Sasa Naelewa Uhusiano Kati ya Biblia na Mungu

03/09/2020

Mwenyezi Mungu anasema, “Kwa miaka mingi, imani ya watu ya kitamaduni (hiyo ya Ukristo, moja ya dini kuu tatu za dunia) imekuwa ni kusoma Biblia; kujitenga na Biblia sio imani kwa Bwana, kujitenga na Biblia ni kufuata imani tofauti tofauti na uzushi, na hata pale watu wanaposoma vitabu vingine, msingi wa vitabu hivi ni lazima uwe ni ufafanuzi wa Biblia. Ni kusema kwamba, kama unasema unamwamini Bwana, basi ni lazima usome Biblia, unapaswa kula na kunywa Biblia, na nje ya Biblia hupaswi kuabudu kitabu kingine ambacho hakihusishi Biblia. Ikiwa utafanya hivyo, basi unamsaliti Mungu. Kuanzia kipindi ambapo kulikuwa na Biblia, imani ya watu kwa Bwana imekuwa imani katika Biblia. Badala ya kusema watu wanamwamini Bwana, ni bora kusema kwamba wanaamini Biblia; badala ya kusema wameanza kusoma Biblia, ni bora kusema wameanza kuamini Biblia; na badala ya kusema wamerudi mbele ya Bwana, ingekuwa vyema kusema wamerudi mbele ya Biblia. Kwa njia hii, watu wanaiabudu Biblia kana kwamba ni Mungu, kana kwamba ni damu yao ya uzima na kuipoteza itakuwa ni sawa na kupoteza maisha yao. Watu wanaitazama Biblia kuwa ni kuu kama Mungu, na hata kuna wale wanaoiona kuwa ni kuu kuliko Mungu. Kama watu hawatakuwa na kazi ya Roho Mtakatifu, ikiwa hawawezi kuhisi Mungu, wanaweza kuendelea kuishi—lakini punde tu watakapoipoteza Biblia, au kupoteza sura na maneno maarufu sana kutoka katika Biblia, basi inakuwa ni kana kwamba wamepoteza maisha yao. … Biblia imekuwa sanamu katika akili za watu, limekuwa ni fumbo katika akili zao, na hawawezi kabisa kuamini kwamba Mungu anaweza kufanya kazi nje ya Biblia, hawawezi kuamini kwamba watu wanaweza kumpata Mungu nje ya Biblia, achilia mbali kuwa na uwezo wa kuamini kwamba Mungu angeweza kujitenga na Biblia wakati wa kazi ya mwisho na kuanza upya. Hili suala haliingii akilini mwa watu; hawawezi kuliamini, na wala hawawezi kulifikiria. Biblia imekuwa kikwazo kikubwa kwa watu kukubali kazi mpya ya Mungu, na imefanya kuwa vigumu kwa Mungu kuipanua kazi hii mpya(Neno Laonekana katika Mwili). Biblia hapo zamani ndiyo iliyonisaidia kumjua Bwana katika imani yangu na mchungaji wetu alisema daima kwamba ndiyo ilikuwa msingi wa imani yetu. Nilidhani imani katika Biblia ilikuwa imani katika Bwana na hata nililiweka neno lake juu ya Bwana. Nilikuwa tayari na vifungu fulani vilivyochakaa kila wakati bila kufikiri juu ya kutenda maneno ya Bwana. Kabla ya kuikubali kazi ya Mwenyezi Mungu ya siku za mwisho na kuona yale yaliyoonyeshwa na maneno Yake, sikuelewa uhusiano kati ya Mungu na Biblia. Makosa niliyokuwa nayo katika imani yangu hatimaye yalisuluhishwa.

Nilikuwa nikiisoma Biblia, kuhudhuria ibada za kanisa kila nilipoweza na kutafuta mahubiri mtandaoni katika wakati wangu wa ziada ili kumwelewa Bwana zaidi. Wakati mmoja, nilipata filamu ya kanisa kwenye YouTube, iliyokuwa nzuri kabisa iitwayo Maskani Yangu Yako Wapi. Ilikuwa ya dhati na yenye kugusa sana Na maneno waliyosoma katika sinema yalionekana kuwa makunjufu na yenye mamlaka. Nilikuwa na hamu kujua walitoka wapi. Nilipoona kwamba lilikuwa Kanisa la Mwenyezi Mungu niliangalia mtandaoni ili kujifunza zaidi kuhusu kanisa hili ambalo lilikuwa limetengeneza sinema hiyo. Lakini kisha nilipata mambo mabaya yaliyokuwa yameandikwa kuhusu kanisa hili na sikuelewa ikiwa mambo hayo mabaya yalikuwa ya kweli au la. Baada ya kufikiria zaidi juu ya hilo, niliamua kutoamini yale ambayo wengine walisema. “Usiamini kila kitu unachosikia.” Nilijua nilipaswa nichunguze mwenyewe nione ikiwa lilikuwa kanisa zuri. Nilipakua sinema nyingine zaidi ili nizitazame. Nilitazama nyingine mbili, Mwamko na Kutamani Sana. Zilinigusa sana. Maneno yaliyosomwa ndani ya filamu hizo yalikuwa yenye nguvu na makuu, na mahubiri yalikuwa ya vitendo sana. Nilijifunza yote kuhusu ukiwa wa makanisa na maana ya kuokolewa kwa kweli ni nini. Sinema zilisema Bwana Yesu alikuwa tayari amerudi kutekeleza hukumu Yake katika siku za mwisho ambayo inatimiza unabii huu wa Biblia: “Kwa maana muda umekuja ambao lazima hukumu ianze katika nyumba ya Mungu(1 Petro 4:17). Nilifurahia sana. Maneno hayo yaliyosomwa katika sinema yalitamkwa na Bwana aliyerejea. Si ajabu yalikuwa yenye nguvu na yanayogusa sana! Nilituma ujumbe na nikawasiliana na washiriki fulani wa kanisa hilo na walikuwa wachangamfu na wa kweli, na mahubiri yao yalitia nuru. Kuzungumza nao lilikuwa jambo zuri sana. Nilianza kwenda kwenye mikutano yao.

Jioni moja nilikuwa nikitaka kupakua sinema zaidi kutoka kwa Kanisa la Mwenyezi Mungu. Nilipokuwa nikitafuta katika uteuzi wao, nikapata moja inayoitwa Toka Nje ya Biblia. Nilichanganyikiwa. Hiyo ilimaanisha nini? Je, kwa nini tunapaswa kutoka Nje ya Biblia? Je, watu wanawezaje kumwamini na kumjua Mungu bila Biblia? Mchungaji alikuwa akisema kila mara kwamba imani yetu lazima iwe na msingi katika Biblia na kuachana nayo ulikuwa uzushi. Si kuiacha Biblia nyuma kulikuwa kumsaliti Bwana? Kwa siku chache zilizofuata niliacha kutazama sinema za Kanisa na kusikiliza nyimbo zao, nikiogopa kupotea. Lakini sikuweza kujizuia ila kufikiria, “Ikiwa Mwenyezi Mungu ni Bwana Yesu aliyerudi nami nimkatae, je, sitakuwa nikiikosa nafasi yangu ya kumkaribisha Bwana?” Nilichanganyikiwa sana, kwa hivyo niliomba na kufunga. Nilimwomba Bwana anionyeshe ikiwa Mwenyezi Mungu kweli ni kurudi Kwake. Usiku wa kwanza ambao nilikuwa nimefunga, sikupokea msukumo wowote kutoka kwa Mungu, kwa hivyo niliona niangalie katika Biblia. Nilisoma Ufunuo 1:8, “Mimi ndiye Alfa na Omega, Mwanzo na tena mwisho, Akasema Bwana, ambaye yuko, na ambaye alikuweko, na ambaye atakuja, Mwenyezi.” Pia, nilisoma Ufunuo 11:16-17, “Na wao wazee ishirini na wanne, ambao waliketi katika viti vyao mbele ya Mungu, walianguka chini kifudifudi, na kumwabudu Mungu, wakisema, Tunakupa shukrani, Ee BWANA Mungu Mwenyezi, ambaye uko, na ulikuwa, utakuwa, kwa kuwa umeichukua nguvu yako kuu, na umetawala.” Ghafla nilihisi aya hizi ni Mungu akijaribu kunielekeza. Ufunuo kinasema, Mungu ataitwa “Mwenyezi” katika siku za mwisho je, si huyo ni Mwenyezi Mungu? Ugunduzi huu ulinifanya nitamani kuendelea kuchunguza Kanisa la Mwenyezi Mungu. Pia niliitazama Toka Nje ya Biblia kwa ukamilifu, ili nijue ilihusu nini hasa, kwa dhati.

Mhubiri mmoja wa injili kutoka Kanisa la Mwenyezi Mungu katika filamu alishiriki haya: “Watu wengi wa dini husema Mungu hawezi kuondoka katika Biblia kuleta wokovu na kitu chochote kisicho katika Biblia ni uzushi. Ni kipi kilichotangulia: Biblia, au kazi ya Mungu? Hapo mwanzo, Yehova Mungu aliumba vitu vyote. Aliufurika ulimwengu Je, Agano la Kale lilikuwepo Mungu alipokuwa akifanya kazi hii yote?” Niliwaza, “Je, ni lazima uulize? Mungu alipoiumba dunia, akaifurika dunia, na akaiteketeza Sodoma na Gomora ikaisha, Biblia haikuwepo.” Aliendelea: “Hakukuwa na Biblia wakati Mungu alifanya kazi hii. Kwanza ilikuwa kazi ya Mungu, na baada ya kukamilika, basi, iliandikwa katika Biblia. Na Bwana Yesu alipokuwa akifanya kazi katika Enzi ya Neema, hakukuwa na Agano Jipya. Hiyo iliandikwa hapo baadaye na wanafunzi Wake, Alipomaliza kazi Yake. Ni wazi kwamba Biblia ni rekodi ya kihistoria tu ya kazi ya Mungu. Mungu hafanyi kazi kulingana na Biblia na hazuiliwi nayo. Kazi Yake ina msingi katika mpango Wake mtakatifu, na vile vile kulingana na mahitaji ya wanadamu. Hiyo ndiyo maana hatuwezi kuifikiria kazi ya Mungu kuwa tu kile kilicho katika Biblia na hatuwezi kuitumia Biblia kuiwekea mipaka kazi Yake. Hatuwezi kusema kuwa kitu chochote nje ya Biblia ni uzushi. Mungu ana haki ya kufanya kazi Yake mwenyewe na anaweza kutenda nje ya mipaka ya Biblia.”

Sasa Naelewa Uhusiano Kati ya Biblia na Mungu

Kusikia hili kulinifungua macho. Hakukuwa na Agano Jipya wakati Bwana Yesu alifanya kazi. Iliundwa na wengine tu baada ya Yeye kumaliza kazi Yake yote kuu. Biblia ni rekodi ya kazi ya Mungu ya zamani. Kwa nini sikuwahi kufikiria juu ya hilo hapo awali?

Mhubiri mwingine katika sinema aliendelea: “Tukisema kwamba kitu chochote nje ya Biblia ni uzushi, hatutakuwa tukiishutumu kazi yote ya Mungu ya zamani pasi na haki? Bwana Yesu alipokuja, Hakufanya kazi kwa msingi wa Agano la Kale, lakini alienda zaidi ya hayo, kama vile mafundisho Yake juu ya toba, kuponya wagonjwa, kutoa pepo, kutofuata Sabato, kusamehe mara sabini mara saba, na zaidi. Hakuna lolote kati ya hayo lililokuwa hata katika Agano la Kale. Mengine hata yalipingana na sheria za Agano la Kale. Je, hiyo inamaanisha kwamba kazi ya Bwana Yesu haikuwa kazi ya Mungu? Makuhani wakuu, wazee na waandishi wote waliishutumu kazi ya Bwana Yesu na maneno Yake kama uzushi kwa sababu hayakulingana na Agano la Kale madhubuti. Wote walimpinga Mungu. Tukifuata maoni ya uwongo ya wanadamu, tukiamini kitu chochote nje ya Biblia kuwa uzushi, je, sisi pia hatutakuwa tukiishutumu kazi ya Bwana Yesu?”

Kisha wakasoma maneno ya Mwenyezi Mungu kuhusu kitu chochote nje ya Biblia kuwa uzushi. Mwenyezi Mungu anasema, “Biblia ni kitabu cha kihistoria, na ikiwa ungekula na kunywa Agano la Kale wakati wa Enzi ya Neema—ikiwa ungeweka katika vitendo kile kilichokuwa kinatakiwa katika wakati wa Agano la Kale wakati wa Enzi ya Neema—Yesu angekukataa, na kukuhukumu; ikiwa ungetumia Agano la Kale katika kazi ya Yesu, basi ungekuwa Farisayo. Ikiwa, leo, utaweka pamoja Agano Jipya na la Kale kula na kunywa, na kuliweka katika vitendo, basi Mungu wa leo Atakuhukumu; utakuwa umebaki nyuma ya kazi ya leo ya Roho Mtakatifu! Ikiwa unakula na kunywa Agano la Kale na Agano Jipya, basi upo nje ya mkondo wa Roho Mtakatifu! Wakati wa kipindi cha Yesu, Yesu aliwaongoza Wayahudi na wale wote ambao walimfuata Yeye kulingana na kazi ya Roho Mtakatifu katika Yeye wakati huo. Hakuichukulia Biblia kama msingi wa kile Alichofanya, bali Alizungumza kulingana na kazi Yake; Hakutilia maanani kile ambacho Biblia ilisema, wala hakutafuta katika Biblia njia ya kuongoza wafuasi Wake. Kuanzia pale Alipoanza kufanya kazi, Aliongoza njia ya toba—neno ambalo halikutajwa kabisa katika unabii wa Agano la Kale. Sio kwamba tu Hakutenda kulingana na Biblia, lakini pia Aliongoza njia mpya, na Akafanya kazi mpya. Na wala Hakurejelea kabisa Biblia Alipohubiri. Wakati wa Enzi ya Sheria, hakuna ambaye aliweza kufanya miujiza Yake ya kuponya wagonjwa na kutoa mapepo. Hivyo, pia, kazi Yake, mafundisho Yake, na mamlaka na nguvu za maneno Yake yalizidi mtu yeyote wakati wa Enzi ya Sheria. Yesu alifanya tu kazi Yake mpya, na ingawa watu wengi walimhukumu kwa kutumia Biblia—na hata wakatumia Agano la Kale kumsulubisha—kazi Yake ilipitiliza Agano la Kale; kama hii haikuwa hivyo, kwa nini watu walimwangika msalabani? Ilikuwa ni kwa sababu haikusema kitu katika Agano la Kale la mafundisho Yake, na uwezo Wake wa kuponya wagonjwa na kutoa mapepo? Kazi Yake ilikuwa ni kwa ajili ya kuongoza katika njia mpya, haikuwa ni kwa makusudi ya kufanya ugomvi dhidi ya Biblia, au kwa makusudi kujitenga na Agano la Kale. Alikuja tu kufanya huduma Yake, kuleta kazi mpya kwa wale waliomtamani sana na kumtafuta. Hakuja kufafanua Agano la Kale au kutetea kazi yake. Kazi Yake bado haikuwa ni kwa ajili ya kuruhusu Enzi ya Sheria kuendelea kukua, maana kazi Yake haikuzingatia Biblia kama msingi wake; Yesu alikuja kufanya tu kazi ambayo Alipaswa kufanya. … Hata hivyo, kipi ni kikubwa: Mungu au Biblia? Kwa nini ni lazima kazi ya Mungu iwe kulingana na Biblia? Je, inaweza kuwa kwamba Mungu hana haki ya kuwa juu ya Biblia? Je, Mungu hawezi kujitenga na Biblia na kufanya kazi nyingine? Kwa nini Yesu na wanafunzi Wake hawakutunza Sabato? Ikiwa Angetunza Sabato na matendo mengine kulingana na amri za Agano la Kale, kwa nini Yesu Hakutunza Sabato baada ya kuja, lakini badala yake Aliitawadha miguu, Akafunika kichwa, Akavunja mkate, na kunywa divai? Je, sio kwamba haya yote hayapatikani katika amri za Agano la Kale? Ikiwa Yesu aliliheshimu Agano la Kale, kwa nini Aliyakataa mafundisho haya. Unapaswa kujua ni kipi kilitangulia, Mungu au Biblia!(Neno Laonekana katika Mwili).

Wahubiri wa injili katika sinema walishiriki hii: “Biblia siyo Mungu. Ni rekodi ya kweli tu ya hatua mbili za kwanza za kazi, ushuhuda wa kazi ya Mungu katika Enzi ya Sheria na Enzi ya Neema. Haiwakilishi kazi Yake yote ya kumwokoa mwanadamu. Rekodi za maneno ya Mungu katika Biblia ni finyu sana. Ni vidokezo tu vya tabia ya maisha ya Mungu. Haiwezi kuionyesha yote kwa ukamilifu. Mungu si mzee kamwe, ni mpya kila wakati. Yeye hutekeleza kazi mpya na kutamka maneno mapya, katika kila enzi. Kwa mfano, Bwana Yesu alipokuja kufanya kazi katika Enzi ya Neema, Alienda zaidi ya Agano la Kale kutekeleza kazi Yake mpya. Mungu hafanyi kazi kulingana na maandiko au hata kuyarejelea. Kuwaongoza wafuasi Wake wote, Yeye haangalii katika maandiko. Kazi ya Mungu daima husonga mbele. Mungu anapoanza enzi mpya na kufanya kazi mpya, Yeye humwongoza mwanadamu kwenye njia mpya na hutuletea ukweli zaidi ili tupate wokovu Wake kamili.” “Mungu hatuongozi kwa kutegemea kazi Yake ya zamani tu. Hiyo ni kusema, Mungu hafanyi kazi Yake kwa kuifuata Biblia kwa sababu Yeye ni Bwana wa Sabato, na (Bwana) wa Biblia. Yeye ana kila haki ya kuenda zaidi ya Biblia, kufanya kazi mpya kulingana na mpango Wake na mahitaji ya wanadamu.” “Katika enzi mpya, kazi ya Mungu haiwezi kuwa sawa na kazi Yake katika enzi nzee. Kwa hivyo, kusema kwamba kuachana na Biblia ni uzushi ni uwongo mtupu.”

Nilielewa kutoka katika hili kwamba Agano la Kale na Jipya ni rekodi za kazi ya Mungu na maneno katika Enzi ya Sheria na Neema, lakini hazionyeshi kazi yote ya Mungu. Nilidhani kweli kwamba nikiiacha Biblia sitakuwa nikiamini. Je, sikuwa nikimchukulia Mungu kuwa sawa na Biblia? Wakati Bwana Yesu alifanya kazi, Hakuongozwa na Agano la Kale. Tukisema kwenda nje ya maandiko ni uzushi, hatutakuwa tukiishutumu kazi ya Bwana Yesu? Ikiwa ningezaliwa katika wakati ambapo Bwana Yesu alikuwa Akifanya kazi, ningeipinga kazi Yake kulingana na imani zangu za uwongo za sasa. Nikiiwekea mipaka kazi na maneno ya Mungu kuwa yale tu yaliyo katika Biblia, nitakuwa nikifanya makosa sawa na yale waliyofanya Mafarisayo ambao walishikilia sana Maandiko ya zamani kumshutumu Bwana Yesu?

Wahubiri wa injili katika sinema walisoma kifungu kingine cha maneno ya Mungu: “Ninachokufundisha ni hulka tu na kisa cha ndani cha Biblia. Sikwambii kwamba usisome Biblia, au uzunguke ukitangaza kwamba haina thamani kabisa, bali kwamba uweze kuwa na maarifa na mtazamo sahihi juu ya Biblia. Usiegemee upande mmoja sana! Ingawa Biblia ni kitabu cha historia kilichoandikwa na wanadamu, pia kinaandika kanuni nyingi ambazo kwazo watakatifu wa zamani na manabii walimhudumia Mungu, vilevile uzoefu wa hivi karibuni wa mitume katika kumhudumia Mungu—yote haya yalishuhudiwa na kujulikana kwa watu hawa, na inaweza kutumika kama rejeleo kwa ajili ya watu wa enzi hii katika kutafuta njia ya kweli. … Vitabu hivi bado vimepitwa na wakati, bado ni vitabu vya enzi ya kale, na haijalishi ni vizuri kiasi gani, vinafaa tu kwa ajili ya kipindi kimoja, na wala sio vya milele. Maana kazi ya Mungu siku zote inaendelea, na haiwezi kusimama tu katika kipindi cha Paulo na Petro, au siku zote ibaki katika Enzi ya Neema, enzi ambayo Yesu alisulubiwa. Na hivyo, vitabu hivi vinafaa tu katika Enzi ya Neema, na wala sio kwa ajili ya Enzi ya Ufalme wa siku za mwisho. Vinaweza tu kuwa na manufaa kwa waumini wa Enzi ya Neema, na sio kwa watakatifu wa Enzi ya Ufalme, na haijalishi ni vizuri kiasi gani, bado havifai kwa kipindi hiki(Neno Laonekana katika Mwili).

Niliposikia hili, niliona kwamba Mwenyezi Mungu hakuwa akiyadunisha yale ambayo Biblia ilisema. Biblia ni rekodi tu ya kazi ya Mungu ya zamani ambayo inaweza kutusaidia kuelewa kazi ambayo Amefanya na Alichohitaji kutoka kwa mwanadamu wakati huo. Lakini Mungu anatekeleza kazi mpya na Biblia imepitwa na wakati. Haiwezi kuwapa watu kile wanachohitaji leo. Nilihisi mwenye kupinga mara ya kwanza nilipotazama filamu ya kanisa, Toka Nje ya Biblia. Nilidhani kwamba imani yetu ilipaswa kuwa na msingi katika Biblia na hiyo ndiyo njia pekee ambayo tungejua jinsi ya kuamini katika Mungu. Nilidhani kuiacha Biblia kulikuwa kumwacha Mungu. Nilikuwa mpinzani kujifunza juu ya kazi ya Mwenyezi Mungu ya siku za mwisho. Nilidhani kwamba Biblia ilimwakilisha Mungu na ni msingi wa imani. Hili lilinionyesha kwamba Biblia ilichukua nafasi ya Mungu moyoni mwangu. Sikumwamini Mungu kweli—niliamini katika Biblia. Kwangu, Mungu alikuwa sawa na Biblia, na kazi Yake ingeaweza kuwa tu katika Biblia. Nilidhani kuwa kitu chochote kando na hilo ulikuwa uzushi. Je, sikuwa nikimpinga na kumkufuru Mungu? Nikiwa nimesumbuliwa na mawazo yangu, nilimshukuru Mungu sana kwa kunionyesha filamu hiyo. La sivyo, kungekuwa na matokeo mabaya.

Watu ambao walishiriki injili katika sinema kisha walisema: “Biblia haiwezi kutoa uzima wa milele ...” Nilishtuka. Maisha ya milele hayatoki katika Biblia? Hiyo inawezekanaje? Nilisikiza walichosema baada ya hapo. “Imani maarufu inasema vinginevyo, lakini ni ukweli usiopingika. Bwana Yesu alituambia, wakati aliwakemea Mafarisayo miaka yote iliyopita: ‘Tafuteni katika maandiko; kwa kuwa ndani yake mnafikiri kuwa mnao uhai wa milele: na nashuhudiwa na hayo. Nanyi hamkuji kwangu, ili mpate uhai(Yohana 5:39-40). Bwana Yesu alituambia, hakuna uzima wa milele katika maandiko. Kwa sababu maandiko yanamshuhudia tu Mungu. Ikiwa watu wanataka ukweli na uzima, Biblia haitoshi hata kidogo. Ukweli na uzima lazima vipatikane kutoka kwa Kristo Mwenyewe pekee. Kumbuka Mafarisayo ambao walishikilia Agano la Kale? Hawakupata uzima wa milele na waliadhibiwa kwa kumpinga na kumshutumu Bwana Yesu. Lakini wafuasi wa Bwana Yesu ambao hawakushikilia Maandiko ambao walikubali kazi na maneno yote ya Mungu ya wakati huo mwishowe walikombolewa na Bwana Yesu.” “Na hivyo, njia pekee ya kupata uzima wa milele ni kumfuata Kristo na nyayo za Mungu.” “Tukiifuata Biblia bila kufikiri kando na kutopata kibali cha Mungu, pia kweli ni kama tu alivyosema Paulo, ‘Lakini andiko limehitimisha vyote chini ya dhambi’ (Wagalatia 3:22). na tutapoteza wokovu. Mungu hufanya kazi mpya katika kila enzi. Yehova Mungu alitoa amri katika Enzi ya Sheria kwa hivyo Waisraeli walijua jinsi ya kumwabudu Mungu vizuri, jinsi ya kuishi duniani, walijua pia dhambi ni nini, na kwamba wangeadhibiwa kwa sababu ya dhambi zao zote. Katika Enzi ya Neema, Bwana Yesu alifanya kazi ya ukombozi, akijitoa Mwenyewe binafsi. Watu walihitajika kukiri na kutubu tu ili wasamehewe na waepuke laana chini ya sheria. Hata hivyo, ukombozi wa Bwana Yesu unaweza tu kusamehe dhambi zetu. Asili yetu bado ni yenye dhambi kwa kina. Mara nyingi sisi hufichua tabia yetu ya kiburi, danganyifu, mbovu na ya ubinafsi na hatuwezi kujizuia ila kutenda dhambi na kumpinga Mungu. Hiyo ndiyo maana Bwana Yesu alitabiri kwamba Atakuja tena kuleta hukumu, kumtakasa na kumwokoa mwanadamu kabisa kutoka katika dhambi. Katika siku za mwisho, Mwenyezi Mungu analeta hukumu akianza na nyumba Yake, kwa msingi wa ukombozi wa Bwana Yesu. Anaonyesha ukweli wote kumwokoa na kumtakasa mwanadamu na kuuangazia mpango Wake wa usimamizi. Anahukumu na kufunua tabia na asili ya wanadamu ya kishetani, Akionyesha tabia Yake takatifu na yenye haki isiyovumilia kosa lolote.” “Maneno yaliyoonyeshwa na Mwenyezi Mungu, hayakuwahi kunenwa na Mungu katika Enzi ya Sheria au Enzi ya Neema. Maneno haya, ni Mungu anayetupa njia ya uzima wa milele. Unabii wa Bwana Yesu unatimia: ‘Bado ningali nayo mengi ya kuwaambieni, lakini hivi sasa hamwezi kuyavumilia. Hata hivyo, wakati Yeye, Roho wa ukweli, atakapokuja, Atawaongoza hadi kwenye ukweli wote(Yohana 16:12-13).”

Kisha wakasoma kifungu kingine cha maneno ya Mwenyezi Mungu. “Kristo wa siku za mwisho huleta uzima, na huleta kudumu kwa njia ya kweli na ya milele. Ukweli huu ni njia ambayo kwayo binadamu atapata uzima, na njia pekee ambayo mtu atamjua Mungu na kuidhinishwa na Mungu. Kama hutatafuta njia ya maisha inayotolewa na Kristo wa siku za mwisho, basi kamwe hutapata kibali cha Yesu, na kamwe hutastahili kuingia lango la ufalme wa mbinguni, maana wewe ni kikaragosi na mfungwa wa historia. Wale ambao wanadhibitiwa na kanuni, na maandiko, na waliofungwa na historia kamwe hawataweza kupata maisha, na kamwe hawataweza kupata njia ya daima ya maisha. Hiyo ni kwa sababu yote walio nayo ni maji machafu ambayo yameshikiliwa kwa maelfu ya miaka badala ya maji ya uzima yanayotiririka kutoka kwenye kiti cha enzi. Wale ambao hawajaruzukiwa maji ya uzima daima watabakia maiti, vitu vya kuchezewa na Shetani, na wana wa Jehanamu. Je, basi jinsi gani wanaweza kumtazama Mungu? Kama wewe kamwe hujaribu kushikilia kwenye siku zilizopita, jaribu tu kuweka mambo kama yalivyo kwa kusimama kwa utulivu, na wala hujaribu kubadili hali kama ilivyo na kuacha historia, basi wewe hutakuwa daima dhidi ya Mungu? Hatua za kazi ya Mungu ni kubwa na zenye nguvu, kama kufurika kwa mawimbi na mngurumo wa radi—ilhali wewe unakaa na kwa uvivu ukisubiri uharibifu, na kujikita katika upumbavu wako na kutofanya chochote. Kwa njia hii, jinsi gani unaweza kuchukuliwa kama mtu anayefuata nyayo za Mwanakondoo? Jinsi gani unaweza kuhalalisha Mungu unayeshikilia kama Mungu ambaye ni daima mpya na si kamwe wa zamani? Na jinsi gani maneno ya vitabu vyako vya manjano yanaweza kukubeba hadi enzi mpya? Yanawezaje kukuongoza katika kutafuta hatua za kazi ya Mungu? Na jinsi gani yanaweza kukuchukua wewe kwenda mbinguni? Unayoshikilia mikononi ni barua ambazo zisizoweza kukuondolea kitu ila furaha ya muda mfupi, sio ukweli unaoweza kukupa maisha. Maandiko unayosoma ni yale tu ambayo yanaweza kuimarisha ulimi wako, sio maneno ya hekima ambayo yanaweza kukusaidia kujua maisha ya binadamu, sembuse njia zinazoweza kukuongoza kuelekea kwa ukamilifu. Je, si tofauti hii hukupa sababu kwa ajili ya kutafakari? Je, si inakuruhusu kuelewa siri zilizomo ndani? Je, una uwezo wa kujiwasilisha mwenyewe mbinguni kukutana na Mungu? Bila kuja kwa Mungu, je, unaweza kujichukua mwenyewe kwenda mbinguni kufurahia pamoja na familia ya Mungu? Je, wewe bado unaota sasa? Basi, Napendekeza sasa acha kuota, na kuangalia Anayefanya kazi sasa, na Anayefanya kazi ya kuwaokoa binadamu siku za mwisho. Kama huwezi, wewe kamwe hutapata ukweli, na kamwe hutapata uzima(Neno Laonekana katika Mwili). Wainjilisti kutoka Kanisa la Mwenyezi Mungu walishiriki maneno haya: “Tukiishikilia tu Biblia katika imani yetu na tusiyakubali matamko ya Mungu katika siku za mwisho, hatutaweza kamwe kufunzwa na maji yaliyo hai ya Mungu. Bila hukumu ya Mungu, hatuwezi kuepukana na mzunguko mbaya wa kutenda dhambi na kukiri. Bila kuzikimbia pingu za dhambi, mtu yeyote anawezaje kuingia katika ufalme wa mbinguni? Ni kwa kukubali hukumu ya Mwenyezi Mungu ya siku za mwisho tu ndiyo tunaweza kufunzwa na maneno ya Mungu, tujue ukweli, tuwekwe huru kutokana na upotovu wetu na tutakaswe. Kisha tutaweza kuingia katika ufalme wa mbinguni.”

Nilihisi mwenye kutiwa nuru na mwenye furaha zaidi nilipokuwa nikitazama na kusikiliza. Ushirika huu ulikuwa wa vitendo. Uzima wa milele haumo katika Biblia—ni ushuhuda tu kwa Mungu. Haimwakilisha Mungu, wala haiwezi kuchukua nafasi ya kazi Yake ya wokovu. Ni Kristo tu ndiye njia, ukweli na uzima. Ni Kristo tu ndiye anayeweza kutupa ukweli na uzima. Kristo wa siku za mwisho, Mwenyezi Mungu, anaonyesha ukweli ili kumwokoa mwanadamu. Nilikuwa mpumbavu sana! Sikuweza kuiachilia Biblia. Nilishukuru sana Mwenyezi Mungu aliniongoza kuisikia sauti ya Mungu na kuyaacha maoni yangu ya upuuzi kuhusu imani. Mwishowe niliikubali kazi ya Mwenyezi Mungu ya siku za mwisho!

Iliyotangulia: Siri ya Majina ya Mungu

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Maudhui Yanayohusiana

Kufichua Fumbo la Hukumu

Na Enhui, MalasiaJina langu ni Enhui; nina umri wa miaka 46. Ninaishi Malaysia, nami nimekuwa mwumini katika Bwana kwa miaka 27. Mnamo...

Neno La Mungu Ni Nguvu Yangu

Na Jingnian, KanadaNimefuata imani ya familia yangu katika Bwana tangu nilipokuwa mtoto, nikisoma Bibilia mara nyingi na kuhudhuria ibada....

Wokovu wa Aina Tofauti

Na Huang Lin, ChinaNilikuwa mwumini wa kawaida katika Ukristo wa Kipaji, na tangu nianze kuamini katika Bwana sikuwahi kukosa ibada....

Leave a Reply

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp