Kusikiliza Sauti ya Mungu na Kumkaribisha Bwana

13/08/2020

Mwenyezi Mungu anasema, “Watu wengi wanaweza kukosa kujali kuhusu kile Ninachosema, lakini bado Nataka kumwambia kila anayedaiwa kuwa mtakatifu wa Mungu anayemfuata Yesu kwamba, mtakapoona Yesu Akishuka kutoka juu mbinguni juu ya wingu jeupe kwa macho yenu wenyewe, huu ndio utakuwa mwonekano wa umma wa Jua la haki. Pengine huo utakuwa wakati wa furaha kubwa kwako, ilhali lazima ujue kuwa wakati utakaposhuhudia Yesu Akishuka kutoka mbinguni ndio pia wakati ambapo utaenda chini kuzimu kuadhibiwa. Huo ndio utakuwa wakati wa mwisho wa mpango wa Mungu wa usimamizi na ndio utakuwa wakati ambapo Mungu atawatunukia wazuri na kuwaadhibu waovu. Kwani hukumu ya Mungu itakuwa imeisha kabla ya mwanadamu kuona ishara, wakati kuna onyesho la ukweli tu. Wale wanaokubali ukweli na hawatafuti ishara, na hivyo wametakaswa, watakuwa wamerudi mbele za kiti cha enzi cha Mungu na kuingia katika kumbatio la Muumba. Ni wale tu ambao wanashikilia imani kwamba ‘Yesu Asiyeshuka juu ya wingu jeupe ni Kristo wa uongo’ watakabiliwa na adhabu ya milele, kwani wanaamini tu katika Yesu ambaye Anaonyesha ishara, lakini hawamkubali Yesu Anayetangaza hukumu kali na Anatoa njia ya kweli ya uzima. Na hivyo itakuwa tu kuwa Yesu Atawashughulikia tu Atakaporejea wazi wazi juu ya wingu jeupe(Neno Laonekana katika Mwili). Maneno ya Mungu yanafichua kuwa, kosa kubwa zaidi ambalo waumini hufanya katika kumkaribisha Bwana, ni kushikilia maana ya wazi ya Andiko, na kumsubiri Arudi akiwa juu ya wingu. Hata wanaposikia kwamba Amerudi na Anafanya kazi ya hukumu katika siku za mwisho, wao hawatafuti au kujaribu kusikiliza sauti ya Mungu. Hakuna anayefikiri kwamba watu watakapomwona Bwana Yesu akishuka juu ya wingu, kazi ya Mungu ya kuwaokoa wanadamu tayari itakuwa imemalizika. Watakuwa wakilia na kusaga meno yao. Kushikilia mawazo bila kutafuta ukweli ni hatari sana! Kwa sababu ya kushikilia mawazo zangu mwenyewe, karibu nikose nafasi yangu ya kumkaribisha Bwana.

Nilikuwa mhubiri katika kanisa la nyumbani. Kufikia waka wa 1996, nilihisi mtupu sana kiroho kiasi kwamba nilikuwa nikisikiliza mahubiri mengine. Na nilisikia, kwamba Umeme wa Mashariki lilishuhudia kwamba Bwana alikuwa Amerejea katika mwili, kwamba Alikuwa akifanya kazi ya hukumu ya siku za mwisho, ndugu wengine tayari walikuwa, wamejiunga na Umeme wa Mashariki. Nilistaajabu na kuwaza, “Bwana amerudi? Inawezekanaje? Biblia inasema, ‘Ninyi wanadamu wa Galilaya, mbona mnasimama mkiangalia mbinguni? huyu Yesu, ambaye amechukuliwa kutoka kwa ninyi kwenda mbinguni, atakuja kwa namna hiyo hiyo ambayo mmemuona akienda mbinguni’ (Matendo 1:11). Bwana anapaswa kurudi juu ya wingu kama mwili Wake wa kiroho uliofufuka. Kwa kuwa hatujawahi kuona kitu kama hicho, mtu yeyote anawezeje kusema kwamba Amerudi? Habari hiyo inayohusu kazi ya Mungu ya hukumu katika mwili, haiaminiki.” Kwa hivyo sikuwahi kusikiliza mahubiri ya Umeme wa Mashariki.

Siku moja, Ndugu Wang aliwaleta wahubiri wengine kanisani kwetu. Alisema kwamba mahubiri yao yalikuwa na nuru ya Roho Mtakatifu na kwamba sote tungejifunza jambo. Nilisisimuka na niliwaalika wale ndugu wengine. Katika mkutano huo, dada wawili waliunganisha Biblia na ushirika wao juu ya maana ya kazi ya Mungu katika Enzi ya Sheria, na ya Neema. Walizungumza kuhusu jinsi tunavyoishi katika mzunguko mwovu wa kufanya dhambi na kukiri, jinsi tulivyo wachafu na wasiostahili kumwona Bwana, na jinsi Biblia ilivyosema kwamba Bwana atatuhukumu na kututakasa Atakaporudi katika siku za mwisho ili kutatua asili yetu ya dhambi. Hivyo ndivyo tutavyokombolewa toka katika dhambi na tutakavyostahili ufalme wa mbinguni. Bwana Yesu alisema, “Bado ningali nayo mengi ya kuwaambieni, lakini hivi sasa hamwezi kuyavumilia. Hata hivyo, wakati Yeye, Roho wa ukweli, atakapokuja, Atawaongoza hadi kwenye ukweli wote(Yohana 16:12-13). Na pia: “Kwa kuwa mimi sikuja ili niihukumu dunia, bali kuiokoa dunia. Yeye ambaye ananikataa Mimi, na hayakubali maneno Yangu, ana yule ambaye anamhukumu: neno hilo ambalo nimelisema, ndilo hilo ambalo litamhukumu katika siku ya mwisho(Yohana 12:47-48). Katika miaka yangu kumi ya imani, sikuwahi kusikia ushirika kama huo. Nilihitaji kusikia zaidi, kwa hivyo niliwaalika kina dada hao nyumbani kwangu ili nisikie ushirika zaidi. Dada mmoja alizungumza juu ya maneno ya Mungu, “Ngurumo Saba Zatoa Sauti—Zikitabiri Kuwa Injili ya Ufalme Itaenea Kote Ulimwenguni.” Alisema kwamba Bwana Yesu alikuwa Amerudi, kama Mwenyezi Mungu, Kristo wa siku za mwisho. Niliposikia maneno ya Mungu yakitaja “Umeme unamulika moja kwa moja kutoka Mashariki kwenda Magharibi,” niligundua kwamba huu ulikuwa Umeme wa Mashariki. Na nilishtuka na kusikitika pia. Inawezekanaje? Sikuwa nimesikia mahubiri kama hayo ya kutia nuru kwa miaka mingi. Nilikuwa nimefurahia sana, nikifikiri kwamba nilikuwa nimepata kazi ya Roho Mtakatifu na kupata riziki ya maji yaliyo hai. Lakini ilikuwa Umeme wa Mashariki! Imeandikwa katika Biblia kwamba Bwana atarudi katika umbo Lake la kiroho, na kutupeleka mbinguni moja kwa moja. Je, wanawezaje kusema kwamba Bwana alikuwa Amerudi akiwa mwenye mwili? Sikuelewa hayo. Sikutaka kusikia neno lingine. Iwapo ningewaacha wanipotoshe, nilidhani kwamba miaka yangu ya imani ingekuwa bure. Na nilitaka tu kuwasindikiza waondoke. Lakini hata hivyo, baada ya kuwa pamoja nao kwa wiki mbili, nilikuwa nimeona kwamba waliishi kwa kudhihirisha ubinadamu mzuri. Na ilikuwa katikati ya msimu wa baridi kwa hivyo kulikuwa na baridi kali, na ilikuwa usiku wa manane. Nilihisi kwamba kuwafukuza kungekuwa ukatili. Nilichanganyikiwa sana kwa muda. Sikujua mapenzi ya Mungu yalikuwa yapi na nilikanganyikiwa. Nilitoa kisingizio cha kwenda chumbani mwangu na nikamwomba Bwana: “Ee Bwana, ushirika wa kina dada hawa hakika una mwanga, lakini ninaogopa kupotoshwa. Nimepotea sana na sijui jinsi ya kujibu. Bwana, tafadhali nionyeshe njia.” Kisha nikakumbuka kwamba Bwana Yesu alitufundisha tuwatendee watu kwa upendo. Kuwafukuza kusingekubaliana na mapenzi ya Mungu. Mapenzi ya Bwana yalikuwa niwaache wakae.

Nilipowakabili wale dada wawili, nilizidiwa sana na hisia. Sikuweza kujituliza. Nilijua kwamba ushirika wao ulitia nuru, na kwamba ulitoka kwa Roho Mtakatifu, lakini ushirika wao kwamba Mungu alikuwa tayari Amerudi katika mwili ulitofautiana na mawazo yangu. Kwa hivyo nilifikiri kwamba nilipaswa tu kuwauliza swali langu. Na kwa hivyo, niliwauliza: “Mnashuhudia kwamba Bwana Yesu amerudi katika mwili. Lakini siwezi kuwaamini. Imeandikwa katika Biblia, ‘Ninyi wanadamu wa Galilaya, mbona mnasimama mkiangalia mbinguni? huyu Yesu, ambaye amechukuliwa kutoka kwa ninyi kwenda mbinguni, atakuja kwa namna hiyo hiyo ambayo mmemuona akienda mbinguni’ (Matendo 1:11). Ni mwili wa kiroho wa Bwana, ambao uliopaa mbinguni, na kwa hivyo mwili Wake wa kiroho ndio Utakaorudi juu ya wingu. Kwa hivyo mnawezaje kusema kwamba Amerudi katika mwili?”

Nilipata jibu langu kutoka kwa Dada Li. “Unabii mwingi wa Biblia huzungumza kuhusu Bwana kurudi katika mwili. Bwana Yesu alisema: ‘Kwa kuwa kama umeme unavyotokea mashariki, na kumulika pia magharibi; ujio wa Mwana wa Adamu utakawa hivyo pia(Mathayo 24:27). ‘Na ninyi pia muwe tayari: maana katika saa kama hii msiyofikiria kuwa Mwana wa Adamu atakuja(Luka 12:40). ‘Kwani kama umeme, unavyomulika chini ya mbingu kutoka sehemu moja, huangaza hadi sehemu nyingine chini ya mbingu; vivyo ndivyo Mwana wa Adamu atakuwa katika siku yake. Bali kwanza lazima apitie mambo mengi, na akataliwe na kizazi hiki(Luka 17:24-25). Maneno ya Mungu yanataja ‘Mwana wa Adamu’ na ‘ujio wa Mwana wa Adamu.’ Maneno ‘Mwana wa Adamu’ yanamaanisha Yule ambaye Amezaliwa na mwanadamu, na Aliye na ubinadamu wa kawaida. Katika umbo Lake la kiroho, hawezi kuitwa ‘Mwana wa Adamu.’ Yehova Mungu ni Roho; Hawezi kuitwa, ‘Mwana wa Adamu.’ Malaika ni roho na hawaitwi ‘Mwana wa Adamu.’ Bwana Yesu aliitwa Kristo, Mwana wa Adamu, kwa sababu Yeye alikuwa Roho wa Mungu mwenye mwili, na Ana ubinadamu wa kawaida.” “Kwa hivyo Bwana Yesu aliposema: ‘ujio wa Mwana wa Adamu’ na ‘Mwana wa binadamu anakuja,’ Alimaanisha kuwa Bwana atarudi, katika mwili katika siku za mwisho.”

Kusikiliza Sauti ya Mungu na Kumkaribisha Bwana

Dada Zhou alisema, “Bwana Yesu alitabiri kurudi Kwake mwenyewe: ‘Bali kwanza lazima apitie mambo mengi, na akataliwe na kizazi hiki.’ Mungu anafanya kazi katika mwili kama Mwana wa Adamu katika siku za mwisho. Watu hawamtambui kama Kristo na wanamchukulia kama mtu wa kawaida. Wale ambao hawapendi ukweli au wasiotafuta kusikia sauti ya Mungu kwa kweli wanampinga na kumkana Kristo. Ulimwengu wa kidini na utawala wa Shetani pia unamshutumu na kumkataa Kristo. Na hii inatimiza unabii: ‘Bali kwanza lazima apitie mambo mengi, na akataliwe na kizazi hiki.’ Kama Bwana angekuja katika umbo Lake la kiroho katika siku za mwisho Akiwa juu ya wingu na kwa utukufu, bila shaka kila mtu angeanguka mbele Yake. Je, unabii huu unaweza kutimia?”

Kisha nilianza kuelewa kwamba kama Bwana angeonekana katika umbo Lake la kiroho katika siku za mwisho, hakuna mtu ambaye angeenda kinyume na Yeye, bali wote wangemfuata. Basi unabii huu, “Bali kwanza lazima apitie mambo mengi, na akataliwe na kizazi hiki.” usingetimia. Nilifikiria jinsi Umeme wa Mashariki unavyoshuhudia kwamba Bwana Yesu amerudi na ulimwengu wa dini na CCP wanashutumu hilo. Je, hiyo haitimizi unabii wa Bwana wa kukataliwa? Kwa hivyo, Mwenyezi Mungu anaweza kuwa Bwana Yesu aliyerudi? Bado sikuelewa kabisa. Biblia kweli inatabiri kuja kwa Mwana wa Adamu, lakini Bwana pia alisema: “Tazama, anakuja na mawingu; nalo kila jicho litamwona yeye, na pia wale waliomdunga: na makabila yote ya ulimwengu yatalia kwa huzuni kwa sababu ya yeye(Ufunuo 1:7). Nilikanganyikiwa.

Kwa hivyo niliwaambia kuhusu jinsi nilivyokanganyikiwa na Dada Li akaniambia: “Bwana ni mwaminifu. Kwa hivyo, kila neno Lake litatimia. Ni suala la wakati tu sasa. Kuna unabii mwingi unaohusu kurudi Kwake. Mbali na Yeye kuja juu ya wingu, kuna pia unabii juu Yake kuwa mwili na kuja kwa siri. Kwa mfano Bwana alisema ‘Tazama, mimi nakuja kama mwizi(Ufunuo 16:15). ‘Na kukawa na kelele saa sita ya usiku, Tazama, anakuja bwana arusi; ondokeni nje ili kumkaribisha(Mathayo 25:6). ‘Lakini juu ya hiyo siku na saa hiyo hakuna mtu anayejua, wala malaika wa mbinguni, isipokuwa Baba yangu tu(Mathayo 24:36). Na Bwana aliposema ‘kama mwizi,’ ‘Na kukawa na kelele saa sita ya usiku,’ na ‘Lakini juu ya hiyo siku na saa hiyo hakuna mtu anayejua,’ Alikuwa akizungumza kuhusu kurudi kwa siri. Katika siku za mwisho, Bwana anarudi kwa njia mbili tofauti sana. Anapata mwili kwa siri kama Mwana wa Adamu na pia Anarudi kwetu hadharani juu ya wingu. Hiyo inamaanisha kwamba, kwanza Anarudi kwetu katika mwili sirini ili kuwahukumu wanadamu kwa ukweli na kufanyiza kundi la washindi kabla ya maafa. Atakapomaliza kuwaokoa wanadamu kwa siri, maafa yatatokea na, Atawatuza wema na kuwaadhibu waovu. Wakati huo tu ndipo Mungu atajidhihirisha kwa mataifa yote na watu wote. Wakati huo ndipo unabii wa Bwana kuja hadharani utakapotimia.” “Wote wanaokubali kazi ya hukumu ya Mwenyezi Mungu na wanaotakaswa upotovu wao, watalindwa na Mungu, wataokolewa na wataingia katika ufalme wa Mungu.” “Lakini wale wanaokataa kazi ya Mwenyezi Mungu ya siku za mwisho, wanaoipinga na kuishutumu, watakuwa wakilia na kusaga meno yao na kuadhibiwa. Na unabii huu utatimia: ‘Tazama, anakuja na mawingu; nalo kila jicho litamwona yeye, na pia wale waliomdunga: na makabila yote ya ulimwengu yatalia kwa huzuni kwa sababu ya yeye(Ufunuo 1:7).” Kisha alisoma maneno haya ya Mwenyezi Mungu. “Watu wengi wanaweza kukosa kujali kuhusu kile Ninachosema, lakini bado Nataka kumwambia kila anayedaiwa kuwa mtakatifu wa Mungu anayemfuata Yesu kwamba, mtakapoona Yesu Akishuka kutoka juu mbinguni juu ya wingu jeupe kwa macho yenu wenyewe, huu ndio utakuwa mwonekano wa umma wa Jua la haki. Pengine huo utakuwa wakati wa furaha kubwa kwako, ilhali lazima ujue kuwa wakati utakaposhuhudia Yesu Akishuka kutoka mbinguni ndio pia wakati ambapo utaenda chini kuzimu kuadhibiwa. Huo ndio utakuwa wakati wa mwisho wa mpango wa Mungu wa usimamizi na ndio utakuwa wakati ambapo Mungu atawatunukia wazuri na kuwaadhibu waovu. Kwani hukumu ya Mungu itakuwa imeisha kabla ya mwanadamu kuona ishara, wakati kuna onyesho la ukweli tu(Neno Laonekana katika Mwili).

Macho yangu yalifunguliwa ghafla. Kurudi kwa Bwana kunafanyika kwa hatua. Kwanza Anapata mwili na Ananena na kufanya kazi kwa siri, kisha Anarudi juu ya wingu hadharani. Nilikuwa nikiwekea mipaka kuja kwa Bwana hadharani tu kwa sababu ya fikira na mawazo yangu. Nilikosea. Sikuthubutu kushikilia mawazo yangu na nilikumbuka maneno ya Bwana. “Kwa sababu kila anayeomba hupata; na yeye ambaye hutafuta hupata; na apigaye hodi atafunguliwa(Mathayo 7:8). Sasa kwa kuwa nilikabiliwa na kurudi kwa Bwana, ilibidi niwe na moyo umchao Mungu na nitafute kwa dhati. Haya ni mapenzi ya Mungu. La sivyo, ningeondolewa na Bwana! Kisha niliwauliza, “Ikiwa Bwana kwanza anakuwa mwili ili Afanye kazi kwa siri. tunawezaje kuwa na hakika kwamba Mwenyezi Mungu ni Mungu katika mwili, Kristo wa siku za mwisho?”

Kisha Dada Li alijibu kwa furaha sana, “Kwa maelfu ya miaka, hakuna mtu ambaye ameelewa siri hii juu ya kupata mwili kwa Mungu kunamaanisha nini hasa.” “Na sasa, Mwenyezi Mungu ametufunulia siri hii.” Kisha alisoma vifungu vifuatavyo. “Maana ya kupata mwili ni kwamba Mungu Anajionyesha katika mwili, na Anakuja kufanya kazi miongoni mwa wanadamu wa uumbaji Wake katika umbo la mwili. Hivyo, ili Mungu kuwa mwili, ni lazima kwanza Apate umbo la mwili, mwili wenye ubinadamu wa kawaida; hili ndilo hitaji la kimsingi zaidi. Kwa kweli, maana ya kupata mwili kwa Mungu ni kwamba Mungu Anaishi na kufanya kazi katika mwili, Mungu katika kiini Chake Anakuwa mwili, Anakuwa mwanadamu.” “Kupata mwili kunamaanisha kwamba Roho wa Mungu Anakuwa Mwili, yaani, Mungu Anakuwa mwili; kazi Anayoifanya katika mwili ni kazi ya Roho, inayothibitika katika mwili, na kuonyeshwa kwa mwili. Hakuna mwingine ila tu mwili wa Mungu Anayeweza kutimiza huduma ya Mungu mwenye mwili; yaani, mwili wa Mungu kuwa mwili pekee, ubinadamu huu wa kawaida—na hakuna mwingine yeyote—anayeweza kuonyesha kazi ya uungu.” “Mungu mwenye mwili Anaitwa Kristo, na Kristo ni mwili uliovishwa na Roho wa Mungu. Mwili huu ni tofauti na wa mwanadamu yeyote aliye wa nyama. Tofauti hii ni kwa sababu Kristo sio wa mwili na damu bali ni mwili wa Roho. Anao ubinadamu wa kawaida na uungu kamili. Uungu Wake haujamilikiwa na mwanadamu yeyote. Ubinadamu Wake wa kawaida unaendeleza shughuli Zake zote za kawaida katika mwili, wakati uungu Wake unafanya kazi ya Mungu Mwenyewe.” “Yeye Aliye mwili wa Mungu Atakuwa na dutu ya Mungu, na Yule Aliye Mungu katika mwili Atakuwa na maonyesho ya Mungu. Kwa maana Mungu Hupata mwili, Ataleta mbele kazi Anayopaswa kufanya, na kwa maana Mungu Amepata mwili, Ataonyesha kile Alicho na Ataweza kuuleta ukweli kwa mwanadamu, kumpa mwanadamu uhai, na Amwonyeshe mwanadamu njia. Mwili usio na dutu ya Mungu kwa kweli sio Mungu mwenye mwili; kwa hili hakuna tashwishi. Kupeleleza kama kweli ni mwili wa Mungu mwenye Mwili, mwanadamu lazima aamue haya kutoka kwa tabia Yeye huonyesha na maneno Yeye hunena. Ambayo ni kusema, kama ni mwili wa Mungu mwenye mwili au la, na kama ni njia ya kweli au la, lazima iamuliwe kutokana na dutu Yake. Hivyo, katika kudadisi[a] iwapo ni mwili wa Mungu mwenye mwili, cha msingi ni kuwa makini kuhusu dutu Yake (Kazi Yake, maneno Yake, tabia Yake, na mengine mengi), bali sio hali ya sura Yake ya nje. Mwanadamu akiona tu sura Yake ya nje, na aipuuze dutu Yake, basi hilo linaonyesha upumbavu na ujinga wa mwanadamu(Neno Laonekana katika Mwili).

Dada Li aliendelea: “Kristo kwa kweli ni Mungu katika mwili. Yeye ni Roho wa Mungu aliyevalia mwili, ambaye Amekuwa mtu wa kawaida, Akifanya kazi na kunena maneno miongoni mwa wanadamu. Mungu mwenye mwili Anaonekana kama mtu wa kawaida, si mtu wa hali ya juu au wa mwujiza. Ana mantiki na hisia zote za mtu wa kawaida. Yeye hata huingiliana na watu pia. Tofauti ni kwamba, mbali na kuwa na ubinadamu wa kawaida, Yeye pia ana kiini cha Mungu. Kristo anaweza kufanya kazi ya Mungu mwenyewe na kutamatisha enzi nzee na kuanzisha mpya. Kiini Chake ni: ukweli, njia, na uzima.” “Anaweza kuonyesha ukweli wakati wowote. Anaweza kuwaruzuku watu na kutatua matatizo yetu, na kutupa njia ya kutenda. Kristo anaweza kufichua siri, kuonyesha tabia ya Mungu, na hekima Yake na uweza Wake. Maneno ya Kristo yanaweza kufanikisha yote. Hakuna mwanadamu anayeweza kufanya hivi.” “Bwana Yesu alionekana kama mtu wa kawaida. Lakini Alikuwa na kiini cha Mungu. Kuonekana Kwake na kazi Yake, vilianzisha Enzi ya Neema na kutamatisha Enzi ya Sheria. Alitupa njia ya toba na kusamehe dhambi zetu, na Alituambia tusamehe sabini mara saba. Alionyesha tabia ya Mungu ya huruma. Pia Alionyesha ishara na miujiza mingi Alipokuwa akifanya kazi, kama vile kuwafanya viwete watembee, kuwaponya vipofu, kutuliza bahari kwa kusema neno moja, kuwafufua wafu, na kuwalisha maelfu ya watu kwa samaki wawili na mikate mitano. Hii ilifichua mamlaka ya Mungu kikamilifu. Kazi na maneno ya Bwana Yesu na tabia ambayo Alionyesha vilikuwa ushahidi mzuri kwamba Yeye kweli alikuwa Mungu katika mwili.” “Ni Mungu pekee Anayeweza kuonyesha ukweli, na kutamatisha enzi nzee na kuanzisha enzi mpya, kuonyesha tabia ya Mungu na hekima Yake. Kando na Mungu, hakuna anayeweza kuonyesha ukweli au kuonyesha kile Mungu alicho, au kufanya kazi Yake. Hivi ndivyo tunavyoamua ikiwa Yeye kwa kweli ni Mungu katika mwili, Kristo wa siku ya mwisho. Jambo la muhimu zaidi ni kuchunguza maneno na kazi ya Kristo. Ikiwa Anaonyesha ukweli, na tabia ya Mungu, na Anafanya kazi ya Mungu, basi Yeye ni Mungu katika mwili. Yeye ni Kristo.”

Kupitia ushirika wake, nilielewa kwamba Mungu katika mwili Anaweza kuonyehsa ukweli, na kufanya kazi ya Mungu. Na huo ndio uhalisi.

Dada Zhou aliongeza: “Hatuwezi kujua ikiwa Mwenyezi Mungu ni Mungu katika mwili kwa kuangalia tu umbo Lake la nje. Lazima tuwe na hakika kutokana na maneno Yake, kazi na tabia Yake. Katika siku za mwisho, Mwenyezi Mungu anafanya kazi ya hukumu, Juu ya msingi wa kazi ya Bwana Yesu ya ukombozi. Ameitamatisha Enzi ya Neema na kuanzisha Enzi ya Ufalme. Mwenyezi Mungu ametamka mamilioni ya maneno. na Ameonyesha mpango wa Mungu wa usimamizi wa miaka 6,000, siri ya Biblia na kupata mwili kwa Mungu. Amefichua jinsi ambavyo Shetani huwapotosha watu na jinsi Mungu anavyowaokoa wanadamu, jinsi Mungu anavyofanya kazi ya kuwahukumu na kuwatakasa watu katika siku za mwisho, jinsi Yeye anavyowaainisha watu kulingana na aina yao na kuamua mwisho na hatima ya watu. Mwenyezi Mungu anaonyesha tabia Yake ambayo kimsingi ni ya haki, Akihukumu na kufunua asili yetu ya kishetani ya kumpinga Mungu na tabia zetu potovu. Anatuonyesha njia ya kuondoa uovu na pia kutakaswa.” Dada Zhou pia alishiriki jinsi alivyopitia hukumu. Alisema, “Sikuona jinsi nilivyokuwa mpotovu, hadi nilipohukumiwa na kujaribiwa, kupogolewa, kuadibiwa na kushughulikiwa kupitia maneno ya Mungu. Niliwamini Mwenyezi Mungu lakini bado nilimpinga kwa sababu ya asili yangu potovu na ya kishetani, kama jinsi nilivyopenda kujionyesha na kuwafanya watu waniheshimu. Niliwakaripia wengine mara kwa mara na niliwalazimisha wafanye kile nilichosema. Nilidanganya kila wakati ili kulinda masilahi yangu mwenyewe, na kadhalika. Kupitia hukumu ya maneno ya Mungu, nilianza kumcha moyoni mwangu kwa sababu ya tabia Yake ya haki. Pia nilianza kulenga kutenda ukweli ili kutatua asili yangu ya kishetani. Kulikuwa na mabadiliko kidogo katika tabia yangu. Je, matokeo ya maneno na kazi ya Mwenyezi Mungu hayatoshi kuthibitisha kwamba Yeye ni Mungu mwenye mwili, kwamba Yeye ndiye Kristo wa siku za mwisho? Kwamba Yeye ni Mungu katika mwili?”

Ushirika wa dada huyo uliuchangamsha moyo wangu. Jambo la muhimu katika kuthibitisha ikiwa Yeye ni Mwana wa Adamu, Kristo katika mwili ni kuona ikiwa Anaweza kuonyesha maneno na tabia ya Mungu, na iwapo Yeye anaweza kutamatisha enzi nzee na kuanzisha enzi mpya. Mwenyezi Mungu ameonyesha ukweli mwingi na Anafanya kazi ili kuwahukumu na kuwatakasa wanadamu. Ameanzisha Enzi ya Ufalme na kutamatisha Enzi ya Neema. Hakika Yeye ndiye Kristo, kurudi kwa Bwana! Sikuwahi kuelewa ukweli hapo zamani. Nilisubiri tu bila kufikiria Bwana arudi juu ya wingu. Sikujisumbua kutafuta niliposikia kwamba Alikuwa amerudi. Karibu nipoteze nafasi yangu ya kuunganishwa tena na Yeye. Nilikuwa mjinga kama nini!

Baada ya hapo, nilikula maneno ya Mwenyezi Mungu. Na nilijifunza ukweli mwingi ambao sikuwahi kuelewa katika imani yangu hapo awali. Nilikuwa na hakika kwamba Mwenyezi Mungu ndiye Bwana Yesu aliyerudi! Nilishiriki kazi ya Mwenyezi Mungu ya siku za mwisho na zaidi ya kina ndugu 100 ambao niliweza kuwasiliana nao. Waliposoma maneno Yake na kusikia sauti Yake, waliguswa sana kiasi kwamba walilia. Walimgeukia Mwenyezi Mungu na walikubali kazi Yake na kuhudhuria karamu ya Mwanakondoo!

Tanbihi:

a. Nakala halisi ya mwanzo inasema “na kwa.”

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Maudhui Yanayohusiana

Sikiliza! Ni Nani Huyu Anenaye?

Na Zhou Li, ChinaKama mhubiri wa kanisa, hakuna jambo linaloumiza zaidi kama udhaifu wa kiroho na kutokuwa na lolote la kuhubiri. Nilihisi...

Kurejea kwa Mwana Mpotevu

Na Ruth, MarekaniNilizaliwa katika mji mdogo kusini mwa China, katika familia ya uumini ambao ulianzia na kizazi cha bibi ya baba yangu....

Leave a Reply

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp