Tunawakaribisha wote wanaotafuta ukweli wawasiliane nasi.

Usitafute Mbinu Mpya Unapomtumikia Mungu

44

Heyi Mji wa Zhuanghe, Mkoa wa Liaoning

Nilikuwa nimechaguliwa karibuni tu kuchukua jukumu la kiongozi wa kanisa. Lakini baada ya kipindi cha kazi ngumu, sio tu kuwa kazi ya kiinjili ilikuwa bila uhai kiasi, lakini ndugu zangu wa kiume na wa kike katika kikundi cha kiinjili walikuwa pia wakiishi katika hali hasi na ya udhaifu. Nikiwa nimekabiliwa na hali hii, sikuweza tena kudhibiti hisia zangu. Ni vipi tena ningeweza kuiamsha kazi ya kiinjili? Baada ya kupiga ubongo wangu, hatimaye nilifikiria suluhisho zuri: Kama ningefanya sherehe ya kila mwezi kwa kikundi cha kiinjili na kuwachagua watu waliojipambanua na wahubiri wa kielelezo, yeyote ambaye angeshinda roho zaidi kwa ajili ya Mungu angepewa thawabu, na yeyote ambaye angeshinda roho chache angeonywa. Hili halingeisisimua shauku yao tu, lakini lingewainua ndugu wa kike na wa kiume waliokuwa hasi na dhaifu. Nilipofikiria hili, nilifurahishwa sana na hili “tendo langu la werevu”. Niliwaza “Wakati huu kwa kweli nitamshangaza kila mtu.”

Nilikwenda kwa kikundi cha kiinjili na nikakieleza wazo langu. Kila mtu alikuwa na furaha sana na tayari kushirikiana. Nilisisimka, na kusubiri kuona likizaa matunda. Lakini siku chache baadaye, ndugu wa kiume na wa kike ambao hawakuwa wameshinda roho zozote walikuwa hasi sana na walikuwa na maoni juu ya mbinu zangu. Walikuwa wakitaka hata kuondoka kwa hicho kikundi cha kiinjili. Nikiwa nimekabiliwa na yote haya, niliduwaa. Sikujua ningefanya nini. Baada ya kusikia juu ya jambo hilo, kiongozi wangu alikuja kwa haraka kufanya ushirika nami, na kushughulikia hali yangu kwa kusoma mawasiliano kutoka kwa Mungu na mpango wa kazi: “Ni nini mwiko mkubwa katika huduma ya mtu kwa Mungu? Mnajua? Wale ambao huhudumu kama viongozi daima hutaka kuwa na ubunifu mkubwa, kuwa wazuri kuliko wengine, kupata hila mpya ili Mungu aweze kuona jinsi kweli walivyo na uwezo. Hata hivyo, hawazingatii kufahamu ukweli na kuingia katika uhalisi wa neno la Mungu. Wao daima hutaka kuringa; si huu ni ufunuo kwa usahihi wa asili ya kiburi? Wengine hata husema: “Kwa kufanya hivi nina uhakika kwamba Mungu atafurahi sana; Yeye kweli atapenda sana. Wakati huu nitaacha Mungu aone, kumpa Yeye mshangao mzuri.” Kama matokeo ya kujionyesha huku, wanapoteza kazi ya Roho Mtakatifu na wanaondolewa na Mungu. Usifanye tu chochote kijacho akilini mwako bila kufikiri. Je, inawezaje kuwa sawa ikiwa huzingatii matokeo ya matendo yako? … Kama wewe si mwenye tabia njema, mwenye kumcha Mungu au mwenye busara katika kumhudumia Mungu, ipo siku utaziudhi amri za utawala za Mungu” (“Bila Ukweli Ni Rahisi Kumkosea Mungu” katika Kumbukumbu za Maongezi ya Kristo). “Mtu anayemtumikia Mungu ni lazima aelewe mapenzi Yake katika vitu vyote. Wakati anapokabiliwa na tatizo lolote, anapaswa kutafuta ukweli, na kazi yote ni lazima ifanywe kwa msingi wa neno la Mungu. Ni kwa njia hii tu anavyoweza kuhakikisha kwamba matendo yake yanafanywa sawa na mapenzi ya Mungu” (“Mambo ya Kanuni Ambayo Yanapaswa Kueleweka kwa Kumtumikia Mungu” katika Kumbukumbu za Kihistoria Zilizochaguliwa za Mipango ya Kazi ya Kanisa la Mwenyezi Mungu). Maneno haya yalinipa utambuzi wa ghafla wa ukweli usiopendeza na hisia ya kina ya hofu na kutetemeka. Niligundua kwamba “sherehe ya tuzo” niliyokuwa nimeipigia ubongo wangu ilikuwa tu kutafuta mbinu mpya ya werevu. Ni jambo ambalo huamsha karaha nyingi sana ndani ya Mungu; ndio mwiko mkubwa mno katika kumtumikia Mungu. Kumtumikia Mungu sio mchezo wa mtoto. Mbele ya Mungu, wanadamu wanapaswa kudumisha moyo wa heshima, na wanapaswa kufuata mipango ya kazi kwa akali na kutenda kulingana na kanuni za kumtumikia Mungu. Wanapokabiliwa na tatizo, ni lazima watafute ukweli. Ni kwa njia hii tu wanavyoweza kuhakikisha kwamba matendo yao yanafanywa sawa na mapenzi ya Mungu. Sasa, Mungu ameniinua ili kutimiza wajibu wangu kama kiongozi. Wakati kazi ya kiinjili haikuwa ikizaa matunda na ndugu zangu wa kiume na wa kike walikuwa hasi na dhaifu, ningepaswa kuwa nimekuja mbele ya Mungu kutafuta nia Yake, kupata kiini cha tatizo, na kisha kutatua tatizo na ukweli kwa njia ya kupata maneno ya Mungu yanayofaa kwa hali ya ndugu zangu wa kiume na wa kike. Kazi yote ninayoifanya ni lazima iwe kwa msingi wa maneno ya Mungu. Lakini nilipokabiliwa na matatizo, sikutafuta ukweli kabisa. Sikutafuta kanuni kwa matendo yangu. Hasa, sikufanya kazi nzuri, lakini niliweka jitihada zangu kwa njia za juujuu. Niliutegemea ujanja wangu mdogo; nilichukua kitu kutoka kwa mbinu za usimamizi wa kiwanda duniani, kuanza sherehe ya tuzo ya kuwachagua watu waliojipambanua. Matokeo yake, sio tu kwamba kazi ya kiinjili haikuzaa matunda, lakini hali ya ndugu wa kiume na wa kike haikutatuliwa, na kwa sababu ya mbinu zangu walizidi kuwa hata hasi kiasi cha kuacha kikundi cha kiinjili. Je, hilo lingekuwaje mimi kutimiza wajibu wangu? Nilikuwa nikifanya uovu tu, na kudhoofisha kwa chini ufanyaji kazi ufaao wa kazi ya kanisa. Nilistahilije kuwa kiongozi? Kama ningeendelea kuwaongoza ndugu zangu wa kiume na wa kike kwa njia hii, wangepotoshwa nami, na mwishowe, kwa njia ya huduma yangu ya shauku, ningekuwa nimezikosea amri za utawala za Mungu na kupata adhabu Yake.

Ilikuwa ni katika ufunuo wa Mungu ambapo hatimaye nilitambua asili yangu ya kishetani ya kiburi na hali ya kutojali: sikuwa na chembe ya uchaji mbele ya Mungu. Niligundua wakati huo huo kwamba mawazo ya mwanadamu ni shimo la maji ya kunuka. Njia yangu “iliyofanywa kwa werevu”, bila kujali ni nzuri kiasi gani, ilikuwa matakwa ya Shetani, na ingeweza tu kumchukiza Mungu. Ingeweza tu kumkosea Yeye na kuvuruga kazi Yake. Kuanzia siku hii kwendelea, niko tayari kukumbuka somo hili na kuweka jitihada zaidi katika kanuni za kumtumikia Mungu, kufanya kila linalowezekana kufuatilia ukweli ili kubadili asili yangu ya kiburi. Katika mambo yote, nitatafuta ukweli, kutafuta kanuni za vitendo vyote, na kushikilia moyo wa kumheshimu Mungu. Nitautimiza wajibu wangu kwa kadri ya uwezo wangu na kuutuliza moyo wa Mungu, kwa uaminifu na utii wa juu sana.

Maudhui Yanayohusiana

 • Sitapumbazwa Tena na Nia Njema

  Meng Yu Mji wa Pingdingshan, Mkoa wa Henan Wakati mmoja nilipokuwa nikitimiza wajibu wangu, niliona kuwa ndugu fulani alikuwa akijaribu kuwafurahisha…

 • Mbona Ujihusishe na Hila Unapomtumikia Mungu

  Ee Mungu! Asante kwa kufunua asili yangu ya kiburi na majivuno. Kuanzia siku hii na kuendelea, hakika nitachukulia hili kama onyo na kuweka juhudi zaidi katika kujua asili yangu. Nitafanya kazi hasa kulingana na mipangilio ya kazi. Kwa kweli nitakuwa mtu mwenye mantiki, anayezingatia kanuni, na aliye na moyo wa uchaji Kwako.

 • Baada ya Kupoteza Hadhi Yangu

  Nikiangalia maneno ya Mungu na nikifikiri juu yangu mwenyewe, niligundua kuwa kile nilichokuwa nikifuatilia hakikuwa ukweli kamwe, wala sikuwa nikitafuta kumtosheleza Mungu, lakini badala yake ilikuwa sifa, faida na hadhi. Nikiwa na hadhi, kujiamini kwangu kuliongezeka mara mia moja; bila hadhi, nilikuwa mwenye harara na wa huzuni sana hivi kwamba singeweza kujisumbua kufanya kazi. Kwa kweli nilijisahau kwa hadhi yangu nikiharakisha pote nikijihusisha mchana kutwa na mambo haya yasiyo na maana na yasiyo na thamani na kupoteza wakati mwingi; na nilipata nini mwishowe? Tabia ya aibu niliyoionyesha leo?

 • Kila Neno la Mungu ni Maonyesho ya Tabia Yake

  Ni sasa tu ninapoelewa kwamba kama napenda kuielewa tabia ya Mungu, ni lazima nijaribu kwa bidii kuelewa na kutafuta ukweli ndani ya kila sentensi ya Mungu. Kwa njia hii, hakika nitafaidika sana. Kuanzia leo kwendelea, natamani kuzingatia kuweka juhudi nyingi zaidi katika maneno ya Mungu, na kutafuta hivi karibuni kuwa mtu ambaye ana ufahamu kiasi wa Mungu.