimi ndiye niliyempangia Ndugu Zhang mambo ya kufanya. Ikiwa angechaguliwa wakati huu kuwa kiongozi wa kikundi, basi ningelazimika kila wakati kufanya kile alichoniambia nifanye, na hiyo ingeonyesha kuwa nilikuwa na hadhi ya chini kumliko. Na kisha ningewezaje kumtazama mtu yeyote tena? Wakati nilipofikiria kuhusu jambo hii, nilihisi mwenye hasira sana. Wakati siku ambayo tulipasa kumchagua kiongozi wa kikundi chetu ilipofika, sikuwa na budi kuhisi woga na akili yangu ilikuwa ikivurugika kila wakati. Napaswa kumpigia nani kura? Ndugu Zhang? Lakini wakati nilipofikiria jinsi ndugu walimtafuta kila wakati ili kujadili shida zao, nilianza kuhisi wivu kidogo na sikutaka tena kumpigia kura. Labda nijipigie kura? Lakini nilijua kuwa sikuwa na uwezo kama Ndugu Zhang, na kama wale ndugu wengine hawangenipigia kura basi singeweza kuwa kiongozi wa kikundi. Nilihisi udhaifu sana wakati huo, kiasi kwamba wazo baya liliibuka akilini mwangu: “Kama siwezi kuwa kiongozi wa kikundi, basi wewe pia hutakuwa.” Na hivyo, niliishia kumpigia kura Ndugu Wu, ambaye kwa kawaida tulipatana vizuri lakini alikuwa na uwezo mdogo. Mwishowe, hata hivyo, Ndugu Zhang bado alichaguliwa kuwa kiongozi wa kikundi. Sikufurahi kuona matokeo haya, lakini hali ya kutokuwa na utulivu ikifuatia, na nilihisi kana kwamba nimefanya kitu kisichokuwa cha uaminifu kabisa. Nikiwa njiani nikirudi nyumbani siku hiyo, nilitafakari kuhusu mawazo na maoni ambayo nilikuwa nimefichua wakati wa upigaji kura. Mbona sikuwa radhi kumpigia kura Ndugu Zhang? Nilikuwa nameogopa kuwa Ndugu Zhang angeinuka kuniliko. Sikuwa nimezama tena katika hali ya kupigania umaarufu na faida? Nilihisi kufadhaika sana. Sikutaka kupigania umaarufu na faida, hivyo kwa nini kila mara nilirudi katika njia zangu za zamani wakati wowote hali ya aina hii ilipoibuka? Nilimwomba Mungu moyoni mwangu na kumuuliza Anipe nuru na kunielekeza ili niweze kupata chanzo cha tatizo hili. Nilipofika nyumbani, niliyaona maneno haya ya Mungu ambayo yanasema: “Shetani hutumia nini kuendelea kumfungia mwanadamu na kumdhibiti? (Umaarufu na faida.) Kwa hivyo Shetani hutumia umaarufu na faida kudhibiti fikira za mwanadamu hadi anachofikiria tu ni umaarufu na faida. Wanapambana kwa sababu ya umaarufu na faida, wanateseka matatizo kwa sababu ya umaarufu na faida, wanastahimili udhalilishaji kwa sababu ya umaarufu na faida, wanatoa kila kitu walichonacho kwa sababu ya umaarufu na faida, na watafanya maoni au uamuzi wowote kwa ajili ya umaarufu na faida. Kwa njia hii, Shetani humfunga mwanadamu kwa pingu zisizoonekana. Pingu hizi zinabebwa na watu, na hawana nguvu ama ujasiri wa kuzirusha mbali. Kwa hivyo, bila kujua, watu huvumilia pingu hizi na kutembea kwenda mbele kwa ugumu mkubwa. Kwa ajili ya umaarufu huu na faida hii, binadamu humwepuka Mungu na kumsaliti, na wanazidi kuwa waovu zaidi na zaidi. Kwa njia hii, hivyo kizazi kimoja baada ya kingine kinaharibiwa katika umaarufu na faida ya Shetani. Tukiangalia sasa vitendo vya Shetani, nia zake husuda ni za kuchukiza? Pengine leo bado hamwezi kuona kupitia nia husuda za Shetani kwa sababu mnafikiri hakuna maisha bila umaarufu na faida. Mnafikri kwamba, iwapo watu wataacha umaarufu na faida nyuma, basi hawataweza tena kuona njia mbele, hawataweza tena kuona malengo yao, siku zao za baadaye zawa giza, zilizofifia na za ghamu. Lakini, polepole, nyote siku moja mtatambua kwamba umaarufu na faida ni pingu za ajabu ambazo Shetani hutumia kumfunga mwanadamu. Hadi ile siku utakuja kutambua hili, utapinga kabisa udhibiti wa Shetani na utapinga kabisa pingu anazoleta Shetani kukufunga. Wakati utakapofika wa wewe kutaka kutupilia mbali vitu vyote ambavyo Shetani ameingiza ndani yako, utakuwa basi umejiondoa kwa Shetani na pia utachukia kwa kweli vyote ambavyo Shetani amekuletea. Hapo tu ndipo utakuwa na upendo na shauku ya kweli kwa Mungu(Neno, Vol. 2. Kuhusu Kumjua Mungu. Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee VI).

Mtu mwenye moyo wa kumcha Mungu ataonyesha taboa ya aina gani? (Hatafanya tu chochote anachopenda au kutenda anavyotaka.) Kwa hivyo mtu anapaswa kufanya nini ili asije akatenda vile atakavyo? (Kuwa na moyo utafutao.) Watu wengine wanaweza kuhisi kwamba kufikiria kwao si sahihi, lakini pia wanahisi kwamba hawataki kusikia maoni sahihi ya wengine, wakifikiria: ‘Mimi kwa kawaida huwa bora kumliko. Nikisikiliza maoni yake sasa, itaonekana kana kwamba yeye ni bora kuniliko! Hapana, siwezi kumsikiliza katika jambo hili. Nitalifanya tu kwa njia yangu.’ Kisha anapata sababu na kisingizio cha kumtenga mtu huyo mwingine. Wakimwona mtu aliye bora kuwaliko, wanamkandamiza, wanaanzisha uvumi kumhusu, au kutumia njia za uovu ili watu wengine wasimheshimu, na kwamba hakuna mtu aliye bora kuliko mtu mwingine, basi hii ni tabia potovu ya kiburi na yenye kujidai, na vile vile ya uovu, udanganyifu na kudhuru kwa siri, na watu hawa hawazuiwi na chochote katika kufikia malengo yao. Wanaishi namna hii na bado wanafikiria kuwa wao ni wazuri na kwamba wao ni watu wema. Hata hivyo, je, wana mioyo inayomcha Mungu? Kwanza kabisa, kuzungumza kutoka katika mtazamo wa asili za mambo haya, je, watu ambao hutenda hivi hawafanyi vile wapendavyo tu? Je, wao hufikiria masilahi ya familia ya Mungu? Wanafikiria tu kuhusu hisia zao na wanataka tu kufikia malengo yao wenyewe, bila kujali hasara inayopatwa na kazi ya familia ya Mungu. Watu kama hawa sio tu wenye kiburi na wa kujidai, pia ni wabinafsi na wenye kustahili dharau; hawajali kabisa kuhusu kusudi la Mungu, na watu kama hawa, bila shaka yoyote, hawana mioyo inayomcha Mungu. Hii ndiyo sababu wanatenda chochote wanachotaka na kutenda kwa utundu, bila hisia yoyote ya lawama, bila hofu yoyote, bila wasiwasi au shaka yoyote, na bila kuzingatia matokeo. Hawamchi Mungu, wanajiamini kuwa muhimu sana, na wanaona kila kipengele chao kuwa cha juu kumliko Mungu na cha juu kuliko ukweli. Mioyoni mwao, Mungu ndiye wa chini zaidi anayestahili kutajwa na Asiye na maana zaidi, na Mungu hana hadhi yoyote mioyoni mwao hata kidogo(“Masharti Matano Ambayo Watu Wanayo Kabla ya Kuingia Kwenye Njia Sahihi ya Kumwamini Mungu” katika Kumbukumbu za Hotuba za Kristo).

Nilipokuwa nikitafakari maneno ya Mungu, niliwaza nyuma kwa kila kitu nilichokuwa nimefikiria na kufanya katika upigaji kura, na nilihisi aibu isiyoweza kutajika. Nilielewa kwamba umaarufu, faida na hadhi ambavyo nilikuwa nikifuatilia kila wakati kwa kweli vilikuwa minyororo isiyoonekana ambayo Shetani hutumia kutufunga, na kwamba ni njia ambayo kwayo Shetani hutudanganya na kutupotosha! Nilifikiria kuhusu kabla ya kumwamini Mungu, wakati nilikuwa nimetazama maoni na mawazo kama hayo ya Shetani kama “Mtu huacha jina lake nyuma popote akaapo, kama vile bata bukini hutetea popote arukapo,” “Watu daima wanapaswa kujitahidi kuwa bora kuliko watu wao wa hirimu,” “Kadiri unavyoteseka, ndivyo utakavyofanikiwa zaidi,” na “Mtu hujitahidi kwenda juu; maji hububujika kwenda chini” kuwa ukweli wa maisha yangu usiohitaji thibitisho na kuwa semi za kweli. Nilikubali maoni haya ya kishetani na nikavutiwa na mamlaka na hadhi, nikachukua ufuatiliaji wa umaarufu, faida na hadhi na kuinuka zaidi ya wengine kama malengo yangu maishani, na nilipambana na kupigana kwa bidii kwa ajili ya haya. Almradi ningeweza kujipatia umaarufu, faida na hadhi, basi ningeweza kuvumilia kiasi chochote cha mateso au uchovu. Baada ya kuanza kumwamini Mungu, niliendelea kuishi kulingana na hizi sumu za Shetani katika ufuatiliaji wangu wa umaarufu, faida na hadhi na nikatafuta kuinuka zaidi ya watu wengine. Vitu hivi vilikuwa vimekuwa maisha yangu kwa muda mrefu, na vilinifanya nisiweze kujizuia kumwasi Mungu na kumpinga Mungu. Nilijua vizuri kabisa kwamba Ndugu Zhang angeifaidi kazi ya kanisa kama kiongozi wa kikundi, lakini nilimwonea wivu kwa kuwa mwenye uwezo sana na niliogopa kushindwa. Kwa hivyo, ili kudumisha cheo mwenyewe na ufahari wangu mwenyewe, niliamua kwamba ni heri mtu ambaye hafai apate cheo cha kiongozi wa kikundi na kazi ya kanisa ipate pigo kuliko kumpigia kura Ndugu Zhang. Niliona kuwa nilikuwa nakataa kukubali uchunguzi wa Mungu katika vitendo vyangu, kwamba sikuwa na hata chembe ya moyo unaomwogopa Mungu, kwamba nilikuwa tu nazingatia fahari na cheo changu mwenyewe kila nilipokumbana na suala na kwamba sikuwa nikiunga mkono kazi ya kanisa kabisa—ni vipi basi tabia kama hiyo ya ubinafsi na ya kudharauliwa isingeweza kumchukiza Mungu na kumfanya Anichukie kabisa? Nilifikiria juu ya maneno ya Mungu ambayo yanasema, “Dhambi Zitampeleka Mwanadamu Jahanamu,” na nilihisi kuwa nilikuwa katika hali ya hatari sana. Ningeendelea hivyo, basi ningekuwa mtu ambaye Mungu anamchukia, kumkataa na kumwondoa. Wakati huo tu, nilifikiria kuhusu Mafarisayo ambao walikuwa wamempinga Bwana Yesu. Ili kulinda vyeo na mamlaka yao hekaluni, hawakutafuta kuonekana kwa Bwana Yesu au ukweli Aliouonyesha hata kidogo, lakini badala yake walisisitiza tu katika kumpinga na kumshutumu Bwana Yesu, kiasi kwamba hata walimsulibisha msalabani, na kwa hivyo walipitia adhabu na laana ya Mungu. Sasa naona wazi kuwa, katika imani ya mtu kwa Mungu, ikiwa mtu hazingatii kutafuta ukweli na kuingia katika ukweli, lakini badala yake anafuata sifa, faida na hadhi, basi mtu anafuata njia ya Mafarisayo katika uasi wao kwa Mungu! Nilipofikiria kuhusu mambo haya, sikuwa na budi kuogopa kufuata njia mbaya, na niliamua papo hapo kujinasua kutoka kwa pingu na uharibifu wa umaarufu, faida na hadhi, kufuata njia ya kufuatilia ukweli na kutekeleza wajibu wangu kwa uaminifu, na kupata sifa za Mungu.

Baadaye, niliyarudia maneno ya Mungu na kusoma: “Wale ambao wanaweza kutia ukweli katika vitendo wanaweza kukubali uchunguzi makini wa Mungu katika matendo yao. Unapokubali uchunguzi makini wa Mungu, moyo wako unawekwa kuwa sawa. Ikiwa daima unafanya tu mambo kwa ajili ya wengine kuona na hukubali uchunguzi makini wa Mungu, je, una Mungu moyoni mwako? Watu kama hawa hawana moyo unaomcha Mungu. Usifanye mambo kwa ajili yako daima na usiyafikirie masilahi, hadhi na sifa yako mwenyewe kila wakati. Pia usiyafikirie masilahi ya mwanadamu. Lazima kwanza uyafikirie masilahi ya nyumba ya Mungu, na uyape kipaumbele. Unapaswa kuyafikiria mapenzi ya Mungu na uanze kwa kutafakari kama umekuwa mwenye najisi katika utimizaji wa wajibu wako au la, kama umefanya kila uwezalo kuwa mwaminifu, kama umefanya kila uwezalo kutimiza majukumu yako, na kufanya kadiri uwezavyo au la, na vile vile kama umefikiria wajibu wako na kazi ya nyumba ya Mungu kwa moyo wote au la. Lazima uyazingatie mambo haya. Yafikirie mara kwa mara, na itakuwa rahisi kwako kutekeleza wajibu wako. … Aidha, ikiwa unaweza kutimiza wajibu wako, kutenda faradhi na majukumu yako, kuweka kando tamaa zako binafsi, kuweka kando dhamira na nia zako mwenyewe, kufikiria nia ya Mungu na kuweka maslahi ya Mungu na nyumba Yake kwanza, basi baada ya kupitia hili kwa muda, utahisi kwamba hii ni njia nzuri ya kuishi: Ni kuishi kwa uhalisi na kwa uaminifu, bila kuwa mtu wa thamani ndogo au asiye na manufaa, na kuishi kwa haki na heshima badala ya kuwa na mawazo finyu au mchoyo. Utahisi kwamba hivi ndivyo mtu anapaswa kuishi na kutenda. Polepole, tamaa iliyo moyoni mwako ya kufurahisha maslahi yako mwenyewe itapungua(“Mpe Mungu Moyo Wako wa Kweli, Na Unaweza Kupata Ukweli” katika Kumbukumbu za Hotuba za Kristo). Maneno haya yalinionyesha malengo niliyopaswa kuwa nayo na mwelekeo ninaopaswa kuchukua ili niwe mwanadamu. Moyo wangu ulijaa mwanga, na kisha nikajua jinsi ya kutenda kwa njia inayolingana na mapenzi ya Mungu. Baadaye, nilichukua hatua kumwelezea Ndugu Zhang juu ya jinsi nilivyokuwa nikiishi katika hali ya kujitafutia umaarufu na faida bila kukoma, na kuhusu jinsi nilivyokuwa nikimwonea wivu, na pia nikamfichulia nia yangu inayostahili dharau wakati wa upigaji kura. Baada ya kunisikiliza, hakunidharau, lakini badala yake alishiriki nami juu ya ukweli kuhusu hali yangu, na pia alizungumza nami wazi kuhusu uzoefu wake na ufahamu wake. Baada ya ushirika huu, mfarakano wowote kati yetu ulitoweka, na nilihisi hisia kuu ya uhuru na wepesi. Baadaye, wakati wowote nilipokuwa na ugumu katika kazi yangu au nilipokumbana na suala ambalo sikulielewa, kila mara nilikuwa nikimtafuta Ndugu Zhang kwa bidii, na daima angeshiriki nami kwa uvumilivu hadi suluhisho litakapopatikana. Kadiri nilivyozidi kutenda maneno ya Mungu kwa njia hii, ndivyo nilivyohisi uhusiano wangu na Mungu na uhusiano wangu na ndugu wengine ukiwa wa karibu zaidi, na matokeo niliyopata katika wajibu wangu pia yalikuwa bora na bora zaidi. Kwa kweli nilipata kufahamu kuwa kwa kuacha umaarufu, faida na hadhi na kuishi kwa kufuata maneno ya Mungu, na kwa kumgeukia Mungu na kutimiza wajibu wake, basi mtu hubarikiwa na Mungu, na basi mtu anaweza kuishi maisha ya haki na yenye heshima kwa hisia ya amani na uhuru moyoni mwake, na uhusiano wake na Mungu utakuwa wa karibu zaidi na zaidi.

Mnamo Oktoba 2017, uchaguzi wa kila mwaka wa kanisa ulianza tena, na nilipendekezwa kama mgombea wa kuwa kiongozi wa kanisa. Niliposikia habari hii, sikuwa na furaha kama nilivyokuwa nayo wakati mmoja, lakini badala yake nilirekebisha hali yangu ya akili ili nipitie kazi ya Mungu. Kushiriki katika uchaguzi haikuwa kwamba ningejitahidi kuwa kiongozi wa kanisa, lakini badala yake ni kwamba nitimize wajibu wangu kama sehemu ya mchakato huu, kujifunza kutafuta ukweli, na kuchagua mtu anayefaa kuwa kiongozi kulingana na kanuni za kanisa kuhusu kuchagua viongozi. Ikiwa ningechaguliwa kuwa kiongozi, basi ningependa tu kutekeleza wajibu wangu kama kiumbe aliyeumbwa kwa njia ya dhati na ya utaratibu ili kumridhisha Mungu; sikutamani kuwa kama nilivyokuwa zamani, nikijitahidi ili nipate umaarufu na faida na kumsababisha Mungu ahuzunike. Kama singechaguliwa, nisingemlaumu Mungu, lakini ningeendelea kushirikiana na Mungu, nitekeleze wajibu wangu kadri ya uwezo wangu na kutii mipangilio na mipango ya Mungu, kwa maana nilikuwa mmoja wa viumbe wa Mungu na ilikuwa ni wajibu wangu kutekeleza jukumu lolote nililopewa, nami napaswa kufanya hivyo kila wakati kwa moyo wangu wote na nguvu zangu zote. Wakati kura zilipohesabiwa na matokeo kutangazwa, niligundua kuwa nilikuwa nimechaguliwa kuwa kiongozi wa kanisa. Sikujisikia kufurahishwa sana, hata hivyo, na sikuhisi tena kuwa mzuri sana au bora zaidi kuwaliko ndugu wengine. Kinyume na hilo, nilihisi kana kwamba hili lilikuwa agizo na jukumu, na nilihisi kana kwamba Mungu alikuwa Akiweka tumaini Lake juu ya mabega yangu. Nilijua kuwa lazima niufuatilie ukweli kwa bidii, nishirikiane na Mungu na nitimize wajibu wangu ili nimridhishe, na nihakikishe kwamba nimeishi kwa kustahili upendo na wokovu ambao alikuwa Akinipa.

Maneno ya Mungu yanasema “Katika maisha yake, kama mwanadamu anatamani kutakaswa na kufikia mabadiliko katika tabia yake, kama anatamani kuishi kwa kudhihirisha maisha yenye maana, na kutimiza wajibu wake kama kiumbe, basi lazima akubali adabu na hukumu ya Mungu, na lazima asiruhusu nidhamu ya Mungu na kipigo cha Mungu kiondoke kwake, ili aweze kujiweka huru kutokana na kutawalwa na ushawishi wa Shetani na kuishi katika mwanga wa Mungu. Ujue kwamba adabu ya Mungu na hukumu ni mwanga, na mwanga wa wokovu wa mwanadamu, na kwamba hakuna baraka bora zaidi, neema au ulinzi bora kwa ajili ya mwanadamu(Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Matukio Aliyopitia Petro: Ufahamu Wake wa Adabu na Hukumu).

Kupitia uzoefu wangu wa vitendo, nilipata kugundua kweli kwamba hukumu na kuadibu kwa Mungu ndivyo nuru inayotuokoa, navyo ni upendo wa kweli kabisa wa Mungu. Ilikuwa ni hukumu na kuadibu, kurudi na ufunzaji nidhamu wa maneno ya Mungu ambavyo viliniwezesha kuona wazi madhara ambayo umaarufu, faida na hadhi vilikuwa vikinisababishia, na ambavyo vilichochea ujasiri wangu na azimio la kuufuatilia ukweli. Wakati nilipoacha umaarufu, faida na hadhi, nilihisi kana kwamba haikuwa tu hadhi ambayo nilikuwa nimeacha, lakini badala yake minyororo ambayo Shetani alikuwa amenifunga nayo, na nilipata kuhisi hali ya amani na furaha katika vina vya roho yangu, ambayo sikuwa nimeiona awali, na hisia ya wepesi na kuachiliwa huru. Ingawa bado ninaweza, hata sasa, kufichua tabia yangu potovu ya kupigania umaarufu na faida, sijadhibitiwa na kufungwa nayo tena. Kupitia uzoefu wangu nimejifunza kwamba, kwa kuufuata ukweli, mtu anaweza kutupilia mbali tabia yake potovu ya kishetani, na kadri mtu anavyotenda ukweli zaidi, ndivyo mtu anavyoweza kuishi kwa kudhihirisha mfano wa mwanadamu na kubarikiwa na Mungu. Kwa kweli nilihisi kuwa kila kitu kidogo ambacho Mungu alifanya kwangu kilikuwa ni Mungu kulipa gharama ya juu. Wokovu wa Mungu kwangu ni wa vitendo sana, na pendo Lake ni kubwa sana na la kweli! Kuanzia siku hii na kuendelea, ningependa kupitia hukumu na kuadibu kwa Mungu hata zaidi, kufuatilia ukweli ili niweze kutupilia mbali tabia yangu potovu ya kishetani haraka iwezekanavyo, na kuishi kwa kudhihirisha mfano halisi wa binadamu ili kuufariji Moyo wa Mungu. Namshukuru Mungu kwa kuniokoa!

Iliyotangulia: Mabadiliko ya Mwigizaji

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Maudhui Yanayohusiana

Kiburi Huja Kabla ya Kuanguka

Na Xinjie, Uchina Mwenyezi Mungu anasema, “Kiburi ndicho chanzo cha upotovu wa mwanadamu. Kadiri watu wanavyozidi kuwa na kiburi, ndivyo...

Kuzaliwa Upya

Yang Zheng Mkoa wa Heilongjiang Nilizaliwa katika familia maskini ya vijijini iliyokuwa nyuma kimaendeleo katika kufikiri kwao. Nilikuwa...

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp