Jaribu la Uzao wa Moabu

24/01/2021

Na Zhuanyi, Uchina

Mwenyezi Mungu anasema, “Kazi yote ifanywayo siku hii ya leo ni ili mwanadamu afanywe msafi na kubadilika; kupitia hukumu na kuadibiwa na neno, na pia kutakaswa, mwanadamu anaweza kuacha nje upotovu wake na kufanywa safi. Badala ya kuichukua hatua hii ya kazi kuwa ile ya wokovu, itafaa zaidi kusema kuwa ni kazi ya utakaso. Kwa kweli hatua hii ni ile ya ushindi na pia hatua ya pili ya wokovu. Mwanadamu anatwaliwa na Mungu kupitia hukumu na kuadibu na neno; kwa kutumia neno kusafisha, hukumu na kufichua, uchafu wote, fikira, nia, na matumaini ya mtu mwenyewe katika moyo wa mwanadamu zinafuliwa(Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Fumbo la Kupata Mwili (4)). “Kufanya kazi sasa kwa uzao wa Moabu ni kuwaokoa wale ambao wameanguka katika giza zaidi. Ingawa walikuwa wamelaaniwa, Mungu yuko tayari kupata utukufu kutoka kwao. Hii ni kwa sababu hapo awali, wote walikuwa watu waliomkosa Mungu mioyoni mwao—kuwafanya tu kuwa wale wanaomtii na kumpenda Yeye ni ushindi wa kweli, na matunda hayo ya kazi ni ya thamani sana na yenye kuridhisha zaidi. Huku tu ni kupata utukufu—huu ndio utukufu ambao Mungu anataka kuupata katika siku za mwisho. Ingawa watu hawa ni wa nafasi ya chini, sasa wanaweza kupata wokovu mkubwa mno, ambao kwa kweli ni kupandishwa hadhi na Mungu. Kazi hii ni ya maana sana, na ni kwa njia ya hukumu ndipo Anawapata watu hawa. Yeye hawaadhibu kwa makusudi, lakini Amekuja kuwaokoa. Kama angekuwa Anafanya kazi ya kushinda katika Israeli wakati wa siku za mwisho ingekuwa ni bure; hata kama ingezaa matunda, haingekuwa na thamani yoyote au umuhimu wowote mkubwa, na Yeye hangeweza kupata utukufu wote(Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Umuhimu wa Kuukoa Uzao wa Moabu). Kusikiliza maneno haya kutoka kwa Mungu kunanifanya nikumbuke jaribu nililipotoa kama uzao wa Moabu.

Nakumbuka mnamo 1993, Mwenyezi Mungu alionyesha Ukweli wa Ndani wa Kazi ya Ushindi (2) na Asili na Utambulisho wa Mwanadamu. Alifichua kwamba nchini China, wateule wote wa Mungu ni uzao wa Moabu. Nilisoma maneno haya ya Mungu wakati huo: “Uzao wa Moabu ni watu duni sana kuliko watu wote duniani. Watu wengine huuliza, je, wafuasi wa Hamu sio duni kuliko wote? Kizazi cha joka kuu jekundu na uzao wa Hamu ni wenye umuhimu tofauti wakilishi, na uzao wa Hamu ni suala jingine. Bila kujali ni jinsi gani wamelaaniwa, bado ni uzao wa Nuhu; asili za Moabu, wakati ule ule, hazikuwa safi: Moabu alitoka katika uzinzi, na hii ndiyo tofauti(Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Ukweli wa Ndani wa Kazi ya Ushindi (2)). “Wale ambao Mimi huokoa ni wale ambao Nimewaamulia kabla zamani na wamekombolewa na Mimi, wakati ninyi ni nafsi hafifu ambazo zimewekwa kati ya wanadamu kama jambo la pekee. Mnapaswa kujua kwamba nyinyi si wa nyumba ya Daudi au Yakobo, lakini ni wa nyumba ya Moabu, ambao ni wanachama wa kabila la Mataifa. Kwa maana Sikuanzisha agano na nyinyi, lakini Nilitekeleza tu kazi na kunena kati yenu, na kuwaongoza. Damu Yangu haikumwagika kwa ajili yenu. Nilitekeleza tu kazi kati yenu kwa ajili ya ushuhuda Wangu. Je, hamjajua hilo?(Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Asili na Utambulisho wa Mwanadamu). Nilishangaa sana. Nilijiuliza, “Je, sisi ni uzao wa Moabu? Je, hii ni kweli? Moabu alikuwa mwana wa Lutu na bintiye. Alitokana na uasherati na hakuwa wa asili safi, kwa hivyo, tunawezaje kuwa uzao wake? Katika kumwamini kwangu Bwana, ilisemekana kwamba sisi ni uzao wa Israeli na kwamba tulikuwa wa nyumba ya Yakobo. Hivyo basi, kwa nini Mungu aseme kwamba sisi ni uzao wa Moabu?” Sikuweza kabisa kukubali haya, lakini nikawaza baadaye, “Maneno yote ya Mungu ni ukweli na Yeye hufichua ukweli pekee. Hilo haliwezi likawa kosa! Kwa nini mimi ni uzao wa Moabu na kwa nini nilizaliwa nchini China?” Nilidhani kwamba kama mmoja wa waliotangulia kupitia hukumu na kuadibu kwa Mungu, kama mmoja wa waliotangulia kupitia kazi ya Mungu ya hukumu na utakaso katika siku za mwisho, na kama mtu ambaye angefanywa kuwa mshindi na mfano kabla ya maafa, hadhi yangu hakika ilikuwa ya juu zaidi kuliko ya wateule wa Mungu katika nchi nyingine yoyote. Lakini ajabu ni kwamba, nilikuwa uzao wa Moabu, na zaidi ya kulaaniwa na Mungu, nilitokana na uasherati. Nilikuwa duni kabisa na aliyeshushwa hadhi zaidi kuliko wanadamu wote. Je, wasioamini wangenionaje kama wangegundua hilo? Je, wanafamilia wangu wasioamini wangesema nini? Nilikuwa nimeacha nyumbani kwangu na kazi yangu kwa ajili ya imani yangu na niliteseka na kujitumia lakini mwishowe nilikuwa tu uzao wa Moabu. Jambo hilo lilikuwa la kufedhehesha na la aibu sana. Nilihisi kwamba sikuwa na budi kuteseka kimyakimya. Katika kipindi hicho cha muda, pindi nilipofikiri juu ya kuwa uzao wa Moabu na matokeo ya uasherati, niliaibika sana na sikuweza kujitokeza mbele ya watu. Nilikaa nyumbani kwa siku kadhaa wakati fulani, bila kula wala kulala, na sikuwa na shauku hata kidogo ya kufanya chochote nyumbani. Nilikuwa nikilalamika tu kila wakati ndani ya moyo wangu, “Nawezaje kuwa mmoja wa uzao wa Moabu? Je, urithi wangu na hadhi yangu vinawezaje kuwa duni sana?” Nilikuwa kama mtu aliyekua katika familia tajiri na aliyejivunia sana, nikidhani kwamba nilikuwa wa uzao bora, lakini siku moja bila kutegemea, nikapata habari kwamba nilikuwa nimetolewa kutoka katika takataka, na sikuwa wa ukoo huo hata kidogo. Nilijawana na huzuni, kutojiweza, na majonzi na sikuweza kabsa kukubali ukweli huu. Nilijawa na kutoridhika, uhasi na suitafahamu. Nilidhani kwamba kama uzao wa Moabu, nililaaniwa na Mungu hataniokoa kamwe. Kadiri nilivyozidi kufikiria hayo, ndivyo nilivyozidi kuhisi kwamba nilikosewa. Ilikuwa kama kwamba kulikuwa na uzito mkubwa sana ulionigandamiza kifuani na nilipumua kwa shida. Nilikwenda kimyakiya bafuni kulia peke yangu…. Kila mtu alikuwa akiteseka wakati huo. Watu wengine walilia kila hilo lilipotajwa.

Tulipokuwa tu tukipitia mateso haya, Mwenyezi Mungu alitoa maneno Yake Umuhimu wa Kuukoa Uzao wa Moabu, Akafichua hali zetu na kutuambia mapenzi Yake yalikuwa yapi. Nilisoma maneno haya kutoka kwa Mungu: “Mwanzoni nilipowapa nafasi ya watu wa Mungu mlikuwa mnaruka juu chini—mliruka kwa furaha zaidi kuliko mtu yeyote. Lakini ilikuwaje mara Niliposema kuwa ninyi ni uzao wa Moabu? Ninyi nyote mlishindwa kustahimili! Ungesema kimo chenu kipo wapi? Dhana yenu ya nafasi ni nzito sana! … Ni mateso ya namna gani ambayo mmestahimili, lakini mnahisi kuwa mmetendewa mabaya sana? Mnafikiri kwamba mara tu Mungu amewatesa hadi kiwango fulani Atafurahi, kana kwamba Mungu alikuja kuwahukumu kimakusudi, na baada ya kuwahukumu na kuwaangamiza, kazi Yake itakuwa imekamilika. Je, ni hivyo ndivyo Nimesema? Je, si hii ni kwa sababu ya upofu wenu? Je! Ni kwamba ninyi wenyewe hamjitahidi kufanya vizuri au kwamba Ninawahukumu kwa makusudi? Sijawahi kufanya hivyo—hilo ni jambo ambalo mlilifikiria wenyewe. Sijafanya kazi kwa njia hiyo kabisa, wala Sina nia hiyo. Kama Ningetaka kuwaangamiza kwa kweli, je, Ningehitaji kuteseka sana hivyo? Ningetaka kuwaangamiza kwa kweli, Ningehitaji kuzungumza nanyi kwa dhati? Mapenzi Yangu ni haya: wakati ambapo Nimewaokoa ndipo Nitakapoweza kupumzika. Zaidi mtu alivyo wa hali ya chini, ndivyo alivyo chombo cha wokovu wangu zaidi. Zaidi mwezavyo kuingia kiutendaji, ndivyo Nitakavyofurahia zaidi. Zaidi mnavyoshindwa kustahimili ndivyo Ninavyofadhaika zaidi. Daima mnataka kuingia kwa mwendo wa furaha kuelekea kiti cha enzi, lakini Nitawaambieni, hiyo sio njia ya kuwaokoa kutokana na uchafu. Njozi ya kukaa kwa kiti cha enzi haiwezi kukufanya kuwa mkamilifu; hiyo si kweli(Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Umuhimu wa Kuukoa Uzao wa Moabu). Nilihisi hatia sana niliposoma maneno haya. Nilikumbuka jinsi ambavyo hapo awali, Mungu aliposema kwamba tulikuwa watu wa ufalme na kwamba tutafanywa kuwa washindi na kuwa mifano, nilianza kuwa mwenye kiburi na sikujua nilikuwa nani, na niliamini kwamba kwa kuwa nilikuwa mmoja wa waliotangulia kukubali hukumu na kuadibu kwa Mungu na mmoja wa waliotangulia kukamilishwa, hakika nilikuwa na hadhi ya juu kuliko wateule wa Mungu kutoka nchi nyingine yoyote. Nilijivuna sana na niliridhika sana. Mungu alipotufichua kama uzao wa Moabu, niliona kwamba nilikuwa wa ukoo duni na kwamba nililaaniwa na Mungu. Nilidhani kwamba Mungu hataniokoa kamwe, kwa hivyo nilitumbukia katika uhasi na sikuweza kuondokana nao. Niligundua tamaa yangu ya hadhi ilikuwa thabiti sana na kimo changu kilikuwa kidogo sana. Kwa kweli, hata ingawa Mungu alitufunua kama uzao wa Moabu, Hakusema kwamba kamwe Hatatuokoa. Hata hivyo, Alipata mwili katika nchi ya joka kubwa jekundu, na Akaonyesha ukweli ili kutuhukumu, kutuadibu, kutunyunyizia na kuturuzuku kusudi sisi watu wachafu na wapotovu zaidi tuweze kupata nafasi ya kuokolewa na Mungu. Hayo yote yametokana na nia njema za Mungu! Lakini sikuelewa mapenzi ya Mungu. Nilidhani kwamba mimi kama uzao wa Moabu na mtu mchafu na duni nitachukiwa na kudharauliwa na Mungu zaidi, na hakukuwa na uwezekano Wake kuniokoa. Nilielewa visivyo na kulalamika na nikawa hasi na kumpinga Mungu. Sikuwa na mantiki kabisa! Muda mfupi baadaye, nilisoma maneno haya ya Mungu: “Hata kama Singesema ninyi ni uzao wa Moabu, je, asili yenu, mahali penu pa kuzaliwa ni ya fahari sana? Hata kama Singesema ninyi ni uzao wake, je, si ninyi nyote ni uzao wa Moabu kwa kweli? Ukweli wa mambo unaweza kubadilishwa? Je, kufichua asili yenu sasa kunaenda dhidi ya ukweli wa mambo? Angalieni jinsi mlivyo wanyonge, maisha yenu, na tabia—je, hamjui kwamba ninyi ni wa chini kabisa kati ya walio chini miongoni mwa wanadamu? Nini mlicho nacho cha kujisifia? Angalia nafasi yenu katika jamii. Je, si mko katika kiwango cha chini kabisa? Je, mnadhani kwamba Nimenena vibaya? Ibrahimu alimtoa Isaka. Nini ambacho mmetoa? Ayubu ilitoa kila kitu. Nini ambacho mmetoa? Watu wengi sana wameyatoa maisha yao, wakafa, wakamwaga damu yao ili kutafuta njia ya kweli. Je, mmelipa gharama hiyo? Kwa kulinganisha, hamna sifa zinazostahili hata kidogo kufurahia neema hiyo kubwa, kwa hivyo ni sawa kusema leo kwamba ninyi ni uzao wa Moabu? Msijione kuwa wakuu sana. Huna chochote cha kujisifia. Wokovu mkubwa kama huo, neema hiyo kubwa imepewa kwenu bure. Hamjatoa chochote, lakini mmeifurahia neema bure. Je, hamuoni haya?(Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Umuhimu wa Kuukoa Uzao wa Moabu). Kila swali la Mungu lilipenya moyoni mwangu. Niliaibika na nikatahayarika sana! Nilikumbuka watakatifu katika enzi zote—walikuwa waaminifu na watiifu kwa Mungu na hakuwahi kumlaumu walipokuwa wakipitia majaribu makubwa. Walikuwa mashahidi wa Mungu na walipata kibali na baraka Zake. Abrahamu alitii amri za Mungu kwa kumtoa Isaka, mwanawe mpendwa zaidi, kwa Mungu. Hakujadili masharti yoyote au kujaribu kubishana na Mungu, bali alitii kabisa. Na Ayubu alipopitia jaribu kubwa na kupoteza mali yote ya familia yake, watoto wake wote na mwili wake kujawa na majipu, bado alimsifu Mungu, akisema, “Yehova alinipa, na Yehova amechukua; jina la Yehova libarikiwe” (Ayubu 1:21). Lakini nilizaliwa katika nchi ya joka kubwa jekundu, nilielimishwa ukanaji Mungu, mageuko na uyakinifu tangu nilipokuwa mdogo. Sikuwahi kujua kwamba Mungu alikuwapo, sembuse kujua jinsi ya kumwabudu. Niliamini tu kusudi nipate neema na baraka za Mungu, ili baadaye niweze kuingia katika ufalme wa mbinguni na niwe na hatima nzuri. Nilipokabiliwa na majaribu fulani, wakati ambapo sikuwa na hadhi na sikupata baraka zozote, nilielewa visivyo na kulalamika tu na nikawa hasi na kumpinga Mungu. Sikuwa mtiifu kwa kweli na sikuwa nikimtendea kama Mungu. Katika miaka hiyo yote ya kuwa muumini, nilikuwa nikifurahia riziki ya maneno ya Mungu bure, na mwongozo wa hatua kwa hatua wa kazi ya Mungu. Mbali na kutofanya wajibu wangu vizuri ili kulipa upendo Wake, pia yote niliyompa kama malipo yalikuwa kumwelewa visivyo na malalamiko, uasi na upinzani. Je, nilikuwa muumini wa aina gani? Hata hivyo, nilikuwa nimejiona kama kipenzi cha Mungu, kama mtu wa maana Kwake na nilidhani kwamba nitakuwa na hadhi ya juu kuliko ya wateule wa Mungu kutoka mahali pengine popote na kwamba nitafaa zaidi thawabu na baraka za Mungu. Nilikuwa mwenye kiburi sana kiasi kwamba sikujua lolote. Sikujijua hata kidogo! Mungu asingefichua asili yangu chafu na duni, bado ningefikiri kwamba nilikuwa mmoja wa makabila 12 ya Yakobo, na kwamba nilikuwa mwana wa Israeli na uzao wa Daudi. Sikuwa na aibu kabisa! Sasa najua utambulisho wangu na hadhi yangu, kwa hivyo mimi hukwepa kujionyesha. Mimi si fidhuli sana kama hapo zamani. Nimepata pia mantiki kiasi mbele za Mungu. Huu ni wokovu wa Mungu kwangu! Sipaswi kuhodhi madai yoyote ya kupita kiasi kwa Mungu, na hata nisipokuwa na matokeo mazuri au hatima nzuri mwishowe, bado nitatii yale ambayo Mungu atayapanga na nitasifu haki Yake.

Baadaye, nilisoma maneno mengine zaidi ya Mwenyezi Mungu na nikaelewa zaidi kuhusu umuhimu wa Mungu kufanya kazi ndani ya uzao wa Moabu. Niliona kwamba hivi ndivyo maneno ya Mungu yasemavyo. “Kufanya kazi sasa kwa uzao wa Moabu ni kuwaokoa wale ambao wameanguka katika giza zaidi. Ingawa walikuwa wamelaaniwa, Mungu yuko tayari kupata utukufu kutoka kwao. Hii ni kwa sababu hapo awali, wote walikuwa watu waliomkosa Mungu mioyoni mwao—kuwafanya tu kuwa wale wanaomtii na kumpenda Yeye ni ushindi wa kweli, na matunda hayo ya kazi ni ya thamani sana na yenye kuridhisha zaidi. Huku tu ni kupata utukufu—huu ndio utukufu ambao Mungu anataka kuupata katika siku za mwisho. Ingawa watu hawa ni wa nafasi ya chini, sasa wanaweza kupata wokovu mkubwa mno, ambao kwa kweli ni kupandishwa hadhi na Mungu. Kazi hii ni ya maana sana, na ni kwa njia ya hukumu ndipo Anawapata watu hawa. Yeye hawaadhibu kwa makusudi, lakini Amekuja kuwaokoa. Kama angekuwa Anafanya kazi ya kushinda katika Israeli wakati wa siku za mwisho ingekuwa ni bure; hata kama ingezaa matunda, haingekuwa na thamani yoyote au umuhimu wowote mkubwa, na Yeye hangeweza kupata utukufu wote. … Kufanya kazi kwenu sasa, uzao wa Moabu, sio kuwafedhehesha kwa makusudi, lakini ni kufichua umuhimu wa kazi. Ni kuwainua sana. Ikiwa mtu ana mantiki na utambuzi, atasema: ‘Mimi ni uzao wa Moabu. Kweli sistahili kuinuliwa kukuu huku na Mungu ambako nimepokea sasa, au baraka hizi nyingi. Kwa mujibu wa yale ninayofanya na kusema, na kulingana na hali na thamani yangu—sistahili kabisa hizo baraka nyingi kutoka kwa Mungu. Waisraeli wana upendo mkubwa kwa Mungu, na neema wanayoifurahia imefadhiliwa kwao na Yeye, lakini hali yao ni ya juu zaidi kuliko yetu. Abrahamu alijitolea sana kwa Yehova, na Petro alijitolea sana kwa Yesu—ibada yao ilishinda yetu kwa mara mia, na kwa msingi wa matendo yetu hatufai kabisa kufurahia neema ya Mungu’(Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Umuhimu wa Kuukoa Uzao wa Moabu). “Wazawa wa Moabu walilaaniwa, na walizaliwa ndani ya nchi hii isiyo na maendeleo; bila shaka, wazawa wa Moabu ni watu walio na hadhi ya chini zaidi chini ya ushawishi wa giza. Kwa sababu hawa watu walimiliki hadhi ya chini zaidi zamani, kazi inayofanywa miongoni mwao inaweza kabisa kuzivunja dhana za binadamu, na pia ni kazi yenye faida kubwa zaidi kwa mpango Wake mzima wa usimamizi wa miaka elfu sita. Ili Afanye kazi miongoni mwa watu hawa ni kitendo kinachoweza zaidi kuzivunja dhana za binadamu; Akiwa na hili Anazindua enzi; na hili Anavunja dhana zote za binadamu; Akiwa na hili Anatamatisha kazi ya Enzi nzima ya Neema. Kazi Yake ya awali ilifanywa Yudea, ndani ya eneo la Israeli; katika mataifa yasiyo ya Kiyahudi Hakufanya kazi yoyote ya uzinduzi wa enzi hata kidogo. Hatua ya mwisho ya kazi Yake haifanywi tu miongoni mwa watu wa mataifa yasiyo ya Kiyahudi; hata zaidi ya hayo, inafanywa miongoni mwa watu waliolaaniwa. Jambo hili moja ndio ushahidi unaoweza zaidi kumwaibisha Shetani; hivyo, Mungu ‘anakuwa’ Mungu wa viumbe vyote ulimwenguni na kuwa Bwana wa vitu vyote, Anayeabudiwa na kila kiumbe mwenye uhai(Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Mungu Ndiye Bwana wa Viumbe Vyote). Nilifikiri kwamba Mungu alikuwa Ameamua hapo mwanzo kwamba Atawaokoa kina nani na kwamba wao walikuwa wateule Wake, kwa hivyo kwa kuwa Wachina walikuwa uzao wa Moabu, kwa kuwa sisi tulikuwa duni zaidi, tulimfahamu Mungu kwa kiasi kidogo zaidi na kumpinga Mungu zaidi, na tulilaaniwa na kukataliwa na Mungu, bila shaka Hatatuokoa. Lakini Mungu hakufanya hivyo hata kidogo. Hakututelekeza kwa sababu sisi ni duni na hakuacha kutuokoa kwa sababu sisi ni wachafu na wapotovu. Badala yake, Yeye mwenyewe Alipata mwili na Akavumilia aibu na mateso mengi ili kuja miongoni mwetu sisi uzao wa Moabu kufanya kazi, kutuhukumu, kutuadibu, kutujaribu, na kutusafisha mara nyingi kwa maneno Yake. Alifanya yote hayo ili kututakasa na kutuokoa. Upendo wa Mungu ni mkubwa sana! Ni kama Bwana Yesu akila kwenye meza moja na wenye dhambi. Kadiri tulivyo wachafu na duni zaidi, ndivyo tunavyozidi kuona jinsi upendo na wokovu wa Mungu ulivyo mkubwa. Mwishowe, Mungu anataka kutuokoa sisi watu tuliopotoka sana, watu wachafu na duni zaidi, kutokana na nguvu za giza za Shetani ili tuweze kuwa na ushuhuda wa kuleta sifa kuu Kwake. Jambo hili ndilo litakalomwaibisha Shetani zaidi. Hili ndilo kusudi la kazi ya Mungu ndani ya uzao wa Moabu! Pia, Kazi ya Mungu ndani ya uzao wa Moabu katika siku za mwisho imeharibu fikira zetu zote, na kutufanya tuone kwamba mbali na Yeye kuwa Mungu wa Waisraeli, Yeye pia ni Mungu wa viumbe wote. Yeye haangalii asili, nchi au kabila letu, iwapo sisi ni Waisraeli au uzao wa Moabu, iwapo tumebarikiwa au kulaaniwa na Mungu. Ilimradi sisi ni viumbe, ilimradi tufuatilie ukweli na tutii kazi ya Mungu, tunaweza kuokolewa na Mungu. Mungu hapendelei na ni mwenye haki kwa kila kiumbe, na Yeye humpa kila mmoja nafasi ya wokovu. Kadiri nilivyozidi kutafakari maneno ya Mungu, ndivyo nilivyozidi kuhisi umuhimu mkubwa wa kazi ya Mungu ndani ya uzao wa Moabu, na jinsi upendo na wokovu wa Mungu kwa wanadamu waliopotoka ulivyo halisi. Lakini kwa bahati mbaya, ubora wangu wa tabia ni duni sana na ufahamu wangu juu ya kazi ya Mungu ni mdogo. Naweza tu kushiriki kiasi kidogo cha hisia na ufahamu wangu, lakini siwezi kutoa ushuhuda mzuri. Nina deni kubwa sana la Mungu kwa kweli.

Ninapokumbuka hayo sasa, nilipopitia majaribu ya kuwa uzao wa Moabu, ingawa niliteseka kidogo wakati huo, nilikuja kujua utambulisho na thamani yangu. Nilielewa kidogo kazi ya Mungu ya kuwaokoa watu na tabia Yake yenye haki, na sijakuwa mwenye kiburi na majisifu sana tangu wakati huo. Nilikuja kuhisi jinsi nilivyo duni na mpotovu, kwamba sistahili upendo na wokovu Wake na sithubutu kutaka mambo ya ajabu tena kutoka Kwake. Bila kujali jinsi Mungu anavyonitendea au kile Anachopanga, niko tayari kukikubali na kutii. Ninataka tu kukubali hukumu na kuadibu kwa maneno ya Mungu kwa uaminifu na kutafuta mabadiliko katika tabia ya maisha yangu. Hata kama mimi ni uzao wa Moabu, bado sina budi kufuatilia ukweli na kuwa shahidi wa Mungu. “Sisi sio Waisraeli, bali ni uzao wa Moabu uliotelekezwa, sisi sio Petro, ambaye hatuwezi kuwa na ubora wa tabia yake, wala sisi sio Ayubu, na hata hatuwezi kujilinganisha na azimio la Paulo la kuteseka kwa ajili ya Mungu na kujitoa kikamilifu kwa Mungu, na sisi tupo nyuma sana, na hivyo, hatustahili kufurahia baraka za Mungu. Mungu bado Ametuinua leo; kwa hiyo tunapaswa kumridhisha Mungu, na ingawa tuna ubora wa tabia au sifa haba, tupo radhi kumridhisha Mungu—tuna azimio hili. Sisi ni uzao wa Moabu, na tulilaaniwa. Hili lilitangazwa na Mungu, na wala hatuwezi kuibadilisha, lakini kuishi kwetu kwa kudhihirisha na maarifa yetu yanaweza kubadilika, na tumeazimia kumridhisha Mungu(“Azimio Ambalo Wazawa wa Moabu Wanapaswa Kuwa Nalo” Mfuateni Mwanakondoo na Kuimba Nyimbo Mpya).

Iliyotangulia: Ukombozi wa Moyo
Inayofuata: Jaribu la Foili

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Maudhui Yanayohusiana

Uzoefu wa Kutenda Ukweli

Hengxin Jiji la Zhuzhou, Mkoa wa Hunan Sio muda mrefu mno uliopita, nilisikia “Mahubiri na Ushirika juu ya Kuingia Katika Maisha,” jambo...

Leave a Reply

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp