Nuru Hafifu ya Maisha katika Pango la Giza la Wakatili
Jina langu ni Lin Ying, na mimi ni Mkristo katika Kanisa la Mwenyezi Mungu. Kabla ya kuanza kumwamini Mwenyezi Mungu, nilitaka siku zote kutegemea uwezo wangu mwenyewe na kufanya kazi kwa bidii ili kufanya maisha yangu yawe bora zaidi, lakini mambo hayakuwa jinsi nilivyotaka; badala yake, nilikumbana na kizuizi baada ya kizuizi, na nikakabiliwa na vipingamizi baada ya vipingamizi. Baada ya kuzongwa na dhiki za maisha za kuleta huzuni, nilihisi kuchoka kimwili na kiakili na niliteseka vibaya sana. Katika`ti ya maumivu yangu na kukata tamaa, dada mmoja alinihubiria injili ya Mwenyezi Mungu ya siku za mwisho. Niliposoma Maneno ya Mungu yaliyosema, “Unapokuwa umechoka na unapoanza kuhisi huzuni kubwa ya ulimwengu huu, usipotoke, usilie. Mwenyezi Mungu, Mlinzi, atakaribisha kuwasili kwako wakati wowote. Yuko kandokando yako akiangalia, akikusubiri urudi” (Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Kutanafusi kwa Mwenye Uweza). sikuweza kuzuia machozi yangu kudondoka. Maneno ya Mwenyezi Mungu ya kutunza kama mama yalinifariji sana, na nilihisi kama yatima ambaye alikuwa amezurura kwa miaka mingi na mwishowe akarudi kwenye kumbatio la mama yake—sikuhisi tena mpweke na asiyejiweza. Tangu siku hiyo na kuendelea, nilisoma maneno ya Mungu kila siku kwa shauku. Kupitia kuhudhuria mikutano na kushirikiana na ndugu katika Kanisa la Mwenyezi Mungu, nilikuja kuelewa ukweli mwingi, na nikaona kuwa watu hawa wote walikuwa wazuri na waaminifu sana. Hakukuwa na mabishano ya wivu kati yao na hakuwa na kupanga njama dhidi ya mwingine, na wakati wowote ambapo mtu angekuwa na tatizo, ndugu wote wangeshiriki juu ya ukweli kwa dhati ili kumsaidia kulitatua. Msaada ulitolewa kila mara bila masharti, na hakuna mtu aliyedai malipo kamwe, na nikiwa kati yao nilihisi uhuru na furaha ambayo sikuwahi kuhisi hapo awali. Nilikuwa na ufahamu wa kina kwamba Kanisa la Mwenyezi Mungu lilikuwa mahali pa utakatifu, na nikawa na hakika kuwa Mwenyezi Mungu ndiye Mungu mmoja wa kweli anayeweza kuwaokoa wanadamu kutoka kwa bahari ya mateso! Hata hivyo, wakati tu nilipokuwa nikifurahia upendo wa Mungu, serikali ya CCP ilinikamata na kunitesa kinyume cha sheria, na ikaharibu maisha yangu ya kuridhisha na ya furaha.
Usiku wa manane mnamo Agosti 12, 2003, nilikuwa nikilala fofofo nilipogutushwa ghafla kutoka usingizini na kishindo kikuu mlangoni, na nikamsikia mtu akipaza sauti, “Fungua! Fungua!” Kabla ya hata kuvalia nguo, nilisikia mshindo mzito, mlango wa chumba changu kilifunguka kwa ghafla, na polisi sita wakali sana na wakatili wakaingia kwa nguvu. Huku nikishtuka, nikawauliza, “Kuna nini?” Kiongozi wa polisi alinikaripia, akisema, “Usijifanye mjinga!” Kisha kwa kupunga mkono wake, alisema kwa sauti, “Fudikiza mahali hapa!” Polisi kadhaa basi walianza kupekua makabati yangu kana kwamba walikuwa majambazi. Muda mfupi baadaye, vyungu na sufuria zangu, nguo zangu, mashiti yangu, vyakula vyangu... yote yalitupwa kila mahali sakafuni, na chumba changu kilikuwa kimevurugwa sana. Baada ya kupekua nyumbani kwangu, walinisukuma na kunivuta hadi kwenye gari la polisi. Walichukua chombo cha kuchezesha diski songamano ambacho nilikuwa tu nimekinunua muda mfupi cha thamani ya Yuani 240, na walichukua Yuani 80 pesa taslimu na kitita cha vitabu vya maneno ya Mungu. Sikuwahi kufikiria tukio kama hili: Hili lilikuwa jambo ambalo lilitokea tu katika programu za runinga, lakini sasa lilikuwa linanitokea. Nilihisi hofu na woga mkubwa, na moyo wangu ulikuwa ukidunda sana. Nilimwomba Mungu kila wakati, nikimtaka Anilinde ili niweze kuwa shahidi Wake, na ili nipate kufa kabla ya kuwasaliti ndugu zangu na kuwa Yuda. Wakati huo tu, maneno ya Mwenyezi Mungu yalinijia akilini ghafla: “Haupaswi kuwa na hofu ya hili na lile. Haidhuru wingi wa matatizo na hatari unazokabili, utabaki thabiti mbele Yangu; usizuiliwe na kitu chochote, ili mapenzi Yangu yaweze kufanyika. … Usiwe na hofu; kwa msaada Wangu, ni nani angeweza daima kuzuia barabara? Kumbuka hiki! Kumbuka!” (Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Matamko ya Kristo Mwanzoni, Sura ya 10). Maneno ya Mungu yalinifariji sana na yaliusaidia moyo wangu kutulia polepole. Yalinifanya nigundue kuwa Yule niliyemwamini ni Mtawala aliyeumba vitu vyote mbinguni na duniani, kwamba vitu vyote viko mikononi Mwake, kwamba Shetani na pepo wako chini ya miguu Yake na kwamba, bila ruhusa ya Mungu, hakukuwa na kitu ambacho Shetani angeweza kunifanyia. Sasa nilijikuta katika wakati muhimu sana katika vita baina ya ya Mungu na Shetani: Wakati huu ndipo Mungu alihitaji niwe shahidi, na ulikuwa wakati wa mimi kupitia maneno ya Mungu na kupata ukweli; nilijua kuwa lazima nishike msimamo na kutenda kulingana na maneno ya Mungu, na kamwe singesujudu au kujisalimisha kwa Shetani!
Gari la polisi lilitoa sauti kubwa na kuvuma huku likiingia katika uwanja wa kituo cha polisi. Mara tu tulipofika, polisi walinisukuma hadi nje ya gari kwa ukali. Nilisonga mbele nikiwa nimepinduka upande mmoja huku mikono ikiwa imenyooshwa na nikasimama tu wakati nilipogonga ukuta kwa kishindo. Niliweza kuwasikia wakicheka kwa jazba nyuma yangu. Kisha walinisukuma hadi ndani ya chumba kidogo, na kabla ya kupata wakati wa kupumua, mmoja wa polisi alisoma orodha ya majina na akaniuliza ikiwa nilimjua yeyote kati yao. Walipoona kwamba sikujibu, walianza kunizingira, wakinipiga ngumi na kunipiga mateke, na kunitukana walipokuwa wakifanya hivyo. Kisha polisi mmoja mwovu akashika nywele zangu na kunivuta nisimame, halafu akanizaba kofi kwa nguvu mara mbili usoni. Kichwa changu kilizunguka na macho yangu yakawa na ukungu, na damu nyekundu kali ikatirirka kutoka kwenye pembe ya kinywa changu.
Kisha mmoja wa polisi akatoa kipande cha karatasi kilichokuwa na orodha ya majina na kukirusha mbele yangu, akisema kwa ukali, “Unajua majina ya watu hawa, siyo? Unaitwa nani?” Nilihisi uchungu sana wakati huo huo kiasi kwamba sikuweza hata kuzungumza na, alipoona kwamba singejibu, polisi watatu wabaya walinishambulia kwa ghafla na kunichapa na kunipiga mateke tena hadi nikapoteza fahamu.
Alfajiri iliyofuata, polisi hao waovu walinipeleka kwa chumba cha mahojiano katika Sehemu ya Upelelezi wa Jinai ya Ofisi ya Usalama wa Umma. Nilipofikishwa ndani ya chumba hicho, niliona wanaume kadhaa wenye miraba minne wote wakinitazama kana kwamba walitaka kuniua. Chumba kilijaa kila aina ya vifaa vya kutesea watu, na mandhari yaliyonikabili yalinifanya niwe na wasiwasi mara moja—nilihisi kana kwamba nilikuwa nimeanguka katika shimo la pepo. Niliogopa kabisa, na hisia za hofu na ukosefu wa usalama zilinijia tena. Nilijiwazia: “Jana, walinitesa vivyo hivyo na hayo hata hayakuwa mahojiano rasmi. Inaonekana hakuna njia ya kuepa kitakachotokea leo. Je, nitaweza kustahimili ikiwa watanitesa kikatili?” Nilimwomba Mungu sala ya dhati: “Ee Mungu, ninaogopa sana hivi sasa, na ninasikitika kwamba sitaweza kuvumilia mateso haya ambayo pepo hawa watafanya niyapitie na nitapoteza ushuhuda wangu. Tafadhali linda moyo wangu. Ni afadhali nipigwe hadi nife kuliko kukusaliti!” Kisha mstari wa maneno ya Mungu ukatokea akilini mwangu: “Kutoka kwa nje, wale walio na mamlaka wanaweza kuonekana kuwa waovu, lakini msiogope, kwa kuwa hii ni kwa sababu mna imani kidogo. Almuradi imani yenu ikue, hakuna kitu kitakachokuwa kigumu mno” (Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Matamko ya Kristo Mwanzoni, Sura ya 75). Maneno ya Mungu yana mamlaka na nguvu. Yalinijaza nguvu ya ndani mara moja, na nikawaza: “Nikiwa na Mungu kando yangu, sitaogopa chochote. Bila kujali jinsi wanavyoweza kuoneysha ubwana wao, wao ni tishio la bure pekee wanaoonekana wakatili kwa nje tu. Hakuna kitu cha kuhofu kutoka kwao, kwa kuwa tayari wameshindwa na Mungu.” Papo hapo, polisi mmoja mwovu alisema kwa sauti, “Tuambie cheo chako katika kanisa ni kipi! Wewe hupiga ripoti kwa nani?” Kwa sababu nilikuwa na maneno ya Mungu kama msaada wangu, sikuhisi hofu hata kidogo, na kwa hivyo sikujibu maswali yake. Alipoona jinsi nilivyokataa kujibu, alinizungumzia kwa sauti kubwa kama mnyama aliyeghadhabishwa: “Msimamisheni mwanamke huyu anayenuka! Msimamisheni kwa ncha zake za vidole apate ladha kali ya jinsi ambavyo sisi hatufanyi mzaha!” Kisha polisi wawili waovu wakanishambulia kwa ghafla na kwa ukali wakapinda mikono yangu nyuma ya mgongo wangu na kuiinua. Ghafla nilihisi maumivu makali mno na nikapiga unyende, na kisha nikazimia…. Nilipoamka, niliona kwamba nilikuwa nimelala sakafuni na kuwa pua yangu ilikuwa imetoa damu. Ilikuwa dhahiri kwangu kwamba, baada ya kupoteza fahamu, polisi waovu walikuwa wamenitupa tu sakafuni. Walipoona kwamba nilikuwa nimeamka, basi walinikokota hadi ndani ya chumba ambacho kilikuwa na giza sana hata sikuweza kuona mkono wangu uliokuwa mbele ya uso wangu. Chumba kilikuwa chenye giza kabisa, baridi na chenye unyevu, kilinuka mkojo na nilipumua kwa shida. Polisi mmoja mwovu alisema kwa ukali alipokuwa akifunga mlango, “Fikiria tena. Usipokiri, tutakunyima chakula hadi ufe.” Nilianguka ghafla kwenye sakafu iliyokuwa baridi sana. Mwili wangu uliuma kote, na sikuweza kujizuia kuhisi dhaifu. Nilifikiri: “Ni sheria isiyoweza kubadilika kwa kiumbe kumwamini Mungu na kumwabudu Mungu, kwa hivyo kuna nini kibaya katika kumwamini Mwenyezi Mungu? Kumwamini Mungu kunaturuhusu tutembee katika njia sahihi, na hii si haramu wala si kosa. Na bado genge hili la ibilisi linanichukulia kana kwamba nimetenda uhalifu unaostahili hukumu ya kifo. Hili ni jambo lisilovumilika kabisa!” Nilipokuwa nikiteseka katika maumivu yangu, nilifikiria wimbo wa maneno ya Mungu: “Hakuna anayeweza kuondoa kazi ambayo imefanywa ndani yenu, na baraka ambazo zimetolewa ndani yenu, na hakuna anayeweza kuondoa yote ambayo mmepewa ninyi. … Kwa sababu ya hili, lazima mjitolee hata zaidi kwa Mungu, na hata waaminifu zaidi kwa Mungu. Kwa sababu Mungu hukuinua, lazima utegemeze juhudi zako, na lazima utayarishe kimo chako kukubali maagizo ya Mungu. Lazima usimame imara mahali ambapo Mungu amekupa, ufuatilie kuwa mmoja wa watu wa Mungu, ukubali mafunzo ya ufalme, upatwe na Mungu na hatimaye kuwa ushuhuda wa kuleta sifa kuu kwa Mungu. Je, wewe una maazimio haya? Kama una maazimio hayo, basi hatimaye una hakika ya kupatwa na Mungu, na utakuwa ushuhuda wa kuleta sifa kuu kwa Mungu. Unapaswa kuelewa kwamba agizo kuu ni kupatwa na Mungu na kugeuka kuwa ushuhuda wa kuleta sifa kuu kwa Mungu. Haya ni mapenzi ya Mungu” (“Huwezi Kusikitisha Mapenzi ya Mungu” katika Mfuateni Mwanakondoo na Kuimba Nyimbo Mpya). Niliendelea kuuimba kichwani mwangu na joto likaenea katika mwili wangu wote. Nilihisi kana kwamba Mungu alikuwa amesimama kando yangu kabisa, Akinifariji na kunitia moyo kama mama mwenye upendo, Akihofia kuwa naweza kuwa dhaifu, kuanguka chini, na kupoteza imani yangu, na Akanionya na kuniagiza kwa upole. Ilikuwa kama kwamba Alikuwa akiniambia kuwa hali hii chungu niliyokuwamo ndani ilikuwa ikinifundisha kwa ajili ya ufalme, kwamba ilikuwa ushuhuda wa ushindi juu ya Shetani ili kupokea baraka za Mungu za milele, kwamba ilikuwa utajiri wa thamani zaidi maishani ambao Mungu angeweza kutoa, na kwamba ilikuwa ushuhuda mzuri unaoletwa haswa kwa ajili ya kuingia katika ufalme. Niliguswa sana kiasi kwamba machozi yalitoka machoni pangu, na nikawaza: “Ee Mwenyezi Mungu, nitakumbuka vizuri kile ambacho Umeniaminia nifanye na ninakubali kuanza mafunzo haya. Nitashirikiana na Wewe kwa bidii na kuwa na ushuhuda adhimu Kwako, na sitakuwa mwoga na kujiruhusu kuwa kichekesho kwa Shetani!”
Asubuhi ya siku ya tatu, polisi kadhaa walinipeleka tena kwenye chumba cha mahojiano. Afisa mwovu wa polisi alinigonga kichwani na kirungu chake, na akasema kwa tabasamu la kinafiki, “Umefikiria jambo hilo tena?” Kisha akanionyesha orodha ya majina ya washiriki wa kanisa na akanitaka niwatambulishe. Nilimwomba Mungu ombi la kimywa: “Ee Mwenyezi Mungu, Shetani amekuja kunijaribu kwa mara nyingine tena, na anajaribu kunifanya nikusaliti na kuwasaliti ndugu zangu. Nakataa kabisa kuendeleza maisha ya aibu kama Yuda. Nakuomba tu kwamba Uulinde moyo wangu, na Unilaani nikifanya chochote kukusaliti!” Nilihisi nguvu ikiibuka ndani yangu papo hapo, na nikasema kwa uthabiti, “Sijui yeyote kati yao!” Mara tu baada ya kusema haya, polisi wawili waovu walinishambulia. Mmoja wao alivuta mguu wangu mmoja, na mwingine akakanyaga goti langu kwa kiatu kigumu cha ngozi. Alipokuwa akikanyaga, alisema kwa ukali, “Hujui mtu yeyote, eh? Kwa kweli hujui mtu yeyote?” Uchungu mkali ulinifanya nipoteze fahamu tena. Sijui nilipoteza fahamu kwa muda gani kabla ya wao kuniamsha kwa kunimwagia maji ya barafu. Mara tu nilipoamka, polisi mwovu aliinua ngumi yake na kunipiga ngumi kifuani, na alinipiga kwa nguvu sana kiasi kwamba ilichukua muda mrefu kabla ya kuweza kuvuta pumzi tena. Polisi mwingine mwovu kisha alinishika kwa nywele, akanivuta hadi kwenye kiti cha chuma na kunitia pingu ili nisiweze kusonga. Alinifunga macho kwa kitambaa kichafu sana. Walibadilishana kati ya kuvuta masikio yangu kuelekea juu kwa nguvu zao zote, na kukanyaga miguu yangu kwa nguvu kadiri walivyoweza—uchungu mkali uliotokana na yote hayo yalinifanya nilie ghafla. Walipoona nikizidiwa na uchungu na huzuni, genge la polisi waovu lilicheka kwa makelele. Kicheko chao kilisikika kana kwamba kilitoka ndani sana ya kuzimu—kilikuwa cha bughudha kukisikia, na kilifanya moyo wangu utetemeke. Nikiwa nimekabiliwa na ukatili kama huo, kwa kweli niliona waziwazi kuwa hawa “Polisi wa Watu,” kama walivyotangazwa kuwa na serikali ya CCP, wote walikuwa tu wanyama wakatili na waovu. Walikuwa tu watu wakatili sana ambao walikusudia tu kuwaumiza watu! Nilikuwa kila mara nikiwafikiria polisi kuwa mashujaa waliopigania haki, ambao waliwafungia watu wabaya korokoroni na kuwalinda watu wema, na kwamba watu wangeweza kuwategemea polisi kila mara walipokuwa katika hatari au shida. Hata ingawa nilikamatwa na kuteswa nao mara kwa mara tangu nianze kumwamini Mungu, sikuwahi kuwachukulia kabisa kama ibilisi Shetani. Sasa, Mwenyezi Mungu alikuwa amenifichulia ukweli wa kweli, na wakati huo tu ndipo nilipoona kwamba walikuwa na nyuso katili na zenye nia mbaya za pepo wa kishetani. Moyoni mwangu, nilimshukuru Mwenyezi Mungu kimyakimya kwa kuyafungua macho yangu ya kiroho hatimaye na kuniwezesha nione wazi wazi tofauti kati ya mema na mabaya; nilihisi kwamba kupitia maumivu haya yote kulikuwa kwa maana katika kujua haya! Mungu asingefanya hivi, nisingezinduka kamwe kutoka katika uwongo na udanganyifu wa Shetani, na ingekuwa vigumu sana kwangu kuepa ushawishi mwovu wa Shetani na kupata wokovu wa Mungu.
Baada ya muda, afisa huyo wa polisi aliuliza, “Bado huzungumzi? Utazungumza au la?” Alipoona kwamba sikusema chochote, polisi wawili waovu walinijia, wakashika kichwa changu na kuanza kutoa kwa kuvuta nyusi zangu. Mmoja wa wanaume ambao walinishikilia alinipiga kofi vibaya mara kadhaa, akinipiga kwa nguvu sana hadi nikawa na kizunguzungu. Fedheha na maumivu vilinisababisha nihisi huzuni na chuki, na nikaangua kilio kutokana na aibu hayo yote. Ah, niliwachukia wakatili hawa wasio na dhamiri ambao walimkufuru Mungu kama nini! Katika maumivu yangi, nilifikiria jinsi Bwana Yesu alivyovumilia fedheha, dharau na vichapo vilivyotolewa na askari ili kuwakomboa wanadamu, na jinsi alivyosulibiwa msalabani, na nilifikiria juu ya maonyo na ushawishi uliorudiwarudiwa na Mungu: “Pengine utayakumbuka maneno haya: ‘Kwa kuwa huzuni yetu nyepesi, ambayo ni ya muda mdogo pekee, inatufanyia utukufu mkubwa na wa daima ambao unazidi kuwa mkuu kabisa.’ Zamani, mlisikia msemo huu, lakini hakuna aliyeelewa maana kamili ya maneno yale. Leo, unajua vyema umuhimu wa maneno yale” (Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Je, Kazi ya Mungu Ni Rahisi Kama Vile Mwanadamu Anavyodhania?). Maneno ya Mungu yaliuletea moyo wangu faraja kuu, na nikagundua kuwa fedheha na maumivu niliyokuwa nikipitia sasa yangekumbukwa na Mungu; maumivu haya yalikuwa yakipitiwa ili kupata ukweli, ulikuwa ushuhuda adhimu, na ilikuwa baraka maishani mwangu. “Kwa kuwa ninamwamini Mungu,” nilidhani, “basi lazima niwe na imani na ujasiri wa kukubali baraka za Mungu, na lazima niwe na ujasiri wa kuwa ushuhuda wa ushindi wa Mungu.” Wakati huo huo, sura ya yule afisa wa polisi ilibadilika, na akasema, “Tuambie kile tunachotaka kujua na nitakuacha uende hivi sasa.” Nilimtazama kwa dharau na kusema, “Labda nife kwanza!” Kwa ghadhabu, aliwaamuru wale polisi wawili waovu wanivute na kunirudisha hadi kwenye seli yenye giza.
Baada ya vikao kadhaa vya mateso ya kikatili, niligongwagongwa na kuumizwa sana, na sikuwa na nguvu yoyote iliyobaki. Mikono na miguu yangu hasa ilikuwa imevimba sana hadi sikuweza kuthubutu kuisongeza hata kidogo. Bila nguvu yoyote, nilibanana pale, kama mwana kondoo aliyesubirikuchinjwa. Wakati wowote nilipofikiria juu ya nyuso katili na tabasamu za kutisha sana za polisi waovu waliposhika na kutumia vifaa hivyo vya kutesea watu, moyo wangu ulijawa na wasiwasi kabisa. Hasa niliposikia nyayo zikikaribia seli yangu, moyo wangu ulidunda haraka na kwa kasi. Hofu na woga vilinijaa wakati huo, na nilihisi kutojiweza na mpweke. Nililia; nililia kweli! Na nikamwamini Mungu: “Ee Mwenyezi Mungu! Naogopa sana hivi sasa, na ninahisi dhaifu sana. Sijui nigeuke kuelekea wapi. Tafadhali niokoe. Sitaki kuwa tena mahali hapa pabaya mno.” Wakati tu nilipokuwa nikihisi dhaifu na mwenye kukata tamaa, maneno ya Mungu yaliibuka ndani yangu, yakinitia moyo na kunifariji: “Katika dunia hii kubwa, ni nani amechunguzwa na Mimi binafsi? … Kwa nini Nimetaja mara kwa mara jina la Ayubu? Na mbona Nimemtaja Petro mara nyingi? Je, mmewahi kufahamu matumaini Yangu kwenu? Mnapaswa kuchukua muda zaidi kuwaza mambo ya aina hii” (Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Maneno ya Mungu kwa Ulimwengu Mzima, Sura ya 8). Maneno ya Mungu yaliniletea imani na nguvu. “Ndiyo!” Nilidhani. “Katika mbingu na dunia yote, ni nani kati ya wanadamu anayeweza kufanya kama tunavyofanya na kukubali yeye binafsi jaribio la Mungu katika pango hili la ibilisi Shetani? Ni nani anayeweza kuinuliwa na Mungu na kuwa na bahati ya kupitia jaribio hili la moto, akiwa amezingirwa na vikosi vya pepo? Mimi ni dhaifu sana na sina nguvu, na bado leo Mungu ananipa upendo kama huu. Kuchaguliwa na Mungu ni baraka ya maisha yangu na ni heshima yangu. Siwezi kuepuka jaribio hili, wala sistahili kujaribu kulikwepa. Badala yake, lazima niwe na heshima, niwe na msimamo thabiti mbele ya Shetani kama Ayubu na Petro walivyofanya, nitumie maisha yangu kushuhudia kwa Mungu na kulitetea jina la Mungu, na nisimfanye Mungu ahuzunike au kusikitika.” Wakati huo, moyo wangu ulijawa na shukrani na fahari. Nilihisi kana kwamba kubahatika kwangu kiasi cha kutosha katika maisha haya kupitia mateso na jaribio ya aina hii kulikuwa kwa kipekee na kwa thamani sana!
Siku ya nne iliwadia, na mara nyingine tena akiwa ameishika ile orodha ya washiriki wa kanisa, yule afisa mwovu wa polisi alinichoma kwa kidole chake, akisema, “Niambie wale wote unaowafahamu na niambie kiongozi wenu ni nani. Ukiniambia, nitakuacha uende. Usiponiambia, basi utafia hapa!” Aliona kuwa bado singemweleza chochote, kwa hivyo akasema kwa sauti kubwa, “Njooni, mwangikeni mikono yake ikiwa nyuma ya mgongo wake. Mwueni sasa hivi!” Wale wadogo wawili waliifungia mikono yangu nyuma ya mgongo wangu papo hapo na wakanining’iniza kwa kuifunga kwa kamba ili niweze kusimama tu kwa ncha za vidole. Afisa wa polisi kisha alitumia vitisho na vishawishi kwangu, akisema, “Kwa nini ujisumbue hivi kutojisalimisha? Unahitaji kuelewa uhalisi wa hali uliyomo ndani. China ni nchi ya Chama cha Kikomunisti na kile tunachosema hutendeka. Ukituambia kile tunachotaka kujua, nitakuachilia uende mara moja, na pia naweza kukupangia kazi. Kama sivyo, nitaifahamisha shule ya mwanako kukuhusu na kisha nimfanye afukuzwe….” Nilipokuwa nikiyasikiliza maneno yake yasiyo na haya, nilihisi kuhuzunika na kuudhika. Ili kukatiza na kuharibu kazi ya Mungu na kuharibu nafasi zetu za kupata wokovu, serikali ya CCP itafanya kila linalowezekana na kutenda uovu wowote! Kama tu maneno ya Mwenyezi Mungu yasemavyo: “Katika jamii ya giza kama hii, ambapo pepo hawana huruma na ni katili, inawezekanaje mfalme wa pepo anayeua watu bila hisia yoyote, avumilie uwepo wa Mungu ambaye ni mwenye upendo, mpole, na mtakatifu? Anawezaje kushangilia na kufurahia ujio wa Mungu? Vikaragosi hawa! Wanalipa upole kwa chuki, wanamtweza Mungu kwa muda mrefu, wanamtukana Mungu, ni washenzi kupita kiasi, hawamjali Mungu hata kidogo, wanapora na kuteka nyara, wamepoteza dhamiri yote, wanaenda kinyume na dhamiri yote, na wanawajaribu watu wasiokuwa na hatia kuwa watu wasiokuwa na uwezo wa kuhisi. … Uhuru wa dini? Haki halali na matakwa ya wananchi? Zote hizo ni njama za kufunika dhambi!” (Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Kazi na Kuingia (8)). Wakati huo huo, nilipata kuona waziwazi sura mbaya ya serikali ya CCP, na nikaona upotovu wake na uhalifu mbaya sana dhidi ya Mbingu. CCP ni adui ambaye anamchukia Mungu na anayempinga Mungu kiasi cha kutotulizika, na ni adui wangu mkuu asiyeweza kupatanishwa nami—siwezi kamwe kujisalimisha kwake! Walipoona kwamba nilisalia kimya, waliniacha nikining’inia hapo na nikapoteza fahamu polepole: Waliniacha nikining'inia hapo siku moja nzima na usiku mmoja mzima. Waliponishusha, nilichoweza kuhisi tu kilikuwa ni mtu kugusa pua yangu. Mtu huyo alipoona kuwa nilikuwa bado nikipumua, aliniacha hapo tu sakafuni. Kupitia ukungu ulioziba akili yangu, niliwasikia wakisema, “Sina wazo lolote. Nimeshangaa mwanamke huyu amekuwa mbabe sana. Yeye ni mbabe kuliko Chama cha Kikomunisti. Waumini hawa wa Mwenyezi Mungu kweli wana mambo!” Niliposikia wakisema hivi, nilihisi hisia isiyoelezeka ikisisimka ndani yangu, na sikuweza kujizuia kutoa shukrani zangu na sifa kwa Mungu, kwa maana ni Mungu aliyekuwa ameniongoza kumshinda Shetani.
Nilifungiwa kwenye seli yenye giza katika Ofisi ya Usalama wa Umma kwa muda wa siku nane. Serikali ya CCP ilifikiria kila hila na kutumia kila mbinu ipatikanayo, na bado hawakupata habari yoyote waliyotaka kutoka kwangu. Hatimaye, yote ambayo polisi waovu waliweza kufanya ni kunituma kwenye kituo cha uzuizi. Wakati huo, walichukua fursa ambazo zilitolewa na familia yangu kunitembelea kupata yuani 3,000 kwa nguvu kutoka kwa mume wangu. Nilikuwa nimefikiria kwamba kituo cha uzuizi kingekuwa bora zaidi, lakini nilikuwa nimekosea. Katika taifa hili la China linalomchukia Mungu, kila kona ina giza kabisa na imejaa vurugu, ukatili na mauaji. Mahali kama hapa haparuhusu kabisa ukweli uwepo, sembuse kuwa na mahali pa muumini wa Mwenyezi Mungu kupata pahali pa usalama. Kuwa ndani ya kituo cha uzuizi kulikuwa kama kutoka katika tatizo moja na kuingia katika jingine kubwa zaidi. Polisi waovu hawakutaka bado kukubali kushindwa, na kwa hivyo waliendelea kunihoji baada ya kufika huko. Kwa sababu hawakuwa wamepata habari yoyote waliyotaka kutoka kwangu, polisi watatu walinivamia mara moja na kunipiga vibaya mno. Niliachwa na vidonda vipya na mavilio ya damu juu ya yale ya zamani ambayo bado hayakuwa yamepona, na nilipigwa vibaya sana hadi wakaniacha nikiwa nimelala kifudifudi sakafuni na nisiyeweza kusonga. Mkuu wa polisi alichuchumaa, akaelekeza kidole kwenye kichwa changu na kunionya, akisema, “Usipokiri, basi usitarajie kuendelea kuishi mahali hapa!” Polisi mmoja mwovu alinijia na kunipiga teke vibaya mara kadhaa zaidi, kisha wadogo wawili wakanivuta hadi kwenye uwanja na kunifungia kwenye mhimili wa simu. Niliachwa nikiwa nimefungiwa pale siku nzima bila kunywa hata tone la maji, na mwili wangu ulikuwa umefunikwa kwa vidonda na mavilio ya damu. Huku wakiogopa kwamba ningefia pale, walinitupa ndani ya seli. Wakati tu nilipokuwa nikichungulia kaburi na nilikuwa nahisi dhaifu sana, dada wawili ambao walimwamini Mwenyezi Mungu na ambao pia walikuwa wamefungwa kwenye kituo cha uzuizi walinijia kwa haraka. Walifungua zipu za nguo zao, wakazifungua na kunishika kwa karibu, wakitumia joto la miili yao kunipasha joto. Ingawa hatukujuana kabisa, upendo wa Mungu ulileta mioyo yetu karibu kwa pamoja. Niliweza kusikia vilio vya dada zangu ambavyo havikuwa dhahiri, na wafungwa wengine wakitujadili, wakisema, “Polisi hawa ni wakatili sana! Watu ambao wanamwamini Mwenyezi Mungu ni wenye huruma sana. Nilidhani ninyi nyote ni watu wa familia moja, lakini kwa kweli hamjuani.” Pia nilisikia wale dada wawili wakisema, “Mungu alimuumba mwanadamu na sisi sote ni familia moja....” Niliishia kupata homa kali, nikawa mgonjwa sana na nikahisi kana kwamba nilikuwa karibu kufa. Polisi waovu hawakugundua hata kidogo, lakini dada walilipa bei ghali mno kununua nguo na dawa kutoka kwao. Kwa uangalifu, walitibu vidonda vyangu na kunitunza kila siku. Chini ya utunzaji wao wa makini, nilianza kupata nafuu polepole. Nilijua huu kuwa upendo wa Mungu: Ingawa Mungu alikuwa ameruhusu dhiki inipate, Alizingatia udhaifu na maumivu yangu siku zote, na Alikuwa amenipangia kila kitu kwa siri, na Akaratibu hawa dada wawili wanitunze na kunifariji. Tulifarijiana na kutiana moyo, na tukiwa na matamanio na malengo sawa akilini, sote tuliwaombea wengine kwa siri, tukimwomba Mungu atupe imani na nguvu ili tuweze kuwa ushuhuda kwa ushindi wa Mungu katika pango hili la pepo.
Kuenda ndani ya kituo cha uzuizi kulikuwa kama kuingia kuzimuni duniani; ndani ya kuta hizo, tuliishi maisha ya kinyama. Hatukupata chakula cha kutosha na tulilazimika kufanya kazi hadi kuwa hoi, tukifanya kazi kuanzia saa moja asubuhi hadi saa nne usiku kabla ya kuweza kurudi kwenye seli zetu—kila siku tulichoka kabisa na nguvu zetu zote zilitumika. Lakini kwa sababu niliweza kushiriki mara kwa mara juu ya maneno ya Mungu na dada hao wawili, ingawa mwili wangu uliteseka sana na kila wakati ulikuwa umechoka, moyo wangu ulihisi amani na ulijawa na mwanga: Mara nyingi wakati huo, nilifikiria wimbo huu wa maneno ya Mungu: “Hivyo, katika siku hizi za mwisho lazima muwe na ushuhuda kwa Mungu. Haijalishi mateso yenu ni makubwa vipi, mnapaswa kuendelea hadi mwisho kabisa, na hata wakati wa pumzi yenu ya mwisho, bado lazima muwe waaminifu kwa Mungu, na kudhibitiwa na Mungu; huku pekee ndiko kumpenda Mungu kweli, na huu pekee ndio ushuhuda thabiti na mkubwa sana” (“Tafuta Kumpenda Mungu Bila Kujali Mateso Yako Ni Makubwa Vipi” katika Mfuateni Mwanakondoo na Kuimba Nyimbo Mpya). Wakati wowote nilipoimba wimbo huu, nilihisi nguvu ya ajabu ikinisaidia, na bila kujua, uchovu, huzuni, na maumivu niliyohisi ndani yangu yote yangetoweka kabisa. Wakati huo huo, niligundua pia kuwa uwezo wangu wa kupitia maumivu haya ulikuwa wema na baraka kubwa zaidi ambayo Mungu angeweza kunipa. Bila kujali jinsi mateso yangu yalivyokuwa makubwa, nilidhamiria kumfuata Mungu hadi mwisho, na hata kama ningekuwa na pumzi moja tu iliyobaki, ningetafuta kumpenda Mungu na kumridhisha Mungu. Huku nikitiwa moyo na upendo wa Mungu, nilikaa siku 20 zilizovumilika kwa ugumu katika kituo cha uzuizi. Katika lile pango la giza la wakatili, ilikuwa nuru ya maisha kutoka kwa Mwenyezi Mungu ambayo iliondoa giza na ambayo iliniwezesha kuendelea kumsifu Mungu na kufurahia riziki ya maisha kutoka kwa maneno ya Mungu—huu ulikuwa upendo na wokovu mkubwa zaidi ambao Mungu angeweza kunipa. Nilipokuwa mwishowe nikiachiliwa huru, polisi waovu bado walinitishia bila aibu, wakisema, “Usifikirie hata kumwambia mtu yeyote kuhusu kile ambacho kimekufanyikia hapa utakapofika nyumbani!” Kuwaangalia hao polisi waovu na nyuso zao za binadamu na mioyo ya wanyama, ubaya wa kutaka kwao kufanya mambo maovu bila kukubali kuyawajibikia, kuliimarisha imani yangu zaidi na azimio langu la kumuacha Shetani na kumfuata Mungu na kushuhudia kwa Mungu. Nilifanya uamuzi kushirikiana na Mungu na kueneza injili, kuleta roho zaidi za wenzangu wanaomilikiwa na ibilisi Shetani kwenye nuru, ili wao pia wapate upendo na wokovu wa Muumba.
Katika uzoefu huu wote wa kuteswa kikatili na serikali ya CCP, ni Mwenyezi Mungu aliyeniongoza katika kila hatua kushinda kuzingira kwa pepo, na kuniongoza kutoka kwenye pango la shetani la wakatili. Jambo hili lilinifanya nigundue kwa dhati: Bila kujali jinsi Shetani anavyoweza kuwa mkali, mkatili na mwenye kuenea pote, atakuwa daima adui wa Mungu aliyeshindwa, na ni Mwenyezi Mungu pekee ndiye mwenye mamlaka ya juu zaidi ambaye anaweza kuwa msaada wetu thabiti, Anayeweza kutuongoza kumshinda Shetani na kushinda kifo, na Anayeweza kutuwezesha kuishi kwa uthabiti katika nuru ya Mungu. Kama tu Mwenyezi Mungu asemavyo: “Nguvu za Mungu za maisha zinaweza kutawala juu ya nguvu zozote; zaidi ya hayo, inazidi mamlaka yoyote. Maisha Yake ni ya milele, nguvu zake za ajabu, na nguvu Zake za maisha haziwezi kuzidiwa na kiumbe yeyote au nguvu za adui. Nguvu za maisha ya Mungu zipo, na hung’aa mwangaza wake ulio mzuri sana, bila ya kujali muda au mahali. Mbingu na dunia zinaweza kupitia mabadiliko makubwa, lakini uzima wa Mungu ni ule ule daima. Mambo yote hupita, lakini maisha ya Mungu hubaki, kwa maana Mungu ni chanzo cha kuwepo kwa mambo yote, na mizizi ya kuwepo kwao” (Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Ni Kristo wa Siku za Mwisho Pekee Ndiye Anayeweza Kumpa Mwanadamu Njia ya Uzima wa Milele). Kuanzia siku hii na kuendelea, natamani kumfuata Mwenyezi Mungu kwa uthabiti, kufanya juu chini kufuatilia ukweli, na kupata uzima wa milele ambao Mungu humpa mwanadamu.
Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?